46:1-51:64 UJUMBE KWA MATAIFA YA KIGENI
46:1-51:64 UJUMBE KWA MATAIFA YA KIGENI
46:1-51:64 UJUMBE KWA MATAIFA YA KIGENI
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
46:1-51:64 UJUMBE KWA MATAIFA YA KIGENI

Ingawa huduma kubwa ya Yeremia ilihusu Yuda, pia aliitwa ili atangaze ujumbe wa Mungu kwa mataifa ya jirani

(taz.l:5,10). Sehemu hii ya kitabu chake ina mkusanyo wa ujumbe ambao nabii aliutangaza kwa mataifa ya jirani katika

muda wa miaka mingi ya huduma yake, (taz.25:13). Katika matangazo hayo nabii anaonyesha kwamba, kama vile

Mungu alivyoshughulika na Yuda katika haki yake, ndivyo anavyoshughulika na mataifa ya jirani ya Yuda katika haki

yake.

Utaratibu wa matangazo hayo haufuati mfululizo wa matukio yaliyosababisha ujumbe wake. Utaratibu wake zaidi

unafuata jiografia ya nchi zilizohusika, ukianza Misri kusini na kuendelea kaskazini na mashariki kuelekea

Mesopotamia. Kilele cha mfululizo wa matangazo kinahusu taifa lililotawala mambo ya nchi nyingi zaidi ya maeneo

yale, yaani Babeli. (Kuhusu mataifa yanayotajwa hapa, taz. ramani iliyopangwa katika Isaya 13-23, ambapo matangazo

mengine kwa mataifa mbalimbali yameandikwa.)

Ujumbe kuhusu Misri (46:1-12)

Wamisri walishindwa na Wababeli mara ya kwanza katika mwaka wa 605 k.K. huko Karkemishi. Vita vile

vilikuwa chanzo cha kumalizika kwa utawala mkuu wa Wamisri katika maeneo yale, navyo viliwaweka Wayuda chini

ya mamlaka ya Wababeli mara ya kwanza (46:1-2). Yeremia anatoa mfano wa askari wa Misri wakijiandaa kwa vita (3-

4). Wanaondoka kwa matumaini makubwa ya ushindi, lakini wanashtushwa na ukali wa mashambulio ya Wababeli.

Wamisri wanageuka na kukimbia, lakini wanakatishwa njia katika Mto Frati (5-6).

Katika mfano mwingine wa vita vile, nabii anaona majeshi ya Misri, yakiongezewa nguvu na askari hodari wa nchi

nyingine, wakisonga mbele kama maji ya Mto Nile wakati wa kujaa na kufurika. Hivyo askari hao wanajiona kuwa na

nguvu kiasi kwamba wangeweza kushinda dunia yote (7-9). Lakini siku hiyo siyo siku ya ushindi wa Wamisri. Ni siku

ya hukumu ya Mungu, na Wamisri wanapata machinjo makali sana (10). Utaalamu wote wa Wamisri wa kutumia dawa

hautaweza kuponya majeraha yao. Habari za kushindwa kwa Wamisri zitavuma mbali kabisa (11-12).

Ujumbe wa pili kuhusu Misri (46:13-28)

Wakati huo Yeremia anatabiri ushindi mwingine wa Wababeli juu ya Wamisri, lakini ushindi huo hautokei katika

nchi ya kigeni, bali katika nchi ya Misri yenyewe (13). Kadiri majeshi ya Babeli yanavyozidi kusonga mbele ndivyo

miji ya Misri inavyoanguka. Miungu ya Misri haiwezi kuwazuia maadui. Askari waliokodiwa wanatoroka kutoka

uwanja wa vita, wakitafuta usalama katika nchi zao wenyewe (14-16). Farao anashtakiwa kuwa mtu wa kujisifu kwa

maneno mengi ya bure, lakini hawezi kufanya lo lote wakati matendo yanapotakiwa (17).

Wababeli hukaa juu ya Misri kwa mfano wa mnara, sawa sawa na Mlima Tabori unavyokaa juu ya nchi ya jirani

yake, na kama Mlima Karmeli unavyokaa juu ya bahari iliyo karibu nao. Wamizri hawawezi kuwapindua Wababeli,

kwa hiyo wajiandae kwa kifungo (18-19). Kama vile wanyama wa kufuga wanavyokimbia baada ya kuumwa na ndege

mkali aumaye (kipanga), ndivyo Wamisri wanavyowakimbia Wababeli wanaowashambulia (20-21). Kwa kutumia

mfano mwingine, Wamisri huwa kama nyoka anayekimbia na kujificha katika pango lake, akitafuta usalama wake. Na

kwa mfano mwingine tena, Wababeli katika mashambulio yao dhidi ya Wamisri huwa kama wakataji wa kuni

wanaokata msitu mzima (22-24).

Ingawa Wamisri pamoja na miungu yao wanaadhibiwa, hawataangamizwa kabisa. Siku moja watainuka tena (25-

26). Kuhusu watu wa Yuda na Israeli, ingawa wamepelekwa kifungoni katika nchi za kigeni, siku moja watarudi tena

katika nchi yao ambapo watafurahia amani na usalama (27-28).

Ujumbe kuhusu Wafilisti (47:1-7) Nabii anaona kwamba Wababeli watateka nchi ya Wafilisti pia, wakipita juu ya

nchi kama mto unaofurika na maji yake yanaenea katika mashamba yote (47:1-2). Farasi wa Wababeli pamoja na

magari yao ya vita yatakaposhuka kutoka kaskazini, Wafilisti watakimbia kwa hofu kuu, kila mtu akiangalia usalama

wake mwenyewe. Hakuna atakayejali shida ya mwenziwe. Msaada wo wote ambao labda ungeweza kutoka Tiro au

Sidoni utakatishwa, na miji ya Ufilisti itaomboleza juu ya kuangamizwa kwake (3-5).

Yeremia anawaona Wafilisti wakimlilia Mungu na kumsihi akomeshe mauaji ya Wababeli. Kisha nabii anajibu kwa

niaba ya Mungu, akisisitiza kwamba hukumu ya Mungu lazima iendelee mpaka imalizike kabisa (6-7).

Ujumbe kuhusu Moabu (48:1-47)

Moabu lilikuwa taifa mojawapo lililojaribu kufanya mwungano wa kijeshi na Yuda dhidi ya Wababeli (taz.27:l-3).

Wakati huo taifa hilo litateswa kwa hasira ya Wababeli. Yeremia anaonyesha mfano wa matukio yake: nchi

imechafuliwa, ngome zimebomolewa, miji imeharibiwa, na wakimbizi kwa shida kubwa wanakimbia mbele ya majeshi

yanayoingia (48:1-6).

Kemoshi, mungu wa kitaifa wa Wamoabi hataweza kuokoa taifa lake. Kwa kweli, atachukuliwa kifungoni pamoja

na viongozi wa dini na wa kiraia wa Moabu. Miji ya Wamoabi itaachwa mahame na ukiwa (7-9). Kwa kuangamiza

Moabu, Wababeli wanatimiza kazi ya hukumu ya Mungu, kwa hiyo hawana budi kutimiza kazi hiyo sawa sawa (10).
Kwa kuwa hapo awali Wamoabi hawakuchukuliwa kifungoni, wanafananishwa na divai iliyoweza kukaa katika

chombo chake tangu mwanzo bila kukorogwa. Lakini wakati huo, kwa kuwa watachukuliwa kifungoni Babeli,

wanafananishwa na divai inayomiminwa kutoka chombo chake (11-12). Watu watapotewa na matumaini yao katika

mungu wao wa kitaifa aliyeonekana kuwa hana uwezo wa kuwaokoa (13). Askari mashujaa wa Moabu watauawa

katika mauaji ya kutisha sana, na maombolezo makubwa yatakuwepo juu ya taifa lililopondwa na kuangamia (14-17).

