Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
BARUA YA MHARIRI
Hello!
Mpendwa msomaji, natumai ni mzima wa
afya na mwingi wa furaha kuwasiliana na
wewe tena katika toleo hili la pili. Nashukuru
kwa kuendelea kuwa sehemu ya wasomaji
wetu tangu tulipotoa toleo la awali, bila wewe
jarida hili halina maana yoyote.
Maoni yaliyotolewa katika jarida lililopita
yametusaidia sana kuboresha toleo hili,
kuanzia usanifu, agenda na idadi ya kurasa.
Tutaendelea kupokea maoni na kuyafanyia
kazi kwa kadri tutakavyoweza. Lengo ni
kuwapa vitu bomba; vyenye kuelimisha,
kuburudisha na kukupa hamasa ya kuwa
sehemu ya mabadiliko katika jamii.
Toleo la pili limejikita katika mambo ya
kidijitali. Kama tunavyofahamu, siku hizi kila
kitu ni kidijitali. Tanzania ni moja ya nchi
ambazo matumizi ya intaneti na simu za
mkononi yanakua kwa kasi kubwa.
Watumiaji wakubwa ni vijana kuanzia miaka
18 mpaka 35. Licha ya fursa lukuki zilizopo
katika ulimwengu wa teknolojia ya kidijitali, ni
vijana wachache wanaochangamkia na
kuzifikia fursa zilizopo. Walau kwa vijana wa
kiume, kwa wakike bado wapo nyuma zaidi.
Toleo hili ni mahsusi kukufungulia njia kijana
mwenzetu kusanuka na kuzibaini fursa
zilizopo ili kukabiliana na tatizo la ajira
ambalo vijana ni wahanga wakubwa.
Nakukaribisha katika ulimwengu wa fursa.
Hassan Kiyungi
2 | MEMA MAGAZINE AUG 2021
YALIYOMO
05 STORY ZA MTEMBEZI | KUNANI MUHEZA?
07 CHIMBO | FURSA ZA KIDIJITALI
09 MMOJA KWA MMOJA
| FURSA NDANI YA UDAKU
14
10 JIBEBE | IMANI NSAMILA: SAFARI YA BWANA LENS
12 TUBONGE | MASWALI NA MAJIBU KUHUSU DIJITALI
13 KOLEZO
| URAIBU WA KIDJITALI, TUNATOBOAJE?
14 GENGE | G.NAKO: MWEUSI MWENYE LADHA ADIMU
16 SOCIAL HIT
| HABA NA HABA HUJAZA KIBABA
19
17 KIZAZI KIPYA | MWAISA MTU MBAD NA STORY ZA MAWIFI
19 WAKILISHA
| TWENZETU MIKOCHENI
MSAFIRI MWENYE VIPAJI LUKUKI | VIPAJIKA
WANAWAKE NA DIJITALI | SAUTI YA MTAA
NDOTO YA MWANDISHI KWA DAKTARI R!SE
|
SMART CLASS, BUKUA KIDIJITALI | UBUNIFU
21
23
24
27
24 10
16 27
7
3 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
LAMEMANS
TUFUATE
Mema Magazine ni jarida linalotoka kila
baada ya miezi minne kwa lugha ya
kiingereza na kiswahili. Ni jarida
linalopatikana kwa njia ya mtandaoni na
nakala ngumu. Tufuatilie katika mitandao ya
kijamii ili kuwa wa kwanza kujipatia nakala
yako.
PAKUA JARIDA
www.memayouth.org/magazine
www.issuu.com/memamagazine
www.issuu.com/memamagazine
MAWASILIANO
S.L.P 36397, Dar Es Salaam
Whatsapp: +255743 813972
Simu/SMS: +255783 765953
mematanzania@outlook.com
MKURUGENZI MTENDAJI
HASSAN KIYUNGI
MHARIRI MKUU
NANCY MBOGORO
MHARIRI MSAIDIZI
ELIAS MAEDA
MHASIBU
ADIOS O. KAKILA
WAPIGA PICHA
MOHAMMED KAYUNGI
IMANI NSAMILA
DIONIZY SHOTS
WACHANGIAJI
ZENA MCHOME
ABBASI ISMAIL
GILLSANT MLASEKO
SECILIA BASILIO
MEDIA CRAFTERS
KATUNI
MWENDA ART
USANIFU
KUZA CREATIVE
UCHAPISHAJI
HNP PRINTING
@MemaMagazine
MUHIMU
Yaliyomo humu ndani ni jukumu la
Mema Tanzania ambao ni
wazalishaji na wasambazaji wa
jarida la Mema na hayawakilishi
mitazamo au maoni ya wafadhili au
wadhamini.
4 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
@MemaTanzania
MAGAZINE
Mema Magazine linachapishwa na kusambazwa na
taasis ya Mema Tanzania. Jarida hili haliuzwi, na
linasambazwa bure kwa njia ya mtandoni na nakala
ngumu. Pindi upatapo nakala hii tafadhali shirikisha na
marafiki zako wa karibu ili kupata elimu. Unaruhusiwa
kuchapisha kwa lengo la kutoa elimu tu na si kwa
biashara.
MEMA TANZANIA TOLEO No. 2 AUG, 2021
Waja leo, huondoki leo
ABBASI ISMAIL
Mambo vipi washikaji? Naitwa Abbasi maarufu Abby boy. Ni
mzaliwa na mkazi wa Muheza, mkoani Tanga. Leo
nakutembeza Muheza ujue yale usiyoyajua. Muheza ni wilaya
kongwe nchini ilianzishwa mwaka 1976. Kihistoria kulipiganwa
vita kati ya Wabondei na Wadigo katika pwani ya Tanga.
Wabondei walichakazwa na kukimbilia maeneo ya Muheza na
walipofika hapo walisema “Hanu Mheza” ikimaanisha hapa
mmekwisha. Kweli Wadigo waliufuata moto kwani
walitembezewa kichapo na kurudi pwani ya Tanga na mpaka
leo Wadigo wapo wengi Tanga mjini na Wabondei wakabaki
kama wenyeji hapa Muheza.
Ukipita Muheza utakuta imepambwa na mandhari ya kuvutia
yenye milima, mito na majengo ya kihistoria yaliyoachwa na
wakoloni. Wilaya ya Muheza ina mitaa mingi maarufu ikiwemo
Magila ambapo kuna shule ya kwanza ya msingi kujengwa
hapa nchini wakati wa ukoloni. Mitaa mingine ni Tongwe,
Ngomeni, Pande, Mtimbwane n.k. Wilaya yetu ina ukubwa wa
eneo la kilomita za mraba 1,470.
Mishe za kibiashara zipo kibao, muhimu kuchangamkia fursa.
Kuna mishe za kilimo kama machungwa, katani n.k. Muheza
ina vivutio vingi vya utalii ikiwemo misitu maarufu ya Amani na
Magoroto maarufu Bali of Africa. Huko kuna mambo mengi ya
kupendeza ambayo huwezi kujutia ikiwemo maporomoko ya
maji, bwawa zuri la kuogelea, wanyama kama farasi na ndege
wengi wazuri. Msitu wa hifadhi ya Amani una vipepeo wa
pekee duniani ambao wananchi huwafuga na kuwauza nje ya
nchi.
5 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA ni
mbunge na moja ya watu maarufu kutoka
Muheza.
Anasema "Mwanzoni nilikuwa na wateja
wachache na kupelekea kupata hasara mara
kadhaa. Nikaamua kuongeza wateja wapya
na njia rahisi niliona ni mitandao ya kijamii.
Nilifungua akaunti Instagram ndipo kasi ya
wateja ikaongezeka kutoka mikoa ya jirani na
kuniongezea mtaji mpaka wa Tsh milioni 5.”
