CONTENTS - Investing In Africa
CONTENTS - Investing In Africa
CONTENTS - Investing In Africa
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
TAARIFA YA MKURUGENZI MKUU

Faida kabla ya kodi iliongezeka

kutoka Shilingi bilioni 3.2 mwaka

wa 2006 hadi Shilingi bilioni 4.2

hali ambayo iliakisi utendaji bora

katika sekta zote za biashara.

Martin Oduor-Otieno,

Mkurugenzi Mkuu

Mwaka wa 2007 ulikuwa na ufanisisi ambapo maendeleo

ya kasi ya biashara yalipelekea ongezeko la faida la asili mia

33. Faida kabla ya kodi iliongezeka kutoka Shilingi bilioni

3.2 mwaka wa 2006 hadi Shilingi bilioni 4.2 hali ambayo

iliakisi utendaji bora katika sekta zote za biashara.

Kufuatia utendaji bora huu, Halmashauri imependekeza

mgao wa faida wa Shilingi 0.70(senti 70) kwa kila hisa hili

likiwa ni ongezeko la asili mia 17 kulinganishwa na mwaka

wa 2006.

Utendaji huu ulisukumwa na mazingira bora ya kiuchumi

ambayo yaliweka msingi bora wa riba na viwango vya

ubadilishanaji fedha za kigeni.

Jumla ya mapato ya shughuli zetu yaliongezeka kwa asili

mia 22 kutoka Shilingi bilioni 12.1 mwaka wa 2006 hadi

Shilingi bilioni 14.8 kutokana na ukuaji thabiti wa mapato

ya riba. Jumla ya mapato ya riba yaliongezeka kwa kima

cha kupendeza cha asili mia 34 kutoka Shilingi bilioni 6.3

hadi Shilingi bilioni 8.5. Mapato kutokana na ubadilishaji

wa fedha za kigeni na ada yalichangia Shilingi milioni 839

(nyongeza ya asili mia 27 mwaka wa 2006) na Shilingi bilioni

4.5( ongezeko la asili mia 20 mwaka wa 2006) kwenye kima

cha msingi cha Kundi.

na mikakati ya huduma kwa wateja. Kiasi kikubwa cha

fedha katika mkondo huu zimetumika katika kuimarisha

muundo msingi na shughuli inayoendelea ya kutekeleza

shughuli zetu kuu za mtandao wa benki.

Tunatarajia kuendelea kutumia fedha katika upanuzi wa

matawi na mashini za ATM kote katika kanda katika jitihada

za kufanya huduma zetu kupatikana zaidi katika soko.

Kulikuwa na ongezeko kubwa la faida katika mashirika

ambayo kwa pamoja yalichangia faida ya jumla ya Shilingi

milioni 268 kwa Kundi. Huku KCB-T na KCB-S zikipata

kasi ya biashara tunatarija mchango mkubwa zaidi kutoka

kwao katika siku za zinazokuja.

Mali ya Kundi ilikuwa kwa asili mia 30 na kuongezeka

kutoka Shilingi bilioni 92.5 hadi Shilingi bilioni 120.5, na

kuiweka KCB miongoni mwa Benki chache katika kanda

zenye mali ya kiasi hicho. Hii ilitokana na ongezeko kubwa

la mali zetu na madeni.

Jumla ya mikopo iliyotolewa iliongezeka kwa asili mia 42

kutoka Shilingi bilioni 45.3 mwaka wa 2006 hadi Shilingi

bilioni 64.3 mwaka wa 2007 kutokana na ongezeko la juhudi

za masoko na utekelezaji wa mfumo bora wa kutayarisha

mikopo.

Tulishuhudia ongezeko la asili mia 20 la gharama za utendaji

kutoka Shilingi bilioni 7.8 mwaka wa 2006 hadi Shilingi

bilioni 9.4 mwaka wa 2007 kwa sababu ya ongezeko la

shughuli za kibiashara, ikiwa ni pamoja na mauzo, mafunzo

Fedha zilizowekwa na wateja ziliongezeka kwa Shilingi

bilioni 17.2 wakati wa kipindi cha mwaka kutoka Shilingi

bilioni 77.2 hadi Shilingi bilioni 94.4 huku kiasi kikubwa

kikiwa ni kutoka kwa akaunti za hundi(Shilingi bilioni 8.9),

22 KCB ANNUAL REPORT & FINANCIAL STATEMENTS 2007