You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
Tujibebe
Kila mtu ana njia yake katika kufikia mafanikio. Bado
na ndoto ya kutimiza mambo mengi katika kazi
yangu, na hata hapa nilipofika nashukuru Mungu.
Binafsi mambo yafuatayo yamechangia kunipa
mafanikio niliyonayo sasa na pengine hata wewe
kijana mwenzangu yanaweza kuchochea ndoto
yako ya kuwa mpiga picha mashuhuri;
Michongo
Katika picha kuna fursa nyingi. Dunia
imehamia katika teknolojia na huwezi
kutenganisha picha na teknolojia. Upigaji picha
imekuwa inachangia sehemu kubwa katika
kusukuma agenda mbali mbali za kisiasa na
kijamii. Kuna fursa za kifedha lakini pia
inaweza kukupenyeza katika fursa
usiyoitegema. Kwa mfano ukihudhuria
mkutano mkubwa wa kimataifa mbali ya pesa
utakayolipwa lakini yale yatakayokuwa
yanazungumzwa utayasikia na kujifunza pia.
Kamera inakupa elimu mpya kila siku ambayo
inakufungulia fursa kibao.
Sasa hivi pia biashara zinahamia kwenye
mitandao ya kijamii. Nyenzo muhimu
inayohitajika ni picha, hivyo kwa mpiga picha
kuna dili utazipata kwa watu wanaofanya
biashara mtandaoni. Binafsi kuna programu
naifanya inayowezesha vijana wa kike
kujifunza upigaji picha na kufungua fursa kwa
upande wao kwa sababu tasnia ya picha
imetawaliwa na wanaume zaidi. Pia picha
inakusaidia kusafiri maeneo tofauti na
kujifunza mila na tamaduni za watu.
Nimefanikiwa kufika Germany, Netherlands,
France, Belgium, Czech Republic, Zimbabwe,
Italy n.k. na kote nimejifunza mambo mengi.
Kupenda unachokifanya. Hii kazi yetu unahitaji
kuipenda sana ili inapotokea hata kazi nyingi
zimekutinga una enjoy kwa sababu ni kitu
unachokipenda. Imenisaidia sana katika upigaji picha
kwa sababu siku zote ni kazi naifanya kutoka moyoni.
Muda mwingi nafanya kazi, na safiri mara kwa mara
sipumziki. Kwangu sioni tatizo kwa sababu na enjoy.
Kujitahidi kujifunza kupitia watu na kuwekeza kwenye
elimu. Kuna wengine wamepata bahati ya kusoma
chuo na wengine mitandaoni. Lakini kwa namna
yoyote uwe ni mtu wa kuitafuta elimu ya upigaji picha.
Elimu isiwe tu ya upigaji picha, kujifunza mambo
mengine kwa sababu kama mpiga picha lazima
utambulike wewe ni mpiga picha wa namna gani.
Kuna mteja anaweza kuhitaji picha ambazo zitatoa
elimu ya mabadiliko ya tabia nchi na wewe hujui nini
maana ya mabadiliko ya tabia nchi hawezi kukupa
kazi. Ukijifunza mambo tofauti ndivyo wateja tofauti
watakufuata kwa sababu ya uelewa wako wa mambo
tofauti.
Kujenga mahusiano na watu. Hizi kazi watu wanavyo
kuzungumzia wakati haupo ndio zinasaidia ndio
inavyoamua kufunga au kukufungulia fursa.
Mahusiano bora ndio kila kitu katika maisha.
Kuchagua unataka kuwa mpiga picha wa namna gani.
Mwanzoni wakati unaanza unaweza kuwa unapiga tu.
Baadae ukachagua ujikite eneo gani ambalo watu hata
wakitaja jina lako wanajua wewe ni mpiga picha wa
aina gani. Inaweza kuwa michezo, sherehe, sanaa n.k.
11 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE