1lzXuhv
1lzXuhv
1lzXuhv
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Taarifa ya Mkurungenzi Mkuu (Yaendelea)

KCB Global MasterCard zinawawezesha wateja wetu

kufanya manunuzi kwenye mfumo huu bila fedha

hata nje ya mipaka. Mfumo huu unawawezesha wale

wenye kadi za Nakumatt Global Prepaid Smart Card

kuzijaza fedha kwenye tawi lolote la KCB, wakala wa

KCB Mtaani, ATM za KCB, Huduma za benki za KCB

kwa simu ya mkononi (KCB Mobi) na hudumu za benki

za KCB kupitia mtandao. Pamoja na hayo, wamiliki

wa Nakumatt Global Prepaid SmartCard wanaweza

kutoa fedha na kufanya manunuzi kupitia mtandao

katika duka lolote la Nakumatt kote Afrika Mashariki

na mahali popote duniani ambapo huduma zinalipiwa

kupitia Master Card.

Tunaendelea vyema katika katika ahadi yetu ya

kuwa Mtoaji wa Huduma za Kifedha Anayependwa

zaidi Afrika mwenye uwezo wa kufika kote duniani.

Katika siku zijazo, ubunifu wa teknolojia umeendelea

kubadilika kunufaisha wateja wetu na kutuwezesha

kutumia kwa pamoja mifumo yetu mbali mbali ya

mawasiliano.

Juhudi za Wafanyakazi

Mafanikio yetu hayangewezekana bila ya kujitolea

na ujuzi wa wafanyakazi wetu, ambao ningependa

kuwashukuru. Tangu kuteuliwa kwangu nimeshuhudia

kujitolea kwa wafanyakazi wetu kwa wateja na kwa

Benki na hili linanipa imani kuu kuhusu ufanisi wa siku

zijazo na ufanisi wa biashara hii.

Pia tumepiga hatua katika lengo letu kuvutia wajuzi

bora zaidi duniani, kokote tunakoweza kuwapata.

Kipindi cha mwaka mmoja uliopita kilishuhudia

kuteuliwa kwa watu wa nyadhifa za juu katika benki

tunapoangalia tajiriba pana katika idara mbalimbali.

Pia tuliainisha sehemu za kampuni ili kuakisi malengo

ya muda mrefu ya mikakati ya kibiashara ya KCB,

ikiwemo kubuniwa kwa Mkuu wa Huduma za Benki

kwa Waislamu, Bancassurance, Maswala ya Kampuni

na Usawazishi na Huduma kwa Wateja.

Malengo ya Jumla

Ingawa Kenya haikuafikia kiwango chake cha ukuaji

cha asili mia 4.9 cha Mapato ya Jumla ya Bidhaa na

Huduma Nchini (GDP) Benki iko mbele kulinganishwa

na malengo ya kifedha yaliyowekwa miaka mitatu

iliyopita. Uthabiti wa misingi ya biashara ndogondogo,

umewapa wateja wetu uwezo wa kukuza mtaji na

kuchochea maendeleo katika sekta mbalimbali za

uchumi wetu. Tutaendelea kutumia ukuaji huu thabiti

kuhimili mkakati wetu wa biashara.

Katika kipindi cha miaka minne ijayo, sekta ya mafuta

na gesi, itakuwa msingi wa kuchangia wingi wa

biashara katika kanda. Uwezo wa sekta

hii ni mkubwa na KCB inajipanga kuingia

katika fursa zitakazopatikana kuipeleka

nchi yetu katika kiwango kingine cha juu

cha ukuaji. Katika siku zijazo, tunatarajia

kuona mabadiliko katika mwelekeo wa

jinsi soko linavyoendelea. Hii ina uwezo

wa kukuza GDP ya kanda na ingawa

huenda tukawa mbele ya wakati, ruwaza

yetu ni kuendelea na ushirika ili kuhimiza

ukuaji katika sekta hii changa.

(Kutoka kushoto) Mkurugenzi wa KCB wa Biashara Rejareja Annastacia Kimtai, Mkurugenzi Mkuu

wa KCB Joshua Oigara, Mkurugenzi wa Uwekaji Benki wa Mashirika, James Agin na Kaimu

Mkurugenzi wa Maswala ya Uhusiano Bora na Usawazishi wa Shirika, Judith Sidi Odhiambo,

wakati wa kuanzishwa kwa Klabu ya wanachama wa KCB Biashara tawi la Masai Mara.

Mwezi Novemba, 2013, Kampuni ya

KCB iliweka saini ya makubaliano na

Benki ya Kimataifa ya Ghana ya mkopo

wa Dola za Marekani milioni 30 au KShs.

bilioni 2.58 kwa viwango vya sasa vya

kubadilisha fedha, ambao utalipwa

katika kipindi cha miaka mitatu. Mkopo

huu utaiwezesha Benki kuboresha

27 28

K C B 2 0 1 3 A n n u a l R e p o r t a n d F i n a n c i a l S t a t e m e n t s