30.01.2013 Views

Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices

Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices

Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Hadithi ya Betty

Utambulisho

A1

Utambulisho

Jina langu naitwa Betty. Nina umri wa miaka 9 na ngozi yangu ni nyeusi na nyororo kama imepakwa

mafuta ya samli. Shingo yangu ndefu na mwanya kwenye meno yangu vinanifanya nionekane binti

mrembo kuliko wote darasani mwetu. Ninapenda kusoma, hasa somo la sayansi, ambalo napenda

kuliko yote. Rafiki yangu wa karibu, Fauzia hukaa karibu na mimi tukiwa darasani. Pia anaishi karibu

na nyumbani kwetu na kila siku tunaenda shuleni na kurudi tukiwa pamoja na wanafunzi wengine,

wavulana kwa wasichana. Wavulana wanapofika nyumbani wanaanza kucheza au kusoma vitabu

vyao. Wakati mwingine wanapaswa kusaidia kukata kuni. Wasichana wote wanatakiwa kwenda jikoni

kupika. Muda pekee tulio nao wa kusoma vitabu vyetu ni wakati tunapokuwa shuleni, lakini hali hii

haitufanyi mimi na Fauzia tuache kusoma. Tutakapokuwa wakubwa tutafanya kazi katika kiwanda

kimojawapo kikubwa huko mjini. Ni ndoto yetu kuwa siku moja tutaenda jijini.

Kijiji chetu ni kidogo sana na karibu watu wote wanafahamiana. Nyumba zimejengwa katika makundi

au miji, na kila nyumba ina jiko la kupikia kwa nje, pamoja na maliwato ya pamoja. Familia nyingi zina

bustani ya pamoja yenye vyakula vingi sana. Ninaishi na wazazi wangu, kaka zangu wakubwa wawili

na dada yetu mdogo mmoja. Shangazi zangu, wajomba na binamu zangu wanaishi kwenye kundi

la nyumba au mji unaofuatia. Mama yangu, shangazi yangu, na karibu wanawake wote wa kijijini

kwetu wanakaa nyumbani wakifanya kazi za bustani na kulea watoto wadogo. Binamu zangu huwa

wananiambia nifute ndoto za kufanya kazi kiwandani kwa sababu wasichana wa kijijini husubiriwa

wakue ili waolewe na kuwa kina mama wa nyumbani. Huwa nawacheka na kuwaambia maisha yangu

kamwe hayatakuwa hivyo. Sijali wanachokisema binamu zangu lakini…

Nenda kwenye Ukatili Watokea na uchukue kadi namba 1.

Hadithi ya Betty B1

Hadithi ya Betty

Ukatili Watokea 1

A2

Ukatili Watokea 1

Leo wewe na Fauzia mnakimbia mkirudi nyumbani kutoka shuleni huku mmejitwika vizuri kichwani vitabu

vyenu kuona ni nani atafika wa kwanza pasipo vitabu vyake kuanguka. Unapofika nyumbani mama yako

anakwambia kesho asubuhi mtaamka mapema na mtaenda sehemu fulani maalumu. Hupati picha halisi

juu ya jambo analozungumzia, lakini huna uhuru wa kumuuliza maswali mengi.

Umelala tongo macho kwa shauku uliyonayo, na leo badala ya kwenda shuleni, mama yako anakuongoza

kuelekea njia iendayo sokoni. Unawazia kwamba huenda anaenda kukununulia nguo mpya. Mnasimama

kwenye kibanda kilichopambwa vizuri. Unawaona wanawake vikongwe wawili wamesimama mlangoni.

Mmoja wao ni mganga anayetibu wanawake kule kijijini. Mwanamke huyo ni maarufu sana na watu

wanasema ndiye mwanamke tajiri sana kuliko wote kijijini. Mama yako anakukumbatia na kukutakia kila

la heri. Kichwa chako kinaanza kuwayawaya huku ukikaribishwa uani ambako kumetapakaa wanawake

wengi wagonjwa. Huko ndani unaona beseni lenye maji, na beseni jingine lina maji ya kijani, visu

viwili, na chini kuna pia sahani yenye pamba. Mwanamke mmoja anakwambia ulale chini. Mwanamke

mwingine anakaribia na kukushika miguu na mikono kwa kuikandamiza chini kwa nguvu. Kabla hujajua

kinachoendelea, tayari imeshavuliwa chupi yako na yule mganga ameanza kukata. Huwezi kuelezea

maumivu makali unayoyapata mwilini, utafikiri kaa la moto limewekwa sehemu zako za siri. Unatoa macho

na kuanza kupiga kelele kwa maumivu lakini mwanamke mmoja anakuziba mdomo, akikwambia maumivu

yatapoa muda si mrefu. Hatimaye maumivu yanapungua taratibu na wale wanawake wanakuweka pamba

yenye unyevunyevu kwenye sehemu za maumivu. Maumivu yanaonekana kusambaa mwili mzima. Mtu

fulani anakunyanyua kutoka chini kwenye uchafu na kukuingiza ndani kwenye mkeka ambapo unalala

kwa maumizi tele.

Masaa yanapozidi kwendelea unawaona wasichana wengine wakiingia na kutoka ndani ya nyumba hiyo.

Moyo wako unashtuka unapomuona Fauzia akiingia, lakini huna nguvu za kumuita akipita na kuingia

kwenye chumba kingine chenye giza. Unapitiwa na usingizi na kulala mpaka wakati wanapokuja kukusafisha

kidonda chako. Pia wanawaletea chakula kizuri mpate kula, lakini hata hivyo maumivu hayatoweki.

Ikiwa unataka kumtafuta Fauzia, nenda kwenye Marafiki na Majirani na uchukue kadi namba 1.

