24.04.2017 Views

Issue 1

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

7

11

Hakukata tamaa akaingia tena

studio nakutoka na kitu ambacho

kilikuwa kinajulikana kwa jina la

‘Kibarua’ ambao alirekodia katika

studio za master j wimbo huo

uliweza kumtambulisha katika

anga za muziki wa kizazi kipya.

Baada ya kuona mafanikio yana -

karibia akaingia tena studio na

kutoka na wimbo ambao uliju -

likana kwa jina la ‘mapepe’

ambao aliufanyia katika studio za

Mambo Jambo.

Hapo ndipo ndoto zake zikaanza

kukamilika akawa anafanya

nyimbo katika studio mbalimbali

akazidi kusimama bila kusita

akaamua kutoa wimbo mwingine

uliojulikana kama ‘Hoi’.

Hoi ndio hasa ulioanza kum -

nyanyua kwani ulipata muda

mkubwa katika vituo vya redio

jambo lililomfanya arejee studio

na kuachia Zaidi Yako.

“Niliamua kuachia nyimbo mfu -

lulizo kwa sababu nina mashairi

ya kutosha kwa hiyo sioni kama

nikiachia hivyo nitaishiwa misitari

na ndio maana nikawa ninaachia

bila hesabu,” anajigamba.

Na huo ndio ukawa mwanzo wa

kujulikana kwa jina la Chidi Ben -

zino kabla kubalidilisha.

“Kipindi cha nyuma nilikuwa

shabiki na mwanachama wa The

Source Magazine ambalo linami -

likiwa na rapa Benzino wa

Marekani ilikuwa kila mwezi

lazima nitumiwe magazine kuto -

kana na kupenda kusoma hilo

jarida.

“Mshikaji wangu wa karibu na

ambaye tulikuwa tunaishi naye

Ilala, Dully Sykes akawa ananiita

Benzino baadhi ya washikaji nao

wakaanza kuniita hivyo jina

likakua baada ya kuona

limezoeleka sana na isitoshe jina

lenyewe siyo langu nikaamua

kulitohoa jina langu la Rashid

nalifupisha likawa Chidi, sikue -

nda mbali sana kwa kuhofia

kupoteza maana ya Benzino na

kutohoa na kuform Benz ukijum -

lisha unapata jina kamili ambalo

lina leta maana Chidi Benz hiyo

ndio historia ya jina langu la kisa -

nii,” anasema.

Mkali huyu wa hip hop ame -

onekana aking’ara sana katika

vituo vya redio mbalimbali hapa

nchini kiasi kwamba unaweza

kusikia sauti yake kila baada ya

dakika mbili katika kituo kimoja

kwa siku moja.

Katika chati ambazo zina

endeshwa katika vituo mbalim -

bali vya redio hapa nchini zaidi ya

nyimbo saba ambazo ziko katika

chati ya juu utakuta zina sauti ya

mwana hip hop huyu kitu amba -

cho hakijawahi kutokea katika

muziki wetu wa kizazi kipya

Ngoma zinazotamba ambazo

ameshilikishwa chidi benz ni

kama ‘Ombi langu’wa msanii

chipukizi anayetoka katika kundi

la Tip Top Conection anayeju -

likana kwa jina la Spark, ‘NEILA

wa msanii Tunda man ‘Bado

umenuna’ wa Marlaw, ‘Hao’ wa

mwanamuziki kutoka katika

nyumba ya vipaji Tanzania House

of Talent (THT) anayejulikana

kama Mwasiti ‘Mchizi wangu

remix ‘ wa kundi la Nako2Nako

na ‘Hapo vipi remix ‘ wa Profesa

Jay, Vidole vitatu wa Taarsis

Masela wa Akudo Impact.

“Ukaribu na utundu pamoja na

umahiri wa kuchezea sauti

yangu ndio vinavyo nipa nafasi

ya kushirikishwa kwenye nyimbo

nyingi. Vile vile mi ni mkali,”

anasema.

Mbali na kutamba na nyimbo

alizoshirikishwa vilevile nyimbo

za Chid ambazo zinafanya vizuri

ni pamoja na ‘Hasira za nini’,

‘Mmenisoma’ pamoja na ‘Naitwa

nani’ aliomshirikisha mwana

dada K-Lynn.

Tofauti na wasanii wengi ambao

kwa sasa wamekuwa

wakilalamika kuwa wanalazimika

kuhonga katika vituo vya redio

Chid anasema kwake hapana.

“Tangu naanza muziki sijawahi

kulipa katika studio wala

sijawahi kuhonga katika redio

yoyote hapa nchini ilinipigiwe

nyimbo zangu nasintakuja

kuhonga kamwe,” anasema.

Anasema anaamini msanii wa

kweli hawezi kuhonga ili kazi

zake ziweze kupigwa kwenye

redio.

Rapa huyo alifanikiwa kutwaa

tuzo za Killimanjaro Music Award

kwa nafasi ya Msanii bora wa Hip

Hop mwaka 2007.

Kwake anaeleza kuwa tuzo hiyo

imempa moyo wa kusonga

mbele zaidi

“Katika gemu hawawezi wakaku -

penda wote lazima wengine

watakuchukia tu,wengi walifurahi

mimi kupata tuzo, kwa vile

nilikuwa na kiwango cha kupewa

tuzo katika kipindi hicho,” anas -

ema.

Miezi kadhaa iliyopita Chidi

alipeleka Albam yake sokoni

ikiwa na nyimbo 17

“Kama nilionyesha mfano wa

albam yangu kukaa namba ONE

katika chati sokoni kwa majuma

kadhaa lakini bado ninaungana

na mwana hiphop kutoka katika

kundi la Tip Top Conection

aitwaye Madee kwa kusema hip

hop haiuzi Lakini mimi chidi benz

nauza.”

Albamu amefanyia katika studio

mbalimbali za hapa nchini, akiwa

amewashirikisha wasanii K-Lyyn,

Wa2pori, AY, Matonya, Mr Ebo,

Dogo Hamidu, Makamua, Ali

Kiba, Maunda Zorro, Gaza

pamoja na K-Voo kutoka Kenya.

”Nimeamua kufanya hivi iliniweze

kuwateka washabiki wao mfano

mtu akiona nimefanya collabo na

Ali kiba na yeye anampenda so

nilazima anunue albam, kingine

ni kwamba nilikuwa najua

kwamba bongo flava inauza

nikaona nikiwaweka hawa na

mimi nitauza, na kweli nikafan -

ikwa kubamba soko.”

Chidi anasema hiphop haiuzi

kutokana na kutokuwepo na

ushirikiano kati ya wasanii

wenyewe, tamaa ya kutaka

kulipwa fedha nyingi tofauti lakini

kubwa zaidi anasema nyimbo

nyingi hazina ujumbe ambao

mashabiki wanataka kuusikia.

Msanii huyu ambaye alitumbuiza

awali wakati wa onyesho la

msanii 50 Cent anasema hiyo

imesaidia pia kupiga hatua.

“Ni bonge la hatua kwangu kwa

sababu mchizi nilikuwa namuona

tu kwenye luninga, magazetini

pamoja na internet, kikubwa zaidi

ni kuona ujanja anaotumia wakati

anapokuwa stejini pamoja na

kumsikia angesema nini juu ya

muziki wetu.”

15

16

19

20

Event

Marlaw

Jirambe Jirambe

Q-jay

Mwasiti

DJ Fetty

A Mchomvu

2008

Prof Jay Dark Master Ngwasuma

48 Hotspot September Edition 2008

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!