Kurejesha Hadhi ya Mwalimu I - Muhtasari.pdf - HakiElimu
Kurejesha Hadhi ya Mwalimu I - Muhtasari.pdf - HakiElimu
Kurejesha Hadhi ya Mwalimu I - Muhtasari.pdf - HakiElimu
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
HakiElimu

Muhtasari Na. 10.3K

Kurejesha Hadhi ya Mwalimu:

Matokeo ya Kujifunza, TDMS, na Bajeti ya mwaka 2010/11

Ufuatao ni muhtasari wa ripoti iliyoandiliwa na HakiElimu inayosisitiza baadhi ya programu katika Mkakati wa

Maendeleo na Menejimenti ya Ualimu (TDMS) ambazo hazijatekelezwa kutokana na ukosefu wa fedha, na inachangia

mawazo kuhusu namna fedha hizo zinavyoweza kutolewa. Kwa tarifa zaidi, soma ripoti kamili.

Kadiri maendeleo ya Tanzania yanavyosonga mbele

ndivyo ambavyo jukumu la kila raia katika mchakato

wa maendeleo hayo linavyozidi kuwa muhimu.

Tukiangalia familia, jamii na taifa tunaona namna

tunavyotegemeana kwa ajili ya mafanikio makubwa

kwa wote. Kwa kutumia juhudi za pamoja na zenye

mshikamano tunapata mafanikio mengi kuliko

ambavyo tungepata kama mtu mmoja mmoja.

Miongoni mwa zana muhimu ambazo raia wa serikali

ya uwakilishi wanaunda kufanikisha malengo yao ya

pamoja ni bajeti ya taifa. Bajeti ni mwongozo

unaosaidia kugeuza kwa ufanisi zaidi fedha kuwa

maendeleo katika utoaji wa huduma, kama vile maji

salama ya kunywa, huduma za afya za kuaminika

zaidi, na barabara bora zaidi.

Kama ambavyo bajeti inavyoweza kuwa na athari

kwa huduma za jamii kama vile maji, afya na

miundombinu, ina athari pia kwenye elimu. Athari

hizi si kwa maendeleo ya vitu kama shule

zinazojengwa, vitabu vilivyonunuliwa na mitihani

iliyotolewa tu. Athari hizo zinatafsiriwa katika

matokeo halisi yanayohitajika katika elimu—

matokeo ya kujifunza ambayo watoto, wanajamii na

raia wamepata uwezo wa kufikiria kwa makini,

kutanzua matatizo magumu zaidi na kupata

ufumbuzi wa kiubunifu kupeleka mbele maendeleo

ya jamii na taifa kwa ujumla.

Ufundi. Madhumni yake ni “kushughulikia mahitaji

yaliyopo ya walimu, na pia ukijaribu kushughulikia

changamoto zinazohusiana na ubora ikiwemo

taaluma ya ualimu, usimamizi na motisha.” Kwa

pamoja, TDMS ina malengo 13 ya kimkakati ikiwemo

“kuajiri na kuwabakiza kazini idadi ya kutosha ya

walimu na wakufunzi wenye ujuzi ili kumudu

ipasavyo ufundishaji wa shule za awali, shule za

msingi, shule za sekondari, elimu ya watu wazima na

elimu isiyo rasmi pamoja na Vyuo vya Ualimu.” Yote

yanalenga kuhakikisha kwamba kizazi kijacho cha

Tanzania kina walimu bora na elimu bora ili waweze

kuleta mabadiliko katika jamii zao na nchi yao.

Ingawa mkakati huu unashughulikia masuala mengi

yanayokera taaluma ya ualimu na matokeo ya

kujifunza, TDMS bado haijapata fedha za kutosha

katika bajeti ya taifa kuwezesha hata kiwango kidogo

cha utekelezaji wake.

