TPCC Annual Report 2008.indd - HeidelbergCement
TPCC Annual Report 2008.indd - HeidelbergCement
TPCC Annual Report 2008.indd - HeidelbergCement
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Malipo kwa Wakurugenzi

Tanzania Portland Cement Company Ltd, Annual Report 2008

Malipo kwa huduma ya ukurugenzi katika Kampuni katika mwaka 2008 yalikuwa kama ifuatavyo:-

TZS

Mwenyekiti 1,000,000 kwa mwaka

Kila mkurugenzi 600,000 kwa mwaka

Pia, kila mkurugenzi alilipwa posho ya dola 1,200 kwa kila kikao cha Bodi au Kamati ya Ukaguzi alichohudhuria. Katika

mwaka husika, malipo ya namna hii kwa wakurugenzi yalikuwa TZS 46,883,304 (2007:TZS 25,919,680).

Tathmini ya Biashara

Mauzo mwaka 2008 yaliongezeka kwa aslimia 4 ikilinganishwa na mwaka 2007. Uzalishaji wa klinka ulishuka kwa asil-

imia 6, hali iliyosababishwa na haja ya kusimamisha mitambo mara kwa mara kupisha kazi za ujenzi wa kiwanda kipya.

Taarifa kamili ya mapato kwa mwaka husika inapatikana ukurasa wa 28 wa taarifa ya hesabu

Uwezo wa Kulipa

Wakurugenzi wamefanya tathmini ya kina juu ya hali ya kifedha ya Kampuni ikiwa ni pamoja na madeni ya muda mfupi

na muda mrefu. Kwa misingi ya tathmini hii ambayo imefanywa kwa kuzingatia mpango wa biashara uliopo, kanuni za

kimataifa za uhasibu na matakwa ya Sheria ya Makampuni Na.12 ya 2002, wakurugenzi wameridhika kwamba Kampuni

ina uwezo wa kuendesha shughuli zake bila matatizo yoyote.

Shughuli za Biashara na Makampuni yenye Uhusiano

Kampuni huagiza malighafi, vipuri na mahitaji mengine ya uzalishaji kwa bei ambazo hufikiwa kwa misingi ya kawaida ya

kibiashara, kutoka Scancem International ANS ambayo inamiliki asilimia 69.25 ya hisa zote za Kampuni. Maelezo ya kina

ya shughuli zinazofanywa na watu au makampuni yenye uhusiano yako aya ya 29 ya taarifa ya hesabu

Masuala ya Mazingira

Ukarabati mkubwa wa mitambo ya uzalishaji ambao umefanyika kati ya mwaka 2002 hadi 2006 umesaidia sana ku-

punguza kutimka kwa vumbi hapa kiwandani. Mfumo wa Udhibiti wa Mazingira umeandaliwa katika mwaka 2008 na

mchakato umeanza ili Kampuni ipate cheti cha Ubora cha ISO 14001 katika mwaka 2009.

Matukio Muhimu

Soko la saruji nchini Tanzania liliendelea kukua katika mwaka 2008. Kampuni iliweza kuzalisha na kuuza saruji nyingi

zaidi kuliko wakati wowote katika historia yake. Ili kukidhi mahitaji ya soko, TPCC iliendelea kuagiza klinka kutoka nje ya

nchi kuziba pengo katika uzalishaji wa bidhaa hiyo.

Mradi wa upanuzi wa kiwanda umeendelea kama ilivyopangwa na kwa gharama kama zilivyo kwenye bajeti. Ujenzi wa

mtambo mpya wa kusaga na kupakia saruji ulikamilika mwezi Agosti na kukabidhiwa rasmi mwezi Oktoba 2008 na hivyo

kuongeza uzalishaji wa saruji maradufu kutoka tani kama 700,000 kwenda tani 1,400,000 kwa mwaka. Mtambo wa

kuzalisha klinka unatarajiwa kukabidhiwa rasmi katika robo-mwaka ya pili ya 2009.

23