Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices
Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices
Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
Utambulisho

Jina langu naitwa Betty. Nina umri wa miaka 9 na ngozi yangu ni nyeusi na nyororo kama imepakwa

mafuta ya samli. Shingo yangu ndefu na mwanya kwenye meno yangu vinanifanya nionekane binti

mrembo kuliko wote darasani mwetu. Ninapenda kusoma, hasa somo la sayansi, ambalo napenda

kuliko yote. Rafiki yangu wa karibu, Fauzia hukaa karibu na mimi tukiwa darasani. Pia anaishi karibu

na nyumbani kwetu na kila siku tunaenda shuleni na kurudi tukiwa pamoja na wanafunzi wengine,

wavulana kwa wasichana. Wavulana wanapofika nyumbani wanaanza kucheza au kusoma vitabu

vyao. Wakati mwingine wanapaswa kusaidia kukata kuni. Wasichana wote wanatakiwa kwenda jikoni

kupika. Muda pekee tulio nao wa kusoma vitabu vyetu ni wakati tunapokuwa shuleni, lakini hali hii

haitufanyi mimi na Fauzia tuache kusoma. Tutakapokuwa wakubwa tutafanya kazi katika kiwanda

kimojawapo kikubwa huko mjini. Ni ndoto yetu kuwa siku moja tutaenda jijini.

Kijiji chetu ni kidogo sana na karibu watu wote wanafahamiana. Nyumba zimejengwa katika makundi

au miji, na kila nyumba ina jiko la kupikia kwa nje, pamoja na maliwato ya pamoja. Familia nyingi zina

bustani ya pamoja yenye vyakula vingi sana. Ninaishi na wazazi wangu, kaka zangu wakubwa wawili

na dada yetu mdogo mmoja. Shangazi zangu, wajomba na binamu zangu wanaishi kwenye kundi

la nyumba au mji unaofuatia. Mama yangu, shangazi yangu, na karibu wanawake wote wa kijijini

kwetu wanakaa nyumbani wakifanya kazi za bustani na kulea watoto wadogo. Binamu zangu huwa

wananiambia nifute ndoto za kufanya kazi kiwandani kwa sababu wasichana wa kijijini husubiriwa

wakue ili waolewe na kuwa kina mama wa nyumbani. Huwa nawacheka na kuwaambia maisha yangu

kamwe hayatakuwa hivyo. Sijali wanachokisema binamu zangu lakini…

Nenda kwenye Ukatili Watokea na uchukue kadi namba 1.

Hadithi ya Betty B1