Bajeti katika Sera ya TDMS

Sh. bil

146

Sh. bil

162

2009

2010

Bajeti Halisi ya TDMS

Sh. bil

25

Sh. bil

50

Ufuatano ni uchambuzi wa namna ya kuboresha

matokeo haya ya kujifunza kwa kurekebisha baadhi

ya taratibu za bajeti. Ufumbuzi muhimu

uliobainishwa ni:

Sh. bil

172

2011

Sh. bil

28

1) Kuwapa motisha walimu waliopangwa

kufundisha shule za pembezoni.

2) Kuwapandisha daraja walimu wa shule

za sekondari wenye leseni na wale wasio

na taaluma.

3) Kuwahakikishia fursa za kuendelea

kitaaluma kwa njia ya mafunzo ya

kujiendeleza kazini.

TDMS ni Nini?

Kwa bahati nzuri Tanzania tayari inao mkakati wa

kushughulikia mambo haya ambao ni TDMS au

Mkakati wa Maendeleo na Menejimenti ya Ualimu.

TDMS ni mpango wa miaka mitano uliopitishwa

mwaka 2008 na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya

Kutoa Motisha kwa Maeneo ya Pembezoni

Miongoni mwa vipengele vya TDMS ni kutoa motisha

kwa walimu wanaofanya kazi katika maeneo ya

pembezoni. Pia zinajulikana kama posho za kufanya

kazi katika mazingira magumu, motisha hizo

zinaweza kuwa posho za kiwango kimoja au

ongezeko kwa asilimia ya mishahara.

Motisha ya maeneo ya pembezoni ni njia makini ya

kubakiza walimu katika maeneo ya vijijini. Sasa hivi

Tanzania inakabiliana changamoto ya walimu wengi

wapya wanaopangiwa maeneo ya pembezoni

hawaripoti kazini, wanahamia shule za mijini, au

wanaacha kazi ndani ya mwaka mmoja, mwenendo

unaogharimu nchi shilingi milioni 511 kwa mwaka.
Muhtasari 10.3K

Hii inasababisha upungufu wa walimu hasa katika

maeneo ya vijijini. Ingawa lengo la taifa ni mwalimu

mmoja kwa wanafunzi 40, utafiti wa Wizara wa hivi

karibuni uligundua shule za vijijini kuwa na wastani

wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 59 na shule moja

kuwa na mwalimu mmoja kwa wanafunzi 283!

Katika kushughulika tatizo hili, kila mwaka Wizara

inapanga walimu wapya wengi zaidi wa kwenda

shule za vijijini kuliko shule za mijini. Mwaka 2008,

ingawa Wizara ilipanga walimu wapya tisa kati ya

kumi kwenda maeneo ya vijijini, mwisho wa mwaka,

walimu wapya wengi zaidi waliishia katika shule za

mijini kuliko shule za vijijini. Kushughulikia tatizo la

upungufu wa walimu wakati hali hii ya walimu

kuacha kazi inaendelea ni kazi bure, ni sawa na

kujaza maji kwenye ndoo inayovuja kwa kasi: maji

mengi yatapotezwa, kuna mashaka kama ndoo itajaa,

na hata ikijaa kwa muda mfupi, itaanza kumwaga

maji tena.

Motisha za maeneo ya pembezoni, zinazosaidia

kutatua tatizo hili, ni sehemu ya TDMS lakini

hazijatekelezwa kutokana na upungufu wa bajeti.

Hili siyo suala la upatikanaji wa fedha za umma,

lakini ni la namna ambavyo fedha za umma

zinatumika. Posho za kufanya kazi katika mazingira

magumu hazijatolewa kwa walimu wakati posho kwa

maofisa wengi wa serikali kuu zinaongezeka sana

mwaka hadi mwaka.

