programu ya hifadhi ardhi shinyanga (hashi) - Equator Initiative
programu ya hifadhi ardhi shinyanga (hashi) - Equator Initiative
programu ya hifadhi ardhi shinyanga (hashi) - Equator Initiative
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
Empowered lives.

Resilient nations.

PROGRAMU YA

HIFADHI ARDHI

SHINYANGA (HASHI)

Tanzania

Miradi ya Equator

Wanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii
MIRADI YA UNDP EQUATOR

Kote duniani, jamiii zinazidi kubuni mbinu zinazonuiwa kuyakidhi mahitaji yao ya kila siku na ya kimazingira. Kuna kazi

chache ambazo zimechapishwa za kuelezea kinagaubaga hizo mbinu bunifu na vile zilianzishwa,vile ziliathiri wakaaji wa

sehemu mbali mbali na vile zimekuwa zikibadilika pindi wakati unapotita. Wachache wamejitokeza kuelezea wazi wazi juu

ya miradi yao, na hata wale ambao wamefanya hivyo ni wakuu wa vijiji ambao wamefanya kuelezea kufaulu kwao.

Mradi huu wa Equator Katika unadhamiria kujaza hili pengo kama njia moja ya kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa

kwake. Masimulizi juu ya huu mradi ni baadhi tu ya mingi ambayo imefaulu na kushinda tuzo za Equator baada ya kukaguliwa

na kutathiminiwa katika kitengo cha makundi ya kijamii yanayo hifadhi mazingira na kuinua maisha ya wanafijiji. Miradi hii

inakusudiwa kuwa mifano ya kuiwa na kuwatia shime kuzungumzia ilivyofaulu ili kuhamasisha ulimwengu juu ya uhifadhi

wa mazingira.

Bonyeza katika ramani ya miradi ya Equator ili upate kupata habari zaidi

Wahariri

Mhariri Mkuu :

Muhariri Meneja :

Wahariri Waliochangia :

Joseph Corcoran

Oliver Hughes

Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Erin Lewis, Whitney Wilding

Wahandishi Waliochangia

Edayatu Abieodun Lamptey, Erin Atwell, Toni Blackman, Jonathan Clay, Joseph Corcoran, Larissa Currado, Sarah Gordon, Oliver Hughes,

Wen-Juan Jiang, Sonal Kanabar, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Rachael Lader, Patrick Lee, Erin Lewis, Jona Liebl, Mengning Ma,

Mary McGraw, Gabriele Orlandi, Juliana Quaresma, Peter Schecter, Martin Sommerschuh, Whitney Wilding, Luna Wu

Uchoraji

Oliver Hughes, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Amy Korngiebel, Kimberly Koserowski, Erin Lewis, John Mulqueen, Lorena de la Parra,

Brandon Payne, Mariajosé Satizábal G.

Shukrani

Equator ingependa kuwashukuru wanachama wa Programu ya Hifadhi Ardhi Shinyanga (HASHI). Picha zote ni za HASHI na Charlie Pye-

Smith, World Agroforestry Centre. Ramani ni za CIA World Factbook na Wikipedia. Masimulizi juu ya mradi huu yalitafsiriwa kwa Kiswahili

na Dr. Ken Ramani.

Nukuu ziada

United Nations Development Programme. 2012. Shinyanga Soil Conservation Programme (HASHI), Tanzania. Equator Initiative Case Study

Series. New York, NY.
PROGRAMU YA HIFADHI ARDHI

SHINYANGA (HASHI)

Tanzania

MAELEZO KUHUSU MRADI HUU

Programu ya Hifadhi Ardhi Shinyanga inafahamika

zaidi kwa Kiswahili kwa kifupi cha HASHI (Hifadhi Ardhi

Shinyanga) iliyodumu kutoka mwaka 1986 hadi 2004 ikiwa

na lengo la kurejesha rutuba ya ardhi iliyoharibika ya mkoa

wa Shinyanga ulioko kaskazini magharibi mwa Tanzania;

mkoa ambao ulipewa jina la “Jangwa la Tanzania” na Rais

wa wakati huo Julius Nyerere katikati ya miaka ya 1980.

Mkoa huu ambao ni ukanda wa miombo umeharibiwa kwa

miongo kadhaa kwa kukata na kuchoma misitu (kwa ajili

ya kutokomeza mbung’o) na kulazimishwa makazi mapya

chini ya mpango wa taifa wa kuanzisha vijiji Tanzania.

Jitihada hizi zilifanywa kwa ushirikiano wa pamoja kati

ya serikali na washirika wa kimataifa, lakini hata hivyo ni

muhimu kutambua kuwa upandaji miti katika eneo hilo

lazima ushirikishe wanajamii ili wawe mstari wa mbele

katika juhudi hizi. Mfumo wa jadi wa kuishi pamoja kwenye

eneo moja, au ngitili ulianzishwa, na wasukuma ambao

ni wakulima na wafugaji walipewa jukumu la kuhifadhi

maeneo ya misitu. Matokeo ni kwamba hadi mwaka 2004,

angalau hekta 350,000 za ngitili zilikuwa zimerejeshwa au

kuanzishwa katika vijiji 833 kwa mkoa mzima.

MUHTASARI

ULISHINDA TUZO YA EQUATOR: Mwaka 2002

ULIANZISHWA: Mwaka 1986

ENEO: Shinyanga kaskazini magharibi mwa Tanzania

WANAOFAIDIKA: 833 villages

MAZINGIRA: 145 bird species, 152 tree and shrub species

YALIYOMO

Historia na Mandhari 4

Majukumu Makuu na Ubunifu 6

Matokeo ya Kimazingira 8

Matokeo ya Kijamii 8

Matokeo ya Kisera 10

Jinsi ya Kudumisha Mradi Huu 12

Wahisani 13

3
Historia na Mandhari

Ukiwa unapatikana upande wa kusini mwa ziwa Victoria, mkoa wa

Shinyanga upo kaskazini magharibi mwa Tanzania na eneo lake

kubwa ni la mazingira ya ukame ukiwa na wakazi karibu milioni

tatu, kwa wastani wa watu 42 kwa kila kilometa ya mraba. Shinyanga

ni moja ya mikoa ya Tanzania maskini zaidi, wenye vilima vya kimo

cha chini na tambarare zenye kipindi kirefu cha kiangazi ukiwa

na wastani wa milimeta 700 za mvua kwa mwaka. Kabila kubwa

la mkoa huu ni Wasukuma ambao hujishughulisha na ufugaji na

kilimo; mazao makubwa wanayozalisha ni mahindi, mtama, uwele,

mihogo, pamba, na mchele. Zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wa mkoa

huu wanamiliki na kuendeleza mifugo kwenye malisho ya jamii zao.

