19.02.2015 Views

Mahusiano ya Walimu na Wazazi katika Malezi ya Watoto - HakiElimu

Mahusiano ya Walimu na Wazazi katika Malezi ya Watoto - HakiElimu

Mahusiano ya Walimu na Wazazi katika Malezi ya Watoto - HakiElimu

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Mahusiano ya Walimu

na Wazazi katika

Malezi ya Watoto

Utafiti kuhusu Mazingira

ya Kazi na Maisha ya Walimu

Tafiti Namba 3

3

MAHUSIANO YA WALIMU

NA WAZAZI KATIKA

MALEZI YA WATOTO

Utangulizi

“… Mwenyekiti wa umoja wa walimu wakuu Dar es Salaam,

Mwalimu Mwantumu Mahinza alisema …. Matokeo mazuri ya

miaka iliyotangulia hayakutokana na hila zilizokuwa zikifanyika,

bali ni utendaji mzuri, uwezo wa wanafunzi na ushirikiano baina

ya wazazi na walimu … hali yakuwapa nafasi na uhuru walimu

wa kupanga na kujituma pasipo kikomo na ushirikiano wa hali na

mali kwa wazazi pia vilichangia mafanikio hayo …” na Mwandishi

wetu, gazeti la Mtanzania, 17 January 2004 Kichwa cha Habari

“Walimu: Hizi ndizo sababu za kushuka kwa elimu Dar”

Mara tu ilipopata uhuru, Tanzania iliweka mikakati ya kufuta ujinga, umasikini na

maradhi. Ili kuchochea kasi ya maendeleo, walimu walipewa nafasi muhimu sana katika

maendeleo ya taifa letu. Pamoja na umuhimu wao, mchango wa walimu umekuwa

hawatambuliwi katika jamii. Walimu wamekuwa wakiishi na kufanya kazi katika

mazingira magumu sana. Nyumba za kuishi zenye hadhi duni kabisa, ufinyu wa

mishahara yao, kutopewa maslahi yao stahiki kisheria kama vile malipo ya uhamisho

na likizo, na hata posho nyingine mbali mbali.

Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya walimu ni ndogo sana ikilinganishwa na idadi ya

wanafunzi waliopo mashuleni. Hali hii imekuwa inawaongezea walimu mzigo mzito wa

kazi ya ufundishaji, ufuatiliaji na uratibu wa maendeleo ya wanafunzi. Hali inazidi kuwa

mbaya karibu kila mwaka kutokana na mwamko uliojitokeza miongoni mwa wazazi,

hususani baada ya kuanzishwa kwa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi

(MMEM) nchini ambapo idadi ya wanafunzi waliosajiliwa darasa la kwanza mwaka

2002 na 2003 imeongezeka maradufu kwa zaidi ya asilimia 500% wakati idadi ya

walimu imeogezeka kwa kiwango kidogo tu.Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 1997,

uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi ulikuwa 1:37 wastani wa taifa, ambapo kufikia

mwaka 2002, uwiano ulikuwa kwa 1:53 wastani wa taifa, japo katika sehemu nyingi

hususan mijini wastani uko juu zaidi ya 1:87 (Ripoti ya Tathmini ya MMEM, 2003).

Pamoja na juhudi kubwa inayofanywa na walimu katika kukabiliana na mabadiliko hayo,

bado wanakosa ushirikiano wa dhati kutoka kwa baadhi ya wazazi. Hali hii imedidimiza

motisha kwa walimu katika kuleta mabadiliko ndani ya shule na kijiji kwa ujumla.

Mahusiano na Wazazi

1

Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kwa kushirikiana na HakiElimu, wamefanya utafiti

kuanzia Septemba 2003 hadi Desemba 2003 juu ya maisha na mazingira ya kazi ya

walimu katika wilaya saba nchini ili kuweza kupata mawazo na mtazamo ya walimu juu

ya hali ya maisha na kazi ya ualimu. Matokeo ya utafiti huo, yanalenga kuchangia katika

mijadala mbali mbali ya serikali juu ya kuboresha hali ya walimu kwa lengo la kuinua

kiwango cha ubora wa elimu inayotolewa nchini. Utafiti umekusanya takwimu za

mahojiano yaliyohusisha watu 298, dodoso 1385 na ‘case study’ 10 katika wilaya saba,

wilaya moja katika kila kanda ya Elimu yaani kanda ya kati, kanda ya nyanda za juu

kusini, kanda ya kaskazini, kanda ya kusini, kanda ya mashariki, kanda ya ziwa na kanda

ya magharibi.

Utafiti huu uliangalia nyanja mbali mbali zinazoweza kuchangia kuboresha au

kudidimiza hali ya maisha na kazi ya walimu. Hii ilikuwa ni pamoja na: Mzigo wa kazi

ya ufundishaji, uwiano wa wanafunzi kwa mwalimu mmoja, maendeleo ya walimu

kitaalamu, athari za UKIMWI katika kufundisha na kujifunza, maisha ya walimu pamoja

na maslahi ya walimu. Taarifa ifuatayo inachambua matokeo ya ‘case study’

yaliyopatikana katika nyanja ihusuyo:

“Mahusiano ya Walimu na Wazazi katika maendeleo ya Elimu.”

Utafiti umeongozwa na Prof. Suleman Sumra na Prof. Verdiana Grace Masanja wa

HakiElimu ambapo Mr. Anthony Mtavangu wa CWT ameshughulikia maswala yote ya

kiutawala kwa upande wa CWT. Watafiti ni Edward Masanja na Mwalimu Finesta Savai

(Ilala), Amina Mnenge na Mwalimu Shaibu Mohamedi (Lindi), Francis Mkwawa na

Mwalimu Isidory Mwangeni (Ludewa), Kemirembe L. Mukyanuzi na Mwalimu Cecilia

Tzahaki (Moshi Mjini), Shaaban Mtengeti na Mwalimu Abel P. Mwangalyagila Manyoni,

Lembris Laanyuni na Mwalimu Oswald Rulatunya (Kibondo) na Dorothy Karoli na

Mwalimu Mafuni Yango (Mwanza).‘Case Study’ hii imeandikwa na Bwana Peter Khalid

na imehaririwa na Prof.Verdiana Grace Masanja.

Matokeo ya Utafiti

Uhusiano mzuri kati ya wazazi na walimu huimarisha na kujenga maendeleo mazuri ya

kazi za walimu na kuifanya kuwa rahisi zaidi. Kuwepo na mahusiano mazuri, hupelekea

mwalimu kujiamini na kuwa na uhakika wa kila anachokifanya kwa kujua anaungwa

mkono na wazazi. Lakini iwapo uhusiano unakuwa si mzuri, mwalimu huishi kwa

wasiwasi na kutokujiamini katika kila jambo analofanya, haswa lile litakalohitaji

kuungwa mkono na wazazi.

2

Mahusiano na Wazazi

“Jamii huwaona walimu ni waonezi”

Nafasi ya wazazi katika kuimarisha nidhamu ya wanafunzi ni kubwa sana. Shule inahitaji

sana ushirikiano mzuri kati yake na wazazi katika nyanja zote zinazohusu

kuwafundisha maadili mema watoto. Kumekuwepo na ushirikiano mdogo katika shule

nyingi, na hii inatokana na muonekano wa jamii kuwa walimu ni waonezi, hupenda

kuwaadhibu watoto bila sababu, na wana chuki kutokana na kutopewa maslahi ya

kutosha.

Walimu walisema kuwa wao ni kama walezi na wanakuwa na jukumu kubwa la

kuwalea watoto katika maadili mema yatakayowajenga. Lakini wamekuwa na wakati

mgumu sana kwa kutokuwepo kwa ushirikiano wa wazazi katika kuangalia taratibu za

kuwarekebisha watoto wao. Kwenye baadhi ya shule walimu walisema, iwapo

mwanafunzi anafanya makosa mara nyingi wanakuwa na taratibu wanazofuata ikiwemo

kumshirikisha mzazi mwenyewe ili aweze kujua kinachoendelea na kushiriki katika

kutoa maamuzi.

Walisema, hatua ya kwanza ni kikao maalum cha walimu ambao huzungumzia matatizo

ya mwanafunzi husika na kuorodhesha matatizo yake yote, baadaye huitwa na

kuelezwa utovu wake wa nidhamu na kuonywa. Iwapo mwanafunzi huyo ataendelea

kutokuwa na nidhamu inayoridhisha, au kuendelea kuvunja taratibu za shule, ndipo

mzazi hushirikishwa kwa kuitwa kwenye kikao kingine na kuelezwa matatizo ambayo

walimu wamekuwa wanayapata dhidi ya mtoto wake.Wote kwa pamoja hukubaliana

aina ya adhabu ya kumpa mtoto wake kama hatua ya kumkumbusha wajibu wake.

Mahusiano na Wazazi

3

Walimu waliohojiwa wamesema ya kuwa wakati mwingine wanapata matatizo na

kukwaruzana na wazazi pale wanapotoa adhabu kwa watoto. Walisema adhabu kwa

mwanafunzi ni sehemu ya kumkumbusha wajibu wake na sio kumuumiza.Walisema ya

kuwa wazazi waliojiingiza katika vyama vya siasa wao kila kitu huona sio haki na mara

nyingi wamekuwa hawataki watoto wao waonywe wala kuadhibiwa hata kama

wametenda kosa. “Wamekuwa wanatuona sisi walimu kama tumewekwa na chama

kilichopo madarakani, kitu ambacho si sahihi”.

Pamoja na kutumika kwa adhabu, bado walimu walisema isitumike kupita kiasi. Iwe tu

ni sehemu ya kutoa onyo na sio sehemu ya kukomoa mwanafunzi.Walisema ya kuwa

ikitumika vibaya inaweza kuleta madhara kwa mwanafunzi kama vile kuleta usugu na

hivyo kumfanya awe jeuri zaidi, kusababisha nidhamu ya woga miongoni mwa

wanafunzi na hata kuleta athari kisaikolojia.

Adhabu ndogo kama hizi ni sehemu ya mafunzo kwa mtoto na mazoezi ya mwili.

“Walimu wapenda maendeleo huwa ni maadui wa wazazi”

Pamoja na kuwepo kwa juhudi nyingi miongoni mwa walimu, ilibainishwa kuwa wapo

wazazi ambao hawapendi walimu wapenda maendeleo. Mwalimu akiwa na juhudi za

kuleta mabadiliko ya elimu katika shule yake anakuwa adui wa baadhi ya wazazi.

Akitoa mfano Mwalimu Fidel Nderego (43) wa Shule ya Msingi Kabare, wilaya ya

Kibondo, anasema kuwa alijitahidi kuweza kubadili sura ya shule ya Kabare kuanzia

mazingira yake kwa kuhamasisha jamii na kuweza kupata majengo mazuri ikiwemo

nyumba za walimu za matofali na kuezekwa kwa bati. Pamoja na juhudi zake, amekuwa

4

Mahusiano na Wazazi

anakutana na vitisho juu ya maisha yake kama alivyosema:

“Kitu ambacho kinanisikitisha ni mapambano ya kushughulika, nimekutana na

vikwazo vingi sana toka kwa wananchi wapinga maendeleo. Niliandikiwa barua

zenye vitisho. Nilitishiwa kuwa nyumba yangu itachomwa na nimekuwa

naviziwa njiani na kupigwa na mawe bila sababu, na watu hao sijawafahamu

hadi leo.”

Akichangia juu ya mahusiano ya wazazi na walimu, Mwalimu Pancracia Mtawali (48)

Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Magereza iliyopo Manispaa ya Moshi alisema, kutokana

na kuwa na hadhi ya chini kwa walimu, wamekuwa wanadharaulika haswa na wazazi

ambao wamejaliwa kuwa na uwezo kidogo. Alisema ya kuwa tofauti hii inasababisha

kuwepo na pengo kubwa kati ya wazazi na walimu na hata miongoni mwa wanafunzi

wenyewe.Akielezea alisema;

“Inakuwa ni vigumu sana kuwazoea wazazi kwani wengi wanaonekana

kutowathamini walimu. Niliwahi kukwaruzana na wazazi kwa sababu unakuta

mzazi anakuwa upande wa mtoto wake mara zote hata kama mtoto huyo

anakosa. Unajua wazazi wengi ni matajiri. Uwezo huo walionao ndio unaowapa

kiburi. Iwapo mwalimu akimbana mwanafunzi mzazi anakuja juu na kutuona

sisi walimu ni dhiki tu inatusumbua. Hii ni kutokana na uduni wa maisha tuliyo

nayo sisi walimu.”

Akiongezea juu ya matatizo aliyowahi kuyapata alisema kuwa, aliwahi kutoa adhabu ya

viboko mbele ya wazazi kwa wanafunzi ambao walivunja sheria za shule kwa kupigana

darasani, pamoja na kuwashirikisha wazazi alijikuta yupo polisi.

“Wanafunzi wawili wa kiume walipigana hadi wakavunja madawati darasani

mwao. Sikuwaadhibu kwanza niliwaelezea juu ya kosa lao na kuwa wamevunja

sheria ya shule. Kila mmoja alitoa maelezo yake kisha nikachukua hatua ya

kuwaita wazazi wao. Wazazi waliitikia wito na kufika shuleni. Tukakubaliana

kuwa waadhibiwe kwa kuchapwa viboko ili kuwarudi. Mimi kama mkuu wa

shule nilipewa jukumu la kutoa adhabu hiyo niliwachapa mbele ya wazazi wao

na kila mzazi alionekana kuridhishwa na uamuzi tuliouchukua pamoja. Kitu

cha ajabu ni pale nilipoitwa polisi kwa ajili ya kujibu shitaka la kumchapa

mwanafunzi baada ya mmoja wa wazazi kwenda kunishtaki. Kwa kweli nilipata

mshituko kwani maamuzi tuliyachukua kwa pamoja halafu iweje anizunguke

na kunishtaki? Baada ya kutoa maelezo polisi ilionekana nilitimiza wajibu kama

ilivyotakiwa na kwa matakwa ya wazazi wenyewe. Kwa bahati nzuri hatukufika

mbali sana kwani baadaye tulisuluhusishwa. Sasa hali kama hii mimi kama

binadamu nitajisikiaje?”

