13.05.2014 Views

PANGANI BASIN WATER BOARD - IUCN

PANGANI BASIN WATER BOARD - IUCN

PANGANI BASIN WATER BOARD - IUCN

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

IUCN WATER AND NATURE INITIATIVE

IUCN WATER AND NATURE INITIATIVE

IUCN IUCN WATER WATER AND AND NATURE NATURE INITIATIVE

INITIATIVE

PANGANI BASIN WATER BOARD 1

PANGANI PANGANI BASIN BASIN WATER WATER BOARD BOARD 1 1

PANGANI BASIN WATER BOARD 1

Basin Delineation Report

Basin Delineation Report

PANGANI RIVER BASIN FLOW ASSESSMENT

Basin Delineation Report

Final Report

Bonde La Pangani: Uchambuzi wa Hali Halisi (Toleo la pili)

Bonde J. King, C. Brown, La Pangani: J. Turpie, B. Clark, Uchambuzi A. Duffel-Graham, wa G. Lugomela, Hali Halisi H. Sadiki, (Toleo B. L. Benno, la A.

pili)

PANGANI RIVER BASIN FLOW ASSESSMENT

Hepelwa, L. T Kaaya, D Salum, L. Lukambuzi, E. Materu, Felix Peter, S. Kamugisha, F. Mahay and H.

Beuster

Basin Delineation 2010 Report

2010

January 2008

Final Report

J. King, C. Brown, J. Turpie, B. Clark, A. Duffel-Graham, G. Lugomela, H. Sadiki, B. L. Benno, A.

Hepelwa, L. T Kaaya, D Salum, L. Lukambuzi, E. Materu, Felix Peter, S. Kamugisha, F. Mahay and H.

Beuster

1 As of 2010, 1 As of Pangani 2010, Pangani Basin Basin Water Water Office Office is known is known as as Pangani Pangani Basin Water Board

1 As of 2010, Pangani Basin Water Office is known as Pangani Basin Water Board

January 2008

Coast Development Authority

Bonde la Pangani:

Uchambuzi wa Hali Halisi (Toleo la pili)

Bonde la Pangani:

Uchambuzi wa Hali Halisi (Toleo la pili)

Programu ya IUCN Afrika Mashariki na Kusini

2009

i

Mchapishaji:

Hatimiliki:

© 2009 Shirika la Kimataifa la Uhifadhi ya Uasili na Maliasili.

Kitabu hiki kinaweza kutolewa chote au sehemu yake kwa njia yoyote kwa

matumizi ya maendeleo ya elimu au matumizi mengine yasiyo ya biashara

bila ya kuomba kibali kutoka kwa mmiliki, ilimradi rejeo litajwe. IUCN

ingependelea kupata nakala ya makala yoyote ambayo itatumia kitabu hiki

kama rejea.

Hairuhusiwi kuuza kitabu hiki, au kukitumia kwa madhumuni mengine ya

kibiashara bila ya idhini ya maandishi ya IUCN.

Jina kamili:

Programu ya IUCN Afrika ya Mashariki, 2009. Uchambuzi wa Hali Halisi

Bonde la Mto Pangani. Toleo la pili, xii + uk.83.

ISBN: 978-2-8317-1191-1

Usanifu na Mpangilio:

Mpiga chapa:

Gordon O. Arara

Kulgraphics Ltd.

1

2 3 4

5

Picha ya 1: Kilele cha Mlima Kilimanjaro; Picha ya 2: Sehemu ya msitu wa

Shiri Njoro; Picha ya 3: Banio la kudhibiti maji yanayoingia katika mfereji wa

umwagiliaji; Picha ya 4: Watoto wakiogelea kwenye hodhi ya maji ya umwagiliaji;

Picha ya 5: Shamba la mkonge; Picha ya 6: Mradi wa umwagiliaji wa mpunga

; Picha ya 7: Kituo cha kupimia usawa wa maji- Chemchemi ya Chemka; Picha

ya 8: Banio la mfereji wa umwagiliaji lililoharibiwa; Picha ya 9: Ukuta wa Bwawa

la Nyumba ya Mungu (mabadiliko ya rangi yanaonesha upunguaji wa kina cha

maji); Picha ya 10: Mchuuzi akiuza maji kutoka kwenye kisima.

6

7 8

9 10

Picha namba 1, 3, 5, 6, 8, 9 hatimiliki ya 2003 ya Kelly West; Picha namba

2 na 7 hatimiliki ya 2002 ya Kim Geheb; Picha namba 4 na 10 hatimiliki ya

2003 ya Ger Bergkamp.

Kitabu hiki kinapatikana: Kitengo cha Huduma za Uchapishaji cha IUCN-ESARO, S.L.P. 68200–00200,

Nairobi, Kenya; Simu ++254 20 890605-12 Faksi ++254 20 890615; Barua

pepe; earo@iucn.org

Uteuzi wa Maumbo ya kijiografia na nyenzo zilizotumika kuwasilisha ujumbe katika kitabu hiki,

hayawakilishi kwa namna yoyote ile maoni ya asasi zinazoshiriki kuhusiana na sheria ya nchi yoyote, au

eneo lake, au mamlaka zake, au kuhusu makazi na uwekaji wa mipaka yake.

Maoni yaliyotolewa na waandishi katika kitabu hiki sio lazima kwamba yanawakilisha maoni ya PBWO,

CDA, WANI au IUCN.

ii

Yaliyomo

Tafsiri ya vifupisho............................................................................................................................v

Dibaji.................................................................................................................................................vii

Muhtasari ........................................................................................................................................viii

A

B

C

Utangulizi wa Uchambuzi wa Hali Halisi wa Bonde la Mto Pangani....................................1

A.1 Maelezo ya jumla ya Bonde la Mto Pangani....................................................................1

A.2 Usimamizi wa Pamoja wa Mabonde ya Mito (wa)............................................................5

A.3 Programu ya Hifadhi ya Maji na Uasili (WANI).................................................................6

A.4 Uchambuzi wa Hali Halisi: madhumuni na matokeo.........................................................7

A.5 Vyanzo vya data ..............................................................................................................7

A.6 Muundo wa Uchambuzi wa Hali Halisi..............................................................................8

Rasilimali za asili zilizopo katika Bonde la Mto Pangani.....................................................9

B.1 Utangulizi.............................................................................................................................9

B.2 Misitu iliyopo katika Bonde...................................................................................................9

B.3 Maji na ardhioevu...............................................................................................................15

B.4 Maeneo yaliyohifadhiwa.....................................................................................................19

B.5 Bayoanuwai na Hifadhi......................................................................................................20

B.6 Uvuvi .................................................................................................................................22

B.7 Udongo..............................................................................................................................23

B.8 Majumuisho ya hoja...........................................................................................................23

Uchumi wa kijamii katika Bonde la Mto Pangani................................................................25

C.1 Maelezo ya jumla...............................................................................................................25

C.2 Shughuli za Viwanda.........................................................................................................27

C.3 Shughuli za Kilimo.............................................................................................................27

C.4 Shughuli za Wafugaji.........................................................................................................31

C.5 Shughuli za Mijini...............................................................................................................32

C.6 Shughuli za Asasi Zisizo za Kiserikali na Mashirika ya Kimataifa .....................................32

C.7 Migogoro............................................................................................................................40

C.8 Majumuisho ya hoja ..........................................................................................................46

D Usimamizi wa Maliasili katika Bonde la Mto Pangani ........................................................47

D.1 Utangulizi.........................................................................................................................47

D.2 Usimamizi wa Serikali, Sheria na Sera............................................................................ 47

D.3 Usimamizi katika ngazi ya jamii........................................................................................52

D.4 Usimamizi wa bonde kimataifa.........................................................................................55

D.5 Ukusanyaji na ufuatiliaji wa data.......................................................................................55

D.6 Majumuisho ya hoja..........................................................................................................57

E

Matatizo na masuala mbalimbali katika Bonde la Mto Pangani......................................58

E.1 Utangulizi...........................................................................................................................58

E.2 Masuala na matatizo ya Bonde la Mto Pangani................................................................58

E.3 Maeneo ya kipaumbele kwa Utendaji................................................................................62

F Hitimisho................................................................................................................................64

F.1 Majumuisho ya Matokeo....................................................................................................64

G Rejea .....................................................................................................................................68

H Kiambatanisho cha 1: Mabonde madogo yaliyojumuishwa kiutawala

katika Bonde la Pangani...................................................................................................... 75

H.1 Utangulizi..........................................................................................................................75

iii

H.2 Bonde la Mto Umba..........................................................................................................75

H.3 Bonde la Mto Msangazi....................................................................................................77

H.4 Bonde la Mto Zigi..............................................................................................................78

H.5 Bonde la Mto Mkulumuzi..................................................................................................82

Orodha ya Majedwali

Jedwali la 1: Aina, matumizi na hadhi ya kisheria ya misitu ya Tanzania...........................................9

Jedwali la 2: Upotevu wa utando wa msitu wa Milima ya Tao la Mashariki katika

Bonde la Mto Pangani..................................................................................................13

Jedwali la 3: Makadirio ya mahitaji ya maji kwa mwaka 1995 na matarajio ya

mahitaji ya maji mwaka 2015.......................................................................................18

Jedwali la 4: Misingi ya Uchumi wa kijamii wa Tanzania na Kenya mwaka 2001.............................26

Jedwali la 5 Idadi ya Mifugo katika baadhi ya maeneo ya Bonde la Mto Pangani (2002) ............. 31

Jedwali la 6: Hati za kutumia maji katika Bonde la Mto Pangani (Tanzania), Mei, 2003..................50

Jedwali la 7: Eneo la misitu chini ya Usimamizi wa Misitu wa Pamoja kwa mikoa...........................54

Orodha ya Michoro

Mchoro Na.1: Bonde la mto Pangani lilivyoenea Tanzania na Kenya..................................................2

Mchoro Na 2: Bonde la Mto Pangani ..................................................................................................3

Mchoro Na 3: Utawala wa Misitu Tanzania .......................................................................................51

Mchoro Na 4: Ramani ya Bonde la Pangani- Utawala ......................................................................83

Orodha ya Picha

Picha ya 1: Ramani ya Bonde la Mto Pangani ..................................................................................33

Picha ya 2: Ramani ya Bonde la Pangani kiutawala ........................................................................34

Picha ya 3: Kilele maarufu chenye barafu cha Mlima Kilimanjaro mwaka

1993 na 2000 .................................................................................................................35

Picha ya 4: Mto Karanga - Moshi......................................................................................................36

Picha ya 5: Mlima Kilimanjaro ...........................................................................................................36

Picha ya 6: Mfereji wa umwagiliaji Wilayani Moshi............................................................................37

Picha ya 7: Chemchemi iliyofunikwa ya Shiri-Njoro..........................................................................38

Picha ya 8: Miteremko kwenye misitu ya Mlima Meru.......................................................................38

Orodha ya Visanduku

Kisanduku cha 1: Usimamizi wa Mahitaji ya maji................................................................................6

Kisanduku cha 2: Taarifa za msingi za misitu ya Bonde la Mto Pangani...........................................10

Kisanduku cha 3: Milima ya Taita.......................................................................................................11

Kisanduku cha 4: Tishio kwa misitu ya Bonde la Mto Pangani..........................................................14

Kisanduku cha 5: Taarifa za msingi za maji na ardhioevu katika Bonde la Mto Pangani ..............15

Kisanduku cha 6: Tishio kwa rasilimali za maji na ardhioevu ya Bonde la Mto Pangani ..................16

Kisanduku cha 7: Tishio kwa maeneo yaliyohifadhiwa ya Bonde la Mto Pangani.............................20

Kisanduku cha 8: Maeneo muhimu sana kwa bayoanuwai ..............................................................21

Kisanduku cha 9: Kundi la kwanza la spishi ya ndege wa Milima ya Usambara

walio hatarini.........................................................................................................22

Kisanduku cha 10: Kasoro za usanifu wa miundombinu ya mifereji ya asili .....................................28

Kisanduku cha 11: Magadi na chumvichumvi....................................................................................30

Kisanduku cha 12: Utawala wa Maji nchini Kenya.............................................................................51

Kisanduku cha 13: Uanzishwaji wa usimamizi wa kijamii katika msitu wa Duru-Haitemba,

Mkoani Manyara ............................................................................................53

Kisanduku cha 14: Mfano wa Chama Cha Watumia Maji..................................................................56

iv

Tafsiri ya Vifupisho

ANR....................... Hifadhi ya Asili ya Amani

ASL....................... Juu ya Usawa wa Bahari

AUWSA................. Mamlaka ya Maji safi na na Maji taka Arusha

BWB...................... Bodi ya Maji ya Bonde

BWO..................... Afisa wa Maji wa Bonde

CBNRM................. Usimamizi wa Maliasili Kijamii

CCM...................... Chama Cha Mapinduzi

CDA....................... Mamlaka ya Maendeleo Pwani (Kenya)

CFR....................... Hifadhi ya Misitu ya Jamii

CFP....................... Mradi wa Misitu Eneo la Chanzo cha Mto

CPRs..................... Rasilimali za Jamii

DFO....................... Afisa Misitu wa Wilaya

DGIS..................... Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi

EACBP.................. Mradi wa Bayoanuwai za kimataifa za Afrika Mashariki

EU......................... Umoja wa Nchi za Ulaya

EU-ACP................. Umoja wa Ulaya – Afrika, Caribbean na Pasifiki

FAO....................... Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa

FBD....................... Idara ya Misitu na Nyuki

GEF....................... Mfuko wa huduma ya Mazingira Duniani

GIS........................ Mifumo ya Habari wa Kijiografia

GOK...................... Serikali ya Kenya

Ha......................... Hekta

IRBM..................... Usimamizi wa Pamoja wa Mabonde ya Mito

IDA........................ Chama cha Maendeleo cha Kimataifa

IUCN..................... Shirika la Kimataifa la Hifadhi ya Uasili

JFM....................... Usimamizi wa Pamoja wa Misitu

KWH...................... Kilowati kwa saa

LGA....................... Serikali za Mitaa

LMIS...................... Skimu ya Umwagiliaji ya “Lower Moshi”

MAFS.................... Wizara ya Kilimo na Chakula

MCM...................... Mita za ujazo Milioni

MGR...................... Hifadhi ya Wanyamapori ya Mkomazi

MMP...................... Mradi wa Usimamizi wa Mikoko

MoU....................... Mkataba wa Makubaliano

MoWLD................. Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo

MTESM................. Mkakati wa Taifa Kuendeleza Sekta ya Maji

MW........................ Megawati

NAWAPO.............. Sera ya maji ya Taifa

n.d......................... Hakuna Tarehe

NEMC.................... Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira

v

NGO...................... Shirika Lisilo la Kiserikali

NPF....................... Mradi Mpya wa Maporomoko ya Mto Pangani

NORAD................. Shirika la Kimataifa la Misaada la Norway

NRM...................... Usimamizi wa Maliasili

NWP...................... Sera ya Maji

NyM....................... Bwawa la Nyumba ya Mungu

PA.......................... Maeneo Yaliyohifadhiwa

PBWB................... Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani

PBWO................... Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani

PRB....................... Bonde la Mto Pangani

PRBMP................. Mradi wa Usimamizi wa Bonde la Mto Pangani

RBM...................... Mradi wa Usimamizi wa Matumizi Bora ya Maji

RBMSIIP............... Mradi wa Usimamizi wa Matumizi Bora ya Maji na Uboreshaji wa Kilimo cha

Umwagiliaji cha Wakulima Wadogo wadogo

RCE....................... Kituo cha Kanda cha viumbe vipatikanavyo kipekee

RHO...................... Afisa Haidrolojia wa Mkoa

RNRO.................... Afisa Maliasili wa Mkoa

SA......................... Uchambuzi wa Hali Halisi

SNV....................... Shirika la Maendeleo la Uholanzi

TANAPA................ Mamlaka ya Hifadhi za Taifa

TANESCO............. Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania

TCMP.................... Ubia wa Usimamizi wa Pwani Tanzania

ICZCDP................. Programu ya Hifadhi na Maendeleo ya Ukanda wa Pwani Tanga

TFAP..................... Mpango wa Utekelezaji wa Misitu Tanzania

TFCG.................... Kikundi cha Hifadhi ya Misitu Tanzania

TIP......................... Shirika la Umwagiliaji Kiasili na Maendeleo ya Mazingira

TPC....................... Kampuni ya Kiwanda cha Sukari Moshi (Tanzania)

UNICEF................. Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Dharura kwa Watoto

UNDP.................... Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa

USAID................... Wakala wa Marekani kwa Maendeleo ya Kimataifa

VNRC.................... Kamati ya Maliasili za Kijiji

VWN...................... Dira ya Maji na Uasili

WANI..................... Programu ya Hifadhi ya Maji na Uasili ya IUCN

WDM..................... Usimamizi wa Mahitaji ya Maji

WHO..................... Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa

WRMA................... Mamlaka ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji (Kenya)

WRM Act............... Sheria ya Usimamizi wa Rasilimalui za Maji ya mwaka 2009

WUA...................... Chama Cha Watumiaji Maji

vi

Dibaji

Madhumuni ya toleo la kwanza la Uchambuzi ya Hali ya Bonde la Mto Pangani yalikuwa kuainisha

rasilimali za asili zilizomo katika Bonde hilo, matukio yanayoziathiri na kutambua maeneo ya kufanyia

kazi. Madhumuni mengine yalikuwa kutambua mashirika, asasi na wadau wengine ambao IUCN ingeweza

kushirikiana nao.

Lengo la WANI ni kuhakikisha kwamba suala zima la ikolojia linazingatiwa katika sera, mipango, na

usimamizi wa mabonde ya mito. Katika maeneo ya mabonde ya kufanyia maonyesho yaliyoteuliwa duniani,

WANI imepania: kuonyesha namna ya kusimamia mfumo ikolojia, kuwawezesha wananchi kushiriki katika

usimamizi endelevu wa rasilimali za maji, kuendeleza usimamizi bora wa vyanzo vya maji na ardhioevu,

kuanzisha na kutumia nyenzo za kiuchumi na vivutio, kuongeza maarifa ya kusaidia kufikia maamuzi na

kutoa mafunzo yatakayoleta mwamko wa matumizi bora ya maji.

Kufuatia mashauriano na wadau katika Bonde na kwa kuzingatia maazimio ya warsha iliyoendeshwa na

Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani (PBWO) kwa ushirikiano na IUCN - Shirika la Kimataifa la Kuhifadhi

Uasili iliyofanyika Moshi, Tanzania, kuanzia tarehe 8 hadi 10 Mei, 2002, Bonde la Mto Pangani nchini

Tanzania na Kenya lilichaguliwa kuwa eneo la maonyesho la WANI.

Ikiwa ni sehemu ya shughuli zake za mradi wa maendeleo katika Bonde la Mto Pangani, IUCN ilimwajiri Mshauri

Mtaalamu Dk. Kim Geheb, kufanya Uchambuzi wa Hali halisi ya bonde hili. Kazi za ugani kwa ajili ya uchambuzi

wa hali halisi zilifanyika mwezi Novemba, mwaka 2002, na ilihusisha mahojiano na wadau mbalimbali katika

bonde. Vyanzo vya ziada vya taarifa vilikuwa ni marejeo ya machapisho pamoja na mjadala wa warsha iliyotajwa

hapo juu, iliyojulikana kwa jina la “Bonde la Mto Pangani: Usimamizi Shirikishi”

Madhumuni ya Uchambuzi wa Hali halisi ni kama yafuatayo:-

• Kuainisha rasilimali mbalimbali zilizomo katika Bonde la Mto Pangani , na kufahamu michakato na

matukio yanayoziathiri.

• Kutambua kwa mapana maeneo ya kiutendaji ambayo yanaweza kushughulikiwa kwa manufaa ya

kimaendeleo.

• Kutambua taasisi na asasi mbalimbali zilizopo, na zenye nia ya kujishughulisha na rasilimali za

maji, ambazo IUCN inaweza kuingia nazo ubia kwa lengo la kuendeleza juhudi za WANI katika

Bonde la Mto Pangani.

Kitabu hiki “Uchambuzi wa Hali Halisi ya Bonde la Mto Pangani“ awali kilitafsiriwa na Ofisi ya Maji Bonde la

Pangani. Bw. Ipyana E. Mwakalinga alikamilisha kwa kuboresha baadhi ya sehemu na kuhariri toleo hili la pili kwa

lugha ya Kiswahili.

Rasimu ya kwanza ya Uchambuzi wa Hali Halisi katika Bonde la Mto Pangani ilikamilika mwishoni mwa mwaka 2002

na kusambazwa kwa wadau kwa ajili ya mapitio na maoni. Katika warsha iliyoandaliwa na PBWO na IUCN mjini

Moshi mwezi Machi 2003, wadau walitoa maoni na kupendekeza marekebisho kadhaa. Maoni na mapendekezo

ya ziada yalipokelewa kutoka PBWO na Mamlaka ya Maendeleo ya Pwani (CDA - Kenya) kwenye mkutano wa

IUCN, PBWO na CDA uliofanyika Nairobi mwezi Mei, mwaka 2003. Mwaka 2009 uchapishaji upya wa Uchambuzi

ya Hali ya Bonde ulihitajika na ikaamuliwa kutumia nafasi hii kufanyia mapitio ya taarifa chache ikizingatiwa kuwa

sheria mpya ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji iliyopitishwa July 2009 na inafanya kazi. Ieleweke kuwa taaarifa

zilizofanyiwa mapitio ni zile tu zinazohusu miuondo ya utawala, mifumo ya kitaasisi, sheria na sera za maji, vilevile

taarifa mpya kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi wa Bonde la Pangani zimeongezewa, lakini

maeneo mengine yote ya uchambuzi yameachwa kama yalivyo. Kazi hii yakufanyia mapitio Uchambuzi ya Hali ya

Bonde la Pangani imegharamiwa na Global Water initiative (mpango wa maji wa dunia) unaofadhiliwa na mfuko

wa Howard G. Buffett (Howard G. Buffett Foundation).

Felix Peter, Helen Lema, Fatuma Omar na Renalda Mukaja kutoka Mradi wa Usimamizi wa Matumizi Bora ya

Rasilimali za Maji uliopo chini ya Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo ya Tanzania walijitolea kutayarisha na

kufanya makadirio ya maeneo katika ramani zilizopo katika kitabu hiki.

vii

Muhtasari

Bonde la Mto Pangani lina eneo la takriban kilomita za mraba 43,650, sehemu kubwa ikiwa nchini

Tanzania na karibu asilimia 5 iko katika Jamhuri ya Kenya. Nchini Tanzania, bonde hili limeenea katika

mikoa minne: Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga. Katika Jamhuri ya Kenya eneo la bonde liko

katika Wilaya ya Taita-Taveta. Mto Pangani unaundwa na matawi makubwa mawili , Mto Kikuletwa na

Ruvu ambayo huunganika katika bwawa la Nyumba ya Mungu lenye eneo la kilomita za mraba 140.

Mto unapotoka katika bwawa hili unajulikana kwa jina la Mto Pangani, ambao hutiririka kwa umbali wa

kilomita 432 kabla ya kuingia Bahari ya Hindi.

Bonde hili lina rasilimali nyingi. Bila shaka maji na ardhi inayofaa kwa kilimo ndizo rasilimali muhimu zaidi

kwa wakazi wapatao milioni 3.7 wa bonde hili waishio upande wa Tanzania. Nyanda za juu za bonde

hupata mvua nyingi zaidi ukilinganisha na uwanda wa chini. Hata hivyo kutokana na msongamano na

ushindani wa kupata ardhi ulioko katika nyanda za juu, wakulima wamelazimika kuanza kumwagilia maji

mashamba yao ili kuinua uzalishaji. Wale walioshindwa kupata ardhi katika nyanda za juu wamelazimika

kutafuta maeneo katika uwanda wa chini wenye mvua haba, ambako kilimo cha umwagiliaji ni wa muhimu

sana. Ugumu wa hali unazidishwa zaidi na mwenendo wa upungufu wa mvua katika bonde.

Ushindani wa kupata ardhi umesababisha rasilimali nyingine katika bonde kama vile misitu, kuingia

katika ushindani wa moja kwa moja na kilimo. Sehemu ya misitu inalindwa kutokana na hadhi yake

ya hifadhi, kama vile Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) ambayo ipo chini ya Mamlaka ya

Hifadhi za Taifa (TANAPA). Misitu mingine inalindwa na idara za misitu za Kenya na Tanzania. Kutokana

na sababu mbalimbali, zikiwemo uhaba wa wafanyakazi na ukosefu wa fedha, misitu hii haifaidi viwango

sawa vya hifadhi ikilinganishwa na ile iliyopo chini ya TANAPA. Kuwepo shinikizo kwenye misitu ya

pwani na Milima ya Tao la Mashariki katika bonde la mto Pangani kunatia wasiwasi mkubwa sana, hasa

ikizingatiwa kuwa maeneo hayo yana kiwango cha juu cha mimea na viumbe adimu ndani yake.

Rasilimali nyingine katika bonde ni madini, ambayo ni pamoja na tanzanite, bati na vito. Nyingine ni

uvuvi, maeneo ardhioevu na vivutio vingi vya utalii.

Rasilimali hizi hutumika kwa namna mbali mbali. Uchambuzi huu wa hali halisi unaweka matumizi hayo

katika makundi yafuatayo:

• Shughuli za viwanda, ambazo ni pamoja na mchango mkubwa wa nishati ya umeme wa

nguvu ya maji katika gridi ya taifa, uchimbaji wa madini na viwanda vya kilimo kama vile

kiwanda cha sukari na vya usindikaji wa katani.

• Shughuli za kilimo: Kwa sehemu kubwa kilimo katika bonde hili ni cha asili na hutegemea

umwagiliaji. Mifereji ya umwagiliaji ina ufanisi mdogo sana, inaweza kupoteza kiasi cha

asilimia 85 ya maji kati ya mahali yanapochukuliwa hadi yanapopelekwa. Kadhalika kuna

kilimo cha umwagiliaji cha viwango vikubwa katika bonde, yakiwemo mashamba ya miwa,

mkonge na maua. Kadiri ya hekta kati ya 29,000 na 40,000 humwagiliwa katika bonde la

Pangani upande wa Tanzania. Kiasi cha maji kinachotumiwa kinakadiriwa kuwa kati ya mita

za ujazo milioni 400 na 480 kwa mwaka.

• Shughuli za ufugaji: Idadi kamili ya mifugo iliyopo katika bonde kwa sasa haifahamiki. Inadhaniwa

kuwa, ifikapo mwaka 2015, ufugaji utatumia mita za ujazo 36,400 za maji kwa siku.

• Shughuli za mijini: Bonde lina miji miwili mikubwa, yaani Arusha na Moshi. Kadri miji hii

inavyokua, mahitaji ya maji yameongezeka katika nyanja mbili: kwa matumizi ya viwandani

na nyumbani, na kama njia ya kuondolea maji taka. Inatarajiwa kuwa, ifikapo mwaka 2015,

mahitaji ya maji mijini katika bonde yatafikia mita za ujazo 163,600 kwa siku.

viii

Kutokana na hali hiyo kuna asasi na mashirika mbalimbali katika bonde, ambayo yanaweza kutumia

madaraka ya viwango tofauti katika kumiliki rasilimali zilizoko katika bonde. Tofauti hii ya viwango vya

madaraka ni msingi wa migogoro mingi ya matumizi ya rasilimali hizo. Uchambuzi huu wa hali halisi

unainisha migogoro hiyo kama ifuatavyo:

• Migogoro itokanayo na viwango: Uhusiano kati ya watumiaji wa maji wa ukubwa na uwezo

tofauti katika bonde la Mto Pangani mara nyingi huelezewa katika hali mbili kinzani. Hivyo

mashamba makubwa yatumiayo mamia ya lita za maji kwa sekunde na kutumia mifumo ya

umwagiliaji maji yenye ufanisi wa hali ya juu, hutofautiana sana na watumiaji wadogo ambao

hutumia maji kidogo na mifumo duni ya umwagiliaji yenye ufanisi mdogo. Tofauti hizi kubwa

za matumizi ndiyo vyanzo halisi vya migogoro. Uchambuzi huu wa hali halisi unatoa mifano

ya migogoro ya aina hii kuwa ni maslahi kati ya watumiaji wa mijini na vijijini; na kati ya

wachimbaji madini wa viwango vikubwa na vidogo.

• Migogoro itokanayo na umiliki: Kitabu hiki kinafafanua umiliki kama haki ya kusimamia

rasilimali. Nchini Tanzania, Usimamizi wa Maliasili Kijamii (CBNRM) umeonekana kama njia

ya kuvutia ya kuongeza ufanisi wa Usimamizi wa Maliasili za Taifa (NRM). Mwenendo huu

haufuatwi sana nchini Kenya. Ukinzani katika mifumo hii unahusiana na matumizi na usanifu

wake. Hapa, jamii zinaweza zisishirikishwe katika kubuni mkakati wa usimamizi, utekelezaji

wake au hata mifumo yake ya kisheria. Hali hii inaweza kudhihirisha kuwa taasisi hizi

hazitimizi wajibu wa usimamizi ulioundwa ili ziufanyie kazi. Mifano ni migogoro ya usimamizi

wa misitu kati ya ngazi ya jamii na serikali; baina ya watumiaji rasilimali wa aina mbalimbali;

na migogoro kuhusu nyanja mbali mbali za usimamizi.

• Migogoro itokanayo na mahali: Watumiaji walioko maeneo ya juu ya mito wana nafasi nzuri ya

kutumia maji kuliko walioko sehemu za chini. Kwa kiwango kikubwa matatizo haya yanaweza

kuonekana kwenye mifereji ya umwagiliaji ambako watumiaji walio karibu na chanzo cha

maji wanaweza kuotesha mazao yanayohitaji kiasi kikubwa cha maji (kama vile mpunga) na

wale walioko mwishoni mwa mifereji wakilazimika kupanda mazao yanayohitaji maji kidogo.

Matatizo makubwa yanayoikabili mitambo ya umeme wa maji iliyoko upande wa chini wa mito

ni mfano mwingine. Mifano ya migogoro ya aina hii ni ile iliyopo kati ya watumiaji wa maji wa

maeneo ya juu ya mto na wa maeneo ya chini ya mto, na migogoro kati ya wazalishaji wa

umeme wa maji na wamwagiliaji wadogo wadogo.

Migogoro juu ya rasilimali ni moja ya ushahidi wa ushindani mkubwa uliopo baina ya watumiaji wa

rasilimali zilizoko katika bonde. Athari ya ongezeko la watu, tofauti ya mgawanyo wa rasilimali na hali ya

kuwa na ukomo husababisha mbinu za matumizi yake mara nyingi kuwa mbaya. Mifano ya uharibifu wa

rasilimali ni kama ifuatayo:

• Misitu iliyopo katika bonde inakabiliwa na hatari ya ukataji hovyo wa miti, kuingiliwa ndani

ya mipaka yake kwa mahitaji ya matumizi ya ardhi, uchomaji wa mkaa na ukusanyaji kuni.

Inakisiwa kuwa karibu asilimia 77 ya misitu ya Milima ya Tao la Mashariki imepotea katika

kipindi cha miaka 2,000 iliyopita kutokana na shughuli za binadamu, wakati kilomita za mraba

41 za misitu asilia ya Kilimanjaro zimetoweka kati ya mwaka 1952 na 1982.

• Ugawaji wa maji katika bonde unakabiliwa na tatizo la mahitaji makubwaambapo imedhihirika

kuwa mahitaji ya rasilimali hiyo yanazidi upatikanaji wake. Sababu kuu ya ongezeko la mahitaji

ni mifumo duni ya umwagiliaji kwa njia ya mifereji yenye ufanisi mdogo. Maeneo ya ardhioevu

katika bonde yapo hatarini kutoweka kutokana na ujenzi wa mabwawa.

• Maeneo yaliyohifadhiwa ya bonde yanakabiliwa na ujangili, na matatizo mengine kama yale

yanayoikabili rasilimali ya misitu.

• Sehemu kubwa ya viumbehai katika bonde inatokana na mazingira ya kipekee ya misitu iliyopo.

Tishio la maisha ya viumbehai hutokea kutokana na hatari inayokabili mazingira.

ix

• Uvuvi katika bonde la Mto Pangani unakabiliwa na shinikizo la uvuvi uliokithiri, na ukuaji wa

magugumaji unaosababishwa na shehena kubwa ya virutubisho. Takriban tani 24 za udongo

kwa hekta kutoka eneo la vyanzo vya mito huingia katika bwawa la Nyumba ya Mungu kila

mwaka. Mwaka 1970, tani 28,509 za samaki zilivuliwa kutoka bwawa la Nyumba ya Mungu.

Upatikanaji wa samaki umekuwa ukipungua kwa kiasi kikubwa tokea hapo, na katika mwaka

1983, tani 2,430 za samaki zilipatikana.

Kuna idadi kubwa ya mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali katika bonde hili yanayotaka

kudhibiti uharibifu uliotajwa na kujaribu kuboresha maisha ya watumiaji wa rasilimali. Katika miaka ya

karibuni, shughuli muhimu za kiwango kikubwa ni zile zilizogharamiwa na Benki ya Dunia kupitia Mradi

wa Usimamizi wa Matumizi ya Rasilimali za Maji na Uboreshaji wa Kilimo cha Wamwagiliaji Wadogo

Wadogo (RBMSIIP), na Mradi wa UNDP-GEF wa Viumbe anuwai wa Afrika Mashariki. Mradi wa kwanza

ulikuwa maalum katika kuimarisha Ofisi ya Maji ya bBonde la Pangani (PBWO) na vilevile kuimarisha

uwezo wa usimamizi wa matumizi ya maji katika bonde.

Juhudi za mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) katika bonde hili ni pamoja na kujihusisha na Usimamizi

Shirikishi wa ukanda wa pwani ya Tanzania na misitu yake ya mikoko, na Kaskazini mwa bonde ni

uboreshaji wa umwagiliaji wa kiasili, na uwezeshaji wa njia za mawasiliano baina ya watumiaji wa ngazi

ya chini wa rasilimali na uongozi wa bonde. Juhudi za ziada zinatilia mkazo hifadhi ya rasilimali za misitu

na wanyamapori katika bonde.

Mfumo wa Utawala wa bonde ni changamano. Nchini Tanzania, ni kawaida kutokea vyombo viwili kutawala

rasilimali moja: Utawala unaotokana na serikali kuu na ule wa serikali za mitaa. Wakati huo huo, Bodi ya

Maji ya Bonde la Pangani (BMBP) imeanzishwa katika bonde kwa lengo la kusimamia rasilimali ya maji

katika bonde zima. Hii maana yake ni kuwa, mara nyingi, mipaka ya mamlaka baina ya watawala wa

rasilimali na wasimamizi inaweza kuwa haieleweki na/ au yenye utata. Aina hii ya utata inajirudia katika

ngazi za chini. Kama ilivyoelezwa awali, Tanzania imegeukia kwa kiasi kikubwa kwenye Usimamizi wa

Maliasili Kijamii (CBNRM) kama njia ya kuboresha usimamizi wa rasilimali zake za asili. Hata hivyo,

hali hii inamanisha kuwa kamati au mashirika mengine ya ngazi ya jamiii yameundwa kushughulikia

rasilimali maalum, na sio maliasili kwa ujumla. Hivyo, kuna Kamati za Maliasili za Vijiji (VNRCs), Vyama

vya Watumiaji Maji (WUAs), Serikali za Vijiji n.k, hali inayozidisha utata katika usimamizi na kuongeza

gharama za uendeshaji kwa kiasi kikubwa.

Nchini Kenya, hivi karibuni rasilimali za maji zimewekwa chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Rasilimali

za Maji (WRMA) inayotumia mabonde ya mito kama maeneo ya msingi ya usimamizi, na ambayo

imekabidhiwa jukumu la kuratibu usimamizi shirikishi wa mabonde hayo na kuhusisha vikundi vya wadau

katika muundo wa usimamizi. Huu ni utaratibu mpya kiasi, unaoweza kukabiliana na vikwazo kuhusiana

na uhusishaji wa wadau katika muundo wa usimamizi, na ugumu wa kushirikisha sekta mbali mbali za

utawala wa mabonde.

Njia hii ya usimamizi kisekta ipo pande zote za mpaka na inajionesha katika hali ambapo idara zinahusika

na usimamizi wa misitu, maji, umwagiliaji, wanyamapori na rasilimali nyingine. Hali hii inaweza

kusababisha malengo ya usimamizi na njia za kuyafikia kwenda sambamba, na hivyo kuleta utata katika

uwezekano wa kuweka usimamizi shirikishi wa bonde. Hata hivyo PBWO imeamua kuhakikisha angalau

idara mbalimbali zinakuwa na mawasiliano baina yao kwa kutuma wawakilishi katika Bodi ya Maji ya

Bonde la Pangani (PBWB). Hata hivyo Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani ina wawakilishi kutoka idara

mbalimbali za serikali ili kuhakikisha kuwa angalau idara hizi zinawasiliana. Kwa mujibu wa sheria mpya

ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji, bodi ina mamlaka ya kuandaa mipango ya usimamizi wa rasilimali

za maji katika bonde, kwa kuwahamasisha na kuwahusisha wahusika wote, wakiwemo wasimamizi na

watumia rasilimali za bonde.

Uchambuzi huu wa Hali Halisi unaeleza kwa ufupi ugumu wa hali na matatizo yaliyotajwa juu kwa kuainisha

masuala mbalimbali ambayo yanahitaji umakini mkubwa katika usimamizi wake. Kimsingi, matatizo ya

mazingira ni matatizo ya kijamii. Kwa urahisi na kwa ajili ya kuonesha hali ya mazingira ya bonde la Mto

Pangani, matatizo haya yanagawanywa kati ya masuala ya mazingira na ya kijamii kama ifuatavyo:

x

Masuala ya mazingira:

• Ukataji miti - husababisha matatizo katika uviaji wa maji ardhini, ongezeko la kasi ya mitiririko

ya maji na hivyo kusababisha mmomonyoko wa udongo, mafuriko na ongezeko la usafirishaji

wa mchangatope.

• Mahitaji ya Ardhi – misitu mingi iko kwenye maeneo muhimu ya kilimo ambayo hupata kiasi

kikubwa cha mvua. Jambo hili ni tishio kubwa kwa hifadhi ya misitu ya bonde hili.

• Shughuli za kilimo: mbinu mbalimbali za kilimo katika bonde hili zilianzishwa wakati idadi

ya watu ilikuwa ndogo sana, na upatikanaji wa rasilimali ulikuwa ni wa kutosha. Kwa kuwa

idadi ya watu imeongezeka mbinu hizo sasa zinaweza kutishia uhai wa mazingira ya bonde

hili. Mifumo iliyopo haina ufanisi wa matumizi ya maji na umwagiliaji wa mfululizo unaweza

kusababisha hali ya chumvi chumvi na/au magadi ardhini.

• Ongezeko la mifugo: suala hili halijulikani sana lakini linadhaniwa kuwa ni tatizo kubwa.

Kutokana na kuongezeka kwa kilimo katika maeneo tambarare ya bonde, ardhi kwa ajili ya

ufugaji imechukuliwa na wakulima, na hivyo kukuza zaidi ukubwa wa tatizo la wingi wa mifugo.

• Maendeleo: maendeleo yasiyosimamiwa katika bonde hili ni chanzo cha uchafuzi wa mazingira

kutokana na njia zisizotosheleza za uondoaji taka.

• Ubora wa maji: ubora wa maji unaathiriwa na uchafuzi, lakini pia maji yanachafuliwa kutokana

na hali ya kijiolojia inayosababisha ongezeko la madini ya floraidi majini.

• Uvuvi unaokithiri: shughuli za uvuvi katika bwawa la Nyumba ya Mungu zinaonekana kukithiri.

Uvuvi pia unatishiwa na ukuaji wa magugumaji kwenye mito na maziwa unaosababishwa na

ongezeko la virutubisho katika bonde.

• Uchimbaji madini: shughuli za uchimbaji madini zisizodhibitiwa katika bonde ni tishio kwa

mandhari yake na manufaa ya ardhi katika siku zijazo. Aidha, hali hiyo ni tishio la uchafuzi wa

mazingira. Uchimbaji wa mchanga mitoni hudhoofisha kingo za mito hiyo.

• Ukosefu wa mwamko wa mazingira baina ya wakazi wa bonde.

Masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa

• Umasikini: Kutokuwepo kwa shughuli za ngazi ya pili na ya tatu katika bonde ambazo ni ajira

katika sekta za biashara na viwanda, wakazi wake wengi hujitafutia maisha katika shughuli za

msingi kama vile kilimo, uvunaji wa mazao ya misitu, uvuvi n.k.

• Migogoro: kwa vile watu wengi hujihusisha na shughuli za msingi, hali ya migogoro huibuka

baina ya watumiaji wadogo, na kati ya watumiaji wadogo na wakubwa.

• Manufaa ya kisiasa: wanasiasa wenye shauku ya kupata kura kutoka kwenye majimbo yao ya

uchaguzi, wakati mwingine huchochea matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali.

Masuala ya usimamizi na utawala

• Sera zisizotosheleza: sera zinazoonekana kuwa sahihi na zilizotungwa vizuri zinaweza zisifae

kwa sababu utekelezaji wake hauwezi kufuatiliwa, na wahalifu hawaadhibiwi.

• Matatizo ya kifedha: Haya hujitokeza karibu katika kila sehemu ya utawala wa bonde, kuanzia

kwenye ugumu wa kutoa malipo ya kutosha hadi kwenye ununuzi wa teknolojia itakayosaidia

ufuatiliaji katika bonde.

xi

• Ukosefu wa Usimamizi Shirikishi: mgawanyo wa kiutawala kati ya ngazi ya mkoa na ya

taifa ukiunganishwa na njia za usimamizi za kisekta unadhihirisha kuwa sehemu kubwa ya

usimamizi wa rasilimali za asili (NRM) katika bonde siyo shirikishi, kwa kuwa sekta au ngazi

moja ya utawala hutumia mbinu ya usimamizi iliyo tofauti na ngazi au sekta nyingine katika

bonde. Tatizo hili vile vile linajitokeza katika ngazi ya kimataifa: hakuna utaratibu uliowekwa

kati ya Kenya na Tanzania wa kuratibu usimamizi wao katika Bonde la Mto Pangani.

• Matatizo na utawala wa jamii: hii huhusiana, kwanza na mchango hafifu unaotolewa na jamii

katika ubunifu, utekelezaji na utiliaji mkazo wa mfumo wa usimamizi wa rasilimali za asili

(NRM) ambao unawaelemea. Pili, nyingi ya njia hizi zinazoshinikizwa kutoka nje ya jamii,

zinataka kuanzishwa kwa kamati za NRM za aina mbali mbali, hali ambayo matokeo yake

ni mkanganyiko mwingi kupita kiasi katika ngazi ya jamii na hivyo kuchochea matatizo ya

kisekta yaliyoelezwa hapo juu, migogoro ya mamlaka na mafanikio duni ya usimamizi.

Kwa kuzingatia masuala yaliyoelezwa hapo juu, Uchambuzi wa Hali Halisi unabainisha maeneo

mbalimbali ya kipaumbele katika utekelezaji kama ifuatavyo:

Kuwepo kwa mikakati ya usimamizi inayounganisha sekta husika kwa ajili ya bonde la Mto Pangani

ikishirikisha majukwaa mbalimbali. Hapana shaka hata kidogo kuwa bonde la Mto Pangani linahitaji haraka

mikakati hiyo ambayo inaweza kukidhi upana na ugumu wa maswaala hayo. Mapendekezo yanayoweza

kufikiriwa ni pamoja na kutengeneza mikakati ya kutambua mahitaji ya maji, kutathmini mahitaji ya maji

ukanda wa chini wa mto kwa ajili ya watu na mazingira, kupanua wigo wa usimamizi wa maji na kuiongezea

jamii wajibu wa kubuni na kutekeleza masuala ya usimamizi shirikishi wa rasilimali za asili (NRM).

Kuwepo kwa mikakati madhubuti ya kuwezesha mazungumzo miongoni na kati ya watumiaji rasilimali na

wasimamizi wa aina mbalimbali na waliohusishwa katika sekta mbalimbali kwa lengo la kuongeza uelewa

katika ngazi zote za usimamizi. Taratibu zinahitajika ili kuhakikisha kuwa fursa za maongezi kati na miongoni

mwa wadau na wasimamizi zinaongezeka kwa kiasi kikubwa, ili kuhakikisha kuwa ubadilishanaji wa habari

kwa pande zote unakuwepo, usambazaji unaboreshwa na elimu ya jinsi wadau wote watakavyoshiriki

katika ustawi wa bonde inatolewa. Ni muhimu uhamasishaji ufanyike kuhusu vipengele vyote na hali ya

usimamizi wa bonde na wadau wake katika ngazi zote za usimamizi na uratibu wake. Sehemu ya ziada

ya eneo hili la kipaumbele ni uanzishaji wa mabaraza yenye uwezo wa kuifanya kazi hii, na kutumika kama

vyombo vya kutatua migogoro, na viungo kati ya ngazi mbalimbali za utawala.

Kuainisha na kuanzisha mfumo sahihi wa ukusanyaji na ufuatiliaji wa data. Eneo hili la utendaji haliishii

katika mifumo ya uendelezaji na ukusanyaji wa data za kihaidrolojia. Tathmini ya Setilaiti na GIS ya

matumizi ya ardhi, viwango vya matumizi na mabadiliko ya kijiografia ni mahitaji ya msingi katika

kupanga mipango na ufuatiliaji wa matumizi ya ardhi. Uundaji wa mbinu za kutathmini na kupima sababu

za msingi za kijamii na za kiuchumi zinazosababisha uharibifu wa mazingira na utumiaji wa rasilimali

uliokithiri pia zinahitaji kutambuliwa. Mifumo kama hii inabidi pia iwe na uwezo wa kutambua mahitaji ya

maji katika Bonde. Mifumo ya data na ufuatiliaji iliyopendekezwa lazima iendane na uwezo wa ndani wa

kifedha na matengenezo.

xii

A

Utangulizi wa Uchambuzi wa Hali

Halisi Bonde la Mto Pangani

A.1 Maelezo ya jumla ya Bonde la Mto Pangani

Bonde la Pangani ni moja kati ya mabonde 9 yaliyoanzishwa na kuchapishwa katika gazeti la serikali kwa

mujibu wa Sheria ya Maji ya 1074 (Usimamizi na Udhibiti) Na. 42 na marekebisho yake Na. 10 ya 1981

(sheria hii ilifutwa na sheria mpya ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji ya mwaka 2009) kwa madhumuni ya

kuhamisha madaraka ya usimamizi wa maji kutoka ngazi ya Taifa na kupeleka ngazi ya mabonde. Bonde

la Pangani lina eneo kadiri ya kilomita za mraba 58,800 1 kiutawala na linajumuisha Bonde la Mto Pangani

na mabonde ya mito midogo ya Umba, Msangazi, Zigi 2 na mito midogo ya pwani, ukiwemo Mkulumuzi.

Uchambuzi huu wa hali halisi unahusu zaidi Bonde la Mto Pangani. Maelezo ya mabonde ya mito midogo

yanayosimamiwa kiutawala na Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani yanatolewa katika Kiambatanisho Na.1.

Bonde la Mto Pangani lina eneo la kilomita za mraba 43,650 1 , kati ya hizo, kilomita za mraba 3,914 1 ziko

Kenya (Mchoro wa 1). Nchini Tanzania, bonde hili lipo katika mikoa ya Kilimanjaro, Manyara, Arusha na

Tanga. Sehemu ya bonde iliyopo Kenya karibu yote ipo katika wilaya ya Taita- Taveta.

Mto Pangani unaundwa na matawi makubwa mawili, ambayo yanatokea katika sehemu ya Kaskazini ya

bonde. Tawi la kwanza ni Mto Kikuletwa unaonzia katika miteremko ya Mlima Meru na miteremko ya Kusini

ya Mlima Kilimanjaro, na la pili ni Mto Ruvu, unaoanzia katika miteremko ya Mashariki ya Mlima Kilimanjaro

na Ziwa Jipe. Mito hii inaungana katika bwawa la Nyumba ya Mungu, lenye eneo la kilomita za mraba 140

(Rohr na Killingtveit, 2002). Mto Pangani 3 hutoka katika bwawa hili, ukitiririka kwa umbali wa kilomita 432

kabla ya kuingia katika Bahari ya Hindi..

Kwa ujumla, bonde hili lina mwinuko mdogo unaoteremka kuelekea upande wa Kusini na Kusini Mashariki hadi

Bahari ya Hindi. Kwa wastani, sura hii ya nchi ijulikanayo kama Nyika za Masai ziko kwenye usawa wa mwinuko

wa mita 800, na sehemu yake kubwa hupata mvua inayozidi kidogo milimita 500 kwa mwaka. Mkabala nayo ni

safu ya milima inayoinuka kutoka uwanda huu ambayo mwinuko wake unafidia kwa kiwango kikubwa matatizo

ya hali ngumu ya uwanda wa nyika. Katika sehemu hii ya juu, kiasi cha mvua kwa mwaka kinafikia milimita 2,000.

Jinsi ilivyo, milima hii ni kama visiwa, wakati ambapo nyanda zinazoizunguka zinaonesha bayoanuwai duni, na

hali ngumu ya kujitafutia riziki, milima hii ni visiwa vya bayoanuwai ya kuvutia na viumbe hai wengi. Binadamu

hawakushindwa kuona ubora wa milima hii, na hata kabla ya ujio wa utawala wa kikoloni nchini Tanzania, milima

iliyopo katika Bonde la Mto Pangani ilikuwa eneo linalokaliwa na idadi kubwa zaidi ya watu katika bonde hili.

1

Tafiti nyingi za awali zinalielezea eneo la chanzo cha mto lililoko kwenye utawala wa Bonde la Pangani nchini

Tanzania kuwa ni kilomita za mraba 56,300, na eneo la Bonde la Mto Pangani katika Tanzania na Kenya kuwa ni

kilomita za mraba 42,000 kulingana na makisio ya planimita yaliyofanywa na S. Kamugisha (1992). Hatimaye taasisi

mbili tofauti (TANRIC ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mradi wa Usimamizi wa Matumizi Bora ya Rasilimali ya

Maji katika Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo) zimekadiria maeneo haya kwa kutumia GIS. Makadirio haya

ya hivi karibuni ni makubwa zaidi kuliko yale ya awali ya makisio ya planimita. Tofauti hizi huenda ni matokeo ya

tafsiri mbalimbali za mipaka ya bonde, hasa upande wa magharibi na tofauti kati ya njia za planimeta na zile za GIS

(Kamugisha na Mwakalinga pers. Wahojiwa, 2003).

2

Baadhi ya Waandishi hutumia tahajia za “Sigi”, “Zigi” ndiyo tahajia inayopendelewa na wakazi wa eneo la chanzo

cha mto huu (Wahojiwa, 2003).

3

Baadhi ya tafiti na ramani zinataja Mto utokao katika Bwawa la Nyumba ya Mungu kuwa ni Ruvu mpaka unapoungana

na Mto Mkomazi, mahali ambapo unakuwa Mto Pangani. Utafiti huu unataja Mto huu kutoka unapotoka Nyumba ya

Mungu hadi unapoingia baharini kuwa ni Mto Pangani.