Kati ya mwaka 1986 na 2004, mkoa wa Shinyanga ulianzisha Mpango

wa Hifadhi Ardhi Shinyanga uliofahamika kwa kifupi kama HASHI

(Hifadhi Ardhi Shinyanga). HASHI ilianzishwa na Rais Julius Nyerere

baada ya kutembelea mkoa huo mwaka 1984 na akashtushwa na

kiwango kikubwa cha ukataji miti. Kwa miaka ya 1980, Shinyanga

ilikuwa inajulikana kama ‘Jangwa la Tanzania ‘. Miongo kadhaa ya

usimamizi mbovu wa ardhi ilichangia kuendelea kuharibika kwa

mazingira katika mkoa wa Shinyanga, lakini mwanzo mkuu wa

uharibifu huu ni mpango wa kukata misitu kipindi cha kabla ya vita vya

pili vya dunia. Hapo awali, mkoa wa Shinyanga ulikuwa umefunikwa

na uoto wa miombo na mshita, ambayo ilitoa lishe kwa mifugo na

mafuta kwaajili ya kilimo na ufugaji kwa wasukuma. Hata hivyo

misitu hii ilikuwa pia hifadhi ya mbun’go, na magonjwa ya vimelea,

na malale ambayo yaliwashambulia binadamu na wanyama. Katika

miaka ya 1920, mamlaka ya kikoloni ilibuni mpango wa kuwalipa

wenyeji kwa kukata miti kwenye maeneo makubwa ya miombo. Hii

kwa kiasi kikubwa ilisaidia mafanikio katika kutokomeza Mbun’go,

na pia kuanzisha maeneo mapya ya malisho kwa ajili ya wasukuma,

lakini kwa upande mwingine ikaathiri uzuri wa mazingira ya mkoa.

Kadiri idadi ya mifugo na binadamu ilivyoongezeka katika nusu ya

mwisho ya karne ya ishirini, mahitaji kwa ajili ya kuni na kilimo pia

yaliongezeka. Hii ilisababisha ufugaji uliokithiri kwenye malisho na

mapori, wakati maeneo makubwa ya ardhi yalikuwa kwa ajili kilimo

cha mazao ya biashara kama vile pamba na tumbaku, na kuacha

ardhi kidogo kwa ajili ya kupanda mazao ya chakula. Zaidi ya hayo,

mpango wa uanzishwaji wa vijiji wa Rais Nyerere wa miaka 1970

ulilazimisha familia nyingi kuyaacha makazi yao kuhamia maeneo

mapya.

Kupotea kwa mfumo wa kijadi wa usimamizi wa rasilimali

Hali hizi zilisababisha mmomonyoko wa mfumo wa kijadi wa

usimamizi wa ardhi ambao wasukuma walitumia kuhifadhi

chakula cha mifugokwaajili ya msimu wa kiangazi. Mfumo huu

unaofahamika kama ngitili ulijumuisha utengaji wa maeneo

maalumu ya kuhifadhi nyasi za mifugo kwa ajili ya matumizi ya

kifamilia au ya jamii kwa kuyaacha maeneo yakiwa na nyasi mpaka

msimu wa mvua unapoanza. Ngitili hugawanywa katika sehemu

kadhaa: kila sehemu ya ngitili lazima itumike yote kwa malisho kabla

ya kuhamia sehemu nyingine. Hifadhi za kifamilia au za mtu mmoja

4
mmoja huanzishwa kwenye ardhi binafsi; maeneo ya hifadhi ya jamii

nzima hutengwa kutoka kwenye maeneo yanayofaa kwa malisho

ya wakati wa kiangazi.Ngitili kwaajili ya jamii nzima mara nyingi

hupatikana kandokando ya mito na kwenye vilima. Chini ya mfumo

wa usimamizi wa kijadi wa umiliki ardhi, umiliki wa ngitili na ardhi

katika mkoa wa Shinyanga ulisimamiwa na sheria ndogo za serikali

za mitaa. Uanzishwaji wa vijiji na sheria ya vijiji vya ujamaa ya mwaka

1975 ilimaanisha kuwa mali zote za kifamilia kama vile nyumba,

mashamba na ngitili viliachwa na wanakaya kuhamia kwenye makazi

ya pamoja. Mfumo mpya wa vijiji, ingawa ulikuwa na manufaa

kiutawala, ulisababisha ugumu wa kuendeleza utaratibu wa kijadi

wa kuhifadhi mazingira.Hali hizi ziliendelea kuathirika kwa sababu

ya kuongezeka kwa idadi ya watu na upanuzi wa maeneo ya kilimo.

Matokeo yake ni kwamba mambo haya yalisababisha kujitokeza

kwa changamoto mbili: uharibifu wa haraka wa ardhi, na ukosefu wa

kuni kwaajili ya nishati. Kaya nyingi zililazimika kusafiri umbali mrefu

zaidi ya kilometa kumi kwaajili kukusanya kuni, jukumu linalofanywa

na wanawake.

HASHI: urithi wa kudumu Shinyanga

Kwa miaka ya 1980 hekta 600 za ngitili zilikuwa zimehifadhiwa. Kuanzia

1986, Hifadhi Ardhi Shinyanga ikahuisha mfumo huu kwa lengo

la kuendeleza uhifadhi wa uoto wa maeneo yaliyotengwa. Mpaka

mwaka 2004, inakadiriwa kuwa hekta 350,000 za ngitili, zikiwemo

hifadhi binafsi za miti, zilikuwa zimehifadhiwa au kuanzishwa katika

vijiji 833 yenye idadi ya watu milioni 2.8.Programu iliendeshwa na

kufadhiliwa na serikali ya Tanzania, na kwa muda mrefu ikisaidiwa

na Mfuko wa Ushirikiano Maendeleo wa Norway (NORAD) na Kituo

cha Kimataifa cha Kilimo cha Misitu (ICRAF). Mafanikio makubwa ya

programu yalitokana na uelewa mzuri kuhusu maswala ya mazingira

wa jamii ya watu wa mkoa huu, wasukuma, ambao ni wafugaji na

wakulima.

