You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
Ndoto iliyotimia haraka
Wakati naanza ku-share vichekesho vyangu sikutegemea ningepata umaarufu haraka hivi, nilijua
itachukua muda mrefu na nilikuwa na imani ipo siku. Nashukuru Mungu watu wamepokea kazi zangu
vizuri. Umaarufu umenisaidia kunifungulia fursa nyingine nyingi kama kupata connection na watu tofauti,
kupokea dili za matangazo na kusambaa kwa brand yangu ya mavazi ya Mwaisa. Watu mpaka wilayani
ndani huko wanaijua.
Kuficha utambulisho
Binafsi sipendi sana kujulikana kwa sababu ya kazi na pia napenda kuwa na maisha binafsi. Napofanyia
kazi asilimia kubwa mwanzoni walikuwa hawajui kama Nyonyoma Mtu Mbad ndiyo mimi. Kuna muda
nilikuwa nawakuta wanacheki video zangu tunacheka bila kujua ndiyo mimi. Baada ya kuanza kufanya
mahojiano na vyombo tofauti vya habari ndiyo wakaanza kunifuatilia.
Mahojiano yangu nilikuwa naficha sura kwa kitambaa, sasa waki-zoom wanajiuliza mbona huyu jamaa
anafanana jina na sura na mshikaji tunayefanya nae kazi? Nikawa nakwepa kwepa baadae wakajua
ndiyo mimi. Ila maeneo mengine watu hawanifahamu kwa sura.
Watu wanacheka lakini maisha yanabadilika
Sikutegemea wakati naanza kama vichekesho vyangu vitabadili maisha ya watu. Kwa mfano
kuna mtu alinipigia simu kutoka Dodoma alikiri ndoa yake ilikuwa inayumba.
Ilifikia mahali mke wake alirudi mpaka nyumbani. Jamaa akawa anamtumia video
zangu na kumkumbushia kipindi walivyokuwa wakifurahi pamoja wakati wakizitazama.
Kweli mwanamke akatuliza hasira na mpaka sasa wanaishi pamoja. Kuna mtu pia
alishawahi nitafuta baada ya kutazama video clip nikimulezea nyani anampiga kofi
mwenzake kwa kula mtaji badala ya faida. Yule dada aliniambia ile video ilimsaidia yeye
na mme wake, biashara yao ilisimama kwa sababu ya kula mtaji wa biashara.
Majina yanakua haraka kuliko mafanikio
Tasnia yetu ina chgangamoto nyingi, majina yetu yanakua haraka kuliko mafanikio
tunayopata. Kikubwa kutokuta tamaa, mbele kuna faida nyingi japo itachukua muda.
Lakini pia sanaa yetu inachelewa kukua ukilinganisha na nchi nyingine mfano chukulia
Kenya. Wenzetu vichekesho vya majukwaani (stand up comedy) walianza muda kwetu
tulichelewa kidogo. Vipaji vipo vya kutosha. Kwa sasa mambo yanaanza kubadilika,
tasnia ya vichekesho watu wameanza kuingalia kwa umakini.
Aminia kipaji chako
Mitandao ya kijamii bahati nzuri watu wengi wapo huko. Vijana
wengi wanaitumia kupandisha video zinazoonyesha vipaji vyao
na wanatoka. Cha msingi upende unachokifanya na usikate
tamaa. Halafu matarajio vijana tusiwe nayo makubwa sana
hasa tunapoanza, tuna expect too much tukikwama tunakata
tamaa.
18 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE