Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
JIBEBE
IMANI NSAMILA
SAFARI YA BWANA LENS NA
MSIMULIZI WA MAZINGIRA
PETER LAZARO
Mwanzo wa Safari
Naitwa Imani Nsamila, ni mpiga picha na
mwanaharakati wa mabadiliko ya tabia nchi.
Tangu nikiwa mdogo napenda kupiga picha.
Wakati nipo shule ya sekondari baba yangu
alikuwa na kamera ndogo ambayo alikuwa
akiitumia katika ofisi yake.
Nikawa naichukua naenda kuwapiga picha
marafiki zangu ambao walikuwa wana bendi
ya muziki, baadhi ya picha zao mpaka leo
ninazo. Awali nilikuwa nafanya tu kwa
mapenzi, nilipomaliza sekondari nikachagua
kusomea fani ya utengenezaji wa filamu
katika chuo cha Kilimanjaro Film Institute
katika jiji la Arusha. Nikiwa mwaka wa tatu
sikufanikiwa kumaliza chuo, nilipata ajali na
kuvunjika mkono. Ilinilazimu nirudi nyumbani
Dar Es Salaam na madaktari walinishauri
nisibebe vitu vizito, ingekuwa ngumu
kuendelea na mafunzo ya utengenezaji filamu
kutokana na kamera tulizokuwa tunatumia
katika mafunzo zilikuwa ni nzito.
Wakati nipo nyumbani nikawa nahudhuria
katika mtandao wa vijana uliofahamika kama
Youth Climate Activist Network uliokuwa chini
ya Norwegian Church Aid. Walikuwa na
programu ya Climate Change Caravan na
tulikuwa tunazunguka maeneo tofauti nchini
kutoa elimu ya mabadiliko ya tabia
nchi.Kipindi cha ugonjwa na baada ya
ugonjwa niliendelea kuwa najitolea kama
mpiga picha.
Novemba 2014 nilitolewa vyuma mkononi na
kurudi katika maisha yangu ya kawaida.
Nikaendelea na shughuli za kupiga picha,
nikawa nakutana na watu tofauti katika mishe
zangu. Mwaka 2015 nilipata kazi ya kushoot
katika taasisi fulani ambao baada ya
kumaliza walipenda sana kazi yangu.
Nashukuru Mungu nimeendelea kupata fursa
tofauti ambazo nyingi zinatokana na watu
ambao nilifanya nao kazi kunipendekeza
zinapojitokeza fursa.
Mfano mwaka 2017 nilibahatika kushuhudia
uchaguzi wa Liberia kama mpiga picha,
uchaguzi ambao ulimpa ushindi aliyekuwa
mchezaji mpira maarufu George Weah.
10 | AUG 2021 MEMA MAGAZINE