Motisha za Maeneo

Pembezoni

KUTOTOLEWA kwa

Walimu Kutokana na

“Ukosefu wa Fedha”

2009 Sh. bil 2

2010 Sh. bil 2.2

2011 Sh. bil 2.4

Jumla ya

Posho za Serikali

2009 Sh. bil 171

2010 Sh. bil 216

2011 Sh. bil 269

Wakati serikali ya Tanzania imeshindwa kutoa hata

asilimia moja ya posho zake zote kwa ajili ya walimu

wanaofundisha vijijini kama motisha ya maeneo ya

pembezoni, nchi jirani zimefanikiwa kutekeleza

motisha ya maeneo ya pembezoni. Kwa mfano,

Uganda ilianzisha posho ya kufanya kazi katika

mazingira magumu kwa kuongeza asilimia 20 ya

mshahara mwaka 2001, na imeongezeka hadi kufika

asilimia 30 mwaka huu. Serikali ya Tanzania

itaendelea kubaki nyuma kwa muda gani?

Kuwapandisha Daraja Walimu wenye

Leseni na Wale wasio na Taaluma

Kipengele kingine muhimu cha TDMS ni

kuwapandisha daraja walimu wenye leseni wawe na

digrii kwa sababu kutokuwa na sifa kwa walimu pia

imekuwa na athari katika matokeo ya kujifunza.

Ingawa serikali ya Tanzania imefaulu kwa kuongeza

uandikishaji wa wanafunzi shuleni na kujenga shule

za sekondari, kwa upande mwingine umesababisha

upungufu wa rasilimali watu.

Ili kukabiliana na upungufu huo, shule za sekondari,

hasa shule za kata zilizojengwa hivi karibuni,

zinalazimika kuwaajiri walimu wenye sifa za chini

kabisa. Kwa mujibu wa utafiti wa Wizara, kwa

wastani, nusu ya walimu wanaofunisha katika shule

za sekondari za serikali wana diploma na nusu wana

digrii. Lakini katika shule za sekondari za kata,

takribani hakuna walimu wenye digrii, na walimu

watatu kati ya kumi wana leseni tu au ni wahitimu

wa Kidato cha VI walioajiriwa na jamii kama walimu

wasio na taaluma. Kiwango duni cha elimu cha

mwalimu alichofikia kinaathiri ubora wa elimu

itolewayo kwa wanafunzi, na inakadiriwa kwamba

shule zote zinalipa shilingi bilioni 59.8 kwa mwaka

kwa walimu hawa wasio na sifa, ingawa michango

yao katika matokeo ya kujifunza ni ndogo sana.

Kama juhudi za TDMS, kuwapandisha daraja walimu

wasio na sifa wawe wataalamu wenye sifa kama

inavyohitajika, zingefanikiwa zingegharimu shilingi

bilioni 7.5 kwa mwaka 2011, lakini inaonekana

kwamba Wizara haijapanga bajeti kutekeleza

shughuli hii. Si lazima iwe hivyo; inaonekana

kwamba kuna fedha nyingi sehemu nyingine.

Kwa mfano, kuangalia elimu ya juu, wakati nchi

nyingine za Afrika kama vile Kenya zinatenga

kiwango sahihi cha asilimia 20 (au moja kati ya kila

shilingi tano) ya fedha zao za elimu kuenda kwa

elimu ya juu, Tanzania imekuwa inaipa elimu ya juu

wastani wa asilimia 26 ya fedha zote za elimu na

kuongeza kipande chake mwaka 2011 kiwe asilimia

36 (au moja kati ya kila shilingi tatu)!

Licha ya kuchukua theluthi ya bajeti ya elimu, elimu

ya juu inatumia asilimia 1.5 ya aina zote za

wanafunzi wanaoandikishwa katika ngazi yoyote ya

elimu Tanzania. Kwa mfano, kulinganisha wanafunzi

wa vyuo vikuu na shule za sekondari, kuna
Muhtasari 10.3K

wanafunzi 118,911 wa vyuo vikuu wakati kuna

1,388,347 (mara 12 ya idadi hiyo) walioandikishwa

katika shule za sekondari za serikali.

Bajeti kubwa na uandikishaji mdogo katika elimu ya

juu inamaanisha kwamba, hata ukiondoa mikopo ya

wanafunzi, bado Wizara inatumia fedha nyingi zaidi

kwa kila mwanafunzi wa chuo kikuu kuliko

mwanafunzi wa shule ya sekondari:

yanasaidia kushughulikia shida kubwa katika mfumo

wa elimu Tanzania, yaani, utoro wa walimu. Utafiti

kutoka Wizarani unaonesha kwamba wastani wa

zaidi ya asilimia 13 ya walimu wa shule za msingi na

za sekondari hawako kazini kwa miezi au hata

miaka :

Idadi ya wanafunzi katika shule za sekondari za

serikali ni mara 12 zaidi ya wale walio katika

vyuo vikuu na vyuo vingine vya serikali.

Hata ukiondoa mikopo ya wanafunzi,

serikali inatumia wastani wa fedha

mara 19 zaidi kwa kila mwanafunzi wa

chuo kikuu kuliko kwa kila mwanafunzi

wa shule ya sekondari.

Kati ya kila walimu 15 wanaolipwa kufundisha,

wawili hawapatikani shuleni.

Zaidi ya upotevu wa maarifa kwa watoto na viongozi

wa baadaye wa Tanzania, utoro huu wa walimu

unakadiriwa kusababisha hasara yenye jumla ya

shilingi bilioni 58.7 kwa mwaka.

Ndiyo, nyenzo za elimu ya juu ni ghali sana na ni

vigumu kutetea bajeti kupunguzwa katika sekta moja

ya elimu kuleta maboresho katika nyingine; lakini, je,

hakuna namna tofauti hii kubwa kati ya elimu ya juu

na ya sekondari inaweza kutatuliwa? Pamoja na

bajeti ya elimu ya juu kuongezeka kuwa shilingi

bilioni 698 mwaka 2011, je, haiwezekani kwa hata

asilimia moja ya hii kuenda kwenye kipengele cha

TDMS kwa kuwapandisha daraja walimu ili

kuboresha elimu ya sekondari? Pamoja na ongezeko

la uandikishaji wa wanafunzi katika shule za

sekondari, bajeti lazima irekebishwe kuhakikisha

kwamba wananchi wengi wanapewa elimu bora, sio

tabaka la wachache tu, ili kujenga taifa bora la

baadaye.

Kuhakikisha Fursa za Kujiendeleza

Kitaaluma

Pia TDMS ina hatua nyingi za kuhakikisha fursa za

kujiendeleza kitaaluma kwa walimu, hasa mafunzo

kazini. Umuhimu wa mafunzo ya walimu kazini si

kufundisha walimu upya ili kuwawezesha

kuwafundisha wanafunzi wao bora zaidi bali pia

Utafiti unapendekeza kwamba njia nzuri ya

kupambana na utoro wa walimu ni kutoa fursa za

kujiendeleza kitaaluma kama vile mafunzo kazini

ambayo yatawafanya walimu wapende kazi yao.

TDMS ya Tanzania ina lengo kuu la “kuhakikisha

mafunzo ya kujiendeleza kazini ya mara kwa mara na

ukuaji wa kitaaluma,” linalolenga ufufuo wa Vituo

vya Walimu (TRC), mahali ambapo walimu

wanaweza kupata mafunzo ya ziada na rasilimali ya

kufundishia. Ingawa kuna vituo vya TRC 600 nchini

kote, vimetelekezwa kwa miaka mingi, vinatoa

huduma chache, na havina rasilimali za kutosha.

Ndiyo sehemu kubwa ya bajeti ya mafunzo kazini

katika TDMS inaelekezwa kuimarisha TRC.

Gharama za sehemu hii ya TDMS kwa mwaka

2010/11 ni shilingi bilioni 22.9, lakini fedha hizi

hazijatolewa kutokana na TDMS kutopewa

kipaumbele cha juu. Vipaumbele hivi lazima

vizingatiwe upya. Ni usimamizi mbaya wa fedha

kuruhusu utoro wa walimu unaogharimu nchi

shilingi bilioni 58.7 kwa mwaka ingeweza

kudhibitiwa na mkakati unaogharimu chini ya nusu

ya kiasi hicho.
Muhtasari 10.3K

Je, Tanzania Inaweza Kumudu

Kutotekeleza TDMS?