Watu wa sehemu zote za Moabu watashtuka wakisikia habari za kuangamia kwa majeshi yao. Taifa lililojivuna

kwa kiburi chake litaaibishwa (18-20), na taifa lenye nguvu sana litapondwa, hukumu ya Mungu inapoenea kutoka mji

mmoja wa Moabu hadi mwingine (21-25).

Watu wale wa Moabu ambao awali waliwadharau na kuwadhihaki Waisraeli na Wayuda, wakati huo wenyewe

wataaibishwa na kudhihakiwa. Watakunywa ghadhabu ya Mungu mpaka watakapolewa na kutapika (26-27). Wamoabi

waliokuwa na kiburi na kuwadharau watu wengine, wakati huo watalazimishwa kukimbia katika aibu na kutafuta

maficho katika mapango na mashimo milimani (28-30). Lakini sasa Yeremia anawaonea huruma anapoona mamlaka

yao yaliyoenea sana yamevunjwa, mavuno yao mashambani na mizabibu vimeharibiwa, na nchi yao yote imechafuliwa

(31-36). Watu hujinyoa nywele na ndevu zao wakijikata kata na kuvaa nguo za magunia kama alama ya maombolezo,

lakini wamechelewa. Taifa la Moabu limekwisha. Limefanana na chombo kilichovunjika na kutupwa jalalani (37-39).

Katika maelezo ya mwisho ya maangamizi, nabii anatoa mfano wa Wababeli wanaoshuka juu ya Moabu kama vile

tai anavyoshuka juu ya mateka yake. Hakuna atakayeweza kutoroka (40-43). Mahali po pote wanapojaribu kukimbilia

hakuna usalama kwa watu wanaoadhibiwa na Mungu (44). Miji ya maana katika Moabu itateketezwa kwa moto na

wenyeji wake watachukuliwa kifungoni (45-46; taz.Hes 21:28-29). Lakini Mungu kwa neema yake, hata katika Moabu

atawahifadhi watu wachache watakaosalia (47).

Ujumbe kuhusu Amoni (49:1-6)

Kama vile taifa la udugu wake Moabu, Amoni lilikuwa jamaa wa mbali wa taifa la Yuda. (Moabu na Amoni

walikuwa wana wa Lutu, na Wayuda walitokana na baba mkubwa wa Lutu, Ibrahimu; taz.Mwa 12:5; 19:36-38.)

Waamoni na Wamoabi waliishi katika sehemu za nyanda za nchi ya mashariki ya Yordani. Maana yake ni kwamba,

walikuwa majirani kabisa wa Yuda na Israeli upande wa mashariki.

Karne moja hivi kabla ya wakati wa Yeremia, Waashuri walikuwa wameteka ufalme wa kaskazini wa Israeli na

kuwapeleka watu wake kifungoni (2Fal 15:29; 17:6). Inavyoonekana, Waamoni, wakati ule walichukua nafasi ya

kujitwalia eneo la kabila la Gadi, yaani kabila la Israeli lililoishi mpakani. Lakini Waamoni walisahau kwamba

Waisraeli bado waliendelea kuwa watu wa Mungu. Yeremia anawaambia Waamoni kwamba nchi yao itatekwa na mji

wake mkuu, Raba, utabomolewa. Wakati huo Waisraeli watatwaa upya nchi yao wenyewe (49:1-2. Malkamu (au

Moleki) alikuwa mungu wa kitaifa wa Amoni).

Waamoni walijivunia utajiri waliojipatia, na hivyo walifikiri wako salama wala hawawezi kushambuliwa. Yeremia

anawaambia kwamba utajiri wa mali hauwezi kuwaokoa maadui wanaposhambulia. Watapelekwa kifungoni (3-5),

ingawa baada ya muda watu wachache watakaosalia watarudi tena (6).

Ujumbe kuhusu Edomu (49:7-22)

Waedomu, ambao ni wazao wa Esau, walijivuna kwamba wao walikuwa werevu kuliko mataifa ya jirani zao.