Kwa mwaka 2004, programu hii ilirithiwa na Kituo cha Usimamizi

wa Rasilimali za Misitu ya Asili na Kilimo cha Misitu (NAFRAC), lakini

mfumo wa ngitili bado unaendelea. Kwa sasa ngitili zinakadiriwa

kuchukua eneo la ukubwa wa hekta 500,000

Faida za uhifadhi wa mfumo wa ekolojia zilizotokana na mradi

wa HASHI ni pamoja na ongezeko la kipato cha kaya kitokanacho

na kilimo na ufugaji, lishe bora, na uhakika wa maisha kwenye

familia ndani ya mkoa. Pia bayoanuai imenufaika na mradi huu

kwa kuongezeka idadi ya miti, vichaka, nyasi, na aina mbalimbali za

mitishamba, pamoja na ndege na spishi kadhaa za wanyama. Aina

mbalimbali za mitishamba zimevunwa na kuuzwa kwa wenyeji kwa

ajili ya kutengeneza dawa. Wakulima wamenufaika pia na kilimo cha

misitu kwa njia mbalimbali kama vile upandaji wa mimea ya mfumo

wa kinaitrojeni iliyosaidia kuongezaa tija katika kilimo. Mradi wa

HASHI na washirika wake wa kimataifa wameweza kutoa mafunzo

kwa walimu zaidi ya 150 kwaajili ya kusambaza uelewa kuhusu

maswala ya mazingira kwenye shule za ndani ya mkoa.

5
Majukumu Makuu na Ubunifu

Kabla ya kuanzishwa kwa HASHI, jitihada za kupanda miti

zilizoanzishwa na serikali ya Tanzania na mashirika ya kimaendeleo

kama vile Benki ya Dunia zilishindwa kwa kiasi kikubwa kuzuia

upotevu wa uoto wa misitu katika mkoa wa Shinyanga. Mkabala wa

mradi wa HASHI ulitofautiana na jitihada zilizotangulia kwa kufanya

kazi karibu zaidi na wenyeji, kwanza kwa kubainisha maeneo

yaliyohitaji kupewa umuhimu zaidi wa uhifadhi, na kuyahifadhi kwa

kutumia mbinu za kijadi. Maofisa misitu walioajiriwa na Idara ya

Misitu na Nyuki ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii walifanya kazi

kwa ukaribu sana na wafanyakazi wa wilaya na wa serikali za vijiji

Kuunganisha maarifa ya jadi na msaada wa kimataifa

Mafanikio ya awali ya mradi yalichangiwa sana na msaada wa kifedha

na kiufundi kutoka nje. Hadi mwaka 1987 HASHI ilikuwa inafanya

kazi kikamilifu, na mwaka 1989 iliweza kuvutia ufadhili wa Shirika la

Ushirikiano wa Maendeleo la Norway (NORAD).

Mwongozo wa kiufundi na mawasiliano ulitolewa Kituo cha Utafiti

wa Kilimo cha Misitu (ICRAF) kilichopo Nairobi, ambacho tangu

mwaka 2002 kinajulikana kama Kituo cha Kimataifa cha Kilimo cha

Misitu. Tafiti za ICRAF zinaonyesha mbinu sahihi za usimamizi wa

uoto na malisho, na kuonyesha mchango wa maarifa ya kijadi na

njia za kienyeji kama vile ngitili katika usimamizi wa ardhi wenye

mafanikio.

Malengo ya awali ya mradi

Katika hatua za awali, mradi ulihusisha shughuli za upandaji miti

na uhamasishaji kuhusu uelewa wa maswala ya mazingira. Katika

vijiji vingi, maofisa misitu wa HASHI walitumia mbegu za miti ya

asili na vipingili vya mizizi kwa kuhifadhi maeneo kwa ajili ya ngitili.

Mahali pengine, upandaji wa miti mipya (miti ya kigeni, na aina za

miti ya asili inayopendelewa na wenyeji) ulifanyika, hasa kuzunguka

maeneo ya karibu na nyumba.

Baadhi ya ngitili zilikuwepo hata kabla ya mpango wa uanzishwaji wa

vijiji, wakati ngitili nyingine zilianzishwa na wakulima na wanakijiji.

Mbali na kuhifadhi ngitili, wanakijiji walihamasishwa kupanda

mti kuzunguka nyumba zao (hasa miti ya matunda na kivuli), miti

kwaajili ya kuonyesha mipaka ya maeneo na mashamba. Hii ilisaidia

kuongeza rutuba na kutoa kuni, na ilisaidia pia kuonyesha mipaka

ya wakulima na kuhalalisha umiliki wa ardhi ndani ya kijiji.

Uelewa kuhusu mazingira uliongezeka na wanakijiji waliwezeshwa

kwa njia mbalimbali. Njia hizi ni pamoja na video, uigizaji, nyaraka,

na makongamano kwa ajili ya kuonyesha uhusiano baina ya uhifadhi

wa ardhi, uhifadhi wa misitu, na uhakika wa maisha.

Mbinu shirikishi ya tathmini vijijini ilisaidia wanavijiji kubainisha

matatizo kuhusiana na maliasili zao na kukubaliana kuhusu mbinu za

utatuzi. Wakulima na wanavijiji walipata mafunzo juu ya namna bora

ya kusimamia ngitili zao. Mathalani, wataalamu wa HASHI na ICRAF

walitoa ushauri kuhusu aina za miti ya kienyeji zilizofaa kuboresha

ardhi ya wakulima au mimea inayofaa kwa mipaka imara.

Ukuaji wa Biashara na mipango

Jamii za vijijini zikiwa zimejitosheleza kimaarifa na kushiriki vya

kutosha katika kuhuisha maarifa ya jadi, wanavijiji katika mkoa

mzima wa Shinyanga walipanua uwigo wa matumizi ya ngitili kutoka

kwenye uhifadhi wa ardhi na nyasi za mifugo hadi kuwa hifadhi

ya maeneo ya miti kwa ajili ya bidhaa mbalimbali za miti, nyasi za

mifugo, kuni, mitishamba, miti ya matunda, asali, wadudu waliwao,

vyote hivyo vimeongeza uhakika wa maisha wakati wa majira ya

ukame. Upanuzi wa matumizi wa ngitili huenda ulisaidia kuongeza

mvuto wake na kiwango cha kukubalika pia kiliongezeka.Wakati

jitihada za kuhifadhi ziliongezeka kidogokidogo siku za mwanzoni,

jitihada hizo za uhifadhi zilipanuka kwa kasi kwenye mkoa mzima

kwenye miaka ya 1990.