Kuna vijana pia ambao wanatumia ushawishi
walionao katika mitandao ya kijamii
kutangaza biashara za makampuni,
kuendesha kampeni za taasis na baadhi
wameanzisha kurasa zinazochapisha maudhui
tofauti ikiwemo udaku na kujipatia wafuasi
wengi hivyo kuwafungulia dili za matangazo
ya biashara.
Kabla ya kuolewa mwaka 2018 alikuwa
akijihusisha na mauzo ya bidhaa mtandaoni.
"Nilikuwa nikifanya biashara ya kuuza nguo za
watoto na wanawake. kupitia Instagram. Akaunti
yangu ilikuwa imefikisha wafuasi zaidi ya elfu 10.
Ni biashara nilianza tangu nikiwa nasoma chuo
na nilikuwa na wateja wengi sana. Baada ya
kuolewa mme wangu hakuwa anapendezwa
navyo wasiliana na wateja mara kwa mara.
Kuepusha mikwaruzano katika ndoa yangu
nikaamua kuachana na biashara ile na kuajiriwa
katika kampuni ambayo mme wangu alinitafutia.
Changamoto za kifamilia hasa kwa wanawake
waliolewa kiukweli zinatukwamisha kujihusisha
na mambo ya dijitali labda uwe na mwenza
muelewa na mambo haya" anasema Aisha.
Utawala wa kijinsia
Licha ya fursa lukuki za kidijitali bado sio wote
wananufaika nazo. Utofauti upo zaidi katika
upande wa jinsia ambapo wanawake ni wachache
kuliko wanaume. “Kwa mtazamo wangu sababu
kama kutingwa kwa majukumu ya familia, ukosefu
wa ujuzi, hofu ya ukatili wa kijinsia zinachangia
wanawake kuwa wachache” anasema Dkt Julieth
Sebba, moja ya vijana wenye ushawishi katika
mtandao wa Twitter. Mtazamo wake unaungwa
mkono na Mariam, mkazi wa Tanga. ambaye
anaamini uchache wa wasichana na wanawake
katika dunia ya kidijitali inachangiwa na uoga wa
kushambuliwa mitandaoni hali inayowarudisha
nyuma katika kuzifilkia fursa zilizopo katika
mitandao ya kijamii.Aisha mkazi wa Tabata jijini
Dar Es Salaam, ni kijana mwenye umri wa miaka
32 ni mke na mama mwenye mtoto mmoja.
8 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
Sheria ya ngoma
Mafanikio hayaji haraka na kwa urahisi hasa
katika kuzifikia fursa za kidijitali. Unahitaji kutia
bidii katika kujifunza ujuzi fulani, hata kama ni
kutangaza biashara yako mtandaoni unapaswa
kufahamu namna gani ya kuandika maudhui,
muda gani, nani unayemlenga n.k.
Jinsi unavyofanyia kazi ujuzi wako ndivyo
unavyozidi kuwa na uelewa wa kutosha na jamii
itatambua ujuzi wako hivyo fursa zitaanza
kukufikia. Jipe muda kujifunza, usikate tamaa.
JIBEBE
IMANI NSAMILA
SAFARI YA BWANA LENS NA
MSIMULIZI WA MAZINGIRA
PETER LAZARO
Mwanzo wa Safari
Naitwa Imani Nsamila, ni mpiga picha na
mwanaharakati wa mabadiliko ya tabia nchi.
Tangu nikiwa mdogo napenda kupiga picha.
Wakati nipo shule ya sekondari baba yangu
alikuwa na kamera ndogo ambayo alikuwa
akiitumia katika ofisi yake.
Nikawa naichukua naenda kuwapiga picha
marafiki zangu ambao walikuwa wana bendi
ya muziki, baadhi ya picha zao mpaka leo
ninazo. Awali nilikuwa nafanya tu kwa
mapenzi, nilipomaliza sekondari nikachagua
kusomea fani ya utengenezaji wa filamu
katika chuo cha Kilimanjaro Film Institute
katika jiji la Arusha. Nikiwa mwaka wa tatu
sikufanikiwa kumaliza chuo, nilipata ajali na
kuvunjika mkono. Ilinilazimu nirudi nyumbani
Dar Es Salaam na madaktari walinishauri
nisibebe vitu vizito, ingekuwa ngumu
kuendelea na mafunzo ya utengenezaji filamu
kutokana na kamera tulizokuwa tunatumia
katika mafunzo zilikuwa ni nzito.
Wakati nipo nyumbani nikawa nahudhuria
katika mtandao wa vijana uliofahamika kama
Youth Climate Activist Network uliokuwa chini
ya Norwegian Church Aid. Walikuwa na
programu ya Climate Change Caravan na
tulikuwa tunazunguka maeneo tofauti nchini
kutoa elimu ya mabadiliko ya tabia
nchi.Kipindi cha ugonjwa na baada ya
ugonjwa niliendelea kuwa najitolea kama
mpiga picha.
Novemba 2014 nilitolewa vyuma mkononi na
kurudi katika maisha yangu ya kawaida.
Nikaendelea na shughuli za kupiga picha,
nikawa nakutana na watu tofauti katika mishe
zangu. Mwaka 2015 nilipata kazi ya kushoot
katika taasisi fulani ambao baada ya
kumaliza walipenda sana kazi yangu.
Nashukuru Mungu nimeendelea kupata fursa
tofauti ambazo nyingi zinatokana na watu
ambao nilifanya nao kazi kunipendekeza
zinapojitokeza fursa.
Mfano mwaka 2017 nilibahatika kushuhudia
uchaguzi wa Liberia kama mpiga picha,
uchaguzi ambao ulimpa ushindi aliyekuwa
mchezaji mpira maarufu George Weah.
10 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
Tujibebe
Kila mtu ana njia yake katika kufikia mafanikio. Bado
na ndoto ya kutimiza mambo mengi katika kazi
yangu, na hata hapa nilipofika nashukuru Mungu.
Binafsi mambo yafuatayo yamechangia kunipa
mafanikio niliyonayo sasa na pengine hata wewe
kijana mwenzangu yanaweza kuchochea ndoto
yako ya kuwa mpiga picha mashuhuri;
Michongo
Katika picha kuna fursa nyingi. Dunia
imehamia katika teknolojia na huwezi
kutenganisha picha na teknolojia. Upigaji picha
imekuwa inachangia sehemu kubwa katika
kusukuma agenda mbali mbali za kisiasa na
kijamii. Kuna fursa za kifedha lakini pia
inaweza kukupenyeza katika fursa
usiyoitegema. Kwa mfano ukihudhuria
mkutano mkubwa wa kimataifa mbali ya pesa
utakayolipwa lakini yale yatakayokuwa
yanazungumzwa utayasikia na kujifunza pia.
Kamera inakupa elimu mpya kila siku ambayo
inakufungulia fursa kibao.
Sasa hivi pia biashara zinahamia kwenye
mitandao ya kijamii. Nyenzo muhimu
inayohitajika ni picha, hivyo kwa mpiga picha
kuna dili utazipata kwa watu wanaofanya
biashara mtandaoni. Binafsi kuna programu
naifanya inayowezesha vijana wa kike
kujifunza upigaji picha na kufungua fursa kwa
upande wao kwa sababu tasnia ya picha
imetawaliwa na wanaume zaidi. Pia picha
inakusaidia kusafiri maeneo tofauti na
kujifunza mila na tamaduni za watu.
Nimefanikiwa kufika Germany, Netherlands,
France, Belgium, Czech Republic, Zimbabwe,
Italy n.k. na kote nimejifunza mambo mengi.
Kupenda unachokifanya. Hii kazi yetu unahitaji
kuipenda sana ili inapotokea hata kazi nyingi
zimekutinga una enjoy kwa sababu ni kitu
unachokipenda. Imenisaidia sana katika upigaji picha
kwa sababu siku zote ni kazi naifanya kutoka moyoni.