Walitumaini kwamba nchi yao ilikuwa salama wala haikuweza kutekwa, kwa sababu milima mirefu ya mipakani

mwake ilitoa nafasi nzuri sanaya kujitetea. Nabii anawaambia kwamba, si hekima wala silaha na nguvu ya kujitetea

vitaweza kuwaokoa na maafa na maangamizi ambayo Mungu aliwapangia (7-8).

Mkulima wa mizabibu huchuma zabibu zilizoiva na kuziacha zisizoiva bado; mwizi avunjaye nyumba huiba vitu

vile tu anavyovitaka na kuviacha vingine katika nyumba, lakini uharibifu wa maadui juu ya Edomu utakuwa kamili.

Hata watu wale watakaojificha katika mapango ya milimani hawataepukana na maafa hayo (9-10). Lakini Mungu

atawaangalia wale watakaokuwa yatima au wajane kutokana na vita vile (11).

Iwapo watu wasiostahili sana ghadhabu ya Mungu wanapaswa kuvumilia adhabu yake, sembuse watu waovu kama

Waedomu. Wataadhibiwa vikali zaidi. Mungu anawahakikishia kwamba miji yao iliyoendelea na kujivuna juu yake,

itaachwa magofu na kuwa mahali pa kutisha (12-13).

Waedomu walijidanganya walipofikiri kwamba, kwa sababu ya ngome zao za kujitetea walizoziweka sehemu

nyingi milimani hawakuweza kushindwa na maadui. Yeremia anawaonya kwamba, haidhum wamekwea milima mirefu

mpaka juu au walijenga ngome imara sana, hakuna kitu kitakachowaokoa na hukumu ijayo (14-16).

Kuangamizwa kwao kutakuwa moja kwa moja. Kama vile Sodoma na Gomora, Edomu itaachwa ukiwa (17-18).

Kama vile simba atokavyo msituni na kushambulia kundi la kondoo, ndivyo maadui watakavyokuja na kuangamiza

Edomu. Hakuna atakayeweza kujitetea dhidi ya jeshi ambalo Mungu atalichagua ili litekeleze hukumu yake (19-20).

Askari wa Edomu hawatakuwa na nguvu dhidi ya washambulizi. Kilio cha Waedomu kitasikika mbali sana kupita
mipaka yao (21-22).

Ujumbe kuhusu Dameski (49:23-27)

Dameski ilikuwa jiji kuu la nchi ambayo hapo kale ilijulikana kuwa Aramu, na baadaye ilijulikana kuwa Shamu au

Siria. Jiji hilo lilitekwa na Waashuri mwaka wa 612 k.K. (2Fal 16:9), lakini Yeremia alipoanza huduma yake, Dameski

bado ilikaliwa na Waashuri hao, ikiwa makao makuu ya mkoa katika ufalme wao. Wakati huo Yeremia anatabiri

kutekwa kwa nchi ya Shamu (Siria) tena, kwa sababu Wababeli walikuwa tayari kuwashinda Waashuri.

Bila shaka unabii huo ulitolewa wakati wa mwanzo wa huduma ya Yeremia, kwa sababu huduma yake ilianza

mwaka wa 627 k.K., na Wababeli waliwashinda Waashuri baada ya miaka 15 tu, yaani mwaka wa 612 k.K. Yeremia

anawaona Washami wakijaa hofu katika hali yao ya kutoweza kujitetea, wakisikia majeshi ya Wababeli yanakaribia

(23-24). Dameski itakuwa uwanja wa majinjio na uharibifu tena, majeshi ya Wababeli yatakapotekajiji hilo (25-27).

Ujumbe kuhusu Kedari (49:28-33)

Hata makabila ya jangwani yanayohama hama kila wakati yatapata taabu kutokana na mashambulio ya Wababeli.

Kabila linalotajwa na Yeremia ni Wakedari walioishi katika eneo liitwalo Hazori. Wakedari waliishi katika mahema,

walifuga kondoo nao walikuwa wafanya biashara hodari (Zab 120:5; Isa 60:7; Eze 27:21). Yeremia anatabiri kwamba

makao yao yatachafuliwa, wanyama wao watachukuliwa, na wao wenyewe watakimbia kwa hofu (28-30).