Mahusiano na Wazazi

5

“Wazazi huvua jukumu la kudhibiti utoro wa watoto wao”.

Wakielezea zaidi walimu walisema katika shule zenye tatizo la utoro, mara nyingi

wazazi hujivua jukumu la kumdhibiti mtoto wao na kuona kuwa mwenye wajibu wa

kuona kama mtoto anaenda shule ni mwalimu. Lakini ukiangalia kwa undani wote

wawili wanatakiwa kushirikiana katika hilo. Akielezea zaidi juu ya majukumu ya wazazi

katika maendeleo ya watoto wao, Mwalimu Hamisi Mapila (36) Mwalimu Mkuu wa

Shule ya Msingi Mnazi Mmoja iliyopo katika wilaya ya Lindi alikuwa na haya ya kusema:

“Jamii yenyewe haitambui sana umuhimu wa shule. Kwani wakati mwingine

mtoto anaweza akachaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari, lakini

wazazi wanasema hawana uwezo wa kumlipia kwa madai ya hali ngumu ya

uchumi, lakini kinakuwa ni kisingizio tu. Pia kwa watoto watoro shuleni, baadhi

ya wazazi huchangia kwani hawasaidii katika kukemea hilo. Watoto watoro

mara nyingi huwa nje ya darasa kwa siku nzima na hata zaidi na wazazi

hawajali.Wakati mwingine watoto hao wanakuwa katika biashara ndogondogo

katika maeneo ya kituo cha basi.”

“Mazingira ya shule ilipo yanaathari kiutendaji”.

Aidha sehemu shule zilipo imeonekana kuwa ni tatizo na kikwazo kikubwa kwa

walimu. Wakitolea mfano, wamesema shule ambazo zimo ndani ya taasisi hasa zile za

kijeshi inatumika amri zaidi toka kwa wazazi kuliko majadiliano. Akitoa mfano

Mwalimu Mwangilika Festo (35) anayefundisha Shule ya Msingi Magereza iliyopo

Manispaa ya Moshi ndani ya maeneo ya Jeshi la Magereza alisema

6

Mahusiano na Wazazi

“Kutokana na eneo shule hii ilipo ndani ya gereza kumekuwepo na ugumu

sana katika kazi yetu. Kuna kutumia nguvu zaidi kuliko majadiliano. Mtoto

akiadhibiwa hapa mzazi hukimbilia polisi haraka, labda kwa ajili ya uhusiano

uliopo. Hali hii inatufanya walimu tuwe waangalifu sana na matokeo yake ni

kushuka kwa vyote, nidhamu ya wanafunzi na maendeleo ya kitaaluma.”

Akizungumzia juu ya ushirikiano wa wazazi na walimu, Mratibu Elimu Kata, Mwalimu

Alex Mpombwe wa kata ya Nkonko iliyopo katika wilaya ya Manyoni, amesema

matatizo yakutokuwepo kuelewana kati ya walimu na wazazi yanatokana na utovu wa

nidhamu wa wanafunzi unaochangiwa na wazazi wenyewe.

Matokeo yake wanafunzi wanajenga chuki na walimu, inafikia hatua ya wanafunzi

kuwasingizia walimu wao kwa wazazi kwani wanajua kuwa wazazi wao watawasaidia.

Na mara nyingi wazazi wamekuwa wanachukua maamuzi kwa jazba na kuwatolea

lugha chafu sana walimu.

Sasa sijui wazazi wanafikiri wanamjengea msingi gani mtoto wao? Aliuliza Mwalimu Alex.

Akitolea mfano binafsi, Mwalimu Alex alisema kuwa alishawahi kusingiziwa na mwanafunzi

kuwa ni mbakaji wakati huo alipokuwa akifundisha.

“Misukosuko waipatayo walimu huathiri maendeleo ya watoto”

Wazazi wanasahau kuwa misukosuko ambayo wanawasababishia walimu huwa na

athari kwa watoto wao pia. Mwalimu Gaudensia M. Shada (30) ni Mwalimu Mkuu

Msaidizi katika Shule ya Msingi Mnazi Mmoja iliyopo Wilaya ya Lindi, shule ambayo

amekuwa akifanya kazi tangu apate ajira mwaka 1996 mwezi wa 8. Mkasa uliomkumba

yeye kutokana na kusingiziwa na mzazi ulileta usumbufu mkubwa hata kwa wanafunzi

pia.

Mwalimu Shada ambaye ni Mwalimu Mkuu Msaidizi na pia mwalimu wa nidhamu kwa

wanafunzi, mwezi Machi 2003 akiwa ofisini aliletewa taarifa kuwa wanafunzi wawili wa

kike wa darasa la sita (tutawaita Somoye na Bella lakini si majina yao halisi) walikuwa

wakipigana darasani, alichukua hatua ya kwenda darasani. Aliwakuta Somoye na Bella

wakipigana, mara walipomuona walitahayari kwa kuwa walijua kuwa ni kosa kupigana

shuleni.

