12.07.2015 Views

constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

47Kiptoo Rop: Asante sana mwenye kiti wa Tume ya Katiba. Jina langu naitwa Paul Kiptoo Rop. Kwanza kabisa, hii mamboya private schools, ningependa serikali ama Katiba, iondoe mambo ya private schools, kwa sababu kulingana na sasa vilemaisha ya Kenya iko, wananchi wengi hawana kazi na matajiri wetu wanapeleka watoto kwa private schools. Hawa wananchiwa kawaida watoto wao hawawezi kupata masomo ya hali ya juu. Sasa hizi private schools, ambazo ni za girls and boys,zitupiliwe mbali kabisa, halafu turudishiwe tu moja ya serikali pekeee yake.Kwa mambo ya hosipitali, tungependa tu kuwe na hospitali za serekali pekeee yake. Kwa sababu hizi private hospitals, kunamadawa nyingi sana zinaibiwa kwa serikali zinapelekwa kwa private hospitals.Halafu, kwa mambo ya powers za President, Rais asiwe above the law. Kwa sababu Rais wenye wamekuwa sasawakiongoza hawa wawili wamepita, wamekuwa wakitumia mamlaka yao vibaya.Kwa mambo ya waalimu na madaktari, madaktari waongezewe pesa, kwa sababu hawa ndio wanatibu wananchi. Mkiachiliamadaktari, hawawezi kushugulikia wananchi wa kawaida. Sina mengi ni hayo tu.Com. Charles Maranga: Thank you. Asante sana na weka sahihi. Next.Mary Njambi- (deaf): Kwa majina yangu naitwa Mary Jambi. Ningependelea Katiba mpya ikitengenezwa, kuwe serikaliikitukumbuka sana. Kwa sababu kama sisi viziwi, hatutambuliwi, katika serikali, tukiwa na kama MP akiwa akitushirikishakatika mambo yetu tutafurahia.Na kulingana na mambo ya shule, kama sisi viziwi shule zetu zimekuwa bei ghali sana, na wazazi wetu, wengine ni masikini,hawawezi tulipia shule. For example anasema yeye alifika Std. 8 na wazazi wake wakakosa pesa ya karo. Kwa hivyoangependelea serikali, elimu yao ikuwe ya bure. Atafurahia sana. Asante.Com. Charles Maranga: Asante sana. Kuna mwingine? Okey.Rose Muthoni - (deaf): Kwa majina yangu naitwa Rose Muthoni. Ameonelea na yeye Katiba mpya itakayo rekebishwa, iweikihusisha the deaf kwa kazi yoyote ya serikali, ili maisha yetu sisi kama viziwi ikuwe inalingana na hearing people.Kama viziwi wenye wako mashambani, nao wako na shida sana kwa sababu wazazi wao hawajaelewa shida zao, nahawajatambua kama kuna elimu ya viziwi. Ningependelea nayo serikali iangalie mambo yetu.Com. Charles Maranga: Thank you. Muambie asante. Next.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!