19.02.2015 Views

Haki Elimu Report ya PETS swa mail.pdf

Haki Elimu Report ya PETS swa mail.pdf

Haki Elimu Report ya PETS swa mail.pdf

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Je, kuna uwajibikaji sahihi

katika utekelezaji wa MMEM II?

Ripoti ya Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha za Umma

(PETS)

Februari 2011

Je, kuna uwajibikaji sahihi katika

utekelezaji wa MMEM II?

Ripoti ya Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha za Umma

(PETS)

Februari 2011

i

Shukrani

Uandaaji wa ufuatiliaji huu, uchambuzi wa takwimu na uandishi wa ripoti hii ulifanywa na Godfrey

Boniventura. Shukrani za pekee ziwaendee Tony Baker ambaye alishiriki katika uandaaji wa dhana za

ufuatiliaji na ukusanyaji wa taarifa.

Uhariri, mrejesho na ushauri ulitolewa na Elizabeth Missokia, Mtemi Zombwe, Fausta Musokwa,

Charles Mtoi, Pius Makomelelo na Robert Mihayo. Pia Tunapenda kuwashukuru David Kagondi, Pius

Makomelelo, Benedicta Mrema, Maisory Chacha ambao walishiriki kukusanya taarifa za ufuatiliaji

huu.

Shukrani nyingi kwa wakurugenzi watendaji na maafisa elimu wa wilaya za Bunda, Morogoro, Nzega,

Iramba, Babati na Njombe kwa ushirikiano wao mzuri ambao uliwezesha utafiti huu kufanyika kwa

urahisi. Pia tunawashukuru marafiki wa elimu waliosaidiana na wafanyakazi wa Hakielimu kukusanya

taarifa ambao ni Peter Kololly, Asia Mtibua, Richard Lucas, Salumu Ally, Bernard Clement, Mary

Talas, Wenseslaus Byabato, Hamis Rashid na Juma Kalwani.

©HakiElimu, 2011 ISBN 978-9987-18-00907

HakiElimu, SLP 79401, Dar es Salaam

Simu: (255 22) 2151852/3, Faksi: (255 22) 2152449

Barua pepe: info@hakielimu.org

Tovuti: www.hakielimu.org

Sehemu yoyote ya kitabu hiki inaweza kutolewa kwa namna yoyote kwa madhumuni ya kielimu na

siyo ya kibiashara, kwa kuzingatia kuwa chanzo kitatajwa na nakala mbili zitapelekwa HakiElimu.

ii

Yaliyomo

Vifupisho

1.0 Utangulizi………………………………………………………………………………………1

1.1 Usuli……………………………………………………………………………….…1

1.2 Malengo ya Ufuatiliaji ...............................……………...............................................2

2.0 Mbinu za Ufuatiliaji ...............................………..........................................................3

2.1 Maeneo ya Ufuatiliaji ...............................……………...............................................3

2.2 Wadau Waliohusishwa Katika Ukusanyaji wa Taarifa .......................................................3

2.2.1 Afisa Elimu ...............................……………............................................... 3

2.2.2 Walimu Wakuu ....................................…………….....................................4

2.2.3 Wazazi ....................................……………...................................................4

3.0 Matokeo ....................................…………….........................................................................5

3.1 Ruzuku ya Mwanafunzi Ngazi ya Wilaya ............................................................5

3.1.1 Ruzuku inayofika Wilayani ............................................................................5

3.1.2 Ruzuku na idadi ya Wanafunzi......................................................................6

3.1.3 Matumizi Mabaya ya Ruzuku Ngazi ya Wilaya ...............................................7

3.2 Ruzuku ya Mwanafunzi Ngazi ya Shule

3.2.1 Ruzuku Inayofika Shuleni ....................................…………….....................8

3.2.2 Uelewa wa Walimu Wakuu Kuhusu Ruzuku ya Mwanafunzi ..........................9

3.2.3 Muda wa Ruzuku Kufika Shuleni ........................................................……10

3.2.4 Hali ya Matumizi ya Ruzuku Shuleni .......................................................10

3.3 Fedha za Maendeleo ....................................................................................……12

3.3.1 Hali ya Ujenzi wa Miundo Mbinu ..............................................................12

3.3.2 Matumizi Mabaya ya Fedha za Maendeleo .................................................13

3.4 Michango ya Wazazi ..............................................................................................16

3.4.1 Mwamko wa Wazazi Kuchangia Elimu ......................................................16

4.0 Ulinganishi wa MMEM I na MMEM II ...........................................................................17

5.0 Hitimisho na Mapendekezo ...............................................................................................18

5.1 Hitimisho ..................................................................................................................18

5.2 Mapendekezo ..........................................................................................................19

Marejeo ........................................................................................................................................ 21

Viambatisho .................................................................................................................................22

iii

Vifupisho

BEST

GBS

MMEM I

MMEM II

PETS

REPOA

URT

Basic Education Statistics of Tanzania

General Budget Support

Mpango wa Kwanza wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi

Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi

Public Expenditure Tracking Survey

Research on Poverty Alleviation

United Republic of Tanzania

iv

1.0 UTANGULIZI

1.1 Usuli

Baada ya kufanikiwa kuongeza udahili wa wanafunzi kwa shule za msingi toka 88% mwaka 2001 hadi

96% mwaka 2006 kupitia Mpango wa kwanza wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM I), Serikali

iliandaa Mpango wa pili wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM II) ambapo utekelezaji wake

ulianza mwaka wa fedha 2007/2008 1 . Moja ya malengo makuu ya MMEM II ilikuwa ni kuboresha

hali ya mazingira ya kujifunzia kwa kujenga miundombinu kama vile madarasa, nyumba za walimu,

vyoo na madawati. Kiambatisho namba 2 kinaonesha miundombinu ambayo ilibainishwa kujengwa au

kununuliwa katika muda wote wa utekelezaji wa MMEM II. Pia ilidhamiria kuboresha mchakato wa

kujifunza na kufundisha kwa kuongeza vifaa kama vile vitabu vya kiada na ziada kwa ajili ya wanafunzi.

Ili kutekeleza adhma hii, MMEM II, ilibainisha kuwa Sh. 10,000 itatolewa kwa kila mwanafunzi wa

shule ya msingi kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa MMEM II. Ruzuku ya

mwanafunzi inalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa kuboresha upatikanaji

wa vitabu vya kianda(Asilimia 40), ukarabati mdogo wa miundo mbinu iliyopo shuleni(Asilimia

20), kuboresha upatikanaji wa madaftari, kalamu,penseli, chaki na vifaa vingine vya kufundishia

walimu(Asilimia 20), uwezo wa kuendesha mazoezi na mitihani mbalimbali(Asilimia 10) na uendeshaji

wa shule (Asilimia 10).

Ikiwa miaka mitatu ya utekelezaji wa MMEM II imepita, na huku bajeti ya sekta ya elimu ikiongezeka

mwaka hadi mwaka, hali halisi ya utekelezaji wa MMEM II bado ina changamoto nyingi. Ndani ya

miaka mitatu ya utekelezaji wa MMEM II, nyumba za walimu 986 2 tu zimejengwa kati ya nyumba

65,808 zilizopangwa kujengwa kati ya mwaka 2007 na 2009. Vyombo vya habari hasa magazeti

vimekuwa vikiripoti kuhusu idadi ya wanafunzi wengi kukaa chini katika shule mbalimbali hapa

nchini (Picha 1). Uwiano wa mwanafunzi kwa kitabu ni 1:5 3 tofauti na lengo la kuwa na uwiano wa

1:1 kwa mwaka 2010. Tatizo hili limekuwa likiathiri mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwani

wanafunzi watano wanasoma kitabu kimoja. Changamoto hizi zote zinaibua maswali! Kama bajeti

ya sekta ya elimu inaongezeka mwaka hadi mwaka 4 na utekelezaji wa MMEM II si wa kuridhisha,

fedha hizi zinatumikaje? Je, fedha zinazopangwa katika bajeti zinawafikia walengwa? Na mipango yote

inatekelezwa kama inavyopaswa? Majibu ya maswali haya yanahitaji ufuatiliaji wa bajeti hasa fedha

zinazotengwa na kutolewa kwa ajili ya utekelezaji wa MMEM II.

MMEM II unabainisha pia umuhimu wa jamii kuchangia michango mbalimbali ili kufanikisha

utekelezaji wa mpango huu na hatimaye kuleta maendeleo ya shule za msingi. Jamii inapaswa kuchangia

asilimia 20 ya gharama za utekelezaji wa MMEM II 5 , na hii inamaanisha kuwa elimu haitolewi bure

kama inavyoelekezwa katika MMEM II. Kutokana na agizo hilo, wazazi wamekuwa wakiombwa na

1

URT (2009), Ripoti ya utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM II)

2

URT (2009), Ripoti ya utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi(MMEM II) na URT (2010), Ripoti ya

utekelezaji wa sekta ya elimu kwa mwaka 2009

3

URT (2010), Ripoti ya utekelezaji wa sekta ya elimu kwa mwaka 2009

4

Hotuba za bajeti za Tanzania tangu mwaka 2007 hadi 2010.

5

Ukurasa wa 38 katika MMEM II umebainisha kuwa michango ya jamii kwa ajili ya utekelezaji wa miundo mbinu ni asilimia 20

6

Ripoti ya utafiti ya HakiElimu ya mwaka 2010, Je, jamii inawezaje kuboresha elimu ya watoto wao?

1

wakati mwingine kushinikizwa 6 kutoa michango mbalimbali kama vile, michango ya mitihani na

mahitaji mengine ya shule. Ripoti ya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma ya Wizara ya Elimu

na Mafunzo ya Ufundi ya mwaka 2009, imebainisha kutolewa kwa michango hiyo na wazazi. Mwaka

wa fedha 2007/2008, jumla ya fedha za michango ya wazazi zilizokusanywa na walimu wakuu ilikuwa

asilimia 7.7 ya fedha iliyotumika kwenye shule 7 . Moja ya mapungufu ya ripoti hii ni kwamba ilitumia

takwimu za walimu wakuu pekee na haikuhoji wazazi ili kufahamu kiwango wanachotoa kwa mwaka

na kama wanatoa michango je, kuna matumizi sahihi ya fedha hizo? Hitaji la majibu ya maswali haya

ya ufuatiliaji wa fedha za utekelezaji wa MMEM II ndio lililotoa msukumo kwa Shirika la HakiElimu,

kufanya ufuatiliaji wa fedha za umma toka serikalini hadi shuleni ukihusisha utekelezaji wa MMEM II

kwa kipindi cha miaka mitatu 8 .

Picha 1: Makala za vyombo vya habari kuhusu matatizo ya elimu hapa nchini.

1.2 Malengo ya Ufuatiliaji

1. Kufahamu kiasi cha fedha za ruzuku ya mwanafunzi na fedha za maendeleo zinazofika shuleni.

2. Kufahamu hali ya matumizi ya fedha za ruzuku na maendeleo, na kubaini mafanikio na

mapungufu yake.

3. Kubainisha kiasi cha fedha wanachochanga wazazi.

4. Kulinganisha hali ya uwajibikaji wa serikali kati ya MMEM I na MMEM II.

7

Fedha hii haihusishi fedha za mishahara ya walimu

8

Kuanzia mwaka wa fedha 2007/2008 hadi 2009/2010

2

2.0 MBINU ZA UFUATILIAJI

Kabla ya kuanza ufuatiliaji, shirika la HakiElimu lilituma barua kwa Wakurugenzi wa wilaya

zilizochaguliwa kuomba kupatiwa kibali cha kufanya ufuatiliaji na baada ya kupata ruhusa, wafanyakazi

wa shirika la HakiElimu walifika katika ofisi ya Mkurugenzi wa wilaya husika, kujitambulisha

na kuonana na Afisa Elimu kwa ajili ya mahojiano. Katika kila wilaya, Afisa Takwimu wa elimu

alishirikiana na watafiti wasaidizi wakati wa kufanya mahojiano na wakuu wa shule na pia kuhakiki

takwimu zinazotolewa na walimu wakuu. Kwa kuwa ufuatiliaji huu ulidhamiria kufahamu hali ya

matumizi ya fedha katika utekelezaji wa MMEM II, miaka mitatu ya fedha kuanzia 2007/2008 hadi

2009/2010 ilihusishwa kwa kuzingatia kuwa mwaka wa fedha 2007/2008 ndio ulikuwa mwaka wa

kwanza wa utekelezaji wa MMEM II. Pia ukusanyaji wa taarifa ulifanyika mwezi Oktoba 2010 katika

mwaka wa fedha 2010/2011 ambapo tayari mwaka wa fedha 2009/2010 ulikuwa umemalizika tangu

mwezi Juni 2010.

2.1 Maeneo ya Ufuatiliaji

Ufuatiliaji wa fedha za umma ulihusisha wilaya sita toka mikoa sita ambayo ilichaguliwa kwa kutumia

uchaguzi nasibu toka kanda ya Ziwa (Mara), Magharibi (Tabora), Mashariki (Morogoro), Nyanda za

juu kusini (Njoluma), Kati (Singida) na Kaskazini (Manyara). Baada ya kuchagua mikoa, uchaguzi

nasibu ulitumika kupata wilaya moja toka kila mkoa, wilaya hizo ni Manispaa ya Morogoro, Nzega,

Iramba, Bunda, Njombe na Babati (Kiambatisho namba 1). Jumla ya shule 24 zilihusishwa katika

ufuatiliaji huu, ambapo shule nne zilichaguliwa toka kila wilaya kwa kutumia uchaguzi nasibu. Katika

shule nne za kila wilaya, shule mbili zilikuwa za mjini na shule mbili za vijijini. Kabla ya kuchagua

shule, Mtafiti Msaidizi aliomba kupatiwa orodha ya shule za mjini na vijijini toka kwa Afisa Elimu na

ndipo shule mbili zilichaguliwa toka kila kundi.

2.2 Wadau Waliohusishwa katika Ukusanyaji wa Taarifa

2.2.1 Afisa Elimu

Afisa Elimu wa shule za msingi ni msimamizi mkuu wa michakato na mikakati yote ya utoaji elimu ya

msingi katika ngazi ya wilaya. Na pia ndiye anayepokea fedha toka kwa Mtunza Hazina wa wilaya na

kuzipeleka shuleni. Katika ngazi ya wilaya, Afisa Elimu wa wilaya wa shule za msingi na Afisa Takwimu

wa shule za msingi walihojiwa ili kuelezea kiasi cha fedha za ruzuku na maendeleo walizopokea

toka hazina katika kipindi cha mwaka 2007/2008 hadi 2009/2010; na pia kueleza kiasi cha fedha

kilichopelekwa kwenye shule nne zilizochaguliwa kwa ufuatiliaji katika wilaya yake. Pia Afisa Elimu

alipatiwa dodoso ili kujaza takwimu mbalimbali za idadi ya shule, idadi ya wanafunzi na pia kutoa

maoni kuhusu fedha za ruzuku na fedha za maendeleo kwa shule za msingi.

3

2.2.2 Walimu Wakuu

Walimu wakuu ni wataalamu waendeshaji wa shule ambao ndio wanapokea fedha toka kwa Afisa Elimu

wa shule za msingi na kuzitumia kutekeleza mipango mbalimbali ya shule. Walimu wakuu walihojiwa

ili kueleza kiasi cha fedha za ruzuku na fedha za maendeleo walichopata katika miaka mitatu ya fedha

(2007/2008 hadi 2009/2010), na jinsi walivyozitumia. Pia walihojiwa kiasi cha michango ya wazazi

walichokusanya katika mwaka wa fedha 2009/2010 9 ili kuweza kubaini kiasi cha fedha wanachochanga

wazazi na jinsi zilivyotumika katika mwaka husika. Ili kuboresha ufuatiliaji huu, kila Mwalimu Mkuu

alitakiwa kugonga mhuri wa shule juu ya dodoso mara baada ya kumaliza kujaza takwimu mbalimbali

zilizohitajika.

2.2.3 Wazazi

Wazazi walihojiwa ili kujua kiasi wanachochanga kwa mwaka, na pia kuelezea jinsi fedha zinavyotumika

kama ni sahihi au si sahihi, na jinsi wanavyoshirikishwa katika taarifa za mapato na matumizi ya

shule. Pia waliulizwa kutoa maoni kuhusu fedha za ruzuku ya mwanafunzi na maendeleo na kama

wanapatiwa risiti mara wanapotoa michango yao. Wazazi kumi walihojiwa katika kila shule, na hivyo

kufanya jumla ya wazazi waliohojiwa kuwa 240. Kigezo kikubwa kilichotumika kuchagua wazazi ni

kwamba mzazi alipaswa kuwa na mtoto anayesoma katika shule iliyochaguliwa kwa ufuatiliaji. Ili

kuwapata wazazi, wanafunzi wawili kwa kila darasa kuanzia darasa la tatu hadi la saba walichaguliwa

kwa kutumia uchaguzi nasibu, na hao wanafunzi 10 ndio walitakiwa kwenda kuwaita wazazi wao kwa

ajili ya mahojiano.