Kwa kuwa kupigana shuleni ni kinyume na sheria za shule hivyo hao wanafunzi

walistahili kupata adhabu.

Mahusiano na Wazazi

7

“Niliwaita hao wanafunzi wawili waliokuwa wakipigana, na kuwaonya mbele ya

wanafunzi wenzao darasani. Kwa sababu walifanya kosa kinyume cha sheria

za shule walistahili adhabu, hivyo niliwachapa fimbo mbili mbili mikononi kila

mmoja. Adhabu kama hii ni ya kawaida hapa shuleni na hasa kwa makosa

kama haya, na wakati mwingine hata wazazi wanaweza kuitwa kuthibitisha

utovu wa nidhamu wa watoto wao na watoto huadhibiwa mbele ya wazazi

wenyewe. Adhabu hii ilishuhudiwa na wanafunzi wa darasa la sita, kwani

ilitolewa mbele yao na Somoye na Bella walionekana kujutia tendo lao la

kupigana baada ya adhabu hiyo.”

Katika hali isiyo ya kawaida, adhabu ndogo aliyoitoa Mwalimu Shada, ilibadili maisha

yake na hata mtazamo aliokuwa nao juu ya utendaji kazi ya ualimu. Hali hii imemfanya

kuathirika kisaikolojia, na kukata tamaa hata kuona kuwa maisha yake yapo hatarini.

Akielezea kwa undani juu ya tukio kubwa lililomtokea ambalo limepelekea hali hiyo,

mwalimu Shada alikuwa na haya ya kusema:

“Nikiwa shuleni nililetewa taarifa ya Polisi ya kutakiwa kufika kituoni kutoa

maelezo ya kumjeruhi mwanafunzi Bella. Nilishtuka sana kwani sikutarajia

kuwa itafikia hatua hiyo. Niliongozana na mwalimu mkuu, ambaye tayari

alikuwa na taarifa ya kuadhibiwa kwa wanafunzi hao wawili.Tulipofika kituoni,

nilielezea kwa kusaidiana na Mwalimu Mkuu tukio zima jinsi lilivyotokea na

hatua zilizochukuliwa. Baada ya melezo hayo Polisi iliridhika na maelezo yangu

na kuona nilikuwa natimiza wajibu kama ilivyostahili. Hivyo walichukua jukumu

la kutusuluhisha na mzazi wa Bella. Walijaribu kumueleza kuwa hayo ni

mambo ya kawaida shuleni. Walimuelimisha mzazi kuwa sisi walimu pia ni

wazazi na walezi hivyo hatuwezi kumuadhibu mtoto kwa lengo la kumuumiza,

bali kumrekebisha ili afuate maadili mema. Na walitoa ushauri wa kuitisha

kikao cha kamati ya shule ili mzazi aitwe kuelezwa zaidi hali ile na pengine

kutafuta muafaka baina yangu na mzazi. Lakini bado mzazi hakuridhika na

uamuzi huo, kwani alitarajia mimi niwekwe ndani. Mwalimu Mkuu ilibidi

aniwekee dhamana ili nisiwekwe mahabusu.

Mwalimu mkuu alifuata ushauri aliopewa Polisi na aliitisha kikao cha dharura

cha Kamati ya shule na mzazi wa Bella alipelekewa taarifa ya kuhudhuria

kikao hicho. Wanakamati waliitikia wito huo mara moja, walihudhuria kikao

hicho, lakini mzazi wake Bella hakuhudhuria kabisa.Taarifa zilizopatikana

baadaye zilisema kuwa mzazi wa Bella hakuhudhuria kikao hicho kwa sababu

eti yeye hawezi kusuluhishwa na Kamati ya shule, na wala Kamati hiyo haina

mamlaka yoyote juu yake. Kamati iliamua kumuacha mzazi afanye kile

anachotaka.”

8

Mahusiano na Wazazi

Lakini kwa upande wa wazazi wa Somoye, kuadhibiwa kwa mtoto wao waliona ni

kitendo sahihi kama hatua ya kumfundisha mtoto. Hawakuchukua hatua kama za mzazi

wa Bella, bali walimuonya mtoto wao na kumtaka kuwa mtiifu kwa walimu wake na

kufuata kanuni na sheria za shule.

Mzazi wa Bella baada ya kukataa suluhisho la polisi na kugoma kuhudhuria kikao cha

kamati ya shule alichukua uamuzi wa kufungua kesi ya madai katika mahakama ya

wilaya ya Lindi. Ili aweze kutimiza lengo alilolikusudia, alizunguka katika hospitali

mbalimbali ili aweze kupatiwa cheti kitakachothibitisha kuwa mtoto wake ameumizwa

sana na pia amepata athari katika ubongo wake.