6
Upandaji miti uliojikita katika uwezo wa wanavijiji na

taasisi

Kusambaa kwa mafanikio ya mkabala wa HASHI kuliletwa na

kiwango chake kikubwa cha kuwawezesha wananchi katika ngazi za

vijiji, tofauti na programu nyingine za maendeleo ya vijiji ya miaka ya

1980. Matumizi ya ngitili kama nyenzo ya kuhifadhi, na kushirikisha

taasisi za kijadi za wasukuma na serikali za vijiji kusimamia uhifadhi

vilichangia sana mafanikio haya. Serikali za vijiji zilizochaguliwa

zilisimamia ngitili za kijumuiya, na kuwa kama mpatanishi wa

mwisho wa migogoro ya umiliki wa ngitili binafsi, wakati kiutendaji,

taasisi za kijadi zilikuwa na majukumu sawa katika vijiji vilivyo vingi.

Mathalani, kila kijiji kiliweka sheria zake za uhifadhi wa ngitili na

usimamizi wake, vijiji vingi vilitumia pia askari wa kijadi yaani

sungusungu na mikutano ya pamoja inayofahamika kama Dagashida

kwaajili ya kutekeleza maamuzi ya uhifadhi. Dagashida huongozwa

wazee wa kimila wa kisukuma, na huamua ni adhabu zipi zitolewe

kwa yeyote anayekiuka taratibu za uhifadhi wa ngitili, kwa mfano

kulisha mifugo kwenye eneo lililotengwa kwa ajili kuotesha.

Kanuni zinazosimamia uhifadhi wa ngitili ni pamoja kutoza faini

(mchenya). Katika kijiji kimoja, wachungaji wanaokamatwa

kuchunga kimakosa katika ngitili wanatozwa shilingi za kitanzania

20,000 (kama dola 14 za kimarekani). Kila adhabu inayofanana na

hiyo kwa wanaokata miti kwenye ngitili. Kwa makosa makubwa,

kama vile kuchoma moto uoto wa maeneo yaliyotengwa, wafugaji

hutozwa ng’ombe mzima aliye hai, ambaye baadaye huchinjwa.

Kama migogoro haitaweza kuamuliwa na Dagashida, basi hupelekwa

katika mahakama za chini na za wilaya kwa ajili ya maamuzi.

Ingawa uanzishwaji wa ngitili haukuwa wa kidemokrasia kwa kila

kijiji, mwelekeo wa jumla ulikuwa kuongezeka kwa uwajibikaji wa

taasisi hizo za kijadi. Maofisa misitu wa HASHI walijitahidi kuzipa

nguvu serikali na taasisi za kijadi kwa kutumia sheria ya Ardhi ya Vijiji

ya mwaka 1999 iliyoruhusu serikali za vijiji kupitisha sheria ndogo

zilizosaidia kuhifadhi ngitili. Sheria hizo ndogo, zikishapitishwa

katika ngazi ya wilaya, zilitambulika na serikali ya kitaifa.

7
Matokeo

MATOKEO YA KIMAZINGIRA

Kuongezeka kwa bayoanuwai halikuwa lengo kuu la programu ya

Uhifadhi wa Ardhi Shinyanga, bali msisitizo ulikuwa kuongezeka

kwa tija ya kilimo katika mkoa mzima. Hata hivyo, urejeshaji wa

bidhaa na huduma zitokanazo na maeneo yenye miti hufanywa kwa

njia ya kuruhusu mimea kukua na kupanda miti ya kienyeji imesaidia

kurejea kwa aina mbalimbali za miti, majani na mitishamba. Baadhi

ya aina za wanyama zimeanza kurejea katika eneo husika.

Kiwango cha urejeshaji miti kwenye maeneo tengefu

Kwa mwaka 1986, kiasi cha hekta 600 za ngitili zilijulikana kuwepo

mkoani Shinyanga. Utafiti kwa vijiji 172 kama sampuli ndani ya

kipindi cha miaka ya 1990 ulionyesha kulikuwepo na ngitili 18,607

(284 za jumuiya, na zilizobaki zikimilikiwa na kaya) zikichukua eneo

la hekta 78,122. Kwa kuzingatia sampuli hii, mameneja wa mradi

wa HASHI walikadiria kuwa zaidi ya hekta 350,000 zilitumika kama

ngitili, na wakazi tisa kati ya kumi kwa kila kijiji kwa jumla ya vijiji 833

vya mkoa wa Shinyanga wanafurahia bidha na huduma zitokanazo

na uhifadhi wa ngitili

Historia ya hivi karibuni kuhusu mradi uliosimamiwa na kituo cha

kimataifa cha kilimo cha misitu inadai kuwa kiwango cha ngitili

kimepunguzwa kwenye taarifa rasmi, inawezekana kuwa kuna zaidi

ya hekta 500,000 za ardhi zilizotengwa.

Karibu asilimia 60 za ngitili zinamilikiwa na watu binafsi, na zilizobaki

zikimilikiwa na serikali za vijiji au taasisi kama vile shule, asasi

za kijamii, makanisa, na misikiti. Inakadiriwa kuwa asilimia 90 ya

wafugaji, na asilimia 50 ya wakulima wanamiliki ngitili zao wenyewe.

Zinatofautiana kwa viwango vya ukubwa na umri.

Kwa upande wa mashariki wa mkoa, eneo lenye mvua kidogo,

ngitili za hekta 500 ni kawaida kuwepo, lakini hupatikana kwa wingi

maeneo ya kati ya mkoa na maeneo ya magharibi ambako kuna

mvua ya kutosha, zinaweza kuwa za ukubwa wa chekta chache. Kwa

mwaka 2003, maeneo yaliyotengwa kwaajili ya jumuiya ni ya wastani

wa hekta 164, wakati maeneo binafsi yana wastani wa hekta 2.3.

Kuimarika kwa mimea na wanyama

Mradi umesaidia kuwepo kwa jumla ya aina 152 za miti na vichaka,

hasa kwa njia ya uhifadhi wa miti michanga kwenye ngitili ambazo

hapo awali yalikuwa maeneo ambayo yalikuwa hayana miti. Zaidi

ya aina 60 za miti zimetumika na wenyeji kwa malengo tofauti,

kama vile dawa za mitishamba, matunda na mbogamboga, nishati,

mbao, ususi, malisho, uzio, na kuezeka. Aina kumi na tatu za nyasi na

ishirini na tano za mitishamba zinapatikana kwenye maeneo ya uoto

yaliyohifadhiwa. Ngitili za jumuiya zinasaidia kuhifadhi maeneo ya

vilima na pembezoni mwa mito, kuzuia mmomonyoko wa udongo,

na kuhifadhi vyanzo vya maji.

Wanyama,kwa hali fulani, wamerejea katika baadhi ya maeneo,

hususani ndege kufuatia kuimarika kwa miombo na migunga.

Jumla ya spishi 145 za ndege zinapatikana Shinyanga ambazo

hapo awali zilitoweka au ilikuwa nadra kuwepo, zikiwemo aina saba

ambazo hupatikana katika maeneo maalumu. Fisi na wanyama

wengine kama vile nguruwe pori, sungura, nk. sasa wanapatikana

kama kawaida kiasi kwamba kumekuwepo na migogoro kati ya

wanyama na binadamu. Kwa ujumla, mbali na uharibifu unaoletwa

na wanyama unaokadiriwa kuwa ni hasara ya dola 63 za kimarekani

kwa kila familia, kwa mwaka kwa kipindi cha 2004, faida za kiuchumi

za kuwepo kwa ngitili katika vijiji vingi zinazidi hasara hiyo.

MATOKEO YA KIJAMII

i. Faida za kukadiriwa: Faida za kiuchumi na kijamii za hifadhi ya

uoto wa ngitili zilikadiriwa mwaka 2004 na kikosi kazi cha watu kumi

kilichowekwa na serikali ya Tanzania na Shirika la Kimataifa la Hifadhi

ya Mazingira, kilichokusanya taarifa za utafiti za kisoko kwa kaya 240

kwa vijiji 12 na uchambuzi mwingine wa data kwa ajili ya kupima

athari chanya za HASHI. Utafiti huu ulikadiria thamani ya pesa

kutokana na ngitili kuwa ni dola za kimarekani 14 kwa mwezi kwa

kila mtu. Hiki ni kiwango kikubwa kwa mtanzania ukizingatia kuwa

kipato cha chini kwa mtanzania wa kijijini ni dola za kimarekani 8.50

kwa mtu mmoja kwa mwezi kwa mwaka 2004.

8
Wastani wa thamani ya rasilimali muhimu 16 zilizovunwa

kutokana na ngitili kwa wilaya ya Bukombe (Monela na

wenzake, IUCN, 2004)

Kwa kaya Dola 1,190

Kwa kijiji Dola 700,000

Kwa wilaya Dola milioni 89.6

Punguzo la muda wa kutafuta rasilimali (Monela na

wenzake, IUCN, 2004)

Kuni

Nguzo

Ezeko

Maji

Malisho

Asilimia za kaya kwa wilaya saba za mkoa wa Sinyanga

zinazotumia bidhaa za ngitili (Monela na wenzake, IUCN,

2004)

Kubadili lishe 22%

Kutoa malisho kwa wanyama 21%

Upatikanaji wa mitishamba 14%

Upatikanaji wa kuni 61%

Kulipia elimu ya watoto 36%

Chanzo: Monela et al, IUCN, 2004.

Saa 2-6 kwa siku

Saa 1-5 kwa uvunaji

Saa 1-6 kwa uvunaji

Saa 1-2 kwa siku

Saa 3-6 kwa uvunaji

Thamani hizi za kipesa zimetokana na matumizi mbalimbali ya

bidhaa zilizovunwa na kila kaya kutoka kwenye ngitili. Kati ya bidhaa

16 za maliasili zinazotokana na ngitili; kuni, mbao na mitishamba

ndizo zilizoonekana kuwa na umuhimu mkubwa kiuchumi kwa

kaya. Mazao mengine yenye umuhimu ni kama vile malisho, nyasi za

kuezekea, nyama pori, matunda, mboga na asali.

ii. Sifa za kuelezeka – kuimarika kwa maisha: Kwa vijiji vilivyofanyiwa

utafiti, zaidi ya asilimia 64 ya kaya zote zilisema kuwa zilikuwa na

hali nzuri kutokana na faida za ngitili. Kikosi kazi kilichoongozwa na

Profesa Monela wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Tanzania,

kilihitimisha kwamba uhifadhi wa ngitili ulidhirisha umuhimu wa

rasilimali miti kwa uchumi wa wananchi wa kawaida na kuwa chanzo

muhimu cha kiuchumi kama nyongeza kwa kilimo kwa maisha ya

wananchi wa Shinyanga.Utafiti ulionyesha pia faida zinazohusiana

na uongezaji wa kipato. Kuendeleza ngitili kumewawezesha

wanakijiji kulipa karo za shule, kununua zana mpya za kilimo, na

kuajiri vibarua kwenye shughuli za kilimo, hasa kutoka na mauzo ya

mbao na bidhaa nyingine za miti. Kipato kilichotokana na ngitili za

jumuiya kimetumika kujenga madarasa, ofisi za kijiji, na vituo vya

afya.

Ngitili binafsi zimechangia pia kuongeza thamani ya ardhi ya

mkulima. Mwelekeo wa kuongezeka kwa maeneo yaliyotengwa

kunaweza kuashiria mabadiliko kutoka kwenye umiliki wa kijumuiya

had umiliki binafsi ndani ya mkoa wa Sinyanga.

Upatikanaji wa matunda, mboga na wadudu waliwao umeweza

kuchangia kuimarika kwa afya za watu, huku upatikanaji wa nyasi

za kuezekea ukisaidia kuboresha makazi. Kupanda kwa tabaka la

maji kulikotokana na uhifadhi wa maeneo kumesaidia upatikanaji

wa maji. Uuzwaji wa dawa za kienyeji umesaidia pia kuimarika kwa

uhakika wa maisha. Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Heidelberg,

Ujerumani walifanya kazi na watafiti wa HASHI na kugundua

matumizi ishirini ya dawa za mitishamba. Waganga wa kienyeji

wa Shinyanga wanawakilisha mfumo wa tiba asilia katika vijiji vya

Tanzania, lakini hata hivyo uvunaji wa mitishamba umechangia

uharibifu wa hifadhi za miti. Umoja wa waganga wa jadi 32 umesifu

mradi wa HASHI kwa kutunza mazingira ambayo huweza kuwapatia

miti ya dawa.