9

Wakati wa majaribio ya dhana za ufuatiliaji wazazi wengi walionekana kutokuwa na kumbukumbu za michango ya

miaka ya nyuma, hivyo ufuatiliaji ulitumia mwaka 2009/2010 ili kuepuka tatizo la wazazi kutokumbuka michago yao

ya miaka ya nyuma.

4

3.0 MATOKEO YA UFUATILIAJI

3.1 RUZUKU YA MWANAFUNZI NGAZI YA WILAYA

3.1.1 Ruzuku Inayofika Wilayani

Jumla ya fedha ya ruzuku iliyopokelewa katika wilaya sita ni Sh. bilioni 2.1 kwa mwaka wa fedha

2007/2008, Sh. bilioni 2.6 kwa mwaka 2008/2009 na Sh. bilioni 1.9 kwa mwaka 2009/2010. Kwa

kuwa jumla ya wanafunzi katika wilaya hizi sita ni 442,334, na 447,614 na 440,541 katika miaka

ya 2008, 2009 na 2010, wilaya hizi zingepaswa kupokea takribani Sh. bilioni 4.4, Sh. bilioni 4.5

na Sh. bilioni 4.4 katika miaka mitatu iliyopita kwa mujibu wa MMEM II. Ukilinganisha fedha

halisi zilizofika kwa miaka mitatu na idadi ya wanafunzi unapata picha kuwa fedha halisi za ruzuku

zilizofika katika wilaya sita ilikuwa Sh 4,909(mwaka 2007/2008,) Sh 5,811(mwaka 2008/2009) na Sh.

4,297(mwaka 2009/2010). Na wastani kwa miaka mitatu ilikuwa Sh 5,005 badala ya Sh. 10,000 kama

ilivyoainishwa katika MMEM II.

Jedwali 1: Tofauti kati ya ruzuku halisi iliyofika wilayani na iliyopaswa kufika wilayani kwa mujibu

wa MMEM II

Mwaka

2007/08

2008/09

2009/10

Idadi ya

wanafunzi

442,334

447,614

440,541

Chanzo: Takwimu za ufuatiliaji

Ruzuku iliyofika

wilayani

2.2 bilioni

2.6 bilioni

1.9 bilioni

Ruzuku iliyopaswa

kufika wilayani

4.4 bilioni

4.5 bilioni

4.4 bilioni

Upungufu

2.2 bilioni

1.9 bilioni

2.5 bilioni

Asilimia

pungufu

50%

42%

57%

Chati 1:

Tofauti kati ya ruzuku halisi iliyofika wilayani na iliyopaswa kufika wilayani kwa mujibu

wa MMEM II.

Ruzuku

(Sh. bilioni)

5

4.5

4

3.5

3

2.5

2

1.5

1

0.5

0

4.4 4.5 4.4

2.6

2.2

1.9

2007/08 2008/09 2009/10

Ruzuku iliyopaswa kufika wilayani

Ruzuku iliyofika wilayani

Chanzo:Takwimu za ufuatiliaji

5

Chati 2:

Mwenendo wa ruzuku kwa kila mwanafunzi iliyofika ngazi ya wilaya kwa miaka

mitatu(2007/08-2009/10)

3.1.2 Ruzuku na Idadi ya Wanafunzi

MMEM II umeainisha kuwa fedha za ruzuku zinapaswa kutolewa kulingana na idadi ya wanafunzi

waliopo wilayani katika mwaka husika. Taarifa za wilaya sita zinaonesha kuwa upelekaji wa ruzuku

wilayani toka serikali kuu hauzingatii idadi ya wanafunzi. Wilaya nyingine zilipokea fedha nyingi zaidi

ilihali zina wanafunzi wachache, wakati wilaya nyingine zilipata fedha kidogo na zina wanafunzi wengi.

Jedwali namba 2 linaonesha kuwa katika mwaka wa fedha 2009/2010, wilaya ya Nzega iliyokuwa na

wanafunzi 90,529 ambao ni wengi zaidi ya wilaya nyingine, ilipata Sh. milioni 316.8 na hivyo wastani

wa ruzuku kwa mwanafunzi ilikuwa Sh. 3,307 ilihali wilaya ya Bunda yenye wanafunzi 81,283 ilipata

Sh. milioni 503.8 ambapo wastani wa ruzuku ni Sh. 6,199. Ugawaji wa fedha za ruzuku bila kuzingatia

idadi ya wanafunzi, umefanya kuwe na tofauti kubwa ya kiwango cha ruzuku kwa mwanafunzi

zinazofika wilayani kati ya wilaya na wilaya. Utafiti huu unaonesha kuwa, kiwango cha chini ni Sh.

1,705 kwa wilaya ya Njombe na kiwango cha juu ni Sh. 6,199 kwa wilaya ya Bunda (Jedwali namba 2).

Jedwali 2: Ulinganifu kati ya fedha zilizofika wilayani na idadi ya wanafunzi

Wilaya

Bunda

Iramba

Babati

Nzega

Morogoro

Njombe

Jumla ya Fedha za ruzuku

zilizofika wilayani (Sh)

503,830,500

514,263,750

303,770,000

316,827,000

112,825,824

130,553,600

2009/2010

Idadi ya

wanafunzi

81,283

85,406

61,254

90,529

45,703

76,366

Ruzuku kwa kila

mwanafunzi (Sh)

6,199

6,021

4,959

3,500

2,469

1,705

6

Chati 3:

Ulinganifu wa ruzuku ya mwanafunzi iliyofika ngazi ya wilaya kwa mwaka wa fedha

2009/2010

Ruzuku(Sh)

7,000

6,000

5,000

4,000

3,000

2,000

1,000

0

6,199 6,021

4,959

2.6

1.9

3,500

2,469

1,705

Bunda Iramba Babati Nzega Morogoro Njombe

Ruzuku kwa kila mwanafunzi

3.1.3 Matumizi Mabaya ya Ruzuku Ngazi ya Wilaya

Katika ngazi ya wilaya kulikuwa na matumizi mabaya ya ruzuku kwa miaka miwili ya fedha iliyopita.

Matumizi haya yanabainishwa kwa kulinganisha wastani wa ruzuku iliyopokelewa ngazi ya wilaya na

wastani wa ruzuku iliyofika shuleni. Katika mwaka wa fedha 2008/2009 tofauti ilikuwa Sh. milioni

208.1 ambayo ni asilimia 8 kati ya fedha iliyofika shuleni na iliyoripotiwa kupelekwa shuleni toka

wilayani (Kisanduku namba 1). Katika mwaka wa fedha 2009/2010 tofauti ilikuwa Sh. milioni

293.4 ambayo ni asilimia 16 kati ya fedha iliyofika shuleni na iliyoripotiwa kupelekwa shuleni toka

wilayani(Kisanduku namba 1). Hii inamaanisha kuwa fedha za ruzuku hazifika kwa walengwa ambao

ni wanafunzi ambao ndio wanahitaji fedha hizi kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kujifunzia na

kufundishia.

Kisanduku 1. Ukokotoaji wa tofauti kati ya fedha zilizofika shuleni na fedha zilizoripotiwa

kupelekwa shuleni toka wilayani.

• Kwa mwaka wa fedha 2008/2009, taarifa za wilaya sita zinaonesha kuwa, wastani wa ruzuku iliyofika

wilayani toka hazina kuu ni Sh. 5,811 kwa kila mwanafunzi na taarifa za wakuu wa shule 24 zinaonesha

kuwa wastani wa fedha za ruzuku zilizofika shuleni ni Sh. 5,346. Hivyo Sh. 465 kwa kila mwanafunzi

zilikomea ngazi ya wilaya ambapo hazikwenda mashuleni. Tukizidisha Sh. 465 na idadi ya wanafunzi

wa wilaya sita ambao ni 447,614 kwa mwaka 2009 tunapata tofauti ya Sh. milioni 208.1 ambayo ni

asilimia 8 kati ya fedha iliyofika shuleni na iliyoripotiwa kupelekwa shuleni toka wilayani. Utofauti huu

ungekuwa wastani kwa wilaya zote 133 za Tanzania, ungekuwa sawa na Sh bilioni 4.6

• Katika mwaka wa fedha 2009/2010, wastani wa ruzuku iliyofika wilayani toka hazina kuu ni Sh.

4,297 kwa kila mwanafunzi na taarifa za wakuu wa shule 24 zinaonesha kuwa wastani wa fedha za

ruzuku zilizofika shuleni ni Sh. 3,631. Hivyo Sh. 666 kwa kila mwanafunzi zilikomea ngazi ya wilaya

ambapo hazikwenda mashuleni. Tukizidisha Sh. 666 na idadi ya wanafunzi wa wilaya sita ambao ni

440,541 kwa mwaka 2010 tunapata tofauti ya Sh. milioni 293.4 ambayo ni asilimia 16 kati ya fedha

iliyofika shuleni na iliyoripotiwa kupelekwa shuleni toka wilayani. Utofauti huu ungekuwa wastani kwa

wilaya zote 133 za Tanzania, ungekuwa sawa na Sh bilioni 6.5.

7

Jedwali 3: Hali ya matumizi ya ruzuku kwa mwanafunzi ngazi ya wilaya(2008/09-2009/2010)

Mwaka Ruzuku iliyofika Ruzuku iliyofika

wilayani(A) shuleni(B)

2008/09

2009/10

5,811

4,297

Chanzo: Takwinu za uchunguzi

5,346

3,631

Ruzuku ambayo

haikufika

shuleni(C)

C=A-B

465

666

Idadi ya

wanafunzi

katika wilaya 6

(D)

447,614

440,541

Jumla ya

Ufujaji ngazi

ya wilaya(E)

E=C x D

208.1 milioni

293.4 milioni

3.2 RUZUKU YA MWANAFUNZI NGAZI YA SHULE

3.2.1 Ruzuku Inayofika Shuleni

Katika shule 24 zilizofanyiwa ufuatiliaji wa ruzuku, wastani wa kiwango cha ruzuku kilichofika shuleni

kwa miaka mitatu iliyopita kuanzia mwaka wa fedha 2007/2008 hadi 2009/2010 ni Sh. 4899 kwa

mwaka 2007/2008, Sh. 5,346 kwa mwaka 2008/2009 na Sh. 3,631 kwa mwaka 2009/2010 kwa kila

mwanafunzi. Katika mwaka wa fedha 2009/2010, ruzuku ya mwanafunzi inayofika shuleni imepungua

zaidi kwa Sh. 1,715 tofauti na mwaka 2008/2009. Wastani wa ruzuku iliyofika shuleni kwa miaka

mitatu ni Sh. 4,736. Pia wastani wa ruzuku ya mwanafunzi iliyofika shuleni kwa miaka mitatu ya

utekelezaji wa MMEM II ni ndogo zaidi ya fedha ambazo zilifika wilayani 10 kwa miaka hiyo.

Kuna tofauti kubwa ya kiwango cha ruzuku kilichofika shuleni kati ya shule na shule. Katika mwaka

2007/2008 kiwango kidogo cha ruzuku kilikuwa Sh. 1,823 ilihali kiwango cha juu kilikuwa Sh.

6,797. Kwa mwaka 2008/2009 kiwango cha chini kilikuwa Sh. 2,222 na kiwango cha juu Sh. 7,849.

Kiwango cha chini kilipungua zaidi mwaka 2009/2010 ambacho kilikuwa Sh. 726 kwa shule ya

msingi Kingorwila (Manispaa ya Morogoro) wakati kiwango cha juu kilikuwa Sh. 8,543 kwa shule

ya msingi Mazoezi (Bunda, Mara). Tofauti hii ndiyo inasababisha baadhi ya shule kuwa na vifaa vingi

vya kujifunzia na kufundishia na shule zingine zinakuwa na vifaa vichache. Hii inafanya pia hata shule

zinazopata ruzuku kidogo kushindwa kufaulisha wanafunzi wengi na hivyo kufanya wanafunzi wengi

kushindwa kuendelea na elimu ya sekondari.

Pia kuna tofauti ya ruzuku inayofika shuleni kati ya shule za vijijini na shule za mjini. Jedwali namba

4 linaonesha kuwa katika miaka mitatu iliyopita shule za mjini zimekuwa zikipata ruzuku kati ya Sh.

5,741, Sh. 5,678 na Sh. 3,712 wakati shule za vijijini zimekuwa zikipata ruzuku kati ya Sh. 4,440, Sh.

4,785 na Sh. 3,550. Matokeo haya yanafanana sana na ufuatiliaji kama huu uliofanywa na Wizara ya

Elimu na Mafunzo ya Ufundi mwaka 2009 ambapo ilibainika pia kuwa shule za mjini zinapata ruzuku

kubwa zaidi ya shule za vijijini. Kama ilivyokuwa kwenye ripoti ufuatiliaji wa fedha za umma (PETS)ya

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ufuatiliaji huu haukuweza pia kubainisha sababu za utofauti

wa fedha za ruzuku kati ya shule za mjini na vijijini.

10

Wastani wa Ruzuku kwa kila mwanafunzi iliyofika wilayani ni Sh.5005

8

Jedwali 4: Ugawaji wa ruzuku kwa shule za mjini na vijijini

Mwaka wa fedha

2007/2008

2008/2009

2009/2010

Chanzo: Takwinu za uchunguzi

Ruzuku kwa shule za mjini(A)

5,741

5,678

3,712

Ruzuku kwa shule za vijijini(B)

4,440

4,785

3,550

Tofauti(A-B)

1,301

893

162

Chati 4: Ulinganifu wa ruzuku kati ya shule za mjini na vijijini

Ruzuku(Sh)

7,000

6,000

5,000

4,000

3,000

2,000

1,000

0

5,741 5,678

4,785

4,440

3,712 3,550

2007/2008 2008/2009 2009/2010

Ruzuku kwa shule za mjini

Ruzuku kwa shule za vijijini

3.2.2 Uelewa wa Walimu Wakuu kuhusu Ruzuku ya Mwanafunzi

Walimu wakuu waliulizwa wataje kiasi cha ruzuku ambacho kila mwanafunzi anapaswa kupata. Licha

ya kuwa katika ngazi ya wilaya uelewa wa ruzuku ni mkubwa, hali ni tofauti katika ngazi ya shule.

Kati ya walimu wakuu 24 waliohojiwa kuhusu uelewa wa ruzuku na kiasi cha ruzuku ambacho kila

mwanafunzi anapaswa kupata kwa mujibu wa MMEM II, walimu 11 kati ya 24(sawa na asilimia

46) hawajui kiasi ambacho kila mwanafunzi anapaswa kupata. Hii inafanya walimu wengi washindwe

kufahamu hata jumla ya fedha wanayopaswa kupata kwa mwaka mzima. Maana jumla ya fedha

inategemea na idadi ya wanafunzi. Sababu kubwa za kutofahamu ni pamoja na walimu kutokuwa

na Kitabu cha MMEM II. Walimu wote 24 waliohusishwa katika uchunguzi huu walibainisha kuwa

hawajawahi kuwa na nakala ya kitabu au waraka wa MMEM II tangu utekelezaji wake uanze. Kama

walimu wakuu ambao ndio watendaji na wadau wakuu katika utekelezaji wa MMEM II ngazi ya shule

hawana nakala ya MMEM II ni dhahiri kuwa hawataweza kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wake

kama vile kuhoji endapo watapata fedha pungufu toka wilayani au kutengeneza mpango mkakati wa

shule unaozingatia malengo na viashiria vya MMEM II.

9

Kisanduku 2

“Mimi sijawahi kupata nakala ya MMEM II na wala sijui huu mpango una maanisha nini. Sijui hata mambo

ambayo sisi walimu wakuu tunapaswa kufanya ili kuboresha mpango”. (Mwalimu Mkuu, Njombe)

“Sina nakala ila niliona kwenye kalenda inazungumzia MMEM II, inasema eti Wizara imeboresha madarasa

na imetoa picha yenye madarasa mazuri. Sasa sijui haya madarasa yako wapi maana haya yangu ni mabovu na

watoto wanakaa chini kama ulivyoona kwenye lile darasa la kwanza na la pili zaidi ya watoto 40 wanakaa chini

kwa kila Darasa”. (Mwalimu mkuu, Morogoro)

3.2.3 Muda wa Ruzuku Kufika Shuleni

Ufuatiliaji huu umebainisha kuwa ruzuku ya mwanafunzi inachelewa kufika shuleni licha ya kwamba

inafika wilayani katika muda muafaka. Kati ya shule 24, ni shule 9(asilimia 37 ndizo zilipata fedha

za ruzuku kwa muda muafaka katika mwaka wa fedha 2009/2010. Kwa shule zinazochelewa kupata

ruzuku, zinapata ruzuku miezi miwili hadi mitatu baada ya kuanza kwa robo ya kila mwaka. Fedha za

robo ya kwanza zinafika kati ya mwezi wa Septemba na Oktoba badala ya mwezi Julai. Na fedha za robo

ya mwisho zinafika mwezi wa Juni badala ya mwezi Aprili. Katika maoni yao walimu wakuu wamekiri

kuwa ucheleweshaji wa ruzuku unaathiri kwa kiwango kikubwa ununuzi wa mahitaji ya kufundishia na

kujifunzia kama vile vitabu na vifaa vya kufundishia. Na hivyo, kurudisha nyuma maendeleo ya elimu

hapa nchini.

Kisanduku 3

“Fedha za ruzuku zinachelewa sana kufika shuleni na ndio maana mmekuta fedha nyingi karibu Tsh milioni

4 hazijatumika katika mwaka husika. Sisi tumepata ruzuku ya robo ya tatu ikiwa pamoja na robo ya nne

mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu” (Mwalimu Mkuu, Nzega.)

“Hii ruzuku inachelewa sana kufika hapa shuleni na kuathiri mipango yetu ya hapa shuleni na mi nashauri

Serikali itoe hizi fedha mapema hata ikibidi mwezi Januari zitoke zote na pia watoe Sh 10,000 kwa kila

mwanafunzi ili tupunguze utegemezi wa wazazi”. (Mwalimu Mkuu, Njombe).

3.2.4 Hali ya Matumizi ya Ruzuku Shuleni

Hali ya matumizi ya fedha za ruzuku katika ngazi ya shule si ya kuridhisha. Kati ya shule 24, shule 14

(asilimia 58) zilishindwa kutumia fedha zote katika mwaka wa fedha 2009/2010. Mwaka wa fedha

2009/2010, asilimia 25 ya fedha za ruzuku zilizofika katika shule 24 hazikutumika. Jumla ya Tsh

milioni 64.2 zilifika katika shule hizo lakini fedha halisi zilizotumika zilikuwa Tsh milioni 48.3. Hii

inamaanisha kuwa kuna baadhi ya mahitaji kama vile vitabu havikununuliwa katika shule hizo na

hivyo kuathiri maendeleo ya elimu katika shule.

10

Picha 2: Ripoti ya mwalimu mkuu inayoonesha jinsi fedha za ruzuku zilivyotumika

Ili kubainisha kama fedha za ruzuku zimetumika ipasavyo, walimu wakuu walitakiwa kuonesha risiti za

matumizi mbalimbali ya ruzuku ya wanafunzi kwa mwaka 2009/2010. Ukaguzi wa risiti za manunuzi

ya vitabu ulitumika na kubaini kuwa ulinganifu wa bei zilizopo kwenye risiti 11 na idadi ya vitabu

vilivyonunuliwa si sawa. Risiti zinaonesha kuwa vitabu vilinunuliwa kwa bei kati ya Sh. 4,000 na Sh.

6,000 ambayo ni wastani wa Sh. 5,000. Lakini tukihusisha jumla ya vitabu vilivyonunuliwa katika

shule 24 na bei ya wastani iliyopo kwenye risiti tunapata picha kuwa hakukuwa na matumizi sahihi ya

fedha za ruzuku zilizotumika kununua vitabu. Katika mwaka wa fedha 2009/2010 jumla ya Sh. milioni

25.7 12 zilitumika kununua vitabu katika shule 24 na vitabu vilivyonunuliwa ni 2,673. Ukigawanya Sh.

milioni 25.7 na idadi ya vitabu utaona kuwa kila kitabu kiligharimu Sh. 9,610, bei hii ni tofauti na

wastani wa bei iliyopo kwenye risiti za manunuzi ya vitabu. Hivyo basi, kwa kila kitabu kuna tofauti

ya Sh. 4,610, na ukizidisha tofauti ya bei (Sh. 4,610) kwa idadi ya vitabu 2,673 tunapata takribani Sh.

milioni 12.3 (asilimia 47.9) zilitumika vibaya katika shule 24 katika ngazi ya shule. Hii inamaanisha

kuwa katika kila Sh. 100 ya ununuzi wa vitabu inayofika shuleni, takribani Sh. 48 13 zinatumika vibaya.

Matumizi mabaya ya fedha za ununuzi wa vitabu yanaashiria kuwa kuna changamoto kubwa kuboresha

mazingira ya kujifunzia na kufundishia hasa katika kuwezesha upatikanaji wa vitabu shuleni ili kufikia

lengo la kuwa na uwiano wa kitabu kimoja kwa kila mwanafunzi kwani hivi sasa uwiano bado ni kitabu

kimoja kwa wanafunzi watano.

11

Hizi ni risiti za shule 5 ambazo ziliweza kupatikana katika shule 5 kati ya 24 za wilaya nne tofauti, hivyo zimetumika kama

sampuli kuwakilisha bei ya wastani kwa shule zote. Risiti 5 ni asilimia 20.8 ya risiti zote ambazo zilitakiwa kuoneshwa na

wakuu wa shule 24

12

Jumla hii imepatikana kwa kujumlisha fedha zote ambazo ziliripotiwa kutumika kununua vitabu na wakuu wa shule

katika mwaka wa fedha 2009/2010.

13

Hii ni asilimia ya fedha zilizofujwa kwenye ununuzi wa vitabu=(12.3/25.7) x100 %= 47.9%

11

Jedwali 5: Ulinganifu wa idadi ya vitabu vilivyonunuliwa na bei halisi

2009/10

Vitabu vilivyo

nunuliwa

katika shule

24(A)

2673

Jumla ya fedha

iliyotumika

kununua vitabu

katika shule

24 (B)

Sh milioni 25.7

Wastani wa Bei

iliyotumika

(C)

(B gawanya A)

Sh 9610

Bei

wastani

iliyopo

kwenye

risiti (D)

Sh 5000

Tofauti ya

Bei

E=(C-D)

Sh 4610

Ufujaji(D)

(E x A)

Sh milioni 12.3

Picha namba 3: Kuonyesha risiti na bei halisi ya vitabu

3.3 FEDHA ZA MAENDELEO

3.3.1 Hali ya Ujenzi wa Miundo Mbinu

Huku hali ya miundo mbinu ikiwa si ya kuridhisha katika shule za msingi, hali ya utekelezaji wa

ujenzi wa miundo mbinu iliyobainishwa katika MMEM II si ya kuridhisha. Katika miaka mitatu ya

utekelezaji wa MMEM II, kati ya shule 24, ni shule 1 tu ilipata fedha za ujenzi wa madarasa. Pia shule

1 ilipata fedha za ujenzi wa nyumba za walimu na shule 2 zilipata fedha za ujenzi wa vyoo na kupokea

madawati kutoka wilayani. Katika matumizi ya fedha hizi, nyumba 1 tu ya walimu imejengwa, darasa

1 limejengwa, vyoo 2 vimejengwa na madawati 24 yamenunuliwa. Hii inaonesha kuwa utekelezaji

wa MMEM II kwa miaka mitatu sio mzuri. Ufuatiliaji wa fedha za maendeleo umebainisha kuwa ni

kiwango kidogo sana cha fedha zinafika shuleni. Kwa mujibu wa takwimu za wakuu wa shule zote 24,

jumla ya Sh. milioni 15.9 tu ndizo zilipokelewa kati ya mwaka wa fedha 2007/2008-2009/2010. Kati

ya fedha hizo, ujenzi wa madarasa ni Sh. milioni 3.1, ujenzi wa nyumba za walimu ni Sh. milioni 10.6

ujenzi wa vyoo ni Sh. milioni 1.6 na Sh. 635,000 kwa ajili ya madawati. Utekelezaji hafifu wa ujenzi

wa miundo mbinu katika shule za msingi umeendelea kuathiri mazingira ya shule na hivyo kuathiri

kiwango cha ufaulu. Hivi sasa uwiano wa choo kwa wanafunzi ni 1:57 kwa wasichana badala ya 1:20,

na kwa wavulana ni 1:55 badala ya 1:20. Pia uwiano wa darasa kwa wanafunzi ni 1:73 badala ya 1:40

(BEST 2010); hii inamanisha kila mwalimu anapoingia darasani anafundisha wanafunzi 73.

