CONTENTS - Investing In Africa
CONTENTS - Investing In Africa
CONTENTS - Investing In Africa
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
RIPOTI YA WAKAGUZI - WAHASIBU

Taarifa zilizoambatanishwa za Benki ya

Kenya Commercial na mashirika yake kama

zilivyoonyeshwa kwenye ukurasa wa 35 hadi 76,

ambazo zinahusisha hesabu ya Kundi na Benki kufikia

tarehe 31 Disemba 2007 na taarifa ya mapato ya Kundi

na Benki, taarifa ya mabadiliko katika hisa za Kundi na

Benki, taarifa ya matumizi ya fedha ya Kundi kwa mwaka

uliomalizika katika kipindi hicho na muktasari wa sera

muhimu za uhasibu na maelezo mengine.

WAJIBU WA WAKURUGENZI KWA TAARIFA ZA

UHASIBU

Wakurugenzi wanawajibikia utayarishaji na uwasilishaji

wa taarifa za uhasibu wa haki kuambatana na kanuni na

viwango vya kimataifa vya uhasibu na mahitaji ya sheria

za kampuni za Kenya. Wajibu huu ni pamoja na upangaji,

utekelezaji na kudumisha udhibiti ambao ni muhimu kwa

utayarishaji na uwasilishaji wa haki wa taarifa za uhasibu

ambazo ziko huru kutokana na upungufu, ama kwa sababu

ya ulaghai au makosa,kuchagua na kutumia sera zinazofaa

za uhasibu na kufanya makadirio ya uhasibu ambayo

yanakubalika kwa wakati huo.

za wahasibu ambazo zinafaa kwa hali hiyo, lakini sio kwa

minajili ya kuwasilisha maoni kuhusu uwezo wa Kundi wa

kudhibiti shughuli zake.

Uhasibu pia unahusisha kutathimini sera sawa za uhasibu

zilizotumika na kukubalika kwa makadirio ya uhasibu

uliofanywa na Wakurugenzi, pamoja na kutathimini

uwasilishaji wa jumla wa taarifa za uhasibu.

Tunaamini kwamba ushahidi wa uhasibu tuliopata unatosha

na unafaa kutoa msingi wa maoni yetu ya uhasibu.

MAONI

Kwa maoni yetu taarifa za uhasibu zilizoambatanishwa

zinaeleza hali halisi ya kifedha katika Kundi hili na Benki

kufikia tarehe 31 mwezi Disemba 2007 na ile ya faida kwa

Kundi hili na matumizi na mapato ya fedha kwa kundi hili

kwa mwaka uliomalizika kuambatana na mahitaji ya sheria

za makampuni nchini Kenya na viwango vya kimataifa vya

kutoa ripoti za uhasibu.

Ripoti kuhusu mahitaji mengine ya kisheria

WAJIBU WA WAHASIBU

Wajibu wetu ni kuelezea maoni huru kuhusu taarifa hizi za

uhasibu kwa msingi wa hesabu zetu. Tulifanya uhasibu

wetu kuambatana na viwango vya kimataifa vya uhasibu.

Viwango hivyo vinatuhitaji kuafiki maadili na kupanga na

kutekeleza hesabu ili kupata hakikisho linalokubalika iwapo

taarifa za uhasibu zimeelezwa kikamilifu.

Uhasibu unahusisha utekelezaji wa kanuni ili kupata

ushahidi wa hesabu kuhusu kiwango cha fedha na

maelezo katika taarifa za uhasibu. Kanuni zilizochaguliwa

zinategemea uamuzi wa wahasibu, ikiwa ni pamoja na

ukadiriaji wa kasoro za taarifa za uhasibu zisizo kamilifu

ama kwa sababu ya udanganyifu au makosa. Katika

kufanya maamuzi hayo, mhasibu anatilia maanani udhibiti

wa kampuni ambao ni muhimu katika utayarishaji na

uwasilishaji wa haki wa taarifa za kifedha ili kubuni kanuni

Kama inavyohitajika na sheria za makampuni nchini Kenya,

tunaripoti kwenu, kuambatana na uhasibu wetu kwamba:

i) Tumepata taarifa zote na maelezo ambazo kadri

tunavyoelewa na kuamini zilikuwa muhimu kwa minajili

ya kufanya uhasibu wetu;

ii) Kwa maoni yetu, vitabu sahihi vya hasibu vimewekwa

na Kundi na Benki, kwa jinsi tulivyoona kutokana na

uchunguzi wa vitabu hivyo;

iii) Hesabu za Kundi na Benki zinawiana na vitabu vya

hesabu.

Nairobi

28 Februari 2008

34 KCB ANNUAL REPORT & FINANCIAL STATEMENTS 2007