You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
Anasema "Mwanzoni nilikuwa na wateja
wachache na kupelekea kupata hasara mara
kadhaa. Nikaamua kuongeza wateja wapya
na njia rahisi niliona ni mitandao ya kijamii.
Nilifungua akaunti Instagram ndipo kasi ya
wateja ikaongezeka kutoka mikoa ya jirani na
kuniongezea mtaji mpaka wa Tsh milioni 5.”
Kuna vijana pia ambao wanatumia ushawishi
walionao katika mitandao ya kijamii
kutangaza biashara za makampuni,
kuendesha kampeni za taasis na baadhi
wameanzisha kurasa zinazochapisha maudhui
tofauti ikiwemo udaku na kujipatia wafuasi
wengi hivyo kuwafungulia dili za matangazo
ya biashara.
Kabla ya kuolewa mwaka 2018 alikuwa
akijihusisha na mauzo ya bidhaa mtandaoni.
"Nilikuwa nikifanya biashara ya kuuza nguo za
watoto na wanawake. kupitia Instagram. Akaunti
yangu ilikuwa imefikisha wafuasi zaidi ya elfu 10.
Ni biashara nilianza tangu nikiwa nasoma chuo
na nilikuwa na wateja wengi sana. Baada ya
kuolewa mme wangu hakuwa anapendezwa
navyo wasiliana na wateja mara kwa mara.
Kuepusha mikwaruzano katika ndoa yangu
nikaamua kuachana na biashara ile na kuajiriwa
katika kampuni ambayo mme wangu alinitafutia.
Changamoto za kifamilia hasa kwa wanawake
waliolewa kiukweli zinatukwamisha kujihusisha
na mambo ya dijitali labda uwe na mwenza
muelewa na mambo haya" anasema Aisha.
Utawala wa kijinsia
Licha ya fursa lukuki za kidijitali bado sio wote
wananufaika nazo. Utofauti upo zaidi katika
upande wa jinsia ambapo wanawake ni wachache
kuliko wanaume. “Kwa mtazamo wangu sababu
kama kutingwa kwa majukumu ya familia, ukosefu
wa ujuzi, hofu ya ukatili wa kijinsia zinachangia
wanawake kuwa wachache” anasema Dkt Julieth
Sebba, moja ya vijana wenye ushawishi katika
mtandao wa Twitter. Mtazamo wake unaungwa
mkono na Mariam, mkazi wa Tanga. ambaye
anaamini uchache wa wasichana na wanawake
katika dunia ya kidijitali inachangiwa na uoga wa
kushambuliwa mitandaoni hali inayowarudisha
nyuma katika kuzifilkia fursa zilizopo katika
mitandao ya kijamii.Aisha mkazi wa Tabata jijini
Dar Es Salaam, ni kijana mwenye umri wa miaka
32 ni mke na mama mwenye mtoto mmoja.
8 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
Sheria ya ngoma
Mafanikio hayaji haraka na kwa urahisi hasa
katika kuzifikia fursa za kidijitali. Unahitaji kutia
bidii katika kujifunza ujuzi fulani, hata kama ni
kutangaza biashara yako mtandaoni unapaswa
kufahamu namna gani ya kuandika maudhui,
muda gani, nani unayemlenga n.k.
Jinsi unavyofanyia kazi ujuzi wako ndivyo
unavyozidi kuwa na uelewa wa kutosha na jamii
itatambua ujuzi wako hivyo fursa zitaanza
kukufikia. Jipe muda kujifunza, usikate tamaa.