17.12.2012 Views

KILIMO CHA VITUNGUU MAJI - The 4-H Global Knowledge Center

KILIMO CHA VITUNGUU MAJI - The 4-H Global Knowledge Center

KILIMO CHA VITUNGUU MAJI - The 4-H Global Knowledge Center

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Bungua mweupe Funza wa Kitunguu

3. Minyoo ya vitunguu (Onion wireworms)

Hawa ni funza ambao mayai yao hutagwa kwenye maeneo yenye

magugu. Wadudu hawa huwa ni tatizo kubwa kwenye sehemu zenye

kutuamisha maji. Kutifulia udongo ili upitishe maji vizuri pamoja na

udhibiti wa maguu ni njia nzuri ya kuwadhibiti wadudu hawa.

Uvunaji

Inapowezekana mwezi mmoja kabla ya kuvuna udongo uanze

kuondolewa polepole ili kuviacha wazi vitunguu kwa ajili ya

ukaukaji mzuri. Zoezi hili linalenga kufanya angalau theluthi moja ya

sehemu ya kitunguu kiwe hakijafunikwa na udongo kwa siku kati ya

7 hadi kumi kabla ya kuvuna ili kuharikisha ukaukaji. Vuna wakati

asilimia 75 ya shingo za vitunguu zimelala. Mara nyingi vitunguu

hung’olewa na kurundikwa kwenye matuta na baadaye kukusanywa

na kuwekwa kwa ajili ya kukata shingo. Mizizi pia inapunguzwa na

vitunguu vinajazwa kwenye magunia tayari kwa kusafirishwa

nyumbani kwa ukaushaji zaidi na kisha kuwekwa galani au kuuzwa.

Ukaushaji

Madhumuni ya kukausha ni kuvifanya vitunguu visiweze kuota kwa

muda na pia kuvifanya visiharibike. Vitunguu vilivyokauka vizuri

huwa na shingo iliyonywea vizuri na ganda kavu. Kama shingo ya

kitunguu haikukauka sawasawa kutatokea hali ya uozo.

Soko la vitunguu

Ukubwa wa vitunguu ni sifa ingaliwayo na wanunuzi. Vitunguu

vidogodogo sana au vinene sana huwa havipendwi. Vitunguu

vinavyopendwa ni vile vyenye wastani wa unene wa sentimita nne.

Vitunguu vilivyochubuka, mapacha na vyenye shingo ya chupa huwa

havipendwi. Vitunguu vilivyooza na vile vilivyobabuka na jua pia

havifai. Kwa Tanzania wakulima wengi wanauza vitunguu kwa

vipimo vya magunia na ama ndoo za plastiki. Kwa miaka kadhaa

vitunguu vimekuwa vikiuzwa kati ya shilingi 20,000/= hadi 30,000/=

kwa gunia.

Hifadhi ya vitunguu

Vitunguu vipya vilivyovunwa huwa havioti upesi. Hifadhi sahihi

hurefusha muda wa kutoota. Kwenye hifadhi ni vizuri vitunguu

vipate hewa yenye mzunguuko mzuri na ndiyo maana maghala ya

kuhifadhia vitunguu yanajengwa kama vichanja ili kuruhusu hewa

kuzunguuka hata kwa kupitia sehemu za chini. Ndani ya ghala

vitunguu humwagwa na kusambazwa kama inavyonyesha kwenye

picha namba.. Vitunguu vinaweza kuhifadhiwa kwa miezi sita au

zaidi bila kuharibika.

Mavuno

Mavuno ya vitunguu yanategeme huduma za shamba pamoja na hali

ya hewa. Vitunguu pia hutofautiana katika mavuno kulingana na aina

ya kitunguu. Kwa wastani vitunguu vinaweza kutoa mavuno kati ya

tani 10 hadi 18 kwa hekta moja.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!