Mkakati wa Maendeleo na Menejimenti ya Ualimu

(TDMS) una hatua ambazo, zikichukuliwa,

zinaweza kuhakikisha elimu bora kwa watoto na

vijana wa Tanzania itakayowezesha ukuaji

endelevu kwa Tanzania na kwa siku za baadaye.

Muhtasari huu umesistiza malengo matatu ya

TDMS yanayoweza kuwezesha ukuaji huo, yaani:

1) K u w a p a m o t i s h a w a l i m u

waliopangwa kufundisha shule za

pembezoni.

2) Kuwapandisha daraja walimu wa

shule za sekondari wenye leseni na

wale wasio na taaluma.

3) Kuwahakikishia fursa za kuendelea

kitaaluma kwa njia ya mafunzo ya

kujiendeleza kazini.

Hata hivyo, hatua hizi bado hazijatekelezwa

kikamilifu, na TDMS inabaki na fedha kidogo sana

kama kipaumbele cha chini kwenye bajeti.

Katika hali ya kusikitisha, kwa kushindwa

kutekeleza mkakati huo taifa hulazimika kulipa

hasara ambazo TDMS ingeweza kuzizuia. Wakati

mwaka 2011 TDMS ingegharimu shilingi bilioni

102, fedha nyingi zaidi huenda zikatumika kwa

vipengele vinavyopunguza ubora wa elimu Tanzania:

Gharama ya walimu wapya wasioripoti vituoni

au wanaotelekeza vituo vyao vya kazi: Sh. mil 511

Gharama ya walimu wenye leseni na wale wasio na

taaluma ambao hawana mchango mkubwa

katika matokeo ya kujifunza: Sh. bil 59.8

Gharama ya utoro wa walimu wa shule za msingi: Sh. bil 47

Gharama ya utoro wa walimu wa shule za sekondari: Sh. bil 11.7

Sh. bil 119

Hapana shaka, gharama za kutotekeleza TDMS

haziishii hapa. Hasara ya rasilimali za taifa

inayotokea kila mwaka kwa wanafunzi wa shule za

msingi na za sekondari wanaomaliza shule bila ya

kufundishwa vizuri na wenye uwezo mdogo

usiowafaa wao wenyewe wala kulisaidia taifa lao

haipimiki. Wakati huo huo, kutafuta rasilimali

zinazotakiwa katika kutekeleza TDMS inaweza kuwa

rahisi kuliko ilivyofikiriwa mwanzo, na kutekeleza

TDMS inaweza kuwa na gharama nafuu zaidi kuliko

kutoitekeleza.

Hatuna budi kukumbusha kwa nukuu ya Darek Bok,

msomi na mwanasheria, ambaye alikaririwa na

Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika hotuba yake ya

mwaka 2008: “Kama unadhani elimu ni ghali basi

jaribu ujinga.” Suala la TDMS linaonesha namna

ilivyo ghali kufanya jambo lisilo na busara. Swali

linalobaki ni: Je, Tanzania itaendelea kulipia ujinga

kwa muda gani ?

Utoro wa Walimu

wa Shule za Msingi

Walimu

wasio na

Sifa

Mkakati wa

Maendeleo na

Menejimenti ya

Ualimu (TDMS)

Walimu Wapya

Wanaoacha Kazi

Utoro wa

Walimu wa

Shule za

Sekondari

HakiElimu inawezesha wananchi

kuleta mabadaliko katika elimu

na demokrasia.

SLP 79401 ● Dar es Salaam ● Tanzania

Simu (255 22) 2151852/3 ● Faksi (255 22) 2152449

info@hakielimu.org ● www.hakielimu.org