12

Picha namba 4: Moja ya madarasa yanayotumika katika shule ya msingi Sofia, wilaya ya Iramba

3.3.2 Matumizi Mabaya ya Fedha za Maendeleo

Ili kupata kiasi cha fedha za maendeleo ambazo zimetumika vibaya kwa shule 24, ulinganifu wa

fedha zilizopelekwa katika shule 14 na fedha walizopokea walimu wakuu ulihusishwa. Maofisa elimu

wa kila wilaya walitakiwa kutaja fedha za maendeleo zilizotumwa kwa kila shule katika shule nne

zilizochaguliwa, na walimu wakuu nao pia walitakiwa kujaza fedha za maendeleo ambazo walipokea

toka wilayani kuanzia mwaka wa fedha 2007/2008 hadi 2009/2010. Mwaka 2007/2008 taarifa za

wilaya sita zilionesha kuwa, jumla ya Sh. milioni 8.1 zilipelekwa katika shule 24. Lakini taarifa za

walimu wakuu zilionesha kuwa jumla ya Sh. milioni 7.7 zilifika shuleni kwa mwaka 2007/2008. Hivyo,

kwa mwaka 2007/2008 jumla ya Sh. 400,000 hazikufika shuleni licha ya kuwa zimeripotiwa na wilaya

kuwa zilipelekwa shuleni. Pia mwaka 2008/2009 fedha zilizopelekwa shuleni ni Sh. milioni 8 na fedha

zilizofika shuleni ni Sh. milioni 6.6, hivyo kiasi cha Sh. milioni 1.4 hakikufika shuleni.

Mwaka wa fedha 2009/2010, Sh. milioni 25.3 zilipelekwa shuleni lakini kiasi cha Sh. milioni 1.6 tu

ndizo zilifika shuleni. Hivyo, kiasi cha Sh. milioni 23.7 hakikufika. Hii inamaanisha kuwa katika miaka

mitatu, hali ya matumizi mabaya ya fedha za maendeleo imekuwa ukiongezeka kila mwaka na kwa

mwaka 2009/2010 iliongezeka maradufu (asilimia 361) tofauti na mwaka 2008/2009. Jedwali namba

8 linaonyesha kuwa wilaya za Iramba, Bunda na Njombe zilitumia fedha vibaya ambapo kwa wilaya ya

Iramba milioni Sh. 16.2 hazikufika shuleni, wilaya ya Bunda ni Sh.milioni 8.9 na wilaya ya Njombe

Sh. Milioni 2.7.

14

Kwa mujibu wa ripoti ya wilaya kuhusu fedha zilizopelekwa shuleni.

13

Jedwali 6.

Mwaka wa

fedha

2007/2008

2008/2009

2009/2010

Jumla

Tofauti kati ya fedha za maendeleo zilizopelekwa shuleni na fedha halisi zilizopokelewa

na walimu wakuu.

Chanzo: Takwinu za Ufuatiliaji

Fedha za Maendeleo

zilizopelekwa katika shule 24 (A)

8.1milioni

8 milioni

25.3 milioni

41.5 milioni

Fedha za Maendeleo zilizofika

katika shule 24 (B)

7.7 milioni

6.6 milioni

1.6 milioni

15.9 milioni

Tofauti

(A-B)

400,000

1.4 milioni

23.7 milioni

25.5 milioni

Chati namba 5. Tofauti kati ya fedha za maendeleo zilizopelekwa shuleni na fedha halisi zilizopokelewa

na walimu wakuu.

Fedha Maendeleo

(Sh. Milioni)

30

25

20

15

10

5

0

25.4

8.1 7.7

8

6.6

1.6

2007/2008 2008/2009 2009/2010

Fedha za Maendeleo zilizopelekwa shuleni

Fedha za Maendeleo zilizofika shuleni

14

Jedwali 7: Tofauti kati ya fedha za maendeleo zilizopelekwa shuleni toka wilayani na fedha halisi

zilizopokelewa na walimu wakuu.

Mwaka 2007/2008 hadi Mwaka 2009/2010

WILAYA SHULE Fedha iliyopelekwa

shule toka wilayani(A)

Fedha iliyofika

shule(B)

Tofauti(A- -B)

MOROGORO KAMBARAGE 3,000,000 3,300,000 (300,000)

MSAVU A 0 0 0

KINGOLWIRA 0 0 0

MCHIKICHINI B 0 0 0

Jumla 3,000,000 3,300,000 (300,000)

NZEGA ISESE Hakuna taarifa 1,598,166 0

NYASA Hakuna taarifa 260,000 0

IMELI Hakuna taarifa 0 0

MWAMALA Hakuna taarifa 0 0

Jumla Hakuna 1,858,166 0

NJOMBE LUSISI 429,382 0

IGIMA 1,218,038 0

SOVI 473,038 0

LUNGUYA 553,038 0

Jumla 2,673,496 0

429,382

1,218,038

473,038

553,038

2,673,496

BABATI KWARAA 0 0 0

GALAPO 0 0 0

LUXMANDA 0 0 0

GIDGWAR 0 0 0

Jumla 0 0 0

IRAMBA SOFIA 3,166,000 0 3,166,000

KYENGEGE 13,375 ,000 375,000 13,000,000

SALALA 0 0 0

KIOMBOI 0 0 0

Jumla 16,541,000 375,000 16,166,000

BUNDA MAZOEZI 5,267,743 3,600,000 1,667,743

BALILI A 6,661,429 0 6,661,429

KASUNGUTI 3,693,177 3,123,000 570,177

KIBARA 3,671,971 3,671,000 0

Jumla 19,294,320 10,394,000 8,899,349

JUMLA KUU 41,408,816 15,927,166 25,481,655

Chanzo: Takwimu za Ufuatiliaji

15

3.4 MICHANGO YA WAZAZI

3.4.1 Mwamko wa Wazazi Kuchangia Elimu

Kwa mujibu wa takwimu za walimu wakuu wa shule 24, Jedwali namba 8 linaonesha kwamba wastani

wa jumla ya Sh. milioni 13 zilikusanywa toka kwa wazazi mwaka wa fedha 2007/2008 hadi 2009/2010.

Hivyo, fedha za michango ya wazazi katika miaka mitatu ilikuwa ni asilimia 16.4 ya jumla ya wastani

wa fedha ruzuku ya wanafunzi zilizopokelewa katika shule 24. Ili kuhakiki kiwango hiki cha michango,

walimu wakuu waliulizwa kama wanatoa risiti kwa wazazi wanaochangia. Walimu wakuu 13 tu kati ya

24 ndio wanatoa risiti. Moja ya sababu iliyobainishwa na walimu wakuu ni kwamba ununuzi wa vitabu

vya risiti na mihuri ya shule ni gharama. Hivyo, ni afadhali watumie daftari kuorodhesha michango

hiyo. Wastani wa fedha wanayochangia wazazi ni kati ya Sh. 2000 hadi 9000 kwa mwaka kwa kila

mwanafunzi. Gharama za uchangiaji zinakuwa kubwa sana kama mzazi ana watoto wengi shuleni au

wanaojiandaa kufanya mitihani ya darasa la saba kwa sababu kuna mitihani mingi sana ya maandalizi,

na hivyo wazazi hulazimika kuchanga fedha nyingi zaidi pindi watoto wao wanapokuwa darasa la saba.

Kisanduku 4

“Michango hii inatuumiza sana kama mimi nina watoto watatu na wawili wako darasa la saba hivyo kwa

mwaka huu wa 2010 nimechangia kama Tsh 9,000 kwa kila mtoto, na huyu wa darasa la pili nimechangia Tsh

4,000.” (Mzazi, Nzega)

“Nimekuwa ninachangia kila mwaka, wakati mwingine nachangia Tsh 3,000 au Tsh 7,000 inategemea mtoto

kama ana mitihani mingi na majaribio mengi. Pia ninachangia kwa mchango wa mlinzi na maji.” (Mzazi,

Morogoro)

Jedwali 8. Tofauti kati ya fedha za maendeleo zilizopelekwa shuleni na fedha halisi zilizopokelewa

na walimu wakuu.