Lakini maafa hayo pia ni hukumu ya Mungu juu ya makabila hayo ya jangwani. Desturi yao ilikuwa kuiba katika

miji iliyoshambuliwa na Wababeli, kisha kukimbilia makao yao ambapo walikuwa mbali na njia za mashambulio ya

Wababeli. Usalama wao waliodhania kuwa nao wakati huo unafikishwa mwisho wake, na mali yao ya wizi itapotea

(31-33).

Ujumbe kuhusu Elamu (49:34-39)

Ujumbe kuhusu ufalme wa kale wa Elamu ulikuja katika mwanzo wa enzi ya Sedekia, yeye Sedekia alipojaribu

kuunda mwungano wa kijeshi na mataifa mengine magharibi ya Babeli, kwa makusudi ya kuzuia kuenea kwa mamlaka

ya Babeli (34; taz.27: 1-3,12).

Ujumbe wa Yeremia hapa unaonyesha kwamba Sedekia alipoteza wakati wake bure. Mamlaka ya Wababeli

yangeenea mbali sana, hata nchi zilizo upande wa mashariki ya Babeli, kama vile Elamu, zingepinduliwa (35-38).

Lakini kupinduliwa kwa Elamu kusingekuwa kwa muda wote (39). Ripoti za historia zinatueleza kwamba baadaye nchi

ya Elamu ilikuwa sehemu ya ufalme wa Uajemi ambao ulipindua Babeli (Ezra 1:2).

Ujumbe kuhusu Babeli (50:1-46)

Hatimaye Yeremia anaona kwamba taifa lile ambalo Mungu alilitumia kwa kuadhibu taifa la Yuda litaadhibiwa

vile vile. Beli au Merodaki, mungu mkuu wa Wababeli, hataweza kuwaokoa watu wake na mashambulio yatakapokuja

juu yao (50:1-3).

Wayahudi ambao wakati huo watakuwa wamejinyenyekeza katika toba mbele ya Mungu, kwa sababu ya kuanguka

kwa Babeli watapewa nafasi ya kurudi katika nchi yao (4-5).(Koreshi wa Uajemi aliposhinda na kupindua Babeli

mwaka wa 539 k.K., mara moja aliwapa Wayuda ruhusa kurudi katika nchi yao; taz.2Nya 36:22-23.)

Viongozi wa Yuda walikuwa na hatia, kwa sababu walipoteza taifa lao katika njia mbaya (6), lakini Wababeli pia

walikuwa na hatia (ingawa walikanusha jambo hili), kwa sababu wao waliwatendea Wayuda kadiri ya mapenzi yao

wenyewe (7). Kwa hiyo, wakati Wayahudi watakaporudi kutoka Babeli (kwa kweli, watakuwa taifa la kwanza kati ya

yale yaliyopelekwa kifungoni litakalopata uhuru), Babeli yenyewe itaadhibiwa (8-10).

Wababeli walijivuna katika kiburi chao kwamba walishinda na kuteka nyara taifa la YAHWEH, yaani Yuda (11).

Wakati huo wataadhibiwa, ghadhabu ya Mungu itakapomiminwa juu yao (12-13). Washambulizi wake watakuwa

wakali sana kwao, kama vile wao walivyokuwa kwa watu wengine. Baada ya kushindwa kwao, watu wote walio

wafungwa wao, watatoroka kwenda katika nchi zao (14-16).

Ufalme wa kaskazini, yaani Israeli, ulitekwa na Waashuri, halafu Uashuru ulitekwa na Wababeli, na hivyo watu wa

Israeli sawa sawa na wale wa Yuda, hatimaye walikuwa chini ya mamlaka ya Babeli. Lakini wakati huo Babeli

itaanguka, na Waisraeli sawa sawa na Wayuda watarudi katika nchi yao, wakiwa watu waliounganika tena na

kusamehewa dhambi zao (17-20).

