Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Waja leo, huondoki leo
ABBASI ISMAIL
Mambo vipi washikaji? Naitwa Abbasi maarufu Abby boy. Ni
mzaliwa na mkazi wa Muheza, mkoani Tanga. Leo
nakutembeza Muheza ujue yale usiyoyajua. Muheza ni wilaya
kongwe nchini ilianzishwa mwaka 1976. Kihistoria kulipiganwa
vita kati ya Wabondei na Wadigo katika pwani ya Tanga.
Wabondei walichakazwa na kukimbilia maeneo ya Muheza na
walipofika hapo walisema “Hanu Mheza” ikimaanisha hapa
mmekwisha. Kweli Wadigo waliufuata moto kwani
walitembezewa kichapo na kurudi pwani ya Tanga na mpaka
leo Wadigo wapo wengi Tanga mjini na Wabondei wakabaki
kama wenyeji hapa Muheza.
Ukipita Muheza utakuta imepambwa na mandhari ya kuvutia
yenye milima, mito na majengo ya kihistoria yaliyoachwa na
wakoloni. Wilaya ya Muheza ina mitaa mingi maarufu ikiwemo
Magila ambapo kuna shule ya kwanza ya msingi kujengwa
hapa nchini wakati wa ukoloni. Mitaa mingine ni Tongwe,
Ngomeni, Pande, Mtimbwane n.k. Wilaya yetu ina ukubwa wa
eneo la kilomita za mraba 1,470.
Mishe za kibiashara zipo kibao, muhimu kuchangamkia fursa.
Kuna mishe za kilimo kama machungwa, katani n.k. Muheza
ina vivutio vingi vya utalii ikiwemo misitu maarufu ya Amani na
Magoroto maarufu Bali of Africa. Huko kuna mambo mengi ya
kupendeza ambayo huwezi kujutia ikiwemo maporomoko ya
maji, bwawa zuri la kuogelea, wanyama kama farasi na ndege
wengi wazuri. Msitu wa hifadhi ya Amani una vipepeo wa
pekee duniani ambao wananchi huwafuga na kuwauza nje ya
nchi.
5 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE
Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA ni
mbunge na moja ya watu maarufu kutoka
Muheza.