You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
ULIZA UJIBIWE
NA ELIAS MAEDA
Je, una swali kuhusu
masuala ya kidijitali?
Tucheki kupitia Whatsapp
na tutakupatia majibu
haraka. Namba ipo katika
ukurasa wa 4.
Mambo vipi? Naitwa Hadija, ni mkazi wa Arusha.
Swali langu, nafanya biashara ya vipodozi nawezaje
kuwafikia wateja wengi katika mitandao ya kijamii?
Kabla hujafikiria kuwafikia wateja kwanza hakikisha
kuwa umetengeneza ukurasa wako kwa namna
ambayo watu wataamini huduma au bidhaa unazouza.
Njia ya haraka ya kufikia wateja wengi ndani ya muda
mfupi ni kwa kulipia matangazo au kuwalipa watu
mashuhuri wakutangazie. Kama kipato chako ni kidogo
unaweza kuanza tu wewe mwenyewe na
kujitengenezea wafuasi wako ambao pia ndio wateja
wako.
Mimi naitwa Zainab naishi ilala. Ninauza mitandio
ya wanawake, nifanyaje akaunti yangu iwe na
followers wengi ?
Unapofanya biashara mtandaoni haupaswi
kuhadaika zaidi na followers. Kumbuka kuwa wewe
upo mtandaoni kutafuta wateja na sio followers.
Wateja wako ndio watakuwa followers wako. Weka
nguvu zaidi kuwafikia watu wengi; kidogo kidogo
utapata wateja ambao watakuwa wanafatilia
biashara yako na hao ndio watakuwa followers wako.
Mtandao upi wa kijamii ni mzuri kwa mimi nayeuza
mchele? Rajab Selaman, Tanga
Swali zuri sana. Mitandao yote ni mizuri ila kwa
mfanyabiashara ni lazima kuzingatia wateja wa bidhaa
au huduma zako wapo wapi zaidi. Mitandao mikubwa
zaidi ni Facebook, Twitter na Instagram; hii mitandao
ina aina zote za watu japo kuwa kwa sasa Instagram
na Facebook inatumika na wengi zaidi Tanzania.
Binafsi ningeshauri uwekeze zaidi kwenye mitandao
hiyo mikubwa mitatu ila chagua mmoja wapo wa
Mwaka huu namaliza chuo na napenda sana
mambo ya digital. Ujuzi gani naweza kujifunza na
kuniingiza hela haraka?
kuanza nao. Hongera sana Andronicus. Sijajua ulivyosema
'haraka ni uharaka wa kiasi gani ila binafsi naamini
kiwanda cha digitali kina fursa nyingi na ni vyema
ukazingatia kujifunza na kupata uzoefu wake kabla
ya kuwaza kupata hela haraka. Hata hivyo, hizi ni
baadhi ya fursa na ujuzi ambao yanaweza kukupa
kipata cha haraka ukiwe kufanya kwenye ubora;
graphics designing, content creation, social media
management, masoko ya mtandaoni
Utaratibu wa kodi TRA ukoje kama nikiwa nauza
biashara yangu online tu? Jennifer, Dar
Sina elimu kubwa sana ya kodi, ila binafsi naamini
kuwa kwa biashara yoyote ile halali ambayo inaingiza
kipato ni lazima itambulike kisheria na kuchangia kodi.
Naelewa hili swala ni gumu kidogo haswa kwa
wanaoanza biashara, ila unaweza kujipanga taratibu
na ukaangalia ni namna gani unachangia kodi au
kufika ofisi za TRA kwa ushauri zaidi. Nadhani wao
wanaweza kuwa na
jibu zuri zaidi.
Naona kuna watu huwa wanauza akaunti.
Nikinunua akaunti na biashara yangu nikahamishia
huko ni sawa? Abdul, Chanika
Sio sawa na wala sikushauri kufanya hivyo. Wewe
upo mtandao kutafuta wateja na sio followeres.
Tengeneza ukurasa wako wa biashara na utakua
taratibu, utakuletea wateja na hao ndio watakuwa
followers wako wa kweli. Wewe unauza biashara ya
mayai unaweza ukaenda kununua ukurasa wenye
wafuasi wengi ukiamini kuwa umepata wateja
kumbe hao wafuasi waliufata huo ukirasa sababu
ulikuwa ukisambaza maudhui ambayo hata
hayaendani na biashara yako.
12 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE