CONTENTS - Investing In Africa
CONTENTS - Investing In Africa
CONTENTS - Investing In Africa
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
TAARIFA YA MWENYEKITI kuendelea

KCB FAMILY FUN DAY

KCB staff members take part in team

building activities during the KCB family

fun day.

wa kwanza na wa mwisho wa shilingi 0.70(senti 70) kwa

hisa ambayo ni asili mia 17 zaidi kuliko shilingi 6 kwa hisa

iliyotolewa mwaka jana kabla ya gawanyiko la hisa kumi

kwa moja.

Tunapoelekea mbele hata hivyo, huenda ikawa muhimu

kuchunguza sera yetu ya mgao wa faida katika kipindi kifupi

kutokana na upanuzi ambao unaendelea hapa nchini na pia

katika kanda kwa kuwa tutahitajika kuendelea kuongeza

mtaji wa kuhimili biashara kupitia baki ya mapato.

KUGAWANYWA HISA NA TOLEO LA HISA 2008

Kufuatia idhini kwa wanahisa ya kugawanya hisa zenu

mwaka wa 2007 kwa uwiano wa hisa kumi kwa kila moja

mtu aliyenayo, shughuli hiyo ilikamilishwa kwa ufanisi na

hisa hizo kuwekwa kwenye akaunti za wenye hisa mwezi

Juni mwaka jana.

Hii imechechemua shughuli katika sehemu ya mauzo ya

hisa za KCB katika Soko la Hisa la Nairobi ambapo hisa

za KCB zinauzwa zaidi miongoni mwa makampuni 20

yaliyoorodheshwa.

Kutokana na ufanisi wa kupanua biashara katika kanda,

mtaji wetu wa kimsingi umeanza kupata shinikizo huku

mahitaji ya biashara yanapoongezeka. Ili kuhimili ukuaji

huu na kuimarisha thamani kwa mwenyehisa, tunahitaji

kuongeza fedha katika mtaji wetu. Halmashauri imepitisha

pendekezo la Usimamizi la kutafuta fedha kupitia mauzo

ya hisa na tutatuma maombi rasmi kutoka kwa mashirika

ya kusimamia hisa iwapo idhini itatolewa katika mkutano

mkuu wa mwaka tarehe 9 Mei, 2008.

Kwa sasa, Usimamizi umeanzisha utaratibu unaohitajika

kutayarisha shughuli ya kuimarisha mtaji.

HALI YA BAADAYE

Licha ya sintofahamu ya kiuchumi iliyosabishwa na ghasia

za baada ya uchaguzi hali ya baadaye ya benki inaonekana

ya kuvutia. Shughuli inayoendelea ya kupanua mtandao

nchini Kenya, uchunguzi wa mara kwa mara wa mipango

na huduma na tabia iliyojikita ya mauzo katika biashara

inamanisha tunaweza kufuata kwa ufanisi malengo yetu

katika soko lenye ushindani la kanda kwa manufaa ya

wanahisa wetu. Taifa lina matumaini makubwa kwamba

kufuatia mpangilio mpya wa serikali ya mseto, shughuli za

kiuchumi zitaanza tena kote nchini.

Tumeweka mkakati wa miaka mitano kusukuma biashara

mbele katika nyanja muhimu kama vile malengo ya kifedha,

upanuzi wa biashara, ubunifu wa mipango, kuendeleza

rasilimali ya binadamu na maendeleo ya teknolojia.

Tunachunguza na kurekebisha mpango huu kila mwaka

kuhakikisha kwamba unaakisi hali halisi ya biashara na

hali ya kiuchumi kwa wakati uliopo na tuna imani kwamba

tutaafikia malengo yetu ya kibiashara kupitia mpango huu.

Nataka kushukuru Halmashauri kwa kunipa usaidizi thabiti

wakati wa kipindi cha mwaka tulipokuwa tunaendelea kutoa

mwelekeo kwa biashara. Bila kujitolea kwao hatungeshinda

changamoto za mwaka wa 2007.

Aidha ninashukuru Usimamizi na Wafanyakazi kwa bidii

yao kubwa katika kuafikia matokeo haya ya kupendeza.

Ufanisi wa Benki hauwezekani pasina kuungwa mkono na

wateja na wanahisa wetu.

Kwa niaba ya Halmashauri ya Wakurugenzi, ningependa

kuwatolea shukurani kwa kuendelea kuunga mkono na kuwa

na imani na Benki yenu. Kwa wanahisa wetu, ningependa

kusema kwamba ufanisi wa biashara hii umetokana na

kutuunga mkono bila kuyumba na nawahakikishia kwamba

daima tutajitahidi kuifanya KCB kuwa benki bora zaidi

katika kanda.

Asanteni

18 KCB ANNUAL REPORT & FINANCIAL STATEMENTS 2007