You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
SOCIAL HIT
‘Mwaka jana (2020) nilipanga kununua friji lakini
kila nikipata hela inakwenda kufanya matumizi
mengine. Siwezi kununua vyakula vingi sababu
vitaharibika hivyo inanilazimu kununua mahitaji
kidogo kidogo ambayo ni gharama kuliko kununua
kwa jumla’ anasema Prisca, kijana mwenye miaka
28 na mkazi wa Kinondoni jijini Dar Es salaam.
Licha ya kufanya kazi na kupata mshahara mzuri,
Prisca ameshindwa kutimiza lengo lake la kununua
friji zaidi ya mwaka mmoja sasa. Hata wewe
pengine una lengo fulani lakini kila ukipata mtonyo
unaishia kwenye matumizi mengine ikiwemo kulipa
madeni.
Tunzaa App!
Aplikesheni inayodhamiria
kuboresha tabia chanya
ya kutunza fedha.
Kutatua changamoto hii Tunzaa Fintech ambayo
ni kampuni changa inayomilikiwa na vijana
wazawa wa kitanzania wamezindua App
inayolenga kuimarisha tabia ya kutunza fedha
kwa watanzania. “Mwaka 2019 tulitembelea Tanga
na Dar kuzungumza na wanawake pamoja na
wanaume ili kuelewa wanapopata pesa
wanazitunza vipi na wanazitumia namna gani. Kati
ya watu tuliozungumza nao vipato vyao kwa
mwezi vilikuwa ni kati ya laki 3 mpaka milioni 6.
Lakini pia moja ya maswali ambayo tulikuwa nayo
ni watu hawatunzi pesa kwa sababu ya matumizi
mabaya, hawana njia nzuri na rahisi za kutunza
fedha na watu wengi hawarudishi kabisa pesa
wanazokopa au hawarudishi kwa wakati”
anasema Ngw’inula Kingamkono ambaye ni
mtaalamu wa teknolojia na mkurugenzi mtendaji
wa Tunzaa Fintech. Wazo la kuja na app ya
Tunzaa lilitokana na changamoto za watanzania
wengi kutokuwa na tabia ya kutunza pesa na
kuziba mwanya wa ukosefu wa njia rahisi, salama
na ya haraka ya kuhifadhi pesa pindi mtu
anapotaka kununua bidhaa kwa malipo ya kidogo
kidogo.
“Sisi hatukutunzii pesa yako. Unapojisajili katika
app ya Tunzaa unachagua aidha Tunzaa au
Nunua Sasa. Ukichagua Tunzaa maana yake
bidhaa au huduma uliyoichagua unahitaji
kuinunua kwa kutunza pesa kidogo kidogo
kulingana na wewe ulivyochagua iwe malipo kwa
siku, wiki au mwezi. Pesa unayolipa inakwenda
moja kwa moja kwa muuzaji husika. Unaponunua
bidhaa unapata point ambazo unaweza kuzitumia
kununua bidhaa au huduma sehemu fulani.”
anaongezea Ngw’inula Kingamkono. Ili mtu aweze
kuwa muuzaji wa bidhaa au huduma, Tunzaa
Fintech hupitia taarifa zote muhimu na pindi
wanapojiridhisha muuzaji ana uwezo wa
kupandisha bidhaa au huduma yake. Malipo
yanafanyika kwa njia ya simu kwa mitandao iliyo
kwenye orodha ya Tunzaa App. Ili kuweza
kuituimia Tunzaa App inabidi kupakua app kisha
kufuata hatua rahisi za kujisajili.
16 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
Kwa sasa Tunzaa App inapatikana katika Google
Playstore (kwa simu zenye mfumo wa Android) na
iStore kwa simu za iPhone.“Sisi bado ni kampuni
changa hatuwezi kuanza mikoa yote kwa mara
moja. Tulichagua kuanza na Dar kwanza kwa
sababu ya watumiaji wengi wa simu janja na
uelewa wa masoko ya mtandaoni ni mkubwa.
Lakini pia kutupa urahisi wa kuthibitisha taarifa za
wauzaji” anamalizia Ngw’inula Kingamkono
maarufu pia kama Unu. Watoto wa mjini Tunzaa
app tunaita ni kibubu cha kidijitali. Pakua kisha
furahia maisha.