constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
24

Elisha Ochieng; (Ziwani resident) Anatuaribia maisha, mnikiwa na pesa yangu kidogo, anaenda kuita serikali, hati sijui nini na

nini.

Wengi wetu wazazi hawafanyi kazi, ningeomba kuwa shule, watoto wawachiliwe wasome bure, hata kama ni mpaka standard

8.

Matibabu pia iwe bure.

Julius Mwangi: Kwanza nataka kushukuru, commissioners kwa kazi nzuri wamefanya na uvumilivu wao.

Sheria zaa ardhi zilizopo sasa zinafinya wanainchi wa kawaida sana, kwa sababu wengi hawana ardhi na watu wale wakubwa

walikuwa tangu wakati wa ukoloni wakinyakua ardhi iliyokuweko na mpaka wakati huu wamezidi kabisa. Tuna taka sheria

ambayo itatumiwa ile kila mwanainchi au familia ipate mahali itaita nyumbani.

Kwa vile kwa mfano, tajiri akija apate mahali mnafanyia kazi, nyinyi ni watu kumi mko pale, mnafanya kazi mnajisaidia na

inasaidi watoto wenu, serikali ina haki ya kuja na kuwafukuza kutoka mahali pale na iwaonyeshi mahali mtaende, sasa iyo

inalete ufukara zaidi. Watu wanazidi kudidimia.

Polisi; wakati polisi wanawashika watu, hasa wanaume wakiwashika wanawake, na kuwapeleka cell, wanawake huwa

wanaumia sana. Mara nyingine wakifika kule, hao wanaume wanawalizimish kufagia, na saa ingine wanaanywa kufagia usiku.

Na saa ingine hao wanawake wanaazimishwa kujipeana mwili zao ili wanunuwe uhuru wao. Kwa hivyo wanawake wawe

wakishikwa na askari wanawake, na wakati wako kwa cell wawe, wanajibika maswala yote kwa askari wanawake.

Interruption: Kuhusu hii maneno ya polisi, je mngetaka warudishwe shule ama, kwa vile wakenya wengi wanalalamika kuwa

polisi wanaumiza watu.

Julius Mwangi: Ninaonelea ya kwamba, kuwe na utaratibu au commission ingine. Kama committee, lakini iwe ni serikali,

sijui iwekwe majeshi ndio watakua juu, wapewe uwezo wa kutawala polisi. Ili wewe ukigandamizwa na polisi, unaweza

kuwastaki kwa hawa, sababu sasa ukudhulumiwa na polisi unaweza kuenda kustaki wapi Wamekuwa wabaya sana na

wamezidi kabisa. Hata unyangaywi ile inafanywa siku hizi, ni hao wanafanya. Na hata ukijua hauna mahali ya kuenda

kuwashtaki.

Mimi ni mhuzaji wa makaa na nimetembea mahali nyingi sana katika Kenya, na hii biashara ilikuwa imefungwa lakini kule

kufungwa nikusema inaendelea kwa njia mbaya, hata kama imefungwa. Ningeuliza serikali iwe ikiwaruhusu watu mahali

wanaishi, kama ni zile miti zimeanguka, zile zimeoza na mahali wanakubaliwa kusafisha mashamba wawe legalized kuwa

wakichoma izo miti, na iwe ni huru mahali wanapeleka wasiulizwe.