“Hawa walimu wamezoea tu kutuendesha, mwaka huu lazima niwafunge tu hata kama

ni kuuza mifungo yangu yote. Nitafunga mmoja mmoja hadi waishe, sababu nitakuwa

nazitafuta”

Alienda katika hospitali ya misheni ya Nyangao na hospitali ya mkoa, Sokoine ambako

aliomba mtoto wake apigwe picha ya mionzi (X-ray). Bahati mbaya au nzuri, hospitali

zote matokeo yalionyesha kuwa mtoto hajaathirika sehemu yoyote zaidi ya

kuonekana na malaria. Mzazi wa Bella hakufurahia matokeo hayo, hivyo aliendelea

kuwashawishi madaktari kuwa mtoto wake alipoteza fahamu baada ya kupewa adhabu

na mwalimu, na kuwa ameathirika kichwani. Lakini daktari anayehusika na magonjwa

ya akili alithibitisha kuwa mtoto ni mzima kabisa wala hajawahi pata athari yoyote

kichwani.

Mwalimu Shada pamoja na Mwalimu Mkuu, waliitwa mahakamani kujibu shitaka la

kumjeruhi mwanafunzi.

Akiendelea kuelezea mwalimu Shada alisema:

“Nilihudhuria mahakamani pamoja na mwalimu mkuu ili kutoa utetezi wangu.

Tulijieleza kwa kina juu ya tukio zima na taratibu zilizochukuliwa. Mahakama

ikaamua kuita mashahidi ili kuthibitisha maelezo yetu na ya mzazi

anayenishitaki. Mashahidi walioitwa ni pamoja na Bella mwenyewe, Somoye na

wanafunzi wa darasa la sita waliokuwepo siku ya tukio.

Wakati wa ushahidi ilionyesha wazi kuwa Bella alifundishwa maneno ya

kusema na mzazi wake, kwani alisema kuwa alichapwa na gongo kubwa sana

ambalo lililetwa mahakamani kama ushahidi, na aliumizwa sana na kupoteza

fahamu. Alielezea kuwa mzazi wake alifika shuleni kumbeba baada ya kuwa

amepoteza fahamu na kumrudisha nyumbani.

Kwa upande mwingine, wazazi wa mwenziwe, Somoye, walimuonya mtoto wao

juu ya kusema uongo hata kama mzazi wa Bella atamtishia kwa hali yoyote

Mahusiano na Wazazi

9

ile. Hivyo alipotoa ushahidi wake alielezea kwa ufasaha kila kitu jinsi

kilivyotokea na hatua nilizozichukua dhidi yao wote wawili. Maelezo ya Bella

yaliendana kabisa na ya wanafunzi wengine wa darasa la sita walipoitwa kutoa

ushahidi wao na pia yalifanana labisa na yangu. Mashahidi walidhibitisha kuwa

maelezo ya Bella ni ya uongo, na kuwa hakuumizwa popote pale na pia

waliondoka naye kurudi nyumbani akiwa anatembea mwenyewe.”

Kwa upande mwingine, mama yake Bella hakutaka kabisa kujihusisha na suala hili tangu

awali. Kwani yeye alikiona kitendo kile kuwa ni sawa, na ni sehemu ya kumuadabisha

mtoto. Katika hatua zote hizo, hakuwahi kufika polisi na hata mahakamani. Hata pale

mahakama ilipotaka kujua kuhusu mama, baba alijibu kuwa yeye ndio anayeshughulikia

suala hilo kwa niaba ya familia. Labda alijua kuwa mama yake Bella ataweza kupingana

na maelezo yake na ya mtoto wake.

Kesi hii ilichukua takribani miezi mitano hadi kutolewa kwa hukumu yake. Katika

kipindi chote cha kuendesha kesi hii, Mwalimu Shada hakuwa akifundisha kwa uhuru

na wakati wote alikuwa na wasiwasi sana juu ya usalama wa maisha yake na familia

yake. Kwani mzazi wa Bella alikuwa akipita kijijini akijitapa kuwa lazima angelifanya

lolote ikiwa ni pamoja na kumfunga gerezani au hata kumdhuru kwa namna yoyote.

Akielezea juu ya muendelezo wa kesi na hukumu iliyotolewa Mwalimu Shada alisema:

“Uongozi wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) ulinisaidia katika utoaji wa

hukumu. Kwani waliitafuta sheria ya adhabu kwa wanafunzi mashuleni ya

mwaka 1979 na kuileta mahakamani kama ushahidi wa hatua niliyoichukua

ilikuwa ndani ya sheria za nchi.