Muda mwingi nafanya kazi, na safiri mara kwa mara
sipumziki. Kwangu sioni tatizo kwa sababu na enjoy.
Kujitahidi kujifunza kupitia watu na kuwekeza kwenye
elimu. Kuna wengine wamepata bahati ya kusoma
chuo na wengine mitandaoni. Lakini kwa namna
yoyote uwe ni mtu wa kuitafuta elimu ya upigaji picha.
Elimu isiwe tu ya upigaji picha, kujifunza mambo
mengine kwa sababu kama mpiga picha lazima
utambulike wewe ni mpiga picha wa namna gani.
Kuna mteja anaweza kuhitaji picha ambazo zitatoa
elimu ya mabadiliko ya tabia nchi na wewe hujui nini
maana ya mabadiliko ya tabia nchi hawezi kukupa
kazi. Ukijifunza mambo tofauti ndivyo wateja tofauti
watakufuata kwa sababu ya uelewa wako wa mambo
tofauti.
Kujenga mahusiano na watu. Hizi kazi watu wanavyo
kuzungumzia wakati haupo ndio zinasaidia ndio
inavyoamua kufunga au kukufungulia fursa.
Mahusiano bora ndio kila kitu katika maisha.
Kuchagua unataka kuwa mpiga picha wa namna gani.
Mwanzoni wakati unaanza unaweza kuwa unapiga tu.
Baadae ukachagua ujikite eneo gani ambalo watu hata
wakitaja jina lako wanajua wewe ni mpiga picha wa
aina gani. Inaweza kuwa michezo, sherehe, sanaa n.k.
11 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
ULIZA UJIBIWE
NA ELIAS MAEDA
Je, una swali kuhusu
masuala ya kidijitali?
Tucheki kupitia Whatsapp
na tutakupatia majibu
haraka. Namba ipo katika
ukurasa wa 4.
Mambo vipi? Naitwa Hadija, ni mkazi wa Arusha.
Swali langu, nafanya biashara ya vipodozi nawezaje
kuwafikia wateja wengi katika mitandao ya kijamii?
Kabla hujafikiria kuwafikia wateja kwanza hakikisha
kuwa umetengeneza ukurasa wako kwa namna
ambayo watu wataamini huduma au bidhaa unazouza.
Njia ya haraka ya kufikia wateja wengi ndani ya muda
mfupi ni kwa kulipia matangazo au kuwalipa watu
mashuhuri wakutangazie. Kama kipato chako ni kidogo
unaweza kuanza tu wewe mwenyewe na
kujitengenezea wafuasi wako ambao pia ndio wateja
wako.
Mimi naitwa Zainab naishi ilala. Ninauza mitandio
ya wanawake, nifanyaje akaunti yangu iwe na
followers wengi ?
Unapofanya biashara mtandaoni haupaswi
kuhadaika zaidi na followers. Kumbuka kuwa wewe
upo mtandaoni kutafuta wateja na sio followers.
Wateja wako ndio watakuwa followers wako. Weka
nguvu zaidi kuwafikia watu wengi; kidogo kidogo
utapata wateja ambao watakuwa wanafatilia
biashara yako na hao ndio watakuwa followers wako.
Mtandao upi wa kijamii ni mzuri kwa mimi nayeuza
mchele? Rajab Selaman, Tanga
Swali zuri sana. Mitandao yote ni mizuri ila kwa
mfanyabiashara ni lazima kuzingatia wateja wa bidhaa
au huduma zako wapo wapi zaidi. Mitandao mikubwa
zaidi ni Facebook, Twitter na Instagram; hii mitandao
ina aina zote za watu japo kuwa kwa sasa Instagram
na Facebook inatumika na wengi zaidi Tanzania.
Binafsi ningeshauri uwekeze zaidi kwenye mitandao
hiyo mikubwa mitatu ila chagua mmoja wapo wa
Mwaka huu namaliza chuo na napenda sana
mambo ya digital. Ujuzi gani naweza kujifunza na
kuniingiza hela haraka?
kuanza nao. Hongera sana Andronicus. Sijajua ulivyosema
'haraka ni uharaka wa kiasi gani ila binafsi naamini
kiwanda cha digitali kina fursa nyingi na ni vyema
ukazingatia kujifunza na kupata uzoefu wake kabla
ya kuwaza kupata hela haraka. Hata hivyo, hizi ni
baadhi ya fursa na ujuzi ambao yanaweza kukupa
kipata cha haraka ukiwe kufanya kwenye ubora;
graphics designing, content creation, social media
management, masoko ya mtandaoni
Utaratibu wa kodi TRA ukoje kama nikiwa nauza
biashara yangu online tu? Jennifer, Dar
Sina elimu kubwa sana ya kodi, ila binafsi naamini
kuwa kwa biashara yoyote ile halali ambayo inaingiza
kipato ni lazima itambulike kisheria na kuchangia kodi.
Naelewa hili swala ni gumu kidogo haswa kwa
wanaoanza biashara, ila unaweza kujipanga taratibu
na ukaangalia ni namna gani unachangia kodi au
kufika ofisi za TRA kwa ushauri zaidi. Nadhani wao
wanaweza kuwa na
jibu zuri zaidi.
Naona kuna watu huwa wanauza akaunti.
Nikinunua akaunti na biashara yangu nikahamishia
huko ni sawa? Abdul, Chanika
Sio sawa na wala sikushauri kufanya hivyo. Wewe
upo mtandao kutafuta wateja na sio followeres.
Tengeneza ukurasa wako wa biashara na utakua
taratibu, utakuletea wateja na hao ndio watakuwa
followers wako wa kweli. Wewe unauza biashara ya
mayai unaweza ukaenda kununua ukurasa wenye
wafuasi wengi ukiamini kuwa umepata wateja
kumbe hao wafuasi waliufata huo ukirasa sababu
ulikuwa ukisambaza maudhui ambayo hata
hayaendani na biashara yako.
12 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
Uraibu wa Kidijitali,
tunatoboaje?
MEDIA CRAFTERS
KOLEZO
Tunatoboaje washikaji?
Umewahi kusikia au kukutana
na neno Detox ?! Tukiwauliza
wataalamu wa afya , watasema
ni utoaji au uepukaji wa sumu
mwilini(huweza kuwa na
maelezo zaidi ya haya).
Sasa kuna kitu kinaitwa Digital
detox. Digital Detox ni kuepuka
au kusitisha matumizi ya vifaa
na majukwaa ya mawasiliano
na habari kwa kipindi fulani ili
kuruhusu muingiliano zaidi na
jamii yako au huweza kuwa
sababu nyingine pia.
Wengi wanaofanya digital
detox hudhamiria kupunguza
/kuondoa digital addiction
(uraibu wa kidijitali); ambao
wenyewe huwa ni matumizi
yaliyopitiliza (na kushindwa
kabisa kujizuia) ya vifaa,
teknolojia na majukwaa ya
kidijitali na hasa mitandao ya
kijamii.
Uraibu wa matumizi ya vifaa
vya kidijitali imekuwa na athari
lukuki ikiwemo kuchelewa
kazini, ajali za barabarani,
kupunguza ubunifu na
uzalishaji, msongo wa mawazo
kutokana na kujilinganisha na
yale unayoyaona katika
majukwaa ya kidijitali n.k.
Digital detox huweza kuwa na
faida nyingi ikiwemo, kukupa
nafasi zaidi ya kujichanganya
na jamii yako, kukupa muda
zaidi wa kufanya shughuli zako
za kikazi au mazoezi.
Kuacha au kupunguza matumizi ya vifaa na
majukwaa ya kidijitali sio jambo la siku moja.
Kumbuka huu ni uraibu kama matumizi ya
madawa ya kulevya au sigara, unahitaji muda
kuweza kupona. Unahitaji muda wa kujifanyia
tathmini binafsi na kujua ungependa uishi vipi
na dunia ya kidijitali pasipo kukuacha na uraibu.
