19.06.2014 Views

rufiji environment management project - Coastal Forests of Kenya ...

rufiji environment management project - Coastal Forests of Kenya ...

rufiji environment management project - Coastal Forests of Kenya ...

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

REMP Technical Report 40: Rangeland Resources in Rufjiji

Kwa ujumla matokeo hayo yanahusu upimaji wa nyasi tu, yanaonyesha kwamba Rufiji ina maeneo

machache yanayoweza kulisha mifugo katika usimamizi wa aina ya “extensive” yaani eneo kubwa

linahitajika kwa wanyama wachache. Maeneo mengi yaliyotathminiwa yalionyesha kuwa yana uoto

mzuri wa nyanda za malisho kwa sababu pengine yalikuwa hayajatumika na wanyama kwa muda

mrefu. Mengine yalikuwa na mapungufu/ au matatizo yaliyojitokeza.

Maeneo ya nyanda za malisho yanayoweza kufikiriwa kuwa yanafaa kwa idadi kadhaa ya mifugo

yametajwa. Eneo lo lote lisitumike kama nyanda za malisho kabla ya tathmini kufanyika kwa

wanyama kulisha katika eneo husika kwa muda maalaum. Kabla ya eneo kutangazwa kuwa nyanda za

malisho utafiti wa kina wa kijamii na kiuchumi lazima ufanyike. Miundo mbinu kwa ajili ya mifugo

katika maeneo yote zilikuwa hakuna. Utafiti huu umeorodhesha mahitaji ya kila kijiji ikijumuisha

majosho, maeneo ya maji, uzuiaji wa mbung’o. Minada inayohitajika na mapendekezo ya wapi

kujengwa yametajwa.

Ushauri ufuatao umependekezwa ili kusaidia Halmashauri ya Wilaya kutengeneza mkakati wa

Kusimamia na Kuendeleza Ufugaji Endelevu.

• Halmashauri ya Wilaya itoe tamko la kuzuia uingiaji wa wafugaji wa asili kutoka Mikoa

mingine hadi hapo Halmashauri, ikishirikiana na vijiji vikamilishe Mkakati wa Kusimamia na

Kuendeleza Ufugaji ambao utatoa matumizi bora na endelevu ya Nyanda za Malisho yaliyopo.

Wakati huo huo wafugaji jadi ambao wamekwishaingia inabidi washirikiane pamoja na wenyeji

wa maeneo husika ili kutenga mipaka kwa ajili ya kugawa maeneo kwa matumizi mbali mbali

kama vile maeneo ya kilimo, uvuvi, misitu, malisho, vyanzo vya maji na njia za mifugo.

• Ramani za uoto wa asili zianzishwe ili zisaidie kama mwongozo kwa Halmashuri ya Wilaya

katika kupanga mipango, utekelezaji na uchanganuaji wa matokeo yaliyofanywa juu ya Utafiti

wa Nyanda za Malisho. Kwa taarifa hizo Halmashauri ya Wilaya pamoja na vijiji vitaweza

kufanya maamuzi yanayofaa hususan usimamizi wa nyanda za malisho yanahitaji kuhusu

mabadiliko ya uoto, msimu hadi msimu. Taarifa za takwimu yazingatiwe mabadiliko

yanayoweza kufuatana na uchomaji moto malisho na wafugaji wa jadi. Hii inaweza kuwa moja

ya njia ya kuelewa matokeo yanayosababishwa na uchomaji moto kwa Wilaya nzima.

• Halmashauri ya Wilaya itenge maeneo ambayo wafugaji wa jadi hawaruhusiwi kuingia na

kukaa, kuruhusiwa kuchungia kwa misimu/majira mbali mbali, kuruhusiwa kwa masharti

yaliyolotolewa na Halmashauri au sheria ndogo za vijiji. Wilaya izingatie kanuni za tahadhari

zinazohusu uzuiaji wa wafugaji wa jadi kuingia katika maeneo ambayo yana wingi wa

bioanuai.

• Pia iwekwe taratibu na kanuni za pekee kuepuka uharibifu wa mazao na upondaji wa miche

katika tambarare ya Mafuriko. Kilimo cha Mlao kitakuwa kigeni kwa wafugaji wa jadi wengi.

• Watumiaji wote wote wa nyanda za malisho wanashauriwa wakae pamoja ili kujadili, kuratibui

na kukisia mabadiliko. Kwa asili mabadiliko mengi ni ya muda mrefu, hivyo mipango ya

kuratibu mbuga inafaa iwe ya muda mrefu. Inafaa watumiaji wa nyanda za malisho wakae

mara kwa mara ilio kujadili na kupima hali ya nyanda kwa vipindi maalum. Halmashauri ya

Wilaya iwe na mpango na bajeti kwa ajili ya kuratibu masuala hayo na inafaa watafutwe

wahisani waweze kusaidia.

• Wafugaji wa jadi, wakazi wa vijiji husika na wataalam wa ugani inafaa wafikirie mahitaji ya

watumiaji wengine wa Nyanda za malisho na ardhi kama vile wachota maji, wavuvi, vimelea

vya mimea na wanyama wadogo, ukadiriaji wa idadi ya mifugo ambao wanaweza kutunzwa

vi

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!