Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices
Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices
Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Familia 2

Mama yako anakusikiliza na kukuhurumia. Hata hivyo, anakwambia kwamba ni jambo la kawaida

kuhisi maumivu wakati wa kujamiana, na kwamba maadamu utazaa mtoto wa kiume, tunza mji

wako, usije ukaleta aibu kwa mume wako, kila kitu kitakuwa sawa. Anakukumbusha kwamba

mumeo alilipa mahari nzito na anakuuliza iwapo umemfanyia jambo lolote lililomuudhi mume

wako. Unapomwambia kwamba ulikuwa mtiifu kwa kila kitu, ndipo anakwambia ukae kwake kwa

siku kadhaa mpaka utakapopata nafuu. Anakuonya kwamba ni lazima urudi kwa mume wako baada

ya majeraha kupona.

Unaangalia vitabu vyako vya shule ya msingi, unafunuafunua kwa shauku lakini ghafla unavitupia

nje kwa hasira kwa sababu unajua hutavitumia tena. Unaviwashia kiberiti na kuvitazama vikiteketea

kwa moto kama yalivyo maisha yako. Unawaza kuhusu Fauzia ambaye pia amekwishaolewa na

hujui anaendeleaje, na pia kama mume wake anaishi naye kwa raha, au kama ndoa yako ndiyo hali

kielelezo ya wanawake wote walioolewa.

Mama yako anahisi moshi na anataka nje kukuchungulia. Anapoona vitabu vinateketea hadi kuwa

majivu, anakaa chini pembeni na wewe. “Ni bora kuziacha ndoto hizo ziteketee, Betty. Unatakiwa

kuzingatia kupata watoto. Isitoshe, kwa nini kesho usiende hospitali kupimwa kama una ujauzito?”

Ikiwa unaamua kwenda kuongea na wazee wa kijijji, nenda kwenye Viongozi wa Kijadi na uchukue

kadi namba 1.

Ikiwa unaamua kwenda moja kwa moja kwenye kliniki, nenda kwenye Huduma za Matibabu na

uchukue kadi namba 1.

Hadithi ya Betty B7