2007/2008

2008/2009

2009/2010

Wastani

Ruzuku iliyofika

shule

84.2 milioni

88 milioni

64.2 milioni

78.8 milioni

Chanzo: Takwinu za Ufuatiliaji

Michango ya

wazazi

11.8 milioni

13.6 milioni

14 milioni

13.1 milioni

Uwiano wa michango ya wazazi na

ruzuku(katika asilimia)

14%

15.5%

21.8%

16.4%

16

Licha ya kwamba MMEM II inataka wazazi wachangie kwa kiwango cha asilimia 20 katika ujenzi wa

miundo mbinu, wazazi wengi bado wana mwamko mdogo wa kutoa michango ya ujenzi na ununuzi

wa miudombinu. Na wanaona kuwa ujenzi wa miundombinu bado ni jukumu la serikali. Kati ya

wazazi waliohojiwa, asilimia 65 walibainisha kuwa ujenzi wa miundo mbinu ni jukumu la serikali.

Kati ya wilaya sita, wazazi wa wilaya ya Babati, Bunda na Nzega wana mwamko mdogo sana wa kutoa

michango ambapo kati ya wazazi waliohojiwa, asilimia 52 ya wazazi ndio walitoa michango kwa mwaka

2009/2010. Mwamko ni mkubwa sana katika wilaya ya Njombe, na Iramba ambapo karibu asilimia

98 ya wazazi waliohojiwa walitoa michango kwa mwaka 2009/2010. Uchunguzi umebainisha kuwa

wilaya zinazotekeleza mpango wa chakula shuleni ndizo ambazo wazazi wana mwamko mkubwa na

hivyo kinachowasukuma wazazi kuchanga ni kwa ajili ya gharama za uandaaji wa chakula cha mchana

kwa wanafunzi ili kuepuka usumbufu wa kuwaandalia watoto chakula cha mchana na pia wanaona ni

sehemu ya majukumu yao ya kila siku.

Kisanduku 5.

“Mpango huu wa chakula umeondoa usumbufu kwa wanafunzi kurudi nyumbani mchana kwa ajili ya chakula

na kurejea tena shuleni, ikizingatiwa kuwa wanafunzi wengi hasa kwa shule za vijijini wanakaa mbali na shule

wanazosoma. Pia mpango huu umesaidia sana kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaohudhuria darasani

sambamba na kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu kwa shule zinazotekeleza mpango huu”. (Mwalimu Mkuu,

Njombe).

4.0 ULINGANISHI WA MMEM I NA MMEM II

Ili kulinganisha MMEM I na MMEM II, ripoti hii inatumia ufuatiliaji wa fedha za utekelezaji wa

MMEM I uliofanywa na REPOA 16 . Zifuatazo ni baadhi ya tofauti kuu za utekelezaji wa MMEM I na

MMEM II.

Katika utekelezaji wa MMEM I, fedha za ruzuku kutoka serikali kuu kwenda ngazi ya wilaya zilitolewa

kama zilivyoainishwa katika mpango. Wastani wa ruzuku iliyopelekwa wilayani kwa kila mwanafunzi

kwa miaka yote ilikuwa Sh. 8,700. Hali ni tofauti kwa MMEM II ambapo wastani wa fedha za ruzuku

zilizopelekwa wilayani ni Sh. 5,005 kwa kipindi cha miaka mitatu ya utekelezaji.

Upelekaji wa fedha za maendeleo shuleni ulikuwa mzuri zaidi katika MMEM I tofauti na MMEM II.

Katika MMEM I, karibu asilimia 85 ya fedha za maendeleo zilizopangwa zilifika mashuleni. Lakini

katika utekelezaji wa MMEM II kuna shule ambazo hazijawahi kupokea fedha zozote katika kipindi

cha miaka mitatu ya utekelezaji wake.

16

REPOA (2004), Public Expenditure Tracking Survey.

17

Kati ya shule 24 zilizohusishwa katika ufuatiliaji, ni shule 5 tu ndizo zilipata fedha za maendeleo.

Hivyo, shule 19 hazijawahi kupokea fedha za maendeleo. Kwa kuwa MMEM I ilitekelezwa kwa

kutengewa fedha maalumu zilizotoka kwa wahisani wa maendeleo na MMEM II unatekelezwa kwa

kutengewa fedha za mfuko wa pamoja wa bajeti (GBS). Ni dhahiri kuwa hii inaweza kuwa ni moja

ya sababu inayoathiri utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu kwa serikali kutenga fedha kidogo za

utekelezaji wa MMEM II tofauti na mpango ulivyobainisha. Katika utekelezaji wa MMEM I, fedha za

wahisani zilielekezwa moja kwa moja kwenye utekelezaji wa mpango, lakini kwa MMEM II, wahisani

wanapaswa kuchangia fedha kwenye mfuko wa pamoja wa bajeti na serikali ndio inaamua kutenga

fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.

5.0 HITIMISHO NA MAPENDEKEZO

5.1 Hitimisho

Ruzuku inayotolewa haiendani na maelekezo ya MMEM II. Katika miaka mitatu ya utekelezaji wa

MMEM II, wastani wa ruzuku inayofika ngazi ya wilaya toka serikali kuu ni Sh. 5,005, hivyo serikali

imekuwa inatoa asilimia 50 ya fedha za ruzuku kwa kila mwanafunzi iliyoanishwa katika MMEM II

ambayo ni Sh. 10,000. Fedha za ruzuku kwa mwanafunzi hupungua kadri inavyoelekezwa shuleni

toka ngazi ya wilaya. Tofauti hii inajitokeza ngazi ya wilaya ambapo mwaka 2008/2009 asilimia 8 ya

fedha haikufika shuleni na mwaka 2009/2010 ni asilimia 16. Kama fedha hii ilipangwa kutolewa kwa

ajili ya kuboresha elimu ya msingi kwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ni dhahiri

kuwa utekelezaji wa MMEM II hautafikia malengo yake kama vile kupunguza uwiano wa kitabu

kwa mwanafunzi toka 1:5 hadi 1:1. Kuendelea kuwa na mazingira duni ya kufundishia na kujifunzia

kutaendelea kuathiri upatikanaji wa elimu bora na pia viwango vya ufaulu, na hivyo kufanya wanafunzi

wengi washindwe kuendelea katika ngazi ya sekondari.

Licha ya kwamba MEMM II umebainisha kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu,

hadithi imekuwa kinyume. Serikali inatoa kiwango kidogo cha fedha za maendeleo kwa ajili ya ujenzi

wa miundombinu ya shule. Ufuatiliaji wa fedha za maendeleo umebainisha kuwa kiwango kidogo sana

cha fedha za maendeleo zinafika shuleni. Kwa mujibu wa takwimu za wakuu wa shule zote 24, jumla

ya Sh. milioni 15.9 tu ndizo zilizopokelewa kati ya mwaka wa fedha 2007/2008-2009/2010. Kama

serikali inatoa fedha kidogo kwa ajili ya uboreshaji wa miundo mbinu, je tutaweza kutekeleza MMEM

II kwa kuzingatia viashiria vya kupima utekelezaji wa MMEM II katika kuboresha miundo mbinu

kwa kujenga nyumba za walimu 87,744, madarasa 60,896, vyoo 107,224 na madawati 821,877?

Kushindwa kuboresha miundombinu hii shuleni kutaendelea kuathiri hali ya ufundishaji kwa walimu,

na pia watoto wataendelea kusoma katika mazingira magumu. Hali hii itaendelea kuathiri upatikanaji

wa elimu bora hapa nchini.

Kwa kuwa wazazi wanachangia michango mbalimbali, elimu ya msingi si bure hapa nchini. Wazazi

wengi bado wanasumbuliwa kutoa michango mbalimbali kwa ajili ya uendeshaji wa shule kama vile

kuchangia gharama za mitihani. Mzazi anapokuwa na mtoto aliye darasa la saba anakuwa na mzigo

18

mkubwa sana kwani analipia fedha nyingi ili mtoto aweze kufanya mitihani mbalimbali ya kujiandaa

na mtihani wa kumaliza elimu ya msingi. Kama fedha ya ruzuku kwa wanafunzi kiasi cha Sh. 10,000

ingekuwa inafika shuleni na kutumika kama inavyobainishwa na MEMM II, ni dhahili kuwa wazazi

wasingesumbuliwa kutoa michango. Na hapa ndio tungeweza kujidai kwa kusema sasa Tanzania inatoa

elimu bure.