Nabii akiendelea kuonyesha mfano wa kuanguka kwa Babeli, anawaona washambulizi wake wakihimizwa wasonge

mbele na kushambulia miji mbalimbali ya Babeli (21-22). Taifa lile ambalo kama nyundo lilivunja mataifa mengine,

wakati huo litavunjwa lenyewe. Ghala zake za chakula zitavunjwa, na askari wake watauawa (23-27). Wafungwa wa

Yuda wakati huo watafunguliwa, nao watarudi nyumbani kwao wakimsifu Mungu kwa kuwakomboa watu wake na

kuwaadhibu kwa haki wanyanyasaji wao (28), lakini Wababeli wenye kiburi wataachwa bila mtu wa kuwasaidia (29-

32). Mungu anawaokoa wanaonyanyaswa, lakini anawaadhibu wale wanaowanyanyasa (33-34).
Haidhuru watawala wa Babeli walikuwa na hekima gani, wachawi wao walikuwa wajanja kiasi gani au askari wao

walikuwa hodari na wenye nguvu gani, wote pamoja watauawa. Majeshi yao ya magari yataangamizwa, na hazina zao

zitatekwa nyara (35-37). Kwa njia ya ukame na vita, nchi yote itaharibika na kuachwa katika hali mbaya, hata watu

wasiweze kuishi huko tena (38-40).

Nabii anaonyesha mfano wa hofu ya mfalme wa Babeli anaposikia habari za ushindi wa haraka wa Waajemi na

majeshi ya mwungano wake yakikaribia kwa kasi (41-43). Mungu akichukua hatua dhidi ya Wababeli, hayatakuwepo

matumaini ya kukimbia. Wababeli wanafananishwa na kundi la kondoo linaloshambuliwa na simba. Kwa hofu kubwa

watapiga yowe wanapofikia mwisho wao wa uchungu na ukatili (44-46).

Kupinduliwa kwa Babeli (51:1-58)

Baada ya kuvuna ngano yake, mkulima anapepeta nafaka zake kwa njia ya kuitupa juu, ili upepo upeperushe

makapi yake, na hivyo anaweza kupata ngano safi. Hali kadhalika Mungu atakapopepeta Babeli, yaani atabagua kati ya

watu wake na watu wa Babeli. Atapeperusha Wababeli katika hukumu yake, lakini atawahifadhi watu wake kwa ajili

yake mwenyewe (51:1-5).

Mungu aliwatumia Wababeli ili kuadhibu mataifa mengine, lakini wakati huo wao wenyewe watakunywa

ghadhabu ya Mungu. Watafanana na mlevi aangukaye asiweze kuinuka tena, na mtu aliyejeruhiwa asiweze kupona.

Wakati huo mataifa yaliyoteswa na kupelekwa kifungoni na Wababeli yatapewa uhuru wao, yaani wafungwa wote

wataweza kurudi nyumbani kwao (6-9). Mungu atahakikisha kwamba hukumu ya mwisho itatekelezwa (10).

Kisha nabii anatoa mfano wa jeshi la Wamedi na Waajemi yakijiandaa kwa mashambulio ya mwisho dhidi ya

Babeli. Anawaonya Wababeli kwamba mwisho wao unakaribia, na baada ya muda mfupi jiji lao litajaa askari wa

maadui (11-14). Miungu yote ya Babeli haitakuwa na uwezo wa kuokoa. Miungu hiyo haina uhai, haina maana wala

haifai. Kuna Mungu mmoja tu wa kweli, naye ndiye aliyeumba na kutawala ulimwengu (15-18). Mungu huyo alichagua

taifa la Israeli, yaani wazao wa Yakobo kuwa watu wake (19). Yeye anatawala historia ya mataifa, akitumia taifa moja

kwa kuadhibu lingine kwa kadiri ya makusudi yake (20-23).