Wanakiji, hasa wanawake, wana uwezo wa kuokoa muda kwa

kutotembea umbali mrefu kutafuta kuni, malisho na majani ya

kuezekea. Hii inawapa nafasi wanaume na wanawake kutumia muda

mwingi kufanya shughuli za kiuchumi, na wakati huohuo kuweza

kulea watoto.

Ngitili zimesaidia kupunguza kero ya kusafiri umbali mrefu kwa

wafugaji na wakulima kwa ajili ya kutafuta malisho wakati wa

kiangazi. Hii imesadia kupunguza wizi wa mifugo na magonjwa.

Maeneo binafsi yaliyotengwa yanasaidia pia kupunguza athari

za vipindi vya ukame, na hivyo kurudi katika hali ya kawaida kwa

haraka.

Mafanikio endelevu ya majaribio ya HASHI yamesaidia kupandisha

hadhi na umuhimu wa serikali za vijiji na mamlaka ya kijadi kwa

wasukuma. Ushushaji wa madaraka kwa ngazi za chini za vijiji

9
Thamani ya bidhaa za ngitili zilizotumika na kaya za wilaya ya Bukombe 2004 (Monela na wenzake, IUCN, 2004)

Bidhaa za ngitili

% ya kaya zinazotumia bidhaa hizi

kwa vijiji vya utafiti

wastani wa kipato cha kaya kwa dola za

kimarekani

Mbao 59 71.74

Kuni 64 13.09

Nguzo 29 2.87

miti ya hifadhi za maji 36 8.97

Maji 21 34.04

Asali 14 2.39

Nyama pori 7 0.72

Wadudu waliawao 36 0.48

Uyoga 36 2.87

Mitishamba 7 10.76

Nyasi za kuezekea 36 2.15

Malisho 7 1.15

Mboga 29 2.15

Matunda 43 2.87

Useramala 14 1,021.60

Ufinyanzi 7 12.91

Jumla ya thamani ya kiuchumi kwa kila kaya kwa

mwaka

Dola za Kimarekani 1,190.77

Chanzo: Monela et al, IUCN, 2004.

umekuwa moja ya sababu muhimu za mafanikio ya HASHI. Kwa

muda mrefu, hii imesaidia kutambuliwa kwa umuhimu wa taasisi za

kijadi na madaraka ya vijiji katika usimamizi endelevu wa maliasili.

Kijiji cha Wigelekeko :utafiti

Kijiji cha Wigeleko kilichopo wilaya ya Maswa mkoani Shinyanga ni

mfano wa mafanikio ya uhifadhi wa ngitili. Miaka ya kati ya 1980,

ulishaji wa malisho na usafishaji wa mashamba kwa ajili ya pamba

vilisababisha ukame na ukosefu wa bidhaa zitokanazo na miti,

majani na maji kwa kaya 408.

Kwa mwongozo wa HASHI, vijiji mwanzoni vilitenga jumla ya hekta

157 za ardhi iliyoharibika ya ngitili za jumuiya na binafsi. Ulishaji

mifugo na ukataji miti vilipigwa marufuku kwa miaka mitano, na

wanakijiji walilisha mifugo yao kwenye ngitili binafsi.

Marufuku ilipoisha, maeneo yaliyotengwa ya jumuiya yaliongezeka

kuwa na miti na vichaka. Serikali ya kijiji na maofisa misitu wa HASHI

walibuni mfumo rahisi wa usimamizi uliodhibiti utafutaji kuni kwa

kupunguza matawi na kudhibiti ulishaji mifugo kipindi cha kiangazi.

Wakulima waliruhusiwa kulima mazao katika maeneo madogo

madogo, lakini kukiwa na uzingatiaji wa kanuni za kuhifadhi ardhi.

Ulinzi wa ngitili za jumuiya ulifanywa na askari wa jadi maarufu kama

sungusungu na kwa kuzingatia sheria ndogo za vijiji.

Mwaka 1997, wanavijiji waliamua kupanua maeneo yaliyotengwa

kwa kuongeza hekta 20 kwa ajili ya kujenga mabwawa madogo ya

kuhifadhia maji kwa matumizi ya nyumbani na kunyweshea mifugo.

Kila kaya ilichangia dola nne kwa ajili ya kujenga bwawa ambalo

lilikamilika mwaka 1998. Mwaka mmoja baadaye, hifadhi ya maji

ilikuwa na maji muda wote na ilikadiriwa kuwa thamani yake ilifikia

dola za Kimarekani 26,500 kwa mwaka. Maji kwa ajili ya mifugo

yalichangia zaidi pato ambalo lilikadiriwa kufikia dola 92,000 kwa

mwaka kwa kuhudumia mifugo 1900. Mwaka 2000 uvuvi ulianzishwa

kwenye bwawa na hivyo kuchangia zaidi uhakika wa maisha. Kuna

umoja wa watumiaji maji wa kijiji cha Wigelekeko ambao husimamia

bwawa kwa idhini ya mkutano mkuu wa kijiji, na huuza maji kwa

watu wa nje.

Mwaka 2001, dola 250 zilizopatikana kutokana na mauzo zilitolewa

kwa ajili ya maendeleo ya kijamii. Ili kupunguza mahitaji makubwa

ya ngitili za jumuiya, theluthi mbili ya wanakijiji wamepanda miti

kwenye mashamba yao, kwa wastani wa miche 100 kwa hekta moja.

MATOKEO YA KISERA

Ukiwa ni mradi wa serikali ya Tanzania, majaribio ya HASHI

yalisaidia kujua kwa kina kuhusu dhima ya uhifadhi wa bayoanuwai

kama jambo la msingi katika kuhakikisha maisha yako salama na

kupunguza umaskini, na hiyo ndiyo jitihada ya msingi ya serikali ya

Tanzania katika kuleta maendeleo.

HASHI imekuwa ni kitu cha msingi kabla ya mabadiliko ya sera

nchini Tanzania ambayo imesaidia sana jamii ziweze kusimamia

maliasili. Mwaka 1998, Tanzania ilifanya mapitio ya sera ya misitu na

kuidhinisha, na sera imetilia mkazo zaidi katika usimamizi shirikishi

na ughatuzi.