5.2 Mapendekezo

Mapendekezo haya yanatolewa ili kusaidia utekelezaji wa MMEM III 17 ambayo itaanza kutekelezwa

baada ya kumalizika kwa MMEM II. Pia itasaidia utekelezaji wa MMES II ambapo utekelezaji wake

umeanza mwaka wa fedha 2010/2011.

a) Serikali haina budi kuwajibika ipasavyo kwa wananchi ili kuhakikisha kuwa utekelezaji wa

mipango mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya elimu inafanikiwa. Hili litafanikiwa pale serikali

itakapoamua kuheshimu mipango ya maendeleo. MMEM I ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa

sababu serikali ilipeleka fedha za ruzuku na maendeleo shuleni kama ilivyobainishwa katika

mpango.

b) Hivi sasa serikali inaandaa MMEM III ambapo utekelezaji wake utaanza baada ya MMEM II

kumalizika 18 na ili kufanikisha utekelezaji wake, wahisani hawana budi kuhimiza fedha zao za

maendeleo zipelekwe moja kwa moja kwenye mpango husika na si kutumia mfuko wa bajeti wa

pamoja. MMEM I ilifanikiwa kiutekelezaji na pia fedha za ruzuku zilizopangwa kwenye mpango

ndizo zilizofika mashuleni kwa sababu ilitumia mtindo wa wahisani wa maendeleo kupeleka

fedha moja kwa moja kwenye mpango au mradi.

c) Kwa kuwa ruzuku inachelewa kutoka wilayani kwenda shuleni, serikali haina budi kubadilisha

mfumo wa upelekaji wa ruzuku shuleni ili kuondokana na ucheleweshaji wa ruzuku. Hii pia

itapunguza matumizi mabaya ya ruzuku katika ngazi ya wilaya. Hili linawezekana kwa sababu

shule zote zina akaunti za benki, hivyo ruzuku ipelekwe moja kwa moja shuleni toka serikali

kuu. Kama serikali itaridhia kutuma fedha za ruzuku moja kwa moja, kuna haja pia ya kuanzisha

mfumo huru wa ufuatiliaji wa ruzuku katika ngazi ya serikali kuu na shule utakaokuwa unahakiki

matumizi ya ruzuku zinazofika shuleni na jinsi zilivyotumika ili kupunguza matumizi mabaya

katika ngazi ya shule na pia kuhakiki fedha zinazotolewa na serikali kuu kwenda ngazi ya shule.

d) Kalenda ya shule za msingi huanza mwezi Januari na kuisha mwezi Desemba wakati kalenda ya

serikali ya mwaka wa fedha inaanza Julai 1 hadi Juni 31. Ili kurahisisha upangaji wa mpango wa

shule na utekelezaji wake serikali haina budi kubadilisha mtindo wa utoaji wa fedha za ruzuku

kwa kutoa fedha za ruzuku kwa awamu moja katika mwezi Januari badala ya mtindo wa robo

mwaka kwa kufuata kalenda ya serikali. Fedha nyingi hazitumiki kwa sababu zinachelewa kufika

na pia kalenda ya shule na ile ya mwaka wa fedha wa serikali zinapishana.

17

Hotuba ya bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya mwaka 2010/2011

19

e) Wasimamizi katika utekelezaji wa MMEM II hasa walimu wakuu hawana budi kupewa maelekezo

na miongozo ya kutosha juu ya MMEM, ili waweze kuufuatilia, kutekeleza na kuusimamia vizuri

katika misingi bora na yenye tija kwa maendeleo ya elimu nchini. Baadhi ya viongozi ngazi ya

wilaya wanafurahia uelewa mdogo wa watendaji hawa kuhusu MMEM kwa manufaa yao binafsi.

20

Marejeo

REPOA (2004). Ripoti ya Ufuatiliaji wa fedha za Umma, Utekelezaji wa MMEM I mwaka 2002

na 2003.

URT (2006). Mpango wa pili wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi (MMEM II).

URT (2009). Ripoti ya Utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi kwa

Mwaka 2007/2008.

URT (2010). Ripoti ya Ufuatiliaji wa Fedha za Umma kwa Mwaka wa fedha 2007/2008, Wizara

ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

URT (2009). Ripoti ya Utekelezaji katika Sekta ya Elimu mwaka 2008

URT (2010). Ripoti ya Utekelezaji katika Sekta ya Elimu mwaka 2009

URT (2010) Basic Education Statistics of Tanzania for 2010

21

Viambatisho

Kiambatisho 1. Sampuli ya Mikoa na wilaya zilizohusishwa kwenye ufuatiliaji

Kanda

Sampuli ya Mikoa

Sampuli ya Wilaya

Idadi ya shule

Ziwa

Mara

Bunda

4

Magharibi

Tabora

Nzega

4

Mashariki

Morogoro

Manispaa ya Morogoro

4

Nyanda za juu-kusini

Njoluma

Njombe

4

Kati

Singida

Iramba

4

Kaskazini

Manyara

Babati

4

Jumla ya Shule

24

Kiambatisho 2. Malengo ya utekelezaji wa MMEM II

Mwaka

Madarasa

Nyumba

Vyoo

Madawati

2007/08

16,485

21,936

29,328

211,467

2008/09

16,485

21,936

29,328

211,467

2009/10

16,485

21,936

29,328

223,122

2010/11

11,441

21,936

19,240

175,815

Jumla

60,896

87,744

107,224

821,871

22

Moja ya malengo makuu ya Mpango wa pili wa Maendeleo ya Msingi (MMEM II) ilikuwa ni kuboresha

hali ya mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa kujenga miundombinu kama vile madarasa, nyumba

za walimu, vyoo na madawati. Pia ilidhamiria kuboresha mchakato wa kujifunzia na kufundishia kwa

kuongeza vifaa kama vile vitabu vya kiada na ziada kwa ajili ya wanafunzi. Ili kutekeleza adhima hii,

MMEM II, ilibainisha kuwa Sh. 10,000 itatolewa kwa kila mwanafunzi wa shule ya msingi kila mwaka

kwa kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa MMEM II kwa ajili ya kununua vitabu, kukidhi gharama

za mitihani, kufanyia ukarabati mdogo na gharama za utawala.

Ikiwa miaka mitatu ya utekelezaji wa MMEM II imepita, hali halisi ya utekelezaji wa MMEM II bado

ina changamoto nyingi. Hivi sasa uwiano wa choo kwa wanafunzi ni 1:57 kwa wasichana badala ya

1:20, na kwa wavulana ni 1:55 badala ya 1:20. Pia uwiano wa darasa kwa wanafunzi ni 1:73 badala

ya 1:40 na uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi ni 1:5 badala ya 1:1. Kama bajeti ya sekta ya elimu

inaongezeka mwaka hadi mwaka na utekelezaji wa MMEM II si wa kuridhisha, fedha hizi zinatumikaje?

Je, fedha zinazopangwa katika bajeti zinawafikia walengwa? Uhitaji wa majibu ya maswali haya ndio

yalishawishi HakiElimu kufuatilia matumizi ya fedha za umma(PETS) katika wilaya sita ambazo ni

Njombe, Morogoro, Nzega, Bunda, Iramba na Babati.

Matokeo ya jumla yanaonesha kuwa ni wastani wa Sh. 4,736 ndizo zilifika shuleni kama ruzuku kwa

mwanafunzi badala ya Sh.10,000. Pia hali ya utekelezaji wa miundo mbinu si ya kuridhisha ambapo katika

shule 24 za wilaya sita ni nyumba 1 tu ya walimu imejengwa, darasa 1 limejengwa, vyoo 2 vimejengwa

na madawati 24 yamenunuliwa kati ya mwaka 2007/08 hadi 2009/2010. Licha ya kwamba fedha kidogo

zinafika shuleni, hali ya matumizi si ya kuridhisha ambapo kwa kila Sh. 100 inayofika shuleni kwa ajili ya

ununuzi wa vitabu Sh. 48 inatumika vibaya.

Matokeo ya ripoti hii yanaweza kutumika kama nyenzo muhimu kwa ajili ya utekelezaji wa mipango

mingine ya maendeleo kama MMEM III na MMES II ili kuboresha sekta ya elimu hapa nchini.

HakiElimu inawezesha wananchi

kuleta mabadiliko katika elimu

na demokrasia

SL P 79401, Dar es Salaam, Tanzania

Simu. (255 22) 2151852/3 • Faksi (255 22) 215244

info@hakielimu.org • www.hakielimu.org

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!