1

Jinsi Mto Pangani unavyoambaa kuelekea Mashariki, na kushukia uwanda wa pwani ya Tanzania,

ndivyo unavyozidi kukabiliana na hali ya hewa na mazingira ya kutatanisha. Kinyume na hali ya hewa

ya Kaskazini, ambayo imebadilika kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka elfu moja kutoka kipindi

kimoja cha barafu hadi kingine, hali ya hewa inayotokana na Bahari ya Hindi imebakia bila mabadiliko

makubwa. Mwambao wote wa pwani ya Afrika Mashariki unaonesha viunga vya misitu ya kale, na hali

yake ya hewa imewezesha misitu hii kuhifadhiwa kutokana na uthabiti wake.

Mabadiliko ya tabianchi katika maeneo mengine barani

Afrika yamebadili kabisa hali ya mazingira, na kusababisha

kwa kiwango kikubwa kutoweka kwa viumbe hai na kuanza

upya mchakato wa hatua za mabadiliko, kiasi cha kufanya

misitu ya mwambao mwa Tanzania ifanane kidogo na

misitu ya sehemu nyingine barani. Katika milima iliyopo

bonde la Mto Pangani, mistiu hii inaonesha kutetereka kwa

bayoanuwai na upatikanaji wake katika maeneo haya.

Leo hii idadi ya watu wanaokadiriwa kufikia milioni 3.7

huishi katika sehemu ya bonde iliyoko Tanzania, wakati

ambapo nchini Kenya idadi ya watu wa Taita -Taveta

inakaribia 40,900. Mtindo wa makazi katika bonde ni

taswira ya kutowiana kwa hali ya mazingira ya bonde

hili. Nchini Tanzania asilimia 90 ya watu wanaoishi katika

bonde hili huishi katika nyanda za juu, asilimia 80 ya hao

kwa njia moja au nyingine hutegemea kilimo kwa ajili ya

mahitaji yao (Mwamfupe, 2002). Mkusanyiko huu wa

makazi huleta msongamano wa watu unaofikia hadi watu

300 kwa kilometa ya mraba. Mwaka 1988, mikoa ya pwani

ya Tanzania ilikuwa na idadi ya watu 28.4 kwa kilometa ya

mraba (ukiacha Dar es Salaam), ongezeko la kutoka watu

18 tu kwa kilometa ya mraba mwaka 1967. Katika Milima

ya Usambara Magharibi, idadi ya watu imekua kwa mara

Mchoro wa 1: Bonde la Mto Pangani

lilivyoenea Tanzania na Kenya (Rejea:Mradi wa

Usimamizi wa Matumizi Bora ya Rasilimali za Maji)

23 tangu mwaka 1900, wakati katika maeneo ya nyanda za juu za Mlima Kilimanjaro, msongamano wa watu

ni mkubwa kiasi cha watu 900 kwa kilomita ya mraba (Gillingham, 1999). Kinyume chake, maeneo ya nyanda

za chini yameonesha kuwa na msongamano mdogo wa kiasi cha watu 65 kwa kilomita ya mraba.

Kihistoria, wakazi wa bonde hili wamekuwa na shughuli za kiuchumi ambazo ni kielelezo cha hali

zilizotofauti za mazingira katika bonde. Nyanda za chini zilikimu wafugaji, wakati nyanda za juu zilikimu

wakulima. Kutokana na ujio wa wakoloni kutoka Ulaya, maeneo makubwa ya ardhi ya kilimo yalitengwa

kwa kilimo cha mashamba makubwa. Katika wilaya ya Taita – Taveta ya Kenya, karibu ardhi yote

ilitengwa kwa ajili ya kilimo cha mkonge. Hali hii ilisababisha kukua kwa kiwango cha kilimo. Johnston

(1946) anasema kuwa, mwaka 1943, umilikaji ardhi katika nyanda za juu za Kilimanjaro kwa wastani

ulikuwa hekta 1.2 kwa mtu mmoja. Katika mwaka 1946, ulikuwa mita za mraba 2.5 tu.

Wastani wa kiwango cha umilikaji wa ardhi katika nyanda za juu za Kilimanjaro umeongezeka tokea

hapo, na Lein (2002) anasema kiwango cha umilikaji ardhi kuwa ni wastani wa hekta 0.6 kwa kaya. Kaya

za nyanda za chini hulima mashamba ya wastani wa eneo la hekta 10.4.

Wastani huo unaelekea kupungua. Kadiri ukubwa wa mashamba katika nyanda za juu unavyokuwa mdogo

zaidi na zaidi, uwezo wake wa kukidhi mahitaji ya maisha ya watu unapungua, na udongo umechoshwa

kutokana na kupanda mazao mfululizo pamoja na umwagiliaji uliokithiri, watu wamelazimika kutafuta

ardhi katika maeneo ya nyanda za chini. Kwa sababu hiyo, idadi ya watu imekuwa kubwa kando ya mito

ya bonde la mto Pangani na umwagiliaji umeenea kwa kiasi kikubwa sana. Matokeo yake, maeneo ya

bayoanuwai yaliyopo hapa na pale katika uwanda wa bonde yako katika shinikizo la kutoweka.

2

Mchoro wa 2: Bonde la Mto Pangani

Angalia pia Picha ya 1, ukurasa wa 33

(Rejea: Mradi wa Usimamizi wa Matumizi

Bora ya Rasilimali za Maji)

3

Kwa hiyo, kiini cha matatizo ya Bonde la Mto Pangani kinahusiana na msogamano wa watu na mahitaji

yao mawili makuu na muhimu kwa kilimo na ufugaji: ardhi na maji. Mwingiliano wa mambo haya, na

mahitaji waliyo nayo watu katika rasilimali za bonde, yamesababisha migogoro ya aina mbalimbali:

Migogoro itokanayo na viwango

Uhusiano baina ya watumiaji maji wa ukubwa tofauti katika Bonde la Mto Pangani mara nyingi unajieleza

katika namma mbili, yaani mashamba makubwa yanayotumia mamia ya lita za maji kwa sekunde na kutumia

mifumo ya umwagiliaji yenye ufanisi mkubwa, tofauti kabisa na watumiaji wadogo wanaotumia maji kidogo na

mifumo duni ya umwagiliaji. Tofauti hizi za viwango vya matumizi haziishii kwenye teknolojia pekee, bali hata

ardhi. Watumiaji wakubwa karibu wakati wote hutumia ardhi kubwa zaidi kuliko watumiaji wadogo. Jambo

jingine tofauti na la pekee ni kuwepo kwa mitambo ya uzalishaji umeme katika bonde. Ardhi inayokaliwa na

mitambo hii siyo kubwa sana, lakini mahitaji yake ya maji ni makubwa sana. Ni dhahiri maji haya hurudishwa

mtoni, hii ikiwa na maana uzalishaji umeme huyaacha maji katika hali na kiasi kile kile kilichochukuliwa. Pamoja

na hayo matumizi hayo ni kwa maslahi ya taifa. Bonde la Mto Pangani huzalisha kiasi kinachofikia asilimia

17 ya umeme wa Tanzania, na vinu vyake vingi vimesanifiwa maalum kwa kutilia maanani mtiririko wa maji.

Iwapo matumizi ya maji kati ya vyanzo vya maji na mitambo ya umeme yatazidi, inabidi mitambo izalishe kwa

kiwango chini ya uwezo wake. Mgogoro uliopo hapa ni kulinda maslahi ya kitaifa dhidi ya watumiaji wadogo.

Migogoro itokanayo na umiliki

Kitabu hiki kinatumia neno umiliki kama haki ya kusimamia rasilimali. Kama ilivyo kwenye sehemu nyingi

ulimwenguni, dhana ya usimamizi kwa misingi ya kijamii katika Tanzania na Kenya ni mpya. Katika nchi

ambazo mifumo ya usimamizi inayotegemea serikali, imedumu kwa zaidi ya nusu karne, bila mafanikio

mazuri na kusababisha ongezeko la matatizo ya mazingira, usimamizi wa maliasili kwa misingi ya kijamii

(CBNRM) unaonekana kuwa chaguo la kuvutia. Kwa hali hiyo nchini Tanzania kuna asasi nyingi mno za

usimamizi wa kijamii. Dhana ya usimamizi wa maliasili kijamii inabakia kuwa mpya sana nchini Kenya.

Ukinzani wa mifumo hii unahusiana na mwenendo wa matumizi na miundo yao. Hapa, jamii zinaweza

zisihusishwe katika uundaji wa mfumo wa usimamizi, utekelezaji wake au hata mifumo yake ya kisheria.

Migogoro itokanayo na mahali

Maeneo ya watumiaji maji yaliyoko juu hutoa nafasi nzuri zaidi ya matumizi ya rasilimali kuliko ilivyo kwa watumiaji

wa maeneo ya chini. Kimsingi, matatizo haya yanaweza kuonekana katika mifereji ya umwagiliaji ambapo

watumiaji walio karibu na chanzo cha maji wanaweza kuotesha mazao yanayohitaji maji mengi sana (kama vile

mpunga) na wale wanaoishi mwishoni mwa mfereji hulazimika kupanda mazao yenye mahitaji madogo ya maji.

Matatizo makubwa yanayoikabili mitambo ya umeme wa maji iliyopo upande wa chini ni mfano mwingine.

Taasisi kuu mbili zinatawala rasilimali ya maji ya Bonde la Mto Pangani. Nchini Tanzania ni Ofisi ya

Maji ya Bonde la Pangani (PBWO), wakati katika Kenya ni Mamlaka ya Usimamizi wa Rasilimali za

Maji (WRMA). Chini ya sheria ya hivi karibuni ya Tanzania, mabonde yote yamewekwa (au yatawekwa)

chini ya ofisi kama hizo. Hata hivyo, mabonde mengine ni madogo mno kustahili kuanzishiwa ofisi

zitakazojitegemea kiusimamizi. Bonde la Pangani limezungukwa na mabonde manne ya aina hiyo (mito

ya Umba, Zigi, Msangazi, na mabonde madogo ya mito ya pwani). Haya kiutawala yanawekwa chini ya

PBWO, na hayakujumuishwa katika uchambuzi wa hali halisi katika kitabu hiki. Hata hivyo, muhtasari wa

taarifa kuhusu mabonde hayo unaambatanishwa(Kiambatanisho Na 1).

Bonde la Mto Pangani linakabiliana na matatizo kadhaa makubwa ya kiusimamizi. Kwa kuzingatia tofauti

kubwa za aina za maliasili za bonde, pamoja na mahitaji na matarajio mbalimbali ya matumizi, haja ya kuwa

na usimamizi shirikishi haiwezi kupuuzwa. Hapo nyuma, njia ile ile ya usimamizi wa ‘kisekta’ kwa bonde hili

ilimaanisha kuwa rasilimali ya wanyamapori ilisimamiwa kipekee tofauti na shughuli za misitu, bila kujua, kwa

upande mwingine kipaumbele cha usimamizi wa maji. Tatizo pia linajitokeza katika utoaji kipaumbele, sekta ya

maji ikidai kuwa maji ni kiungo kinachounganisha rasilimali zote za bonde, lakini watu wa misitu wakilalamika

kuwa sehemu kubwa ya maji ya bonde yanatoka katika misitu iliyo kwenye mamlaka yao kisheria.

4

A.2 Usimamizi wa Pamoja wa Mabonde ya Mito (IRBM)

Kwa vyovyote vile, mfumo wa usimamizi wa maliasili kimabonde ndio unaofaa. Mabonde ya mito

yanahusisha vyanzo na michakato yote ambayo hatimaye itahakikisha kuwa maji yanafika hadi mwisho

wa mto. Hivyo, bonde la mto linahusisha vijito vya awali vya mto, mito midogo na mabonde yake. Pia ni

pamoja na delta iliyohusiana na mto, na maji ya ardhini, ardhioevu na mabwawa yoyote yaliyomo.

Mchanganyiko wa michakato inayohakikisha kuwa maji yanasafiri kutoka kwenye chanzo cha mto hadi

mwisho wake ni mgumu na una mambo mengi. Rasilimali za ziada, kama vile misitu na ardhioevu,

zinachangia mchakato huu. Kiasi cha maji ambacho hatimaye hufika mwishoni mwa mto pia kitategemea

kiasi cha maji yanayochukuliwa kwa matumizi yanapopita katika mkondo wake pamoja na kiwango cha

uvukizaji katika maeneo ardhioevu na mimea ya majini na ya kandokando ya mto. Mwisho, ubora wa

maji yatakayofika mwishoni mwa mto pia utaonesha michakato iliyopo katika bonde kama vile mbinu za

kilimo ambazo huongeza au kupunguza mmomonyoko, maendeleo ya miji au viwanda n.k.

Usimamizi wa Mabonde ya Mito (RBM) unatambua kuwa usimamiaji wa mto hauwezi kutekelezwa kwa

kutenganisha michakato na hali nyingi mbalimbali zinazoathiri mtiririko wa mto na ubora wa maji yake.

RBM hulichukulia bonde la mto kama kitengo cha usimamizi kinachohusisha matumizi na uhifadhi wa

(a) mifumo midogo ya ikolojia (mabonde madogo ya mito, misitu, ardhioevu, maeneo ya milima, ardhi

kame, n.k); na (b) mifumo ya matumizi ya binadamu iliyomo ndani ya eneo la maji (kilimo, umwagiliaji,

uvuvi, usafirishaji, uchimbaji madini, viwanda, n.k). RBM kwa kawaida hufuata kanuni ya kuwa maji

huunganisha mifumo ikolojia iliyomo ndani ya bonde la mto (Howard, 2002).

Usimamizi wa Pamoja wa Bonde wa Mto hujaribu kuleta uwiano wa masilahi ya watumiaji wote waliopo katika

bonde, na wakati huo huo kukuza ufanisi wa matumizi ya rasilimali na kuhakikisha kunaendelea kuwepo maji

ambayo kwayo mifumo hii inategemea (Howard, 2002). IRBM inaweza kufafanuliwa kama ifuatavyo:

”… ni mchakato unaokuza uratibu wa maendeleo na usimamizi wa maji, ardhi na rasilimali

zinazohusiana nazo ili kuzidisha ustawi wa kiuchumi na kijamii kwa njia ya usawa bila ya

kuathiri uendelevu wa mifumo muhimu ya ikolojia (GWP, 2002:1).

IRBM hushughulika na rasilimali kwa mapana zaidi iwezekanavyo. Inabidi kuziangalia rasilimali za maji

kwa mtazamo mzima wa mifumo ya kijamii, kiuchumi na kiikolojia ya mkoa au nchi. Kiutendaji, hii ina

maana ya kuwa sera na programu katika maeneo mengine ya rasilimali hazina budi kuchambuliwa kwa

makini ili kuona jinsi zinavyoathiri mahitaji yanayoshughulikiwa na sekta ya maji (GWP, 2002) IRBM

inayapa mazingira umuhimu sawa na watu katika mahitaji ya rasilimali za maji. IRBM lazima ifanye kazi

kulingana na malengo yaliyokubaliwa na wadau wa bonde walio wengi na kufuata kanuni za usimamizi

wa rasilimali za maji, usimamizi wa mfumo ikolojia, uhifadhi wa bayoanuwai, usimamizi endelevu wa

maliasili na ufufuaji wa mfumo ikolojia. (Howard, 2002).

Sehemu muhimu ya Usimamizi wa Pamoja wa Bonde wa Mto ni mpango wa matumizi ya ardhi. Kwa

kuwa mambo mengi sana yanayotokea kuhusu maji yanahusu maendeleo ya ardhi, ni muhimu matumizi

ya ardhi yasimamiwe kwa njia ambayo itahakikisha upatikanaji wa maji na kwamba michakato ya

kihaidrolojia haiingiliwi. Kwa mfano, ukuaji wa miji mara nyingi umekuwa na athari kubwa kwa rasilimali

ya maji kutokana na ongezeko kubwa la majitaka. Kwa njia hiyo hiyo, misitu na kilimo vinaweza kuwa na

athari kwa wingi na ubora wa maji.

Mifano ya mapendekezo ya usimamizi wa matumizi ya ardhi ni pamoja na (a) kugawa kanda-hapa

maeneo maalum hubainishwa ambamo aina fulani za matumizi ya ardhi hukatazwa. Kwa mfano kanda

za maji ya kunywa, au maeneo ambayo ujenzi hupigwa marufuku kutokana na hofu ya mafuriko. (b)

hatua za kulinda udongo na kudhibiti mmomonyoko, kama vile kilimo cha kontua, au ushauri wa upandaji

wa miti (c) kanuni za uondoaji taka, kama vile kuweka maeneo ya kutupa taka (GWP,2002).

5

Kisanduku cha 1: Usimamizi wa Mahitaji ya Maji

Usimamizi wa Mahitaji ya Maji (WDM) umetokana na kutambua kuwa (a) mahitaji ya maji yanaongezeka

bila ya kuambatana na ongezeko la upatikanaji wa maji; (b) matokeo yake, gharama ya

kuongeza usambazaji wa maji hupanda kwa sababu uchukuaji maji kutoka katika vyanzo vipya

unakuwa mgumu zaidi. Gharama zinazoambatana na uanzishaji wa teknolojia au mbinu mpya ya

uchukuaji maji inawezekana zisikubalike. WDM, basi, inajaribu kuokoa maji yachukuliwayo kutoka

vyanzo vilivyopo vya maji, yalete manufaa kwa vyote viwili, uchumi na mazingira. WDM inaweza

kufafanuliwa kama mkakati wa kuboresha matumizi fanisi na endelevu ya rasilimali za maji kwa

kuzingatia masuala ya kiuchumi, kijamii na kimazingira (Wegelin-Schuringa, 1998). Lengo kuu la

WDM ni kuchangia katika utoaji huduma za maji na uondoaji majitaka kwa ufanisi na usawa. IUCN

inaamini kuwa hili linaweza kufikiwa kupitia utumiaji wa vivutio mbalimbali vya kiuchumi, kukuza

ufanisi na usawa wa matumizi ya maji na vile vile hatua kadhaa za kuhifadhi maji zitakazolenga

katika kukuza uelewa juu ya uhaba na tabia ya asili ya kumalizika kwa rasilimali hii. WDM huchukua

hatua mbalimbali zinazolenga kuleta usimamizi endelevu. Nazo ni pamoja na:

• kulinda ubora wa maji

• kupunguza upotevu wa maji

• kuboresha ugawaji wa maji baina ya watumiaji

• kuweka mfumo sahihi wa upangaji bei

• hatua za kuhifadhi maji

A.3 Programu ya Maji na Uasili (WANI)

IUCN (shirika la kimataifa la kuhifadhi uasili) inasaidia kupata utatuzi wa busara wa changamoto

zinazotukabili duniani katika maendeleo ya jamii na utunzaji wa mazingia. IUCN inafadhili tafiti za

kisayansi, na inasimamia miradi na huunganisha serikali za kimataifa, asasi zisizo za kiserikali, mashirika

ya Umoja wa Mataifa, makampuni na jamii katika kutunga na kutekeleza sera, sheria na utendaji bora.

IUCN ni mtandao wa masuala ya mazingira ulio mkubwa kuliko yote duniani. Ni umoja wa kidemokrasia

wenye wanachama 1,000 kutoka serikali na asasi zisizo za kiserikali, mashirika na wanasayansi 10,000

wa kujitolea katika nchi zaidi ya 160. Ina waajiriwa wataalamu 1,100 katika ofisi zake 62 na mamia ya

washiriki kutoka jamii, asasi na sekta isiyo rasmi ulimwenguni kote. Makao makuu yake yapo Gland,

karibu na Geneva, Uswisi.

IUCN ilizindua mpango wa maji na uasili (Water and Nature Initiative (WANI)) mwaka wa 2001. WANI ni

mpango wa utendaji unaofanya kazi na washiriki 80 katika nchi 30 katika kuhusisha kwa kiasi kikubwa

mambo ya mazingira na jamii wakati wa utayarishaji wa mipangao ya usimamizi wa rasilimali za maji.

Mpango wa WANI hutumia menejimenti ya mfumo wa ikologia kama mkakati wa usimamizi uwiano na

wa pamoja wa ardhi maji, bayoanuai na jamii. WANI husaidia katika utatuzi wa kuchagua katika mtanziko

wa maendeleo ya jamii na hifadhi ya rasilimali zilizo majini kwa kutanzua migogoro ya matumizi ya maji,

na kufufua mito na kuchochea maendeleo ya jamii.

WANI huandaa na kuonyesha njia sahihi ya utendaji katika kutekeleza usimamizi wa rasilimali za maji

wa uwiano. Husaidia katika kufanyia mageuzo ya kudumu na kujenga uwezo wa jamii unaohitajika

katika kutekeleza mageuzi hayo. Katika awamu ya kwanza, kuanzia mwaka wa 2001 hadi mwaka wa

2008 WANI ilifanya kazi katika mabonde ya maji 12 katika nchi zaidi ya 30 ulimwenguni kote, kazi

iliyogharimu dola za Marekani 40m. Sehemu kubwa ya fedha hizi zilitolewa na Wizara ya Mambo ya Nje

ya Uholanzi. Miradi ya majaribio ya WANI ilionyesha nama hali ya watu na mifumo ya ikolojia inavyoweza

kunufaika kwa kutumia usimamizi endelevu wa mabonde ya maji. Miradi ya WANI ni washiriki wa jumuia,

wanachama wa IUCN, jamii za kiraia na serikali.

6

WANI inasaidia kufanya mabadiliko kwa kuunganisha vipaumbele vya maendeleo, huduma zitolewazo

na mifumo ya ikolojia, utawala bora wa rasilimali za maji, ushiriki wa wadau, mapato endelevu ya fedha,

kujifunza na uongozi.katika utendaji.

Toleo la kwanza la Uchambuzi ya Hali ya Bonde llikuwa tokeo la kazi ya awali katika bonde la Pangani

na liliweka msingi wa miradi iliyofuata awamu ya kwanza ya WANI ilianza kufanya kazi katika bonde lote

la Pangani na kufuatana na matokeo ya kazi hii Ofisi ya Maji Bonde la Pangani iliweza kupata ufadhili

wa nyongeza kutoka Kamisheni ya Ulaya kupia msaada wa mfuko wa maji wa Umoja wa Ulaya, Mfuko

wa Mazingira wa Ulimwengu (Global Environment Facility) kupitia Shirika la Maendeleo la Umoja wa

Mataifa (UNDP).

A.4 Uchambuzi wa Hali halisi: madhumuni na matokeo

Uchambuzi wa Hali halisi ni hatua muhimu ya mradi wa IUCN. Ni uchambuzi wa hadhi, hali, mienendo na

masuala muhimu yanayoathiri mifumo ikolojia, watu na taasisi katika hali ya kijiografia ya ngazi yoyote

(jamii, taifa, kanda, kimataifa)’ (IUCN, 1999:1). Madhumuni ya Uchambuzi wa Hali halisi ni kutoa tathmini

inayotosheleza dhamira ya kipaumbele au maeneo ya utendaji yatakayoendelezwa.

Kwa mantiki hii madhumuni ya Uchambuzi huu ni kama yafuatayo:

• Kutambua rasilimali zilizomo katika Bonde la Mto Pangani na michakato na matukio yanayoziathiri.

Uchambuzi utayaonesha maeneo hayo maalum ambayo yanahitaji kushughulikiwa ili kuyanusuru,

kwa kuzingatia ushahidi unaoonesha kuwa uwiano kati ya upatikanaji wa riziki ya kutosha kwa

wakazi wa Bonde hili na uendelevu wa rasilimali za Bonde umeharibiwa.

• Kutambua maeneo ya utendaji kwa mapana ambamo hatua zinaweza kuchukuliwa kwa manufaa.

Uchambuzi unatambua kuwa nyingi ya hatua hizo zinaweza zisiwe ndani ya utaalam wa IUCN.

Hivyo utataka kuainisha mashirika, vikundi au taasisi nyingine ambazo IUCN inaweza kuingia

nazo ubia kadri inavyotaka kuendeleza juhudi za WANI katika Bonde la Mto Pangani.

A.5. Vyanzo vya data

Uchambuzi huu wa Hali halisi umefanyika kwa kutumia data zilizopatikana kutokana na vyanzo vikuu viwili:

• Taarifa iliyochapishwa. Umuhimu wa kipekee upo katika matokeo ya tafiti juu ya Usimamizi

wa Rasilimali za Maji zilizofanyika katika Bonde la Mto Pangani, ambazo ni juhudi za pamoja

kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Teknolojia na Sayansi cha Norway.

Kwa nyongeza, Uchambuzi wa Hali halisi pia umetumia taarifa ya warsha iliyoitwa “Bonde la

Mto Pangani: Mapendekezo ya Usimamizi Shirikishi”, iliyofanyika hoteli ya “Kilimanjaro Crane”

, Moshi, Tanzania, tarehe 8 –10 Mei, 2002.

• Mahojiano yasiyoandaliwa kikamilifu baina ya mwandishi na wadau wa Bonde la Mto

Pangani. Waliohusika ni pamoja na watawala wa maji, watu wa misitu, jamii za wakulima,

wahifadhi wa wanyamapori na watumiaji binafsi wa maji. Mahojiano yalifanyika Arusha, Moshi,

Hale, Tanga na Dar es Salaam kati ya Novemba 12 na 22, 2002. Mahojiano, wahojiwa na

ushirikishwaji wa taasisi zao vimetolewa kama sehemu ya rejea za waraka huu.

Uchambuzi huu wa hali halisi umefanyiwa mapitio na idadi kubwa ya wadau wa Bonde la Mto Pangani.

Wakati wa warsha iliyofanyika Moshi-Tanzania, kati ya tarehe 10 na 12 Machi, 2003, Uchambuzi wa

Hali halisi uliwasilishwa kwa wadau kwa ajili ya mapitio na maoni. Mwezi Mei, 2003, maoni ya nyongeza

yalipokelewa kutoka Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani na Mamlaka ya Maendeleo ya Pwani (CDA

Kenya). Marekebisho yaliyopendekezwa hatimaye yalizingatiwa na yamejumuishwa.

7

A.6 Muundo wa Uchambuzi wa Hali halisi

Uchambuzi huu wa hali halisi unaanza kwa maoni ya jumla ya rasilimali za bonde hili na matatizo

yanayozikabili. Kisha unaangalia shughuli za rasilimali watu katika bonde, uchumi wao, matatizo na

vikwazo vya upatikanaji wa rasilimali. Kisha uchambuzi unaendelea kuangalia matatizo na masuala

ambayo wadau mbalimbali wanaona kuwa yapo katika bonde kama msingi wa kujadili muundo wa

Usimamizi wa Maliasili za bonde. Katika sura nyingi, uchambuzi umefupisha dondoo muhimu ambazo

msomaji anatakiwa kuzifahamu na kuzizingatia kadiri anavyoendelea na sehemu za uchambuzi

zinazofuata. Mihutasari hii imewekwa pamoja katika hitimisho la kitabu hiki, ambapo majadiliano yatarudi

kwenye madhumuni yake, na kuangalia jinsi matatizo yaliyotambuliwa, juhudi za usimamizi ambazo

zimechukuliwa na mapendekezo ambayo yamefikiriwa kwenye kitabu hiki kwa pamoja yanaweza kuwa

kichocheo na msingi wa uchukuaji wa hatua muafaka na ushirikiano wa WANI.

8

B Maliasili za Bonde la Mto Pangani

B.1 Utangulizi

Utangulizi wa Uchambuzi huu wa Hali halisi umetoa mwanga kuhusu rasilimali anuwai zilizomo katika Bonde

la Mto Pangani. Katika sura hii, tunaanza kwa kuangalia misitu iliyopo katika bonde, mchango wake na tishio

la hifadhi ambalo linatoa changamoto kwa misitu hiyo. Mfumo kama huo huo utatumika kuangalia rasilimali za

ziada katika bonde, zikiwemo maji na maeneo ardhioevu, maeneo yaliyohifadhiwa na bayoanuwai. Sura hii

itahitimishwa kwa muhtasari wa dondoo muhimu. Sura hii kimsingi inahusika na rasilimali za maji na viumbe

hai. Mashapo ya madini yaliyopo katika bonde hayakuzingatiwa sana kutokana na ukosefu wa data.

B.2 Misitu ya Bonde

Mgawanyo wa misitu, aina na hadhi yake kisheria nchini Tanzania iko kama ifuatavyo:

Jedwali la 1: Aina, matumizi na hadhi ya kisheria ya misitu nchini Tanzania.

Hekta 1,000 %

Aina ya Msitu

Misitu (mingine mbali ya misitu ya mikoko) 1,141 3.4

Misitu ya Mikoko 115 0.3

Misitu ya Mbao 32,299 96.3

Jumla 33,555 100.0

Matumizi ya Ardhi ya Misitu

Eneo la misitu ya uzalishaji 23,810 71.0

Eneo la misitu inayohifadhiwa (hasa maeneo ya vyanzo vya mito) 9,745 29.0

Jumla 33,555 100.0

Hadhi ya Kisheria

Hifadhi ya Misitu 12,517 37.3

Misitu/misitu ya mbao katika mbuga za taifa, n.k. 2,000 6.0

Ardhi ya misitu isiyohifadhiwa 19,038 56.7

Jumla 33,555 100.0

(Rejea: Lambrechts et al., 2002).

Misitu ya Bonde la Mto Pangani huwakilishwa na aina kuu tano: (a) Misitu ya milima ya Afrika (b) Misitu ya Mikoko

(c) Misitu ya Mwambao (d) Misitu ya Miombo (e) Misitu ya kandokando ya mito. Misitu hii inaweza kuwa ya hifadhi,

uzalishaji au misitu isiyokuwa na hadhi maalum. Misitu ya Pwani na ya milima ya Afrika, kutokana na upekee

wake wa bayoanuwai, hupata nafasi ya kufikiriwa zaidi. Shughuli za kimataifa za bayoanuwai katika misitu hii pia

zinasaidia upatikanaji zaidi wa data kuliko ilivyo kwenye aina nyingine za misitu. Hili linajionesha katika kitabu hiki.

Sehemu kubwa ya uwezo wa Bonde la Mto Pangani katika upatikanaji wa maji inachangiwa na

misitu yake. Kwa mfano kwenye Mlima Kilimanjaro, kiasi cha asilimia 96 ya maji yanayotiririka

kutoka mlimani chanzo chake ni kwenye ukanda wa msitu pekee (Lambrechts et al., 1992), na

Mlima Kilimanjaro unakadiriwa kutoa asilimia 60 ya maji yanayoingia Bwawa la Nyumba ya Mungu,

na asilimia 55 ya maji yatiririkayo juu ya ardhi katika bonde (Rohr na Killingtveit, 2002).

9

Kisanduku cha 2: Taarifa za Msingi za Misitu iliyomo katika Bonde la Mto Pangani

Misitu ya Bonde la Mto Pangani ni muhimu kwa haidrolojia yake kwa sababu:

• hurekebisha kasi ya maji, huzuia mmomonyoko wa udongo, huhifadhi maji na kuboresha

ubora wa maji;

• huchangia katika matengenezo na hifadhi ya mkusanyiko wa jeni;

• hutoa mbao na madawa kwa matumizi ya jamii .

Kuna aina kuu tano za misitu katika Bonde:

• Misitu ya mikoko: Hutoa mchango mkubwa katika kuhifadhi ukanda wa pwani. Huhifadhi

mashapo laini yaliyoko kando ya bahari kutokana na mmomonyoko, huzuia masimbi na

hutumika kama virutubisho. Miti yenyewe na matope kuzunguka mizizi yake ni makazi

muhimu kwa viumbe mbalimbali vya majini na maficho yao.

• Misitu ya pwani ya Afrika Mashariki: Hii ni misitu ya kipekee iliyoko Afrika Mashariki na

ina bayoanuwai na viumbe wengi. Iko katika uwanda wa pwani kati ya misitu ya mikoko na

Milima ya Tao la Mashariki.

• Misitu ya milima ya Afrika (Afromontane): Misitu ya Milima ya Tao la Mashariki ina kiwango

cha juu cha bayoanuwai na viumbe wengi kama ilivyo katika misitu ya pwani. Katika Milima

ya Kilimanjaro na Meru, misitu hii haionyeshi anuwai inayofanana, lakini inatoa mchango

muhimu kihaidrolojia.

• Misitu ya kandokando ya mito: hii huimarisha kingo za mito, na mto Pangani unapotiririka

kupitia nyanda za chini zilizo kavu na kame, huwa maeneo ya kipekee ya miti na vichemchemi

kwa matumizi ya binadamu na wanyama pori.

• Msitu wa miombo: hii inajumuisha kundi kubwa la miti ya jamii ya mnondondo (Brachystegia,

Isoberlinia na Julbernadia). Tofauti na misitu ya mvua, misitu ya miombo haisongamani sana kiasi

cha kuzuia mwanga usifike ardhini. Matokeo yake ni kuwa, nyasi hufunika eneo kubwa la ardhi

chini ya msitu, na wakati wa msimu wa mvua, nyasi hukua hadi kufikia kimo cha mita moja.

Misitu ya vyanzo vya maji inafanya kazi tatu muhimu (Akitanda, 2002):

• Misitu huchangia kwenye hifadhi ya maji kwa kurekebisha kasi ya maji, kuzuia mmomonyoko wa

udongo, kuweka akiba ya maji na kuboresha ubora wa maji.

• Huhifadhi mkusanyiko wa jeni: Misitu kama ile ya unyevunyevu ya kitropiki huonesha viwango

vya juu sana vya bayoanuwai, na huchangia udumishaji wa mkusanyiko wa jeni wa dunia.

• Misitu hutoa mazao kwa ajili ya matumizi ya jamii, kama vile mbao na mimea ya madawa.

Misitu ya Mikoko

Misitu ya mikoko hutoa mchango mkubwa katika kuhifadhi ukanda wa pwani. Huhifadhi mashapo laini

yaliyoko kando ya bahari kutokana na mmomonyoko, huzuia masimbi na kutumika kama virutubisho.

Miti yenyewe na matope kuzunguka mizizi yake ni makazi muhimu kwa viumbe mbalimbali wa majini

na wale wajifichao. Wakati wa mawimbi makubwa, mamia ya aina za samaki huhamia katika misitu ya

mikoko ili kujipatia chakula au mazalio. Samaki wengi na kamba hutegemea mikoko kama sehemu za

kulelea vifaranga vyao. Miti ya mikoko ni migumu sana na hivyo inastahimili mchwa na kuvu. Inatumika

kwa shughuli mbalimbali. Matawi ya Rhizophora, Ceriops na Bruguiera ni marefu na yamenyooka, kwa

hiyo hutumika maalum kama miti ya kujengea ingawa hutumika pia kama nguzo, na katika utengenezaji

wa mitego ya samaki na samani. Katika miaka ya karibuni, mikoko pia imetumika kutengeneza mkaa na pia

10

hukusanywa kama kuni. Misitu ya mikoko iliyoko karibu na miji hutumika kwa wingi kwa madhumuni haya.

Mikoko inaweza kupunguzwa matawi ili kuongeza ukuaji wake na upandikizaji upya pia ni rahisi. Hata hivyo

hakuna shughuli yoyote kati ya hizi inayofanyika katika mwambao wa Tanzania (Richmond, 1997).

Karibu mwambao wote wa pwani ya Tanzania umepambwa na misitu ya mikoko. Katika eneo la Bonde

la Mto Pangani, inapatikana katika mkoa wa Tanga pekee, ambako karibu asilimia 11 ya mikoko ya

Tanzania hupatikana. (Bwathondi na Mwamsojo, 1993) Hii ni pamoja na hekta 753 za misitu ya mikoko

iliyosongamana kuzunguka mdomo wa mto Pangani (Kijazi, 2002).

Misitu ya Pwani ya Afrika Mashariki

Misitu ya pwani ya Afrika Mashariki iko katika uwanda wa pwani, kati ya Milima ya Tao la Mashariki na mikoko

ya pwani. Misitu hii imetawanyika sana, na viunga vya misitu vimetenganishwa na maeneo ya mifumo ikolojia

nusu kame. Imeenea kati ya mwinuko wa mita 500 na 1,000 juu ya usawa wa bahari. Tabia muhimu ya misitu

ya pwani (ambayo ipo pia katika misitu ya Milima ya Tao la Mashariki) ni ile ya kuitegemea hali ya hewa

ya Bahari ya Hindi na uthabiti wa kihistoria iliyoipatia. Kwa kuwa pekee katika uwanda wa pwani ya Afrika

Mashariki, kujitenga kwa misitu hii kutoka mifumo mingine ya misitu ya Afrika kumesababisha viwango vya

juu vya upatikanaji wa spishi (tazama hapa chini) (Burgess et al.,1996). Inasadikiwa kuwa kuna misitu 76 ya

pwani nchini Tanzania (Burgess et al.,1996). Mingi ipo katika uwanda wa nyasi wa pwani kati ya mdomo wa

mto Pangani hadi chini ya milima ya Usambara (tazama Baker na Baker, 2001).

Misitu ya milima ya Afrika (Afromontane)

Milima ya Tao la Mashariki inaambaa kutoka

mpaka wa Tanzania na Zambia hadi milima

ya Taita nchini Kenya. Inahusisha milima ya

kale ya fuwele iliyopo Mashariki ya Tanzania

na Kusini Mashariki ya Kenya ambako

inakabiliana moja kwa moja ya hali ya

hewa ya Bahari ya Hindi. Katika Bonde la

Mto Pangani inahusisha milima ya Pare ya

Kaskazini na Kusini, milima ya Usambara

ya Mashariki na Magharibi na Milima ya

Taita. Milima hii ni ya zamani sana, na

kipindi cha karibuni zaidi cha uharibifu wa

miamba iliyoiathiri kilitokea miaka milioni 7

iliyopita. Kwa kulinganisha, lava ya zamani

zaidi katika Mlima Kilimanjaro ina umri wa

miaka milioni 1 tu. (Burgess et al., 1996).

Ukaribu wa milima hii na bahari pia

umefanya hali yake ya hewa kubaki kuwa

thabiti kabisa. Wakati wa zama za mwisho

za barafu, hali ya joto la uso wa bahari ya

Hindi haikubadilika. Hivyo, ingawa zama

Kisanduku cha 3: Milima ya Taita

Milima ya Taita ni Milima pekee ya Tao la Mashariki katika

Kenya. Milima hii na misitu yake inachukua spishi zaidi

ya 2,000 za mimea yote (flora) na wanyama wote (fauna),

ambapo aina 13 kati ya hizo zinapatikana kwa wingi.

Mimea 67 ya asili inayojulikana, ikiwemo kahawa mwitu

(Coffee fademi), husitawi milimani. Milima ya Taita ni Eneo

Muhimu la Ndege (IBA), na ina spishi tatu zinazopatikana

kwa wingi: Taita Apalis, Taita Thrush na Taita White – eye.

Misitu ya milima hii pia ina utajiri wa amfibia (wanyama

waishio majini na nchi kavu), wadudu na viumbe vingine.

Ni kilomita za mraba 6 tu ndizo zinazobaki katika Milima

ya Taita, zikiwa zimegawanyika katika viunga 13 vya

misitu. Newmark (1998) anakadiria kuwa mabaki haya

ya milima huwakilisha asilimia 2 tu ya mtandao wa misitu

hii miaka 2,000 iliyopita. Milima ya Taita imepoteza misitu

zaidi kuliko mlima wowote wa Tao la Mashariki.

za barafu zinaweza kuwa zimebadili hali ya hewa katika sehemu nyingine za Afrika, haikufanya hivyo kwa

milima ya Tao la Mashariki. Kwa hiyo milima hii imefaidi kipindi kirefu sana cha uthabiti wa mazingira, na pia

imetengwa na misitu mingine na kwa hakika, kati ya msitu mmoja na mwingine (Burgess et al.,1996).

Matokeo ya mabadiliko haya ni kuwa tabia za viumbe hai vya milima hii ni za namna mbalimbali na

zinaainishwa na viwango vya juu vya upatikanaji kwa wingi au unaokaribia kuwa kwa wingi (tazama

chini). Inawezekana kuwa kwa kiasi fulani kiwango cha chini cha spishi anuwai na upatikanaji wake

katika Mlima Kilimanjaro ni matokeo ya uchanga wake.

11

Msitu wa Mlima Kilimanjaro umegawanyika katika aina mbalimbali za uoto: kanda ya savana, eneo la kilimo

na misitu lililo na watu wengi, ukanda wa misitu, ukanda wa mimea (alpine) mirefu kiasi na mirefu. Kwa

mifumo ikolojia na bayoanuwai, ukanda wa misitu ni muhimu zaidi katika mlima huu, na una karibu nusu ya

spishi zote za mimea ya milima huu (Lambrechts et al., 2002).

Misitu ya kandokando ya mito (Riverine)

Misitu ya kandokando ya mto kuzunguka sehemu ya Kinamasi ya Kirua inaweza kugawanywa katika

makundi saba kama ifuatavyo (IVO-NORPLAN, 1997):

• Uoto wa kando ya mto: huu ni pamoja na uoto unaokwenda hadi mita 50 kila upande wa kingo za mto.

Kwa upande wa mashariki, spishi kuu ni Cyperaceae (mf. Cyperus alticulatus C. laevigatus) Gramineae

(mf. Phragmites mauritianus, Echnochloa Colonum) na Typhaceae (eg. Typha domingensis). Pale

ambapo kina cha ukingo wa mto ni kirefu Ficus Sur na Acacia Zanzibarica ndizo maarufu. Ukingo wa

magharibi umetawaliwa na Ficus sur, Trichilia emetica, Elaeis guineense, jamii ya Mchenje/Msesewe

(Albizia graberrima, Antidesma Venosum na A. Zanzibarica). Tabaka la vichaka vya kando ya mto

linatawaliwa na spishi kama vile Sesbania Sesbans na Phyllanthus muellerianus.

• Ardhi ya kinamasi cha Cyperus na Sesbania: katika maeneo ambayo maji hutuwama wakati wote, spishi

kama Cyperus axaltatus na Typha domingensis ndizo zinazotawala. Katika maeneo yale ambayo hupata

mafuriko kwa vipindi, Sesbania sesbands, Cyperus Laevigatus na Mkongoe (Acacia Xanthophloea) ndio

aina za pekee za miti zinazohusishwa na aina hii ya uoto. Hii ni aina ya uoto iliyo maarufu sana kwenye

eneo la kinamasi la Kirua, ingawa ni maarufu zaidi katika ukingo wa mashariki wa mto kuliko ukingo wa

magharibi. Kwa upande wa mashariki, inaweza kutanda hadi kilomita 3 kutoka mtoni, wakati ambapo

umbali mrefu zaidi ni kiasi cha mita 700 tu kutoka mtoni kwa upande wa magharibi wa mto.

• Nyanda za nyasi za Sporobolus pyramidalis na Cynodon dactylon: Jamii ya Poaceae ndio

inayotawala hapa, ikiambatana na miti michache iliyotawanyika na vichaka. Katika eneo la

Kinamasi la Kirua, aina hii ya uoto inaenea katika eneo kubwa zaidi. Inaweza kutokea kama

viunga au maeneo makubwa ya nyasi.

• Misitu ya mbao ya Mkongoe (Acacia Xanthophloea): Aina hii ya uoto hutawaliwa na spishi ya

Acacia, ambayo hufikia urefu wa hadi mita 18, na ikiwa na utando ulioziba eneo la kiasi cha

asilimia 20 ya eneo la ardhi. Aina hii ya uoto ina thamani kubwa kijamii na kiuchumi kwa wakazi

wa eneo hili oevu.

• Jangwa lenye vifungu vya Suaeda monoica: Aina ya uoto inayojieleza, ambayo kwa kawaida

hupatikana mbali kidogo na mto baada ya sehemu za uoto wa nyasi.

• Eneo la vichaka vya mpoma wa Afrika (Commiphora africana): Mwendelezo wa ukanda wa

eneo la vichaka linalotawaliwa na C. Africana ambao hupatikana chini ya Mwinuko wa Martin.

Kwa kawaida, kila kichaka kina urefu pungufu ya mita 6, na utando wake unaziba zaidi ya

asilimia 20 ya eneo la ardhi.

• Ardhi ya kilimo: Mnamo mwaka 1997, kilimo katika eneo la Kinamasi cha Kirua kilikomea kuwa

cha maeneo madogo, na kutawaliwa na mazao yanayohitaji maji mengi kama migomba na

miwa, pamoja na mahindi.

Misitu ya miombo

Misitu ya Miombo imeenea katika eneo la asilimia 50 ya Tanzania na ni uoto wa aina moja ulio mkubwa

zaidi katika Afrika ya Mashariki. Misitu ya miombo ya Afrika Mashariki ni mfumo uliodhoofishwa wa spishi

ya miombo iliyoenea sana katika Afrika ya Kati (Rogers, 1997).Inaweza kuelezewa kama ifuatavyo; ‘miti

inayopukutisha majani isiyokuwa na miiba (yenye spishi chache zenye miiba) inayojitokeza katika maeneo

ya mvua za msimu mmoja katika ardhi chakavu kijiolojia, yenye asidi, na ya mchanga. Inajulikana kwa miti

ya jamii ndogo ya Caesalpinoideae, hususan spishi za jamii ya myombo (Brachystegia na Julbernadia).

12

Tabaka la vichaka linatofautiana kwa unene, asilimia ya ueneaji na spishi zilizomo. Mara nyingi hutawaliwa

na Mgoto/Mtobwe (Diplorhynchus na Combretum spp). Utando wa ardhi hutofautiana kutoka kwenye nyasi

nyingi hadi kwenye vichaka haba na nyasi ndogo ndogo. Muundo na spishi zilizomo kwa kiwango kikubwa

unadumishwa na mioto ya vipindi vya msimu (Rogers, 1996:301). Kiasi cha kilomita za mraba millioni 3 za

Afrika zimefunikwa na misitu ya miombo. Katika Bonde la Mto Pangani imeenea zaidi katika maeneo ya

mwambao, pande zote mbili za Kaskazini na Kusini mwa mdomo wa Mto Pangani.

Tishio na Hadhi ya Hifadhi

Kwenye Mlima Kilimanjaro, misitu inaendelea kutishiwa kuingiliwa zaidi na zaidi kutokana na uvamizi wa kilimo,

ambacho kinatokana na ongezeko la idadi ya watu. Vitisho vingine vya ziada ni ukataji wa miti kwa ajili ya mbao,

uanzishwaji wa mashamba ya miti ya mbao laini, moto, uvunaji haramu uliokithiri wa miti ya mbao, ujangili

na urinaji haramu wa asali (Yanda na Shishira, 2001). Katika sehemu zote isipokuwa katika mitelemko ya

Kaskazini, ukataji haramu wa magogo hufanyika kwa wingi katika maeneo ya msitu yaliyo chini ya mita 2,500,

ilikoenea zaidi miti ya kafuri, seda na miti mingine ya asili (Lambrechts et al., 2002). Tishio la ziada ni pamoja

na uanzishaji wa ‘vijiji vya misituni’ (ambako viko 18 kwenye eneo la hekta 215) ndani ya hifadhi ya msitu.

Mashamba pia yanazidi kuwa ya kawaida katika hifadhi. Mwezi Agosti, mwaka 2001, kulikuwa na matanuru 125

ya mkaa yaliyoonekana katika mitelemko ya Kusini Mashariki ya mlima (Lambrechts et al., 2002). Uchungaji wa

mifugo hufanyika kufikia kilomita 8 ndani ya msitu, na katika mwezi Agosti, mwaka 2001 wanyama wafugwao

814 walihesabiwa, wengi wao wakiwa kwenye mitelemko ya Kaskazini ya mlima (Lambrechts et al., 2002).

Kati ya mwaka 1952 na 1982, eneo la misitu ya asili ya Kilimanjaro ilipungua kwa kilomita za mraba 41. Maeneo

ambapo awali misitu ya asili ilikuwepo sasa nafasi yake imechukuliwa na kilimo au uoto ulioharibiwa. Kingo za misitu

ya hifadhi ndizo zilizoharibiwa vibaya zaidi, (Yanda na Shishira, 2001) hususan kwenye sehemu zijulikanazo kama

‘ukanda wa nusu maili’. Mnamo mwaka 1941, serikali ya kikoloni ilitenga eneo la hifadhi ya msitu wa Kilimanjaro

kama eneo la msitu wa kilimo. Ukanda huu umeenea kati ya Mito Kikuletwa na Sanya, na mwendo wa nusu maili

kwenda juu ya mlima kutoka kwenye ukingo wa hifadhi. Huu ‘ukanda wa nusu maili’ ulikusudiwa kupandwa miti

ikuayo haraka kwa ajili ya matumizi ya jamii za Wachaga waishio chini ya hifadhi, ambako uhaba wa ardhi ulizuia

upandaji wa miti (Baldwin, 1946). Leo, kadiri ya asilimia 66 ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya mashamba ya

misitu yamekuwa ya kilimo au yamesafishwa, (Lambrechts et al., 2002).

Jedwali la 2: Upotevu wa utando wa msitu wa Milima ya Tao la

Mashariki katika Bonde la Mto Pangani

Msitu Msitu wa asili Idadi ya Viunga Msitu Upotevu wa tando

(km 2 ) vya misitu uliofungwa wa asili wa

(km 2 ) msitu (%)

Pare ya Kaskasini 151 2 28 50

Pare ya Kusini 333 5 120 73

Usambara Magharibi 328 17 245 84

Usambara Mashariki 413 8 221 57

Taita 6 13 4 98

Rejea: Newmark, 1998:4)

Katika Bonde la Mto Pangani, Milima ya Tao la Mashariki ipo kwenye maeneo yenye msongamano mkubwa wa

watu. Katika Milima ya Usambara Magharibi kwa mfano, idadi ya watu imeongezeka kwa mara 23 tangu 1900

(Newmark, 1998). Katika mazingira ya kijamii yenye sifa ya umaskini, umuhimu wa ardhi ya kilimo hauwiani kwa

kiasi kikubwa. Shinikizo linalowakilishwa na tatizo hili kwenye hifadhi zilizobaki za misitu katika bonde linatisha.

Ikidhaniwa kuwa Milima ya Tao la Mashariki, kihistoria ilikuwa karibu muda wote imejaa misitu, asilimia yake 77

itakuwa imepotea kutokana na shughuli za binadamu na/au moto katika miaka 2,000 iliyopita (Newmark, 1998).

Tatizo la ziada ni kuwa mingi ya michakato hii imesababisha kutokea kwa viunga vya misitu, na spishi za wanyama

13

mara nyingi haziko tayari kuvuka nafasi wazi kati ya viunga vya misitu. Hii ina maana kuwa katika viunga kimoja

kimoja, mkusanyiko wa jeni hupungua na uhai wa spishi huhatarishwa kutokana na kuzaliana wenyewe kwa

wenyewe. Katika Bonde la Mto Pangani upotevu huu ni kama inavyoonyeshwa katika jedwali la 2.

Hadhi ya msitu kuwa “msitu wa hifadhi” inaonekana kushindwa kupunguza viwango vya ukataji miti. Katika Hifadhi

ya Msitu ya Nilo (hekta 5872.1), katika Milima ya Usambara, kuna hekta 33.8 za ‘kilimo chini ya msitu’, hekta 372.3

za kilimo cha ‘wakulima wadogo wadogo’, hekta 37.2 za ardhi tupu na hekta 1.9 za makazi ya binadamu (Cordeiro,

1998). Misitu ya Pwani ya Tongwe-Muheza ilikuwa na eneo la hekta 1,202, lakini ni hekta 300 tu za msitu zilizobaki,

wakati ambapo Hifadhi ya Msitu wa Gombero imefyekwa kabisa kwa ajili ya kilimo (Baker na Baker, 2002).

