programu ya hifadhi ardhi shinyanga (hashi) - Equator Initiative
programu ya hifadhi ardhi shinyanga (hashi) - Equator Initiative
programu ya hifadhi ardhi shinyanga (hashi) - Equator Initiative
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
Historia na Mandhari

Ukiwa unapatikana upande wa kusini mwa ziwa Victoria, mkoa wa

Shinyanga upo kaskazini magharibi mwa Tanzania na eneo lake

kubwa ni la mazingira ya ukame ukiwa na wakazi karibu milioni

tatu, kwa wastani wa watu 42 kwa kila kilometa ya mraba. Shinyanga

ni moja ya mikoa ya Tanzania maskini zaidi, wenye vilima vya kimo

cha chini na tambarare zenye kipindi kirefu cha kiangazi ukiwa

na wastani wa milimeta 700 za mvua kwa mwaka. Kabila kubwa

la mkoa huu ni Wasukuma ambao hujishughulisha na ufugaji na

kilimo; mazao makubwa wanayozalisha ni mahindi, mtama, uwele,

mihogo, pamba, na mchele. Zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wa mkoa

huu wanamiliki na kuendeleza mifugo kwenye malisho ya jamii zao.

Kati ya mwaka 1986 na 2004, mkoa wa Shinyanga ulianzisha Mpango

wa Hifadhi Ardhi Shinyanga uliofahamika kwa kifupi kama HASHI

(Hifadhi Ardhi Shinyanga). HASHI ilianzishwa na Rais Julius Nyerere

baada ya kutembelea mkoa huo mwaka 1984 na akashtushwa na

kiwango kikubwa cha ukataji miti. Kwa miaka ya 1980, Shinyanga

ilikuwa inajulikana kama ‘Jangwa la Tanzania ‘. Miongo kadhaa ya

usimamizi mbovu wa ardhi ilichangia kuendelea kuharibika kwa

mazingira katika mkoa wa Shinyanga, lakini mwanzo mkuu wa

uharibifu huu ni mpango wa kukata misitu kipindi cha kabla ya vita vya

pili vya dunia. Hapo awali, mkoa wa Shinyanga ulikuwa umefunikwa

na uoto wa miombo na mshita, ambayo ilitoa lishe kwa mifugo na

mafuta kwaajili ya kilimo na ufugaji kwa wasukuma. Hata hivyo

misitu hii ilikuwa pia hifadhi ya mbun’go, na magonjwa ya vimelea,

na malale ambayo yaliwashambulia binadamu na wanyama. Katika

miaka ya 1920, mamlaka ya kikoloni ilibuni mpango wa kuwalipa

wenyeji kwa kukata miti kwenye maeneo makubwa ya miombo. Hii

kwa kiasi kikubwa ilisaidia mafanikio katika kutokomeza Mbun’go,

na pia kuanzisha maeneo mapya ya malisho kwa ajili ya wasukuma,

lakini kwa upande mwingine ikaathiri uzuri wa mazingira ya mkoa.

Kadiri idadi ya mifugo na binadamu ilivyoongezeka katika nusu ya

mwisho ya karne ya ishirini, mahitaji kwa ajili ya kuni na kilimo pia

yaliongezeka. Hii ilisababisha ufugaji uliokithiri kwenye malisho na

mapori, wakati maeneo makubwa ya ardhi yalikuwa kwa ajili kilimo

cha mazao ya biashara kama vile pamba na tumbaku, na kuacha

ardhi kidogo kwa ajili ya kupanda mazao ya chakula. Zaidi ya hayo,

mpango wa uanzishwaji wa vijiji wa Rais Nyerere wa miaka 1970

ulilazimisha familia nyingi kuyaacha makazi yao kuhamia maeneo

mapya.

Kupotea kwa mfumo wa kijadi wa usimamizi wa rasilimali

Hali hizi zilisababisha mmomonyoko wa mfumo wa kijadi wa

usimamizi wa ardhi ambao wasukuma walitumia kuhifadhi

chakula cha mifugokwaajili ya msimu wa kiangazi. Mfumo huu

unaofahamika kama ngitili ulijumuisha utengaji wa maeneo

maalumu ya kuhifadhi nyasi za mifugo kwa ajili ya matumizi ya

kifamilia au ya jamii kwa kuyaacha maeneo yakiwa na nyasi mpaka

msimu wa mvua unapoanza. Ngitili hugawanywa katika sehemu

kadhaa: kila sehemu ya ngitili lazima itumike yote kwa malisho kabla

ya kuhamia sehemu nyingine. Hifadhi za kifamilia au za mtu mmoja

4