Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices
Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices
Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
Ukatili Watokea 2

Hujui hata kidogo kwamba kuna hatima tofauti inayokungoja. Kwenye siku ya mwisho ya kumaliza shule ya

msingi, unarudi nyumbani ukiwazia juu ya kujiunga na shule ya sekondari. Kwa siku chache za mwanzo wa

likizo, unawasaidia wanawake wengine katika kazi za nyumbani na unazungumza na Fauzia. Siku moja usiku,

ukiwa unaanza kupata usingizi, unamsikia juujuu mama yako akiongea na shangazi zako. Unanyatia karibu na

kuwasikiliza kisiri huku wakipanga maandalizi ya harusi yako. Unaamka na kuwauliza juu ya nini kinachoendelea.

Mama yako anakwambia, “Kuna tajiri mmoja kijijini ambaye anataka kutoa mahari kwa ajili yako! Anataka

mke atakayemzalia mtoto wa kiume. Wake zake wengine wawili wamemzalia watoto wa kike tu. Betty tunajua

utailetea sifa familia hii.” Unakosa la kusema.

Asubuhi inayofuatia, kila mtu anajiandaa tayari kwa harusi yako. Wanawake wanapaka mwili wako kwa

mafuta na manukato za mitishamba kukuandaa kwa harusi yako jioni hiyo na nguo nzuri sana zimeshonwa

kwa ajili yako. Siku ya harusi yako ndipo unakutana na mumeo kwa mara ya kwanza. Ni mzee sana. Watu

wanaokuzunguka wanafurahi na kusherehekea. Wewe huelewi kihalisi aina ya maisha utakayoishi na mzee

huyu. Unajawa na hofu.

Usiku wa kwanza wa ngono baada ya harusi kuisha anatoboa utando wa ngozi ulioziba pamoja na kovu

lililotokana na kukeketwa. Maumivu unayopata wakati wa kushiriki tendo la kujamiana ni makali sana karibu

sawa na yale ya wakati ulipokeketwa. Lakini unajaribu kuvumilia na kutimiza wajibu wako kwa uadilifu, ukifanya

kazi za bustani kwa bidii, kutunza mji, na kujaribu kadri uwezavyo kujizuia kulia kwa maumivu unayopata wakati

wa kujamiana. Kuna siku nyingine unahisi kama uke wako unapasuliwa lakini unajua kwamba kama mke wa

mtu hupaswi kulalamika.

Ni pale tu maumivu yanapongezeka zaidi ambapo unaamua kutafuta msaada.

Ikiwa unataka kwenda kwenye kituo cha afya kilicho karibu na wewe, nenda kwenye Huduma za Matibabu

na uchukue kadi namba 1.

Ikiwa unaamua kuomba ushauri kutoka kwa wazee wa kijiji, nenda kwenye Viongozi wa Kijadi na uchukue

kadi namba 1.

Ikiwa unaamua kuongea na mama yako, nenda kwenye Familia na uchukue kadi namba 2.

Hadithi ya Betty B5