Kwa kutumia ushahidi uliotolewa na wanafunzi waliokuwa mashahidi na yangu

mwenyewe na uthibitisho wa matokeo ya vipimo vya hospitali na wa sheria ya

elimu kuhusu adhabu kwa wanafunzi shuleni, mnamo tarehe 14 Julai 2003,

mahakama iliniona sina kesi ya kujibu na hivyo kuniachia huru. Mahakama

ilimshauri mzazi wa Bella iwapo hakuridhika na hukumu hiyo, anaruhusiwa

kukataa rufaa kwenye mahakama ya juu zaidi. Hajafanya hivyo hadi leo, bali

ameendelea kunitishia maisha na kuwa atanitesa kwa namna nyingine yoyote

ile.”

Wafanyakazi wenzake ikiwemo walimu wa shule mbalimbali ndani ya kata yake,

viongozi wa elimu wilayani na viongozi wa Chama cha Walimu, walikuwa wakimfariji

sana tangu kesi hiyo ilipoanza. Lakini alielezea kuwa msaada wao ulikuwa ni wa

maneno ya faraja tu. Kwani mwenendo mzima wa kesi umemgharimu pesa nyingi,

kwani alikuwa na jukumu la kuwasafirisha wanafunzi ambao walikuwa ndio mashahidi

wake, pia kuhakikisha kuwa wanapata chakula wanapokuwa mahakamani. Kwani

makao makuu ya wilaya ambako kesi ilikokuwa inasikilizwa ni umbali wa kilometa 24

toka hapo shuleni. Gharama zote hizo alikuwa anazitoa mfukoni mwake, si msaada

10

Mahusiano na Wazazi

wowote toka kwa walimu wenzake, si chama cha walimu na wala muajiri wake

aliyechangia angalau sehemu ndogo sana ya gharama katika kesi hii.

“Kesi hii imeniathiri sana kisaikolojia. Kwani nilikuwa natimiza wajibu wangu

kama mwalimu wa nidhamu, pili nilikuwa ndio mwalimu mkuu kwa wakati huo,

kwani mwalimu mkuu alikuwa nje ya kituo, na tatu nilikuwa ni mwalimu wa

kike ambaye kisheria ndiye ninayetakiwa kuwaadhibu watoto wa kike. Badala

ya wazazi kutambua wajibu wangu wananiadhibu kwa kunipeleka

mahakamani, hivi haki iko wapi?

Nilijaribu kuomba uhamisho ili nirudi nyumbani kwetu. Lakini nilipata faraja

toka kwa maafisa elimu wilayani kuwa hiyo ni misukosuko ya kawaida kazini.

Pia namshukuru mume wangu kwani alinipatia msaada mkubwa sana kipindi

chote cha kesi, ingawaje na yeye alikuwa tayari kulipiza kisasi. Tatizo kubwa

tunalolipata katika eneo hili sisi walimu, ni kwamba unapokuwa mchapa kazi

sana basi huchukiwa sana na wazazi kwa madai kuwa unawasumbua watoto

wao, na hii ni kero kubwa kwa shule. Lakini wale walimu ambao ni walevi,

hupendwa sana na kuonekana ni wenzao.”

Kwa kipindi chote cha miezi mitano ya ufuatiliaji wa kesi hii, wanafunzi wamekuwa

wakiathirika pia. Mwalimu Shada amekuwa akifuatilia kesi yake, na hivyo kutohudhuria

madarasa, wanafunzi waliokuwa wanatoa ushahidi nao pia wamekuwa hawahudhurii

madarasa. Aidha walimu waliokuwa wanampa faraja Mwalimu Shada walikuwa

wanahudhuria mahakamani ili kuweza kuonyesha mshikamano na kutaka kujua hatima

ya mwenzao na hivyo wanafunzi wa madarasa mengine nao walikosa masomo.

Akitoa maoni yake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mnazi Mmoja Mwalimu Hamisi Mapila

(36) alisisitiza umuhimu wa kujua sheria na kanuni mbalimbali za sekta ya elimu.

Alisema kutokujua sheria kunaweza kuwa na madhara makubwa katika utendaji wa

kazi za walimu. Akitoa mfano alisema, kama si msaada wa CWT kuleta sheria ya

adhabu kwa wanafunzi mahakamani kama ushahidi labda Mwalimu Shada

angelionekana ametenda kosa, au kesi ingelichukua muda mrefu zaidi. Aidha Mwalimu

Mapila alikitaka Chama cha Walimu kuwasaidia walimu ambao ndio wanachama wake,

kwa namna yoyote ile kama kutoa pesa pale zinapohitajika au kuwatafutia wanasheria

pale wanapopata kesi kama hizo za kiutendaji kwani wao huchangia chama hicho.

“Mwalimu Shada alikuwa anatakiwa kuwalipia wanafunzi nauli kila

anapokwenda mahakamani, ilifikia hatua aliishiwa kabisa. Lakini ilikuwa ni

bahati kuwa mume wake ni mfanyabiashara hivyo alisaidia katika hilo. Sasa si

wote wenye uwezo kama huo. Hali kama hii inaonyesha wazi kuwa kama si

hivyo, Mwalimu Shada angelishindwa kujitokeza katika kesi hiyo na madhara

yake wote tunayafahamu.” Alisema Mwalimu Mapila.

Mahusiano na Wazazi

11

Kwa upande mwingine walimu walitoa chagamoto kwa serikali hususani Wizara ya

Elimu, kuhakikisha kuwa wanajenga misingi mizuri ya mawasiliano kati ya wizara na

shule.Walisema kuwa hawana muongozo ulio wazi na hivyo inawaweka mahali pabaya

kiutendaji kazi.Walisisitiza kutaarifiwa mabadiliko yoyote yanayotokea katika sekta ya

elimu, na kusambaziwa machapisho yote ya sekta hii ili kuwaweka katika nafasi nzuri

ya kuelewa taratibu zilizopo.Aidha walisema kwa kauli moja kuwa, wao wataendelea

kutimiza wajibu wao kama inavyopaswa na kufuata sheria na taratibu za nchi, na hata

kama mtoto Bella atavunja tena taratibu za shule ataadhibiwa tu kufuata sheria, kama

ni viboko atachapwa. Kinyume na hapo labda mzazi wake amuhamishe katika shule

nyingine ambayo anaona hatoweza kuadhibiwa iwapo atavunja sheria za shule.

Hivi sasa mtoto Bella hana amani wala furaha tena awapo shuleni. Kwani wanafunzi

wenzake wamekuwa wakimsumbua na kumuona kama mtu hatari na muongo

mkubwa.Wamekuwa wakimuambia kuwa baba yake alitaka kusababisha mwalimu wao

afungwe, na wamekuwa wakimuuliza, je wangelipata faida gani?

Ilibainika kuwa mzazi wa Bella hakuwa na sababu za msingi za kufungua kesi ile, bali

alikuwa anajaribu kuchochea uhasama baina ya walimu na wazazi. Pia alikuwa anatafuta

njia za kujikosha kwani alikuwa anakabiliwa na shutuma nyingi za kutowatendea haki

watoto wake. Ilibainishwa kuwa huyu mzazi amewahi kumkosesha mtoto wake

kuendelea na masomo ya sekondari kwa kutomlipia ada ndogo inayotakiwa katika

shule za serikali pamoja na kuwa na uwezo wa kulipia. Matokeo yake huyo mtoto hivi

sasa yupo tu nyumbani pasipo shughuli yoyote.

Aidha ilibainishwa kuwa mzazi huyu hana historia nzuri ya kuishi kwa amani na

wanakijiji wenziwe. Amekuwa ni mtu wa matatizo na mzushi wa mitafaruku mingi

katika jamii. Hali hii inaweza ikawa na athari kwa wazazi wengine wenye mitazamo

kama yake na hivyo kujenga mizizi ya uhasama kati ya wazazi na walimu katika

utekelezaji wa majukumu na taratibu zinazotakiwa.

Ushirikiano kati ya shule na wazazi ni wa muhimu sana katika kujenga misingi bora ya

maendeleo kwa watoto.Walimu kama walezi hukaa na watoto kwa muda mrefu zaidi

pengine kuzidi hata wazazi wenyewe. Iwapo wazazi watatilia mkazo yale maadili na

nidhamu wanayofundishwa mashuleni ni wazi kuwa watajenga jamii yenye nidhamu na

kuheshimika. Muungano mzuri wa wazazi na walimu umeweza kukuza maendeleo ya

shule kitaaluma miongoni mwa shule zilizo na ushirikiano wa karibu na wazazi.

Zile zenye wazazi wenye mtazamo tofauti zimekuwa zikilegalega nyuma kwa miaka

mingi.

12

Mahusiano na Wazazi

HakiElimu

Dhira

Dhira ya HakiElimu ni kuiona Tanzania ikiwa mahali ambapo

watoto wanafurahia haki ya kupata elimu bora ya msingi,

pale ambapo shule zinaheshimu utu na haki za binadamu wote,

na pale ambapo elimu inakuza usawa, ubunifu, udadisi na demokrasia

Dhamira

HakiElimu inafanya kazi kufikia usawa, ubora, haki za binadamu na demokrasia katika elimu kwa

kuwezesha jamii kubadili shule na mfumo wa uundaji wa sera za elimu,

kuchochea mijadala yenye ubunifu na kuleta mabadiliko,

kufanya utafiti yakinifu, kudadisi, uchambuzi na utetezi na

kushirikiana na wadau kuendeleza manufaa ya pamoja na haki za jamii

HakiElimu Tafiti

PO Box 79401 • Dar es Salaam • Tanzania

Tel. (255 22) 2151852 / 3 • Fax (255 22) 2152449

info@hakielimu.org • www.hakielimu.org

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!