Unaweza kutumia mbinu zifuatazo kama
mwongozo wa kuacha au kupunguza tatizo
uraibu wa majukwaa na vifaa vya kidijitali hasa
simu;
Zima 'notifications'
Hizi ni taarifa ambazo unazipokea kutoka katika akaunti za
majukwaa ya kidijitali ambayo unayafuatilia kama Facebook,
Instagram, Youtube n.k. Unapozima ‘notifications’ inakusaidia
kupunguza shauku ya kujua yale yanayoendelea katika majukwaa
ya kidijitali na kuwekeza muda wako katika mambo mengine.
Jichanganye na watu
Vifaa vya kidijitali hasa simu vimetusogeza karibu kiasi kwamba hatuoni
umuhimu wa kutembeleana na kukaa pamoja kwa sababu
tunawasiliana katika whatsapp groups, Facebook n.k. Muda ambao
huna kazi ya kufanya tembelea marafiki, ndugu au majirani. Itakusaidia
kuboresha mahusiano na watu na kuepuka tatizo husika.
Usilale na simu
Kwa mujibu wa mtandao wa Time To Log Off, zaidi ya asilimia 45%
ya watu hutumia simu badala ya kulala wanapokuwa kitandani. Hii
inachangia kukosa muda wa kutosha wa kulala na kuathiri mwili na
akili. Unapoweka simu mbali kwa mfano chumba tofauti itakupa
ugumu kuweza kuifuata mpaka ukiwa na matumizi nayo muhimu tu.
Kuwa na ratiba maalum
Nafahamu inaweza kuwa ni rahisi kwa kusema lakini si kwa kufanya.
Moja ya dalili kubwa ya uraibu wa mitandao ya kijamii ni kufikiria sana
uchapishe maudhui gani au kufuatilia muda wote nani kachapisha nini,
unakosa hadi raha simu ikizima chaji au ikiishiwa bando. Hii
inakusababishia msongo wa mawazo. Usianze na pupa. Unaweza
kuweka ratiba wiki ya kwanza kila siku utatumia mitandao ya kijamii
masaa 6 tu au utatumia kuanzia saa 8 mchana mpaka saa 2 usiku.
Kila wiki ukipunguza saa 1 taratibu utaondoa uraibu na kuzoea kabisa.
13 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
Leo tumeamua kukoleza na hizi mbinu chache tu. Kumbuka hizi mbinu sio sheria, unaweza
kubuni mbinu zako kulingana na mazingira au majukumu uliyonayo. Kikubwa sote tuweze
kushinda tatizo hili. Mbinu gani unadhani kwako zinafaa kuweza kupambana na uraibu wa
matumizi ya vifaa na majukwaa ya kidijitali? Tutumie ujumbe kwa njia ya Whatsapp au SMS
kupitia namba zilizopo katika ukurasa wa mawasiliano tupeane madini zaidi. Amini mtu
wangu..!
SOCIAL HIT
‘Mwaka jana (2020) nilipanga kununua friji lakini
kila nikipata hela inakwenda kufanya matumizi
mengine. Siwezi kununua vyakula vingi sababu
vitaharibika hivyo inanilazimu kununua mahitaji
kidogo kidogo ambayo ni gharama kuliko kununua
kwa jumla’ anasema Prisca, kijana mwenye miaka
28 na mkazi wa Kinondoni jijini Dar Es salaam.
Licha ya kufanya kazi na kupata mshahara mzuri,
Prisca ameshindwa kutimiza lengo lake la kununua
friji zaidi ya mwaka mmoja sasa. Hata wewe
pengine una lengo fulani lakini kila ukipata mtonyo
unaishia kwenye matumizi mengine ikiwemo kulipa
madeni.
Tunzaa App!
Aplikesheni inayodhamiria
kuboresha tabia chanya
ya kutunza fedha.
Kutatua changamoto hii Tunzaa Fintech ambayo
ni kampuni changa inayomilikiwa na vijana
wazawa wa kitanzania wamezindua App
inayolenga kuimarisha tabia ya kutunza fedha
kwa watanzania. “Mwaka 2019 tulitembelea Tanga
na Dar kuzungumza na wanawake pamoja na
wanaume ili kuelewa wanapopata pesa
wanazitunza vipi na wanazitumia namna gani. Kati
ya watu tuliozungumza nao vipato vyao kwa
mwezi vilikuwa ni kati ya laki 3 mpaka milioni 6.
Lakini pia moja ya maswali ambayo tulikuwa nayo
ni watu hawatunzi pesa kwa sababu ya matumizi
mabaya, hawana njia nzuri na rahisi za kutunza
fedha na watu wengi hawarudishi kabisa pesa
wanazokopa au hawarudishi kwa wakati”
anasema Ngw’inula Kingamkono ambaye ni
mtaalamu wa teknolojia na mkurugenzi mtendaji
wa Tunzaa Fintech. Wazo la kuja na app ya
Tunzaa lilitokana na changamoto za watanzania
wengi kutokuwa na tabia ya kutunza pesa na
kuziba mwanya wa ukosefu wa njia rahisi, salama
na ya haraka ya kuhifadhi pesa pindi mtu
anapotaka kununua bidhaa kwa malipo ya kidogo
kidogo.
“Sisi hatukutunzii pesa yako. Unapojisajili katika
app ya Tunzaa unachagua aidha Tunzaa au
Nunua Sasa. Ukichagua Tunzaa maana yake
bidhaa au huduma uliyoichagua unahitaji
kuinunua kwa kutunza pesa kidogo kidogo
kulingana na wewe ulivyochagua iwe malipo kwa
siku, wiki au mwezi. Pesa unayolipa inakwenda
moja kwa moja kwa muuzaji husika. Unaponunua
bidhaa unapata point ambazo unaweza kuzitumia
kununua bidhaa au huduma sehemu fulani.”
anaongezea Ngw’inula Kingamkono. Ili mtu aweze
kuwa muuzaji wa bidhaa au huduma, Tunzaa
Fintech hupitia taarifa zote muhimu na pindi
wanapojiridhisha muuzaji ana uwezo wa
kupandisha bidhaa au huduma yake. Malipo
yanafanyika kwa njia ya simu kwa mitandao iliyo
kwenye orodha ya Tunzaa App. Ili kuweza
kuituimia Tunzaa App inabidi kupakua app kisha
kufuata hatua rahisi za kujisajili.
16 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
Kwa sasa Tunzaa App inapatikana katika Google
Playstore (kwa simu zenye mfumo wa Android) na
iStore kwa simu za iPhone.“Sisi bado ni kampuni
changa hatuwezi kuanza mikoa yote kwa mara
moja. Tulichagua kuanza na Dar kwanza kwa
sababu ya watumiaji wengi wa simu janja na
uelewa wa masoko ya mtandaoni ni mkubwa.
Lakini pia kutupa urahisi wa kuthibitisha taarifa za
wauzaji” anamalizia Ngw’inula Kingamkono
maarufu pia kama Unu. Watoto wa mjini Tunzaa
app tunaita ni kibubu cha kidijitali. Pakua kisha
furahia maisha.
KIZAZI KIPYA
Afisa Misitu mvunja mbavu
MEMA TEAM
Binafsi sipendi sana kujulikana kwa sababu ya
kazi na napenda kuwa na maisha binafsi.
