1lzXuhv
1lzXuhv
1lzXuhv
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Taarifa ya Mwenyekiti (Yaendelea)

Wakurugenzi Wakuu wasio tekeleza majukumu ya siku

hadi siku.

Misingi ya Halmashauri ya KCB inaweka msisitizo

kwenye majukumu nyeti ya kibiashara na hutoa fursa

kwa Halmashauri ya Wakurugenzi kujifahamisha vyema

na biashara ili kutekeleza majukumu yao kikamilifu. Tuna

imani kuwa biashara inasimamiwa kwa busara na kwa

kuzingatia masharti yote ya kisheria.

Mwaka wa 2013 kulifanyika mabadiliko katika

Halmashauri ya Wakurugenzi. Kulingana na Kanuni za

Huduma za Wakurugenzi, Bw. Joseph Isaac Adongo

alistaafu kutoka kwa Halmashauri. Bw. Tom Ipomai

ambaye mlimchagua katika Mkutano Mkuu wa Mwaka

uliopita alijiunga na Halmashauri ya Wakurugenzi.

Pamoja na hayo, Bi. Catherine Adongo Kola na

Prof. Peter Kiko Kimuyu walichaguliwa tena kwenye

Halmashauri. Aidha, Halmashauri pia ilimchagua

mwenyekiti mpya, Bw. Ngeny Biwott, ambaye alichukua

hatamu kutoka kwa Mhandisi Musa Ndeto. Bw. Collins

Otiwu aliteuliwa kwenye Halmashauri kufuatia kuajiriwa

kwake kuwa Msimamizi Mkuu wa Fedha. Halmashauri

pia ilimteua Bw. Joseph Kania kuwa Katibu mpya wa

Kampuni. Nawakaribisha Wakurugenzi wapya kwenye

Halmashauri na kuwashukuru wale wote wanaoondoka

kwa mchango wao.

Kama mnavyofahamu, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni,

Bw. Joshua Oigara, alichukua hatamu Januari, 2013.

Katikati ya 2013, Halmashauri ilichunguza upya ajira

za wasimamizi wakuu katika Kamati Simamizi (EXCO)

ambazo ziliidhinishwa pia na Benki Kuu ya Kenya. Kamati

Simamizi ya Kampuni (EXCO) sasa inawajumuisha

Mkurugenzi Mkuu, Msimamizi Mkuu wa Fedha, Afisa

Mkuu wa Biashara nchini Kenya, Mkurugenzi wa

Mikopo wa Kampuni, Mkurugenzi wa Wafanyakazi,

Mkurugenzi wa dhidi ya athari za kifedha, Mkururgenzi

Mkuu wa Teknolojia na Katibu wa Kampuni. Hili ni kundi

la watu wachache na lenye ujuzi mkubwa wa kufanya

kazi lililoundwa kuambatana na mikakati ya sera ya

Kampuni. Halmashauri ina imani kamili na kundi hilo

linapoanza kuielekeza KCB kutoka mkondo wa kuwa

benki bora hadi ule wa kuwa benki thabiti zaidi.

Safari endelevu

Mnamo 2013 Halmashauri ya Kampuni ya KCB

iliidhinisha Mfumo Endelevu kwa Benki.

Halmashauri imejitolea kutoa rasilimali

zifaazo kwa utekelezaji wa mipango

ambayo itahakikisha uzingativu wa Benki

kwa Kanuni Endelevu.

Kutoka kushoto; Mkurugenzi wa KCB wa Biashara Rejareja, Annastacia Kimtai, Mwenyekiti

wa Kampuni ya KCB, Bw. Ngeny Biwott, Mke wa Naibu Rais, Bi. Rachel Ruto na Dkt.

Solomon Joloimat, wakati Bi. Ruto alipotembelea ofisi ya Mwenyekiti.

Halmashauri inahusika moja kwa moja

katika utekelezaji sahihi wa Maendeleo

Endelevu ya Kijamii, Mazingira Endelevu,

Uchumi Endelevu na Uthabiti wa

Kifedha. Hii itahakikisha kuwa Kampuni

ya KCB itakuwa taasisi endelevu

miongo inayokuja. Pia tutafanya kazi na

washikadau kuendeleza ajenda yetu kwa

kutumia ushirika uliopo katika juhudi zetu

za kuafikia ulimwengu endelevu. Katika

kuafikia hili, Benki itaendelea kuwekeza

27 16

K C B 2 0 1 3 A n n u a l R e p o r t a n d F i n a n c i a l S t a t e m e n t s