Kwenye Mlima Meru, matatizo yanayoikabili misitu yanafanana na yale yanayoutishia Mlima Kilimanjaro,

nayo ni kama yafuatavyo (Bwoyo, mhojiwa):

• Ukataji haramu wa miti – Misitu ya milimani huvunwa miti inayovutia kibiashara ya mireteni

(Juniper) na Mshio (Olea Capensis).

• Malisho – Wakati wa msimu wa kiangazi, jamii za jirani hulisha mifugo yao ndani ya msitu.

• Uhaba wa ardhi – upande wa Mashariki wa mlima, uvamizi wa ardhi ni tatizo kubwa

linaloongezeka.

• Kutokuungwa mkono - katika baadhi ya vijiji, mradi wa msitu wa maeneo ya vyanzo vya maji

(CFP – utakaoelezwa chini) huungwa mkono kwa kiwango kidogo na viongozi wa vijiji, ambao

baadhi yao wanahusika binafsi na uvunaji wa msitu.

• Moto – hili lilikuwa tatizo kubwa kati ya miaka ya 1998 na 1999.

Kisanduku cha 4: Tishio kwa Misitu ya Bonde la Mto Pangani

• Mahitaji ya ardhi: kadri msongamano wa watu unavyoongezeka na uchumi unavyobaki kuwa duni,

mahitaji ya ardhi ya kilimo huongezeka, na hivyo, misitu hukatwa kutoa nafasi ya kilimo.

• Mahitaji ya mbao: misitu mingi iliyobaki katika PRB ina spishi za mbao zenye thamani ya kiuchumi,

ambayo, jinsi inavyoadimika, ndivyo inavyopata bei kubwa. Miti pia hukatwa kwa ajili ya kuni na

utengenezaji wa mkaa.

• Mahitaji ya malisho: idadi ya mifugo katika bonde inaonekana kuongezeka. Jinsi ardhi ya kilimo

inavyoongezeka, ardhi ya malisho hupungua, na wafugaji hupanda milima kutafuta malisho.

• Makazi ya msituni: kadri watu wanavyojitahidi kutafuta kuongeza ardhi ya kilimo na malisho, hivyo

pia hufanya makazi ndani ya mipaka ya misitu.

• Udhaifu wa Sheria: licha ya hadhi ya uhifadhi wa misitu mingi ya bonde, mamlaka haziwezi kutekeleza

sheria zinazotakikana kwa sababu ya uchache wa wafanyakazi, mishahara duni na rushwa. Kwa

nyongeza, Idara ya Misitu na Nyuki na Mradi wa Misitu ya vyanzo vya maji inapatiwa fedha karibu

zote na wahisani pekee, hali inayoibua maswali kuhusu uendelevu wake. Mwisho, ushirikishwaji wa

jamii katika usimamizi wa misitu ya bonde ni dhana ngeni na kwa sasa haijawa na ufanisi mkubwa.

• Uendelezaji wa misitu: uendelezaji wa misitu ya mashamba badala ya misitu ya asili huongeza

matatizo ya uhifadhi.

• Kugawanyika kwa misitu: Jinsi shinikizo linavyozidi kwenye misitu ya bonde mara nyingi hugawanyika

vipande vipande. Spishi nyingi za msituni haziwezi kuvuka nafasi wazi kati ya msitu, na hivyo

kusababisha matatizo ya uhifadhi wa bayoanuwai.

• Moto: Kwa kawaida huanzishwa na binadamu ama makusudi (ili kuharibu misitu inayodhaniwa

kuhifadhiwa isivyostahili na iliyozuiliwa) au kwa kawaida zaidi, ajali (kwa mfano, kutokana na ajali

wakati wa kuchoma mkaa au kurina asali kutoka kwenye mizinga).

14

• Fedha – CFP haipati fedha zozote kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake kutoka serikalini.

Bwoyo (mhojiwa) anadai kuwa kwa sababu ya mchango muhimu wa misitu katika Bonde la Mto

Pangani, kiasi cha fedha lazima kitengwe kwa ajili ya CFP kutoka kwa makampuni yazalishayo

umeme wa maji au Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani (angalia pia Evans, 1997).

B.3 Maji na ardhioevu

Mto Pangani unaundwa na matawi ya mito mikubwa miwili: Mto Ruvu, ambao hutokea kwenye miteremko

ya Mashariki ya Mlima Kilimanjaro; na Kikuletwa, ambao hutokea kwenye Mlima Meru na mitelemko ya

Kusini ya Mlima Kilimanjaro. Mito ya Ruvu na Kikuletwa huungana katika Bwawa la Nyumba ya Mungu,

lenye eneo la kadiri ya kilomita za mraba 140 (Rohr na Killingtveit, 2002). Maji yanayoingia katika bwawa

yanakaribia kuwa mita za ujazo 43.37 kwa sekunde (TANESCO, 1994). Mto unapotoka kwenye bwawa,

huitwa Mto Pangani, na hutiririka kwa kilomita 432 kabla ya kuingia katika Bahari ya Hindi, ambako

humwaga maji ya kiasi cha kilomita za ujazo 0.85 kwa mwaka (Vanden Bossche na Beracsek, 1990).

Ndani ya Bonde la Mto Pangani, Mlima Kilimanjaro ndio sehemu yenye umuhimu wa pekee

kihaidrolojia(Lambrechts et al., 2002). Kama ilivyoelezwa awali, mvua kwenye mlima huu zinakadiriwa

kutoa asilimia 60 ya maji yanayoingia katika Bwawa la Nyumba ya Mungu, na asilimia 55 ya maji ya juu

ya ardhi katika Bonde (Rohr na Killingtveit, 2002). Pia, cha muhimu – ingawa kiasi hakijulikani, ni maji

yatokanayo na kuyeyuka kwa barafu kutoka milimani. Barafu inayoyeyuka kutoka mlimani huipa nguvu

chemchemi kuu katika hifadhi maarufu ya Taifa ya Amboseli nchini Kenya. Myeyuko pia huzipa nguvu

chemchemi ambazo mradi wa Ugavi wa Maji wa Nol Turesh ya Kenya hutegemea, unasambaza maji

kwenye miji kadhaa mashuhuri ya Kenya, ikiwa ni pamoja na Machakos na Kajiado.

Maji katika Bonde la Mto Pangani kwa kiasi kikubwa hutokana na mvua, ambayo mgawanyo wake hauko

sawa ndani ya bonde. Kwa wastani, bonde hili hupata mita za ujazo 34, 773.4 kwa mwaka na kiasi cha

wastani cha upoteaji maji kwa uchavushaji ni milimita 1,410 kwa mwaka. Kwa kuzingatia tofauti za mvua,

bonde hili, linaweza kugawanywa katika mifumo miwili ya kihaidrolojia.

Maeneo ya nyanda za juu yanachukuliwa kuwa ni yale yaliyoko mita 900 juu ya usawa wa bahari, kama vile

mitelemko ya Milima Meru na Kilimanjaro, pamoja na maeneo ya Milima ya Usambara na Pare, ambayo

hupata mvua kati ya milimita 1,200 na 2,000 kwa mwaka. Misimu ya mvua huwa miwili katika maeneo haya,

nyingi ikiwa kati ya miezi ya Machi na Mei na kidogo kati ya miezi ya Oktoba na Novemba. Mvua katika

kipindi cha kwanza inaweza kuzidi milimita 600 kwa mwezi, na milimita 300 katika kipindi kinachofuata.

Kisanduku 5: Taarifa za Msingi za Maji na Ardhioevu

katika Bonde la Mto Pangani

• Maeneo ya nyanda za juu ya Bonde la Mto Pangani hupata mvua nyingi kuliko nyanda za chini.

Hivyo kilimo kinafanyika zaidi kwenye nyanda za juu wakati nyanda za chini zinafaa kwa ufugaji.

• Sehemu kubwa ya maji ya Mto Pangani hutokana na mvua na myeyuko wa barafu.

• Kiasi kikubwa cha maji yanayoingia kwenye Bwawa la Nyumba ya Mungu yanatoka Mlima

Kilimanjaro. Yaliyobaki yote yanatoka Mlima Meru na Milima ya Pare Kaskazini.

• Matumizi makuu ya maji katika Bonde hili ni umwagiliaji mashamba. Uzalishaji umeme na uvuvi

ni matumizi ya muhimu ya ziada, kama yalivyo mahitaji ya mijini na viwandani.

• Bonde la mto Pangani lina rasilimali kubwa ya maeneo ardhioevu, ikiwa ni pamoja na ziwa Jipe

na Chala, na Bwawa la Nyumba ya Mungu. Yote haya husaidia uvuvi. Bonde hili lina rasilimali

nyingi za kinamasi, ingawa mchango wake kihaidrolojia na bayoanuwai haujulikani sana.

15

Juu ya bwawa la Nyumba ya Mungu, kwa

ujumla mvua imepungua tangu uwekaji

wa kumbukumbu ulipoanza mwanzoni

mwa miaka ya 1930. Mfumo wa sasa

wa mvua kwa kawaida hutofautiana kwa

asilimia 10 kutoka wastani. (Mkhandi na

Ngana, 2001).

Maeneo yaliyo chini ya mita 900 hupata

mvua kidogo zaidi katika Bonde hili,

ikipungua kufikia milimita 500 kwa mwaka

(Mkhandi na Ngana, 2001). Kwa hakika

asilimia 50 ya Bonde la Mto Pangani

inachukuliwa kuwa kame au nusu kame

(Rohr na Killingtveit, 2002).

Vyanzo vya ziada vya maji katika

bonde hili ni chemchemi. Baadhi ya

chemchemi zilizo kubwa katika bonde

hili huchangia kadri ya mita za ujazo 20

kwa sekunde za maji yaingiayo bwawa

la Nyumba ya Mungu, kiasi ambacho

kinakuwa muhimu sana wakati wa

kiangazi ambapo mchango wa mvua

hupungua (Rohr et al., 2002). Sehemu

kubwa ya chemchemi zinazozalisha maji

katika Bonde imejikusanya zaidi katika

maeneo matatu ya mkoa wa Kilimanjaro:

Kambi ya Choka, Rundugai na Chemka

Kisanduku 6: Tishio kwa rasilimali za maji na

ardhioevu ya Bonde la Mto Pangani

• Ifikapo mwaka 2015, mahitaji ya maji katika Bonde

hili yanatarajiwa kuwa mara mbili, wakati huo huo

kuna ushahidi uhaba wa maji umekuwepo tangu

miaka ya 1940.

• Maeneo muhimu ya matatizo ni ongezeko la mahitaji

ya umwagiliaji na mijini. Katika umwagiliaji, upotevu

wa maji unaweza kufikia kiasi cha asilimia 85.

• Kadri idadi ya watumiaji maji inavyoongezeka,

pamoja na ushindani baina yao, kuna uwezekano

wa migogoro baina ya watumiaji maji kuongezeka.

• Uvuvi katika Bwawa la Nyumba ya Mungu

unasemekana kuwa katika matatizo makubwa

kutokana na uvuvi uliokithiri.

• Sehemu kubwa ya eneo ardhioevu kubwa zaidi katika

Bonde hili - Kinamasi cha Kirua – imekauka kutokana

na utaratibu wa mtiririko wa maji yanayotoka kwenye

Bwawa la Nyumba ya Mungu kudhibitiwa.

• Kiasi kikubwa cha virutubisho vinavyoingia kwenye

Ziwa Jipe vimestawisha kwa wingi mafunjo na Typha

ambazo zinatishia kulifunika ziwa.

(Rohr et al., 2002). Chanzo cha maji ya chemchemi iliyotajwa mwisho haijulikani na kiwango cha maji

kitokacho hubaki kuwa sawa kwa mwaka mzima. Mfumo wa mvua kwenye Mlima Kilimanjaro, ambao

uko upande wa Kaskazini wa chemchemi, unaonekana kutokuwa na athari yoyote kwenye utoaji wa

maji wa chemchemi hiyo (Rohr et al. 2002). Nchini Kenya, Mto Lumi hukusanya maji kutoka mitelemko

ya Kusini ya Mlima Kilimanjaro na ndio chanzo kikuu cha maji ya Ziwa Jipe. Karibu maji yote ya mto

yanayoingia kwenye ziwa hili yanatoka kwenye chemchemi (Musyoki, 2003).

Kiasi cha asilimia 5 ya maji yote yanayotumika katika Bonde la Mto Pangani yanatoka katika vyanzo vya

chini ya ardhi. Visima virefu vitoavyo zaidi ya mita za ujazo 100 kwa saa vimechimbwa kwenye ukanda

wa Kahe wakati visima vinavyotoa kati ya mita za ujazo10–50 kwa saa vimechimbwa katika ukanda

wa Sanya na Miamba ya Karoo ya Tanga. Uongezekaji wa maji ya chini ya ardhi kwa kiasi kikubwa

unatokana na mvua na mito (Makule n.d.).

Mto Pangani unapotoka kwenye Bwawa la Nyumba ya Mungu, hukabiliwa na mahitaji yafuatayo

(Mujwahuzi 2001):

Kiasi cha chini kwa kuzalisha umeme.................................mita za ujazo 24 kwa sekunde

(Firm Power Production)

Umwagiliaji..........................................................................mita za ujazo 7 kwa sekunde

Matumizi ya nyumbani .......................................................mita za ujazo 1-2 kwa sekunde

Jumla..................................................................................mita za ujazo 32-33 kwa sekunde

16

Hata hivyo, Sarmett (Mhojiwa) anaeleza kuwa, ni mara chache sana Nyumba ya Mungu huwa na uwezo

wa kutoa mita za ujazo 22 kwa sekunde.

Bwawa la Nyumba ya Mungu ndiyo hifadhi kubwa zaidi ya maji katika bonde hili. Nyingine tatu zilizopo

ni: ziwa Ambusseli, na maziwa Chala na Jipe yaliyoko mpakani mwa Tanzania na Kenya. Maziwa haya

huonekana mara nyingi kwenye mipango ya umwagiliaji na ya kihaidrolojia ya wilaya ya Taita -Taveta ya

Kenya. Usawa wa maji ya Ziwa Jipe na eneo lake hubadilika kwa kiwango kikubwa kutokana na kiasi

cha mvua. Hivyo, eneo lake hutofautiana kutoka kilomita za mraba 28 (1947) hadi kilomita za mraba 18

(1954), wakati kiasi cha maji yaliyomo hutofautiana kutoka mita za ujazo milioni 20 hadi 60, (Musyoki

na Mwandotto, 1999). Ndani ya Kenya sehemu ambayo ni chanzo cha maji ya Ziwa Jipe kuna sehemu

ya Mbuga ya Taifa ya Tsavo Magharibi, kilomita za mraba 48.5 za kinamasi, kilomita za mraba 435

za mashamba ya mkonge na kilomita za mraba 196.5 za kile kinachoelezwa kuwa ni ‘ardhi ya umma’

iliyotengwa kwa ajili ya Mpango wa Makazi wa Ziwa Jipe (Musyoki na Mwandotto 1999). Kiasi cha

mchangatope unaokadiriwa kufikia tani 300,000 huingia kwenye ziwa kwa mwaka (Musyoki, 2003).

Ziwa Chala liko kwenye kreta ndogo ya volkano ya miteremko ya kusini ya Mlima Kilimanjaro. Lina

kina cha kati ya mita 85 na 90 na lina eneo la kiasi cha kilomita za mraba 3.15. Lina kiasi cha maji ya

kati ya mita za ujazo milioni 300-350 (Musyoki na Mwandotto 1999). Kwa ubora, maji yake ni mzuri

sana, na kwa sababu hii yanaonekana kuwa ndiyo chanzo cha ukuaji wa maeneo ya miji ya pwani ya

Kenya. Viwango vya matumizi ya maji kwa siku zijazo vinatazamiwa kufikia mita za ujazo 7 kwa mwaka

(Musyoki, 2003). Hali yake ya mwinuko inamaanisha kuwa maji yanaweza kusafirishwa kwa nguvu ya

mteremko hadi yanakotakiwa.

Bonde la Mto Pangani linadhaniwa kuwa na hekta 90,000 za kinamasi, sehemu yake kubwa ikiwa ni

Kinamasi ya Kirua iliyopo Kusini mwa Bwawa la Nyumba ya Mungu. Vinamasi hivi tayari vimekwisha

athirika kwa kiasi kikubwa kutokana na udhibiti wa mtiririko wa maji ya mto kutoka bwawani, na maeneo

makubwa ya kinamasi yamekauka. Hata hivyo, bado yanadhaniwa kuhifadhi kiasi kikubwa cha maji

ya Mto Pangani. Laiti kama Mto ungeelekezwa njia na mfereji kuchimbwa kupitia kwenye kinamasi,

ongezeko la mita za ujazo milioni 42.4 zingeyafikia mabwawa yaliyoko upande wa chini ya mto kwa

mwaka (IVO - NORPLAN,1997). Uoto wa ardhi hizi za kinamasi umeelezewa juu kuwa ni mifano ya

misitu ya kandokando ya mito.

Ardhi nyingine ya Kinamasi ni Ruvu (karibu kilomita za mraba 35) ambayo iko mahali Mto Ruvu

unapotoka kwenye Ziwa Jipe, na kinamasi iliyopo mahali mito ya Ruvu na Kikuletwa inapokutana na

kuingia Nyumba ya Mungu. Eneo la kinamasi lililotajwa mwisho linasemekana kuwa na kilomita za

mraba 40 (Baker na Baker 2001).

Tishio na hadhi ya Hifadhi

Katika sehemu ya Bonde iliyoko Tanzania, makisio na matarajio ya mahitaji ya maji kwa mwaka 1995 na

2015 yanaonyeshwa kwenye Jedwali la 3.

Katika Wilaya ya Taita – Taveta iliyoko katika sehemu ya bonde upande wa Kenya, mahitaji ya maji

yanakadiriwa kufikia mita za ujazo 5,625 kwa siku. Hadi kufikia mwaka 2005 mahitaji yanatazamiwa

kuongezeka kufikia mita za ujazo 8,844 kwa siku, na kufikia mita za ujazo 12,521 kwa siku ifikapo

mwaka 2015 (Mpango wa Maji wa Wilaya ya Taita – Taveta wa mwaka 1995, kama inavyonekana katika

Musyoki, 2003). Kutokana na mahitaji ya maji kukadiriwa kuwa mara mbili itakapofika mwaka 2015,

shinikizo kwa rasilimali za maji katika bonde linafikiriwa kuwa kubwa mno. Tayari bonde linachukuliwa

kuwa lina matumizi makubwa ya maji, na kwa kukosekana msisitizo wowote mkubwa wa udhibiti hadi

sasa, inaonekana hakuna uwezekano wa tishio hili kupungua.

17

Jedwali la 3: Makadirio ya mahitaji ya maji mwaka 1995 na

matarajio ya mahitaji ya maji mwaka 2015

Mahitaji ya maji m 3 /siku

Matumizi 1995 2015

Mijini 71,200 163,600

Vijijini 52,000 83,500

Mifugo 30,500 36,400

Mkonge 1,300 1,300

Jumla 155,000 284700

(Rejea: IVO- NORPLAN, 1997)

Upo ushahidi wa kutosha wa matatizo ya maji. Mujwahuzi (2001) anabainisha kuwa katika kituo 1DC1

cha Mto Ruvu, wastani wa mtiririko wa maji kwa mwezi umepungua kutoka mita za ujazo 14.2 kwa

sekunde kati ya mwaka 1958 – 65 hadi mita za ujazo 11.45 kwa sekunde kati ya mwaka 1987-97. Vijito

vingi katika nyanda za juu za bonde havitiririshi maji wakati wa msimu wa kiangazi (mwezi Septemba

hadi Februari) kwa sababu ya wingi wa shughuli za umwagiliaji. Baada ya maji kuchukuliwa kwa ajili

ya umwagiliaji, Mto Rau hukauka kabisa (Mujwahuzi 2001). Mahitaji ya maji kutoka kwenye mito ya

Kikafu na Weruweru huwa ni kati ya asilimia 90 –125, ambayo ni makubwa zaidi ya kiasi cha maji

kinachopatikana kwa uhakika mtoni cha asilimia 80. (Mwamfupe, 2002). Maji yanayotoka katika Bwawa

la Nyumba ya Mungu, huchepushwa kwa matumizi mbalimbali kabla ya kufika kwenye maporomoko

ya Pangani. Mara nyingi na hususan wakati wa kiangazi, maji yanayofika hayatoshelezi kuendesha

mitambo ya kituo cha umeme wa maji iliyopo hapo (Lugeiyamu, Mhojiwa). Ushahidi wenye nguvu sana

wa tatizo la maji unaweza kuwa ni ongezeko la idadi ya migogoro inayohusiana na maji katika bonde hili.

Migogoro hii inaangaliwa kikamilifu hapa chini.

Kati ya mwaka 1992 na 1989, eneo la kilele cha barafu cha Mlima Kilimanjaro lilipungua kwa asilimia 75

kutoka kilomita za mraba 12.5 hadi kilomita za mraba 2.6. Kati ya mwaka 1989 hadi 2000 karibu robo

ya barafu iliyosalia ilitoweka. Kuhusu sababu ya badiliko hili la ghafla na haraka, lawama zinaelekezwa

katika shughuli za binadamu, ingawa hili kwa vyovyote haliko dhahiri (Hastenrath na Greischar, 1997).

Kama upunguaji huu utaendelea Bonde la Mto Pangani hivi karibuni litakoma kupata maji yatokanayo

na kuyeyuka kwa barafu.

Ukuaji wa magugu aina ya Typha kwenye Ziwa Jipe unasemekana kutodhibitiwa vya kutosha kiasi

kwamba magugu haya yamekaribia kufunika ziwa. Mwelekeo huu ni dhahiri umetokana na virutubisho

na mchangatope unaochukuliwa na maji kutoka kwenye Mlima Kilimanjaro na Milima ya Pare Kaskazini.

Mchangatope umepunguza kina cha Ziwa na kusababisha kupanda kidogo kwa usawa wa maji. Uingiaji

wa virutubisho kwenye ziwa unadhaniwa kusababisha ongezeko la alikali na/au magadi na kusababisha

mayungiyungi kutoweka. Uingiaji wa mchangatope pia huathiri bwawa la Nyumba ya Mungu, lakini hili si

tatizo kwa sasa kutokana na bwawa kuwa na eneo kubwa la kuhifadhi maji.

Kama ilivyojadiliwa awali, udhibiti wa Mto Pangani umepunguza mafuriko katika kinamasi ya Kirua, na hivyo

maeneo makubwa ya kinamasi kukauka. Kwa kiasi cha utoaji wa maji cha mita za ujazo 25 kwa sekunde kutoka

NYM, kinamasi kinafurika, lakini wakulima waliovamia ardhi hii hulalamika vikali (Ngula, Mhojiwa). Bwawa la

Nyumba ya Mungu husaidia uvuvi ambao hufanyika kwa kiwango kikubwa, kama itakavyojadiliwa zaidi chini.

18

B.4 Maeneo Yaliyohifadhiwa

Katika Tanzania, Bonde la Mto Pangani lina hifadhi moja ya akiba ya wanyamapori (Mkomazi – kilomita

za mraba 3,276), wakati sehemu za Hifadhi za Taifa za Kilimanjaro (kilomita za mraba 756) na Arusha

(kilomita za mraba 137) pia zipo katika bonde hili. Sehemu ya Mbuga ya Hifadhi ya Taifa ya Tsavo

Magharibi nchini Kenya (kilomita za mraba 9,065) pia inaangukia katika bonde hili, na inapakana na

hifadhi ya akiba ya Wanyamapori ya Mkomazi. Sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Sadani iko katika bonde hili,

lakini haitajadiliwa hapa. Kihoja, hifadhi za misitu pia ni maeneo yaliyohifadhiwa, lakini haya hayajadiliwi

hapa (angalia juu). Zote hizi zina mchango wenye thamani kwa uchumi wa Tanzania kwa kuvutia watalii.

Kilimanjaro pekee hupokea wageni wapatao 67,000 kwa mwaka (WCMC, 1987).

Mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu zaidi uliosimama wenyewe duniani na mrefu zaidi kuliko yote katika

Afrika. Una mwinuko wa mita 5,000 juu ya uwanda wazi wenye milima na mabonde wa wastani wa

mita 800 juu ya usawa wa bahari (Lambrechts et al., 2002). Mbuga hii ni eneo lililohifadhiwa zamani

zaidi katika Afrika, likiwa limepata hadhi hii mwanzoni mwa karne ya 20. Mnamo mwaka 1921 mbuga hii

ilitangazwa kuwa hifadhi ya msitu, na kisha, katika mwaka 1973, eneo lililo juu ya mita 2,700 za kontua,

lilipewa hadhi ya Hifadhi ya Taifa. Kwa sasa, mbuga hii ina eneo la hekta 75,353 na imezungukwa na

hekta 107,828 za hifadhi ya misitu (Lambrechts et al,2002). Mnamo mwaka 1987 Mbuga ya Hifadhi

ya Taifa ya Kilimanjaro iliwekwa katika orodha ya maeneo ya Urithi wa Dunia, ikiwa eneo la saba la

Tanzania la Urithi wa Dunia (Lambrechts et al.,2002).

Hifadhi ya akiba ya Wanyamapori ya Mkomazi ni mwendelezo wa Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Magharibi

ya Kenya. Kama zilivyo Hifadhi za Taifa za Tsavo na Arusha, Mkomazi ipo katika mpango wa kituo cha

uendelezaji wa wanyama cha ukanda wa Somali – Masai (Somali – Maasai Regional Centre of Endemism,

RCE). Inatanda toka mpakani mwa Tanzania na Kenya hadi chini ya milima ya Pare na Usambara Magharibi.

Hifadhi hii ina tabia ya misitu ya savana, na mpaka mwaka 1988, wafugaji kutoka makabila mbalimbali

waliruhusiwa kunufaika na malisho yake. Homewood na Brockington (1999) wanaeleza kuwa ingawa

hifadhi hii ina manufaa makubwa kwa Tanzania kwa kuwa na hazina kubwa ya bayoanuwai umuhimu wake

umefunikwa kwa kiasi kikubwa na kanda nyingine zenye hazina kubwa zaidi za bayoanuwai, bila kusahau

Milima ya Pare na Usambara. Keith Eltringham et al., (1999) alibainisha kuwepo kwa spishi 102 za wanyama

wanaonyonyesha (mamalia) ndani ya Mkomazi, wakiwemo Faru weusi walioletwa tena hivi karibuni.

Mbuga ya Taifa ya Arusha iko kwenye kingo za Mlima Meru (mita 4,565) na ilianzishwa mwaka 1967.

Mbuga ina mazingira ya aina nyingi mbalimbali, mifano mizuri ni pamoja na misitu ya milimani kwenye

Mlima Meru, Maziwa ya Kreta ya Momela na nyanda za chini za nyika za savana na misitu ya miombo.

Orodha ya ndege waliopo katika mbuga hii ina spishi 400, na ni moja ya mbuga chache za Tanzania

ambazo mbega weusi na weupe huonekana kwa kawaida. Mbuga hii inapakana na Hifadhi ya akiba ya

Wanyama ya Mlima Meru yenye eneo la kilometa za mraba 300. Mbuga ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha

inaaminika kuwa na msongamano mkubwa zaidi wa twiga duniani.

Barabara kuu ya Nairobi-Mombasa hutenganisha Mbuga za Hifadhi za Tsavo Magharibi na Tsavo Mashariki.

Hifadhi hizi zilizoanzishwa mwaka 1948, kwa pamoja zinaunda mbuga ya hifadhi ya Taifa kubwa kuliko

zote nchini Kenya, na moja ya maeneo makubwa zaidi yaliyohifadhiwa duniani. Mnamo mwaka 1983,

mipaka ya Kaskazini Magharibi ya hifadhi ya Tsavo Magharibi ilipanuliwa na kuchukua vilima vya Chyulu

ambavyo ndivyo chanzo kikuu cha chemchemi za Mzima ambazo ni maarufu katika mbuga hii. Lita milioni

225 za maji hububujika kutoka kwenye chemchemi hizi kila siku, ambayo huipatia maji Mombasa, jiji la

pili kwa ukubwa nchini Kenya. Zaidi ya watu 150,000 hutembelea Tsavo Magharibi kila mwaka. Sura ya

makunyanzi ya hifadhi hii ilisababishwa na milipuko ya zamani ya volkano, iliyoacha mikondo ya mtiririko

wa lava yake, maeneo ya vipande vya lava na pia koni ndogo ndogo za volkano. Mbuga hii ina idadi kubwa

zaidi ya tembo walioko Kenya. Eneo la mbuga la Ngulia limekuwa moja ya maeneo muhimu sana nchini

Kenya ya hifadhi ya faru. Milima ya miamba iliyoko Ngulia ndiyo kituo muhimu cha mapumziko kwa ndege

wahamaji wanaotoka katika Kizio cha Kaskazini, ambao wengi wao ni adimu sana.

19

Tishio na hadhi ya Hifadhi

Mwishoni mwa miaka ya 1980, Idara ya

Wanyamapori nchini Tanzania iliona Mkomazi

kuwa ni eneo lililoishiwa na mimea na

wanyama. Miongoni mwa matatizo yaliyoikabili

mbuga ilikuwa kutoweka kwa faru. Katikati ya

miaka ya 1960 kulikuwa na takriban faru 150

katika hifadhi hii, lakini spishi hii ilimalizwa,

hasa kutokana ujangili. Mnamo mwaka 1997

faru waliletwa tena kwenye hifadhi hii (Keith

Eltringham et al., 1999) pamoja na mbwa

mwitu. Hali ya mbuga hii kuwepo jirani na

mpaka wa Kenya inaleta tishio la ujangili.

Kisanduku cha 7: Tishio kwa Maeneo

yaliyohifadhiwa ya Bonde la Mto Pangani

• Sehemu kubwa ya mbuga katika Bonde la Mto

Pangani ziko katika tishio la ujangili.

• Hatari zinazoikabili Mbuga ya Taifa ya Kilimanjaro

zinahusiana zaidi na kuingiliwa katika hifadhi yake

ya misitu na uvuniaji wa mbao.

• Idadi kubwa ya watalii katika Mlima Kilimanjaro

husababisha matatizo makubwa ya utupaji

hovyo na kiasi kikubwa cha taka, kwani takataka

huganda na haziozi

Kilimanjaro haionekani kukabiliwa na tishio la aina hii la ujangili. Hapa, tishio lipo hasa kwenye mipaka ya

hifadhi ya misitu, ambako ukataji miti, kilimo, ukusanyaji wa kuni na uchomaji wa mkaa umeshamiri. Tatizo

la ziada kwenye mbuga hii ya hifadhi ya taifa ni idadi kubwa ya wageni wanaoitembelea, ambao huacha

takataka nyingi , ambazo haziwezi kuoza katika hewa nyepesi na baridi sana ya mlimani.

Maeneo yanayozunguka Mbuga ya Taifa ya Arusha yana idadi kubwa ya watu na inasemekana mbuga

inakabiliwa na tishio la kuingiliwa na shughuli za binadamu na kiwango kikubwa cha ujangili (WCMC, 1985).

Mbuga ya Taifa ya Tsavo Magharibi inakabiliwa na matatizo makubwa ya ujangili. Uuaji wa tembo katika

mbuga siku zilizopita mara nyingi ulikuwa ukielezewa mfululizo katika vyombo vya habari. Zaidi ya hayo,

mbuga hii iko katika ukanda wa ukame na hali ya hewa inayobadilika badilika, hali inayoifanya mbuga hii

kuwa katika hatari ya moto. Mioto pia ni tatizo katika Mlima Kilimanjaro, kama ilivyojadiliwa hapo juu.

Rasilimali nyingine za wanyamapori pia hupatikana katika bonde zima, wakiwemo wengi wa wanyamapori

wanaopatikana katika misitu ya milima ya Tao la Mashariki na ile ya Pwani. Tishio kwa msitu huu uliotajwa

mwisho ni kubwa sana (angalia chini). Katika nyika za Masai za uwanda wa chini wa bonde, wanyama

wenye kwato hupatikana, wakati mto na maeneo ardhioevu mengine yana hazina ya wanyama pori pia.

B.5 Bayoanuwai na hifadhi

Kenya na Tanzania zina utajiri mkubwa wa rasilimali za bayoanuwai. Kulingana na idadi ya spishi kwa

eneo, Kenya ina kiwango cha juu cha tatu kwa mamalia anuwai katika Afrika, cha pili kwa ndege anuwai

na cha tatu kwa reptilia anuwai.

Tanzania ina kiwango cha juu cha pili kwa reptilia, amfibia na mimea anuwai katika bara la Afrika (Rodgers

et al., 2001). Misitu ya Tao la Mashariki na ile ya Pwani ni moja kati ya ‘sehemu 25 zenye umuhimu mkubwa

kwa bayoanuwai’ duniani. Bayoanuwai na upatikanaji wa spishi adimu zinazohusiana nazo katika milima

hii hazina mfano wake duniani. Kadri ya asilimia 30 ya spishi za mimea kama 2000 hivi na zaidi ya asilimia

80 ya makundi ya buibui na majongoo hupatikana katika milima hii pekee. Mimea maarufu ya urujuani

(Saintpaulia) inatipakana kiasili katika misitu ya Milima ya Tao la Mashariki na Pwani pekee.

Walau spishi nne za mamalia, tano za ndege, nne za amfibia, ishirini na saba za watambazi (reptilia), arobaini

za vipepeo, ishirini za majongoo, mia nne za mimea na idadi isiyojulikana ya nzi, aina za mende na wanyama

wengine wasio na uti wa mgongo hupatikana katika misitu ya pwani ya Afrika Mashariki pekee (Burgess et

al., 1996). Kiwango hiki cha uadimu kimetokea kwa sababu ya kujitenga kwa misitu hii na misitu mingine ya

Afrika, kuwepo kwake kwa miaka mingi na ukweli kwamba hali ya hewa ya Bahari ya Hindi imebaki thabiti

bila mabadiliko kwa muda mrefu sana.

20

Matokeo yake, vitishio ambavyo vinakabili

nyingi ya spishi hizi vinahusiana na

uhifadhi wa mazingira yao. Kwa kuwa

sehemu kubwa ya misitu ya Tao la

Mashariki na ile ya Pwani iko hatarini,

spishi zake nyingi za wanyama ziko

hatarini (angalia kisanduku hapo chini).

Katika Mlima Kilimanjaro spishi za mimea

2,500 zimetambuliwa, zikiwemo spishi

130 za miti kutoka jenasi (spishi zenye sifa

zinazofanana) 100 na jamii 50. Spishi 170

za vichaka zimetambuliwa kutoka misitu ya

milima huu, na hii iko kwenye zaidi ya jenasi

100 na jamii 40 (Lambrechts, et al., 2002).

Spishi 140 za mamalia zimetambuliwa

kuwepo mlimani, ikiwemo kundi kubwa

zaidi linalojulikana duniani la mindi

(Abbot’s duiker), spishi iliyo hatarini sana

ulimwenguni (Lambrechts et al., 2002).

Mbuga hii ina panya wadogo wapatikanao

katika eneo hili pekee, spishi nne na spishi

ndogo za vipepeo zipatikanazo kipekee,

mimea ya aina 6 ya kipekee, kuvumwani

kumi na mbili wanaopatikana eneo hili

pekee na mmea aina ya liverworts (Baker

na Baker, 2001).

Papa dume (Carcharrhinus leucas) walio

adimu na hatarini mara chache huogelea

kuelekea juu katika Mto Pangani kutoka

kwenye delta zake, na wameonekena

katika mkondo wake kuelekea juu hadi Jambe (TANESCO, 1994). Hata hivyo, mbali na papa, hakuna

spishi zozote kati ya 41 za samaki wa mto huu, zinazofikiriwa kuwa hatarini. Kuna spishi kadhaa zilizoko

kwa wingi kukiwa na samaki wa aina mbili za “cyprinids” (Barbus paegnstecheri na Labeo coubie), aina

moja ya “characin” (Rhabdalestes leleupi) na aina tatu za “cichlids” (Ctenochromis pectoralis, Oreochromis

korogwe na O. pangani) (TANESCO, 1994).

Jenasi ya perege, Oreochromis, imepata jina lake kutoka lugha ya kilatini la Mlima ‘Chromis’ ambalo Gunther

aliipa mwaka 1889 baada ya kugundua Orechromis hunterti katika Ziwa Chala, lililopo kwenye miteremko

ya Mlima Kilimanjaro (Dadzie et al, 1988). Kwenye Ziwa Jipe aina mbili za ziada za perege walio adimu

zinapatikana: Perege jipe na perege girigan. Orechromis esculentus wanaopatikana katika Ziwa Victoria

pekee 4 , wamepandikizwa katika Bonde, na wamekuwa ni sehemu kubwa ya samaki wanaovuliwa kutoka

Bwawa la Nyumba ya Mungu. Perege wa ziada wa kigeni, T. rendalii, wamevuliwa kutoka Ziwa Chala.

Tishio na hadhi ya Hifadhi

Kisanduku cha 8: Sehemu zenye umuhimu

mkubwa wa bayoanuwai

Sehemu zenye umuhimu mkubwa wa bayoanuwai huteuliwa na

Shirika la Hifadhi la Amerika, Conservation International. Ni maeneo

ambayo yana aina mbali mbali za spishi duniani, lakini ambayo

wakati huo huo, yameathiriwa na kubadilishwa sana na shughuli za

binadamu. Mimea anuwai ndiyo kigezo cha uteuzi wa maeneo hayo,

kwa kuwa mimea ni msingi wa anuwai katika kuainisha kisayansi

makundi mengine. Ili kustahili hadhi hii, lazima eneo liwe na walau

spishi 1,500 za mimea inayopatikana katika eneo hilo pekee, kwa

ukamilifu asilimia 0.5 ya jumla ya mimea inayojulikana ulimwenguni.

Kwa nyongeza, asilimia 70 au zaidi ya makazi ya asili ya eneo hilo

lazima yawe yameharibiwa au kubadilishwa.

Kati ya hizo, sehemu 25 zenye umuhimu mkubwa zaidi wa

bayoanuwai duniani zinachukua asilimia 1.4 tu ya eneo la dunia,

lakini zina asilimia 44 ya mimea inayojulikana duniani, na asilimia 35

ya wanyama wote wenye uti wa mgongo wanaojulikana duniani.

Sehemu hizo muhimu mara nyingi ni ‘visiwa’ vya bayoanuwai

vilivyozungukwa na maeneo ya bayoanuwai duni kiasi.

Kama ilivyo kwa Milima ya Tao la Mashariki, maeneo haya

kiasili yamepata bayoanuwai yake kama matokeo ya hali za

mazingira ambazo hazikubadilika kwa kipindi kirefu.

Mbali na sehemu za umuhimu mkubwa wa bayoanuwai za

Misitu ya Tao la Mashariki na ile ya Pwani, kuna sehemu

nyingine nne za namna hiyo katika Afrika. Madagascar na

visiwa vya Bahari ya Hindi, Misitu ya Guinea ya Afrika ya

Magharibi, Jimbo la Cape maarufu kwa maua na Karoo zenye

utomvu katika pwani ya kusini magharibi ya Afrika.

Tishio kuu linalokabili bayoanuwai ya Bonde la Mto Pangani linahusiana na uharibifu wa makazi. Kiwango

cha juu sana cha wingi wa bayoanuwai huendana na viwango vya juu vya upekee na anuwai za makazi

katika bonde, hususan misitu yake ya milima ya Afrika na ya pwani. Kwa mfano, karibu spishi zote za

ndege zinazopatikana katika bonde hili pekee, pia huchukuliwa kuwa spishi za eneo hili tu, na hivyo

kuwa hatarini zaidi kudhuriwa kutokana na uharibifu na kugawanyika kwa makazi.

4

Katika hali ya mabadiliko ya kushangaza, spishi hii sasa imetoweka kabisa katika Ziwa Viktoria

21

Kisanduku cha 9: Kundi la 1 la spishi za ndege wa Milima ya Usambara lililo hatarini

Walio hatarini sana

• Mbayuwayu mwenye mdomo mrefu (Orthotomus moreaui): hawakujulikana mpaka mwaka 1931

na bado ni spishi inayojulikana kidogo

Wasio salama (wenye kuweza kudhuriwa)

• Bundi wa Sokoke (Octus ireneae): waligunduliwa mnamo mwaka 1965 katika msitu wa Arabuko-

Sokoke ya pwani ya Kenya, ambapo ilichukuliwa kama spishi inayopatikana hapo pekee mpaka

kundi lingine lilipogunduliwa katika milima ya Usambara mnamo mwaka 1995.

• Bundi Tai wa Usambara (Bubo vosseleri): Waligunduliwa kati ya misitu ya uwanda wa chini wa

Usambara katika mwaka 1992, baada ya kufikiriwa kama ndege wa msongamano mdogo wa

mwinuko wa juu hapo awali.

• Zuwanende bakajeupe/kirumbizi (Swynnertonia Swynnertoni): aligunduliwa katika Usambara

pekee mnamo mwaka 1990.

• Zuwanende wa pwani ya Mashariki (Shepperdia gunningi): aligunduliwa katika milima ya Usambara

mnamo mwaka 1992.

• Zuwanende mabaka meusi wa milimani (Modulatrix orostruthus): uadimu wake katika milima ya

Usambara ya Mashariki huenda ni matokeo ya kugawanyika vipande vipande kwa mistiu.

• Chozi wa Amani (Hedydipna pallidigaster): alielezwa kwanza na Sclater na mtaalamu maarufu wa

elimu ndege, Moreau, katika mwaka 1935, ndege huyu mdogo sana anafahamika kutoka sehemu

tatu tu za Afrika Mashariki. Katika milima ya Usambara, ni eneo la kilomita za mraba 320 tu la

makazi yanayofaa ndiyo limebaki (Cheke et al., 2001).

• Chozi mwenye mistari (Anthreptes rubritorgues): anajulikana kutoka sehemu nne tu katika Tanzania.

Makazi yake makubwa zaidi ni milima ya Udzungwa.

• Kwera wa Usambara (Ploceus nicolli): kwera hupatikana katika milima ya Usambara pekee ambako,

Zimmerman et al., (1996) anakadiria wamebaki chini ya 100.

Walio hatarini kidogo:

• Tai-miraba kusi (Circaetus fasciolatus): Awali alidhaniwa kuwa mkazi wa kawaida katika misitu

ya pwani inayotanda kutoka Kaskazini Mashariki ya Kenya hadi Kaskazini Mashariki ya Afrika ya

Kusini. Sasa anafikiriwa kutishiwa na msongamano wa binadamu na matumizi yaliyokithiri ya misitu

ambayo ni makazi yake makuu. Makadirio ya jozi moja kwa kilomita za mraba 100 yanabaki katika

kiwango hicho (Ferguson-Lees na Christie, 2001).

• Kulukulu (Tauraco fischeri); kwa kawaida hupatikana msituni pote. Anatishiwa na biashara ya

Kimataifa ya ndege mwitu.

Hofu ya uharibifu wa makazi haya ya msitu yenye thamani imefanya misitu ya pwani ya Tanzania na

Milima ya Tao la Mashariki ipate uangalizi wa Kimataifa. Hakika yote ina hadhi ya Eneo Muhimu la

Ndege (IBA) (Baker na Baker, 2001), inayowezesha kulenga uangalizi wa Hifadhi ya Kimataifa kwenye

hii mifumo ikolojia ya kupendeza na nyepesi kudhuriwa. Hata hivyo, ni misitu michache sana ya Tao la

Mashariki au ya Pwani katika bonde ambayo siyo hifadhi ya misitu.

B. 6 Uvuvi

Samaki mara nyingi ni chanzo muhimu cha protini ya wanyama kwa jamii za vijijini za Afrika. Mwaka

1970, uvuvi katika bwawa la Nyumba ya Mungu ulikimu wavuvi 3,161, ambao walivua tani 28,509 za

samaki kwa ujumla wao. Kufikia mwaka 1983, kulikuwa na wavuvi 1,342, ambao waliweza kupata tani

2,430 za samaki (Vanden Bossche na Bernacsek, 1999).

22

Typha na mafunjo hutanda karibu katika nusu ya uso wa Ziwa Jipe, na karibu yakwamishe shughuli za

uvuvi upande wa Tanzania wa ziwa (Sarmett na Kamugisha, 2002). Kwa upande wa Kenya wa Ziwa

Jipe, wanavijiji 200 katika vijiji vitatu wanasemekana kutegemea uvuvi wa ziwani. Mbali na matatizo

yanayohusiana na magugu maji, ziwa kujaa mchangatope pia ni tishio kwa uvuvi (Musyoki, 2003).

Wanavijiji wanaoishi kuzunguka Kinamasi ya Kirua chini ya bwawa la Nyumba ya Mungu wanalalamikia

upungufu wa samaki kutokana na taratibu za kudhibitiwa mtiririko wa maji kutoka bwawani (Sarmett na

Kamugisha, 2002).

B.7 Udongo

Sehemu kubwa ya Bonde la Mto Pangani ina safu ya jiolojia ya fuwele na mawe ya chokaa, pamoja na

viunga vya mashapo kutoka ziwani. Karibu zaidi na pwani, jiolojia ni ya mashapo ya katika mlango wa

mto. Maeneo karibu na Mlima Meru na Mlima Kilimanjaro kwa asili ni Volkano za alikali zenye rutuba

nyingi (Geological Survey, 1960). Mchanganyiko huu wa udongo wenye asili ya ziwa na ile ya volkano,

na vilevile maeneo yenye wastani wa juu wa mvua kwa mwaka umezifanya sehemu za Bonde la Mto

Pangani kuonekana kama eneo zuri la uzalishaji chakula nchini Tanzania.

Matatizo makuu kuhusiana na udongo wa Bonde la Mto Pangani ni kupungua kwa rutuba ya ardhi,

na upotevu wa udongo kutokana na mmomonyoko. Stoorvogel na Smaling (1990) walikadiria kuwa

ardhi inayofaa kwa kilimo katika Tanzania hupoteza kilogramu 27 za Naitrojeni, kilogramu 9 za Fosfeti

na kilogramu 21 za Potasiamu kwa hekta kwa mwaka kwa mwaka 1983. Walikadiria kwamba ikifikia

mwaka 2000, viwango hivi vya upotevu vitaongezeka na kufikia kilogramu 32 za Nitrogen, kilogramu

12 za Fosfeti na kilogramu 25 za Potasiam ikiwa upotevu wa virutubisho ulioonekana mwaka 1983

haukubadilika. Kwa naitrojeni na fosforasi, viwango hivi vya upotevu ni sawa na tani 251,448 na tani

115,1122 kwa mwaka. Stoorvogel na Smaling walieleza kuwa upotevu huu ulitokana na mambo matatu:

kwanza uvunaji wa kawaida wa mazao ambapo virutubisho vingi hupotea. Pili, uondoaji wa mabaki

ya mazao. Kwa mfano, maharage yanapovunwa katika wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, mmea

mzima unang’olewa toka ardhini. Tatu, kutokana na mmomonyoko, hususan kutokana na kilimo katika

mitelemko mikali (Kaihura et al. 2001). Ifahamike kwamba si kilimo chote katika Bonde la Mto Pangani

ni cha kiharibifu (Kaihura et al. 2001).

B.8 Majumuisho ya hoja

Rasilimali za Bonde la Mto Pangani zinatumika kwa kiwango kikubwa sana. Katika sehemu hii, kwanza

tunatoa muhtasari wa mchango muhimu unaotolewa na rasilimali hizi katika bonde na katika sehemu ya

pili, tunatoa muhtasari wa hatari zinazozikabili.

Rasilimali za Bonde la Mto Pangani

• Misitu ina mchango muhimu sana katika haidrojia ya bonde, inarekebisha kasi ya maji, kupunguza

mmomonyoko, kuhifadhi na kusafisha maji. Misitu iliyopo Bonde la Mto Pangani inatoa mchango

muhimu kwa bayoanuwai ya ulimwengu. Katika misitu ya bonde hili baadhi ya spishi za kiwango

cha juu cha upatikanaji kwa wingi ulimwenguni na bayoanuwai hupatikana.

• Maji katika Bonde la Pangani ni ya muhimu kwa uchumi wa kilimo wa bonde, uzalishaji wa umeme,

maendeleo ya miji, mahitaji ya viwandani na majumbani, na kwa ajili ya mifugo. Vinamasi pia

katika bonde huchangia sana katika hifadhi na urekebishaji mwenendo wa maji.

• Bonde hili lina maeneo manne yaliyohifadhiwa. Kilimanjaro, kipekee ina mchango muhimu katika

uchumi wa taifa kutokana na utalii, na pia huhifadhi spishi nyingi ya mimea na wanyama.

• Bayoanuwai ya bonde hili kwa kiasi fulani haina mfano ulimwenguni, na ni eneo la shughuli nyingi

za Kimataifa za masuala ya hifadhi.

23

• Uvuvi katika Bonde la Pangani unatoa mchango muhimu wa chakula na kiuchumi kwa jamii za

vijijini katika bonde.

• Ardhi ndiyo msingi mkuu wa uchumi wa kilimo wa bonde hili. Historia ya mlipuko wa volkano ya

eneo hili na viunga vya mashapo ya mto yenye rutuba, huchangia katika umaarufu wa Bonde la

Mto Pangani kuwa eneo la kutegemewa kwa uzalishaji chakula nchini Tanzania.

Tishio kwa rasilimali za Bonde la Mto Pangani

• Misitu iliyopo katika bonde inahatarishwa na ukataji miti, uingiliwaji eneo lake la pembezoni,

mahitaji ya ardhi, utengenezaji wa mkaa na ukusanyaji wa kuni.

• Upatikanaji wa maji katika Bonde unahatarishwa na mahitaji makubwa mno ambayo yamedhihirisha

kuwa rasilimali za maji zinaonekana kuelemewa. Chanzo kikuu cha mahitaji hayo ni mifumo duni

ya mifereji ya umwagiliaji. Vinamasi vya bonde hili vinahatarishwa na utaratibu wa udhibiti wa maji

kwa kutumia mabwawa.

• Maeneo yaliyohifadhiwa katika bonde yanahatarishwa, kwa upande mmoja na ujangili, na kwa

upande mwingine, vitisho sawa na vile vinavyokabiliwa na rasilimali za misitu.

• Sehemu kubwa ya bayoanuwai ya bonde imepatikana kutokana na safu za aina ya kipekee za

makazi katika misitu yake. Matokeo yake, hatari ya kutoweka kwa bayoanuwai zinatokea kwa

sababu ya tishio kwa makazi.

• Uvuvi katika bonde unatishiwa na shinikizo la uvuvi lililokithiri, na ukuaji wa magugu unaosababishwa

na kiasi kikubwa cha virutubisho.

• Viwango vya chini vya kurudishia rutuba na matumizi ya pembejeo, na vile vile viwango vya juu

vya mmomonyoko, vinahatarisha udongo katika bonde.