Hakika Nyonyoma
Babe Mama aibua mgodi
Naitwa Hakika Nyonyoma Mwapongo, wengi mnanifahamu kama Mwaisa Mtu Mbad. Safari ya kuanza
kutambulika kama mchekeshaji ilianza mwaka 2018-2019. Nilianza kuchekesha kwa kutumia wanyama
tangu muda mrefu lakini sikuwa na post kwa sababu ya ofisini, si unajua ofisi za umma ingeonekana
sipo serious na kazi. Mara nyingi nilikuwa nafanya vinaishia for fun. Nilikuwa nikizitengeneza nampatia
baby mama wangu, si unajua Mwaisa mambo ya Mtu Mbad kumchekesha mama watoto. Yeye alikuwa
akizi share katika mitandao ya kijamii kama Whatsapp Status na Instagram. Marafiki zake walikuwa
wakiziona wanazipenda, eeh shemeji shemeji kwanini usipost kwenye page yako. Eeeh Mwaisa
sokapohapa, mimi nafanya for fun tu. Baada ya baby mama kuni shawishi sana ndiyo nikaanza kuzipost
kwenye page yangu ya Instagram. Baada ya miezi kama mitatu Nyonyoma Mtu Mbad nikaanza
kusambaa kwenye mitandao.
Mawifi wa kinyakyusa si mchezo
Nakumbuka kuna video nilitumia ya samaki aina ya Penguin wakionyesha tabia
ya mawifi wa Kinyakyusa. Nyonyoma alimpeleka mchumba wake Mbeya
kwenda kumtambulisha nyumbani kwao. Basi wakawa wanamdhihaki, “we
Nyonyoma yaani unaleta kibonge na ujanja wote huo” ile video ika-trend
kinoma. Kuanzia hapo watu wakaanza kufuatilia kwa wingi page yangu na
video watu wakawa wanazi share katika mitandao tofauti.
Wanyama na sauti
Kitaaluma mimi ni Afisa Misitu, wanyama nakutana nao katika kazi
zangu mara kwa mara. Kwangu haikuwa ngumu kuchagua mtindo wa
kuwatumia wanyama na kuingiza sauti kwa sababu wanyama
nawafahamu vizuri. Lakini pia tangu utotoni nilikuwa ni mtu wa utani,
tunaweza kuwa tumekaa nje na kina mama ghafla kuku akipita naanza
kumuigiiza kama mtu anaongea, basi watu watacheka. Sanaa yangu
inawasilisha maisha ya watu tofauti. Wanafunzi wa chuo ni mashabiki
wangu wakubwa kwa sababu huwa nazungumzia changamoto zao
nyingi, si unajua mtu anadaiwa ada, boom limechelewa au kazinguana
na mwalimu wake. Video zangu huwa zinagusa maisha yao halisi.
17 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
Ndoto iliyotimia haraka
Wakati naanza ku-share vichekesho vyangu sikutegemea ningepata umaarufu haraka hivi, nilijua
itachukua muda mrefu na nilikuwa na imani ipo siku. Nashukuru Mungu watu wamepokea kazi zangu
vizuri. Umaarufu umenisaidia kunifungulia fursa nyingine nyingi kama kupata connection na watu tofauti,
kupokea dili za matangazo na kusambaa kwa brand yangu ya mavazi ya Mwaisa. Watu mpaka wilayani
ndani huko wanaijua.
Kuficha utambulisho
Binafsi sipendi sana kujulikana kwa sababu ya kazi na pia napenda kuwa na maisha binafsi. Napofanyia
kazi asilimia kubwa mwanzoni walikuwa hawajui kama Nyonyoma Mtu Mbad ndiyo mimi. Kuna muda
nilikuwa nawakuta wanacheki video zangu tunacheka bila kujua ndiyo mimi. Baada ya kuanza kufanya
mahojiano na vyombo tofauti vya habari ndiyo wakaanza kunifuatilia.
Mahojiano yangu nilikuwa naficha sura kwa kitambaa, sasa waki-zoom wanajiuliza mbona huyu jamaa
anafanana jina na sura na mshikaji tunayefanya nae kazi? Nikawa nakwepa kwepa baadae wakajua
ndiyo mimi. Ila maeneo mengine watu hawanifahamu kwa sura.
Watu wanacheka lakini maisha yanabadilika
Sikutegemea wakati naanza kama vichekesho vyangu vitabadili maisha ya watu. Kwa mfano
kuna mtu alinipigia simu kutoka Dodoma alikiri ndoa yake ilikuwa inayumba.
Ilifikia mahali mke wake alirudi mpaka nyumbani. Jamaa akawa anamtumia video
zangu na kumkumbushia kipindi walivyokuwa wakifurahi pamoja wakati wakizitazama.
Kweli mwanamke akatuliza hasira na mpaka sasa wanaishi pamoja. Kuna mtu pia
alishawahi nitafuta baada ya kutazama video clip nikimulezea nyani anampiga kofi
mwenzake kwa kula mtaji badala ya faida. Yule dada aliniambia ile video ilimsaidia yeye
na mme wake, biashara yao ilisimama kwa sababu ya kula mtaji wa biashara.
Majina yanakua haraka kuliko mafanikio
Tasnia yetu ina chgangamoto nyingi, majina yetu yanakua haraka kuliko mafanikio
tunayopata. Kikubwa kutokuta tamaa, mbele kuna faida nyingi japo itachukua muda.
Lakini pia sanaa yetu inachelewa kukua ukilinganisha na nchi nyingine mfano chukulia
Kenya. Wenzetu vichekesho vya majukwaani (stand up comedy) walianza muda kwetu
tulichelewa kidogo. Vipaji vipo vya kutosha. Kwa sasa mambo yanaanza kubadilika,
tasnia ya vichekesho watu wameanza kuingalia kwa umakini.
Aminia kipaji chako
Mitandao ya kijamii bahati nzuri watu wengi wapo huko. Vijana
wengi wanaitumia kupandisha video zinazoonyesha vipaji vyao
na wanatoka. Cha msingi upende unachokifanya na usikate
tamaa. Halafu matarajio vijana tusiwe nayo makubwa sana
hasa tunapoanza, tuna expect too much tukikwama tunakata
tamaa.
18 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
ni Kama Njia Maisha
baba, dada, kaka, Maisha tunapitia,
Mama,
kwamba ni karaha, bali ni kuvumilia,
Sio
Shule ya sekondari Mikocheni ni moja ya shule ya kwanza kuwa na Mema
Club nchini tangu zilipoanza rasmi Oktoba 2018. Kuna vijana kibao
ambao walianza kuwa wanachama tangu wakiwa kidato cha kwanza na
mwaka huu wanamaliza kidato cha nne. Ni kama mtoto ambaye tangu
amezaliwa hajawahi kuhama mji, na sasa yupo tayari kukusimulia hadithi
ya tangu utotoni. Pia, Sia na Subira walitema vina na mashairi moto moto.
Naitwa Hassana Ali. Wakati najiunga na club sikuwa
najiamini. Nikiwa kidato cha pili nilichaguliwa kuwa
makamu wa rais wa Mema Club.
Hapo nilionyesha uwezo wangu wa uongozi,
kuliniongezea ufaulu na kuchaguliwa kuwa kiranja wa
elimu. Mema Club siku zote itaendelea kuwa familia
yangu.
Nakumbuka wakati najiunga na klabu tulikuwa
tunafundishwa elimu ya hedhi. Sio siri nilikuwa najihisi
aibu, unawaza washikaji watanichukuliaje kujifunza
mambo yanayohusu wanawake. Taratibu aibu
iliniisha hata washikaji zangu nikawa napiga na
ostory za afya ya uzazi ile fresh tu.
Kuwa sehemu ya klabu kumenibadili sana mtazamo
na kunianda kuwa kijana muwajibikaji.
Naitwa Beatrice Ulindula. Kuchaguliwa kuwa kiongozi
wa Mema Club kulinipa hamasa ya kutambua
nafasi yangu katika jamii ni ipi. Unapokuwa kiongozi
inabidi uwe mstari wa mbele kwa kuonyesha
uwajibikaji kwa watu wengine.
Kuwa kiongozi katika klabu ni mwanzo wa kutimiza
ndoto yangu ya kuwa kiongozi siku za usoni. Safari
yangu inaanzia katika klabu.
