You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
Nilipofika chuo, nilianza kufanya comedy
kwa kuji-record video fupi kisha naziweka
katika akaunti yangu ya Instagram. Baadae
kazi zangu zilianza kufuatiliwa sana na
nikaona nahitaji kukua zaidi. Nikaanza
kushiriki katika vichekesho vya jukwaani
(stand-up comedy). Awali nilifanya kama
msanii wa kujitegema baadae nikapata
bahati ya kuwa sehemu ya familia ya Watu
Baki, japo bado sijawa mwaanachama rasmi.
Watu Baki imekuwa ni familia, najifunza
mambo mengi kutoka kwao. Ni kundi lenye
vipaji lukuki na wengine tayari wameshakuwa
na majina makubwa.
Watu Baki nafanya nao mazoezi na kushiriki
katika tamasha linalofanyika The Base Club
kila alhamis. Mwaka huu kuna rafiki yangu ni
mchekeshaji pia alikuja na wazo la kuanzisha
kundi letu litakalo husisha wanachuo wenye
vipaji vya uchekeshaji, ndipo Unicomedy
ilipoanza. Tumekuwa tukiandaa matamasha
yetu wenyewe yanayofanyika chuoni na nje
ya chuo. Kazi yangu imenipa heshima kwa
mwaka huu kupewa tuzo ya mchekeshaji
bora chuoni kwetu.
Mwaka huu Unicomedy tumefanikiwa
kuandaa matamasha mawili na yote
yalifanya vizuri. Mwanzoni tulifanyia London
Lounge, Ubungo. Watu walihudhuria wengi na
baadhi kukosa viti. La pili tukahamia ukumbi
mwingine.
Kati ya vitu ambavyo haviwezi kuepukika ni
mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii
inasaidia sana kusukuma kazi zangu kufika
mbali. Japo changamoto ukishakuwa
maarufu watu wanaanza kutumia jina lako
hali inayowapa ugumu watu wanaponitafuta.
Mitandao imesaidia sana kujenga brand
yangu na kuonyesha uwezo wangu kwa
watu. Napgia simu na kupata mialiko kuperform
katika sherehe tofauti.
Mitandao pia imenikutanisha na ma-star
wakubwa, wengine ni role model wangu.
Mfano Kendrick Mulamula kutoka Kenya,
tuliwasiliana kupitia mitandao ya kijamii na
kubadilishana namba. Mpaka leo
tunawasiliana vizuri tu. Mpaka sasa
nimefanikiwa kufanya kazi na wasanii
wakubwa tofauti kama Idris Sultan ambaye ni
role model wangu, Francis Nalimi na wengine
kutoka Watu Baki.
Comedy kwa sasa sio kama zamani ambapo
ili uonekane mchekshaji uvae kiajabu ajabu
na watu kukuona kama kituko. Na ilichangia
sana malipo madogo ukilinagnisha na
wasanii wengine wa bongo movie kwa
sababu tulionekana kama vituko tu.
Mtazamo hasa kwa Dar umebadilika sana.
Changamoto bado mikoani kama kule kwetu
Simiyu bado waigizaji wengi wamekuwa na
mtazamo wa vituko badala ya vichekesho.
Kama mwanafunzi changamoto kubwa
nayopitia ni kupigana vizinga, wanafunzi
wengi wanafikiri nina hela nyingi. Wakiona na
star mkubwa wanajua jamaa
ameshayapatia, ukimnyima hela anahisi
umemkazia. Pia nyumbani wana-support
lakini kwa mashaka. Wazazi wananilipia ada
wanahisi sanaa inaweza kuniharibia masomo.
Ila taratibu wanazidi kuelea hii ni kazi na kwa
upande wa masomo haina athari yoyote ile.
22 | AUG 2021MEMA MAGAZINE