Sustainability Performance: At a glance (31 March 2012) - Safaricom
Sustainability Performance: At a glance (31 March 2012) - Safaricom
Sustainability Performance: At a glance (31 March 2012) - Safaricom
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
Executive summary

Ni mwanzo wa safari ya kusisimua

Nafurahia mno fursa ya kuwasilisha kwenu taarifa hii ya kwanza ya

kudumisha usitawi inayoashiria mfululizo wa mafanikio. Ni tukio muhimu

na la kusisimua kwetu sisi kama Shirika la hapa Kenya, kwa vile ni

dhihirisho la kujitolea kwetu kuzidi kupania faida na kuwajibika kusimamia

vyema mchango wetu katika uchumi, jamii, mazingira na kwenye jumuiya

tunakoendeshea shughuli zetu na tunakoendelea kuungwa mkono.

Kwa vile hii ni taarifa yetu zinduzi, ndiposa ikawa na taswira ya safari

ya kusisimua ambayo sisi kama kampuni na pia kama watu binafsi

tumeianza. Kudumisha usitawi na kuripotiwa kwake kunajumuisha mengi

zaidi ya utaratibu, sera na desturi za kibiashara, ni falsafa na mpangilio wa

maadili yanayoongoza na kufafanua maamuzi kwote katika kampuni, na

inaonyesha hali mambo itakavyokuwa katika mstakabala wetu.

Ujumbe Wa

Mwenyekiti

Bw. Nicholas Nganga

Ubunifu bado unasalia

kuwa kichocheo

muhimu cha ukuaji na

tunaendelea kuangazia

utoaji wa bidhaa na

huduma zinazoongezea

thamani katika maisha

ya wakenya

Tunawasilisha kwenu taarifa hii tukiwa na

msimamo huo, taarifa yenye maelezo yaliyo wazi

na yanayojumlisha hali halisi ya mafanikio yetu na

malengo yetu katika siku zijazo. Hii ni moja tu kati

ya ripoti nyingi zitakazokujieni, na inawakilisha

kigezo kinachoonyesha mahala tulipo sasa na

mwanzo wa gumzo linaloendelea juu ya safari ya

kusisimua tunayodhamiria kuanza.

Mambo mapya yanayojiri na

Mashaka yake

Hali yetu ya siku zijazo inategemea zaidi

baadhi ya matukio yanayojiri humu nchini

na katika eneo hili. La muhimu kutajwa

hapa ni mwelekeo wa athari ya mabadiliko

ya uchumi wa ulimwengu, teknolojia yenye

kasi inayobadilika kila kunapokucha na huku

mipaka ikiendelea kunywea. Miongoni mwa

baadhi ya mashaka yanayotukabili kwa

sasa ni, kupanda mara kwa mara kwa bei ya

mafuta na kubadilikabadilika kwa kima cha

ubadilishanaji pesa za kigeni hali ambayo

inaathiri mno mazingira ya biashara yetu, lakini

tumeendelea kuwasilisha matokeo mazuri na

faida tunayopata tumeitumia kuwekeza zaidi

katika muundo msingi wetu, kukiwa na zaidi ya

KShs Bilioni 25 za faida itokanayo na mauzo ya

rasilimali zikiwekezwa katika kipindi cha mwaka

wa kifedha wa 2012/13

Ni jambo lililo wazi kuwa utekelezaji wa

sheria pia unaathiri udumishaji wa usitawi

wetu na tuko mstari wa mbele kuanzisha

mashauriano na serikali pamoja na mamlaka

mbali mbali za kusimamia utekelezaji kanuni,

huku tukilinda na kusaidia biashara hii kwa

ujumla kupitia kuimarisha maelewano na

mipango yenye manufaa.

Ubunifu unaendelea kuwa

kichocheo muhimu

Ubunifu bado unasalia kuwa kichocheo

muhimu cha ukuaji na tunaendelea kuangazia

utoaji wa bidhaa na huduma zinazoongezea

thamani katika maisha ya wakenya. Mfano

mzuri wa ubunifu wetu ni M-PESA, huduma

yetu ya uhawilishaji pesa kupitia simu ya

mkononi. Kukiwa na wateja zaidi ya milioni

15 na mawakala zaidi ya 39, 000, M-PESA

inaendelea kupata ukuaji imara na kuchangia

pakubwa kuboresha hali ya wakenya na jinsi

wanavyoendesha shughuli zao za kila siku.

Kutekeleza uwajibikaji wa

maswala ya jamii

Vile vile tunajivunia mchango ambao taasisi

ya Safaricom Foundation inaendelea

kutoa katika kuboresha maisha ya

wakenya. Safaricom Foundation, ambayo

ilisajiliwa mwaka wa 2003, ni taasisi huru

ya kuchangisha pesa za kusaidia wale

wasiojiweza katika jamii. Ni hazina ya

amana inayotusaidi kutekeleza ahadi yetu ya

kuwekeza katika uwajibikaji kwenye Jumuiya

na inaangazia masuala mbali mbali ya kijamii

kama vile afya, elimu, uwezo wa kiuchumi na

ulindaji wa mazingira. Mpango unaostahili sifa

hapa, ni ile kampeni ya Kenyans for Kenya

ambapo Safaricom Foundation na idara zote

za Safaricom kwa ujumla walihusika sana

katika kuhamisisha wakenya kuchangia pesa

za kusaidia wahanga wa baa la njaa.

Mtazamo wa siku zijazo

Mambo tunayoyapa umuhimu zaidi mwakani

yanategemea ari yetu wa kuboresha huduma,

bidhaa bora zinazotutofautisha na washindani

wetu, kuongeza thamani kwenye hudunma na

utoaji huduma za kipekee kwa wateja. Tutafikia

haya huku tukizingatia zaidi athari yetu kwenye

mazingira yetu, kwenye biashara hii na uchumi

wa Kenya kwa ujumla, haya yote yakienda

sambamba na ahadi yetu ya kuwa shirika

linalochukuana na matakwa ya raia.

16 Safaricom Sustainability Report 2012 Safaricom Sustainability Report 2012 17

Executive summary