24

C Uchumi wa Jamii katika

Bonde la Mto Pangani

C.1 Maelezo ya jumla

Inakadiriwa kuwa kuna watu wapatao milioni 3.7 katika Bonde la Mto Pangani, asilimia 80 wakitegemea

ama moja kwa moja au kwa njia moja au nyingine, kilimo kwa maisha yao. Asilimia 90 ya idadi ya wakazi

wa bonde hili huishi katika sehemu za ukanda wa juu. Msongamano huo wa makazi hufikia watu 300

kwa kilomita moja ya mraba. Katika maeneo ya nyanda za juu za Kilimanjaro kuna watu 900 kwa kilomita

moja ya mraba yenye wastani wa vishamba vya hekta 0.2 tu kwa kaya. Wakati huo huo, katika maeneo

ya nyanda za chini kulikuwa na watu 65 tu kwa kilometa ya mraba, na kila kaya ililima wastani wa eneo

la hekta 10.4 (Lein, 2002).

Shughuli za kiuchumi katika Miji na viwanda ndani ya bonde si kubwa kiasi cha kutosha kuchukua

nguvu kazi hii. Matokeo yake, idadi ya watu ambayo inazidi kukua, hupata riziki yake kutokana na kilimo,

ambacho kwa sehemu kubwa ni cha umwagiliaji. Kadiri matumizi ya maji yanavyoongezeka, ndivyo

migogoro inavyoongezeka. Mahitaji ya maji ni ishara ya mahitaji makubwa zaidi ya kufikia aina zote za

rasilimali, ikiwemo ardhi, mazao ya misitu, malisho, madini na hatimaye kujipatia riziki. Kujipatia riziki

kunaweza kuelezwa kama ifuatavyo:

“….. njia ya kujihakikishia maisha …Ndani yake kukiwa na rasilimali kwa ujumla wake, shughuli

na mazao yanayowezesha kuishi. Inategemea umiliki wa, au upatikanaji wa mazao au shughuli

za uzalishaji. Upatikanaji wa riziki hupimwa kwa kutumia vipimo vyote viwili vya mali -yaani

hifadhi na vyombo- na upatikanaji wa chakula na fedha “(Conway na Barbier, 1990: 117).

Dhana ya kufikia rasilimali ni kigezo cha muhimu sana katika kuamua kuwa utafutaji wa riziki ni wa

mafanikio au la (cf. Ellis, 2000). Hivyo ina maana kuwa pale ambapo rasilimali inayotegemewa na jamii

inakuwa haba, basi upatikanaji wake unapungua. Kadiri rasilimali zinavyokuwa haba zaidi, basi hatua

watakazochukua watu ili kujaribu kujipatia rasilimali zinaweza kuwa mbaya zaidi, na kuwa vigumu zaidi

kwa rasilimali husika kudumu. Mtindo huu hatimaye unaweza kufikia mahali ambapo utafutaji riziki

ukapuuza uwezo wa rasilimali kujizalisha upya.

Jambo linalokuza matatizo yanayohusiana na mahitaji ya riziki ni kama rasilimali zinazohusika ni

Rasilimali za Pamoja za Jamii (CPRs). Hizi ni rasilimali ambazo zina tabia mbili za msingi zinazofanana;

(a) ‘zinapunguzika’. Upunguzaji wa kiasi cha maji sehemu ya juu ya mto husababisha upungufu wa

kiasi cha maji sehemu ya chini ya mto. Vivyo hivyo, mvuvi anayevua kilogramu 100 za samaki anafanya

kuwe na kilogramu 100 pungufu za samaki kwa ajili ya wavuvi wengine. (b) Ni vigumu au haiwezekani

‘kuzikinga’ rasilimali za pamoja za jamii. “Kulinda” kisitiari inamaanisha matatizo makubwa ya kuzisimamia.

Kutokana na asili zao, rasilimali za pamoja za jamii (kama vile bahari, angahewa au mikondo ya mto)

haziwezi kujengewa uzio, na pia ni vigumu sana kuzifuatilia na kuzisimamia. Rasilimali za pamoja za

jamii kwa hiyo, husimamiwa vizuri zaidi kwa pamoja, kukiwa na mchango wa watumiaji wote. Ikiwa

mtindo huo wa usimamizi wa pamoja haupo, zitakuwa hatarini sana kuwa wazi kuingiliwa’, ambapo

muundo wa utumiaji ni wa ‘huru-kwa-wote’, watumiaji wa rasilimali wakichukua zaidi ya wanachohitaji

leo kwa kuhofia kuwa wanaweza wasipate kitu kesho. Mitindo ya utumiaji kama hiyo ina viwango vya juu

sana vya ushindani baina ya watumiaji, na thamani halisi zinazohusiana na hifadhi ya rasilimali hazijaliwi

kabisa. Wakati rasilimali zinapotumika katika mtindo kama huu, ‘mwisho wa wanyonge’, unasemekana

kuwa umewadia na kutoweka kwa rasilimali kunakuwa ni jambo la wazi.

Kwa viwango mbalimbali, na kutegemeana na aina ya rasilimali, rasilimali nyingi za Bonde la Mto Pangani

zina tabia ya kuwa wazi kuingiliwa na matatizo makubwa sana kutokana na utafutaji wa riziki. Mahusiano

yanayoainisha utumiaji wa rasilimali za bonde mara nyingi yanaelezwa kama yenye kuhitilafiana. Ili

25

kurahisisha na kufafanua matatizo haya, sura hii inazingatia matakwa ya shughuli mbali mbali za kiuchumi,

ikianzia na shughuli za viwanda ambazo ni pamoja na uzalishaji wa umeme, na kisha kuendelea kuangalia

sehemu kubwa ya uchumi wa bonde, ambayo ni kilimo. Shughuli nyingine pia zinazingatiwa, na sura hii

inamalizia na tathmini ya migogoro ya kawaida katika uendelezaji wa bonde hili.

Jedwali la 4:Taarifa ya msingi ya uchumi wa kijamii wa Tanzania na Kenya

mwaka 2001 isipokuwa ikionyeshwa vinginevyo

Kenya

Tanzania

Idadi ya watu Milioni 29 Milioni 32

Kwango cha ongezeko la idadi ya watu kwa mwaka, mwaka 2000 2.6 2.8

Kiwango cha vifo vya watoto wachanga kwa 1000 waliozaliwa hai 75.0 91.0

Kiwango cha vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka 5 kwa 117.0 142.0

1000 waliozaliwa hai

Uwezekano wa kufa, wanaume < miaka 5, (katika kila 1000) 100.0 157.0

Uwezekano wa kufa, wanawake < miaka 5, (katika kila 1000) 99.0 148.0

Matarajio ya umri wa kuishi wakati wa kuzaliwa (wanaume) 47.3 44.4

Matarajio ya umri wa kuishi wakati wa kuzaliwa (wanawake) 48.1 45.6

Asilimia ya upatikanaji wa maji salama ya kunywa 44.0 66.0

Asilimia ya upatikanaji wa usafi wa kutosha 85.0 86.0

Asilimia ya watoto waliozaliwa na uzito mdogo1 16.0 14.0

Asilimia ya watoto waliodumaa (wastani na kiasi kikubwa)2 33.0 42.0

Asilimia ya watoto waliodhoofika )3 6.0 6.0

Wastani wa kula kalori kwa mtu kwa siku (1999)4 1,886.0 1,940.0

GNP (Dola za Kimarekani) kwa mtu 340.0 210.0

Dondoo

1 kuzaliwa na uzito mdogo mara nyingi kunaashiria shinikizo la uzazi wakati kijusi kiko tumboni, kama

vile kuugua (ikiwemo utapiamlo).

2 Kudumaa ni aina ya kudumu ya utapiamlo unaotokana na kutopata lishe ya kutosha, iliyo bora, kwa

kipindi kirefu

3 Kudhoofika ni aina hatari na kali, ya utapiamlo iletwayo na kutopata lishe ya kutosha, iliyo bora, kwa

kipindi kifupi.

4 FAO imeweka mahitaji ya nguvu ya chini kabisa kwa binadamu kuwa kilo kalori (kcal) 2,600 kwa siku

Rejea: UNICEF; 2001; FAO, 2001; WHO, 2001

26

C.2 Shughuli za viwanda

Kuna uwezekano kuwa shughuli iliyo kubwa zaidi ya viwanda katika Bonde la Mto Pangani ni uzalishaji wa

umeme. Mzalishaji mkuu wa umeme ni Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), linalomilikiwa

na serikali, ambalo linamiliki mitambo minne ya uzalishaji umeme wa maji katika Mto Pangani. Nayo

ni Nyumba ya Mungu (yenye uwezo wa MW 8), Hale (MW 21) na Mitambo mipya ya Maporomoko ya

Mto Pangani (MW 68). Mitambo hii ya umeme imeunganishwa na gridi ya taifa na huchangia kadiri ya

asilimia 17 ya jumla ya nishati ya umeme wa maji unaozalishwa nchini (Ngula, 2002). Mahitaji ya kiasi

cha maji kwa uzalishaji wa uhakika (Firm power) kwa mitambo ya umeme ni kadiri ya mita za ujazo

24 kwa sekunde, ambapo mahitaji ya juu kabisa ni mita za ujazo 45 kwa sekunde. Mitambo ya “Old

Pangani” hufanya kazi mara chache kutokana na ukosefu wa maji ya kutosha (Lugeiyamu, Mhojiwa).

Wakati wa msimu wa kiangazi, upungufu wa maji unaweza kusababisha uzalishaji wa umeme katika

bonde kupungua hadi MW 32 (Sarmett na Kamugisha, 2002).

Kuna shughuli nyingi za uchimbaji wa madini katika Bonde la Mto Pangani. Hizi ni pamoja na machimbo

ya bati eneo la Korogwe, machimbo ya tanzanaiti na fosfati katika mkoa wa Arusha, na machimbo ya

mawe ya chokaa katika mkoa wa Tanga (Mkuula, 1993). Vito johari pia vinapatikana kwa kiasi cha

kutosha, na asilimia 80 ya hifadhi za tanzanaiti ijulikanayo duniani inapatikana Mererani, kilomita 50

Kaskazini Mashariki ya Arusha. Uchimbaji wa mchanga kwa shughuli za ujenzi hufanyika zaidi katika

kingo za mito, na katika sehemu za bonde kwa upande wa Kenya, uchimbaji wa rubi hufanyika.

Viwanda vingine katika bonde ni vile vinavyohusiana na kilimo, kama vile vya uzalishaji wa sukari na vya

mchakato wa usafishaji wa katani. Katika wilaya ya Taita-Taveta nchini Kenya, uzalishaji wa katani ndio

shughuli kuu ya kilimo.

C. 3 Shughuli za Kilimo

Watu wa jamii ya Wachaga wameishi katika miteremko ya Mlima Kilimanjaro kwa miaka kati ya 300 hadi

450. Umilikaji wao wa ardhi kwa ajili ya kilimo umegawanywa katika namna mbili. Kwanza ni “shamba”,

ambapo yametengwa maeneo maalum katika ukanda wa chini ya mlima ambapo mvua si ya uhakika, na

umwagiliaji wa kadiri unahitajika sana. Matumizi ya ardhi ya shamba yalikuwa yakisimamiwa na machifu wa

Kichaga, ambao waliwapangia wakulima sehemu za ardhi kwa msimu. Ingawa mkulima aliweza kutumia

ardhi kwa kipindi kirefu, haikuwa mali yake hata kidogo (Johnston, 1946). Aina ya pili ya umilikaji ardhi ya

uchaga ni ‘kihamba’, ambacho kilitengwa kwa matumizi binafsi ya wakazi wa uchagani. Kihamba kilikuwa,

na bado kinalimwa kwa kiwango kikubwa. Hata katika miaka ya 1940, wakati wa maandishi ya Johnston

(1942), kulikuwa na ardhi ndogo sana ya kihamba iliyobaki ambayo ingeweza kutumika kama malisho,

hivyo mifugo mingi ilifungiwa na kulishwa mazizini. Katika maeneo yale ambapo mkazo wa kilimo ulikuwa

juu, na hakikupatikana kihamba kingine, machifu wa Kichaga walipaswa kubadilisha ardhi ya shamba kuwa

kihamba, matokeo yake, kitendo hiki kilichangia kuhamisha kilimo kilichokuwa kimezidi katika miteremko

ya juu, kwenda katika miteremko ya chini ya milima. Wachaga hawakuweza kujitanua mpaka mlimani

kwa vile eneo hili lilikwishatengwa kama hifadhi ya msitu, na hawakuweza kujitanua kwenye maeneo ya

mteremko wa kati kwa kuwa hii ilikuwa ardhi iliyotengwa kwa ajili ya walowezi wa kizungu (Lein, 2002).

Kutokana na hali hii ya msongamano mkubwa wa kilimo, Wachaga walibuni mifumo ya mifereji ya maji

kutoka kwenye vyanzo vya asili hadi kwenye mimea yao. Mfumo huu unasemekana kuwa mmojawapo wa

mifumo ya zamani sana (inafikiriwa kuwa ulianza katika karne ya 18, Gillingham, 1999) na mifumo mikubwa

zaidi ya mifereji ya umwagiliaji katika Afrika (Rohr et al., n.d.). Ili kupata maji hayo ya mfereji, ilibidi mtu awe

mwanachama wa bodi ya mfereji, ambayo iliongozwa na wazee wa mifereji ambao maagizo yao yalibidi

wakulima wayafuate kwa kuhofia adhabu ya faini au kuzuiliwa kutumia maji ya mfereji (Johnston, 1946).

Wajumbe wa bodi ya mfereji pia walitegemewa kushughulikia utunzaji wa mifereji. Watumiaji wa maji ambao

waliyachukua kutoka katika mifereji inayomilikiwa na watu binafsi ilibidi walipe ada ya kufanya hivyo.

27

Licha ya ukubwa wa kilimo na shinikizo la idadi ya watu kwenye ardhi ya kihamba, taratibu za kijadi za

utawala na uzuiaji migogoro zinaonekana kuwa na ufanisi. Johnston (1942) alisema “…….ni jambo la

kuvutia kuwa, pamoja na kuwa na mfumo wa mifereji yenye utata , lakini mambo yanaendeshwa vizuri

sana na wazee wa mifereji, kiasi kwamba idadi ya mashauri yatokanayo na migogoro ya haki ya kutumia

maji imekuwa ndogo sana” (uk. 4).

Kwa upande wa kusini, msongamano wa shughuli za kilimo katika milima ya Usambara, pia ulianza

kuwa wa matatizo machoni mwa wakoloni. “Ulazima wa wenyeji kulima mfululizo kwenye kingo za mlima

hufanya mmonyoko wa udongo kuwa tatizo kubwa sana, na maeneo makubwa ya ardhi ….huchukuliwa

na maji (Dobson 1940:3). Wasambaa walikabiliwa na matatizo yaliyofanana na yale ya Wachaga. Maeneo

ya miteremko ya kati ya milima yalikuwa na hali ya hewa iliyowapendeza wakulima wa Kijerumani,

ambao walitenga maeneo makubwa ya ardhi kwa ajili ya kilimo cha mkonge.

Maji katika jamii ya Wasambaa yalichukuliwa kuwa ni mali ya jamii, na mtu ambaye alikuwa na chanzo

cha asili cha maji katika ardhi yake hakuweza kuzuia watu kutoka nje kuyatumia. Wamiliki wa ardhi

waliweza kuwatoza faini wafugaji iwapo mifugo yao iliharibu mazao yao, au kama maji yalichafuliwa.

Maji kutoka kwenye mfereji, ambayo yalitumiwa sana katika miaka ya awali ya 1940, yalikuwa ni mali

ya wale waliochimba mfereji huo (Dobson 1940).“Mfereji ulipokuwa unachimbwa, wenye mashamba

waliamua baina yao wenyewe kuhusu nani apate maji na kwa siku zipi”(uk. 22). Aidha, licha ya ukubwa

wa kilimo na msongamano wa watu, migogoro ya haki ya kutumia maji ilikuwa michache. “Kulionekana

kuwa na migogoro michache kiasi cha kushangaza” aliandika Dobson (1940) ….” lakini kwa suala la

mifereji mirefu sana, wazee kwa ujumla walimweka mtu anayeaminika kusimamia na kuhakikisha kuwa

kila mmoja anapata mgao wake wa maji kwa usawa na hakuna maji yanayopotea bure …” (uk. 22).

Tofauti na Wachaga, Wasambaa hawakutaka

kabisa kuteremka chini ya milima kutafuta vyanzo

mbadala vya ardhi ya kilimo. Kutokuwepo kwa

migogoro ya haki ya kutumia maji na ukweli

kuwa kuhamia kwenye nyanda za chini lilikuwa ni

jambo la hiari, inaonesha kuwa msongamano wa

kilimo haukuwa mkubwa katika miaka ya 1940,

kama ilivyo leo.

Bonde la Mto Pangani wakati wa kipindi cha

ukoloni, lilikuwa eneo muhimu la maendeleo,

lililokuwa na mashamba makubwa ya kahawa,

mkonge, ngano na shughuli za uzalishaji sukari

zilizoanzishwa ndani ya bonde hili. Hivyo, mahitaji

ya wafanyakazi yaliongezeka, na hivyo kuwavutia

wahamiaji kutoka sehemu yote ya nchi na hata

kutoka nje ya nchi kama vile Rwanda, Burundi na

Msumbiji (Mbonile, 2002)

Haijafahamika wazi ni eneo kiasi gani la Bonde

la Mto Pangani linamwagiliwa kwa sasa. Kwa

eneo la bonde ambalo liko upande wa Tanzania,

Mujwahuzi (2001) anakadiria kuwa hekta 40,000

zinamwagiliwa, Rohr et al. (n.d.) anasema

kuwa hekta 29,000 zinamwagiliwa kwa ufanisi,

wakati ambapo Ngula (2002) anakadiria kuwa

hekta 31,075 katika Bonde la Mto Pangani

zinamwagiliwa.

Kisanduku cha 10: Kasoro za usanifu

wa mifereji ya asili

Kwa mujibu wa Mwamfupe (2001), matatizo ya

usanifu wa mifereji ya asili katika Bonde la Mto

Pangani ni kama yafuatayo:

• Maji mengi hupotea pale yanapochukuliwa

kwa sababu ya nyenzo duni (mashina ya

migomba) zinazotumiwa kuchepusha maji

yaingie katika mifereji ya kumwagilia;

• Muundo wa vishamba ni duni

–hayakusawazishwa, jambo linalosababisha

maji kutuwama, yakisababisha chumvi chumvi

na mazao haba.

• Mifereji haikujengwa imara na ina kingo

dhaifu, jambo linalosababisha maji kuzivunja.

Matatizo mengine ni kuwa mara nyingi wakulima

huhusisha kiasi cha maji cha kuchukua na ukubwa

wa ardhi ambayo wanahitaji kuimwagilia, na si

kwa maji yanayopatikana. Maji yanayochukuliwa

hayarudishwi mtoni, na mara nyingi hutuama.

Si kawaida kwa wakulima kujenga mitaro ya

kurudisha maji kwenye vyanzo vya maji. “Mifumo

ya ya umwagiliaji ya Tanzania ni upotezaji tu wa

maji” ( Nasari, Mhojiwa)

28

Katika sehemu ya bonde iliyoko Kenya, mahitaji pekee makubwa ya maji ya Ziwa Jipe ni umwagiliaji.

Eneo linalotegemea Ziwa hili upande wa Kenya lina miradi 10 ya umwagiliaji yenye ujumla wa hekta

1,717. Eneo hili linatarajiwa kuongezeka. Mpango wa Umwagiliaji maji wa Ziwa Jipe utakuwa kwenye

mwambao wa Ziwa Jipe na utachukua eneo la hekta 77.2 na utahitaji mita za ujazo 308 za maji kwa

saa (Musyoki na Mwandotto 1999). Kwa sasa, kiasi kikubwa cha maji kinachukuliwa kutoka sehemu

ambayo mto Lumi unatiririka kupitia Kenya, ambamo ndani yake kuna miradi 21 ya maji. Jumla ya kiasi

kinachochukuliwa katika eneo la Kenya la Bonde la ziwa hili ni mita za ujazo 77,274 kwa siku. Mita za

ujazo 54,681 za ziada huchukuliwa wakati wa kipindi cha mafuriko (Musyoki na Mwandotto, 1999).

Kwa mujibu wa Ngula (2002) mahitaji ya maji kwa sasa ndani ya sehemu ya bonde iliyoko Tanzania

ni mita za ujazo milioni 807.99 kwa ufanisi wa umwagiliaji wa asilimia 20. Umwagiliaji katika bonde

hili hutumia kati ya mita za ujazo milioni 400 na 480 za maji kwa mwaka (Mujwahuzi, 2001). Mgao wa

matumizi haya unaonekana kutokuwa na usawa – nusu ya jumla ya matumizi yote ya maji katika bonde

ikiwa imesongamana kuzunguka Mlima Kilimanjaro. Hapa, mifereji ya jadi 500 ya umwagiliaji yenye

urefu wa jumla wa kilomita 1800, huchukua maji ya kadiri ya mita za ujazo milioni 200 kwa mwaka kutoka

kwenye mito ya mlima huu (Gillingham, 1999). Rohr et al. (n.d.) anarejea kazi inayoonesha kuwa, kati

ya mwaka 1997 na 2007, kwa kila ongezeko la asilimia 1.5 la idadi ya watu wa bonde hili, mtiririko

wa mito katika msimu wa mvua haba hupungua kwa mita za ujazo 8 kwa sekunde. Katika mkoa wa

Kilimanjaro asilimia 80 ya matumizi ya maji ni kwa umwagiliaji (Ngana 2001). Maeneo ya Wilaya za Hai

na Moshi Vijijini (kuzunguka Mlima Kilimanjaro) yanaonesha msongamano mkubwa zaidi wa mifereji ya

jadi barani Afrika (Tagseth, 2002). Matokeo yake, viwango vya mmomonyoko wa ardhi kutoka kwenye

Mlima Kilimanjaro viko juu (Mtalo na Ndomba, 2002). Tani 24 za udongo kwa hekta kutoka eneo la

vyanzo vya mito husafirishwa na kuingia katika bwawa la Nyumba ya Mungu kila mwaka (Mtalo na

Ndomba, 2002).

Umwagiliaji wote huu unatumia mifereji 2000 ya jadi ya Bonde la Mto Pangani (Mujwahuzi, 2001),

ambayo inawiana na asilimia 80 ya eneo la bonde linalomwagiliwa (Mwamfupe 2001). Hata hivyo

huenda hii si ishara ya ukubwa wa kilimo. Tagseth (2002), kutokana na data za eneo lake la utafiti lenye

sehemu tatu kusini mwa Wilaya ya Moshi Vijijini, anasema kwamba kiasi cha maji yanayotumika kwa

kweli kimepungua kati ya mwaka 1940 na 1993, kama ilivyopungua idadi ya mifereji.

Sababu za umwagiliaji ziko za namna mbili. Katika maeneo ya uwanda wa juu, wastani wa ukubwa

wa shamba ni kati ya hekta 0.1 na 0.2. Hapa msongamano wa watu uko kati ya watu 700 – 1000 kwa

kilomita ya mraba (Mwamfupe, 2001). Ili kufidia udogo huo wa mashamba na kuhakikisha kuwa ardhi

iliyopo inazalisha kadiri iwezekanavyo, umwagiliaji unafanyika. Eneo la chini la bonde, katika maeneo

ya mashamba ya asili, mashamba ni makubwa zaidi (hekta 0.8 – 1.5) na msongamano wa kilimo ni

mdogo (Mwamfupe, 2001). Hata hivyo, hapa mvua hazina kanuni maalum, na umwagiliaji unafanyika ili

kupunguza athari mbaya za hali ya hewa.

Ni wazi kuwa kwa viwango hivi vya umwagiliaji, watumiaji wa maji wa maeneo ya juu ya mto wako

mahali pazuri zaidi kuliko watumiaji walioko upande wa chini. Upungufu wa maji katika bonde hili ni

jambo la kawaida sana. Utafiti wa Mwamfupe (2001) umefanyika katika sehemu mbili: Makuyuni, katika

miteremko ya Kilimanjaro, na Kahe, chini zaidi ya mlima. Wahojiwa wake walisema kuwa hawapati maji

ya kutosha kwa umwagiliaji. Sehemu kubwa ya wahojiwa - ambao wengi wao walitoka Kahe - walitupia

lawama za upungufu huu kwa ukame wa muda mrefu; wakifuatiwa na wale - hasa kutoka Makuyuni –

ambao walilaumu ongezeko la matumizi na mahitaji ya maji. Ni asilimia 7.3 tu waliolaumu matatizo ya

maji kuwa yametokana na usanifu usiofaa wa mifereji.

Ni muhimu kutambua kuwa sehemu kubwa ya sababu za kutobadilika kwa mifumo hii ya umwagiliaji wa

asili, licha ya ufanisi mdogo, ni kwa sababu ya gharama zinazohusika kuweza kupata mifumo mbadala

ya umwagiliaji yenye ufanisi, inayohitaji matengenezo madogo na ya kudumu. Ni muhimu pia kutambua

kuwa usanifu wa mfereji unaweza kuleta manufaa ya kijamii na kiuchumi ambayo ni makubwa kuliko

hasara zinazotokana na usafirishaji maji wenye ufanisi mdogo.

29

Kisanduku cha 11: Magadi na chumvichumvi

Magadi ni kuwepo kwa ziada ya ‘sodiamu inayobadilishika’ (chumvi chumvi za sodiamu zenye uwezo

wa alikali ya ‘haidrolisis’) na kusababisha mpenyo na ucheu duni wa udongo. Chumvi chumvi ipo

sana katika maeneo kame na nusu kame kwa kuwa hakuna maji ya kutosha kuondoa chumvichumvi

zilizojikusanya katika sehemu ya mizizi ya mimea. Hali ya chumvichumvi inaweza kutokea pale uingiaji

chumvi unapozidi uondoaji wake kwa kufurika au kuchujwa. Kati ya matatizo mengi yanayohusiana

na chumvichumvi ardhini ni athari yake katika ufyonzaji wa udongo na uwekaji unyevu. Uvunjaji wa

vitu asili katika udongo husababisha tabaka lake la juu kujigandamiza, na kusababisha upenyezaji

wa maji kutoka tabaka la juu kwenda eneo la mizizi uzuiliwe. Katika Bonde la Mto Pangani, tatizo la

chumvi limetolewa taarifa katika miradi kadhaa ya umwagiliaji, ikiwemo Musa Mwijanga, Kikafu Chini

(yote wawili katika Wilaya ya Hai) na Mawala (Wilaya ya Moshi Vijijini) (Misana na Makoi, 2001), na

vile vile katika baadhi ya miradi mikubwa ya binafsi ya umwagiliaji katika bonde (Sahib, 2002).

Kiasi cha uoto katika bonde kimepungua, kikichangia katika kupungua kwa mtiririko wa maji wakati

wa kiangazi, na kutishia upatikanaji wa riziki. Wakulima wamekabiliana na upungufu wa maji kwa njia

kadhaa. Wamepunguza kiasi cha kahawa wanayolima, na kupendelea kulima nyanya, ambazo zinahitaji

muda mfupi kustawi na zina soko zuri 5 . Mwamfupe (2001) pia anaeleza kuwa kahawa inatelekezwa kwa

sababu ya kupanda na kushuka kwa bei. Kaya za wakulima pia zimepanua wigo wa kujipatia maisha

kwa kujitafutia mapato yasiyotokana na kilimo. Kinachoshangaza ni kuwa aina ya shughuli mbadala

zinatofautiana kulingana na eneo analotoka mkulima. Shughuli mbadala walizozipata kaya za nyanda za

juu ilikuwa pamoja na ushonaji, utengenezaji wa redio na televisheni, utengenezaji wa saa na ushonaji

wa viatu. Katika nyanda za chini, shughuli mbadala ilikuwa pamoja na uuzaji wa majani ya kulishia

ngo’mbe, uvunjaji mawe, utengenezaji mkaa na kazi za vibarua. Mwamfupe (2002) anadokeza kuwa hii

ni kwa sababu eneo la nyanda za juu limeendelea zaidi na lina maeneo ya miji zaidi kuliko maeneo ya

nyanda za chini, hivyo fursa za kuingia katika sekta ya huduma ni kubwa zaidi.

Miongoni mwa matatizo yanayotokana na wingi wa shughuli za umwagiliaji ni magadi na chumvichumvi.

Katika maeneo matatu ya utafiti (yote katika Wilaya ya Moshi Vijijini) wa Misana na Makoi (2001), maji

ya umwagiliaji, hayakuwa sababu ya chumvichumvi, ingawa kumekuwa na kukwama kwa kiwango

kidogo hadi kikubwa cha upenyaji wa maji katika tabaka la juu la udongo kwa maeneo yote ya utafiti.

Katika maeneo mawili umwagiliaji ulichangia katika kusababisha magadi. Wanasema, maji yenye ‘ubora

mzuri’ yanahitajika ili kushughulikia tatizo hili. Umwagiliaji haukuonekana kuathiri rutuba ya udongo

isipokuwa katika eneo moja. Misana na Makoi (2001) walipendekeza matumizi ya viwango vya chini vya

mbolea za aina mbalimbali kutatua tatizo hili la kutotosheleza kwa rutuba ya udongo. Wanatoa rai kuwa

chumvichumvi zinaweza kuchujwa vizuri kwa umwagiliaji, lakini pale maji yanaposimama basi tatizo hili

halitatuliki kwa vile inasababisha mabadiliko ya kimuundo kwa tabaka la udongo wa juu, ikiathiri upenyaji

wa maji kutoka udongo wa juu kwenda kwenye sehemu ya mizizi ya mmea.

Mashamba makubwa zaidi katika Bonde ni shamba la miwa la Kampuni ya Sukari (TPC) (hekta 17,000),

Skimu ya Umwagiliaji ya Moshi (Lower Moshi Irrigation Scheme) chini ya Programu ya Maendeleo ya

Kilimo Kilimanjaro (KADP - hekta 6,320), na Shamba la Kahawa la Burka, Arusha.

TPC ipo kusini ya mji wa Moshi, na ilianzishwa kwa mara ya kwanza na wawekezaji wa Kiholanzi katika

miaka ya mwanzo ya 1930. Ilitaifishwa mwaka 1980, na kubinafsishwa tena mwaka 2000 kwa wawekezaji

5

Ni lazima itambulike kuwa kupanda na kushuka kwa bei katika soko la dunia la kahawa, na vile vile kwa bidhaa

nyingine za kilimo na ubadilikaji wa mitindo ya uchumi wa kitalii, vyote huchangia katika kubadilisha uthabiti wa

uchumi wa Bonde lenyewe na kuathiri uwezo wa wakazi wake kupata riziki ya kutosha.

30

wa Mauritius (Deep River Bean Champ Sugar Estate, Mauritius) na wa Kifaransa (Group Quartier Francais

Reunion Island). Shamba hili lina ukubwa wa hekta 17,000 ambapo hekta 5,750 kati ya hizo kwa sasa zina

miwa. Inafikiriwa kuongeza eneo hili kufikia hekta 7,500 katika siku za karibuni (Sahib, 2002).

Eneo hili linapata milimita 450 tu za mvua, hivyo umwagiliaji ni lazima kwa kilimo cha miwa. Kiasi cha

upungufu wa maji kwa mimea umekadiriwa kwa kiwango cha chini zaidi cha milimita 1,200 kwa mwaka

hivyo kuhitaji matumizi ya umwagiliaji yanayotofautiana kati ya milimita 1,500 – 1,900 kwa mwaka

kutegemeana na mfumo na mbinu za umwagiliaji. Takriban nusu ya shamba humwagiliwa kwa kutumia

mabomba ya juu, wakati sehemu iliyobaki inamwagiliwa kwa mifereji ya juu ya ardhi. Mito iliyopo katika

mpaka wa upande wa Magharibi wa shamba hutoa sehemu ya maji ya umwagiliaji, na yaliyobaki

huchukuliwa kutoka hazina ya maji ya chini ardhi kupitia visima virefu vinavyotoa maji mengi (meta za

ujazo 500 kwa saa) (Sahib, 2002).

Nchini Tanzania, maji yanaweza kuchukuliwa kisheria iwapo tu watumiaji wana hati ya haki ya kutumia

maji, ambayo, kwa Bonde la Pangani, hutolewa na Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani (PBWB), na

kupangiwa ada kutegemeana na aina ya matumizi ya maji. Bodi hii inakabiliana na matatizo makubwa

katika kutekeleza mfumo wa vibali vya maji kwani watumiaji wengi wa viwango vidogo wanaamini kuwa

maji ni ‘zawadi kutoka kwa Mungu’. Ingawa wanataka kutumia maji kisheria, kiasili hawaamini kuwa

wanapaswa kulipa kwa kufanya hivyo. Hata hivyo watumiaji wengi wa viwango vikubwa hulipa ada ya

matumizi ya maji (Sarmett, Mhojiwa).

C. 4 Shughuli za Wafugaji

Kati ya mwaka 1994 na 1995, mifugo ilichangia asilimia 30 ya pato la taifa (GDP) la Tanzania. Nchi

inakadiriwa kuwa na hekta milioni 60 za ardhi nzuri kwa ufugaji, na inaaminika kuwa inaweza kuhifadhi

mifugo milioni 20. Nchi inakadiriwa kuwa na mifugo milioni 16 kwa sasa.

Kuna data chache kuhusu wafugaji katika Bonde la Mto Pangani. Mnamo mwaka 1995, mifugo katika

Bonde ilikadiriwa kuhitaji mita za ujazo 30,500 za maji kwa siku, wakati inategemewa kuhitaji mita za

ujazo 36,400 kwa siku ifikapo mwaka 2015 (IVO-NORPLAN, 1997). Idadi kamili ya mifugo katika Bonde

kwa sasa haijulikani. Tarakimu za karibuni zaidi zilizopatikana kwa utafiti huu ni za mwaka 2002, na

zimechukuliwa kutoka wilaya na manispaa mbalimbali katika Bonde zima (Jedwali la 4).

Jedwali la 5: Idadi ya mifugo katika baadhi ya maeneo ya Bonde la Mto Pangani (2002)

Mkoa Ng’ombe *Mbuko Punda

Wilaya ya Simanjiro, Mkoa wa Manyara 305,075 133,000 11,000

Manispaa ya Arusha na Wilaya ya Arumeru, 470,000 461,450 21,991

Mkoa wa Arusha

Mkoa wa Kilimanjaro 568,689 534,420 12,380

Mkoa wa Tanga 421,261 378,442 Hawakuhesabiwa

Wilaya ya Taita – Taveta (Kenya) 37,800 40,277 Hawakuhesabiwa

Jumla 1,765,025 902,972

Rejea: Marejeo mbalimbali. *‘mbuko’ ni mchanganyiko wa mbuzi na kondoo.

31

C. 5 Shughuli za Mijini

Bonde la Mto Pangani lina maeneo makuu mawili ya miji. Upande wa Kaskazini, iko miji ya Moshi na

Arusha ambayo iko karibu karibu sana. Mwaka 1995, matumizi ya maji mijini katika bonde yalikadiriwa

kuwa mita za ujazo 71,200 kwa siku, na yanakadiriwa kufikia mita za ujazo 163,600 kwa siku ifikapo

mwaka 2015 (IVO-NORPLAN, 1997). Ujazo wa maji yanayotumika kwa sasa, Sarmett na Kamugisha

(2002) wanakadiria kuwa wa chini, na si zaidi ya mita za ujazo 1.1 kwa sekunde.

Manispaa ya Arusha ina idadi ya watu kati ya 250,000 na 350,000 (wanaoitegemea mamlaka). Ingawa

maji mengi zaidi yanayotoka Mlima Meru yanatumika kwa umwagiliaji na matumizi ya nyumbani, mtumiaji

mkubwa kuliko wote wa maji kibiashara ni Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Mjini Arusha (AUWSA). Ina

visima 15 na wastani wa uwezo wa mita za ujazo milioni 7.4 kwa mwaka (Sechambo, 2002). Mamlaka

pia inapata maji kutoka chemchemi mbili zenye wastani wa jumla wa karibu mita za ujazo milioni 6.4 kwa

mwaka (Sechambo, 2002).

Mito pia hutumika kutupia takataka za mji. Manispaa ya Moshi, Ngana (2001) anasema inatupa majitaka

moja kwa moja katika mito, wakati Mkuula (1993) anadai kuwa mito ya Themi (karibu na Arusha),

Karanga, Njoro na Rau (karibu na Moshi) yote inachafuliwa na takataka za viwanda vya mijini.

C.6 Shughuli za NGO na mashirika ya kimataifa katika Bonde la

Mto Pangani

Kuna mashirika mengi yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi katika Bonde la Mto Pangani, na mashirika

machache ya kimataifa. Katika sehemu hii, inaeleweka kuwa mashirika haya kimsingi hayana mahitaji

katika maliasili za bonde, bali shughuli zao mara nyingi zinalenga katika Usimamizi wa Maliasili (NRM),

kuhifadhi, kuendeleza na kudumisha kazi za kujitafutia riziki. Kuna shughuli nyingi za mashirika yasiyo ya

kiserikali na wahisani wa kimataifa kuliko vile inavyofikiriwa. Haya yatakayojadiliwa hapa chini yanaweza

kuweka msingi kwa shughuli za usimamizi shirikishi katika bonde, kama itakavyoelezwa katika hitimisho.

Asasi Zisizo za Kiserikali (NGO’s)

PAMOJA ni NGO ya Kitanzania inayoamini kuwa majadiliano ni muhimu katika hali ya migogoro. Inatoa

hoja kuwa kama sauti za vikundi vya jamii visivyo rasmi na vya pembezoni zinasikiwa na kusikilizwa

na watunga sera na watoaji wa maamuzi, watendaji wenyeji wanaweza kuchangia kwa ufanisi ulinzi

na ukarabati wa vyanzo vya maji, na wakati huo huo wakiongeza ufanisi wa uzalishaji wa kiuchumi na

matumizi ya maji (PAMOJA, 2002:3). Wanasema, makubaliano ya pande mbili, yanafanya kazi nzuri

zaidi kuliko sheria. Hivi sasa, PAMOJA imeonekana kutambulika na Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani,

kuwa ni njia itakayowezesha majadiliano na maelewano ya pande mbili baina yake na watumiaji maji wa

bonde kuendelezwa.

Ukiwa umezinduliwa mwaka 1992, Mradi wa Mpango wa Kazi ya Misitu Tanzania (TFAP) katika Milima

ya Pare ya Kaskazini ulijihusisha na matatizo kadhaa makubwa, yakiwemo msongamano mkubwa wa

watu, mashamba madogo, uchakavu wa udongo na viwango vya kutisha vya kuvamiwa kwa misitu.

Kwa kutumia njia ya kuandaa mipango ya usimamizi wa maeneo maalum, na kwa ushirikiano na jamii

za eneo la mradi, mradi uliweza kuboresha rutuba ya udongo, kupunguza kasi ya mtiririko wa maji na

kuimarisha kingo za mito. TFAP pia ilijaribu kutumia mifumo ya umwagiliaji iliyoanzishwa na kutumiwa na

Wapare kwa karne nyingi. Hata hivyo, ukubwa wa mashamba, umebaki kuwa mdogo, na zao pekee la

biashara lililolimwa katika eneo hili lilikuwa kahawa, linalofanya Mndeme (n.d.) atoe hoja kuwa uanzishaji

wa fursa za kutafuta kipato kwa njia isiyo ya kilimo na ubadilishaji wa msingi wa zao la biashara itakuwa

muhimu kwa mafanikio ya baadaye ya mradi huu (rejea: Mndeme, n.d.).

Shirika la Umwagiliaji wa Kiasili na Maendeleo ya Mazingira (TIP) lilisajiliwa Tanzania tangu mwaka 1999.

Shirika hili lilirithi mali na shughuli za mradi wa awali wa miaka 13 uliokuwa ukifadhiliwa na wahisani ulioitwa

32

Picha ya 1: Bonde la Mto Pangani

(Rejea: Mradi wa Usimamizi wa Matumizi Bora ya Maji)

33

34

Picha ya 2: Bonde la Pangani - Utawala

(Rejea: Mradi wa Usimamizi wa Matumizi Bora ya Maji)

Picha ya 3: Kilele maarufu cha theluji cha Mlima Kilimanjaro

katika mwaka 1993 (juu) na mwaka 2000

(Rejea: Bergkamp et al. 2003)

35

Picha ya 4: Mto Karanga - Moshi (Kim

Geheb 2002)

Picha ya 5: Mlima Kilimanjaro

(Kim Geheb, 2002)

36

Picha ya 6: Mfereji wa umwagiliaji katika

Wilaya ya Moshi Vijijini. Picha ya juu

inauonesha karibu na chanzo chake,

wakati ya chini inauonesha karibu na

mwisho wake. (Kim Geheb, 2002)

37

Picha ya 7: Chemchemi iliyojengewa Shiri-Njoro. Ukuta unaogawanya maji katika sehemu ya mbele

inaelekeza maji kuingia katika mifereji ya kijiji, wakati lango la udhibiti lililojengewa katika jengo imara

la zege kwa nyuma linayaelekeza maji kwenda Moshi.

(Kim Geheb, 2002)

Picha ya 8: Miteremko yenye msitu katika Mlima Meru (Kim Geheb, 2002)

38

Programu ya Umwagiliaji wa Kiasili. Kama ilivyokuwa kwa Programu ya awali, lengo kubwa la TIP ni kusaidia

kwenye uondoaji umaskini na kuendeleza upatikanaji wa chakula kwa jamii ya wakulima wadogo wadogo

wa umwagiliaji wa kiasili kwenye maeneo teule ya Tanzania kwa kuboresha njia za kijadi za umwagiliaji. TIP

inasisitiza mpango wa matumizi ya ardhi kuwa ni msingi wa usimamizi wa bonde, na inatoa hoja kuwa, kama

hatua ya kuanzia, bonde hili lazima ligawanywe katika maeneo madogo madogo. Katika kila moja, lazima

kuwe na bodi ya eneo dogo yenye wawakilishi kutoka katika kila kijiji kilichomo kwenye eneo hilo. Kila bodi

ya eneo dogo itakuwa na wawakilishi kwenye Bodi ya Maji ya Bonde (Mjata, Mhojiwa).

TIP inafanya kazi kupitia Hati ya Muafaka (MOUs) baina yake na wilaya nne za Tanzania: Same na Mwanga

katika mkoa wa Kilimanjaro, Lushoto mkoani Tanga na Arumeru katika mkoa wa Arusha. Huwafikia wateja

na wahitaji wengine kwa njia ya mikataba na shughuli mbalimbali pale wanapohitajiwa (Mjata, 2002).

Programu ya Hifadhi na Maendeleo ya Kanda ya Mwambao wa Tanga (TCZCDP) ina ubia na Halmashauri ya

Wilaya za Pangani na Muheza, Halmashauri ya Manispaa ya Tanga, Mamlaka ya Mkoa wa Tanga, Wahisani

wa Irish Aid, na IUCN kwa ajili ya ushauri wa kiufundi na kiusimamizi. Madhumuni ya jumla ya TCZCDP ni

matumizi endelevu ya rasilimali za pwani. Programu hii ina lengo la kuinua hali ya jamii za pwani mkoani kwa

kuboresha afya ya mazingira ambayo wanayategemea na kuzipanua njia za matumizi ya mazingira ya pwani.

TCZCDP ilianza kazi zake mwaka 1987 na shughuli zake zinaendelea (Mgongo 2002).

Ubia wa Usimamizi wa Mwambao wa Tanzania (TCMP) ni juhudi za pamoja kati ya Baraza la Taifa la

Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Kituo cha Rasilimali za Pwani/Chuo Kikuu cha Kisiwa

cha Rhode na USAID. Ubia huu ulianzishwa mwaka 1997 ili kuendeleza na kutumia mfumo wa kitaifa

wa usimamizi wa mwambao. Mfumo huu uko kwenye msingi wa mikakati yenye lengo la kuendeleza

mpango wa usimamizi shirikishi wa ukanda wa pwani wa Tanzania na kuanzisha shughuli endelevu za

uchumi zenye kutunza mazingira katika eneo hili (Luhikula 2002).

Kikundi cha Hifadhi ya Misitu Tanzania (TFCG) kilianzishwa mwaka 1985, na kinakuza uhifadhi wa misitu

yenye bayoanuwai nyingi katika Tanzania. Kati ya mafanikio ya kikundi hiki, ni ushawishi wa uundaji wa

Mbuga ya Taifa ya Udzungwa, mbuga ya kwanza nchini Tanzania ya msitu wa mvua; ununuzi wa Msitu

wa Mazumbai katika Milima ya Usambara Magharibi kwa madhumuni ya utafiti wa Chuo Kikuu cha Dar es

Salaam; na kushawishi EU-IUCN/Wizara ya Mifugo na Kilimo kufadhili Mradi wa Hifadhi na Maendeleo ya

Usambara Mashariki. Kati ya shughuli zake za sasa katika Bonde la Mto Pangani ni kuendeleza mfumo

wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu (JFM) kwa msitu wa Ambangulu (Milima ya Usambara Magharibi)

kati ya jamii za wenyeji, serikali za mitaa na shamba la chai lililopo karibu. Kutokana na kufanya kazi

kwa pamoja na jamii zilizo jirani na Msitu wa Kambai (Milima ya Usambara Magharibi), TFCG imeweza

kupanda miti 600,000. Huko Ngulwi (Milima ya Usambara Magharibi), TFGG inajaribu kupanda miti

katika miteremko iliyoachwa wazi bila miti na kuanzisha programu ya utalii wa ikolojia.

Shughuli za Kimataifa Katika Bonde

Inasadikiwa kuwa programu ya usimamizi bora ya maji na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji cha

wakulima wadogo wadogo (RBMSIIP) ndiyo mradi mkubwa zaidi ya yote uliotekelezwa katka Bonde la

Mto Pangani. Huu ni mradi wenye sehemu kubwa mbili ulitekelezwa na Wizara ya Maji na Maendeleo

ya Mifugo kupitia Idara yake ya Rasilimali za Maji, na Wizara ya Kilimo na Chakula kupitia Idara ya

Umwagiliaji. RBMSIIP awali ilibuniwa kama mpango wa miaka sita (1996/97 – 2001/02) ukifadhiliwa

na mfuko wa mkopo wa IDA pamoja na serikali. Kufuatia mapitio ya nusu kipindi katika mwaka 2001,

tarehe mpya ya mradi kukamilika ilipelekwa mbele kwa mwaka mmoja kufikia mwezi Juni mwaka 2003

kukamilisha shughuli zilizopangwa.

Madhumuni makuu ya mradi huu ni kuimarisha uwezo wa serikali kusimamia rasilimali zake za maji

kwa njia shirikishi na pana ambayo italeta usawa, ufanisi na maendeleo endelevu ya rasilimali na

kushughulikia masuala ya mazingira yahusianayo na maji katika ngazi ya taifa na katika mabonde ya

mito Rufiji na Pangani; na kuboresha ufanisi wa umwagiliaji wa miradi iliyoteuliwa ya umwagiliaji wa kiasili

39

wa mashamba ya wakulima wadogo katika mabonde haya mawili yaliyokusudiwa. Mafanikio makuu ya

mradi mpaka sasa ni mapitio ya sera ya maji ya taifa na kuandikwa rasimu ya sera mpya ya maji. Rasimu

hii iliidhinishwa na Serikali ya Tanzania mnamo mwezi Julai 2002.

Mradi wa UNDP GEF wa Bayoanuwai ya kimataifa ya Afrika ya Mashariki (EACBP) ni mradi wa kikanda

unaofadhiliwa na Huduma ya Mazingira Duniani (GEF) kupitia UNDP, na katika Tanzania, unatekelezwa

na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Mradi huu unafanya kazi kwa kutumia

miundo ya utawala iliyopo katika kanda hii, na ushirikishaji mkubwa wa jamii kama nguzo yake. Lengo kuu

la mradi ni kupunguza kiwango cha upotevu wa bayoanuwai katika maeneo ya mipakani yaliyochaguliwa

katika Afrika ya Mashariki. Mradi una malengo mawili yanayohitaji utekelezaji wa haraka. La kwanza

ni kuunda mazingira yanayowezesha ambayo mawakala wa serikali na jamii kwa pamoja wanaweza

kurekebisha matumizi ya rasilimali; la pili ni kuweka uwiano wa upatikanaji na mahitaji, mambo ambayo

huathiri hifadhi na matumizi bora ya bayoanuwai. Katika eneo la bonde, EACBP imekuwa ikifanya kazi

katika Hifadhi ya Msitu ya Shegena, ambao ni msitu mkubwa zaidi katika Milima ya Pare ya Kaskazini,

ambapo ilifanyika jitihada ya kuanzisha mfumo wa JFM na jamii za wenyeji.

PRBMP hutoa taarifa nyingi za kisayansi na huanzisha mabaraza ya ushirikishwaji kwa madhumuni ya

kuimarisha usimamizi wa rasilimali za maji wa pamoja unaojumuisha mabadiliko ya hali ya hewa duniani,

matumizi ya maji kwa usawa na utawala bora wa maji kwa ajili ya kujipatia riziki na kutunza mazingira kwa

ajili ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo. Ofisi ya Maji Bonde la Pangani inatekeleza mradi huu kwa msaada

wa kitaaluma kutoka IUCN (shirika la kimataifa la kuhifadhi uasili) Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV)

na asasi isiyo ya serikali inayoitwa PAMOJA. Mradi unafadhiliwa na mpango wa IUCN wa hifadhi ya maji na

uasili, serikali ya Tanzania, Mfuko wa Maji wa Umoja wa Ulaya, Mfuko wa Mazingira wa Ulimwengu (Global

Environment Facility) kupitia Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

C.7 Migogoro

Kama ilivyoelezwa hapo juu, watumiaji wa maji wanapaswa kisheria kupata kibali cha kutumia maji

kitolewacho na Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani. Gharama vibali vya kutumia maji zinategemea aina

ya matumizi ya maji. Watumiaji wadogo mara nyingi hawapendi kuomba hati na kulipa ada ya maji,

wakitoa hoja kuwa maji ni ‘zawadi kutoka kwa Mungu’. Kwa mujibu wa Mujwahuzi (2001) kuna hati za

maji 1,028 katika bonde zenye uwezo wa kuchukua mita za ujazo 30.7 kwa sekunde. Hata hivyo, kuna

matoleo ya ziada ya maji 2,094 yenye uwezo wa kuchukua mita za ujazo 40 kwa sekunde. “Migogoro

iliyopo sasa na inayotazamiwa kuwepo hapo baadaye ya matumizi ya maji katika bonde, ni matokeo

ya maendeleo ambayo hayakuratibiwa tangu zamani na yanayoongezeka sasa ya rasilimali za maji za

bonde hususan juu ya Bwawa la Nyumba ya Mungu” (Mujwahuzi, 2001:131).

Migogoro katika Bonde la Mto Pangani, hata hivyo, haiishii kwa watumiaji maji peke yao. Katika mifano

inayotolewa hapo chini, itaonekana wazi kuwa migogoro mingi inayoikabili sekta ya maji ipo pia kwa

sekta nyingine zinazotumia rasilimali, na kati ya matumizi na mahitaji mbalimbali juu ya rasilimali. Aina

za migogoro iliyobainishwa hapa inarahisisha kueleza utatanishi wa hali ya juu na asili ya ushindani

unaoanzisha migogoro. Uchambuzi huu wa Hali halisi unaiweka migogoro hii katika makundi matatu

makuu, yaliyobuniwa ili kutoa maoni ya jumla ya aina mbalimbali na viwango vya migogoro iliyopo katika

bonde. Makundi haya hayatengani, ikichukuliwa kuwa ni kawaida kwa migogoro ya maliasili na mahitaji

ya riziki kuwa matatizo yanayoathiri upatikanaji wa rasilimali yanaingiliana, na mara nyingi yanazidishana.

