Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Wote wakaanza kumwuliza: “Kazi yako ni kazi gani? nawe umetoka wapi? nchi yako

ni nchi ipi? nawe u mtu wa kabila gani?” (mstari 8).

Ni hapo sasa Yona alipoamka kabisa. Mawimbi hayakumhofisha Yona, maana

aliwaambia, “Nami namcha BWANA, Mungu wa mbingu, aliyeziumba bahari na nchi

kavu” ( mstari 9). Alikiri kuwa alikuwa amejaribu kuutoroka uso wa BWANA na watu wale

wakaogopa mno walipotambua nguvu za Mungu ambaye Yona alimwabudu. Ni lazima jambo

fulani litendeke, maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka na tufani ikiongezeka zaidi.Basi

wakamwuliza, “Basi tukutende nini, ili bahari itutulilie?” ( mstari 11). Naye akawajibu,

“Nikamateni, mnitupe baharini; basi bahari itawatulilia; kwa maana ninajua ya kuwa ni

kwa ajili yangu tufani hii imewapata” (mstari 12).

Na ingawa watu walikuwa na nia na hofu ya kutaka kuokoa maisha yao, wazo hili la

kumtupa kwa makusudi Yona baharini liliwaogopesha sana. Walijaribu kuipeleka meli

kuelekea nchi kavu, lakini walishindwa. Watu wakamlilia BWANA. Ikaonekana kuwa ni lazima

wafanye kama Yona alivyokuwa amewaambia, uku wakimwomba ili Mungu asiwahsabie

dhambi hiyo, maana walimwamini Yona, kuwa ni Mungu aliyeleta mawimbi hayo kw sbabu

yake.

Basi wakamkata Yona, wakamtupa baharini nayo bahari ikatulia. Yoha alikuwa ameongea

kweli-Mungu wake ni kwelindiye aliyeumba bahari na nchi kavu. Wakamtolea dhmbihu ili

kuonyesha shukrani na wakeweka nadhiri ya kumtumikia BWANA. Kwa hiyo wale watu

wakapona kwa kuwa walimpeleka katika mauti.

Hata hivyo, Yona hakufa, Kwa upendo na rehema za ajabu, alikuwa ameshamwadaa

samaki mkubwa kummeza .Yona akawa katika tumbo la la samaki yule mkubwa muda siku

tatu mchanana usiku.

YONA ANALITII NENO LA MUNGU: Yona 2 na 3

Wakati Yona kw mwujiza alikuwa ndani tumbo la samaki mkubwa,alimkumbuka

Mungu,na akakumbu upumbavu wake wa kujaribu kukimbia ili asifanye kazi ya

Mungu.Aliomba na Mungu akamsamehe, akaahidi kuwa atafanya kama Mungu

alivyomwagiza.Kwa hiyo Yoona akajinyenyekeza na akatumbu kwa kutokutii agizo la Mungu.

“BWANA akasema na yule samaki, naye kmtapika Yona pwani” (Yona 2:10).

Ndipo neno la BWANA likamjia Yona mara ya pili, akiagizwa aondoke akarihubiri neno la

Mungu kule Ninawi. Ulikuwa ni mji mkubwa sana, yapata kama km 80 mzunguko wake. Ikawa

Yona alipoingia katika mji alianza kupaza sauti yake ili kila mmoja asikie, “Baada ya siku

arobaini Ninawi utaangamizwa” (mstari 3:4)

Watu wa Ninawi wakaogopa sana hiyo hukumu ambayo Yona alikuwa anaitangaza nao

“wakamwamini Mungu”

Na ikawa Mfalme aliposikia habari hii akaondoka katika kiti cha enzi akavua mavazi yake

ya kifalme akavaa magunia na akakaa katika majivu, hii ikiwa ni ishara ya huzuni na

kutubu.Na watu wote kuanzia aliyekuwa mdogo mpaka aliyekuwa mkuu, wakafanya hivyo

hivyo.Mfalme akatangaza kuwa kila mtu asile chakula na “wakamlilie Mungu kwa nguvu”

na wageuke, wakaache njia zao mbaya.Mfalme wa Ninawi akasema, “Ni nani ajuaye

kwamba Mungu hatageuka na kughairi, a kuiacha hasira yake kali, ili tusiangamizwe?”

(mstari 9)

Mungu alipoona jinsi walivyotubu na kugeuka kuziacha njia zao mbaya, kwa kweli Mungu

aliwaonyesha rehema na hakuwaangamiza.

FUNDISHO KWETU

Habari hiiinazungumzia sana kuhusu kutubu.Mungu aliwataka watu wa Ninawi watubu

kwa ajili ya njia zao mbaya au Mungu awaangamize.