01.01.2015 Views

CONTENTS - Investing In Africa

CONTENTS - Investing In Africa

CONTENTS - Investing In Africa

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

TAARIFA YA MKURUGENZI MKUU kuendelea

DONATION

Maria Immaculate Children’s Centre

celebrate upon recieving their donation

from KCB.

kutumia mfumo huo mpya kufika robo ya tatu ya mwaka

wa 2008.

Nembo yetu inaendelea kuwa thabiti katika soko ambapo

uchunguzi wa hivi majuzi uliofanywa na kampuni ya

Steadman iliorodhesha KCB ya nne miongoni mwa nembo

maarufu zaidi kwenye soko kwa alama 75 (Safaricom-85,

Kenya Airways-78, Coca Cola-77). Tutaendelea kuimarisha

utambuzi wa nembo yetu kupitia kwa udhamini wetu mkuu

kama vile KCB Kenyan National Rally Championships,

KCB Safari Rally, KCB Pro-AM Golf Tour na KCB/Athletics

Kenya National Cross Country Championships, miongoni

mwa shughuli nyingine za kibiashara.

Pia tuliwekeza kwa kiasi kikubwa katika shughuli za

maendeleo ya kijamii za kuhifadhi mazingira, kupitia

mikakati yetu ya upanzi wa miti, maendeleo ya uwaminishi

na mikakati ya shughuli za maslahi ya jamii.

Wafanyakazi wetu walihusika katika upanzi wa miti kama

sehemu ya siku ya jamii ya KCB na katika kusaidia shule

zenye mahitaji wakati wa wiki ya jamii ya KCB.

Ili kuimarisha uwezo wa wafanyakazi wetu wa kutoa

huduma bora zaidi, tuliendelea kuwapa mafunzo ya hali

ya juu katika huduma kwa wateja na nyanja nyingine za

usaidizi wa kibiashara. Uchunguzi wa kuangalia kuridhika

kwa wateja uliotolewa hivi majuzi unaonyesha imariko la

jumla katika kuridhika kwa wafanyakazi katika nyanja zote

zilizoangaziwa na kuimarika kwa kiasi kikubwa kwa ubora

wa uongozi katika bashara.

Kulikuwa na mabadiliko kadhaa katika wasimamizi wakuu

wa biashara baada ya kuondoka kwa Mkurugenzi Mkuu

wa zamani, Terry Davidson na kuteuliwa kwangu kuchukua

mahali pake. Nimefurahishwa na usaidizi ninaopokea

kutoka kwa Halmashauri na Wasimamizi wakuu na nina

imani kwamba nina kundi thabiti la kuelekeza Benki hii

katika ufanisi wa baadaye. Katika kufanya marekebisho,

Halmashauri ilibuni nyadhifa za naibu wa mkurugenzi mkuu,

Biashara za kundi na Uthibiti wa biashara na kumteua

Peter Munyiri na Samuel Kimani kusimamia vitengo hivyo.

Wakurugenzi wawili wa idara(Philip Ilako-Huduma za benki

kwa mashirika na Kalyan Mukherjee-Hazina) pia walitoka

kwenye kampuni baada ya kumalizika kwa vipindi vyao vya

kuhudumu na nafasi zao kutwaliwa na John Mark Wandolo

na Timothy Kabiru, mtawalio.

Ningependa kuwashukuru washirika wote kwa usaidizi

wao ambao umepelekea ufanisi huu mkubwa na hasa

wafanyakazi wa KCB kwa juhudi zao na kujitolea katika

ufanisi huu. Aidha nina wingi wa shukrani kwa wateja na

wenyehisa kwa imani yao kwetu.

Shukrani zangu za dhati ziwaendee Wakurugenzi wa

Halmashauri kwa kutupa majukumu ya kusimamia shirika hili

na kwa kuendelea kutuunga mkono na kutupa mwelekeo.

Tuna imani kwamba tunaweza kudumisha msukumo huu

katika siku zijazo na kwa pamoja kuifanya KCB kuwa benki

bora zaidi katika kanda na kwingineko.

Asanteni.

24 KCB ANNUAL REPORT & FINANCIAL STATEMENTS 2007

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!