Hivyo, migogoro ya viwango inaweza kuzidisha migogoro ya umiliki na kinyume chake. Makundi haya ni:

migogoro ya viwango, migogoro ya umiliki na migogoro ya mahali.

Migogoro inayotokana na viwango

Uhusiano kati ya watumiaji wa maji wa ukubwa na uwezo tofauti katika Bonde la Mto Pangani mara

nyingi huelezwa katika namna mbili zinazokinzana. Hivyo, mashamba makubwa yanayotumia mamia ya

lita za maji kwa sekunde na kutumia mifumo ya umwagiliaji yenye ufanisi mkubwa, yanatofautiana kabisa

40

na watumiaji wadogo wanaotumia maji kidogo na mifumo ya umwagiliaji iliyo duni sana. Itambulike kuwa

migogoro kama hiyo hiyo inaweza kutokea pia ndani ya jamii, kati ya taasisi zilizokabidhiwa madaraka

(kama vile serikali za vijiji) na wanajamii wengine. Tofauti kubwa hizi ni sababu ya kutosha kwa migogoro

kuzuka. Mifano ya aina hizi za migogoro ni kama ifuatayo:

Mamlaka ya Maji safi na Majitaka Moshi dhidi ya Kijiji cha Shiri-Njoro

Shiri – Njoro ni kijiji kilichopo kando ya barabara ya Moshi – Arusha, karibu na mji wa Moshi. Moshi ni eneo la mji

linalokua kwa haraka sana likisaidiwa kwa kiwango kikubwa na kilimo. Kadiri mji huu unavyokua, ndivyo mahitaji

ya maji yanavyoongezeka pia. Mnamo mwaka 2000, wahandisi kutoka Mamlaka ya Maji safi na Maji taka ya

Manispaa ya Moshi (MUWSA) walifika Shiri-Njoro na kujengea mfuniko chemchemi kuu ya jamii. Chemchemi

hiyo hutoa lita 218 kwa sekunde, na MUWSA ilipata kibali cha kutumia maji ya lita 116 kwa sekunde. Kijiji

kilikuwa na mifereji mitatu inayotoka katika chemchemi hiyo, kila mmoja ukiwa na kibali cha kuchukua lita 30

kwa sekunde. MUWSA , kwa hiyo, ilitakiwa kuacha kiasi cha maji cha kutosha mahitaji ya mifereji ya jamii.

Hata hivyo, MUWSA, huchukua maji kadiri ya lita 24 kwa sekunde zaidi ya ilivyoruhusiwa. Serikali ya

Kijiji cha Shiri – Njoro inadai kuwa haiwezi kuendelea kutumia kikamilifu mifereji yake mitatu kutoka

kwenye chemchemi, na kwamba jamii pamoja na uchumi wake wa kilimo vimeathirika vibaya. Ni nia

yao kuipeleka MUWSA mahakamani na wanasema “tutauza mbuzi na mbwa wetu ili tupate fedha” za

kufanya hivyo (Wahojiwa: Serikali ya Kijiji cha Shiri – Njoro).

Afgem na wachimbaji wadogo wa Mererani

Tanzanaiti ni madini ya mawe ya thamani yenye rangi ya zambarau ya kibuluu, yanayopatikana Tanzania pekee.

Eneo la ardhi yenye tanzanaiti inasemekana lipo katika eneo la kilometa za mraba 20 tu huko Mererani. Eneo hili

limegawanywa katika safu ya vitalu, A, B, C na D. Kitalu C chenye kilomita za mraba 8 kinasemekana kuwa na

mashapo ya madini mengi zaidi, tani milioni 2.2 za tanzanaiti kwa makisio. Tanzanaiti iligunduliwa katika eneo hili

mwaka 1967, na mji wa Mererani sasa una wakazi 75,000 (Majtenyi na Muindi, 2001). Ni makazi yenye ‘vurugu na

uhalifu yanayoweza kufananishwa na mji wa machimbo ya dhahabu wa California (Lovgren, 2001:1).

Mnamo mwaka 1999, Kampuni ya Kimataifa ya Afrika ya Kusini, (Afgem Ltd.), ilitafuta na kupata miliki ya

miaka 13 ya uchimbaji madini katika Kitalu C.Ilipofika mwaka 2001, Afgem ilishawekeza dola za kimarekani

milioni 8 katika miliki hiyo, na dola nyingine milioni 12 zingefuata mara Kampuni itakapoanza uzalishaji

kamili (Majtenyi na Muindi, 2001).

Hata hivyo, Afgem si wachimbaji madini pekee waliopo Mererani. Kwa kweli shughuli hii inatawaliwa na wachimbaji

wadogo 10,000, ambao wanapinga shughuli za Afgem kwa sababu zifuatazo (Majtenyi na Muindi, 2001):

• Wanaishutumu Afgem kwa kujaribu kuhodhi uchimbaji wa tanzanaiti katika eneo hili, na kwa kujaribu

kuwaondoa wachimbaji wadogo kutoka eneo hili. Afgem inajibu vikali hoja hiyo kuwa: asilimia 70

ya miliki yake inachimbwa kinyume cha sheria. Katika shimo la pili kati ya mawili ya mgodi wake,

wafanyakazi waligundua njia ya chini kwa chini inayokwenda mpaka kwenye eneo la machimbo ya

wachimbaji wadogo katika Kitalu B (Lovgren, 2001).

• Mara baada ya kupata miliki, Afgem ilianza kuzungushia uzio Kitalu C. Hata hivyo wachimbaji

wenyeji wanadai kuwa, mipaka kati ya sehemu hizi nne haiko wazi na kwamba Afgem haina haki ya

kulitenga eneo hilo.

• Inadaiwa kuwa Afgem ilijaribu hata kupiga chapa vito vyake kama alama ya ubora na uhalali.

Wachimbaji wenyeji wanatoa rai kuwa hii kwa kweli, ni hila ya kuhakikisha kuwa vito vyao

vinaonekana kuwa vya bandia, hali inayowalazimisha kuuza vito vyao kwa wakala wa Afgem tu.

Mwaka 2000, mara Afgem ilipotaka kuzungushia uzio eneo la miliki yake, wachimbaji wadogo waliwavamia.

Askari wa ulinzi wa Afgem walifyatua risasi, wakawaua wachimbaji wadogo saba na kujeruhi wengine

wengi. Mwezi Aprili, 2001, lilifanyika shambulio jingine na kijana mmoja aliuawa. Mwezi Mei uliofuata,

wachimbaji wadogo makumi kadhaa walijeruhiwa wakati wachimbaji 400 walipovamia Kitalu C, wakitaka

Afgem iondolewe kwenye eneo hilo (Majtenyi na Muindi, 2001).

41

Kutoka hapo wachimbaji wadogo wakaifungulia mashitaka Kampuni ya Afgem, wakidai kuwa askari wake

wa usalama waliwatesa wachimbaji wadogo sita. Katika hati ya mashitaka mahakamani, walidai pia kuwa

leseni ya uchimbaji ya Afgem ni batili, kwamba viongozi wa Kampuni huwapekua isivyo halali watembea

kwa miguu na wamewazika wachimbaji wadogo 30 katika mgodi uliotelekezwa. Kutokana na kugubikwa

na hali hii ya vurugu, Waziri wa Nishati na Madini akatangaza Mererani kuwa eneo lililodhibitiwa, na

askari polisi hufanya doria katika kipande cha barabara kinachounganisha mji na barabara kuu eneo la

uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro, umbali wa km. 14. Vilevile serikali imeunda kamati mbili

kuchunguza mapigano hayo (Majtenyi na Muindi, 2001).

Afgem inaungwa mkono na Serikali ya Tanzania, ambayo inatoa rai kuwa kuifukuza kampuni hiyo itakuwa

kinyume na sera inayotetea Sheria ya Madini ya Mwaka 1998. Zaidi ya hayo, Mkuu wa Mkoa, anatoa hoja

kuwa kuifukuza Afgem itakuwa sawa na kukubali kushindwa na uhalifu (Majtenyi na Muindi, 2001).

Migogoro inayotokana na umilki

Kitabu hiki kinafafanua umiliki kama haki ya kusimamia rasilimali. Nchini kote Tanzania (na kiasi fulani cha

Kenya), Usimamizi wa Maliasili Kijamii, umeonekana kuwa ni njia bora ya kuongeza ufanisi wa Usimamizi wa

Maliasili za Taifa. Hivyo Vitengo vya Usimamizi wa Fukwe katika uvuvi, Kamati za Maliasili za Vijiji katika misitu

na Vyama vya Watumiaji Maji kwenye mikondo ya mito, vyote vimeundwa. Ukinzani katika mifumo hii unatokana

na jinsi vinavyotumiwa na kuundwa. Hapa, jamii zinaweza zisihusishwe katika uundaji wa mifumo ya usimamizi,

utekelezaji wake au hata mifumo yake ya sheria. Hali hii inaweza kufanya taasisi hizi zishindwe kutimiza

kazi za usimamizi zilizokusudiwa kutekelezwa. Kwa kuongezea, mitindo ya aina hii ya utekelezaji inaweza

kusababisha taasisi mpya za wenyeji zilizoundwa za usimamizi wa rasilimali kuingia kwenye mgogoro na taasisi

za kijamii zilizokuwepo awali. Litakalokuwa dhahiri kutokana na mifano itakayotolewa hapa chini ni kuwa umiliki

unahusiana na haki ya kuchagua matumizi ya rasilimali, na uwezo wa kuwazuia wengine wasiitumie kwa kazi

tofauti. Hivyo, migogoro ya umiliki pia itahusisha migogoro baina ya aina tofauti za watumiaji wa rasilimali.

Mgogoro wa usimamizi wa Msitu wa Duru – Haitemba

Msitu wa Duru – Haitemba ni msitu wa miombo wenye eneo la hekta 40,000. Katika kingo za msitu

huu kuna vijiji vinane vilivyoanzishwa zamani, ambavyo wakazi wake walikuwa na udhibiti wa msitu –

ingawaje haukuwa imara sana. Utengenezaji mkaa, ulimaji ndani ya msitu na makazi, na uchomaji moto

wa misitu, vyote vilipigwa marufuku. Kutokana na mwongozo wa sera ya serikali, mnamo mwaka 1983 vijiji

hivi vilianza hatua ya kuomba umiliki wa ardhi ya vijiji, ikiwa ni pamoja na miinuko ya misitu inayopakana

navyo. Mnamo mwaka 1985 hata hivyo, Msitu wa Duru – Haitemba uliteuliwa kuwa hifadhi ili kuhakikisha

kuendeleza uzalishaji wake wa siku zijazo, kuhakikisha uhifadhi wake, na likiwa ni jambo geni (wakati ule),

kuufanya msitu ujigharamie wenyewe kwa usimamizi wake kwa kupitia kwa mfano, uwekaji wa vibali vya

kuutumia, au faini. Udumishaji wa uhifadhi wa msitu ulikuwa ufanywe kupitia idadi kubwa ya walinzi wa

msitu. Wawakilishi wa vijiji waliwaonesha waziwazi maofisa msitu wa serikali kuwa ingawaje wanaunga

mkono uhifadhi wa msitu, hawakupenda kuukosa msitu wao kwa ajili ya kufanikisha jambo hili. Mara

tu walinzi wa Msitu walipoanza kazi, shughuli zote za jumuia zilizofanana na hizi ziliachwa. Mashamba

yalilimwa ndani ya msitu, uchomaji mkaa ulianza, ukataji miti ulianza na watu wa nje ya vijiji walipoona

kuwa udhibiti wa serikali ulikuwa ni sawa na kuwa ‘huru-kwa-wote’, walianza kuleta ng’ombe wao msituni

kuwalisha. “Kwa kuondoa hali ya umiliki kwa wenyeji, hata kama ni kwa udhaifu kiasi gani haki za wenyeji

ziliungwa mkono na sheria au zilitekelezwa kwa vitendo, serikali pia iliondoa ulinzi wa kijadi, au utambuzi

katika jamii kwa ujumla kuwa misitu haikuwa mali ya umma…” (Wiley, 1999:53-54). (Rejea: Wiley,1999).

Migogoro baina ya watumiaji rasilimali wa aina tofauti

Jinsi ardhi inavyozidi kuwa adimu katika maeneo ya juu ya Bonde la Mto Pangani, wakulima wanatafuta

ardhi ya ziada na nafasi za umwagiliaji maji kwenye maeneo ya chini. Mapema mwaka 1946, Johnston

alisema kuwa “…kadiri Wachaga wanavyopanua makazi (vihamba) yao kuelekea upande wa chini ya

mitelemko ya Mlima Kilimanjaro, ndivyo watakavyoanza kuwachukia wageni ambao machifu hapo awali

42

waliwaruhusu kufanya makazi” (uk.4). Mgogoro huu baina ya watu wa makabila mbalimbali huzidi pale

ambapo mahitaji ya pande zote ni ardhi na maji. Mahitaji tofauti ya rasilimali hata hivyo, siyo lazima

yaondoe msingi wa mgogoro. Sehemu kubwa ya ardhi katika maeneo ya nyanda za chini za bonde kiasili

zilitumiwa na wafugaji wa Kimasai. Wamasai wanachukulia uhamiaji kuingia kwenye ardhi yao ya jadi

kama uvamizi kwenye eneo lao, na ubadilishaji wa eneo zuri kwa malisho kwa matumizi mengine.

Wilaya ya Simanjiro iko upande wa Kusini wa mji wa Arusha na ndani yake kuna mji wa Machimbo wa

Mererani. Mwaka 1995, asilimia 85 ya wakazi wake 65,000 walikuwa ni wafugaji wa Kimasai. Ufugaji mara

nyingi huchukuliwa kuwa ni njia muafaka zaidi ya matumizi ya ardhi katika ardhi kame na nusu kame za Afrika.

(cf Warren,1995). Mifumo hii, hata hivyo, huchukulia kiwango fulani cha rasilimali kuwa cha kudumu. Taasisi

za usimamizi wa rasilimali za mifugo, mitindo ya maisha inayohusiana na miundo ya kijamii mara nyingi

hujengwa katika msingi wa kuwa eneo lao halitabadilishwa matumizi yake. Hali haikuwa hivyo Simanjiro.

Ardhi ya jadi ya malisho ya Wamasai wa Simanjiro imekuwa katika tishio kutoka pande tatu:

• Kilimo cha Biashara: hadi kufika mwaka 1994, hekta 50,000 za ardhi ya Simanjiro zilikuwa zimetengwa

kwa matumizi ya kilimo cha mashamba makubwa ya kati ya hekta 90 na 13,000. Mashamba haya

yalizalisha zaidi maharage kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Uholanzi. Ili kuwakatisha tamaa na kuwazuia

wafugaji kuchungia ng’ombe wao katika mashamba haya, mabaki yote ya mimea huchomwa mara tu

baada ya mavuno (Ole Sikar, 1996:1)). Wenye ardhi pia waliwakamata ng’ombe, waliwatoza faini watu

walioingia bila ruhusa, na ole Sikar anadai kuwa, waliwapiga risasi mifugo na wachungaji wao.

• Uchimbaji madini – wa viwango vidogo na vikubwa, umezuia maeneo makubwa ya ardhi ya

Simanjiro ambayo ama yameharibiwa vibaya kiasi kwamba hayatoi malisho mazuri, au

yamefungwa kabisa kwa kuchungia wanyama.

• Utalii: Kama ilivyokuwa kwa wafugaji ndani na kuzunguka Hifadhi ya Wanyamapori ya Mkomazi,

ardhi ya Simanjiro imetengwa kwa madhumuni ya kuwalinda wanyamapori. Wamasai wa wilaya hii

wanatoa hoja kuwa hii haina umuhimu, ikichukuliwa kwamba wameishi pamoja na wanyamapori kwa

karne nyingi. ‘Kaya zimelazimishwa kuacha kuchunga wanyama wao katika maeneo haya. Wakati

huo huo wanyamapori wameruhusiwa kula majani pamoja na wanyama wafugwao katika maeneo

ya asili ya kuchungia kama vile nyanda tambarare za Simanjiro’ (ole Sikar, 1996:2). Kwa nyongeza,

Wamasai wanalalamika, wanyamapori huambukiza mifugo yao maradhi. Wamasai wa Simanjiro

hawakufidiwa kwa malisho yaliyopotea wala mifugo iliyokufa kwa magonjwa ya wanyamapori.

Mielekeo hii imetokea kinyume na misingi ya sera rasmi ya serikali inayotaka kuwepo,hususan, uwekezaji

wa viwango vikubwa katika kilimo na viwanda unaokusudia kukidhi mahitaji ya nchi zaidi ya maslahi ya

wafugaji wenyeji. Hivyo mikakati inayokusudiwa kufikia malengo ya taifa inaweza kusababisha ugumu

wa kutatua matatizo ya usimamizi wa ndani, na matatizo ya kutumia rasilimali zenye ugumu kuzisimamia

hivyo kusababisha matumizi yaliyokithiri na migogoro mahali hapo. Kwa maana hii, migogoro ya Simanjiro

na maeneo mengine ya Wamasai pia ni migogoro ya viwango, na hutoa kielelezo cha mfano wa jinsi

migogoro ya viwango inavyoweza pia kuwa migogoro ya umiliki wakati huo huo.

Wilaya ya Taita–Taveta nchini Kenya haina kinga ya migogoro hii.Theluthi mbili ya ardhi ya wilaya iko chini

ya wamiliki wawili tu wa ardhi na halmashauri ya jimbo. Matokeo yake, idadi kubwa ya wenyeji wa Taita–

Taveta wanakaa katika maeneo kinyume cha sheria. Vilevile kuna mgogoro mkubwa kati ya watu wasio

na ardhi na wale wanaomiliki ardhi. Migogoro kama hii inaleta utata sana katika usimamizi wa maliasili za

wilaya, tatizo ambalo linakwenda hadi kwenye sekta ya maji.Wakazi wasio rasmi wanaolima katika eneo

hili nusu kame wanategemea zaidi umwagiliaji (Musyoki, pers.comm.). Hata hivyo, hawana vibali vya maji

kama inavyotakiwa wawe, na maji mengi zaidi hata hivyo, yanatumiwa katika maeneo ya juu ya mto na

makampuni makubwa ya katani wilayani. Kwa kiasi fulani katika juhudi za kushughulikia mgogoro wa eneo

hili, serikali imenunua hekta 9,700 katika jitihada za kutafuta ardhi kwa ajili ya wakulima wadogo wadogo.

43

Migogoro kati ya mitazamo inayotofautiana ya usimamizi wa maji: mfano

kutoka Mlima Kilimanjaro

Tagseth (2002) anaonelea kuwa kushindwa kwa mifumo ya utawala rasmi katika bonde kutambua haki za kimila

za maji na utawala wake umekuwa chanzo cha mgogoro kati ya maslahi ya kimila na utawala rasmi wa Bonde la

Mto Pangani. Moja ya njia iliyotumiwa na utawala rasmi katika bonde ni utumiaji wa milango (banio) ya kudhibiti

maji. Inasemekana kuwa, kwa kuwa jamii za wamwagiliaji wa viwango vidogo hawakushirikishwa kwanza,

walichukulia udhibiti huo kama ukiukaji mkubwa wa haki zao za kupata maji. Kwa sehemu kubwa, milango hiyo

imehujumiwa au imeharibiwa kabisa (Mchoro wa 4).Katika maeneo mengine, wanavijiji wamechimba sehemu

mpya za kuchukulia maji katika kingo za mto kuzunguka milango ya kudhibiti maji (Shishira, 2002).

PAMOJA (2002) inaeleza kuwa jamii zilizoko katika bonde zinachukulia kupata maji kama moja ya haki zao za

msingi, na hawaridhiki na jitihada za serikali za kuweka ada na sheria kwa matumizi yake. Sehemu kubwa ya

ukinzani wa jamii kwa utawala wa Bonde la Mto Pangani unatokana na mtazamo wao kuwa watumiaji wakubwa

wa kibiashara wanapendelewa kuliko wao wenye matumizi madogo zaidi ya maji. PAMOJA inadai kuwa utaratibu

wa Serikali wa amri kutoka juu kwenda chini, ambao hauna majadiliano ya pande mbili, huleta ugumu wa

kutatua migogoro. Wanafikiri kuwa njia za majadiliano, zina uwezo wa “kutoa mwelekeo kwenda mbele na

kuyafikia mahitaji na dhamira za watunga sera, watunga sheria na jamii kadhalika” (PAMOJA 2002:2).

Katika Mlima Kilimanjaro, Mwenyekiti wa kamati ya mfereji alikuwa akisimamia kijadi mfereji wa umwagiliaji.

Daima wenyeviti huwa wanaume, na wanapatikana kutokana na ukoo wa mtu ambaye ndiye aliyechimba

mfereji huo. Mfereji hupitia kwenye ardhi ya watumiaji mbalimbali maarufu wa maji, wengi wao wakiwa wanahitaji

kuyatumia kwa madhumuni ya umwagiliaji. Ili kuweza kupatiwa maji, watumiaji lazima wawachangie

wafanyakazi wa ukarabati ambao mara kwa mara hufanya doria kwenye mfereji kukagua uharibifu. Sheria

mbalimbali za ziada zinasimamia matumizi ya maji, kama vile nyakati ambazo maji yanaweza kuchukuliwa,

zamu za matumizi ya maji baina ya watumiaji na kadhalika. Sheria hizi sio kuwa hazibadiliki. Hii ni muhimu

kwa sababu baadhi ya watu walio kando kando ya mifereji wanaweza kuhitaji maji kidogo kuliko wengine,

wakati wengine wanahitaji maji mengi zaidi. Gillingham (1999) anaelezea njia tano ambazo watu wanaohitaji

maji zaidi kuliko vibali vyao vinavyoruhusu wanaweza kupata maji ya ziada: ya kwanza ni ‘kuazima’

maji - mtu anayehitaji maji zaidi anaweza kuazima maji kutoka kwa mtu anayemfahamu kuwa anahitaji maji

kidogo. Hii ndiyo njia inayotumika zaidi ya kupata maji ya ziada kwa mtu anayehitaji. Njia ya pili ni ya kupata

maji ya ziada kutoka kwenye mfereji wa jirani. Njia ya tatu ni kununua maji – hapa, mtu aliyetumia maji

kidogo kuliko anayohitaji anaamua kuuza yaliyobaki kwa mtu anayemjua kuwa anahitaji maji mengi kuliko

mgao wake. Kwa vile maji yanachukuliwa kuwa ni ‘zawadi kutoka kwa Mungu’, hivyo si halali kuyanunua

wazi wazi. Wauzaji hukwepa ukweli huu kwa kutoa kazi kwa mnunuzi, na hivyo wakiulizwa husema kuwa

mnunuzi anaazima mabaki ya mgao wao wa maji. Njia ya nne ni kumwagilia usiku wakati ambapo hakuna

mgao wa maji. Mwisho, njia ya tano ya kupata maji ya ziada ni kwa kuiba, kwa mfano kumwagilia wakati ni

siku ya zamu ya mtu mwingine, ingawaje hii haitokei mara kwa mara (Gillingham, 1999).

Sheria kuweza kubadilika badilika, Gillingham (1999) anaeleza, ‘….ni muhimu kwa ufanisi wa mgao

na uendelevu wa mfumo wa umwagiliaji …… kama watumiaji wote wa mifereji wangelazimika kutumia

mgao wao rasmi tu, mfumo wa umwagiliaji wa kutumia mifereji ungetosheleza mahitaji ya umwagiliaji

ya watumiaji mifereji wachache sana’. Gillingham anasema mfumo huu ni wa kutegemewa, kwa sababu

wizi hauruhusiwi chini ya mfumo rasmi wa ugawaji wala chini ya kanuni za kazi – laiti kama mfumo huu

ungekuwa si wa kutegemewa, watu wasingechangia ukarabati wa mifereji. Uhusiano mkamilifu baina ya

sheria rasmi na za kazi unachukua muda mrefu kukua – mifereji ya kwanza kwenye Mlima Kilimanjaro

ilichimbwa katika karne ya 18. Katika maeneo ya nyanda za chini, ambako makazi yameanza hivi

karibuni, hali ya hewa imekuwa kavu zaidi, watu wametawanyika zaidi na tofauti za kijamii zimekuwa

kubwa zaidi, hivyo uhusiano kati ya sheria rasmi na za kazi sio mkubwa sana.

Sheria hizi zinasisitiza usawa wa jamii na kupunguza migogoro. Hazikai vizuri na sheria mpya, zinazoshinikizwa

kutoka nje ambazo zinataka matumizi bora ya maji. Kwa nyongeza, sheria hizi mpya zinataka kuanzisha

Vyama vya Watumiaji Maji (WUAs), ambavyo si sawa na Kamati za Mifereji. Vyama vya watumiaji maji

44

vinategemewa kukusanya ada kutoka kwa watumiaji maji ambazo zitachangia kulipia kibali cha kutumia maji,

inayopatikana kutoka Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani. Katika utamaduni ambapo maji yanaonekana kuwa

ni ‘zawadi kutoka kwa Mungu’, wazo kuwa ni lazima maji yalipiwe halina mantiki. Kwa nyongeza, Gillingham

anahofia kuwa sheria zilizoamriwa kutoka nje hazielekei kufanikiwa kuliko zile zilizotokea ndani ya jamii,

ambazo zimebadilishwa kulingana na sifa za utamaduni na mazingira ya jamii kwa muda wa kipindi kirefu.

Gillingham anaamini kuwa kutooana kati ya mchakato wa usimamizi katika ngazi ya wenyeji na ile ya ngazi

ya nje kunaweza kuhatarisha mafanikio ya juhudi za usimamizi zilizoanzia nje.

Migogoro inayotokana na mahali

Watumiaji maji waliopo katika maeneo ya juu ya mto wapo mahali pazuri zaidi pa kupatia maji kuliko watumiaji

wa eneo la chini. Kama msingi wake mkubwa, matatizo haya yanaonekana katika mifereji ya umwagiliaji

ambapo watumiaji walio karibu na chanzo cha maji wanaweza kulima mazao yanayohitaji maji mengi sana.

Kwa mfano, mpunga wa kumwagiliwa unahitaji lita 3,000 za maji kutoa mavuno ya kilogramu moja. Watumiaji

waliopo mwishoni mwa mfereji, wanalazimika kulima mazao yanayohitaji maji kidogo. Matatizo makubwa

yanayoikabili mitambo ya umeme wa maji iliyoko katika maeneo ya chini ya mto ni mfano mwingine.

Skimu ya Umwagiliaji ya “Lower Moshi”

Kabla ya kuanzishwa kwa Skimu ya Umwagiliaji ya “Lower Moshi” mnamo mwaka 1987, kulikuwa na kiwango

kidogo sana cha kilimo cha mpunga wa umwagiliaji katika eneo hili, na wakulima walitegemea kuvuna kadiri ya

tani 2 za mpunga kwa hekta. Kufuatia kukamilika kwa skimu hiyo, mavuno yaliongezeka kufikia tani 8 kwa hekta,

hali iliyoshawishi wakulima wa nje ya mradi kujaribu kuiga mbinu za kilimo za skimu hiyo. Matokeo yake, mahitaji

ya maji yaliongezeka sana, kiasi cha kusababisha tatizo la kudumu la upungufu wa maji katika maeneo ya upande

wa chini ya skimu. Skimu yenyewe imekabiliwa na upungufu wa maji kwa sababu ya matumizi makubwa ya maji

katika maeneo ya juu, na imelazimika kupunguza eneo la umwagiliaji kutoka hekta 2,300 hadi 647 mnamo mwaka

1994. Wakulima waliohusishwa katika Skimu hawakufurahia kabisa hali hiyo, walieleza kuwa mgao wao wa maji

ulifuata programu iliyopangwa vizuri. Watumiaji wa maeneo ya upande wa juu hawakuwa na programu kama hii,

hivyo walisababisha upungufu wa maji katika eneo la Skimu. Zaidi ya hayo, wakulima walidai kuwa watumiaji maji

wa maeneo ya upande wa juu walikuwa na ushawishi katika serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), (chama

tawala cha Tanzania), hivyo wasingeweza kubughudhiwa (Mujwahuzi, 2001; 134 na 136).

Mgogoro baina ya wamwagiliaji wadogo na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania

TANESCO inadai kuwa inahitaji angalau mita za ujazo 40 kwa sekunde kuendesha mitambo ya umeme

wa maji ya Maporomoko ya Pangani . Baada ya maji kufunguliwa kutoka katika Bwawa la Nyumba ya

Mungu na kuingia mto Pangani, maji ya nyongeza yanaungana na mto huo kupitia vijito vyake vichache.

Hata hivyo hadi maji yafikapo kituo hicho, mara nyingi huwa hayatoshelezi kuendesha mitambo. “Wakati

mwingine tunakuwa na maji kidogo mno kiasi kwamba inabidi tufunge kituo na kuacha maji kujikusanya

kwa usiku mzima, ili tuweze kufungua tena asubuhi” (Lugeiyamu, Mhojiwa).

Kadiri ardhi inavyokuwa adimu zaidi na zaidi katika sehemu za juu za bwawa la Nyumba ya Mungu,

kilimo katika eneo la upande wa chini wa bwawa pia kimeongezeka. Kwa kuwa hali hapa ni ya joto zaidi

na mvua ni haba, haja ya kumwagilia ni kubwa zaidi. Kwa hiyo, Meneja wa kituo cha uzalishaji umeme

cha maporomoko ya Pangani analalamikia uchukuaji wa maji usiodhibitiwa ambao unasababisha wao

kupata kiasi cha maji kisichotosheleza mahitaji. Anafafanua kuwa wakati ambapo maji kwa ajili ya

mitambo yake yamepungua, maeneo ya umwagiliaji hayapungukiwi. “Wamwagiliaji wadogo hawatumii

umeme, hivyo hawayaelewi matatizo haya” (Lugeiyamu, Mhojiwa).

Wakati huo huo, udhibiti wa uchukuaji wa maji umepungua. Wakati mradi mpya wa Maporomoko ya

Pangani ulipojengwa, kulikuwa na fedha za kujengea milango (banio) ya kudhibiti maji kwenye sehemu

muhimu za kuchukulia maji kutoka mitoni na ufuatiliaji wake. Kwa vile utoaji wa fedha umepungua,

ufuatiliaji umekuwa siyo wa mara kwa mara, milango ya kudhibiti uchukuaji maji imeharibiwa na /au vituo

vipya vya kutolea maji vimeanzishwa kwenye kingo za mito.

45

Matokeo ya hali hii ni kupungua kwa uzalishaji wa umeme. Katika mwezi Aprili mwaka 1999, kituo cha uzalishaji

umeme cha maporomoko ya Pangani kilizalisha kWh milioni 45. Mwezi Aprili mwaka 2002 zilizalishwa kWh

milioni 25. Ni dhahiri kuwa hili lina athari ya wazi kwenye uvutiaji wa uwekezaji kwenye mtambo. TANESCO,

kwa sasa, inataka kubinafsishwa. “Kama mtambo wa kuzalisha umeme wa Nyumba ya Mungu una uwezo

wa kuzalisha MW 8 na tunaweza kutoa 3 tu, ni nani atakayewekeza kwetu?” (Lugeiyamu, Mhojiwa).

C.8 Majumuisho ya hoja

Kwa undani wake, matatizo yanayokabili matumizi ya rasilimali katika Bonde la Mto Pangani yanahusiana

na ongezeko la watu katika mazingira ya viwango vikubwa vya umasikini. Umasikini na uharibifu wa

mazingira mara nyingi huonekana vinahusiana (cf. WCED, 1987). Matatizo ya kusimamia Rasilimali za

Jamii (CPRs) mara nyingi yanafikiriwa kuongezeka kunapokuwa na idadi kubwa ya watu wanaohusika,

hususan pale umoja wao wa kijadi unapokuwa dhaifu (cf. Ostrom, 1990). Muundo na kazi za utafutaji

maisha vijijini unaweza kuhatarishwa endapo uwezo wa watu wa vijijini wa kutawala na kujihakikishia

njia za kutosha za kujipatia riziki zitakuwa hatarini.

Sura hii imepitia matatizo haya kwanza kwa kuainisha ‘vivutio’ vikuu ndani ya bonde. Baada ya hapo

ikaendelea kuangalia migogoro mbalimbali iliyomo baina yao. Dondoo muhimu zinazoweza kupatikana

kutokana na majadiliano haya ni kama ifuatayo:

• Shughuli muhimu katika bonde ni pamoja na shughuli za viwanda (umeme, madini na kilimo),

kilimo (mashamba makubwa na madogo, yote kwa kiasi kikubwa yanategemea umwagiliaji),

shughuli za ufugaji (hususan katika nyanda za chini), na shughuli za mijini ambazo zinakua.

Sura hii ililenga kimsingi kwenye matumizi ya maji ya shughuli hizi. Waliofanya kazi kati ya

shughuli hizi mbalimbali na wingi wa maliasili ndani ya bonde hili ni pamoja na mashirika yasiyo

ya kiserikali na wakala wa wahisani wa kimataifa. Mamlaka yao kimsingi ni kuhifadhi na/ au

kuendeleza na kuwezesha upatikanaji wa riziki vijijini.

• Ni muhimu kutambua kuwa idadi ya watu katika bonde hili ni kubwa, na kwamba kwa wengi wao, riziki

hupatikana kutokana na kilimo, na kwamba kuna mengi yanayoashiria kwamba wako hatarini kiuchumi.

Kwa kuongezea, utofauti na utajiri wa rasilimali za bonde hili una maana kuwa wenye shughuli kubwa

kubwa wanavutiwa na bonde hili, na uwekezaji wa kutosha umefanyika. Kati ya shughuli hizi za viwango

vikubwa na shughuli za viwango vidogo vya kujipatia riziki, kuna mwanya mkubwa wa migogoro.

• Sura hii inaigawa migogoro katika makundi makuu matatu yanayohusiana. Kundi la kwanza

linahusiana na migogoro ya viwango, ambapo imeelezwa kuwa watumiaji wadogo wadogo

mara nyingi inabidi washindane dhidi ya watumiaji wakubwa kwa rasilimali hizo hizo. Kundi

la pili linahusiana na migogoro ya umiliki. ‘Umiliki’ hapa una maana ya haki ya mtu kusimamia

rasilimali zake, na mgogoro hutokea baina ya vyanzo tofauti vya usimamizi na kipaumbele.

Daraja la tatu la mgogoro linahusiana na mahali. Hapa, jinsi mahali pa kundi la watumiaji wa

rasilimali panavyoweza kuwaingiza kwenye mgogoro na watumiaji wa mahali pengine, ni jambo

lililoangaliwa. Mfano mzuri wa mgogoro kama huo ni ule baina ya watumiaji wa maeneo ya juu

na wale wa maeneo ya chini ya mto.

• Kwa hiyo, ni wazi kuwa tofauti ya rasilimali katika Bonde la Mto Pangani husababisha pia aina

tofauti za migogoro. Changamoto ya Bonde la Mto Pangani ni kwa kiasi gani menejimenti

inaweza kushughulikia migogoro ya viwango vyote na matatizo ya ugawaji wa maliasili

yanayoambatana.

46

D

Usimamizi wa Maliasili katika

Bonde la Mto Pangani

D.1 Utangulizi

Sura hii inaangalia Usimamizi wa Maliasili za Bonde la Mto Pangani. Katika sehemu ya kwanza, utawala

‘rasmi’ wa bonde unaangaliwa. Mikono mingi ya serikali inalitawala bonde hili. Hili pekee ni tatizo kwa

sababu inaweza kumaanisha kuwa juhudi za tawi lolote zinaweza kudhoofisha shughuli za matawi mengine.

Kwa mfano, juhudi za hifadhi ya maji zinaweza kudhoofishwa na shughuli za maendeleo ya umwagiliaji.

Zaidi ya hayo, serikali kuu inaweza kutaka kutekeleza sera za taifa katika bonde bila kuzingatia hali ya

mahali, mahitaji na matatizo ya rasilimali. Mwishowe, humaanisha pia kupatikana usimamizi ambao kwa

kiwango kikubwa ni mwelekeo wa kisekta unaosababisha,idara za misitu kutokuwa na habari, kwa mfano,

kuhusu juhudi za uendelezaji wa wanyamapori. Wakati juhudi za uendelezaji wa wanyamapori zinaweza

zisihusike na misitu moja kwa moja, huwa zinahusika na usimamizi wa jumla wa bonde, ambao sekta hizi

zote ni sehemu yake muhimu. Sehemu ya kwanza ya Sura hii inazingatia shughuli za sekta kuu mbili katika

Bonde: maji na misitu, na kuzitathmini katika mtazamo wa utoaji huduma ya usimamizi.

Sehemu ya pili inazitathmini shughuli za usimamizi katika ngazi ya jamii, wakati ya tatu inazingatia

usimamizi wa bonde kuvuka mipaka ya nchi. Sehemu ya nne inashughulikia matatizo ya ufuatiliaji na

ukusanyaji data katika bonde. Sehemu ya mwisho itatoa muhtasari wa matokeo ya Sura hii.

D. 2 Usimamizi wa Serikali, Sheria na sera

Utawala wa maji: sheria na sera

Sheria mama ya kusimamia rasilimali za maji Tanzania ni Sheria ya Usimamizi wa Rasilimalui za Maji ya

mwaka 2009 inayoweka misingi ya kutekeleza Sera ya Maji 2002. Sheria hii inafuta sheria ya zamani ya

Udhibiti wa Matumizi ya Maji ya mwaka 1974. Sheria ya Udhibiti wa maji ilianzisha mfumo wa kusimamia

rasilimali za maji kwa kufuata mipaka ya mabonde. Kwa mujibu wa sheria hiyo na marekebisho yake

ya 1981 mabonde 9 yalianzishwa na kuchapishwa katika gazeti la serikali lakini ilichukua miaka 10 kwa

mamlaka (ofisi za maji) za kudhiti matumizi ya maji kuanzishwa Ofisi ya Maji Bonde la Pangani ilikuwa

ya kwanza kuanzishwa mwaka 1991 ikifuatiwa na Ofisi ya Maji Bonde la Rufiji mwaka 1993, kufikia 2004

ofisi za mabonde yote 9 zilikuwa zimeanzishwa. Kuanzishwa kwa ofisi ya Pangani ilitokana na shauku ya

wafadhili wa mradi wa umeme kwenye maanguko ya Pangani kuwa maji yasingetosha kwa mradi huo

kama kusingekuwa na udhibiti wa matumizi ya maji ya mto Pangani na wakati huohuo migogoro mingi ya

matumizi ya maji inajitokeza na kuongezeka katika mabonde ya Pangani na Rufiji.

Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji inaweka mfumo wa kisheria na kitaasisi kwa usimamizi

wa mabonde ya mito kama sera inavyoelekeza na imeweka ngazi tatu za usimamizi: Taifa, Bonde na

Mabonde madogo. Serikali za mitaa na vyombo vya kijamii au jumuiya za watumia maji ni washirika

wakuu katika baadhi ya taasisi hizi na Waziri anaweza kukasimu baadhi ya majukumu kwa vyombo hivi.

Maji ni rasilimali ya umma na yamekasimiwa kwa Rais kwa faida ya raia; hivyo kitaifa Waziri mwenye

dhamana ya maji ni msimamizi mkuu wa shughuli zote za rasilimali za maji na mwenye mamlaka ya

rufaa. Waziri anao wajibu wa kutayarisha wa Sera ya Taifa na mkakati, kuteua Wajumbe wa Bodi ya Maji

ya Taifa, Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji na Maafisa wa Maji wa Bodi za Madonde. Waziri anaunda

Bodi za Maji za Mabonde na kamati za mabonde madogo na kuwezesha uratibu na upangaji mipango

wa kisekta. Waziri anasaidiwa na Mkurugezi wa Rasilimali za Maji, kushauriwa na Bodi ya Maji ya Taifa

katika masuala ya uratibu wa sekta mbalimbali kuhusu mipango na usimamizi shirikishi wa rasilimali za

47

maji. Mkurugenzi ni mshauri mkuu wa Serikali juu ya masuala yote ya rasilimali za maji, anasimamia na

kuratibu shughuli za Bodi za Mabonde, kuandaa Mpango wa Kitaifa wa Rasilimali za Maji na kutayarisha

mkakati wa utekelezaji wake, kuratibu utayarishaji wa mipango ya mabonde na kwa ujumla kuhakikisha

uratibu wa maendeleo ya rasilimali za maji, usimamizi na udhibiti wake.

Bodi mpya za maji zina mamlaka katika mambo yote yanayohusu ugawaji usimamizi na kulinda rasilimali

za maji katika bonde husika na uandaaji wa sera na mipango inayolenga katika usimamizi na uendelezaji

wa rasilimali za maji na kuzuia uchafuzi wa maji. Bodi za maji zina uwezo wa kisheria na kiutendaji katika

kuandaa mipango ya maji inayojumuisha mipango ya sekta zingine na mipango ya wilaya. Bodi huratibu

shughuli za sekta mbalimbali katika mambo yanayohusu maji, zinaidhinisha utoaji wa vibali vya kutumia

maji, hufuatilia, hutathmini na kuidhinisha ujenzi wa miundo mbinu ya maji na kwa ujumla hufuatilia hali ya

mito, maji chini ya ardhi, mabwawa na maziwa, ardhioevu na hutekeleza sheria. Bodi za maji humshauri

mkurugenzi wa maji na huratibu shughuli za kamati za mabonde madogo. Afisa wa Maji wa Bonde ni

mtendaji mkuu wa bodi mwenye majukumu ya kusimamia shughuli zote za bodi na ni katibu wa bodi. Bodi

ya maji ya Pangani inategemewa kufanya kazi kwa kufuata mfumo wa kitaasisi kama unavyoelekezwa na

Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji ya mwaka 2009.

Ofisi ya Maji Bonde la Pangani hushawishi uundaji wa vyombo vya watumiaji maji na kwa kawaida wakulima

wadogo wadogo wanaotumia chanzo kimoja cha maji na miundombinu moja ya kuchukua maji wanajiunga

katika umoja wa watumiaji maji ambao huomba kibali cha kutumia maji kwa niaba ya wanaumoja wake.

Ingawa vyombo vya watumiaji wa maji ni vya manufaa kwa washiriki mitazamo ya watu wengine ni kuwa

vyombo vya watumiaji wa maji ni vya manufaa kwa ofisi ya bonde kwani hukusanya ada ya maji kutoka

kwa mtumiaji maji mmoja mmoja. Umoja wa watumiaji wa maji hukusanya maduhuli kutoka kwa washiriki

wake kwa ajili ya uendeshaji wa mradi na kiasi kidogo hutumika katika kulipia ada ya hutumia maji.

Ofisi ya Maji ya Bonde inahimiza uundaji wa Vyama vya Watumiaji Maji (WUAs), na kwa hakika, maji kwa

ajili ya umwagiliaji yanaweza kuombwa na vyama hivyo pekee. Hili linasemekana kuwa linarahisisha

shughuli za utawala, kwa sababu Ofisi ya Bonde itakuwa inashughulika na Vyama badala ya watu

wengi binafsi. Vyama vya watumiaji maji vinatarajiwa kukusanya ada kutoka kwa watumiaji maji ambayo

hatimaye itatumika kulipia hati zao za maji.

Mwanzoni mwa miaka ya 1990, wenye hati za maji katika Bonde la Mto Pangani walitumia jumla ya mita

za ujazo 33.4 kwa sekunde, lakini ukaguzi uliofanywa na Ofisi ya Bonde mwaka 1992/93 ulionesha kuwa

matumizi halisi yalifikia mita za ujazo 48 kwa sekunde (Mujwahuzi, 2002). Kuna hati za maji 567 za kudumu

katika mikoa minne ya Tanzania ambayo imo katika Bonde la Mto Pangani, wakati ambapo hati za muda

zilizotolewa ni 300. Hata hivyo, kuna karibu matumizi mara mbili zaidi yanayofanyika bila ya hati za maji

(Jedwali la 6). Karibu asilimia 46 ya hati za kudumu na za muda zilizotolewa zinatoka mkoa wa Kilimanjaro.

Karibu asilimia 66 ya matumizi ya maji yasiyo rasmi kisheria katika bonde hutokea katika mkoa huu.

Kwa hiyo ni wazi kuwa kuna matatizo makubwa katika kufuatilia matumizi ya maji na katika kutekeleza vifungu

vya sheria ya maji ya Tanzania. Baadhi ya matatizo yanayoikabili Ofisi ya Maji ya Bonde ni haya yafuatayo:

• Ingawa kuna vituo vingi vya upimaji/ufuatiliaji katika eneo lote la bonde, uendeshaji wake siyo

sahihi, na mara nyingi data zinapingana kwa sababu vituo vinakwama kufanya kazi. Ufuatiliaji

kwa kutumia watu pia unafanyika lakini wakusanyaji data mara nyingi hawalipwi vizuri na hukosa

motisha ya kukusanya data hizi. Matokeo yake, hati za maji hutolewa bila kujua kwa hakika kiasi

cha maji kinachopaswa kugawanywa. Data muhimu za ziada, kama vile data za mtiririko wa maji

kwa ajili ya mahitaji ya mazingira, hazipatikani, na Ofisi ya Bonde haifahamu ni kiasi gani cha maji

ni lazima kibakizwe katika bonde kwa matumizi ya mifumo ikolojia (Sarmmet, Mhojiwa)

• Kwa vile matumizi mengi ya maji hayana hati za kisheria, si rahisi kwa Ofisi ya Maji Bonde la

Pangani kujua kiasi halisi cha maji kinachukuliwa.

• Ofisi ya Maji ya Bonde la Mto Pangani na ofisi za mabonde mengine hazina uwezo wa kitaasisi

na kifedha wa kusimamia kufuatilia na kudhibiti matumizi yote ya maji katika bonde. Ndiyo maana,

milango mingi ya kudhiti maji iliyojengwa na ofisi ya bonde la Pangani katika makutano ya mifereji

na mito mwaka wa 1994 ilibomolewa na wananchi ambao hawakutambua matumizi yake na

48

ambao walikuwa hawataki kulipa ada za maji. Uharibufu huu ungeweza kuzuilika kama wahusika

wangeelewa manufaa ya milango hiyo na kama serikali za mitaa zingehusishwa mapema katika

kuandaa mpango wa ujenzi huo.

• Ofisi ya Maji Bonde la Pangani inapaswa ijitegemee kiutawala na kifedha. Hata hivyo, watumiaji wengi

wa maji wanaamini kuwa maji ni ‘zawadi kutoka kwa Mungu’, na hukataa kulipia hati zao za maji, pamoja

na viwango kuwa vya chini sana. Hivyo Ofisi ya Bonde inakabiliana na matatizo makubwa ya uhaba wa

fedha. Sheria iko kimya kuhusu jinsi ya kuwashughulikia wadaiwa. Matokeo yake, karibu asilimia 60 ya

madai ya ada ya matumizi ya maji kwa mwaka hayalipwi (Sarmett na Kamugisha, 2002).

• Sheria ya usimamizi wa rasilimali za maji hajaweka uhusiano wa moja kwa moja kati ya Bodi ya Maji

Bonde la Pangani na Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs) au ngazi za chini za utawala kusaidia

uwakilishi katika bodi ya bonde na kamati za mabonde madogo. Hata hivyo, Waziri anaweza

kukasimu utekelezaji wa jukumu lolote kwa mamlaka ya serikali za mitaa kama ilivyoelekezwa

katika sheria. Maafisa wa Maji si sehemu ya mamlaka za serikali za mitaa na hawana majukumu

sawa katika bonde, lakini ni muhimu wakafanya kazi pamoja kwa misingi ya shabaha moja lakini

yenye utekelezaji tofauti. Kufanya kazi na LGAs na mkusanyiko wa wadau wengine na mahitaji

mbalimbali ya kisekta ni changamoto kwa Maafisa wa Maji ambao wanatakiwa kuwa weledi kwa

mtazamo huu. Kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji, Bodi za Mabonde

zinatakiwa kujumuisha mipango ya Wilaya ndani ya mipango ya usimamizi wa rasilimali za maji

wa mabonde yao ambayo itakuwa na nguvu za kisheria kwa wahusika wote ndani ya bonde.

• Mipaka ya kisheria ya utawala wa Ofisi ya Bonde ni Bonde la Mto Pangani, ambalo halifuati

mipaka rasmi ya kiutawala. Katika bonde hili, Ofisi ya Maji Bonde Pangani inatakiwa kufanya kazi

na serikali za mitaa nyingi sana.

• Mabonde ya mito yana idadi kubwa ya rasilimali zinazohusiana na mabadiliko ya rasilimali moja

yanaweza kuwa na athari kwa rasilimali nyingine. Katika Bonde la Mto Pangani, upangaji wa mipango ni

wa mgawanyiko, kwa misingi ya kisekta, kimkoa au kiwilaya. Bodi za maji zina mamlaka na zinaagizwa

na sheria ya maji kuandaa mipango jumuishi ya usimamizi wa rasilimali za maji katika mabonde yao

ambayo itakuwa na nguvu za kisheria kwa uendelezaji, usimamizi na utunzaji wa maji wowote.

Utawala wa maji nchini Kenya unaongozwa na Sheria ya Maji ya Mwaka 2002 (RoK, 2002). Mpaka sasa,

kadiri usimamizi wa mabonde kwa mapana unavyohusika (kipengele ambacho kimo katika Sheria ya Maji),

Mkakati wa Usimamizi wa Rasilimali za Maji wa Taifa (RoK, 2003) unakuwa na umuhimu mkubwa.

Sheria ya Maji ilianzisha Mamlaka ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji (WRMA) yenye jukumu la

usimamizi na utawala wa sehemu kubwa ya rasilimali za maji za Kenya. Kuna asasi kadhaa zilizopangwa

chini ya WRMA, ambazo zinaelezwa katika Kisanduku kifuatacho. Hapa, ushirikishwaji wa wadau katika

usimamizi na utawala wa Sheria unazingatiwa.

Kitengo cha usimamizi ambacho WRMA inategemewa kulenga ni eneo la chanzo cha mto, ambalo linatakiwa

kuliaainisha. Kila eneo la chanzo cha mto linapaswa kuwa na Kamati ya Ushauri (CAAC) ya watu 15, walioteuliwa

na WRMA, na kuwa na wawakilishi kutoka sekta mbalimbali za wadau binafsi na za umma. Chini ya Sheria ya

Maji, CAAC ina wajibu wa ‘kuwashauri maafisa wa mamlaka hii (WRMA) katika ofisi stahiki ya mkoa kuhusu:

a) hifadhi, matumizi na mgao wa rasilimali ya maji;

b) utoaji, urekebishaji, ufutaji au ubadilishaji wa kibali chochote [cha maji]; na

c) masuala mengine yoyote yanayoambatana na usimamizi mzuri wa rasilimali ya maji (RoK, 2000: 953).

