CONTENTS - Investing In Africa
CONTENTS - Investing In Africa
CONTENTS - Investing In Africa
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
TAARIFA YA MWENYEKITI kuendelea

KCB JUBA

Outside view of KCB Juba branch.

Viwango vya riba baina ya mabenki katika kipindi hicho

hicho viliongezeka kutoka asili mia 6.3 mwishoni mwa 2006

hadi asili mia 7.0 mwezi Desemba 2007. Viwango vya riba

vilivyodumishwa viliendelea kuwa muhimu katika mipango

ya uwekezaji.

MASOKO YA KIFEDHA

Shilingi ya Kenya ilikuwa na imariko kuu dhidi ya sarafu

muhimu za kimataifa na kuwa na viwango vya chini zaidi vya

ubadilishanaji ikilinganishwa na miaka iliyotangulia. Shilingi

iliimarika dhidi ya Dola ya Marekani, Pauni ya Uingereza na

Euro mwezi Desemba mwaka wa 2007 hadi Shilingi 62.50,

Shilingi 124.80 na Shilingi 89.90 kulinganishwa na Shilingi

69.40, Shilingi 136.30 na Shilingi 91.40 mwezi Desemba

mwaka wa 2006 mtawalio. Kuimarika kwa Shilingi kuliakisi

kuingia kwa fedha za kigeni katika kipindi cha mwaka

huo. Ufanisi huu umedhoofishwa na ghasia za baada ya

uchaguzi na kupelekea kudidimia kwa thamani ya Shilingi.

Biashara katika Soko la Hisa ilionyesha viwango vya chini

kutokana na hali ya sintofahamu miongoni mwa wawekezaji

wakati wa mwaka wa uchaguzi. Kigezo cha kampuni

bora 20 katika soko la Hisa la Nairobi kilipungua kwa asili

mia 4 kutoka alama 5,645.7 mwezi Desemba, 2006 hadi

alama 5,444.8 mwezi Desemba 2007. Hata hivyo mtaji

wa jumla wa soko hilo uliongezeka kutoka Shilingi bilioni

792 mwishoni mwa 2006 hadi Shilingi bilioni 851. Thamani

ya jumla ya hisa zilizouzwa katika soko la Hisa la Nairobi

ilipungua kwa asili mia 7 kutoka Shilingi bilioni 95 mwishoni

mwa mwaka wa 2006 hadi Shilingi bilioni 89 mwaka wa

2007, lakini jumla ya hisa zilizouzwa ziliongezeka kwa kiasi

kikubwa ikilinganishwa na miaka iliyotangulia.

Hisa za KCB ambazo kufuatia gawanyiko zilikuwa zikiuzwa

kwa shilingi 24 ziliimarika na kufikia shilingi 28.50. Mtaji wa

jumla uliongezeka hadi shilingi bilioni 56.9 mwaka wa 2007

kutoka shilingi bilioni 48.1 mwaka wa 2006. Ongezeko hili

lilikuwa linaakisi shinikizo la kuimarika kwa bei ya hisa na

kiasi kikubwa cha hisa zilizotolewa. Kutoka na gawanyo

hilo, hisa zilizotolewa ziliongezeka kutoka hisa milioni 199.6

hadi hisa milioni 1,996.

Kuambatana na imariko la uchumi, sekta ya benki iliendelea

kuonyesha ukuaji bora mwaka wa 2007. Wakati wa kipindi

hicho, mali za sekta hiyo ziliongezeka kutoka kiwango

kikubwa cha shilingi bilioni 760 mwaka wa 2006 hadi

shilingi bilioni 910 mwaka wa 2007. Hii hasa ilitokana na

ongezeko la fedha kwenye akaunti, mtaji wa ziada pamoja

na hifadhi ya faida iliyotoa nafasi zaidi ya uwekezaji katika

hati za dhamana za serikali na ukopeshaji.

Aidha kulikuwa na imariko la jumla la mikopo iliyolipwa

huku visa vya kutolipwa kwa mikopo vikipungua, ongezeko

la thamani ya mali na toshelezo la uwiano wa mtaji pamoja

na kuimarika kwa faida katika sekta kwa jumla.

UPANUZI WA MAENEO NA MASHIRIKA

Ili tuwe benki ya kanda, Halmashauri iliidhinisha kuanzishwa

kwa tawi la benki nchini Uganda na ikaanza shughuli zake

mwishoni mwa mwezi Novemba mjini Kampala. Soko

limepokea vyema biashara hiyo mpya na Halmashauri

imekubaliana na mipango ya Usimamizi ya kuongeza

matawi zaidi nchini humo.

Matawi mengine ya kanda yanaonyesha dalili njema na

kuna mipango ya kuongeza huduma zaidi Kusini mwa

Sudani ambapo tuna mipango ya kufungua matawi manne

zaidi mwaka wa 2008 na Tanzania ambapo kuna mipango

ya kuongeza matawi 20 zaidi katika muda wa miaka miwili

ijayo. KCB-U inatarajia kuwa na matawi sita mwaka wa

2008.

Kwa ujumla, matawi hayo ya benki kwa pamoja yalikuwa

na faida ya shilingi milioni 363 kabla ya kodi licha ya

faida kiasi kutoka KCB-T(Shilingi milioni 0.2) na hasara ya

shilingi milioni 49.2 kutoka KCB-U kutokana na gharama za

kuianzisha. Shirika la S&L liliendelea kuimarika huku faida

yake ikiongezeka maradufu wakati wa kipindi hicho kutoka

shilingi milioni 130 mwaka wa 2006 hadi shilingi milioni

277 mwaka wa 2007. Shirika hili ambalo linaongoza kwa

utoaji wa mikopo ya ujenzi wa nyumba nchini lina mpango

wa kupanua huduma zake katika mataifa ya kanda ndani

ya mwaka wa 2008 na tunaamini kwa kuwa lina ushindani

16 KCB ANNUAL REPORT & FINANCIAL STATEMENTS 2007