Jina langu ni Sarafina Thobias. Kuwa katika klabu
kumenipa nafasi ya kuonyesha kipaji changu cha
kuigiza ambacho watu hawakuwa wanakifahamu.
Maigizo tofauti tumekuwa tukianda shuleni
yenye kuelimisha na kuburudisha. Huu ni mwanzo
wa kutimiza ndoto.
19 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
Ushairi
ya Mwanamke Tohara
kale hadi sasa, tohara imesambaa,
Tangu
na bara, wanawake walalama,
Visiwani
na vijana, wote wanalalamika,
Watoto
kwa mwanamke, si sawa nakwambia.
Tohara
wamejaa, ngariba wasio na maana,
Vijijini
vijana, kupata hiyo tohara,
Wanalazimisha
wakiambizana, ushupavu utapata,
Eti
kwa mwanamke, si sawa nina kwambia.
Tohara
nimeshafikia, naanza kuwausia,
Mwisho
kwa nia, kuanza kutokomeza,
Watanzania
kwa rabana, janga hili litaisha,
Naapa
kwa mwanamke, si sawa nina kwambia.
Tohara
Shairi hili limetungwa na Subira Hassna
ni kujipanga, hata kama ni fukara,
Maisha
ni kama njia,kila mtu anapitia.
Maisha
yetu ni ndefu, yapasa kupambania,
Safari
tufue dafu, mbali sana kufikia,
Vijana
ni wafu, na ilhali tuna afiya,
Tusijifanye
ni kama njia,kila mtu anapitia.
Maisha
Shairi hili limetungwa na Sia Kalula
WAKILISHA
Naitwa Rigeye Ally, ni mwanafunzi wa kidato
cha nne shule ya sekondari Mikocheni. Nilikuwa
pia rais wa Mema Club kuanzia mwaka 2019
mpaka 2021. Mimi ni kiongozi na nina jiamini
katika kuongoza. Ndoto yangu ni kuwa daktari
wa binadamu na kiongozi. Wanafunzi
wenzangu huniita Mema, kwa sababu nilikuwa
rais wa Mema Club tangu nikiwa kidato cha pili
mpaka cha nne. Awali sikuwa najua kama nina
karama ya uongozi.
Mara nyingi nilikuwa mstari wa mbele kutuliza
kelele katika klabu na kujitolea kufundisha
wengine masuala ya hedhi. Wanafunzi
wenzangu walianza kuvutiwa na mimi na kisha
wakanichagua kuwa kiongozi wao. Kujitolea
katika kufundisha wenzangu, kunyamazisha
kelele na kuhudhuria siku za klabu kulisaidia
kuaminiwa na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa
klabu. Umaarufu wa uongozi wangu ulichochea
pia kuchaguliwa kuwa kiongozi wa mazingira
na afya shuleni.
Kujitolea katika kufundisha
wenzangu,kunyamazisha kelele
na kuhudhuria siku za klabu
kulisaidia kuaminiwa na
kuchaguliwa kuwa kiongozi wa
klabu.
Changamoto niliyopitia kubwa ni
wakati wa COVID19. Wasimamizi
wetu hawakuwa wanakuja kwa
tahadhari ya mikusanyiko na
mwalimu mlezi alienda
masomoni. Klabu ikawa haiendi
sawa. Baadhi ya viongozi
walihama klabu. Ila nilisimama
sana imara wakati huo.
Niliendelea kusimamia na
kufundisha kupitia vitabu vya
afya ya uzazi Mema Tanzania
walivyotuachia.Ilinisaidia sana
kunijenga kujiamini na kuwa
kiongozi bora zaidi.
Klabu yetu imekuwa inatupa
motisha kufanya vyema katika
mitihani. Kuwa kiongozi wa
Mema Club kumenipa motisha
ya kuamini naweza kuwa
kiongozi.
Rigeye Ally
Ndoto yangu ni udaktari
20 | AUG 2021MEMA MAGAZINE
VIPAJIKA
NIKIZA JR
MSAFIRI MWENYE VIPAJI
Karibu katika kisima cha vipaji. Ninaweza
kuigiza, kukuvunja mbavu na utangazaji pia.
Yote haya nafanya na bado nakomaa na
kitabu katika chuo cha NIT, shahada ya
Computer Science.. Kwa majina naitwa
Justine Nikiza, jukwaani nafahamika kama
Nikiza Jr.
Nilianza kuigiza tangu nikiwa darasa la 4
shule ya msingi Nkololo B, Simiyu. Nilikuwa
nafanya maigizo kwenye mahafali mbali
mbali shuleni kwetu na kwenye matamasha
mengine yaliyokuwa yakihusisha shule
tofauti. Baada ya kumaliza shule ya msingi,
kipaji kilinoga nilipojiunga shule ya sekondari
Nyegezi iliyopo Mwanza. Tofauti na Simiyu,
Mwanza ni jiji. Kama una kipaji rahisi watu
kukiona na kupata shavu la kushiriki
mashindano na matamasha mbali mbali.
Kwa upande wa elimu nilichagua kusoma
Computer Science kwa sababu napenda
kompyuta. Nahitaji kufahamu mifumo mbali
mbali ya kompyuta inavyofanya kazi
Nisingeweza kusomea sanaa sababu tayari
vipaji ninavyo vya kuzaliwa. Siamini kipaji mtu
anaweza kufundishwa ila ni karama mtu
anazaliwa nayo na kuendeleza kwa
kuitendea kazi na kukinoa kwa kujifunza kwa
watu wengine walioendelea.
21 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
Nilipofika chuo, nilianza kufanya comedy
kwa kuji-record video fupi kisha naziweka
katika akaunti yangu ya Instagram. Baadae
kazi zangu zilianza kufuatiliwa sana na
nikaona nahitaji kukua zaidi. Nikaanza
kushiriki katika vichekesho vya jukwaani
(stand-up comedy). Awali nilifanya kama
msanii wa kujitegema baadae nikapata
bahati ya kuwa sehemu ya familia ya Watu
Baki, japo bado sijawa mwaanachama rasmi.
Watu Baki imekuwa ni familia, najifunza
mambo mengi kutoka kwao. Ni kundi lenye
vipaji lukuki na wengine tayari wameshakuwa
na majina makubwa.
Watu Baki nafanya nao mazoezi na kushiriki
katika tamasha linalofanyika The Base Club
kila alhamis. Mwaka huu kuna rafiki yangu ni
mchekeshaji pia alikuja na wazo la kuanzisha
kundi letu litakalo husisha wanachuo wenye
vipaji vya uchekeshaji, ndipo Unicomedy
ilipoanza. Tumekuwa tukiandaa matamasha
yetu wenyewe yanayofanyika chuoni na nje
ya chuo. Kazi yangu imenipa heshima kwa
mwaka huu kupewa tuzo ya mchekeshaji
bora chuoni kwetu.
Mwaka huu Unicomedy tumefanikiwa
kuandaa matamasha mawili na yote
yalifanya vizuri. Mwanzoni tulifanyia London
Lounge, Ubungo. Watu walihudhuria wengi na
baadhi kukosa viti. La pili tukahamia ukumbi
mwingine.
Kati ya vitu ambavyo haviwezi kuepukika ni
mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii
inasaidia sana kusukuma kazi zangu kufika
mbali. Japo changamoto ukishakuwa
maarufu watu wanaanza kutumia jina lako
hali inayowapa ugumu watu wanaponitafuta.
Mitandao imesaidia sana kujenga brand
yangu na kuonyesha uwezo wangu kwa
watu. Napgia simu na kupata mialiko kuperform
katika sherehe tofauti.
Mitandao pia imenikutanisha na ma-star
wakubwa, wengine ni role model wangu.
