19.06.2014 Views

rufiji environment management project - Coastal Forests of Kenya ...

rufiji environment management project - Coastal Forests of Kenya ...

rufiji environment management project - Coastal Forests of Kenya ...

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

REMP Technical Report 40: Rangeland Resources in Rufjiji

Muhtasari Wa Taarifa

MSHAURI BINGWA WA UOTO WA NYANDA ZA MALISHO KUHUSU

TATHMINI YA UOTO WA NYANDA ZA MALISHO KATIKA MAENEO

YALIYOTAJWA KWA LENGO LA KUWA NA MKAKATI WA

KUSIMAMIA NAKUENDE LEZA MIFUGO WILAYA YA RUFIJI

Wilaya ya Rufiji ni miongoni mwa wilaya sita zinazounda Mkoa wa Pwani na ambayo iko kusini zaidi

ya wilaya zingine. Wilaya hii ina ukubwa wa eneo za mraba km² 13,339 na imegawanyika katika

makundi manne(4) ya aina za udongo kama ifuatavyo:-

• Udongo wa kichanga uliokosa mbolea uliogubikwa na miti aina ya Miombo na aina nyingine za

Misitu ya Pwani yenye ukubwa wa eneo km² 4,250 (pamoja na eneo la Selous Game Reserve

lenye ukubwa wa eneo za mraba km² 3,400).

• Udongo mwekundu laini wa kichanga wenye asili ya kugubikwa na Misitu ya Pwani wenye

ukubwa wa eneo la mraba km² 2,700.

• Bonde la Mafuriko la Mto Rufiji lenye udongo tifu tifu uliochanganyika na udongo wa

mfinyanzi wenye ukubwa wa eneo la mraba km² 1,700. Aina hii ya udongo una kiasi kidogo

cha mchanga uliotawaliwa na nyasi ndefu na miti ya hapa na pale.

• Udongo laini wa kifinyanzi wa chumvi chumvi ulioko maeneo ya Delta uliogubikwa na misitu

ya mikoko (kapa) na mbuga za nyasi zenye ukubwa wa km² 1,300.

Wilaya inapata wastani wa mvua kati ya mm 1200 kwa maeneo ya pwani mpaka mm 600 magharibi

mwa maeneo ya mafuriko ya Mto Rufiji. Wilaya huwa inapata mvua za aina mbili yaani mvua kubwa

za Masika zinazoanza katikati ya mwezi wa March na kumalizika mwishoni mwa mwezi Mei; pia kuna

mvua za Vuli zinazoanza katikati ya mwezi wa Novemba na kukatika mwezi Januari.

Ni eneo kiasi tu ya bonde la Mafuriko la Mto Rufiji ndilo lenye udongo wenye rutuba nzuri inayofaa

kwa kilimo. Tena ni kwa sababu ya kilimo cha kupumzisha ardhi au kulazimishwa kupumzishwa kwa

sababu ya mafuriko ya mwaka yanapotokea ambayo husababisha maeneo hayo kutokulimwa. Kiasi

cha makisio ya hektari 45,000 ambazo ziko katika ukanda wa Mafuriko zinazofaa kwa Kilimo ni

hektari 15,000 ndizo zinazolimwa kila mwaka. Kiasi cha hektari zipatazo 25,000 zilizo na misitu ya

pwani na ambazo zimetawaliwa na Milima ya Kaskazini yenye udongo mwekundu zimefyekwa kwa

ajili ya kilimo. Kutokana na hali hiyo kuna maeneo machache yaliyobaki ambayo kiendelevu yanafaa

kwa kilimo wilayani.

Kwa asili, wananchi wa wilaya hii huwa wanapata viini lishe vya protini kutokana na uvuvi, uwindaji

na ufugaji wa kuku. Ni wananchi waishio katika Delta tu walio na ng’ombe ,mbuzi na kondoo.

Sababu moja inayowafanya wananchi wa maeneo hayo kutokufuga wanyama wakubwa (mbuzi,

kondoo na ng’ombe) ni uwingi wa mbung’o. Kwa hiyo ni wazi kuwa idadi ya wanyama wakubwa kwa

asili ni kidogo/asilimia chache ya wanyama wakubwa zaidi sana wanamilikiwa na wafanyakazi

wahamiaji wa serikali.

Tangu mwaka 2002 kumekuwa na mabadiliko makubwa kutokana na wafugaji wa jadi na wakulima

wafugaji kuingia wilayani toka mikoa na wilaya zingine kwa ajili ya kutafuta malisho na maji.

Wafugaji hao wameingia na idadi kubwa ya mifugo.

Mpaka sasa wilaya inakadiriwa kuwa na idadi ifuatayo ya mifugo:-

iv

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!