10
Hii ilizingatia mipango ya usimamizi wa bayoanuwai kwa misitu

yenye matumizi mengi. Jamii pia zilihimizwa kushiriki katika

usimamizi wa misitu, kutenga maeneo yaliyoharibiwa ili yaweze

kusimamiwa. Hii ilikamilishwa kwa sheria ya Misitu ya mwaka 2002.

Umiliki wa ardhi: suala nyeti

Jambo lililokwamisha kupanuka kwa mfumo wa ngitili ni utata

kwenye sheria ya Tanzania kuhusu umiliki wa ardhi. Kukosekana

kwa uhakika wa miliki, au hisia kuwa hakuna uhakika na umiliki,

vilichangia kwa miaka ya 1990 kuwazuia watu binafsi kuendelea

kuwa na maeneo yaliyotengwa, na hali imeendelea kupunguza fursa

za miradi ya HASHI kupanuka katika mikoa mingine nchini. Ingawa

ngitili zilikuwa zimekubalika na kusajiliwa chini ya mradi wa HASHI,

umiliki wake bado hauko wazi katika sheria ya sasa ya Tanzania.

Vijiji kwa pamoja vina hati miliki kwa kupitia mipaka yake halali,

wakati kaya zikipata hati kwa maeneo yao wanayolima na umiliki

huo huridhiwa na mkutano wa kijiji. Sehemu ya ardhi ya kijiji iliyobaki

baada ya kuwagawia wakulima hubaki kama eneo la kijiji kwa ajili ya

matumizi ya kijumuiya chini ya usimamizi wa serikali ya kijiji.

Hii ardhi ambayo imetengwa kwa matumizi ya jumuiya inaweza

kutumika kama ngitili, lakini bado kigezo cha uchaguzi wa

matumizi ya hayo maeneo kuwa ngitili hakiko wazi kwenye sheria,

na kwahiyo ni haki ipi ya ardhi inayohusika. Jambo lililochangia

kukwamisha jitihada za uhifadhi ni kwa kusisitiza kuhusu maeneo

yaliyotengwa: serikali za vijiji na mikutano ya wanakijiji wanaogopa

kutangaza ngitili kama maeneo yaliyotengwa kwa kuogopa serikali

kuu kuyachukua na kubadili matumizi yake kwa kuyaweka chini ya

wilaya au kwa shughuli za kitaifa.

Maswala ya umiliki yanaweza kuingilia kati uanzishwaji wa ngitili

kwenye maeneo binafsi. Wamiliki binafsi wa ardhi wasio na hati

miliki za maeneo yao wamekuwa wakisita kuanzisha au kupanua

ngitili kwa kuhofia migogoro ndani ya jamii.

Kwa wakati mwingine, upimaji wa mipaka umesaidia kuwa na hati

miliki za jumuiya na watu binafsi zisizo na mashaka yoyote. Mbali na

hilo, kupanuka kwa mahitaji ya ardhi kutokana na kuongezeka kwa

watu na wanyama kumesababisha kuzuka kwa migogoro ya umiliki

ardhi na ugomvi kuhusu maeneo ya kulishia mifugo.

Sera ya Ardhi ya mwaka 1997 na Sheria ya Ardhi ya Kijiji ya Mwaka

1999 vimetoa mwelekeo utakaovisaidia vijiji kupata hati miliki za

vijiji, na watu binafsi kupata hati zao ndani ya eneo la kijiji, na hivyo

kusaidia uanzishwaji rasmi wa ngitili

Mabadiliko haya ya kisera yaliwezesha serikali za vijiji kupitisha sheria

ndogo kuzilinda ngitili zao kwa kutumia sheria za kijadi na walinzi

wa vijiji. Kuweka sheria maalumu ya kusimamia umiliki na haki ya

kutumia ardhi iliyotengwa kama ngitili za jumuiya na kuepusha

matatizo ya umiliki. Kuzitambua rasmi ngitili za kifamilia na binafsi

chini ya sheria ya Tanzania kama kundi maalumu la usimamizi wa

ardhi ambapo itakuwa rasmi kusambaza mfumo wa ngitili.

11
Jinsi ya Kudumisha Mradi Huu

JINSI YA KUDUMISHA MRADI HUU

Mradi wa HASHI uliisha mwaka 2004 na ukarithiwa na Kituo cha

Usimamizi wa Kilimo cha Misitu (NAFRAC), kilichopo Shinyanga.

Shughuli zake zimeendelezwa, ila kwa kuonyesha kiwango kikubwa

cha uendelevu, umiliki wa wenyeji, na uwezo uliojengwa kwa miaka

kumi na nane tangu mradi uanzishwe.

Wakati wa uhai wa mradi, jitihada kadhaa zilifanyika kupanua

shughuli zilizoanzishwa na wafanyakazi wa HASHI na watafiti kutoka

kituo cha kimataifa cha kilimo cha misitu. Matokeo yake mradi

uliwanufaisha makumi elfu ya familia za wakulima. Tangu mwaka

2004 wafanyakazi wa serikali za vijiji wameendelea kuhamasisha

kilimo cha misitu na usimamizi wa ardhi ulio endelevu. Katika wilaya

ya Shinyanga, wakulima wa mfano walibainishwa kwa kila kata na

kupewa ushauri wa kiufundi na vifaa. Tangu mwaka 1998, zaidi ya

walimu 150 wamepata mafunzo kwa ajili ya kuhamasisha maswala

ya mazingira kwenye shule, wakipata msaada toka kwa Ofisa Maliasili

wa Wilaya. Mikoa mingine miwili, Mwanza na Tabora walianza nao

kutekeleza mradi kama wa HASHI kwaajili ya kuhifadhi maliasili.

Moja ya sababu kuu ya kudumu kwa mfumo wa ngitili ni kwamba

unaendelea kutoa matunda ya kiuchumi kwa wakulima na wafugaji

ndani ya mkoa. Maeneo yenye miti yameonyesha kuwa na faida;

ngitili kwa malisho ya mifugo; na uanzishwaji wa teknolojia za kilimo

cha misitu kama vile kupandikiza matunda kumeongeza kipato

kwenye familia.