Mfano Kendrick Mulamula kutoka Kenya,
tuliwasiliana kupitia mitandao ya kijamii na
kubadilishana namba. Mpaka leo
tunawasiliana vizuri tu. Mpaka sasa
nimefanikiwa kufanya kazi na wasanii
wakubwa tofauti kama Idris Sultan ambaye ni
role model wangu, Francis Nalimi na wengine
kutoka Watu Baki.
Comedy kwa sasa sio kama zamani ambapo
ili uonekane mchekshaji uvae kiajabu ajabu
na watu kukuona kama kituko. Na ilichangia
sana malipo madogo ukilinagnisha na
wasanii wengine wa bongo movie kwa
sababu tulionekana kama vituko tu.
Mtazamo hasa kwa Dar umebadilika sana.
Changamoto bado mikoani kama kule kwetu
Simiyu bado waigizaji wengi wamekuwa na
mtazamo wa vituko badala ya vichekesho.
Kama mwanafunzi changamoto kubwa
nayopitia ni kupigana vizinga, wanafunzi
wengi wanafikiri nina hela nyingi. Wakiona na
star mkubwa wanajua jamaa
ameshayapatia, ukimnyima hela anahisi
umemkazia. Pia nyumbani wana-support
lakini kwa mashaka. Wazazi wananilipia ada
wanahisi sanaa inaweza kuniharibia masomo.
Ila taratibu wanazidi kuelea hii ni kazi na kwa
upande wa masomo haina athari yoyote ile.
22 | AUG 2021MEMA MAGAZINE
na Instagram 4.37% na jumla ya watu milioni 5.4 wanatumia
46.86%
ya kijamii. Wanawake wanaotumia mitandao ya kijamii ni
mitandao
37% na wanaume 63%. Kwa mtazamo wako, ni sababu zipi
asilimia
ufinyu wa wanawake kuingia katika ulingo wa fursa za
zinachochea
Sema nasi kupitia namba yetu ya Whatsapp iliyopo
kidijitali?
wa mawasiliano.
ukurasa
Sauti ya Mtaa
Kwanini wanawake ni wachache
katika fursa za kidijitali?
Nicholaus Mukasa
-Arusha
Ni ukweli ni wachache sana, kwa mfano ni asilimia 27% tu ya
wanawake ndio wanaotumia intaneti duniani. Kuna sababu
nyingi. Kwa uchache kwanza ni uelewa wa teknolojia. Wadada
wengi bado hawafahamu jinsi ya kutumia kwa usahihi
teknolojia za simu na kompyuta ambapo ndipo fursa zote za
kidijitali zipo. Uwezo wa kifedha pia kwa wanawake wengi sio
mzuri hivyo inakuwa ni ghali kwa wao kununua teknolojia za
kidijitali ambazo ni gharama. Wanawake pia wanafanyiwa
ukatili katika mitandao kama kutukanwa. Kwao wanaona sio
sehemu salama kuweza kushiriki na kujikuta wapo wachache
katika matumizi ya mitandao na fursa zake.
Wanawake wanauelewa mdogo juu ya elimu nzima
ya kidijitali. Wengi wanachojua nikijiunga Instagram
au Facebook ni kutuma picha, kuangalia likes na
comments nilizopata. Kumbe kuna fursa nyingi mbali
ya kushare tu picha na kutoka huyoo. Mimi
napofanya kazi sasa boss wangu nilikutana nae
kupitia mtandao wa Twitter. Usalama mitandaoni ni
mdogo kwa wanawake. Mfano mwanamke anaweza
ku-post picha akiishia kudhalilishwa na kutumiwa
messages za vitisho. Mwisho anaona hii sio sehemu
sahihi kwangu anaacha kutumia na fursa zinampita.
Happie Thomas
-Dar Es Salaam
Wanawake tuna dhana mambo yanayohusu dijitali au teknolojia
ni mambo magumu na jamii ni kama imeshajenga mtazamo vitu
vigumu ni vya wanaume. Hata mimi mwenyewe mambo kama
graphics designing naona ni vyema zaidi kufanywa na wanaume.
Ni kama tumeamua mambo yanayohusu sayansi tumeamua
kuwaachia wanaume. Wanawake mara nyingi tumekuwa wazito
kujifunza zinapotokea fursa za mafunzo tofauti na wanaume
utakuta mara nyingi wanakuwa wepesi kuzichangamkia. Nadhani
inatokana na sababu niliyosema hapo awali, kwamba mambo
haya ni kama tumeshajijengea dhana ni mambo ya wanaume.
Mwajabu Galmos
-Zanzibar
mujibu wa mtandao wa Statista, mpaka Februali 2021,
Kwa
ilikuwa na watumia wa Facebook asilimia 27.41%, Twitter
Tanzania
23 | AUG 2021MEMA MAGAZINE
Namna gani ningeweza kushika
vitu na kufanya majaribio ya kisayansi.
Nashukuru wazazi na walimu hasa wa
Loyola niliposoma O-Level waliniamini na
kunitia moyo na niliweza kuvuka kikwazo.
Mbali ya udaktari, una ujuzi gani
mwingine?
Nina ujuzi katika kufanya utafiti, kuandika na
kusimamia miradi,ufuatiliaji
na tathmini ya miradi, uzalishaji wa maudhui
na ujuzi wa dijitali.
Changamoto zipi unakumbana nazo
katika udaktari?
Upotoshaji wa taarifa za afya
hasa
katika mitandao ya kijamii hali
inayosababisha kuzuka kwa
baadhi ya taarifa potofu.Lakini
nikizungumzia kwa ujumla bado
kuna uhitaji wa
kuboresha mazingira ya kazi za
madaktari na watoa huduma
wa afya kwa ujumla ili kufanya
kazi kwa ufanisi.
Pia tuna changamoto ya
mfumo wetu wa elimu ambao
unatuanda wote kufikiria mstari
mmoja yaani kila mmoja ajiriwe.
Tutengeneze madaktari watakaohitimu na
uwezo wa kufikiri nakuboresha afya za
wagonjwa wao kwanzia kwenye mazingira
wanayotoka na mitindo yao ya maisha.
Wenye uwezo wa kutengeneza solutions za
changamoto za afya.
Tangu umeanza kuwa daktari,
muelimishaji na mtafiti umepata
mafanikio kiasi gani?
Mafanikio makubwa ya kwanza ni
kubadilika kimtazamo kwa kupata ujuzi
tofauti. Kufanya kazi maeneo tofauti
kumenibadilisha kifikra na kuwa na ufahamu
wa mambo mengi yanayohusiana na afya
kwa ujumla. Ujuzi pia kama graphics
designing, digital skills,project management
vimenipa mafanikio makubwa.
Kutoa huduma na watu
wakapona/kujikinga na maradhi
ni mafanikio makubwa sana.
Kwa mafanikio mengine mwaka 2017 nikiwa
chuo mwaka wa nne nilibahatika kupata
tuzo kutoka MILEAD (Maremi Institute of
Leadership and Development) nchini Ghana.
Tangu mwaka wa kwanza nilikuwa na wenzangu
tunafanya shughuli tofauti za kutoa elimu na
huduma za afya. Watu waliona nastahili kushiriki
hayo mashindano, na nilifanikiwa kushinda kati ya
wasichana 27 na mtanzania nilikuwa peke yangu.
Tulienda Ghana na kupewa mafunzo ya uongozi.
Mwaka 2020 pia nilipata heshima ya utambuzi
kutoka taasisi ya Launchpad na ubalozi wa
Sweden kwa kuchaguliwa kuwa miongoni mwa
wanawake 100 waliofanya mabadiliko chanya
katika jamii kwa mwaka huo. Pia nimepata
heshima kwa kufanya kazi na mashirika makubwa
ya kimataifa kama UNICEF na vyombo vya habari
kama Clouds, Redio France International, DW n.k.
kama muelimishaji katika kipindi cha COVID19.