Mamlaka halisi ya usimamizi wa Sheria ya Maji (ikiwa ni pamoja na uwezo wa kumtia mtu nguvuni, kushtaki

na kutoa vibali vya maji) yako mikononi mwa WRMA. Aidha imepewa wajibu wa kuendeleza mkakati wa

maji wa taifa ambao ulichapishwa mwaka 2003 (Rok, 2003). Mkakati huo unaelezea uhusishwaji wa

wadau katika usimamizi na utawala wa maji ya Kenya kama ifuatavyo: Sera ya Maji ya Taifa (NWP)

inatambua hali ambapo mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na jamii zitakuwa na majukumu makubwa

katika sekta ya maji ikiwa ni pamoja na usimamizi wa rasilimali za maji. Kwa hali hii itahitajika watendaji

wapya kupatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo …. (RoK 203:73).

49

Jedwali la 6: Hati za kutumia maji katika Bonde la Mto Pangani (Tanzania), Mei 2003

Mkoa Hati za Hati za Maombi Bila Hati Jumla

kudumu muda ya hati ya hati zisizotumika

kwa muda

Arusha 184 135 57 141 144 661

Manyara 3 3 2 10 0 18

Kilimanjaro 264 138 118 1224 203 1947

Tanga 116 24 25 488 118 771

Jumla 567 300 202 1863 465 3397

Dondoo

Hati ya kudumu: Hati ya iliyotolewa kuwa ya kudumu na inayotumika.

Hati ya muda: Hati iliyotolewa kwa muda, ili mwombaji amalizie ujenzi wa mifumo ya kupitisha maji kama

inavyotakiwa na PBWO. Kwa kawaida mtumiaji hupewa mwaka mmoja wa kufanya hivyo, baada ya muda

huo lazima aombe kuongeza muda kama hajamaliza.

Maombi ya hati: Ombi linalotolewa kwa PBWO, ambayo inashughulikia maombi hayo kwa kufuata taratibu

zilizopo kabla ya kufikisha katika kikao cha PBWB kwa ajili ya idhini na utoaji wa kibali.

Bila ya hati: hawa ni watumiaji wasio na hati ya kisheria (wanatumia bila hati). Nusu ya hawa wanakisiwa kila

mmoja anachukua lita 10 kwa sekunde; makadirio haya yanahitaji kuthibitishwa.

Hati zisizotumika kwa muda: Hizi ni hati zilizotolewa, lakini wamiliki wake kwa sasa hawatumii maji. Kama

hati haitumiki kwa miaka mitatu, hufutwa. Tathmini ya hati na matumizi ya maji inahitajika ili kubainisha idadi

ya hati zilizolala katika bonde hili, na kupitisha uamuzi kama zifutwe au la.

Rejea: Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani.

Mkakati unasisitiza uhifadhi wa mazingira katika maeneo yote ya vyanzo vya mito, na unatoa mwongozo

wa sera ufuatao:

‘Kuhakikisha maendeleo endelevu ya kimazingira, yanayolenga katika ushirikishaji na uimarishaji

wa thamani ya mazingira na utiliaji maanani upangaji wa mipango ya rasilimali za maji, usimamizi

na maendeleo na kuongeza ufahamu wa [sic] athari zake kwa afya ya binadamu, maendeleo na

maliasili nyingine. Mkazo kimsingi utazidishwa kwenye kufafanua, kuboresha na kuweka wazi

taasisi na michakato itakayohusika katika ushirikishwaji wa masuala ya mazingira katika usimamizi

wa rasilimali za maji kwa ujumla (RoK, 2003:23).

Kwa nyongeza, Mkakati huu unasisitiza kuhifadhi vyanzo vya mito, hususan katika kuhifadhi misitu ya

Kenya ambayo inapungua kwa kasi kubwa:

‘Maeneo ya vyanzo vya maji yanahitaji … kuainishwa na kuonyeshwa katika mchoro na programu

za uhifadhi na ulinzi zianzishwe na wizara zinazohusika na misitu. Kwa nyongeza, kanda za hifadhi

ya maji ya chini ya ardhi zitahitajika kuainishwa kuepuka umalizikaji wa rasilimali hii ili kukuza

usimamizi shirikishi wa vyanzo vya mito. Wadau wote watahimizwa kutumia rasilimali zao katika

kulinda vyanzo vya maji vya nchi yao (RoK, 2003:33).

Katika hali hii, Sera ya Maji ya Kenya inaeleza misingi ambayo usimamizi wa rasilimali za Bonde la Mto

Pangani zinazovuka mipaka ya nchi unaweza kufanyika, ikitiliwa maanani kuwa ukataji miti kwenye

mitelemko ya Mlima Kilimanjaro (nchini Tanzania) huathiri moja kwa moja kina na ubora wa maji ya Ziwa

Jipe (nchini Kenya).

50

Kisanduku 12: Utawala wa Maji Kenya

• Waziri wa Maji: Hudhibiti rasilimali zote za maji kulingana na Sheria ya Maji ya Mwaka 2002.

• Mkurugenzi wa Maji: humsaidia Waziri kutekeleza kazi zake.

• Mamlaka ya Usimamizi wa Rasilimali ya Maji (WRMA): inafanya kazi ya usimamizi wa rasilimali ya maji.

• Kamati ya Ushauri ya Eneo la chanzo cha mto (CAAC): huwashauri maafisa wa WRMA kwa masuala

ya usimamizi wa maji yanayohusiana na eneo la chanzo cha mto lililoko chini ya mamlaka yake.

• Hifadhi ya Maji ya Taifa na Shirika la Mabomba (NWC & PC): kwa niaba ya Waziri, hushughulika na

uendelezaji wa miradi ya taifa inayotoa huduma ya maji mengi ya matumizi kwa wenye leseni na

watoaji wengine wa huduma za maji

• Bodi ya Rufaa ya Maji (WAB): husikiliza na kuamua kesi yoyote ya mtu mwenye kibali au mali ambayo

inaathirika moja kwa moja na uamuzi wa kisheria wa Mamlaka.

• Vyama vya Watumiaji wa Rasilimali ya Maji: husaidia mamlaka katika ulinzi wa rasilimali za maji

katika ngazi ya chini kabisa.

Utawala wa misitu, sheria na sera

Usimamizi wa misitu ya Tanzania

umegawanywa kati ya mamlaka kuu mbili.

Mlinzi mkuu wa misitu ya taifa ni Idara ya Misitu

na Nyuki (FBD), ambayo iko chini ya Wizara ya

Maliasili na Utalii. Ofisi ya Rais pia ni mhusika

katika usimamizi wa misitu ya Tanzania kwa

kupitia kazi zinazofanywa na tawala za mikoa

na serikali za mitaa. Chombo cha tatu cha

usimamizi ni Mamlaka ya Hifadhi za Taifa

(TANAPA) ambazo husimamia misitu iliyopo

katika mipaka ya mbuga za hifadhi za Taifa

(Lambrechts et al., 2002).

Kama ulivyo utawala wa maji wa sasa, utawala

wa misitu pia una pande mbili. Katika ngazi ya

mkoa, Afisa Maliasili wa Mkoa (RNRO) hukaa

kwenye Sekretarieti ya Mkoa akiwakilisha

misitu. Wanaowajibika kwa RNRO ni Maafisa

Watendaji wa Wilaya, ambao chini yao kuna

Maafisa Maliasili wa Wilaya.

Serikali kuu

FBD

RNRO

FCFO

Serikali za Mitaa

Mkurugenzi

Mtendaji (Wilaya)

DNRO

DFO

Utawala wa mkoa hauna mamlaka ya kisheria

kwenye Misitu ya Eneo la Chanzo cha Mto. Mradi

wa Misitu ya maeneo ya vyanzo vya mito (CFP)

ulizinduliwa mwaka 1976 na Idara ya Misitu na

Nyuki. Katika mkoa wa Arusha, hekta 118,921

za misitu zimo kwenye mradi. Katika mkoa wa

Kilimanjaro ni hekta 138,785 wakati ambapo

Tanga ni hekta 107,499 (Kijazi 2002). Misitu

ya maeneo la vyanzo vya mito huchukuliwa

kuwa ‘maeneo muhimu yaliyohifadhiwa’ na

yanatawaliwa kutoka kwenye ofisi ya CFP katika

Misitu ya vyanzo

vya maji wilayani

Misitu ya

uzalishaji

Misitu

Misitu ya Hifadhi

ya asili

Mchoro wa 3: Utawala wa misitu nchini

Tanzania

51

makao makuu ya Idara ya Misitu na Nyuki, ambayo huwajibika kwa serikali kuu. Wanaowajibika kwenye ofisi

ya CFP ni Mameneja wa Misitu ya maeneo ya vyanzo vya mito wa mikoa- mmoja kwa kila mkoa. Mameneja

wa wilaya wa misitu ya maeneo ya vyanzo vya mito huwajibika kwa Meneja wa Mkoa. Mameneja hawa

hupata fedha moja kwa moja kutoka kwenye ofisi ya CFP, na lazima wawe na mpango wa usimamizi kwa

kila msitu ulio chini ya mamlaka yao. Ngazi hizi mbili tofauti za utawala zinaonyeshwa kwenye Mchoro wa 2.

Katika ngazi ya wilaya, Maafisa wa Misitu wa Wilaya (DFOs) hutekeleza shughuli za Idara ya Misitu na Nyuki,

ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa mapato. Mara nyingi, misitu ya asili na ya uzalishaji huwa chini ya utawala

wa wilaya, lakini misitu ya eneo la chanzo cha mto inaweza pia kuwa chini yao. Kwa vile Maafisa Misitu wa

Wilaya hukusanya mapato kwa niaba ya Idara ya Misitu na Nyuki, hivyo wale wote wenye elimu ya diploma

au zaidi hulipwa na Idara ya Misitu na Nyuki (Kijazi na Nashanda, Wahojiwa).

Sera ya Misitu ya mwaka 1998 inahimiza ushirikishwaji wa jamii katika usimamizi wa maliasili na hii ni

pamoja na zile jamii zinazopakana na hifadhi ya misitu ya mikoko. Mkakati wa Usimamizi unataka juhudi

zifanyike ili kujumuisha jamii za wenyeji katika shughuli mbalimbali kutoka kwenye upangaji hadi kwenye

utekelezaji. Shughuli hizo ni pamoja na udhibiti wa uvunaji, upandaji mikoko katika maeneo yaliyo wazi,

shughuli za ulinzi kama vile doria, na uhamasishaji (Kijazi, 2002).

Nchini Kenya, misitu kwa kiasi kikubwa haijasimamiwa kikamilifu, ukweli unaoonyeshwa na kiwango cha

ukataji miti cha kutisha kiasi cha kusababisha asilimia 2 hadi 3 tu ya nchi kubaki na misitu. Hatua za

haraka za urekebishaji zinazofanywa na serikali, ikiwa ni pamoja na marekebisho muhimu katika Idara

ya Misitu na uanzishaji wa sheria mpya ya Misitu, hazijazaa matunda. Katika sehemu ya Bonde la Mto

Pangani iliyoko Kenya kuna hifadhi za misitu chache zilizosalia, isipokuwa viunga vidogo vidogo vya

misitu katika Milima ya Taita, kiwakilishi pekee cha Milima ya Tao la Mashariki nchini Kenya. Matatizo

mengi yahusianayo na uharibifu wa misitu yanayotokea Kenya yanahusiana na ukataji miti kuvuka

mpaka wa Tanzania, hali inayotoa mfano mzuri wa haja ya kuwa na mkakati wa kutosha katika usimamizi

wa kimataifa wa bonde.

D.3 Utawala wa ngazi ya jamii

Mawazo kuhusu usimamizi wa pamoja wa rasilimali, hivi karibuni, yamekuwa ndio chaguo linalopendelewa

katika usimamizi wa maliasili. Mara nyingi (lakini sio mara zote) wadau wanaohusika katika mpango

wa usimamizi ni serikali na jamii zinazotumia rasilimali. Katika hatua hii ya majadiliano ya kina, dhana

ya usimamizi wa pamoja haieleweki vizuri, kwa upande mmoja, kwa sababu ya kuwepo kwa haja ya

kuendeleza mifumo ya Usimamizi wa Maliasili ambayo inalenga moja kwa moja mahali na jamii.

Mara nyingi, katika hatua hizi za mwingiliano katika usimamizi, menejimenti hutumia taasisi kama sehemu

ya utawala wake. Taasisi ni “…sheria za kuendesha mambo katika jamii au, kuwa rasmi zaidi … vikwazo

vilivyobuniwa na binadamu ili kutengeneza mifumo ya maingiliano ya binadamu“ (North, 1993:3). Kwa hali

hii, taasisi huweka vikomo ambavyo ndani yake maisha ya watu huendeshwa. Lazima tahadhari ichukuliwe

ili kuelewa kuwa taasisi sio matokeo tuli, bali ni hatua pana ambazo hubadilika ili kukabiliana na misukumo

kutoka nje, mabadiliko ya ndani, migogoro na shinikizo nyingine. Taasisi za jamii zinaweza kufanya kazi

muhimu katika kujitafutia njia ya kuendeleza uchumi wake na hasa, jinsi inavyopokea uchumi kutoka nje.

Taasisi sio mashirika, ambayo mafanikio na utendaji wake daima unategemea taasisi.

Katika maandishi mengi kuhusu usimamizi wa rasilimali za pamoja, ni taasisi za kijadi ndizo zinazopendekezwa

kuwa msingi wa maendeleo ya usimamizi wa pamoja (angalia mifano katika Berkes, 1989 na Mackay na

Acheson, 1983). Kila mara hawa wanachukuliwa kuwa ushahidi kwamba jamii zina uwezo wa kusimamia

rasilimali zao. Hata hivyo taasisi zina kazi maalum na ni za muda, na zinaendelezwa kutegemeana na

mahitaji maalum ya kijamii na kiuchumi katika wakati na mahali maalum (North, 1993; Ostrom, 1990 Crean

na Gehib 2001). Hivyo taasisi za kijadi zilizoundwa kusimamia misitu huenda zilifanya kazi katika mazingira

ambayo vibali vya utumiaji vilikuwepo, masoko yalikuwa haba, na watu walikuwa wachache. Kinyume cha

hali hiyo, taasisi hizi inawezekana hazikuwa na thamani kubwa kiusimamizi. Hata hivyo zinabaki na mvuto

kwani huenda zinaweza kuwa na mvuto kijamii na kiutamaduni, kuliko zilivyo taasisi ngeni, zilizotoka nje.

52

Kundi la pili la taasisi za muhimu za usimamizi ni miundo na mashirika ya serikali ambayo yamekuwepo

kwa muda mrefu wa kutosha kiasi kwamba jamii inayaona kuwa ya ‘kawaida’ katika mazingira ya maisha

yao ya kila siku. Kwa maana hii, miundo kama hii imefanywa kuwa rasmi kwa jamii ya wenyeji.

Kama ilivyojadiliwa kabla, Tanzania imekuwa na bidii ya kuanzisha taasisi za Usimamizi wa Maliasili za

Jamii (CBNRM) katika maeneo yake yote ya rasilimali. Katika Bonde la Mto Pangani, miongoni mwa

taasisi muhimu zaidi ni Vyama vya Watumiaji Maji na Kamati za Maliasili za Vijiji (VNRCs). Zote hizi mbili

zinazingatiwa katika sehemu hii.

Tagseth (2002) aliainisha aina mbili za uongozi wa mifereji katika ngazi ya kijiji. Wa kwanza kati ya

hizi umelenga katika vikundi vya watumiaji visivyo na majina na visivyo rasmi vilivyoelezwa hapo juu,

vikiongozwa na mwenyekiti ambaye hupanga watumiaji katika vikundi kazi ili kukarabati mifereji kwa malipo

ya kugawiwa maji. Wenyeviti wamekuwa wakimiliki mifereji yao kwa vizazi vingi. Mfumo huu wa kihistroria

wa uongozi wa mifereji na maji yake humaanisha kuwa uongozi unaona kuwa kutafuta kibali cha kutumia

maji ya mfereji, kwa mfano kutoka Ofisi ya Maji Bonde la Pangani, kuwa jambo geni kabisa.

Aina ya pili ya uongozi wa mifereji ulioainishwa na Tagseth (2002) ni utaratibu rasmi zaidi. Kiongozi wake

anachaguliwa au kuteuliwa. Kuna sheria nyingi zaidi zinazotawala, kwa mfano, michango kwa skimu

hiyo na ugawaji wa maji. Ugawaji wa maji unapangwa kwa kutumia ada ya uanachama, faini zitokanazo

na uvunjaji wa sheria na pengine rushwa.

Ni wazi kuwa aina ya kwanza kati ya taasisi hizi mbili si rasmi, ambayo inaweza isivutie mifumo ya

utawala wa serikali yenye bidii ya kuunda miundo ya kirasimu na ya kueleweka. Hata hivyo, pia ina

misingi ya itikadi za asili za jamii ambayo huenda inamaanisha kuwa (a) inaweza kuwa bora zaidi katika

kushughulikia matatizo na migogoro ya wenyeji; na (b) inalingana zaidi na mitazamo na mawazo ya

wenyeji. Kwa maana hii, taasisi ya kwanza, isiyo rasmi, inaweza zaidi kushughulikia viwango vya juu

vya tofauti za kijamii, rasilimali na kiutamaduni zilizopo katika Bonde la Mto Pangani, wakati ile ya pili

isingeweza kushughulikia mawazo kama haya, yasiyo na sababu.

Awali, mawazo yanayoshutumu uanzishaji na utekelezaji wa Vyama vya Watumiaji Maji yalijadiliwa.

Ilidaiwa kuwa licha ya msisitizo wa jamii uliomo katika dhana hii, Vyama vya Watumiaji Maji bado viliweka

vikwazo kwa jamii ambazo hazikuviheshimu sana (PAMOJA, 2002). Hata hivyo ni lazima isisitizwe kuwa

taasisi kama hizi, mbali na kuingizwa kwa nguvu katika jamii, bado ‘zinaweza kufanywa kuwa za jamii’;

kwa maana kwamba zinaweza kupindishwa kukidhi mahitaji ya jamii na ili zisihatarishe matakwa ya

Kisanduku cha 13: Uanzishwaji wa usimamizi wa kijamii katika

msitu wa Duru-Haitemba, Mkoani Manyara

Hapo juu, mgogoro ulioibuka kati ya wanajamii wanaoishi kandokando ya msitu wa Duru-Haitemba na serikali

ya Tanzania wakati msitu ulipogeuzwa kuwa hifadhi umeelezewa. Mara ilipodhihirika kuwa msitu huu haufaidiki

na usimamizi wa serikali, na kwa vile serikali za mitaa zilibakiwa na rasilimali chache za kuweza kuwahudumia

wafanyakazi wa msitu, iliamuliwa kuzipa jamii nafasi ya kuuendesha msitu wao wenyewe. Sharti pekee

lililowekwa ni ufanisi: kwamba Duru-Haitemba inabaki bila kukaliwa na watu, kwamba hali yake iliyoharibiwa

inarejeshwa ilivyokuwa na kwamba mazao yake yavunwe kwa uendelevu.

Hatua za awali zilizochukuliwa na jamii zilianza kwa kuugawa msitu katika kanda ambazo kila jamii inazozizunguka

zingewajibika nazo. Kisha mpango rahisi sana wa usimamizi ulitolewa kwa kila kanda. Mipango hii ilieleza (a) ni

nani alipaswa na hakupaswa kuutumia msitu, (b) matumizi ya msitu ambayo jamii zilijiruhusu kuyatumia, (c) ni

matumizi gani yangeweza kufanyika kwa mgao unaosimamiwa na kijiji na mfumo wa vibali tu; na (d) ni matumizi

gani ya msitu ambayo yalizuiwa kabisa. Wavamizi walifukuzwa mara moja, uchomaji mkaa, uwindaji na ukataji

miti vilipigwa marufuku, na wakataji magogo wasiokuwa wenyeji ‘walihimizwa’ kuondoka. Maeneo yaliyoharibiwa

yalifungwa yasitumiwe na jamii, wakati ambapo sheria nyingi mbalimbali zilisaidia kuhakikisha kuwa matumizi

yoyote yaliyofanyika yalikuwa endelevu. Misimu mipya ya “kufungwa” na “kufunguliwa” ilianzishwa ikiruhusu

aina fulani za matumizi zifanyike katika maeneo fulani na nyakati fulani za mwaka (kama vile ulishaji mifugo).

Mwisho vijana wa kiume kutoka katika jamii walipelekwa kufanyia doria msitu, na kuzawadiwa sehemu ya faini

walizofanikiwa kukusanya (Rejea: Willy, 1999)

53

jamii ya kujitafutia riziki. Hata hivyo hii haina maana kuwa taasisi ndiyo itakuwa inafanya usimamizi

uliotarajiwa. Ili hili litokee, malengo ya usimamizi kwa namna fulani pia lazima yazuie hofu za jamii, na

kwa kiasi fulani kuhakikisha kuwa inachangia katika kukidhi matarajio yao. Ili hili litokee, jamii lazima

ishiriki katika majukumu muhimu ya kupanga na kutekeleza mifumo ya usimamizi, hususan mifumo

inayohusiana na utoaji wa adhabu.

Mradi wa misitu ya maeneo ya vyanzo vya mito (CFP) katika Tanzania unasimamia misitu kwa pamoja

na jamii za wenyeji zinazopakana na misitu 23 ya aina hiyo kwa majaribio. Asilimia 36.5 ya misitu katika

mikoa mitatu ya Tanzania inayochangia Bonde la Mto Pangani iko chini ya Usimamizi wa Misitu wa

Pamoja (JFM: Jedwali la 6). Sehemu kuu ya jamii katika juhudi hizi ni Kamati za Maliasili za Vijiji (VNRC).

Kila kamati ina wajumbe kati ya 8 na 15 ambao wamechaguliwa kidemokrasia. Angalau wajumbe wawili

lazima wawe wanawake. Kadiri ya kamati 129 (asilimia 70) za Maliasili za Vijiji zinashiriki katika kupanga

na kufanya maamuzi, vile vile kuhamasisha wanavijiji katika Usimamizi wa Misitu wa Pamoja. Rasimu

ya mipango ya usimamizi kwa ajili ya Hifadhi ya Misitu ya Jamii (CFRs) tisa zilizopewa kipaumbele

imetolewa, ikiwemo Mlima Kilimanjaro, Chome na Kindoroko katika mkoa wa Kilimanjaro na hifadhi ya

Kwani/Tongwe na msitu wa kilima cha Mafi katika mkoa wa Tanga.

Idara ya Misitu na Nyuki pia imetekeleza Mradi wa Usimamizi wa Mikoko (MMP), ambao ulizinduliwa

mnamo mwaka 1988. Hii ilianza na utayarishaji wa mpango wa usimamizi kwa mifumo ikolojia ya mikoko

ya Tanzania bara. Mkakati wa usimamizi uliobuniwa ulihitaji juhudi zifanywe kuhusisha jamii za wenyeji

katika shughuli mbalimbali, kuanzia upangaji hadi utekelezaji. Shughuli hizo ni pamoja na kudhibiti uvunaji,

upandaji wa mikoko katika maeneo ilikopungua, shughuli za ulinzi kama vile doria, na uhamasishaji.

Mradi wa Usimamizi wa Mikoko umehusisha vijiji 100 kati ya 130 vilivyo karibu na misitu ya mikoko katika

usimamizi wake. Zaidi ya hayo, mradi umekuwa ukiboresha msitu wa mikoko kwa kukata mitambaazi

katika hekta 430, na kukuza shughuli mbadala za uzalishaji kwa jamii za wenyeji, kama vile shughuli za

kilimo cha mimea ya baharini na ufugaji nyuki (Kijazi, 2002).

Mradi wa Usimamizi wa Mikoko umerudisha upya uhai wa misitu ya mikoko katika hekta 1,300 kati ya hekta

2,000 zilizokusudiwa, ambapo hekta 100 zilifanyiwa kazi kwa njia ya kujitolea na wanavijiji na mashirika

yasiyo ya kiserikali yanayojishughulisha na mazingira. Ufanisi wa misitu iliyopandwa upya unatofautiana

kwa asilimia kutoka 80 hadi 40. Hali ni duni zaidi katika maeneo ambayo kilimo cha mpunga kinafanyika,

kama vile Delta ya Mto Rufiji, kutokana na baadhi ya wamiliki wa mashamba kutokubali kuruhusu mikoko

kukua upya.

Kamati za Maliasili za Vijiji zinashirikiana na menejimenti ya mradi kwa kuangalia taratibu za uvunaji.

Chini ya usimamizi huu, mapato ya Serikali Kuu yameongezeka kutoka TSh. milioni 12 mwaka 1999/2000

hadi milioni 17 mwaka 2001 kutokana na uuzaji wa miti ya ujenzi na ada za usimamizi kutoka kwenye

visima vya chumvi (Kijazi, 2002).

Mpaka sasa katika kubuni shughuli mbadala za uzalishaji, mradi wa usimamizi wa mikoko ulipeleka

mizinga 830 ya asili na 28 ya kisasa ya nyuki katika misitu ya mikoko mnamo mwaka 2001. Zaidi ya

hayo, kilimo cha mimea ya baharini kinafanyika katika mwambao wa pwani.

54

Jedwali la 7: Eneo la misitu chini ya Usimamizi wa Misitu wa Pamoja kwa mikoa

Mkoa Eneo (Hekta) Idadi ya vijiji vilivyohusishwa

Arusha* 7,0248 70

Kilimanjaro 122,996 63

Morogoro 58,579 33

Tanga 15,233 19

Jumla 267,056 185

(Rejea: Kijazi, 2002). * inajumuisha na Mkoa wa Manyara

Katika mchakato wa uhamasishaji, programu ya kutoa elimu ya ikolojia ya mikoko ilifanyika katika shule

za msingi 47 katika Kanda za Kaskazini na Kusini. Mikutano ya vijiji, programu za redio, na maonesho

ya majadiliano ya video yalitumika pia.

D.4 Usimamizi wa Bonde kimataifa

Nyenzo za kusimamia rasilimali za Bonde la Mto Pangani, kati ya mataifa wafadhili ya Kenya na Tanzania

hazitoshelezi. Jitihada za kurekebisha tatizo hili kwa kiasi kikubwa zinategemea juhudi za IUCN-EARO za

kuhifadhi Ziwa Jipe. Nchini Kenya Mamlaka ya Maendeleo ya Pwani (CDA) ina madaraka ya kuratibu na kupanga

maendeleo ya sehemu ya bonde iliyoko Kenya. Mnamo mwaka 1993, iliamuliwa kuwa CDA ijitahidi kuandaa

mpango kabambe wa usimamizi na maendeleo kwa ajili ya sehemu ya bonde iliyoko Kenya, pamoja na kutafuta

njia za kushughulikia matatizo mahsusi ya Ziwa Jipe. CDA iliona kuwa ni lazima ishirikiane na mamlaka za aina

yake za upande wa Tanzania (Howard, 1999).

Mnamo mwaka 1994, CDA na Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani (PBWO) walikutana Mombasa, Kenya ili

kujadili masuala ya pamoja na njia zitakazowawezesha kufanya kazi pamoja ili kuendeleza mfumo wa usimamizi

ulioratibiwa kwa ajili ya bonde, ardhioevu na maji ya Ziwa Jipe. Mwaka 1996, PBWO na CDA zilikamilisha tathmini

ya mahitaji ya eneo la chanzo cha maji na ardhioevu ya Ziwa Jipe. Katika mwaka 1999, CDA, PBWB na wadau

wengine walishiriki katika warsha ya kuanzisha mfumo wa kusimamia Ziwa Jipe (Howard, 1999).

PBWO hivi sasa imelifikisha shauri la magugu maji yaliyoko Ziwa Jipe katika Bunge la Jumuia ya Afrika

Mashariki kwa kufanyiwa kazi. Kutoka hapo, kasi imepungua, na haja ya kuendeleza mfumo wa kuweza

kuratibu usimamizi kati ya nchi mbili hizi unabaki kuwa muhimu kuliko wakati mwingine wowote. Hili ni

dhahiri zaidi ikitiliwa maanani maendeleo ya hivi karibuni ya Kenya ambayo yameshuhudia uanzishwaji

wa mamlaka za Usimamizi wa Rasilimali za Maji. Umuhimu wa uundwaji wake kwa Bonde la Mto Pangani

na jinsi watakavyoshirikiana na wenzao wa Tanzania bado haifahamiki.

D.5 Ukusanyaji wa data na ufuatiliaji

Wasiwasi unaoibuka mara kwa mara baina ya wataalam waliohojiwa kwa ajili ya Uchambuzi huu wa hali

halisi na katika maandishi kuhusu Bonde la Mto Pangani unahusiana na ukosefu wa data za kutosha

katika Bonde hili. Mara kwa mara, wasiwasi huo unalenga kwenye ukosefu wa data za kihaidrolojia,

na wasiwasi ni kwamba mfumo wa sheria inayohusu utoaji wa hati za maji lazima uweze kujua wingi

wa maji yaliyopo. Katika mito iliyopo Bonde la Mto Pangani, kuna vituo vingi vya kihaidrolojia. Kwa

sababu mbalimbali – kama vile udhaifu wa utunzaji na kumalizika kwa betri – vituo vingi kati ya hivi

havikuendeshwa kwa muda wa kutosha kitakwimu. Wakati mwingine, vituo hivi vimeacha kufanya kazi

baada ya miaka miwili tu, na hakuna kilichofanyika kuvirejesha katika hali ya utoaji huduma.

Inawezekana kuchukua vipimo kwa kutumia watu, lakini motisha za kufanyia hivyo kwa fundi, kama wanavyodai

watoa habari, lazima ziwianishwe na mafao yake ambayo hayatoshelezi. Mara nyingi wahojiwa wameonekana

kupendelea uendelezaji wa mfumo wa haidrolojia unaojiendesha wenyewe ambao vipimo vinavyofanywa na watu

vinaweza kulinganishwa navyo, na ambavyo vinaweza kuwa uti wa mgongo wa mfumo wa ufuatiliaji wa kutosha.

Kwa hakika, ufuatiliaji, sio ukusanyaji wa data pekee. Kuzitafsiri data hizo katika mfumo wa taratibu za

matumizi kutakuwa na manufaa endapo kutakuwa na kanuni fulani inayounga mkono ili kuhakikisha

kuwa data hizi zinatoa mchango muhimu katika kazi za usimamizi. Hivyo, kujua ni samaki kiasi gani

wapo katika Bwawa la Nyumba ya Mungu haina maana kama taarifa hiyo haiwezi kutafsiriwa katika

utendaji wa usimamizi. Katika hali inayofanana na hiyo, uendelezaji wa mfumo wa ukusanyaji data za

haidrolojia wa kujiendesha wenyewe hauna maana kama utumiaji haramu wa maji hauwezi kuzuiliwa.

55

Kisanduku cha 14: Mfano wa Chama cha Watumiaji Maji

Chama cha Watumiaji Maji cha Tegemeo, Kijiji cha Kawaya, Wilaya ya Hai

Chama cha Watumiaji Maji cha Tegemeo kilianzishwa mwaka 1999 na PBWO ili kutatua tatizo la

ugawaji wa maji katika vijiji vitano wilayani Hai. Watu 5,000 hutumia maji ambayo Tegemeo huchukua,

lakini ni watu 300 tu ambao wamesajiliwa nacho. WUA inasema watu wanahitaji kuelimishwa kuhusu

manufaa ya uanachama. Manufaa hayo ni (a) kwamba watajifunza kuhusu sera na sheria za maji,

(b) wanaweza kupata kibali cha kutumia maji kwa urahisi zaidi, (c) kwamba wanaweza kuvutia

wahisani na shughuli za NGO (d) wanaweza kurekebisha miundombinu yao ya maji kwa urahisi

zaidi wakiwa kama kikundi; na (e) wanaweza kutatua matatizo yao kama kikundi. Vyanzo vyao vikuu

vya maji ni chemchemi kadhaa. Maji huingizwa kwenye mifereji ya kijadi, ambayo mara nyingi huwa

imepewa majina ya watu ambao waliichimba hapo zamani. Baadhi huwa mirefu sana-ulio mrefu

zaidi una kilomita 14. Tegemeo kwa sasa ina hati tatu za maji zenye jumla ya lita 720 kwa sekunde,

na imeomba kuongezewa. Chama hukusanya ada kutoka kwa watumiaji wenye mashamba, na kila

mtumiaji analazimika kulipa bila kujali kama ni mwanachama au la.

Watumiaji walioko mwanzoni mwa mfereji hufaidika zaidi ya wale walioko mwishoni. Chama kina sheria

ndogondogo zinazowapangia kiasi cha maji ambacho watumiaji walioko kwenye chanzo cha mfereji

wanaruhusiwa kutumia, lakini watu hudanganya. Tatizo lingine wanalokabiliana nalo ni kuwa eneo hilo

ni tambarare sana. Kwa kutokuwepo na mteremko, maji daima hutuwama na hayatiririki. Matatizo ya

ziada yanayowakabili ni pamoja na:

• Migogoro kati ya watumiaji wa maji wa sehemu ya juu na ya chini.

• Ulimaji katika maeneo ya chanzo cha maji na ukataji miti.

• Wakulima wa mpunga mara nyingi hawarudishi maji yasiyotumika kwenye mfereji.

• Chumvichumvi.

• Wafugaji huleta mifugo yao kunywa maji miferejini na kuharibu kingo zake.

• Eneo la huduma la WUA ni kubwa mno na mara nyingi huwa vigumu kwa wanachama kufika

kwenye eneo la tatizo.

• Maji siyo safi. Wakati wa mvua kina cha maji ardhini hupanda na kufanya vyoo vifurike. Baadhi

ya watu hawayachemshi maji wanayochota na hupata maradhi

• Umwagiliaji kwa vipindi virefu hupunguza rutuba ya ardhi.

Chanzo: Jumuiya ya Watumiaji Maji Tegemeo na Serikali ya Kjiji cha Kawaya

Pia ni muhimu kusisitiza kuwa data za vipimo vya kiufundi vya mabadiliko ya rasilimali (kama vile

upunguaji wa mtiririko wa maji, au mabadiliko ya eneo la msitu) hutoa tu taarifa kuhusu matokeo ya

mienendo na michakato itokeayo kwingineko, mara nyingi katika uga wa kijamii na kiuchumi (ingawaje

siyo mara zote k.m. mabadiliko ya hali ya hewa). Kama sababu za mabadiliko ya kimazingira na maliasili

zina asili ya kijamii na kiuchumi, ni muhimu kuendeleza mifumo yenye nguvu ya ufuatiliaji wa tofauti za

uchumi wa jamii, kinachosababisha hali hiyo na kuendeleza migogoro. Mifumo hii lazima pia iwe na

uwezo wa kutambua mahitaji ya maji katika bonde.

56

D.6 Majumuisho ya hoja

Utawala wa maliasili za Bonde la Mto Pangani ni wa kisekta. Shughuli za idara za misitu sio lazima ziwe

zimeoanishwa kwa kiasi kikubwa na kukiuka mpango wa usimamizi wa Bonde la Mto Pangani, bali matokeo

ya sera za misitu, kama ilivyo kwa shughuli za taasisi zinazohusika na usimamizi wa maji zinavyoshughulikia

Sera ya Maji ya Taifa. Hali hii ya kisekta huenda chini hadi kwenye mikakati ya utawala ya ngazi za jamii.

Hivyo Kamati za Maliasili za Vijiji zinazotumika katika Usimamizi wa Pamoja wa Misitu sio sawa na Vyama

vya Watumiaji Maji. Jamii zilizo jirani na maeneo ya uvuvi na yaliyohifadhiwa, zinaweza pia zikalazimika

kuunda Vitengo vya Usimamizi wa Fukwe na kamati za hifadhi ya wanyamapori kama ilivyo kwenye sera

za Idara ya Wanyamapori na Idara ya Uvuvi. Wingi wa kupita kiasi wa taasisi za vijijini nchini Tanzania

unazifunika zile zilizoundwa hapo awali kama vile Serikali za Vijiji. Mara nyingi, kazi ambazo kila kikundi

kinafanya hazitofautiani na kazi zinazofanywa na vikundi vingine. Hatimaye, taasisi hizi zote hazina budi

kushughulika mgao wa haki wa rasilimali katika jamii, matumizi endelevu na uhifadhi wake.

Kutokana na majadiliano ya hapo juu, dondoo zifuatazo zinatiliwa mkazo:

• Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji ya mwaka 2009 inaipa mamlaka ya kiutetendaji Bodi ya Maji

ya Bonde la Pangani kuandaa mipango ya usimamizi wa bonde na ambayo itakuwa msingi wa ugawaji

wa maji. Sheria hii mpya imeweka mfumo wa ngazi za utawala zenye ufanisi na mfumo wa kitaasisi

ulio wazi ambao unaonyesha majukumu ya kila mmoja katika kutekeleza sera na sheria. Usimamizi

wa maji Kenya umegawa katika mabonde 6 (kuna mabonde 5 lakini bonde la Ziwa Victoria limegawa

katika maeneo mawiili, Kasikazini na Kusini) kama ifuatavyo: Ziwa Victoria kasikazini, Ziwa Victoria

Kusini. Bonde la Ufa, Athi, Tana, na Iwaso Ng’iro. Sehemu ya bonde la Pangani upande wa Kenya

huangukia katika bonde la Athi. Sheria ya maji 2002 ya Kenya imeweka mfumo mpya wa kitaasisi wa

kusimamia na kutunza rasilimali za maji katika ngazi ya taifa, mabonde na mabonde madogo.

• Idara ya Misitu na Nyuki inaonekana kutokuwa na mipango yoyote ya aina hii ya kuundwa upya,

na utawala wa misitu katika bonde unabaki kuwa wa pande mbili kati ya watawala wa ngazi ya

taifa na ile ya mkoa, na kati ya nchi mbili ambamo Bonde la Mto Pangani limo.

• Sera zote, ya maji na ya misitu katika bonde hili zinazidi kutilia mkazo matumizi ya taasisi za kijamii

katika utekelezaji wake. Wasiwasi umejitokeza kuhusu ni kiasi gani taasisi hizi zimeshinikizwa

kuingia katika jamii. Kama jamii hazikushirikishwa katika uundaji na utekelezaji wa taasisi hizi,

kunaweza kuwa na matokeo yasiyofaa katika usimamizi wake. Kulielewa tatizo hili kunaweza kutoa

mafunzo kwa Kenya ambayo inataka kujumuisha watumiaji katika usimamizi wa rasilimali za taifa.

• Usimamizi wa kimataifa wa bonde ni muhimu. Zipo mamlaka, hata hivyo, zenye madaraka

ya kulisimamia na kuliendeleza Bonde hili katika pande zote mbili za mpaka wa Tanzania na

Kenya, na majadiliano yanayolenga katika kutambua ufumbuzi wa matatizo ya usimamizi wa

bonde hili yameanza.

• Mfumo wa ukusanyaji na ufuatiliaji wa data katika bonde unaonekana kuwa dhaifu, bila ya kujali

sekta ya rasilimali. Sura hii imetahadharisha kuwa kutilia mkazo ukusanyaji wa data kama

jambo muhimu kwenye mfumo wa usimamizi hakutakuwa na maana iwapo data hizo haziwezi

kusaidia ufuatiliaji kamili wa usimamizi. Pia inasisitiza haja ya kuanzisha njia za ufuatiliaji wa

mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, na kubainisha mahitaji ya maji katika bonde, kama nyongeza

kwenye vipimo vya kiufundi vya mabadiliko ya rasilimali.

Sura inayofuata inatoa muhtasari wa ‘masuala’ yanayolikabili Bonde la Mto Pangani. Inaanzia

na muhtasari wa masula yaliyopatikana kutoka katika kumbukumbu za warsha ya hivi karibuni

ya Bonde la Mto Pangani, pamoja na yale yaliyojitokeza wakati wa mahojiano yaliyofanyika

kwa ajili ya Uchambuzi huu wa Hali halisi. Sura hii inayatathmini masuala haya kama msingi

wa uwekaji wa maeneo ya kipaumbele kwa ajili ya kuyafanyia kazi, na mapendekezo kuhusiana

na hali hii yanatolewa katika sehemu yake ya mwisho.

57

E

Matatizo na masuala ya Bonde la Mto Pangani

E.1 Utangulizi

Sura hii msingi wake ni vyanzo viwili vya taarifa. Cha kwanza ni kumbukumbu za warsha kuhusu Bonde

la Mto Pangani, iliyofanyika Mei, 2002 mjini Moshi. Cha pili ni mahojiano yaliyofanyika kwa ajili ya

Uchambuzi huu wa hali halisi. Sura hii inajaribu kuunganisha maoni ya wadau mbalimbali katika Bonde

la Mto Pangani kama msingi mkuu wa kuweza kutambua maeneo ya kipaumbele kwa ajili ya utendaji wa

siku zijazo. Masuala ya Bonde la Mto Pangani yamegawanywa kati ya masuala ya mazingira, masuala

ya uchumi wa jamii na siasa, masuala ya usimamizi na utawala, maeneo ya utafiti, na mwisho, mawazo

ya wahojiwa kuhusu nini kipewe kipaumbele katika usimamizi wa bonde. Kwa misngi ya masuala haya,

sehemu ya hitimisho inorodhesha maeneo kadhaa ya kipaumbele kwa ajili ya kuyafanyia kazi.

Takriban katika kila jambo, masuala yaliyoangaliwa hapa chini yanajitokeza katika mazingira ya ukuaji wa

haraka na wa kiwango kikubwa cha idadi ya watu na ongezeko la msongamano wa watu. Hali ya rasilimali

za bonde kuwa na kikomo inafanya ongezeko la watu na ukuaji wa polepole wa maendeleo katika bonde

kusababisha uwezekano wa kuleta matatizo na masuala yaliyoangaliwa hapa, au pengine kuyazidisha.

E.2 Matatizo na masuala ya Bonde la Mto Pangani

Masuala ya mazingira

Kati ya matatizo ya bonde hili, kubwa zaidi ni ukataji miti, tatizo ambalo huathiri moja kwa moja uwezo

wa kuhifadhi maji, huongeza kasi ya mtiririko wa maji na hivyo kusababisha mmomonyoko wa udongo

katika bonde. Upande wa chini wa mto, mchakato huo huweza kusababisha mafuriko kutokea na hivyo

wingi wa mchangatope kwenye mikondo ya maji katika bonde kuwa mkubwa.

Katika hatua nyingne, ukataji miti umesababishwa na mahitaji makubwa ya mazao ya misitu. Mingi ya misitu

iliyobaki katika bonde ina mbao zenye thamani kubwa, ambazo kunapokosekana mfumo imara wa ufuatiliaji

na utoaji adhabu, hukatwa kwa urahisi. Misitu pia hukatwa kwa ajili ya utengenezaji wa mkaa, pamoja na

kuni kukidhi mahitaji ya nyumbani. Zaidi ya hayo, misitu ya bonde mara nyingi imo kwenye maeneo muhimu

ya kilimo. Misitu ya Tao la Mashariki, kwa mfano, iko katika maeneo ya mwinuko ambayo mvua ni nzuri.

Kadiri idadi ya watu kwenye bonde inavyoongezeka na idadi ya wakazi katika kingo za misitu huongezeka na

kuzidisha hatari ya moto katika misitu. Moto pia hutumika kwa kusafisha ardhi kwa ajili ya kilimo.

Katika sehemu nyingi, kilimo kinachotumika kilianzishwa wakati ambapo rasilimali zilikuwa nyingi zaidi

kuliko zilivyo hivi sasa, na huenda kisiweze kuendana na hali ya uhaba wa rasilimali uliopo. Hivyo,

sehemu kubwa ya kilimo cha umwagiliaji wa kijadi kilichopo katika bonde hili hakina ufanisi kabisa na

kilianzishwa katika mazingira ambapo kulikuwepo na maji ya kutosha kwa kila mtu. Kwa vile uchukuaji wa

maji umeongezeka kutegemeana na msongamano wa watu, mifumo hii ya kilimo inaweza kuwa na athari

kubwa kwa mazingira ya bonde. Mashinikizo haya yamesababisha kujitokeza kwa kilimo kwenye kingo

za mto, ndani ya mabonde ya vijito na kwenye vyanzo vya chemchemi. Ongezeko la mchangatope lina

madhara kwenye mkondo wa mto (inaweza kusababisha kubadili mkondo) pamoja na viwanda vilivyoko

eneo la chini la mto, hususan mabwawa yatumikayo kuhifadhi maji kwa ajili ya nishati ya umeme.

Wingi wa shughuli za kilimo katika bonde hili umesababisha udongo kuendelea kuchoka kwa vile nafasi

ya mfumo wa mzunguko wa mazao imechukuliwa na kilimo cha mwaka mzima. Kwa vile ardhi sasa

ni nadra kuachwa bila mazao, inabidi imwagiliwe maji ili kuendelea kutoa mazao. Mifumo ya kijadi ya

uchukuaji maji ina ufanisi mdogo sana na kiasi cha maji kinachoifikia mimea kinaweza kufikia asilimia

85 pungufu ya kiasi kilichochukuliwa kutoka kwenye chanzo. Umwagiliaji wa kurudiarudia huongeza

uwezekano wa kuongeza chumvichumvi na/au magadi kwenye udongo. Zaidi ya hivyo, kiasi kikubwa

sana cha maji yanayochukuliwa kutoka kwenye vyanzo katika bonde hili, kimepunguza mtiririko wa maji,

inadhaniwa kuwa ni pamoja na kiasi cha maji yanayohitajika kwa ajili ya mazingira.

58

Katika maeneo ya nyanda za chini ya bonde hili inaonekana kuwa idadi ya mifugo imeongezeka kwa kiasi

kikubwa, wakati ambapo kiasi cha malisho kimepungua kutokana na maendeleo ya kilimo. Hii imesababisha

kujitokeza kwa tatizo la ufugaji wa kupita kiasi na matokeo yake ni uharibifu wa ardhi ya wafugaji.

Kadiri maendeleo yanavyoongezeka ndani ya bonde bila ya mifumo ya uondoaji taka inayoambatana

nayo, pia ndivyo uwezekano wa uchafuzi katika ngazi ya jamii na ya bonde kwa ujumla unavyoongezeka.

Matatizo ya ubora wa maji pia yanajitokeza kwa sura tofauti – hali ya viwango vya floraidi kuwa juu

inaweza kuwa na matokeo mabaya kwa watu waishio kando kando ya mito.

Kama ilivyo katika sehemu nyingine za Tanzania, uvuvi uliokithiri katika bonde ni tatizo, uvuvi wa pwani

na katika bwawa la Nyumba ya Mungu ukiwa ndiyo suala lenye uzito mkubwa. Katika Ziwa Jipe ukuaji wa

magugumaji umekuwa mkubwa kiasi cha kukwamisha uvuvi. Magugu hayo yametokana na ongezeko

la virutubisho vinavyoingia na maji yatokayo kwenye maeneo ya kilimo kwenye Mlima Kilimanjaro na

Milima ya Pare Kaskazini. Kwingineko katika bonde, magugumaji aina ya “water hyacinth” ni tatizo.

Matatizo yanayokabili ardhi ya kinamasi ya bonde hili yanatofautiana. Kwa upande mmoja, ukaushaji

wa maji kwenye vinamasi una matokeo mabaya kwa urekebishaji wa mtiririko wa mto, pamoja na

bayoanuwai zinazotegemea ardhioevu. Kwa upande mwingine, uelekezaji wa mikondo ya maji (pamoja

na ile inayopita kwenye ardhi ya kinamasi) unaweza kuongeza kiasi cha maji kitakachopatikana sehemu

za chini za mto, hususan kwa ajili ya uzalishaji wa umeme. Siyo tu maji yanayobaki katika vinamasi

hivyo hupunguza mtiririko wa mto, bali pia ongezeko la viwango vya mchavusho vinavyosababisha.

Uchimbaji madini usiodhibitiwa unaweza kuathiri sura ya nchi, na unaweza hata kusababisha uchafuzi

kama uchimbaji huo unahitaji mchakato unaotumia kemikali. Uchimbaji wa mchanga kwenye mikondo

ya mito unaweza kuharibu uimara wa kingo za mito.

Nyingi za tabia zilizotajwa hapo juu hutokana na uelewa mdogo kuhusu mazingira. Kwa upande

mmoja, haya yanahusiana na ukosefu wa data kuhusu mtiririko wa maji kwenye bonde na kiasi cha maji

yanayohitajika kutosheleza mahitaji ya mazingira. Kwa upande mwingine, wengi wa watu walioko katika

bonde hili hawana uelewa wa athari za mazingira yatakayotokana na shughuli zao za kiuchumi.

Ukubwa wa matumizi ya rasilimali, maendeleo, uendeshaji na mabadiliko ndani ya bonde vina matokeo

mabaya kwa bayoanuwai za bonde hili. Bonde lina baadhi ya rasilimali za bayoanuwai za pekee duniani

zenye viwango vya juu vya spishi zinazopatikana katika sehemu hiyo na spishi nyingi zinazozuiliwa.

Sehemu kubwa ya spishi hizi (lakini kwa vyovyote si zote) ziko kwenye misitu. Wakati rasilimali nyingi za

kimsingi za bonde zikiwa kwenye tishio kutokana na njia zilizoelezwa juu, rasilimali hizi za bayoanuwai

zinakabiliwa na hatari zilizo dhahiri na mbaya kabisa.

Masuala ya kiuchumi wa jamii na kisiasa

Kama ilivyo kwa watu wengine wa Tanzania, wakazi wengi wa Bonde la Mto Pangani sio matajiri. Ingawa

bonde hili lina miji mingi, lakini siyo mikubwa kiasi cha kuweza kupokea ziada ya nguvukazi iliyoko

vijijini. Wengi (kama si karibu wote) wa wakazi wa bonde hili hawana elimu ya kutosha na/au hawana

stadi za kutosha. Kwa hali yoyote ile, hata kama stadi zingekuwepo, kuna shaka kama soko la ajira

limeendelezwa vya kutosha kuweza kuwaajiri wote. Maendeleo katika bonde - kama ilivyo kwingineko

nchini Tanzania - yameshindwa kuzalisha nafasi mbadala za kuingiza mapato zinazooana na viwango

vya ufundi na stadi vya wakazi wa bonde.

Matokeo yake, njia pekee iliyopo ya kujipatia riziki kwa wengi walioko katika bonde ni ile ya msingi , yaani riziki

kutokana na utumiaji wa moja kwa moja wa rasilimali za bonde iwe ni misitu, uvuvi, rasilimali za wanyamapori

au, la muhimu zaidi, kilimo. Kwa walio wengi, mafanikio ya shughuli hizi ndogo ndogo, yanahusiana

moja kwa moja na upatikanaji wa ardhi na maji. Kadiri idadi ya watu inavyoongezeka, ndivyo pia migogoro

inavyoongezeka baina ya watumiaji wa aina na viwango mbalimbali. Kwa matokeo hayo, Uchambuzi huu wa

Hali halisi umewasilisha mifano ya migogoro ambayo hutokea kati ya watumiaji maji wa upande wa juu na wa

chini wa mto, pamoja na ule wa kati ya watumiaji wa viwango vikubwa na wa viwango vidogo.