Nishati, kaboni na uhusiano na kilimo

Miradi mipya imesaidia kuimarisha uhifadhi na urejeshaji wa

misitu. Idara za serikali za vijiji zimehamasisha matumizi ya majiko

yanayotumia nishati kidogo. Hii imesaidia kupunguza mzigo wa

kutegemea sana maliasili za misitu, pamoja na kupunguza muda

ambao familia huupoteza kutafuta kuni. Kikundi cha wanawake cha

Upendo ni moja ya asasi za kijamii zinazohamasisha matumizi ya

majiko yasiyotumia nishati kubwa, kwa wanachama wake na kwa

wale wa vijiji vya jirani.

Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa kuna uwezekano kwa

hifadhi za miti za mkoa wa Shinyanga kuzalisha kaboni, na mradi

wa miaka minne unaosimamiwa na shirika la taifa la maendeleo

ya viwanda vya asili na mazingira (TaTEDO), kwa kushirikiana na

kampuni iitwayo Development Associates Ltd (DASS) ambayo hutoa

msaada wa kiufundi; na ambayo kwa sasa inatafiti jinsi ambavyo

jamii za vijijini zinavyoweza kunufaika na pesa zitakazotolewa

kupitia mradi wa kupunguza hewa ya ukaa itokanayo na ukataji miti

na uharibifu wa misitu (REDD+).

Pia Tanzania hivi karibuni ilizindua mkakati wake wa kuinua kilimo

nchini ujulikanao kama ‘Kilimo Kwanza’. Mkakati huu umelenga

kutenga pesa zaidi kwa ajili ya kilimo, kuhamasisha sekta binafsi

kuwekeza katika kilimo, na kuwa na matumizi ya sayansi na

teknolojia katika kubadili maeneo makame yaweze kufaa kwa kilimo.

Imependekezwa kuwa mradi huu utatumia sana majaribio ya HASHI,

kusaidia kuboresha na kusaidia zaidi maeneo makavu yanayotumika

kwa kilimo na ufugaji nchini Tanzania.

Changamoto za mazingira na kijamii

Kuna maswala kadhaa yanayoweza kukwamisha mafanikio yaliyopo,

ukuaji, na kupanuka kwa mfumo wa ngitili. Kubwa kati ya haya ni

ongezeko la idadi ya watu ambalo linatishia kuondoa mafanikio

yaliyofikiwa ya mradi wa HASHI.

Mwaka 1988, mkoa wa Shinyanga ulikuwa na wakazi milioni 1.77.

Mwaka 2002, idadi ya wakazi imefikia 2.8. Ongezeko la idadi ya

watu limekuwa likikua kwa asilimia 2.9 kwa mwaka na kukadiriwa

kuwa sasa hivi mkoa unakadiriwa kuwa na wakazi kama milioni 3

au asilimia 70 ya wakazi wameongezeka mkoani shinyanga tangu

mradi ulipoanza. Mifugo nayo imeongezeka kwa kiwango kikubwa.

12
Kwa muktadha huu, mafanikio ya HASHI yanaonekana kuwa ya

maana, lakini ongezeko la watu vijijini limesababisha matumizi

makubwa na uharibifu wa maeneo mengi ya ngitili. Changamoto hii

imefanya kuwa ngumu kwasababu ya kuzidi kwa migogoro kati ya

wanyama na binadamu, hasa kwa maswala ya uharibifu wa mazao.

Moja ya athari za ongezeko la idadi ya watu na ongezeko la

mahitaji ya ardhi ni ongezeko la mauzo yasiyodhibitiwa ya ngitili

zinazomilikiwa na watu binafsi. Kumekuwepo na mashauri kadhaa

ambapo akina baba wanagawiawa vijana wao wa kiume ngitili zao,

na hivyo kupunguza ukubwa na tija itokanayo na ngitili. Wakulima

wilayani Maswa, kwa mfano, waliripotiwa mwaka 2004 kupunguza

ukubwa wa ngitili zao binafsi na kulazimika kulishia mifugo ile

yenye mahitaji zaidi wakati wa msimu wa ukame. Mabadiliko haya

yanaweza kuathiri uwezo wa kaya na jamii kuendana na mabadiliko

ya hali ya hewa na changamoto nyingine za tabianchi.

WAHISANI

• Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania: chini ya rais Julius

Nyerere ilianzisha mradi mwaka 1986

• Shirika la Ushirikiano wa Mandeleo la Norway (NORAD): lilitoa

ufadhili wa muda mrefu kwa HASHI

• Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Kilimo cha Misitu (ICRAF):

kilitoa ushauri wa kiufundi na kisayansi na kuwasaidia maofisa

misitu wa HASHI

• Mamlaka za serikali za vijiji na wilaya

13
MAREJELEO YA ZIADA

• Ghazi, P., Barrow, E., Prof. Monela, G. and Mlenge, W. 2005. Regenerating Woodlands: Tanzania’s HASHI Project, in World Resources Report

2005, pp. 131-138. http://pdf.wri.org/wrr05_full_hires.pdf

• Barrow, E. and Mlenge, W. ‘Forest Restoration in Shinyanga, Tanzania’, in Fisher, R.J., Maginnis, S., Jackson, W.J., Barrow, E., and Jeanrenaud,

S. 2005. Poverty and Conservation: Landscapes, People and Power. IUCN, Gland, Switzerland, and Cambridge, UK. pp. 61-71. http://data.

iucn.org/dbtw-wpd/edocs/FR-LL-002.pdf

• Pye-Smith C. 2010. A Rural Revival in Tanzania: How agroforestry is helping farmers to restore the woodlands in Shinyanga Region. ICRAF

Trees for Change no. 7. Nairobi: World Agroforestry Centre. http://www.worldagroforestry.org/downloads/publications/PDFs/B16751.

PDF

• HASHI Soil Conservation Project video (Vimeo) http://vimeo.com/36989655

Masimulizi kuhusu miradi mingine, bonyeza hapa:

Equator Initiative

Environment and Energy Group

United Nations Development Programme (UNDP)

304 East 45th Street, 6th Floor

New York, NY 10017

Tel: +1 646 781-4023

www.equatorinitiative.org

Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ndio unaoendesha miradi ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa kote ulimwenguni

kwa kutoa mwito wa mageuzi na kuelekeza mataifa kwa maarifa, na malighafi ili kusaidia watu kujiimarisha kimaisha.

Mradi huu wa Equator huleta pamoja Umoja wa Mataifa , serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, wafanyibiashara na makundi ya

mashinani ili kutambua na kuimaliza maendeleo himili kwa watu na jamii kwa jumla.

©2012 Haki Zote ni za Mradi wa Equator