11.07.2015 Views

BArAzA Kuu LA WAiSLAMu TAnzAniA - Health Policy Initiative

BArAzA Kuu LA WAiSLAMu TAnzAniA - Health Policy Initiative

BArAzA Kuu LA WAiSLAMu TAnzAniA - Health Policy Initiative

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

BAKWATA S&D Guidelines.FINAL2.indd, Spread 5 of 8 - Pages (10, 3) 3/5/2009 5:05 PMMaazimio ya Utekelezaji kwaViongozi wa KiislamuAzimio la 1: Kuwakinga wasioambukizwa na Virusi vya UKIMWI na UKIMWINi jukumu la viongozi wote wa Kiislamu kuwakinga watu ambao hawajaambukizwa na Virusi vya UKIMWI kwakutoa elimu sahihi juu ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Hii itatusaidia sisi na jamii nzima kuepukana na atharimbaya zinazotokana na kuenea kwa ugonjwa huu. Hii ni pamoja na kuondokewa na nguvu kazi ya na kuongezekakwa umasikini miongoni mwa jamii na taifa kwa ujumla. Kinyume chake ni madhara kwetu sote bila kujali nafasiyetu katika jamii. Mwenyezi Mungu anatueleza kuwa:pengine kuliko hata ugonjwa wenyewe. Ni kutokana na msingi huu wa Sera ya Baraza,BAKWATA imeona ipo haja ya kuandaa na kusambaza mwongozo wa namna Uislamuunavyoshughulikia tatizo la unyanyapaa kwa Maimamu na viongozi wengine wa Kiislamu.Lengo la muongozo huu ni kutoa muongozo wa Kiislamu katika kushughulikia tatizola unyanyapaa hasa unaotokana na UKIMWI. Ni matarajio yetu kuwa mwongozo huuutatoa msaada kwa viongozi wa Kiislamu katika kulishughulikia tatizo la unyanyapaa naubaguzi katika jamii kwa mujibu wa mafundisho ya Qur’an na Sunna za Mtume wetuMuhammad (S.A.W.).Unyanyapaakwa kiasi kikubwaunaathiri afya yamgonjwa penginekuliko hata ugonjwawenyewe.“Iepukeni fitina ambayo haitowafika (na kuwadhuru) waliofanya peke yao, bali pia wale watakaoona (uharibifu)huo unafanywa na wasikataze.”[Qur’an 8:25]Hivyo ni jukumu letu kuzuia tatizo la unyanyapaa na ubaguzi liwe linatokea kwetu au kwa jamaa zetu. Hililinawezekana iwapo tutafanya pamoja kutokomeza unyanyapaa na ubaguzi. Hivyo, viongozi wa Kiislamuwanawajibu wa kuwaelimisha waumini wa Kiislamu athari mbaya inayotokana na unyanyapaa na ubaguzi kwa watuwanaoishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.Azimio la 2: Jukumu la kuielimisha jamii juu ya athari za unyanyapaa na ubaguziViongozi wa Kiislamu wanapaswa kuwaelimisha waumini wa Kiislamu kuwa unyanyapaa na ubaguzi ni kinyume namafundisho ya Uislamu. Mbinu mbalimbali zitumike kuwaelimisha Waislamu na jamii kwa ujumla juu ya madharaya unyanyapaa na ubaguzi, sio kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI tu, bali kwa jamii nzima.Azimio la 3: Jukumu la kuielimisha jamii juu ya hadhi ya mwanadamuViongozi wa Kiislamu wanapaswa kukumbuka na kuwaelimisha waumini wa Kiislamu juu ya hadhi aliyonayomwanadamu yeyote, awe Muislamu au asiwe Muislamu. Awe na virusi au awe hana virusi. Kama tulivyoona katikaQur’an kuwa Mwenyezi Mungu anasema kuwa:“Bila shaka tumemuumba mwanadamu kwa umbo lililo bora kabisa.” [Qur’an 95: 4]Hii itasaidia kuimarisha mapenzi na huruma miongoni mwa wanajamii wakiwemo watu wanaoishi na Virusi vyaUKIMWI na UKIMWI na hivyo kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa jamii na kufanikisha kazi muhimuya kutokomeza unyanyapaa na ubaguzi hasa kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.Azimio la 4: Kuwatendea wema wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWIViongozi wa Kiislamu wawaelimishe waumini mafundisho ya Uislamu juu ya kuwatendea wemawatu bila kujali itikadi zao, kwa kuzingatia hadhi na heshima ambayo Mwenyezi Mungu (S.W.) amempamwanadamu.10 3

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!