Babeli itaadhibiwa kwa sababu ya jinsi ilivyofanya ukatili kwa Wayuda (24). Inaonekana kuwa imara na isiyoweza

kushindwa kama mlima mkubwa, lakini Mungu ataiponda kuwa vipande vipande, itakuwa mahali pa ukiwa wala

haitajengwa tena (25-26). Nabii anatoa mfano mwingine jinsi majeshi ya mataifa mbalimbali yanavyounganika ili

yapigane vita na Babeli (27-29). Huko Babeli watu wanahangaika wakati ngome zao zinapotekwa, na habari za

kushindwa kwa majeshi yao zinapopelekwa kwa mfalme kwamba majeshi yake yamepata hasara kubwa. Yanapondwa

kama vile nafaka zinavyokanyagwa katika uwanja wa kuzipiga piga (30-33).

Itikio la kupinduliwa kwa Babeli (51:34-58)

Nabii anakumbuka maombi mengi ya watu wa Yuda ambao mara nyingi walilalamikia juu ya tamaa na ukatili wa

Wababeli usiokuwa na mwisho. Walimsihi Mungu ashughulike na taifa hilo kwa sababu ya ukatili waliotendewa, na

wakati huo Mungu yuko tayari kujibu maombi yao (34-35).

Mungu atatekeleza mambo mazuri kwa watu wake naye ataadhibu Babeli kwa njia ya kuiangamiza. Taifa litatekwa

nyara na jiji lao litaachwa kuwa fungu la kifusi (36-37). Wababeli walioua kondoo kama simba, wakati huo

watachinjwa wenyewe kama kondoo (36-40). Jiji lao lililokuwa na mamlaka na kiburi (ambalo pia liliitwa Sheshaki),

pamoja na mungu wake, Beli, litashindwa na kuaibishwa. Askari wa maadui wataingia jijini kama maji ya bahari

yanapofurika, na hivyo mamlaka yake juu ya mataifa yaliyofungwa yanavunjwa (41-44).

Yeremia anawaonya watu wa Mungu wasisitesite wala wasitie mashaka kwa sababu ya mivumo ya matatizo

mbalimbali huko Babeli. Wawe tayari kukimbia nafasi inapopatikana (45-46). Babeli lazima iangamizwe kwa sababu

ya dhambi zake nyingi, na hasa dhambi yake dhidi ya watu wa Mungu. Mtawala mwenye kiburi ataaibishwa, na mataifa

ya kila mahali yatafurahi (47-49).

Wakitazamia mambo hayo yatakayotokea, wafungwa kutoka Yuda wanapaswa kuacha ulalamishi wao wa siku zote

kwamba wameaibishwa, na hekalu la Mungu limetukanwa na kudharauliwa na majeshi ya Babeli. Wakati umewadia

ambapo watu waanze kufikiri sana kuhusu kurudi Yerusalemu, kwa sababu mwisho wa Babeli unakaribia (50-53).

Mungu wa Israeli (YAHWEH) ndiye aliyeamua uharibifu wa Babeli. Yeye ndiye Mungu mwenye mamlaka yote na

mfalme wa pekee. Kazi yake ya hukumu italeta uharibifu juu ya jiji na mauti juu ya wenye mamlaka wote wa taifa (54-

57). Hata kuta imara sana za jiji hazitaweza kuwazuia maadui ambao Yeye atawatuma ili washambulie jiji hilo (58).

Yeremia atuma ujumbe wake Babeli (51:59-64)

Baada ya kuandika maelezo hayo ya kuanguka kwa Babeli, Yeremia alituma ujumbe wake Babeli kwa mkono wa

Seraya, ili ausome kwa wafungwa walioishi huko. (Seraya alikuwa ndugu yake Baruku, na inavyoonekana alikuwa

afisa wa mahakama; ling.mst.59 na 32:12). Wakati huo Seraya alifuatana na mfalme Sedekia aliyetembelea Babeli

katika mwaka wa nne wa utawala wake (59-62).
Baada ya kuwasomea wafungwa mane no ya Yeremia, Seraya afungie jiwe katika gombo lake na kulitupa katika

Mto Frati, ambao kando yake jiji la Babeli lilijengwa. Jambo hilo lilikuwa mfano kwamba jiji hilo lingezama wala

lisingeinuka tena kamwe (63-64).