59

Ni dhahiri kuwa migogoro ni ishara moja ya ushindani kwa ajili ya rasilimali. Kadiri hali hii inavyozidi

kuenea katika maeneo ya juu ya mto katika bonde, wakulima wanalazimika kuelekea upande wa chini

wa mto ili kujaribu kilimo katika hali isiyotosheleza ya kilimo. Kama ilivyojadiliwa mapema, jambo hili

huwanyang’anya ardhi wafugaji na hivyo kuwaingiza wakulima kwenye mgogoro na wafugaji.

Kama ilivyoelezwa hapo juu, matumizi makubwa ya ardhi katika bonde hili yanaweza kuwa na matokeo

mabaya kwa mazingira. Kwa kweli, matokeo haya yanaweza moja kwa moja kuathiri uwezo wa ardhi

kusaidia kwenye matumizi ya kiuchumi yatakayofanyika kwayo. Katika hali nyingine, msaada wa kisiasa

wa kubadili au kuzuia mienendo hii haupo, au huwa ni kinyume, kwa wanasiasa kuwahimiza watu

kutumia rasilimali kwa wingi ili wao waweze kujipatia kura.

Tatizo la mwisho la kisiasa lililotolewa na wahojiwa lilikuwa lile la Serikali Kuu ya Tanzania, katika juhudi

zake za kutekeleza sera, inaweza kufanya maamuzi ya usimamizi yahusianayo na rasilimali bila ya

kuwashirikisha watawala na wasimamizi wa rasilimali katika bonde. Kilichotia wasiwasi hasa ni miradi

mikubwa ya maendeleo (kama vile miradi ya umwagiliaji na vibali vya uchimbaji madini) vilivyoonekana

kusababisha migogoro ya ziada ya ndani au kuathiri vibaya hali ya rasilimali.

Masuala ya usimamizi na utawala

Sheria na sera za usimamizi wa maliasili za bonde hili, mara nyingi zinajitosheleza, lakini zinafanya

kazi pale tu zinapopata msaada wa usimamizi na ufuatiliaji wa kutosha wa utekelezaji wa kisheria.

Ufuatiliaji sio tu uwezo wa kuangalia matumizi haramu ya rasilimali, bali pia uwezo wa kupima uzalishaji

na mabadiliko ya rasilimali. Kwa mfano, kukosekana kwa mtandao wa kutosha wa ufuatiliaji wa mtiririko

wa maji maana yake ni kuwa mamlaka zinazohusika na maji hazijui kiasi cha maji kinachopita katika

bonde, kwa hiyo haziwezi kutoa vibali vya matumizi ya maji kwa msingi huo. Vivyo hivyo, hakuna njia

yoyote ya kufuatilia na kupima sababu za kijamii na kiuchumi ambazo zinasababisha sehemu kubwa ya

uharibifu wa mazingira na utumiaji wa kupita kiasi wa rasilimali.

Wafuatiliaji waliowekwa na taifa kuangalia mienendo ya matumizi ya rasilimali wanaweza wakashindwa

kufuatilia rasilimali hizo kama hawalipwi vizuri. Ujira duni unaweza pia kuwa sababu ya kuwafanya maafisa

wapokee rushwa hivyo kutoangalia matumizi haramu ya rasilimali. Viwango vya chini vya utaalamu, au

kukosekana kwa teknolojia ya kutosha kunaweza pia kuzidisha matatizo ya ufuatiliaji.

Matatizo ya fedha yanaweza kuathiri sehemu nyingine za mfumo wa usimamizi. Kwa kukosekana kwa fedha

za kutosha kwa mfano, inakuwa vigumu kuona jinsi mfumo wa kufaa wa ufuatiliaji unavyoweza kutekelezwa

ndani ya bonde bila ya kujali rasilimali zinazohusika. Ukosefu wa fedha unaweza pia kusababisha hata data

zinazoweza kukusanywa zisiweze kuchambuliwa au matokeo yasiweze kutafsiriwa kwa usahihi. Mwisho,

matatizo ya fedha yanaweza pia kukwamisha maendeleo ya uwezo na ufanisi wa usimamizi.

Zaidi ya hayo, usimamizi unaweza kudhoofishwa kutokana na namna unavyopangwa. Katika Bonde la Mto

Pangani, tatizo hili linaonekana kutokea katika ngazi mbili. Kwa upande mmoja, menejimenti siyo shirikishi,

kiasi kwamba shughuli za usimamizi katika sekta moja, kama vile maendeleo ya umwagiliaji- zinaweza kuwa

na athari kubwa katika sekta nyingine kama vile hifadhi ya maji. Kwa upande mwingine, mipaka ya mamlaka

mara nyingi hutokea kuwa na utata, kwa kuingiliana kwa mamlaka za kiutawala au kwa hakika mamlaka

za kisheria zisizotosheleza. Hivyo, mfumo wa Tanzania wa serikali kuu na serikali za mitaa husababisha

kuwapo kwa watendaji wakuu wa kiutawala wawili wanaohusika katika usimamizi wa kila rasilimali moja.

Nchini Kenya, madaraka ya kimaendeleo ya Mamlaka ya Maendeleo ya Pwani yanaonekana kuingiliana na

yale ya Mamlaka iliyoundwa hivi karibuni ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji.

Jamii za watumiaji rasilimali zinaweza kutatua mengi ya matatizo ya utata wa kiutawala na ufuatiliaji

usiotosheleza kwa kupitia viwango mbalimbali vya ushirikishwaji. Katika Bonde la Mto Pangani,

utekelezaji wa mchakato huu umekabiliwa na matatizo kadhaa. Kwanza, mifumo mingi ambayo

imekusudiwa jamii zihusishwe katika usimamizi imefikishwa kwao, bila kuishirikisha jamii katika

kubuni muundo wa utawala, katika utekelezaji wa mikakati ya usimamizi au kuadhibu wahalifu. Pili,

kwa kuwa jamii inaweza isiwe na mchango mkubwa katika muundo na utekelezaji wa usimamizi,

aina hizi za mifumo kwa kweli zinaweza kudhoofisha uwezo wa jamii kukidhi mahitaji ya maisha au

60

uwezo wao wa kushindana vizuri na watumiaji wengine wa rasilimali. Tatu, aina nyingi za ‘kamati’ za

rasilimali mbalimbali zimeundwa kote katika bonde, badala ya kuziongezea mamlaka serikali za vijiji

zilizokuwepo kabla. Hivyo, utawala wa ngazi ya vijiji umefanywa kuwa mgumu na kamati nyingi za

Usimamizi wa Maliasili zina majukumu yanayoingiliana au kukinzana. Mwisho, njia za mawasiliano kati

ya mamlaka kuu za usimamizi wa maliasili na jamii zinaweza kuwa hazijaendelezwa kiasi cha kutosha.

Matokeo yake, mahitaji na maoni ya jamii yanaweza yasizingatiwe au yasitambuliwe. Kwa namna hiyo

hiyo, malengo ya usimamizi wa rasilimali au hifadhi ya mamlaka za usimamizi wa maliasili zilizowekwa

chini ya makao makuu hazitaeleweka au hata kueleweka vibaya kwa ujumla na jamii.

Mchakato wa kiutawala na wenye urasimu unaweza kukwamisha au kudhoofisha shughuli za usimamizi

zilizokusudiwa kwa nia njema. Kwa mfano, jamii za watumiaji wa rasilimali zimepewa madaraka ya

kutunga sheria ndogo ndogo ambazo zinatambuliwa na serikali kuu, mamlaka za mkoa na wilaya. Hata

hivyo, hatua ya kuziidhinisha itachukua muda mrefu kiasi kwamba juhudi za jamii na msukumo wa

uongozi unadhoofishwa na mamlaka kuonekana kutoziunga mkono.

Bonde la Mto Pangani ni rasilimali inayovuka mipaka ya nchi. Utaratibu unaohitajika ili kuhakikisha kuwa

usimamizi unalingana kwa pande zote Kenya na Tanzania haupo.

Maeneo ya Utafiti

Matatizo yaliyotajwa hapo juu, mara nyingi yanazidishwa na ukosefu wa data sahihi na za kutosha juu

ya mienendo na michakato inayoipa Bonde la Mto Pangani sura yake, na kuathiri usimamizi wake.

Haieleweki wazi jinsi ongezeko la idadi ya watu katika bonde litakavyoathiri rasilimali zake hapo baadaye.

Wala haieleweki vizuri ni aina gani za mbinu za usimamizi wa maliasili zitakazotumiwa, zinazoweza

kufanya kazi katika misongamano kama hii ya watu.

Mengi ya mahitaji ya utafiti katika bonde hili yanahusu maji na haidrolojia. Hivyo, wakati idadi ya matoleo

ya maji yenye hati yanajulikana, uchukuaji usio halali uliojilimbikiza haujulikani. Kwa nyongeza kiasi cha

maji yanayohitajika ili kudumisha mifumo ya mazingira ya bonde pia hakijulikani. Athari za kuelekeza maji

ya Mto Pangani katika eneo la Vinamasi vya Kirua zinahitaji utafiti wa ziada (angalia IVO-NORPLAN,

1997). Mchango wa theluji ya kilele cha Mlima Kilimanjaro kwenye mtiririko wa maji ya Bonde hili

haujulikani, kama ilivyo kwa matokeo ya upunguaji wa theluji hiyo.

Mwisho, utafiti mdogo umefanywa ili kubainisha shughuli za usimamizi zinazofaa ambazo zitaweza

kuendana na tabia na matatizo mahsusi ya bonde hili. Haieleweki jinsi maji yanavyoweza kusambazwa

kwa kiasi cha kutosha na kwa usawa kati ya watumiaji wa maeneo ya juu ya mto na wale wa chini.

Hakuna ufahamu wa jinsi mfumo wa usimamizi unavyoweza kufuatiliwa na kutekelezwa kwa ufanisi

katika mazingira ya utoaji fedha usiotosheleza na usio wa kudumu, mchango mdogo wa kiufundi, viwango

vya chini vya stadi na ushirikishwaji duni wa jamii. Muhimu zaidi, uendelezwaji wa mifumo ya usimamizi

inayoweza kuendelea kuwepo chini ya vikwazo kama hivi hapo baadaye haujatokea. Mwisho, misingi ya

kitaasisi yenye ufanisi ya usimamizi shirikishi wa rasilimali za Bonde bado haijaanzishwa.

Usimamizi wa Bonde la Mto Pangani

Majadiliano yaliyofanyika wakati wa warsha ya mwezi Mei 2002 kuhusu Bonde la Mto Pangani, pamoja na

mahojiano yaliyofanyika ili kusaidia Uchambuzi huu wa Hali halisi, yalipendekeza mambo kadhaa ambayo

menejimenti ya bonde inaweza kuyafikiria. Kati ya hayo ilikuwa hoja kuwa wakazi wa bonde wanahitaji

kufahamu kuhusu Bonde la Mto Pangani na majukumu yake. Kumeibuka malalamiko kwamba bonde hili la

mto halitambuliwi vya kutosha kama kitengo cha utawala, na kuwa watawala na wenye urasimu waliokabidhiwa

madaraka wanashindania kudumisha msisitizo wa utawala wa nchi kimkoa na kitaifa. Wahojiwa walisema fedha

zinazotolewa zinatakiwa ziwe za kutosha na taratibu zinazohusika za utoaji wa fedha ziwe zenye ufanisi.

Menejimenti ya bonde itahitaji kuhakikisha kuwa idara za serikali zinashirikiana na taasisi nyingine za

usimamizi. Data zenye ubora wa hali ya juu zinahitajika kukusanywa ili kuipa taarifa menejimenti, na

menejimenti lazima iwe shirikishi. Mwisho, kati ya mapendekezo kadhaa ya mipango ya kitaifa iliyotolewa

ni kuwa usimamizi wa Bonde la Mto Pangani uunganishwe na mikakati ya kudhibiti ongezeko la watu.

61

Kwa kuwa wengi wa washiriki wa Warsha na watu waliohojiwa kwa ajili ya Uchambuzi huu wa Hali

halisi wametoka kwenye sekta ya maji, mapendekezo mengi ya usimamizi yaliyokusanywa yalihusiana

moja kwa moja na matumizi ya maji na sheria zake. Hivyo, ilipendekezwa kuwa menejimenti itakuwa

na haja ya kufuata mipango ya kazi iliyo wazi ambayo lazima iwe na hatua za kuchukuliwa kutokana na

upotevu wa maji na matumizi ya maji yasiyo ya ufanisi. Menejimenti itatakiwa kuwa na uwezo wa kutoa

mgao wa maji ya kutosha na kwa usawa, na matumizi haramu au yasiyofaa ya maji lazima yafuatiliwe

na kuchukuliwa hatua za kisheria. Matoleo ya maji lazima yawe na hati ili uchukuaji uweze kufuatiliwa.

Wahojiwa walidai kuwa, menejimenti ya bonde pia lazima iwe na uwezo wa kurekebisha uharibifu wa

vyanzo vya maji, na Ofisi ya Bonde lazima iwe na muundo ulioboreshwa wa ukusanyaji ada.

Baadhi ya washiriki wa warsha walikuwa na maoni kuwa upungufu wa maji haukutambuliwa vya kutosha

katika sera za Tanzania na kwamba hili lilihitaji kurekebishwa. Ili kuhakikisha kuwa maoni ya wadau

yanawakilishwa inavyofaa kwenye menejimenti ya maji ya bonde, wito ulitolewa kuwe na uwakilishi mzuri

zaidi wa wadau katika Bodi ya Maji ya Bonde. Mwisho, mkakati wa kutosha unahitajika ili kusimamia

utekelezaji wa Sera mpya ya Maji ya Tanzania.

Baada ya Baraza la Mawaziri kuidhinisha sera mpya ya maji Julai 21, 2002 Mkakati wa Taifa Kuendeleza

Sekta ya Maji (MTESM), uliandaliwa. Mkakati unaainisha namna sera ya maji itakavyotekelezwa na

unaeleza mabadiliko ya ki-sheria na kitaasisi yanayohitajika ili kufikia malengo yaliyoainishwa katika

mkakati huo. Kuhusu mifumo ya kitaasisi mkakati unasema: Maji ni rasilimali ya taifa na kimataifa ambayo

upatikanaji wake haufuati mipaka ya vijiji, wilaya, mikoa, au nchi na zinaweza kusimamiwa vizuri katika

mabonde na bodi za mabonde na kamati za mabonde madogo. Uwakilishi wa halmashauri za wilaya na

serikali za mitaa katika bodi na kamati hizo unahakikisha kuwa kuna sauti ya waliochaguliwa kidemokrasia

katika maamuzi yanayohusu uhifadhi, usimamizi, ugawaji, uendelezaji na utumiaji wa rasilimali za maji.

Pia mkakati unahimiza uainishaji wa maeneo ya sera za sekta muhimu yanayohusu rasilimali za maji

ili yawiane na Sera ya Maji na kuweka wazi wajibu wa kila mhusika katika mfumo unaoweka bayana

majukumu na wajibu na kuepuka kufanya shughuli kwa kurudia au nyingine kusahaulika. Sheria ya maji

ya 2009 ilitungwa ili kuweka mfumo wa kisheria wa usimamizi wa rasilimali za maji.

E. 3 Maeneo ya Kipaumbele ya Kufanyiwa kazi

Kwa msingi wa majadiliano hapo juu, maeneo matatu ya kipaumbele yameainishwa:

1. Uendelezaji wa mikakati ya usimamizi shirikishi ya Bonde la Mto Pangani pamoja na mabaraza

yanayoambatana nayo. Bila shaka Bonde la Mto Pangani linahitaji kwa haraka mikakati ya usimamizi

shirikishi ambayo inaweza kuendana na masuala mbalimbali na yenye utata ambayo yameelezwa katika

Uchambuzi huu wa Hali halisi. Kwa hivyo, inapendekezwa kuwa eneo la kwanza la kipaumbele ambalo

linahitaji kufikiriwa ni uendelezaji wa mikakati hiyo. Katika hatua hii, mkazo unaelekezwa kwenye sehemu

zifuatazo za mkakati huo:

• Ushirikishaji ni muhimu katika mtazamo wa mazingira wa wapangaji mipango na watawala ili

kuhakikisha kuwa menejimenti inafuata mikakati ya mipango ya jumla, na ya bonde lote yenye

uwezo wa kushughulikia rasilimali mbalimbali na matatizo yanayolikabili bonde.

• Ni muhimu Bonde la mto lionekane kama kitengo cha utawala ambamo ndani yake ushirikishwaji

wa usimamizi utatokea na migogoro ya rasilimali itatatuliwa. Pia ni muhimu kuwa matumizi ya

bonde la mto kama kitengo cha utawala yasiwe kinyume cha ukamilifu wa utawala wa kitaifa

na kimkoa na malengo ya sera.

• Chombo cha ziada cha utawala ambacho kinaweza kufikiriwa ni kufuata mfumo wa Usimamizi

wa Mahitaji ya Maji (WDM) (angalia A.2 hapo juu). Kwa kuzingatia ushahidi uliopo, kuwa

upatikanaji wa maji katika bonde umeelemewa, na kwamba mahitaji ya sasa yanazidi

upatikanaji, utekelezaji wa mifumo ambayo itasaidia kuhifadhi maji na kuhimiza matumizi bora

ingekuwa wa muhimu katika mazingira ya usimamizi shirikishi wa bonde.

62

• Upo umuhimu wa kubuni mikakati ambayo katika hatua zake za awali, inaweza kutekelezwa

kwa kuongezwa kadiri mipango na upatikanaji wa fedha unavyoruhusu. Kwa kukosekana

msaada wa kutosha wa mipango na kifedha, mikakati pekee ambayo inaweza kufanya kazi

kupitia matumizi ya haraka na yasiyo na uhakika inaweza kushindikana. Uwezekano mmoja

ni kulenga mipango kwenye mabonde madogo (sub-basin).

• Wingi wa taasisi za kijamii zinazoshughulika na sekta zote zitumiazo maliasili unatatanisha na

hauna ufanisi kiutawala. Hivyo, inafaa kutafuta njia ambazo taasisi za mahali husika zenye

mwelekeo mpana zinaweza kuendelezwa kuwa na uwezo na madaraka ya kutatua matatizo

yote ya usimamiazi wa maliasili katika eneo lake. Kila taasisi itahitaji msaada wa taifa, hususan

katika kuweka sheria ndogondogo za jamii, na kusaidia juhudi za usimamizi za jamii.

• Mipango ya matumizi ya ardhi lazima ifikiriwe kuwa ni sehemu muhimu ya mkakati wa mpango

shirikishi toka mwanzoni.

• Mikakati ya mipango ioane na uelewa wa uwezo na hali ya kifedha kwa baadaye. Haina maana

sana kuanzisha mikakati ya mipango inayotegemea msaada wa fedha, data na mipango

ambavyo ama vitatoweka mara fedha za wahisani zitakapokosekana, au ambayo haioani na

msingi wa muundo wa kitaasisi wa bonde.

2. Uanzishaji wa mikakati inayofaa kuwezesha mazungumzo miongoni na kati ya watumiaji rasilimali

na wasimamizi wa aina mbalimbali na kushirikishwa katika sekta mbalimbali kwa lengo la

kuboresha uelewa katika ngazi zote za usimamizi. Zinahitajika taratibu za kuhakikisha kuwa fursa

za mazungumzo kati na miongoni mwa wadau na wasimamizi zinakuzwa, ili kuhakikisha kuwa

upashanaji habari wa pande mbili unakuwepo, usambazaji habari unaboreshwa na kujua jinsi

wadau wote wanavyofanya kazi katika ustawi wa bonde zima. Ni muhimu uhamasishaji ufanyike

kuhusu nyanja zote za hali na usimamizi wa bonde na wadau wake katika ngazi zote za usimamizi

na uratibu wake. Inapendekezwa kuwa yaanzishwe mabaraza kwa madhumuni haya, ambayo

yatakuwa na mamlaka hadi kwenye usuluhishi wa migogoro.

Kwa nyongeza, mabaraza hayo yangeweza kuwa na uwezo wa kiutawala na utendaji, ambao

sekta zote za utawala katika bonde zinawakilishwa. Kipengele muhimu cha mchakato huu ni

kuhakikisha kuwa njia za kutosha za mawasiliano na mazungumzo zinaanzishwa kati ya ngazi za

juu za utawala na zile za chini kabisa, ngazi ya jamii.

Uwezekano wa kutumia redio na njia nyigine za habari lazima zifikiriwe kama njia zinazoweza

kutumiwa katika uanzishaji wa mazungumzo na zinazofaa kwa usambazaji na ubadilishanaji wa

taarifa. Tahadhari lazima ichukuliwe kuhakikisha kuwa wadau wote na wasimamizi wanafahamu

maendeleo ya sera mpya na mabadiliko katika utawala na kanuni za rasilimali. Majukumu ya

mabaraza yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya ushirikishi lazima yapanuliwe ili kuhusisha wajibu

wa majadiliano na kupashana habari. Juhudi hizi zingeweza kusaidiwa na juhudi za ughani

ambazo pia zingeweza kutumika kupata maoni na kero za jamii husika.

3. Kubainisha na kuendeleza mfumo wa kutosha wa ukusanyaji na ufuatiliaji wa data. Eneo hili la

utendaji halikomei katika uendelezaji wa mifumo ya ukusanyaji data kwa ajili ya data za kihaidrolojia.

Tathmini ya matumizi ya ardhi kwa kutumia Setilaiti na Mfumo wa Habari wa Kijiografia (GIS),

viwango vya matumizi ya ardhi na mabadiliko ya kijiografia ni mahitaji ya msingi katika kuendeleza

upangaji na ufuatiliaji wa matumizi ya ardhi. Kwa nyongeza, njia zitakazofaa kufuatilia na kupima

mabadiliko ya kijamii na kiuchumi na kuongezeka kwa migogoro zinahitajika kuainishwa na

kutekelezwa. Mifumo ya data na ufuatiliaji iliyopendekezwa lazima iendane na uwezo wa ndani

wa kifedha na uendeshaji. Mwisho, matumizi ya mashirika ya kijamii ya usimamizi wa maliasili,

kama njia ya ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali pia lazima yazingatiwe.

63

F Hitimisho

F. 1 Majumuisho ya Matokeo

Itakumbukwa kuwa lengo la awali la Uchambuzi wa Hali halisi lilikuwa kubainisha rasilimali zilizopo

katika Bonde la Mto Pangani na michakato na matukio yanayoziathiri.

Bonde la Mto Pangani lina aina nyingi sana za rasilimali. Baadhi ya rasilimali hizi, na kazi muhimu

zinazofanya katika bonde ni kama zifuatazo:

• Misitu, inafanya kazi muhimu katika haidrolojia ya Bonde, ya kurekebisha kasi ya maji, kupunguza

mmomonyoko, kuhifadhi na kutakasa maji. Aidha, inatoa mchango muhimu wa Bonde la Mto

Pangani kwa bayoanuwai ya dunia.

• Maji katika bonde la mto Pangani ni muhimu kwa uchumi wa kilimo, uzalishaji wa umeme, mahitaji ya

mijini, majumbani, viwandani na mifugo. Maji yanaendeleza maisha ya viumbe vyote katika bonde.

• Bonde hili lina maeneo manne yaliyohifadhiwa. Mlima Kilimanjaro, kipekee una mchango muhimu

sana katika uchumi wa utalii wa taifa, na pia unahifadhi spishi nyingi za mimea na wanyama.

Hifadhi ya wanyamapori ya Mkomazi na Mbuga ya Taifa ya Tsavo Magharibi ni mifano ya Kituo

cha kanda ya Masai-Somali cha Spishi zipatikanazo eneo hilo pekee (Regional Centre of

Endemism).

• Bayoanuwai ya bonde hili haina mfano wake ulimwenguni, na ni eneo lenye umuhimu mkubwa

kimataifa katika masuala ya hifadhi.

• Uvuvi katika bonde la mto Pangani unatoa mchango muhimu wa lishe na uchumi kwa jamii za

vijijini katika bonde.

• Udongo wenye rutuba wa volkano katika bonde la mto Pangani ndio msingi wa uchumi wake wa

kilimo, na kulifanya kuwa ‘eneo muhimu la uzalishaji mazao nchini Tanzania’.

• Uchimbaji madini unatoa mchango muhimu katika uchumi wa taifa na katika kutoa ajira. Manufaa

yake ni lazima yafikiriwe dhidi ya athari zake mbaya, ikiwa ni pamoja na uchafuzi wa mazingira

na udhoofishaji wa kingo za mito.

Hatari zinazokabiliwa na rasilimali za bonde karibu zote zinahusiana na utumiaji uliokithiri. Kiini cha

hatari hizi kinahusiana na ongezeko la idadi ya watu katika mazingira ya umaskini uliokithiri. Umaskini na

uharibifu wa mazingira mara nyingi vinaonekana kwenda pamoja (cf. WCED, 1987). Matatizo ya Usimamizi

wa Rasilimali za Jamii (CPRs) mara nyingi yanafikiriwa kuongezeka kunapokuwa na idadi kubwa ya

watu waliohusishwa, hususan pale mshikamano wa tamaduni zao unapokuwa dhaifu (cf. Ostrom, 1990).

Muundo na uwezo wa kufanya kazi za kujipatia riziki vijijini unanaweza kuhatarishwa wakati uwezo wa

watu wa vijijini kumiliki na kutunza vyanzo vya kutosha vya kujipatia riziki unapotishiwa.

Hapo juu, wadau wa bonde na shughuli zao zilielezwa kama ifuatavyo:

• Shughuli kuu katika bonde ni za viwanda (umeme, uchimbaji madini na kilimo), kilimo (kilimo

cha viwango vikubwa na viwango vidogo, vyote vikitegemea kwa sehemu kubwa umwagiliaji),

shughuli za wafugaji (hususan katika maeneo ya nyanda za chini), na shughuli zinazokua za

mijini. Mashirika yasiyo ya kiserikali na mawakala wa wahisani wa kimataifa wanafanya kazi kati

ya shughuli hizi mbalimbali na maliasili nyingi zilizopo katika bonde hili. Wajibu wa mashirika

haya kimsingi ni kuhifadhi na/au kuendeleza na kuongeza uwezo wa utafutaji riziki vijijini.

64

• Ni muhimu kutambua kuwa, idadi ya watu katika bonde hili ni kubwa. Sehemu kubwa ya idadi hii ya

watu riziki yao inatokana na kilimo, na kuna mengi yanayoonesha kuwa wako hatarini kiuchumi. Kwa

nyongeza, aina mbalimbali na utajiri wa rasilimali uliopo katika bonde hili huwa kivutio cha shughuli za

viwango vikubwa, na hivyo uwekezaji mkubwa umefanyika. Baina ya shughuli hizi kubwa za uwekezaji

na zile zilizo ndogo ndogo za kujitafutia riziki, uwezekano wa kuwepo migogoro ni dhahiri.

• Uchambuzi huu wa Hali halisi umeigawa migogoro ya Bonde la Mto Pangani katika makundi

makuu matatu. Kundi la kwanza linahusiana na migogoro ya viwango, ambayo ilitolewa hoja

kuwa watumiaji wa viwango vidogo mara nyingi inabidi washindane dhidi ya mahitaji makubwa

zaidi ya wenye nguvu katika kuwania rasilimali moja. Eneo la pili la migogoro lililobainishwa

lilihusiana na migogoro ya umiliki. ‘Umiliki’ hapa unahusiana na haki ya mtu ya kusimamia

rasilimali. Ilielezwa kuwa utaratibu wa kuzipangia jamii za watumiaji rasilimali aina tofauti za

vyama na/ au kamati zitakazosimamia rasilimali hizo unazidi kupata umarufu nchini Tanzania.

Matumaini ni kuwa uundaji wa taasisi kama hizi utatoa matokeo bora ya usimamizi. Hata hivyo,

kulikuwa na hoja kuwa namna taasisi hizi mara nyingi zilivyolazimishwa kuiingizwa katika jamii,

ambazo awali hazikuwa na mchango katika ubunifu, malengo au kanuni zake, zingeweza

kudhoofisha ubora wa matokeo ya kazi zao. Kundi la tatu la migogoro linahusiana na mahali.

Hapa, jinsi eneo la kikundi cha watumiaji rasilimali linavyoweza kuwaingiza katika mgogoro na

watumiaji wa mahali pengine, ilizingatiwa. Mfano mzuri wa mgogoro wa aina hii wa ‘mahali’

unaotokea kati ya watumiaji wa sehemu ya juu ya mto na wale wa chini ya mto ulitolewa.

Hapa, watumiaji wa upande wa chini ya mto huathiriwa na matumizi yaliyokithiri ya watumiaji

wa upande wa juu.

Sura D ilieleza kuwa utawala wa maliasili za Bonde la Mto Pangani ni wa kisekta. Shughuli za Idara ya

Misitu na Nyuki hazikulazimika kuoanishwa na baadhi ya seti ya mikakati mipana na mikuu ya usimamzi

wa Bonde la Mto Pangani, bali inafuata sera ya misitu na nyuki kama shughuli za Ofisi ya Maji Bonde la

Pangani zinavyofuata Sera ya Maji ya Taifa.

Utawala huu wa kisekta unapenya hadi kwenye mikakati ya utawala katika ngazi ya jamii. Hivyo, Kamati za

Maliasili za Vijiji vya Tanzania zilizotumika katika Usimamizi wa Pamoja wa Misitu si sawa na Vyama vya

Watumiaji Maji. Jamii zilizo karibu na maeneo ya uvuvi na yaliyohifadhiwa, pia zinaweza kulazimika kuunda

Vitengo vya Usimamizi wa Fukwe na kamati za ulinzi wa wanyamapori kwa mujibu wa sera za Idara ya

Wanyamapori na Idara ya Uvuvi. Wingi wa asasi za vijijini nchini Tanzania umezifunika zile zilizoundwa

hapo awali kama Serikali za Vijiji. Mara nyingi, kazi ambazo kikundi kimoja kinatakiwa kifanye hazitofautiani

na kazi ambazo vikundi vingine vinafanya. Hatimaye inabidi asasi zote hizi zijishughulishe na ugawaji wa

haki wa rasilimali katika jamii, matumizi yake endelevu na kuzilinda kutokana uvamizi wa watu kutoka nje.

Nchini Kenya, kinyume chake, kuna vikundi vichache sana vya namna hiyo, ingawa sera mpya za

maliasili zinazidi kutaka kuwashirikisha watumiaji katika miundo yake ya usimamizi.

Sura D ilitilia mkazo vipengele vifuatavyo:

• Sheria ya maji inaipa madaraka bodi ya maji kuandaa mipango ya usimamizi wa wa rasilimali za

maji ambayo itakuwa msingi wa kugawa maji Sheria mpya imeweka mfumo wa ngazi za utawala

zenye ufanisi na mfumo wa kitaasisi ulio wazi ambao unaonyesha majukumu ya kila mmoja katika

kutekeleza sera na sheria. Sera mpya ya maji ya Kenya inaelekeza uundwaji wa mamlaka ya

usimamizi wa rasilimali za maji unaohusisha wadau wote katika kusimamia rasilimali za mabonde.

• Idara ya Misitu na Nyuki inaonekana kutokuwa na mipango yoyote inayofanana na hii ya

kujipanga upya, na utawala wa misitu katika bonde unabaki kati ya tawala mbili za ngazi ya

taifa na mkoa. Nchini Kenya, uundaji upya wa Idara ya misitu bado haujatoa matunda. Hii

inaweza kuwa na matokeo ya ustawi mdogo kwa sehemu ya Bonde iliyoko Kenya, ambayo

inapata matatizo hasa yatokanayo na ukataji miti nchini Tanzania.

• Sera zote, ya maji na ya misitu katika bonde zinazidi kutilia mkazo matumizi ya mashirika

ya kijamii katika utekelezaji wao. Kwa upande wa Tanzania, kuna hofu juu ya kiasi ambacho

mashirika haya yamepandikizwa katika jamii. Ikiwa jamii hazikushirikishwa katika ubunifu na

65

utekelezaji wake, matokeo ya usimamizi yanaweza yasiwe ya kuridhisha. Mafunzo wanayoyapata

Watanzania kutokana na uzoefu huu yanaweza kuwa na manufaa katika ubunifu na utekelezaji

wa mifumo ya namna hii huko Kenya.

• Mtandao wa ukusanyaji na ufuatiliaji wa data katika bonde unaonekana kuwa duni, bila kujali

sekta ya rasilimali. Sura hii imetahadharisha kuwa kusisitiza ukusanyaji data kama jambo muhimu

kwa mfumo wa usimamizi hakuna maana ikiwa data hazitawezesha ufuatiliaji wa kiusimamizi.

Dhumuni la pili la Uchambuzi wa Hali halisi lilikuwa kubainisha kwa mapana maeneo ya utendaji ambamo

hatua zinaweza kuchukuliwa kwa manufaa.

Sura E ilitumia kumbukumbu za warsha kuhusu Bonde la Mto Pangani na mfululizo wa mahojiano na

wadau wa bonde kuorodhesha matatizo na masuala ya bonde. Kwa msingi huo maeneo matatu ya

kipaumbele cha utendaji yalibainishwa. Maeneo haya yalikuwa:

• Kuendeleza mikakati ya usimamizi shirikishi kwa ajili ya Bonde la Mto Pangani pamoja na

mabaraza yanayoambatana nayo. Bila shaka Bonde la Mto Pangani linahitaji mikakati ya

usimamizi shirikishi inayoweza kuendana na masuala mbalimbali na yenye utata yaliyoelezwa

katika uchambuzi huu wa hali halisi.

• Uanzishaji wa mikakati inayofaa kuwezesha mazungumzo miongoni na kati ya watumiaji

rasilimali na wasimamizi wa aina mbalimbali na kushirikishwa katika sekta mbalimbali kwa

lengo la kuboresha uelewa katika ngazi zote za usimamizi. Inahitajika mifumo ya kuhakikisha

kuwa nafasi za mazungumzo baina na kati ya wadau na wasimamizi zinaongezwa, ili

kuhakikisha kuwa kunakuwepo na upashanaji taarifa wa pande mbili, usambazaji wa taarifa

unaboreshwa na maarifa ya jinsi wadau wote wanavyotimiza wajibu wao katika ustawi wa

bonde hili unafikiwa. Ni muhimu uelewa ujengwe kwenye vipengele vyote vya hali na usimamizi

wa Bonde na wadau wake kwenye ngazi zote za usimamizi na uratibu wake. Vipengele vingine

vya ziada katika eneo hili la kipaumbele ni uanzishaji wa mabaraza yenye uwezo wa kufanya

kazi hii, pamoja na kufanya kazi kama nyenzo ya kuondoa migogoro, na kupunguza tofauti kati

ya ngazi mbalimbali za utawala.

• Kuainisha na kuendeleza mfumo wa kutosha wa ukusanyaji na ufuatiliaji wa data. Eneo hili

la utendaji halikomei katika uendelezaji wa mifumo ya ukusanyaji data kwa ajili ya data za

kihaidrolojia. Tathmini za Setilaiti na GIS za matumizi ya ardhi, viwango vya matumizi na

mabadiliko ya kijiografia ni mahitaji ya awali katika kupanga na ufuatiliaji wa matumizi ya ardhi.

Kuendeleza mbinu za kutathmini na kupima sababu za kijamii na za kiuchumi za uharibifu

wa mazingira na matumizi yaliyokithiri ya rasilimali pia zinahitajika kutambuliwa. Mifumo hiyo

lazima pia iwe na uwezo wa kutambua mahitaji ya maji katika bonde. Mifumo ya data na

ufuatiliaji inayopendekezwa lazima ioane na uwezo wa ndani kifedha na uendeshaji.

Lengo la tatu ya Uchambuzi wa Hali Halisi ilikuwa ni kutambua mashirika mengine, shughuli au asasi

ambazo IUCN inaweza kuingia nazo ubia wakati inapojaribu kuanzisha juhudi za WANI katika Bonde

la Mto Pangani.

Katika kifungu cha C6, ushiriki wa mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya kimataifa ulizingatiwa

na kufanyiwa tathmini kufuatana na mchango wao muhimu katika kuendeleza na kutekeleza mikakati

ya usimamizi shirikishi kwa ajili ya bonde hili. Hapa tunauendeleza zaidi ule uchambuzi na kupendekeza

njia ambazo asasi hizi zinaweza kuchangia katika usimamizi shirikishi wa Bonde la Mto Pangani.

• Utaalamu wa PAMOJA uko kwenye eneo la kukuza majadiliano, hususan kati ya Serikali

na shughuli za kijamii. Utaalamu huu unaweza kutoa mchango wa muhimu sana katika

kuunganisha mipango na utawala wa serikali na ngazi ya chini ya jamii katika usimamizi wa

rasilimali. Wakati huo huo, ni muhimu kuwa matatizo na mawazo ya jamii yazingatiwe vya

kutosha katika utoaji maamuzi na utendaji wa serikali. PAMOJA ina uwezo wa kuhakikisha

kuwa hili linafanyika.

66

• Shirika la Umwagiliaji maji Kiasili na Uendelezaji wa Mazingira (TIP) lina uzoefu sawa na

PAMOJA, na linaweza kuboresha matumizi yake. Hata hivyo, la kuvutia zaidi ni michango ya

kiufundi ambayo TIP inaweza kutoa katika kusanifu na kuendeleza miundombinu itakayoboresha

usafirishaji maji (mifereji ya umwagiliaji ) na utawala wake.

• Uzoefu wa Mpango wa Utendaji wa Misitu Tanzania (TFAP) wa kuendeleza ngazi ya jamii na

kuishirikisha katika ufumbuzi wa matatizo ya rasilimali , unaonekana kuwa wa manufaa katika

Bonde la Mto Pangani. Uendelezaji wa mifumo hii kwa jamii zinazoishi kando ya misitu ya bonde

hili ungekuwa ni jambo la kufurahiwa kwa mpango wowote wa usimamizi katika bonde. Kama

ingeunganishwa na shughuli za Kikundi cha Hifadhi ya Misitu Tanzania (TFCG), ueneaji wa

juhudi hizi ungeongezeka zaidi, mashirika yote haya mawili yangefaidika kwa pamoja kutokana

na kubadilishana uzoefu na maarifa na mkakati wenye ufanisi wa kushughulikia upotevu na

uharibifu wa misitu ungeanzishwa.

• Programu ya Hifadhi na Maendeleo ya Kanda ya Pwani ya Tanga (TCZCDP) ina uzoefu muhimu

kivitendo katika uundaji wa mkakati wa usimamizi shirikishi wa maliasili, ambao Bonde la Mto

Pangani ungeweza kujifunza kutoka kwake na kuweza kujijenga kiuwezo, ikieneza mafunzo

haya kuelekea juu na mbali zaidi kutoka eneo la mamlaka ya kisheria la TCZCDP. Eneo la

mamlaka ya kisheria la Ubia wa Usimamizi wa Pwani ya Tanzania (TCMP) ni kubwa zaidi, na

kwa sababu hiyo, shirika hili lingeweza kuwa na uzoefu wa hali ya juu wa usimamizi shirikishi

wa maeneo makubwa yenye aina nyingi sana za maliasili.

• Mradi wa Usimamizi wa Usimamizi wa Matumizi Bora ya Maji na Uboreshaji wa Kilimo cha

Umwagiliaji cha Wakulima Wadogo wadogo (RBMSIIP) ni mradi pekee uliojaribu kutumia mwelekeo

wa kimabonde katika kutatua matatizo ya Bonde la Mto Pangani. Kwa nyongeza, pia umejaribu

kushirikisha masuala ya hifadhi ya maji na juhudi za maendeleo ya maji. Maarifa yaliyomo kwenye

Mradi huu katika maeneo haya ni muhimu sana katika kuendeleza mikakati ya usimamizi kwa ajili

ya bonde. Zaidi ya hayo, uzoefu wa Mradi huu katika kuendeleza mtandao wa ukusanyaji data za

kihaidrolojia kwa ajili ya bonde pia ni wa manufaa makubwa kwa Bonde la Mto Pangani.

• Uzoefu wa Mradi wa Bayoanuwai za kimataifa za Afrika Mashariki (EACBP) wa UNDP-GEF

katika usimamizi wa rasilimali za kimataifa ni muhimu kwa Bonde la Mto Pangani. Kwa

nyongeza, uzoefu wa EACBP wa uundaji na utekelezaji wa usimamizi wa pamoja wa misitu

kijamii ungeweza kuwa wenye manufaa kwa usimamizi shirikishi wa bonde.

Ofisi ya Maji Bonde la Pangani inashirikiana na baadhi ya mashirika haya na kwa hiyo hii inaweza kuwa

orodha ya manufaa kwa kumbukumbu ya baadaye.

67

G

Rejea

Published sources:

Akitanda, P. 2002. South Kilimanjaro catchment forestry management strategies: perspectives and

constraints for integrated water resources management in Pangani Basin. In Ngana, J. O.

(ed.) Water resources management: the case of Pangani River Basin. Issues and approaches.

Dar es Salaam, Dar es Salaam University Press: 152 – 160.

Baker, N. E. and Baker, L. M. 2001. Tanzania. In Fishpool, L. D. C. and Evans, M. I. (eds.) Important

bird areas of Africa and its associated islands: priority areas for conservation. Newbury and

Cambridge, UK, Pisces Publications and BirdLife International (BirdLife Conservation Series

No. 11).

Baldwin, R. R. 1946. Native Authority afforestation on Mt. Kilimanjaro. Tanzania Notes and Records 21

(1946): 81 – 84.

Bergkamp, G., Orlando, B. and Burton, I. 2003. Change: Adaptation of water resources to climate change.

IUCN/WANI. Gland, Switzerland and Cambridge, UK, World Conservation Union.

Berkes, F. (ed.) 1989. Common property resources: ecology and community based sustainable

development. London, Belhaven Press.

Burgess, N., FitzGibbon, C. and Clarke, P. 1996. Coastal Forests. In: McClanahan, T. R. and Young, T.

P. (eds.) East African ecosystems and their conservation. New York, Oxford University Press:

329 – 359.

Bwathondi, P. O. J. and Mwamsojo, G. U. J. 1993. The status of the fishery resource in the wetlands of

Tanzania. G. L. and Crafter, S. A. (eds.) Wetlands of Tanzania: proceedings of a seminar on

the wetlands of Tanzania, Morogoro, 27 – 29 November, 1991. IUCN, Gland, Switzerland:

49 – 60.

Cheke, R. A., Mann, C. F. and Allen, R. 2001. Sunbirds: A guide to the sunbirds, flowerpeckers,

spiderhunters and sugarbirds of the world. Helm Identification Guides. London, Christopher

Helm.

Conway, G. R. and Barbier, E. B. 1990. After the green revolution: sustainable agriculture for development.

London, Earthscan Publications Ltd.

Cordeiro, N. J. 1998. A preliminary survey of the montane avifauna of Mt Nilo, East Usambaras, Tanzania.

Scopus 20 (May 1998): 1 – 18.

Crean, K. and Geheb, K. 2001. Sustaining appearances: sustainable development and the fisheries of

Lake Victoria. Natural Resources Forum 25 (2001): 215 – 224.

Dadzie, S., Haller, R. D. and Trewavas, E. 1988. A note on the fishes of Lake Jipe and Chale [sic.] on the

Kenya – Tanzania Border. Journal of the East African Natural History Society and National

Museum 78 (192): 46 –51.

Dobson, E. B. 1940. Land tenure of the Wasambaa. Tanzania Notes and Records 10 (1940): 1 – 27.

Ellis, F. 2000. Rural livelihoods and diversity in developing countries. Oxford, Oxford University Press.

Evans, T. D. 1997. Records of birds from the forests of the East Usambara lowlands, Tanzania, August

1994 – February 1995. Scopus 19 (1997): 92 – 108.

FAO (Food and Agricultural Organization), 2001. Food Balance Sheets. www.fao.org. Rome, Food and

Agricultural Organization.

68

Ferguson-Lees, J. and Christie, D. A. 2001. Raptors of the world. Boston, Houghton Mifflin Company.

Geological Survey, 1960. Summary of the geology of Tanganyika. Part II: Geological map. Dar es

Salaam, Geological Survey, Ministry of Mines and Commerce.

Gillingham, M. E. 1999. Gaining access to water: formal and working rules of indigenous irrigation

management on Mount Kilimanjaro, Tanzania. Natural Resources Journal 39 (3): 419 – 441.

GWP, 2002. Policy guidance and operational tools. ToolBox: Integrated Water Resources Management,

Version 1. Global Water Partnership.

Hastenrath, S. and Greischar, L. 1997. Glacier recession on Kilimanjaro, East Africa. Journal of Glaciology

43 (145): 455 – 459.

Homewood, K. and Brockington, D. 1999. Biodiversity, conservation and development in Mkomazi Game

Reserve, Tanzania. Global Ecology and Biodiversity 1999 (8): 301 – 313.

Howard, G. (ed.). 1999. Lake Jipe Cross-border Planning Workshop on a Proposal for the Development of

Mechanisms for Trans-boundary Management of a Shared Ecosystem. 13th - 15th October,

1999, Moshi (Tanzania and Taveta (Kenya). IUCN - The World Conservation Union, Eastern

Africa Regional Programme. Nairobi, December, 1999.

Howard, G. 2002. Integrated River Basin Management (IRBM). In: The Pangani River Basin: Options for

Integrated Management. Report on a Workshop held at the Kilimanjaro Crane Hotel, Moshi,

Tanzania, 8 – 10 May, 2002. Nairobi, IUCN – EARO: 92 - 95.

IUCN, 1999. Situation Analysis: an IUCN approach and method for strategic analysis and planning based

on the experience of IUCN Regional and HQ programmes. Prepared by the M&E Initiative.

Revised July 1999. Gland, The World Conservation Union (IUCN).

IVO – NORPLAN 1997. Pangani River Training Project Feasibility Study. PBWO – TANESCO, Pangani

Falls Redevelopment. IVO International and NORPLAN A/S.

Johnston, P. H. 1946. Some notes on land tenure on Kilimanjaro and the kihamba of the Wachagga.

Tanzania Notes and Records 21 (1946): 1 – 20.

Kaihura, F. B. S., Stocking, M. and Kahembe, E. 2001. Soil management and agrodiversity: a case

study from Arumeru, Arusha, Tanzania. Paper presented to the symposium on Managing

Biodiversity in Agricultural Systems, Montreal, Canada, November 8 - 12, 2001.

Keith Eltringham, S., Morley, R. J., Kingdon, J., Coe, M. J. and McWilliam, N. C. 1999. Checklist:

Mammals of Mkomazi. In Coe, M. J., McWilliam, N. C., Stone, G. N. and Packer, M. J. (eds.).

Mkomazi: the ecology, biodiversity and conservation of a Tanzanian Savanna. London, Royal

Geographical Society (with the Institute of British Geographers): 505 – 510.

Keith Eltringham, S., Cooksey, I. A., Dixon, W. J. B., Raine, N. E., Sheldrick, C. J., McWilliam, N. C. and

Packer, M. J. 1999. Large mammals of Mkomazi. In Coe, M. J., McWilliam, N. C., Stone, G. N.

and Packer, M. J. (eds.). Mkomazi: the ecology, biodiversity and conservation of a Tanzanian

Savanna. London, Royal Geographical Society (with the Institute of British Geographers):

485 – 504.

Kijazi, A. S. 2002. Catchment and mangrove management programmes: activities and environmental

concerns in the Pangani Basin. In: The Pangani River Basin: options for management.

Report of a Workshop held at the Kilimanjaro Crane Hotel, Moshi, Tanzania, 8-10 May 2002.

December 2002. Nairobi, IUCN – EARO: 36 - 40.

Lambrechts, C., Woodley, B., Hemp, A., Hemp, C. and Nnyiti, P. 2002. Aerial survey of the threats to Mt.

Kilimanjaro forests. Dar es Salaam, GEF Small Grants Programme, UNDP.

69

Lein, H. 2002. Migration, irrigation and land-use changes in the lowlands of Kilimanjaro, Tanzania. In

Ngana, J. O. (ed.) Water resources management: the case of Pangani River Basin. Issues

and approaches. Dar es Salaam, Dar es Salaam University Press: 28 – 38.

Lovgren, S. 2001. All That Glitters. With Rena Singer and David Enrich. U.S. News & World Report, 131

(6), 13/8/2001.

Luhikula, G. 2002. The Tanzania Coastal Management Partnership (TCMP): a partner in conservation. In:

The Pangani River Basin: Options for Integrated Management. Report on a Workshop held at the

Kilimanjaro Crane Hotel, Moshi, Tanzania, 8 – 10 May, 2002. Nairobi, IUCN – EARO: 86 – 90.

Majtenyi, C. and Muindi, M. 2001. Tanzania: big is beautiful at Merelani. New African, Oct. 2001, Issue 400.

Makule, D. E. n.d. The Pangani Basin Water Resources Management. http://srdis.ciesin.columbia. edu/

cases/tanzania-019.html

Mbonile, M. J. 2002. Rural population mobility in the Pangani Basin, Tanzania. In Ngana, J. O. (ed.)

Water resources management: the case of Pangani River Basin. Issues and approaches.

Dar es Salaam, Dar es Salaam University Press: 14 – 27.

McCay, B. J. and Acheson, J. M. (eds.) 1987. The question of the commons: the culture and ecology of

communal resources. Tucson, University of Arizona Press.

McClanahan, T. R. and Young, T. P. (eds.) 1996. East African ecosystems and their conservation. New

York, Oxford University Press.

Mgongo, E. N. E. 2002. Tanga Coastal Zone Conservation and Development Programme: activities

and concerns in the Lower Pangani River Basin. In: The Pangani River Basin: Options for

Integrated Management. Report on a Workshop held at the Kilimanjaro Crane Hotel, Moshi,

Tanzania, 8 – 10 May, 2002. Nairobi, IUCN – EARO: 81 – 85.

Misana, S. and Makoi, J. 2001. The impact of irrigation on soil fertility and salinity/sodicity in the Pangani

River Basin. In Ngana, J. O. (ed.). Water resources management in the Pangani River Basin:

challenges and opportunities. Dar es Salaam, Dar es Salaam University Press: 83 – 103.

Mjata, P. J. 2002. The Traditional Irrigation and Environmental Development Organisation (TIP). In: The

Pangani River Basin: Options for Integrated Management. Report on a Workshop held at the

Kilimanjaro Crane Hotel, Moshi, Tanzania, 8 – 10 May, 2002. Nairobi, IUCN – EARO: 78 – 80.

Mkhandi, S. and J. O. Ngana 2001. Trend analysis and spatial variability of annual rainfall. In Ngana,

J. O. (ed.). Water resources management in the Pangani River Basin: challenges and

opportunities. Dar es Salaam University Press, Dar es Salaam. 150pp.: 11 - 20

Mkuula, S. 1993. Pollution of wetlands in Tanzania. In: Kamukala, G. L. and Crafter, S. A. (eds.) Wetlands

of Tanzania: proceedings of a seminar on the wetlands of Tanzania, Morogoro, 27 – 29

November, 1991. IUCN, Gland, Switzerland: 85 – 93.

Mpemba, E. B. 1993. Wildlife resources and tourism in wetlands of Tanzania. In: Kamukala, G. L. and

Crafter, S. A. (eds.) Wetlands of Tanzania: proceedings of a seminar on the wetlands of

Tanzania, Morogoro, 27 – 29 November, 1991. IUCN, Gland, Switzerland: 61 – 66.

