1lzXuhv
1lzXuhv
1lzXuhv
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
Taarifa ya Mkurungenzi Mkuu

katika kushughulikia mahitaji ya wateja wetu, hali ya

maisha na maridhisho. Ili kuendelea katika hili, Benki

imewekeza kwa kiwango kikubwa katika mafunzo

ya wafanyakazi, muundo msingi wa Teknolojia ya

Habari na Mawasiliano, ili kuchapua ubunifu huu

ambao umebadilisha huduma za Benki kuwa za

dijitali. Mwaka ujao, wateja watakuwa na chaguo la

kufurahia orodha ya huduma zetu, tajiriba ya huduma,

ushauri na kupata huduma kwa kubonyeza kidude

mtu akiwa anastarehe nyumbani kwake au ofisini

pamoja na kupeleka huduma hizi katika biashara zetu

za Kimataifa.

Mafanikio yetu makubwa ni kuanzishwa kwa huduma

ya KCB M-Benki, huduma ya benki ya simu ya

mkononi ambayo inawawezesha wateja walioko na

wanaokuja kufungua na kuendesha akaunti za benki

kwenye simu zao. Huduma hii inatoa maridhisho

na muda kwa mteja, na imetuwezesha kupanua

huduma zetu za benki kujumuisha kupatikana kwa

huduma za mikopo, malipo ya bili na ununuzi wa

bidhaa madukani. Huduma hii ambayo ni ya kwanza

katika soko la Kenya, inawawezesha wateja kufungua

akaunti za benki bila ya kufika wenyewe kwenye

matawi na kuwawezesha kupata moja kwa moja

huduma zetu za benki.

Ufanisi wa KCB M-Benki umeiwezesha benki kuafikia

lengo lake la kujumuisha ushirika wa kifedha katika

huduma zake. Watu wasio na akaunti wanaweza

kutumia fursa ya huduma hii kujifungulia akaunti na

kuendesha akaunti hizo wapendavyo. Ufanisi wa

huduma hii ni dhahiri, huku idadi kubwa ya wateja

ikichagua KCB kama chaguo la kwanza la benki.

Pamoja na hayo, kuanzishwa kwa huduma ya Internet

Banking, KCB i-Bank, mwezi Novemba 2013,

kumeridhisha ongezeko la idadi kubwa ya wateja huku

idadi yao ikifika kima cha milioni 2.5, huu ukiwa ukuaji

mkubwa. KCB i-Bank huwapa wateja wetu huduma

ya papo hapo kote nje ya mipaka yetu na huduma

mahususi ya habari kwa wateja ili kubainisha akaunti

zao. Hii inawawezesha kupunguza gharama za karatasi

na taarifa za kifedha zinazotumwa kwa njia ya posta.

Pamoja na hayo, mteja anaweza kutekeleza shughuli

za benki, kulipa bili kupitia mtandao na kupata taarifa

kupitia mtandao. Internet Banking inawawezesha

wateja kupata huduma za fedha za kigeni kukiwa na

matumizi kidogo ya karatasi na utendaji wa hali ya juu.

Uwekezaji katika Teknolojia

Mnamo mwaka wa 2007, KCB ilianza safari yake ya

dijitali kwa kutekeleza mfumo wa mawasiliano wa

huduma zake. Malengo makuu ya utekelezaji huu

yalikuwa kuipa Kampuni ya KCB jukwaa maridhawa

ambalo lingetoa huduma bora zaidi kwa wateja wake na

kuimarisha uwezo wa kutoa huduma zinazoendeshwa

kiteknolojia. Ufanisi uliopatikana

katika kutekeleza mfumo huo mpya

umetuwezesha kuanzisha Kituo Kikuu

cha Mawasiliano cha KCB, Wakala wa

Benki wa KCB, ATM ng’amuzi za KCB,

Huduma za KCB Kupitia Tawi lolote,

Huduma za KCB za simu za mkononi,

KCB Internet Banking, Huduma za

Benki za KCB kwa walio nchi za nje,

na huduma nyingine zinazoendeshwa

kiteknolojia na washirika mbali mbali

katika sekta ya mawasiliano.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya KCB Sudani Kusini, Charity Muya-Ngaruiya, akitia saini kitabu

cha Wawekezaji wakati wa warsha ya Uwekezaji iliyofanywa Juba. Akiangalia ni Mkurugenzi

Mkuu wa KCB Joshua Oigara.

Kampuni ya KCB inapania kuwa

kiongozi katika utumizi wa teknolojia

kuendesha ajenda yetu ya kifedha.

Wakati wa mwaka, tuliboresha tovuti

yetu ili iwe na mvuto na yenye kutoa

huduma mbalimbali. Tovuti hiyo ya

27 26

K C B 2 0 1 3 A n n u a l R e p o r t a n d F i n a n c i a l S t a t e m e n t s