30.01.2013 Views

Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices

Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices

Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Marafiki na Majirani 1

Unachowaza ni kumtafuta Fauzia, lakini kila ukijaribu kuinuka ili ukamtafute, maumivu kwenye uke

wako yanakuwa makali sana. Hivyo, unalala tena chini kwenye giza peke yako huku ukijiuliza ni kwa

nini mama yako alikuleta huku. Unaogopa sana kwa sababu maumivu hayaishi na huwezi kufanya

lolote zaidi ya kuendelea kulia tu. Hatimaye baada ya siku tatu ndefu, unaanza kutembea pole pole

uani ukimtafuta Fauzia. Maumivu yanasambaa miguuni kama moto. Baadaye unamuona amekaa

chini ya mti akinywa chai. Anatabasamu kwa udhaifu anapokuona. Mnakaa pamoja lakini hakuna

anayeongea sana kati yenu huku wale vikongwe wakiendelea kuwaangalia kwa ukali. Unataka

kumsimulia kuhusu maumivu makali ya kisu ambayo amekua nayo mwilini tangu siku hiyo. Unataka

kujua ikiwa yeye pia alitaka kupiga mayowe na wakamziba mdomo.

Baada ya dakika chache Fauzia anasema anataka kujilaza chini. Unatambua kwamba hata yeye

anapitia maumivu makali sana. Unamshika mkono wakati analala na mnamuomba Mungu kwamba

wote mpone kwa haraka. Kwa siku kadhaa zinazofuatia, wewe, Fauzia na wasichana wengine walioko

pale mnajifunza mengi zaidi kuhusu namna ya kuwa mwanamke. Wanawake wale wakongwe

wanawapaka dawa za miti shamba kwenye vidonda vyenu kila siku jioni, lakini cha kwako hakionekani

kupona. Fauzia anaendelea kukujulia hali, na hatimaye mnaweza kutembea bila kuhisi maumivu

makali. Balaa linaonekana kufikia mwisho pale mnapoambiwa ni wakati wa kurudi shuleni.

Huku ukifurahia kurudi tena shuleni na kuendeleza ndoto yako aa kufanya kazi kwenye kiwanda kule

jijini, maumivu kwenye kidonda yanaendelea kukutisha kama hayataishia.

Miaka inapita.

Sasa unakaribia kushuhudia ndoto zako zikitimia. Unatimiza miaka kumi na mitatu, kwa maana hiyo

mwaka unaofuatia utaanza kusoma shule ya sekondari. Lakini kabla ya hapo…

Nenda kwenye Ukatili Watokea na uchukue kadi namba 2.

Hadithi ya Betty B3

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!