Mtalo, F. W. and Ndomba, P. M. Estimation of soil erosion in the Pangani Basin upstream of Nyumba ya

Mungu Reservoir. In Ngana, J. O. (ed.) Water resources management: the case of Pangani

River Basin. Issues and approaches. Dar es Salaam, Dar es Salaam University Press: 196

– 210.

Mujwahuzi, M. R. 2001. Water use conflicts in the Pangani Basin. In Ngana, J. O. (ed.). Water resources

management in the Pangani River Basin: challenges and opportunities. Dar es Salaam, Dar

es Salaam University Press: 128 – 137.

70

Musyoki, M. M. 2003. The situation analysis of the Kenyan part of the Pangani River Basin Catchment: the Lake

Jipe Watershed and system. Mombasa, Kenya: The Coast Development Authority, April 2003.

Musyoki, M. M. and Mwandotto, B. A. J. 1999. Presentation of results/reports on the assessment of

management needs for the watershed wetlands and waters of Lake Jipe. Paper presented at

the Lake Jipe Cross-border Workshop, 13th - 15th October, 1999.

Mwamfupe, D. 2001. Shortage of water for irrigation and farmers’ response: a case study of Makuyuni

and Kahe wards of Kilimanjaro Region, Tanzania. In Ngana, J. O. (ed.). Water resources

management in the Pangani River Basin: challenges and opportunities. Dar es Salaam, Dar

es Salaam University Press: 73 - 82.

Mwamfupe, D. G., 2002. The role of non-farm activities in household economies: a case study of Pangani

Basin, Tanzania. In Ngana, J. O. (ed.) Water resources management: the case of Pangani River

Basin. Issues and approaches. Dar es Salaam, Dar es Salaam University Press: 39 – 47.

Newmark, W. D. 1998. Forest area, fragmentation, and loss in the Eastern Arc Mountains: implications for the

conservation of biological diversity. Journal of East African Natural History 87 (1998): 1 – 8.

Ngana, J. O. 2001. Integrated water resources management: the case of the Pangani River Basin. In

Ngana, J. O. (ed.). Water resources management in the Pangani River Basin: challenges

and opportunities. Dar es Salaam, Dar es Salaam University Press: 1 - 8.

Ngula, D. E. P. 2002. Pangani River Basin: power generation and the environment. In: The Pangani

River Basin: options for management. Report of a Workshop held at the Kilimanjaro Crane

Hotel, Moshi, Tanzania, 8-10 May 2002. December 2002. Nairobi, IUCN – EARO: 67 – 71.

North, D. 1990. Institutions, institutional change and economic performance. Cambridge, Cambridge

University Press.

Nshubemuki, L. 1993. Forestry resources in Tanzania’s wetlands: concepts and potentials. In: Kamukala,

G. L. and Crafter, S. A. (eds.) Wetlands of Tanzania: proceedings of a seminar on the wetlands

of Tanzania, Morogoro, 27 – 29 November, 1991. IUCN, Gland, Switzerland:

Ole Sikar, T. Conflicts over natural resources in Maasai district of Simanjiro, Tanzania. Forests, trees and

people - Newsletter No. 30, March 1996.

Ostrom, E. 1990. Governing the commons: the evolution of institutions for collective action. Cambridge

University Press, Cambridge.

PAMOJA, 2002. Dialogue on Water: A concept paper on water resource use and management of conflicts

in the Pangani River Basin: the possible role of PAMOJA. Moshi, PAMOJA.

Richmond, M. D. (ed.) 1997. A guide to the seashores of Eastern Africa and the Western Indian Ocean

Islands. SIDA/Department for Research Cooperation, SAREC.

Rodgers, A. Mugabe, J. and Muthenge, C. 2001. Beyond Boundaries: Regional Overview of Transboundary

Natural Resource Management in Eastern Africa. In Biodiversity Support Program, Beyond

Boundaries: Transboundary Natural Resource Management in Eastern Africa. Washington,

D.C., U.S.A.: Biodiversity Support Program.

Rodgers, W. A. The Miombo Woodlands. In McClanahan, T. R. and Young, T. P. (eds.) East African

ecosystems and their conservation. New York, Oxford University Press: 299 - 325.

RoK (Republic of Kenya) 2002. Kenya Gazette Supplement. Acts, 2002 (no. 9); The Water Act, 2002.

Nairobi, October 24th, 2002. Nairobi, The Government Printer.

RoK (Republic of Kenya) 2003. The First National Water Resources Management Strategy. Nairobi,

Ministry of Water Resources Management and Development, April 2003.

71

Røhr, P. C. and Killingtveit, Å. 2002. Study of two catchments on the hillside of Mt. Kilimanjaro. In Ngana,

J. O. (ed.) Water resources management: the case of Pangani River Basin. Issues and

approaches. Dar es Salaam, Dar es Salaam University Press: 211 – 231.

Røhr, P. C. , Ngana, J. and Killingtveit, Å. 2002. Investigations of Chemka Spring, Kilimanjaro Region,

Tanzania. In Ngana, J. O. (ed.) Water resources management: the case of Pangani River

Basin. Issues and approaches. Dar es Salaam, Dar es Salaam University Press: 265 - 272.

Røhr, P. C., Killingtveit, Å., Nderingo, G. M. and Kigadye, P. E. n.d. Water and environmental conflicts in

the Pangani River Basin – hydropower or irrigation? Undated manuscript.

Røhr, P. C., Killingtveit, Å Rumambo, O. H. 2002. Brief report on the River Basin Management Project in

Tanzania. In: The Pangani River Basin: options for management. Report of a Workshop held

at the Kilimanjaro Crane Hotel, Moshi, Tanzania, 8-10 May 2002. December 2002. Nairobi,

IUCN – EARO: 44 – 48.

Sahib, I. 2002. The Tanzania Planting Company. In: The Pangani River Basin: options for management.

Report of a Workshop held at the Kilimanjaro Crane Hotel, Moshi, Tanzania, 8-10 May 2002.

December 2002. Nairobi, IUCN – EARO: 72 – 73.

Sarmett, J. D. and Kamugisha, S. M. 2002 Control of water utilisation in the Pangani Basin: the role

of PBWO and PBWB. In: The Pangani River Basin: options for management. Report of a

Workshop held at the Kilimanjaro Crane Hotel, Moshi, Tanzania, 8-10 May 2002. December

2002. Nairobi, IUCN – EARO: 19 – 24.

Schechambo, F. 2002. Forest valuation and economic policies: learning from Mount Meru Forest Reserve.

In Ngana, J. O. (ed.) Water resources management: the case of Pangani River Basin. Issues

and approaches. Dar es Salaam, Dar es Salaam University Press: 161 – 169.

Sishira, E. K. 2002. Land use change and sustainability of water resource utilisation in The Pangani

River Basin downstream of the Nyumba ya Mungu. In Ngana, J. O. (ed.) Water resources

management: the case of Pangani River Basin. Issues and approaches. Dar es Salaam,

Dar es Salaam University Press: 83 – 89.

Sjöholm, H. and Luono, S. 2002. The green forest pastures of Suledo - Maasai communities organise

to save their forests and secure their livelihoods. Forests, trees and people - Newsletter

No. 46, September, 2002.

Stoorvogel, J. J. and Smaling, E. M. A. 1990. Assessment of soil nutrient depletion in subsaharan Africa:

1983 - 2000. Vol. 1, Main Report. Wageningen, The Netherlands, Winand Staring Centre for

Integrated Land, Soil and Water Research.

Tagseth, M. 2002. Local practises and changes in farmer-managed irrigation in the Himo Catchment,

Kilimanjaro. In Ngana, J. O. (ed.) Water resources management: the case of Pangani River

Basin. Issues and approaches. Dar es Salaam, Dar es Salaam University Press: 48 - 63.

TANESCO, 1994. Environmental Impact Assessment of the redevelopment of the hydroelectric power

station at Pangani Falls: Baseline studies: mitigation of adverse impacts and monitoring the

attainment of intended mitigation. IVO – NORPLAN Joint Venture.

URT (United Republic of Tanzania), 2002. National Water Policy. Dar es Salaam, Ministry of Water and

Livestock Development.

Vanden Bossche, J.-P. and Bernacsek, G. M. 1990. Sourcebook for the inland fishery resources of

Africa. Vol. 1. Cifa Technical Paper 18/1. Rome, Food and Agricultural Organization.

Warren, A. 1995. Changing understandings of the nature of environmental paradigms. Transactions of

the Institute of British Geographers NS 20 (1995): 193 - 203.

72

W.C.E.D. 1987. Our common future. Oxford, O.U.P for the World Commission on Environment and

Development.

W.C.M.C. (World Conservation Monitoring Centre). 1985. Arusha National Park Factsheet. www.unep.

wcmc. org

W.C.M.C. (World Conservation Monitoring Centre). 1987. Kilimanjaro National Park Factsheet. www.

unep. wcmc.org

Wegelin-Schuringa, M. 1998. Water Demand Management and the Urban Poor. The Netherlands, IRC

International Water and Sanitation Centre.

West, K. 2002. The Water and Nature Initiative Challenge. In: The Pangani River Basin: Options for

Integrated Management. Report on a Workshop held at the Kilimanjaro Crane Hotel, Moshi,

Tanzania, 8 – 10 May, 2002. Nairobi, IUCN – EARO: 95 – 96.

WHO (World Health Organization). 2001. National health statistics. www.who.org. Geneva, World Health

Organization.

Wily, L. 1999. Moving forward in African community forestry: trading power, not use rights. Society and

Natural Resources 12 (1999): 49 – 61.

Wilson, D. C., Medard, M. Harris, C. K. and Wiley, D. S. 1996. Potentials for comanagement of the Nile perch

fishery – Lake Victoria, Tanzania. Paper presented at the ‘Voices from the Commons’ conference,

International Association for the study of common property, Berkeley, CA, June 5-8, 1996.

UNICEF (United Nations International Children’s Emergency Fund). 2001. The State of the World’s

Children 2000. www.unicef.org. New York, UNICEF.

Yanda, P. Z. and Shishira, E. K. 2001. Forestry conservation and resource utilisation on the southern

slopes of Mount Kilimanjaro: trends, conflicts and resolutions. In Ngana, J. O. (ed.). Water

resources management in the Pangani River Basin: challenges and opportunities. Dar es

Salaam, Dar es Salaam University Press: 104 - 117.

Zimmerman, D., Turner, D. Pratt, D Willis, I. 1996. Birds of Kenya and Northern Tanzania. London,

Christopher Helm.

73

Wahojiwa

Burra, R., Mshauri, PAMOJA, Arusha tarehe 13, Novemba, 2002

Bwoyo, D., Meneja Misitu wa Eneo la Chanzo cha Mto, Arusha, tarehe 22, Novemba, 2002

Fundi, H., Mtaalam wa Haidrolojia wa Mkoa, Mkoa wa Tanga, Tanga, tarehe 18, Novemba 2002.

Kijazi, A., na Nashanda, E. Idara ya Misitu na Nyuki, Dar es Salaam, tarehe 15, Novemba, 2002

Lugaiyamu, J., Meneja, Mfumo wa Mitambo ya Umeme wa maji Pangani TANESCO, Hale, tarehe 18, Novemba,

2002

Mihayo, J. M., Mkurugenzi, Rasilimali za Maji, Dar es Salaam, tarehe 15, Novemba, 2002

Mjata, P.J., Afisa Mipango wa Matumizi ya Ardhi, TIP, Moshi, tarehe 21, Novemba, 2002

Msuha, M. Afisa ndege, Chama cha Hifadhi ya Wanyama pori cha Tanzania, Dar es Salaam, tarehe 14,

Novemba, 2002

Nasari, J., Mhaidrolojia wa Mkoa, Mkoa wa Arusha, Arusha, tarehe 13, Novemba, 2002

Ngana, J., Profesa Mwandamizi wa Utafiti, Taasisi ya Tathmini ya Rasilimali, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,

tarehe 14, Novemba, 2002

Ngula, D., Meneja- Utafiti na Maendeleo, TANESCO, tarehe 14 Novemba, 2002

Rumambo, O., Mshauri wa Usimamizi wa Bonde, Mradi wa Usimamizi wa Mabonde ya Mito, Wizara ya Maji na

Maendeleo ya Mifugo, Dar es Salaam, tarehe 15, Novemba, 2002

Salehe, J., Meneja Mradi wa Taifa, UNDP/GEF- Mradi wa Bayoanuwai za kimataifa za Afrika ya Mashariki,

Arusha, Novemba, tarehe 22, Novemba, 2002

Sarmett, J., Afisa wa Maji, Ofisi ya Maji Bonde la Pangani, Dar es Salaam, tarehe 14, Novemba, 2002

Serikali ya Kijiji cha Shiri – Njoro, Moshi, tarehe 22, Novemba, 2002;

Tegemeo na Serikali ya kijiji cha Kawaya- Kawaya, tarehe 21, Novemba, 2002.

Waliohojiwa kwa ajili ya kiambatanisho cha 1

Aram, F. V. – Mamlaka ya Maji safi na Majitaka Mjini Tanga.

Denis, E. M. –Ofisi ya Mhandisi wa Maji Wilaya ya Handeni.

Fundi, H. – Afisa wa Haidrolojia wa Mkoa wa Tanga

Hamisi, H. – Mratibu, Hellen Keller International (APOC)

Kisheru, N. – Afisa Maliasili wa Mkoa, RAS Tanga

Lyimo, Z.C.- Afisa Mifugo wa Mkoa, RAS Tanga

Maggid, R.E. B. – Mratibu, Mradi wa CDTI Tanga.

Malange, J. P. –Mhandisi wa maji Mkoa wa Tanga, RAS Tanga

Materu, E.A. – Maabara ya Maji Tanga

Matiku, W. – Misitu ya Eneo la Vyanzo vya Mito Usambara Mashariki

Mwakibuzi, H. – Afisa Mipango wa Wilaya, Muheza

Mzee, R. S. – Hifadhi ya Asili Amani

Mtemi, A. - Hifadhi ya Asili Amani

Sesame, M. – Ofisi ya Mhandisi wa Maji Wilaya ya Handeni

Tungu, L.S. M. – Afisa Kilimo wa Mkoa, RAS Tanga

74

H. Kiambatanisho cha 1: Mabonde madogo

yaliyojumuishwa kiutawala katika

Bonde la Pangani 6

H.1 Utangulizi

Bonde la Mto Pangani lina eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 43,650. Bonde hili limezungukwa na

mabonde madogo yanayojitegemea, amabayo si sehemu hasa ya Bonde la Mto Pangani kihaidrolojia.

Kiutawala yapo chini ya Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani (PBWO) kwa sababu ni madogo mno kustahili

kuwa na ofisi za mabonde yao yenyewe. Eneo linalosimamiwa kiutawala na Ofisi ya Maji ya Bonde la

Pangani ni pamoja na Bonde la Mto Pangani, mabonde madogo ya Umba, Zigi 7 , Msangazi, Mkulumuzi

na mito midogo ya pwani, yote pamoja hufanya jumla ya kilomita za mraba 58,510. Katika kiambatanisho

hiki, taarifa kuhusu mabonde haya ya nyongeza zimetolewa kwa muhtasari kama msingi ambapo

shughuli za mradi katika Bonde la Mto Pangani zinaweza kupanuka baadaye ili kujumuisha mabonde

haya ya ziada. Mabonde yanayohusika ni:

• Bonde la Mto Umba (kilomita za mraba 8,070)

• Bonde la Mto Msangazi (kilomita za mraba 5,030)

• Bonde la Mto Zigi (angalia mito ya Pwani)

• Bonde la Mito ya Pwani (kilomita za mraba 2,080 ikiwemo Zigi na Mkulumuzi): mbali na

Mkulumuzi mito mingi ya Eneo la Chanzo cha Mito ya Pwani ni ya msimu.

Kila moja ya maeneo haya ya vyanzo vya mito linajadiliwa kipekee.

H.2 Bonde la Mto Umba

Bonde la Mto Umba lina eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 8,070 (kilomita za mraba 2,560 kati ya

hizo ziko nchini Kenya), ambapo mdomo wa Mto Umba uko eneo la Vanga katika pwani ya Kenya. Mto

huu una mtandao mkubwa wa vijito vingi vikitokea katika miteremko ya Kaskazini Magharibi ya Milima

ya Usambara. Vijito hivi huingia katika mto Umba kutokea Kusini. Mto huu unapata vijito vichache sana

kutoka Kaskazini. Eneo hili hupata mvua ya wastani wa milimita 600 kwa mwaka.

Hifadhi ya wanyamapori ya Umba, ambayo awali ilikuwa sehemu ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Mkomazi,

ipo katika bonde hili. Uoto wa asili wa mbuga hii unachukua eneo kubwa la chanzo cha mto huu:

vichaka vya aina ya Savana ya ukame iliyotawanyika na miti mifupi. Miteremko ya milima katika bonde

inafunikwa na msitu wa milima ya Afrika. Bonde la Mto Umba lina watu wachache. Matumizi makubwa

ya ardhi katika sehemu yake ya Kaskazini ni hifadhi ya wanyamapori, wakati ufugaji wa ngo’mbe ni

matumizi makubwa ya ardhi upande wa Kusini.

6

Kiambatanisho hiki kimetayarishwa na Ofisi ya Maji Bonde la Pangani

7

Baadhi ya Waandishi hutumia tahajia ‘Sigi’, ‘Zigi’ ndio tahajia inayopendelewa na wakazi wa eneo la chanzo cha

mto (pers. Comm., 2003).

75

Kilimo na Umwagiliaji

Kilimo kinachotegemea mvua kinafanyika zaidi kuliko kilimo cha umwagiliaji. Hata hivyo, mbali na

mabonde ya Mkomazi na Luengera, ambayo yapo katika eneo la Bonde la Mto Pangani, miradi mingi

midogo ya umwagiliaji iliyopo au iliyopendekezwa katika mkoa wa Tanga ipo katika bonde la mto Umba

na vijito vyake. Miradi hii ni pamoja na Mnazi, Kitivo, kijiji cha Kivingo Mnazi na mradi wa umwagiliaji

wa Mwakijembe. Zao linalomwagiliwa zaidi ni mpunga, likifuatiwa na mahindi. Katika sehemu za juu za

bonde; mbogamboga na viazi mviringo pia vinalimwa kwa kumwagiliwa. Eneo lililo chini ya mpango wa

umwagiliaji kwa ujumla linakadiriwa kuwa hekta 1475, likitumia kiasi cha maji kinachokadiriwa kuwa mita

za ujazo 25.2 x 106 kwa mwaka.

Maliasili

Maeneo yaliyohifadhiwa

Hifadhi ya wanyamapori ya Umba ina eneo la kilomita za mraba 450 likipakana na mbuga ya Taifa ya

Tsavo ya Kenya. Wanyamapori wanaopatikana katika hifadhi hii ni pamoja na nyati, tembo, simba na

aina nyingi za swala. Tishio kubwa linaloikabili hifadhi hii ni ujangili unaofanywa na wenyeji na watu

wanaoingia katika eneo hili kutoka Kenya.

Misitu

Eneo la Chanzo cha Mto Umba hapo awali lilikuwa na utajiri wa misitu mingi ambamo zilikuwemo spishi

za miti kama Mkarambati na Mkingu. Mkarambati unatumika zaidi kwa kutengeneza sanaa za uchongaji,

miti ya kujengea na samani. Inavunwa kwa wingi na inadhaniwa kuwa spishi iliyo hatarini kutoweka.

Uvunaji haramu wa misitu kwa ajili ya kutengeneza mkaa pia hufanyika.

Ili kushughulikia tazizo la uvunaji haramu wa misitu, njia za usimamizi wa misitu kijamii zimeanzishwa na

wanavijiji kama vile vijiji vya Mwakijembe, Mwanyumba, Mavovo na Daluni.

Madini

Bonde la Mto Umba lina utajiri wa mashapo ya madini, hususan kuzunguka maeneo ya Mghwashi na

Kararani, johari ya bluu inapatikana, pamoja na ‘tomalini’ ya kijani na ganeti ya waridi. Uchimbaji madini

kwa sasa unafanywa na wachimbaji wadogo ambao hawana masoko ya ndani, na hulazimika kuuza vito

johari vyao kwa njia ya magendo nchini Kenya (Kisheru, Mhojiwa)

Mgogoro wa matumizi ya maji

Kuna migogoro kati ya watumiaji maji kutokana na ugavi usiotosheleza, hasa katika maeneo ambako

kilimo cha umwagiliaji kinafanyika.

Mtandao wa ukusanyaji data

• Kituo cha Mto Umba kilichoko Mlalo (Namba IB 1): kituo kidogo, chenye safu ya geji 0-3 m: kituo

hiki kinafanya kazi, “rating curve” inahitaji kuboreshwa.

• Kituo cha Mto Umba kilichoko Mwakijembe (Namba IB 4A): kituo kikuu, chenye safu ya geji

0-4m; Kituo kina kiingiza data aina ‘orpheus’, kinafanya kazi japo kinahitaji marekebisho.

• Kituo cha Mto Mbalamo kilichoko Kivingo (Namba IB1A): kituo kidogo chenye safu ya geji 0-2m.

Kinahitaji ukarabati.

• Kituo cha Mto Bombo kilichoko Kwamkole (Namba IB 5): kituo kidogo, kinachofanya kazi, kina

safu ya geji 0-3m.

• Kituo cha mvua cha Mlalo (Namba 94.38068); kinafanya kazi na kiko katika hali nzuri.

• Kituo cha hali ya hewa cha Mnazi (Namba 94.38075): kinafanya kazi vizuri, kina vifaa vya upimaji

vya kawaida na kinachojiendesha chenyewe.

76

H. 3 Bonde la Mto Msangazi

Bonde la Mto Msangazi lina ukubwa wa kilomita za mraba 5,030 na linafikiriwa kujumuisha maeneo

ya vyanzo vyembamba vya mito vilivyotanda kutoka Magharibi mpaka Mashariki, karibu upana mzima

wa mkoa wa Tanga. Linapakana na Bonde la Mto Pangani kwa upande wa Kusini. Vijito vingi hutiririka

wakati wa majira ya mvua nyingi kuliko kawaida katika maeneo yake ya juu. Hata hivyo katika sehemu

za upande wa chini wa mji wa Handeni, mto Msangazi hutiririka kwa utaratibu wa kawaida wakati wa

msimu wa masika.

Bonde lina sura ya nchi inayofanana, na linaweza kuainishwa kama vilima, ingawa sehemu za chini

ambako kuna mashamba ya mkonge na minazi ni tambarare. Uoto uliopo ni vichaka na miti michache

ya savana. Mbali na kilimo cha mtawanyiko, sehemu kubwa ya ardhi haijatumika kiuchumi. Wastani wa

mvua kwa mwaka ni kadiri ya milimita 900.

Idadi ya watu

Bonde la Mto Msangazi limeenea wilaya tatu za mkoa waTanga: Kilindi, Handeni na Pangani. Idadi

ya watu katika eneo lilopo katika wilaya ya Kilindi ilikuwa 31,177 mwaka 2002, na Handeni walikuwa

141,263. Idadi hii inawakilisha kadiri ya asilimia 44 ya idadi ya watu wa wilaya hizi mbili. Idadi ya watu

katika bonde la mto Msangazi katika wilaya ya Pangani ni watu 10, 298.

Matumizi ya ardhi

• Kilimo: kilimo ni cha kujikimu. Mazao yanayolimwa ni pamoja na mahindi, mihogo, maharage,

ndizi, miwa na aina mbalimbali za mboga. Zao jipya lililoanzishwa hivi karibuni, mirongeronge,

inatumika kwa kutengeneza mafuta ya kupikia na usafishaji wa maji.

• Mifugo: idadi ndogo ya ng’ombe, mbuzi na kondoo hufugwa katika bonde.

Maliasili

Maji

Mji mkubwa katika bonde la mto Msangazi ni Handeni (watu 7,700). Kiasi kikubwa cha maji kwa

matumizi ya mji huu huchukuliwa kutoka Mto Pangani. Kwa nyongeza, mji huu hupata maji kutoka

kwenye visima virefu viwili: Nderema (mita za ujazo 9 kwa saa) na Mnazini (mita za ujazo 12

kwa saa). Visima hivi huhudumia asilimia 35 ya wakazi wa mji huu. Chanzo cha mwisho cha

maji cha mji huu kinatoka katika moja ya vijito vya mto Msangazi, ambacho kimejengewa bwawa

dogo. Bwawa hili lina uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo 22,500, na kadiri ya mita za ujazo 12

huchukuliwa kwa saa.

Misitu

Misitu ya Bondo na Kwamsisi yote miwili ipo katika bonde hili. Spishi za miti zinazopatikana ni

mtondoro, mpingu, mninga na mkomba.

Wanyamapori

Wanyamapori wavumilivu hupatikana sehemu za juu za maeneo ya chanzo cha mto, ikiwa ni pamoja

na nguruwe mwitu, kima, nyani na palahala. Katika sehemu ya chini ya maeneo ya chanzo cha mto

(katika Wilaya ya Pangani) kuna Mbuga ya Taifa ya Sadani, ambamo kuna tembo, twiga, na aina za

paa/palahala

Madini

Bonde la mto Msangazi halina madini muhimu yanayojulikana.

77

Matatizo na migogoro Inayoweza kutokea

• Kuingiliwa na kilimo kuzunguka vyanzo vya maji, zikiwemo kingo za mto.

• Mioto ya vichakani/misituni: Haya ni matatizo makubwa, moto huwashwa ili kusafisha vichaka

kwa ajili ya kilimo.

• Uvunaji haramu wa miti: kwa ajili ya mbao, miti ya kujengea na mkaa. Miti ya mbao inayotakiwa

sana ni mninga, mpingu, mtondoro na mkomba.

• Kuna mgogoro unaoibuka kati ya wafugaji na wakulima juu ya maeneo ya kunyweshea

mifugo.

Magonjwa

Magonjwa yanayotokea kwa wingi katika bonde la mto Msangazi ni malaria na homa ya matumbo.

Kipindupindu na magonjwa mengine yanayosababisha kuharisha hutokea mara chache.

Mtandao wa ukusanyaji data

• Kituo cha Mto Msangazi kilichoko Kideleko (Namba IE 3): kituo kidogo, kinafanya kazi, kina geji

0-1m

• Kituo cha Mto Msangazi kilichoko Kwedilomba (Namba IE 1): kituo kinafanya kazi, safu ya geji

0-2m, kina kiingiza data aina ya ‘Thalamides’.

• Kituo cha hali ya hewa cha Handeni (Namba 95.38079): kinafanya kazi pamoja na kituo

kinachojiendesha chenyewe.

• Kituo cha mvua kilichoko Kwedilomba: kinafanya kazi.

Mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi katika Bonde

la mto Msangazi

• World Vission (shirika lisilo la kiserikali)

• HADEA (Chama cha Maendeleo Handeni)

• HIAP – Mradi Shirikishi wa Kilimo mseto Handeni (lilimaliza shughuli zake mwaka 2002)

• Ded-GTZ-Msaada wa kiufundi na ushauri katika wilaya (maji)

H.4 Bonde la Mto Zigi

Mto wa kudumu wa Zigi huanzia katika miteremko ya mashariki ya Milima ya Usambara, na una vijito

vikuu viwili vinavyotiririka kutoka Kaskazini na Kusini (Muzi na Kihuhwi). Baada ya kuungana, Mto Zigi

hutiririka kuelekea Mashariki na kuingia katika Bahari ya Hindi kupitia Bwawa la Mabayani, chanzo kikuu

cha maji kwa Jiji la Tanga.

Maeneo ya juu ya chanzo cha mto Zigi ni ya milima, ambayo kwa sehemu kubwa ina misitu minene

iliyopakana na mashamba ya chai. Sehemu zake za chini ni za vilima vyenye vichaka vya aina ya savana

kame na miti mifupi, pia mashamba ya mkonge. Katika ukanda wa pwani, minazi na michikichi iko kwa

wingi. Kwa ujumla eneo zima la bonde hili lina uoto wa kutosha na hatari ya mmomonyoko ni ndogo.

Mvua katika Bonde la Mto Zigi ni za misimu miwili. Hata hivyo, mgawanyo wake hutofautiana kati

milimita 1,000 mpaka 2,000. Wastani wa mvua kwa mwaka unakadiriwa kuwa milimita 1,200 hadi

milimita 1,400.

78

Maliasili

Misitu

Kuna hekta 30,000 za msitu katika eneo la Chanzo cha Mto Zigi, ambao unajumuisha msitu wa eneo

la vyanzo cha mito wa Usambara Mashariki (EUCF), ambao ni sehemu ya misitu ya Milima ya Tao la

Mashariki. Umuhimu wa misitu ya eneo la chanzo cha mto ni pamoja na:

• Utoaji mbao na mimea ya dawa kwa jamii;

• Misitu hii ni chanzo cha Mto Zigi, ambao hutoa maji ya matumizi ya nyumbani kwa Jiji la Tanga;

• Kuhifadhi maji kwa kurekebisha kasi ya mtiririko wa maji, kuzuia mmomonyoko wa udongo,

kuboresha upenyaji wa maji kwenye hazina ya maji ya ardhini na ubora wa maji;

• Ni makazi ya viwango vya juu sana vya bayoanuwai, na huchangia kudumisha makundi ya jeni

kidunia;

• Misitu ya kwenye genge la Milima ya Usambara Mashariki huzuia mmomonyoko na mporomoko

wa ardhi.

Bayoanuwai na maeneo yaliyohifadhiwa

Hifadhi ya Asili ya Amani (ANR) ilianzishwa mwaka 1997 na ina jumla ya eneo la hekta 8,380. Hifadhi hii

iko kwenye misitu ya vyanzo vya mito ya Usambara Mashariki (EUCF). Milima ya Usambara Mashariki

ni fungu la mlima lililo kubwa zaidi katika safu ya Milima ya Tao la Mashariki. Hifadhi ya Asili ya Amani ina

misitu mirefu ya kuvutia ya milimani na misitu inayopukutisha majani ya nyanda za chini zenye wastani

wa kikomo cha mwinuko cha mita 850.

Kibayolojia, Hifadhi ya Asili ya Amani ina utajiri mkubwa wa mchanganyiko wa spishi. Milima ya Usambara

Mashariki inachukuliwa kama kituo cha kidunia cha mimea anuwai. Miongoni mwa jenasi na spishi za mimea

inayopatikana katika hifadhi hii ya msitu pekee ni ‘Saintapaulia’ (spishi 9), Cynometra (spishi 4), ‘Streptokapus’

(spishi 2), Impatients katae, Vernonia amaniencis, Dolichometra leucantha na Cordia peter;

Kwa kuongezea, Milima ya Usambara Mashariki inatambuliwa kuwa ni ya pili kwa kuwa na aina mbalimbali

za wanyama barani Afrika. Baadhi ya mamalia wa Hifadhi ya Asili ya Amani wamewekwa kwenye kundi

la walio hatarini kutoweka duniani, kama vile Popo Matunda wa Afrika Mashariki (Myonyctaris relicta),

Panya wadogo (wanaofanana na tembo) wekundu na weusi (Rhyncoyon petersi), Nguchiro wenye mikia

yenye manyoya (Bdeo-grade crassicaud omnivore) na Palahala wa Abbot (Cephalophus spadix).

Halmashauri ya Kimataifa ya Kuhifadhi Ndege (ICBP) imeainisha misitu ya milimani na ya nyanda za

chini ya Usambara ya Mashariki kama eneo maalum la ndege wanaopatikana kipekee (EBA). Spishi kumi

na tatu za ndege walio hatarini kutoweka duniani, kama vile Bundi Tai wa Usambara (Bubo vosseleri)

Kwera Usambara (Ploseus nicolli), Chozi Pwani (Anthreptes pallidigaster), na Kolokolo domorefu

(Apalismoreaui moreaui), wanajulikana kuwa huishi katika Hifadhi ya Asili ya Amani.

Miongoni mwa spishi za amfibia za Hifadhi na Misitu hii, spishi za watambaazi, wanyama wasio na uti

wa mgongo na bayoanuwai pia hupatikana kwa wingi kipekee katika sehemu hii kwa kiwango cha juu

sana. Amfibia wengi huzaliana na kujipatia makazi ndani na kandokando ya Mto Zigi, ambao pia hufanya

makazi kwa spishi nyingi za watambaazi na wadudu.

Maji na Udongo

Hifadhi ya Asili ya Amani ni mojawapo ya maeneo ya chanzo cha maji iliyo muhimu sana katika Milima ya

Usambara Mashariki. Misitu ya mvua ya milimani ambayo huenea sehemu kubwa zaidi ya Hifadhi hii hutoa

mchango muhimu katika haidrolojia ya Mkoa wa Tanga. Mto Zigi hutoa maji kwa matumizi ya nyumbani

kwa Jiji la Tanga (lenye watu 300,000), viwanda vilivyopo, mashamba na jamii zinazopakana nayo.

Bwawa la Mabayani liko katika Mto Zigi, ambalo maji yake hukimu Jiji la Tanga. Hodhi yake ni takriban

mita 3,500 kwa urefu na wastani wa upana wa mita 400. Hapo awali (mwaka 1978), hodhi hii ilikuwa na

79

uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo milioni 7.7, lakini kiasi hiki kimepungua polepole kutokana na kujaa

kwa mchangatope kunakosababishwa na mmomonyoko na mporomoko wa ardhi. Mashapo ya ziada

yanatokana na mimea iliyong’olewa na maji ya mafuriko, maji machafu yatokanayo na mchakato wa

kuponoa katani na mata zizalishwazo katika bwawa lenyewe na jamii za mimea na wanyama wadogo

wadogo wanaoishi katika maji, samaki na wanyama wengine wasio na uti wa mgongo.

Uozaji wa mata za viumbe hai unahitaji hewa ya oksijeni, hali inayosababisha uondoaji oksijeni kwenye maji

yanayozizunguka. Kuwepo kwa virutubisho hivyo pia kunachochea uzalishaji wa mimea zaidi, na kusababisha

uzalishaji zaidi wa mata za viumbe hai na hatimaye upunguaji wa oksijeni chini ya bwawa. Mchanganyiko wa

michakato hii ya uingiaji wa virutubisho na hatimaye uondoaji wa oksijeni vinaweza kusababisha ongezeko la

viwango vya virutubisho, ingawa hakujapatikana ushahidi wa jambo hii kutoka kwenye bwawa hilo. Hata hivyo,

shaka ya kuwa hii inaweza kutokea ipo, na yafuatayo ni mapendekezo ya hatua zinazoweza kupunguza:

• Kufuatilia ulimbikizaji wa masimbi/mata za viumbe hai katika bwawa;

• Kuondoa mara kwa mara magugu ya majini (mfano hyacinth na makabichi ya Mto Nile) kutoka

bwawani kwa mikono, kibayolojia au kwa mashine.

• Kudhibiti ubora na ujazo wa maji machafu kutoka viwanda vya katani vilivyopo eneo la juu la

mto;

• Kutambua uwiano wa kiasi cha mimea ya majini ambayo huzolewa kupitia njia ya kupunguzia

maji ya bwawa hili. Ikiwa kiasi ni kidogo, mbinu za kuongeza lazima zitafutwe.

Uvuvi

Uvuvi unafanyika zaidi katika pwani ya Bahari ya Hindi, ambako mdomo wa Mto Zigi ndipo ulipo. Uvuvi

mdogo mdogo upo katika mkondo wake, ukilenga samaki kama kambare, perege, ningu, ngogogo, kuyu

na wengineo. Uvuvi katika bwawa la Mabayani umepigwa marufuku kwa sababu maji yake yamekusudiwa

kama chanzo cha maji ya matumizi ya nyumbani kwa Manispaa ya Tanga.

Ardhi

Matumizi makuu ya ardhi katika bonde ni kilimo, kinachofanyika zaidi katika ngazi ya kiwango kidogo.

Mazao kama mahindi, mihogo, ndizi na matunda yanalimwa, wakati mazao ya biashara ni mkonge, chai na

misitu (kama mradi wa Shamba la Mitiki la Longuza).Kwa kiasi kidogo, ufugaji wa ng’ombe pia hufanyika.

Matatizo

• Uharibifu wa misitu: hii hutokea hasa kama matokeo ya uvunaji haramu wa miti kwa ajili ya mbao,

kuni miti ya kujengea, usafishaji kwa ajili ya kilimo, nk., na husababisha kuongeza kasi ya mtiririko

wa maji juu ya ardhi, wakati ikipunguza kiasi cha maji kinachopenya ardhini.

• Uondoaji wa maji machafu: Maji machafu yanayoondolewa kutoka viwanda vya katani bila

kusafishwa au yasiyosafishwa kikamilifu husababisha uondoaji oksijeni katika maji ambayo uchafu

huu huingia, na hufanya kazi kama virutubisho, hivyo kusaidia kukuza ongezeko la virutubisho.

• Matumizi ya kemikali za kilimo: ingawa hakujapatikana data juu ya athari ya kemikali za kilimo

kwenye vyanzo vya maji katika bonde hili, upo uwezekano kuwa mabaki ya kemikali za kilimo hufikia

vyanzo vya maji kupitia maji ya mvua. Kutegemeana na aina ya kemikali ya kilimo na kiwango cha

kukolea, afya ya binadamu na viumbe vya majini inaweza kuathirika kwa mabaki hayo. Katika eneo

la chanzo cha Mto Zigi, kemikali za kilimo, yakiwemo madawa ya kuulia wadudu, dawa za mimea

na mbolea hutumika zaidi katika mashamba ya chai ya Amani na vitalu vya miti (Materu, Mhojiwa).

• Makazi ya binadamu karibu na vyanzo vya maji: hii husababisha uharibifu wa ardhi na ukusanyikaji wa

mabaki kuongezeka katika maji, uchafuzi wa maji kwa upenyaji wa kinyesi kutoka vyooni au utupaji wa

kinyesi moja kwa moja, na pia kiasili na kikemikali kwa utupaji wa taka ngumu katika maji.

80

• Magugu ya majini: spishi kadhaa za magugu ya majini hupatikana katika Mto Zigi na Bwawa

la Mabayani, kwa mfano magugumaji “water hycinth” (Eichhornia crassipes), makabichi ya Nile

(Pistia stratiotes) na water ivy, (Lpomoea aquatica). Magugumaji yana uwezo wa kufunika uso

wa maji kiasi cha kuathiri ubora wa maji. Hali hii pia inaweza kuathiri afya za binadamu kwa

kuboresha hali zinazohitajika kuwezesha vijidudu vya maradhi kuzaliana, ambavyo ni muhimu

katika mzunguko wa maisha ya pathojeni mbalimbali za binadamu, kama vile mbu (malaria), na

konokono (kichocho).

• Mbinu duni za kilimo: matumizi ya moto kwa kusafisha mashamba, kilimo kwenye miteremko ya

milima, ukataji miti na shughuli nyingine za binadamu katika maeneo ya vyanzo vya maji yanaweza

kuchafua maji kwa kuongeza tope katika maji, rangi na shehena ya masimbi, hususan wakati wa

msimu wa mvua. Sababu hizi zinafikiriwa kusababisha ongezeko la tope katika Bwawa la Mabayani

mwezi Desemba, 1999 kutoka kipimo cha NTU 20-30 hadi NTU 1,400 (Materu, Mhojiwa).

• Magonjwa: Ugonjwa wa Usubi hutokea katika Wilaya ya Muheza, Bonde la Mto Zigi. Husababishwa

na mnyoo (filaria) anayeitwa Onchocerca volvulus. Kimelea hiki huambukizwa kwa binadamu

kwa kuumwa na nzi wadogo weusi. Mbali na upofu, ugonjwa huu pia unasababisha matatizo

makubwa ya ngozi. Nzi hawa huzaliana katika maji yanayotiririka kwa kasi yaliyo na oksijeni

nyingi. Magonjwa mengine katika Bonde la Mto Zigi yanayohusiana na maji ni kipindupindu, homa

ya matumbo na malaria (Maggid, Mhojiwa)

Migogoro iliyopo na Inayoweza Kutokea

• Mgogoro unatarajiwa kutokea kati ya watumiaji maji wa Manispaa ya Tanga na mji wa Muheza.

Upatikanaji wa maji kwa mji wa Muheza kwa sasa hautoshelezi mahitaji, na kuna pendekezo la

kuchukua maji kutoka mto Zigi ambao ni tegemeo pekee la watu wa Jiji la Tanga kwa sasa.

• Mgogoro kati ya matumizi ya maji majumbani na mahitaji ya mazingira: kiasi cha chini kabisa cha

mtiririko wa maji unaotakiwa kuhimili mfumo ikolojia chini ya bwawa la Mabayani hakijulikani.

• Mgogoro kati ya wachafuzi na wasimamizi wa maji: kwa mfano, mgogoro kati ya wasimamizi wa maji

na wenye shughuli za kilimo, pale wasimamizi wa maji wanapojaribu kudhibiti uchafuzi wa maji, kwa

mfano, uchafuzi utokanao na mchakato wa viwanda vya mashamba ya mkonge (Mjesani, Kibaranga,

Lanconi na Bamba), na uchafuzi kutokana na madawa ya kilimo kutoka mashamba ya chai.

Mtandao wa ukusanyaji data

• Kituo cha mto Zigi kilichopo Lancon (Namba IC 1): kituo kikuu, kinafanya kazi, kina safu ya geji

0-10m; kituo kina kiingiza data cha aina ya ‘orpheus’.

• Kituo cha mto Zigi kilichopo Miembeni (Namba IC 2); kituo kidogo, kinafanya kazi na kina safu

ya geji 0-4m; “rating curve” inahitaji kuboreshwa.

• Kituo cha mto Zigi kilichopo Kisiwani (IC 4); kituo kidogo chenye safu ya geji 0-3m. Kipo maalum

kwa matumizi ya misitu ya Bonde la Mto Zigi. “rating curve” inahitaji kuboreshwa. Geji ya 0-1m

imechukuliwa na mafuriko.

• Kituo cha mto Muzi kilichopo Msakazi (ICA 1): kinafanya kazi, lakini “rating curve” inahitaji

kuboreshwa

Kutuo cha mvua cha Zigi-Lancon: kinafanya kazi.

• Vituo vya usawa wa maji na mvua vya Bwawa la Mabayani: vinafanya kazi.

• Vituo vya mvua vya ziada katika bonde vinavyoendeshwa na taasisi mbalimbali, kama vile Msitu

wa Longuza, Msitu wa eneo la vyanzo vya mito, Usambara Mashariki (EUCF) n.k.

81

H.5 Bonde la Mto Mkulumuzi (na mito ya Pwani )

Mito ya pwani huanzia katika genge linaloenda sambamba na pwani kwa umbali wa kilomita 20-30.

Wastani wa mvua katika eneo hili la chanzo cha mto ni milimita 1,100. Ikolojia inalingana kwa kiasi.

Miteremko ya awali ni vilima kwa ujumla, na polepole inakuwa tambarare kadiri inavyoingia uwanda

wa pwani. Minazi, michikichi na mikorosho inatawala uoto. Mkonge pia hustawishwa katika mashamba

makubwa. Matatizo ya mmomonyoko wa udongo hayajaonekana katika maeneo haya..

Mito mingi ya pwani hutiririka kwa vipindi vifupi tu katika msimu wa mvua na huwa mikavu kwa kipindi

kinachobaki cha mwaka. Mto pekee wa kudumu ni Mkulumuzi. Eneo la chanzo cha mto huu ni kilomita

za mraba 337, ambalo lipo upande wa Kusini la eneo la chanzo cha Mto Zigi. Chanzo chake kipo katika

Msitu wa Magoroto.

Maliasili

Maji

Mto Mkulumuzi ni chanzo cha maji cha mji wa Muheza, wenye idadi ya watu wapatao 25,700.

Kilimo

Kilimo katika eneo hili kwa kiwango kikubwa ni cha kujikimu, isipokuwa mkonge, ambao hulimwa katika

viwango vya kibiashara. Mazao ya kujikimu yalimwayo ni pamoja na mahindi, ndizi, mihogo, mpunga, na viazi

vitamu. Matunda (hususan machungwa), nazi, korosho na viungo hulimwa kama mazao ya biashara.

Mifugo

Ufugaji katika maeneo haya si mkubwa sana. Idadi ndogo ya ngo’mbe wa maziwa, mbuzi na nguruwe

hufugwa.

Uvuvi

Ingawa uvuvi ni shughuli inayofanywa na watu wengi katika pwani, hakuna shughuli kubwa ya uvuvi

inayofanyika katika maeneo ya vyanzo vya mito ya pwani.

Migogoro muhimu iliyopo

• Makazi: Mahitaji makubwa ya ardhi ya makazi yametokea baada ya mashamba ya Mkonge kufa,

na wafanyakazi kufukuzwa.

• Maji yasiyotosheleza kwa mji wa Muheza.

Mtandao wa ukusanyaji data

• Kituo cha mto Mkulumuzi kilichoko Upare (hakijasajiliwa): kituo kipya cha upimaji maji mtoni,

kilicho na kiingiza data cha aina ya ‘Thalimedes’

• Kituo cha mto Msimbazi kilichopo Lugongo: kituo kipya cha upimaji maji mtoni chenye safu

ya geji 0-2m.

• Kituo cha hali ya hewa cha Mlingano (chini ya wizara ya Kilimo na Chakula): kinafanya kazi.

Mashirika yanayofadhili

• Irish Aid: hufadhili programu shirikishi zilizopangwa katika eneo hili

• TASAF-Mfuko wa hifadhi ya jamii

• NORAD: hufadhili Programu ya Usafiri na Usafirishaji Vijijini (VTTP)

• IUCN: inajishughulisha na Hifadhi ya Mazingira ya Pwani, kwa ushirikiano na Ireland Aid

• AXIOS International: husaidia yatima na watoto walio katika mazingira magumu

• GTZ: husaidia miundombinu ya afya, ufadhili wa ugawaji wa madawa ya msingi kwa vituo vya afya

• APOC/CDTI: Udhibiti wa ugonjwa wa Usubi

82

Mchoro Na 4: Utawala wa Bonde la Pangani

Angalia pia picha ya 2, ukurasa wa 34

(Rejea; Mradi wa Usimamizi wa Matumizi Bora ya Maji)

83

Coast Development Authority

IUCN – Shirika la Kimataifa la Hifadhi ya Uasili

Likiwa limeanzishwa mwaka 1948, Shirika la Kimataifa la Hifadhi ya Uasili linakutanisha pamoja nchi, mawakala wa nchi

na mashirika mbalimbali yasiyo ya serikali katika ubia wa pekee duniani: zaidi ya wanachama wake 1000, wameenea

katika nchi zaidi ya 160.

Kama shirika, IUCN inalenga kushawishi, kutia moyo na kusaidia jamii ulimwenguni kuhifadhi hadhi na anuwai ya uasili

na kuhakikisha kwamba matumizi yoyote ya maliasili yanafanywa kwa stahili na yanakuwa endelevu kiikolojia.

Shirika la Kimataifa la Hifadhi ya Uasili linategemea nguvu ya wanachama wake, mitandao na ubia katika kuendeleza

uwezo wao na kusaidia muungano wa kilimwengu wa kulinda maliasili katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kiulimwengu.

Programu ya Maji na Uasili ya IUCN (WANI)

Programu ya Maji na Uasili ya IUCN (WANI) ni mpango wa utekelezaji wa miaka 5 wa kuonesha kwamba usimamizi

wenye misingi ya mifumo ya ikolojia na ushirikshwaji wa wadau utasaidia katika kukabiliana na changamoto zihusuzo maji

kwa sasa – kuhuisha mito na kuidumisha rasilimali hii kwa manufaa ya wengi.

Ofisi ya Bonde la Pangani (PBWO)

Marekebisho ya sheria ya matumizi ya maji (Na. 10 ya 1981) ya Tanzania yalianzisha utaratibu wa Usimamizi na

Ugawaji wa maji kufuata mipaka ya kihaidrolojia. Kutokana na hiyo Ofisi ya Maji Bonde la Pangani ilianzishwa mwaka

1991. Majukumu yake makuu ni kudhibiti na kusimamia matumizi ya maji, kwa kuzingatia ubora na wingi wake katika

Bonde la Pangani.

Mamlaka ya Maendeleo ya Pwani (CDA)

Mamlaka ya Maendeleo ya Pwani ni Mamlaka ya Maendeleo ya Kanda iliyoanzishwa kufanikisha mipango shirikishi ya

maendeleo, uwezeshaji, uanzishwaji, uratibu na utekelezaji wa miradi na programu ndani ya eneo la mamlaka, ambalo ni

Jimbo la Pwani lote na Wilaya ya Ijara na Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Kenya (EEZ).

Mpango wa Maji wa Dunia (Global Water Initiative)

Mpango wa Maji wa Dunia unaofadhiliwa na mfuko wa Howard G. Buffet ulianzishwa Septemba 2006 kwa lengo la kuhakikisha jamii

zilizopo katika mazingira hatarishi duniani zinapata huduma ya maji safi na salama bila kuathiri hadhi, haki, utamaduni na mazingira

yao ya asili. Malengo mkakati ya mpango huu ni kusaidia usimamizi wa pamoja wa rasilimali maji katika nchi zilizoainishwa, kuanzisha

na kuendeleza umoja wa watumia maji katika maeneo yao, na pia kueneza ushawishi hata nje ya mipaka ya eneo la mpango huu

ili kufikia wigo mpana zaidi. Mpango unalenga katika kuanzisha ubia baina ya asasi mahsusi katika kanda tatu za kijiografia duniani

kama ifuatavyo: Afrika Mashariki (Ethiopia, Kenya, Tanzania na Uganda), Afrika Magharibi (Burkina Faso, Ghana, Mali, Niger na

Senegal) na Amerika ya Kati (El Salvador, Guatemala, Honduras na Nicaragua). Asasi zinazohusika katika mpango huu kwa sasa ni

“Action against Hunger (AAH), CARE, Catholic Relief Services (CRS), International Institute of Environment and Development (IIED),

International Union of Conservation of Nature (IUCN), Oxfam America na SOS Sahel”

Katika kanda ya Afrika ya Mashariki, mpango huu unajulikana kama mkakati wa kukabiliana na ukame (GWI Running Dry) na

unaratibiwa na ofisi ya kanda yenye makao yake Addis Ababa, Ethiopia (chini ya kivuli cha CARE International, Ethiopia).

Pangani Basin Water Board

P.O. Box 5978

Hale Tanga Tanzania

Tel ++ 255 27 2640836

Fax ++ 255 27 2641031

E-mail: pbwo@panganibasin.com

IUCN Eastern and Southern Africa

Regional Office

P.O. Box 68200-00200

Nairobi Kenya

T: +254 20 890605-12;

W:+254 20 249 3561/65/70

M: +254 724 256 804 or + 254 734 768 770

F:+254 20 890615

E-mail: earo@iucn.org

Coastal Development Authority (CDA)

P.O. Box 1322

Mombasa Kenya

Tel + 254 41 22440

E-mail: cda@africaonline.co.ke

IUCN Water and Nature Initiative

Rue Mauverney 28

CH-1196 Gland

Switzerland

Tel + 41 22 999 0001

Faxl + 41 22 999 0002

E-mail: waterandnature@iucn.org

GWI Running Dry Program

CARE International in Ethiopia

P.O.Box 4710; Addis Ababa, Ethiopia

Phone: +251-11-618 3294 Ext 160

Fax: +251-11-618 3295

Web: http://www.care.org.et

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!