Una wafuasi zaidi ya elfu 14 katika mtandao wa
Twitter, nini siri ya kuwa na wafuasi wengi?
Watu wanatafuta taarifa muhimu hasa za afya.
Tangu nilipojiunga Twitter nimekuwa nikiwasilisha
maudhui na dondoo muhimu hivyo watu kuvutiwa
na ukurasa wangu. Pia ku-engage na watu kama
kujibu comments na jumbe zao ilisaidia kujenga
mahusiano ya kibinadamu. Pia vijana tukumbuke
si kitu kinakuja haraka. Inabidi kujifunza namna ya
kutumia mitandao kwa kusoma na kuhududhuria
mafunzo mbalimbali.
Watu walio katika kada ya afya kuna umuhimu
gani wa kutumia teknolojia ya kidijitali hasa
mitandao ya kijamii?
Ni rahisi kusambaza taarifa kwa haraka hasa za
afya lakini pia kuna fursa ya kufanya utafiti na
kujifunza. Hivyo ni muhimu sana kujua matumizi
sahihi ya mitandao ya kijamii au teknolojia ili
kuboresha maisha na huduma kwa jamii.
Usingekuwa daktari ungekuwa nani?
Ahahaha! Sijui kwa kweli. Ila pengine ningekuwa
mwandishi wa habari sababu tangu mdogo
napenda kudadisi na kufuatilia
mambo.
Una ushauri gani kwa binti na kijana mwenye
ndoto ya kuwa mwanasayansi?
Kuamini unaweza, kuwa na lengo na kuzidi
kumuomba Mungu akuwezeshe kutimiza ndoto
yako. Ukitia juhudi na kufanya kazi kwa bidii ndoto
yako itatimia. Pia kuwa karibu na watu ambao
wameshafikia sehemu ambayo unafikiria kufika.
Julieth tunashukuru kwa kuchonga nasi,
tuna amini kuna mengi tumejifunza toka kwako.
Ahsanteni sana kwa kunipa nafasi hii.
25 | AUG 2021MEMA MAGAZINE
DID YOU KNOW?
We have all it takes to develop and strengthen
your relationship with your audience.
ABOUT US
We are trusted and professional digital, media-tech, and audio-visual experts with a dedicated
team that fulfil and deliver output to its clients at optimum level. We deploy skillful and
innovative human-centered designs in approaching and undertaking each and every task.
We are more than fit to serve you with the best up-to-date technologies in taking your brand
above the top notch.
WHAT WE DO
Public and Media Relation
Content Creation and Dissemination
Digital Marketing
Audio-Visual Production
Web Platforms and Apps Development
REACH US
0655 921 330 welcome@mediacrafters.co.tz
www.mediacrafters.co.tz @MediaCraftersTz
SMART CLASS
BUKUA KIDIJITALI, FURSA KWA WALIMU
MEMA TEAM
Ulishawahi kufikiria itafikia kipindi watu watachagua
kubaki nyumbani na kusoma kupitia mifumo ya
kimtandao badala ya kwenda shuleni? Janga la
COVID19 lilitupa funzo juu ya uwezekano wa jambo
hili.Wakati wa COVID19, mwezi March 2020 shule
zilifungwa na tulishuhudia vituo kadhaa vya Tv na
majukwaa ya kidijitali yakitoa elimu kwa wanafunzi.
Moja ya majukwaa hayo ni Smart Class ambao
wanatoa huduma ya mafunzo kwa wanafunzi wa shule
za msingi na sekondari kwa njia ya mtandao na nje ya
mtandao. Adam Duma, ni moja ya waanzilishi wenza
wa Smart Class na hapa anatuelezea kuhusu ubunifu
huu.
Mlipata wapi mtaji?
UBUNIFU
Unapoanzisha wazo lazima uangalie nani anaweza
kuwekeza pesa zake. Hili wazo lilikuja mimi bado
nipo chuo mwaka wa pili, kuna mwalimu wa Chuo
Kikuu cha Dar Es Salaam nilimshirikisha na akawa
tayari kuwekeza baadhi ya pesa kutoka kwenye
mshahara wake kama mtaji. Mimi niliomba msaada
wa kifedha kutoka nyumbani na pia yule mwalimu
alikuwa na rafiki yake anafanya kazi Nokia na yeye
aliungana nasi na hatimaye tukaanzisha kampuni.
Siku zilivyozidi kusonga tukaanza kupokea pesa
kutoka kwa wafadhili tofauti.
Smart Class ni nini?
Ni jukwaa la mtandaoni linalokutanisha walimu, wazazi
na wanafunzi na inapatikana nchini Tanzania na
Kenya kwa njia ya tovuti kutoa mafunzo ya ziada
maarufu ‘tuition’. Makundi yote haya matatu yanajisajili
bure na kisha kuanza kutumia huduma hii. Smart Class
inamuunganisha mwanafunzi au mzazi ambao ndio
wasimamizi wa taaluma kwa watoto wao na kisha
anachagua aidha asome ‘online’ au mwalimu amfuate
nyumbani. Mafunzo yanapokamilika, mwanafunzi
anatupatia ripoti ya huduma aliyopewa na malipo
yanafanyika Smart Class kisha mwalimu hupokea 85%
na 15% hubakia kwetu. Gharama za mafunzo
zinatofautiana kulingana na muda na mfumo wa
utolewaji wake, kwa ‘online’ ni nafuu kuliko kufuatwa
nyumbani ‘offline’.
Wazo liliibuka vipi?
Wazo tulianza nalo mwaka 2018 pamoja na wenzangu
wawili wakati huo tulikuwa Chuo Kikuu
cha Dar Es Salaam. Tulifanya utafiti kwa takribani
mwaka mmoja ili kubaini ni namna gani tutaweza
kutatua tatizo la ajira kwa walimu wakati wakisubiri ajira
za kudumu kutoka serikalini na kuondoa pengo la elimu
bora. Baada ya kufanya utafiti tulishiriki katika
maonyesho ya Research Innovation Week 2019
yanayoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na
mapokeo tuliyoyapata ndio yalitushawishi njia pekee ya
kutatua changamoto hii ni teknolojia na wazo la Smart
Class tukaanza kulifanyia kazi na kuizindua rasmi
mwaka huo huo.
Mapokeo kwa waTanzania yakoje?
Mapokeo ni mazuri kwa maana ya idadi ya
watumiaji tulio nao ambao kwa Tanzania wanafika
12,000 (walimu, wazazi na wanafunzi). Shule
zilipofungwa kipindi cha COVID19 naweza kusema
kwetu ilikuwa ni neema kwa sababu kulikuwa na
ongezeko kubwa la watumiaji wa jukwaa letu.
Changomoto iliyopo kwa Tanzania kunapoibuka
teknolojia mpya watu wengi huwa wanakuwa
wagumu kuipokea kwa haraka. Ila taratibu watu
wanazidi kuelea huduma tunayotoa.
Mliwezaje kufika Kenya?
Kwanza tulifikiria kujitanua Kenya kutokana na
uelewa mkubwa uliopo kule katika masuala ya
teknolojia. Kuna watumiaji wengi wa intaneti,
kwenda kule ilikuwa ni kulifikia kwa urahisi soko
ambalo tayari lipo. Kuna jamaa yetu anaitwa
Kimathi aliacha kazi na kusimamia mchakato
mzima wa kuanzisha Smart Class Kenya na ndio
msimamizi pamoja na watu wengine watatu.
Kenya tunawatumiaji zaidi ya 5,000 wa Smart
Class.
Mnajionaje miaka 5 ijayo?
Kuwa jukwaa kubwa la elimu Afrika. Kwa
mwalimu, mzazi au mwanafunzi anaweza kuipata
Smart Class kwa kutembelea
www.smartclasstz.com na kuanza kutumia
huduma zetu.
27 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
Dr. Julieth Sebba
NO TIME TO GIVE UP