Ikiwa unaamua kwenda nyumbani kumuona mama yako, nenda kwenye Familia na uchukue kadi

namba 1.

Hadithi ya Betty B2

Hadithi ya Betty

Marafiki na Majirani 1

A3

Marafiki na Majirani 1

Unachowaza ni kumtafuta Fauzia, lakini kila ukijaribu kuinuka ili ukamtafute, maumivu kwenye uke

wako yanakuwa makali sana. Hivyo, unalala tena chini kwenye giza peke yako huku ukijiuliza ni kwa

nini mama yako alikuleta huku. Unaogopa sana kwa sababu maumivu hayaishi na huwezi kufanya

lolote zaidi ya kuendelea kulia tu. Hatimaye baada ya siku tatu ndefu, unaanza kutembea pole pole

uani ukimtafuta Fauzia. Maumivu yanasambaa miguuni kama moto. Baadaye unamuona amekaa

chini ya mti akinywa chai. Anatabasamu kwa udhaifu anapokuona. Mnakaa pamoja lakini hakuna

anayeongea sana kati yenu huku wale vikongwe wakiendelea kuwaangalia kwa ukali. Unataka

kumsimulia kuhusu maumivu makali ya kisu ambayo amekua nayo mwilini tangu siku hiyo. Unataka

kujua ikiwa yeye pia alitaka kupiga mayowe na wakamziba mdomo.

Baada ya dakika chache Fauzia anasema anataka kujilaza chini. Unatambua kwamba hata yeye

anapitia maumivu makali sana. Unamshika mkono wakati analala na mnamuomba Mungu kwamba

wote mpone kwa haraka. Kwa siku kadhaa zinazofuatia, wewe, Fauzia na wasichana wengine walioko

pale mnajifunza mengi zaidi kuhusu namna ya kuwa mwanamke. Wanawake wale wakongwe

wanawapaka dawa za miti shamba kwenye vidonda vyenu kila siku jioni, lakini cha kwako hakionekani

kupona. Fauzia anaendelea kukujulia hali, na hatimaye mnaweza kutembea bila kuhisi maumivu

makali. Balaa linaonekana kufikia mwisho pale mnapoambiwa ni wakati wa kurudi shuleni.

Huku ukifurahia kurudi tena shuleni na kuendeleza ndoto yako aa kufanya kazi kwenye kiwanda kule

jijini, maumivu kwenye kidonda yanaendelea kukutisha kama hayataishia.

Miaka inapita.

Sasa unakaribia kushuhudia ndoto zako zikitimia. Unatimiza miaka kumi na mitatu, kwa maana hiyo

mwaka unaofuatia utaanza kusoma shule ya sekondari. Lakini kabla ya hapo…

Nenda kwenye Ukatili Watokea na uchukue kadi namba 2.

Hadithi ya Betty B3

Hadithi ya Betty

Familia 1

A4

Familia 1

Zimepita siku chache tangu ukeketwe na kutembea kurudi nyumbani ni maumivu makali sana. Mama

yako anashangaa kukuona. Anakuuliza umekuja kufanya nini nyumbani na ni nani aliyekuruhusu

kurudi, kwani ulitarajiwa kubaki kwa wale wanawake vikongwe mpaka baada juma moja kupita.

Unaanza kulia huku unamshikilia. “Lazima urudi,” anakwambia. “Watapata wasiwasi, huwezi kurudi

nyumbani mpaka kazi ikamilike.” Unaelezea yaliyokufikia kwa kukeketwa na kisu, ukidhani mama

yako hakuwaruhusu wakukekete alipokwambia mlikuwa mnaenda mahali maalumu.

Unamwambia kuhusu maumivu makali unayopata, kwamba hata kutoa mkojo ni vigumu sana.

Anakusikiliza kwa makini na anakupaka dawa fulani za miti shamba kwenye kidonda. Unaumia

kidogo lakini anakuhakikishia kwamba dawa hiyo itakuponya. Daima anaendelea kukwambia juu ya

jinsi ananvyojivunia juu yako kwa hutoaibisha familia. Anasema kwamba sasa wewe ni mwanamke

halisi na kwamba wanaume wengi watatamani kukuoa kwa sababu ulitunza ujana wako. Huelewi

chochote lakini anaahidi kukupikia chakula kile ukipendacho utakaporudi nyumbani kwa sababu

wewe ni binti jasiri. Kisha anakusindikiza nje ya lango na kukuambia ni muhimu urudi kule haraka na

ukaungane na wasichana wenzako walioko huko. Anakuambia ujikaze na usijali sana maumivu kwa

kuwa wanawake wote lazima wateseke.

Unarudi kule kibandani bila kugunduliwa na mnafundishwa jinsi ya kuwa mke halisi pamoja na kuwa

mama. Polepole maumivu yanaanza kupungua, na wasichana wengi wanapopona, kunafanyika

sherehe kubwa ambapo watu wote kijijini wanakuja kusherehekea kupatikana kwa wanawake wapya.

Unaporudi shuleni, walimu wako wanakutambua kwa namna mpya na wewe anaanza kujivunia kwa

kukeketwa. Majuma yanageuka miezi, na kila muhula unapopita, unapata shauku zaidi ya kujiunga

na shule ya sekondari, lakini…

Nenda kwenye Ukatili Watokea na uchukue kadi namba 2.

Hadithi ya Betty B4

Hadithi ya Betty

Ukatili Watokea 2

A5

Ukatili Watokea 2

Hujui hata kidogo kwamba kuna hatima tofauti inayokungoja. Kwenye siku ya mwisho ya kumaliza shule ya

msingi, unarudi nyumbani ukiwazia juu ya kujiunga na shule ya sekondari. Kwa siku chache za mwanzo wa

likizo, unawasaidia wanawake wengine katika kazi za nyumbani na unazungumza na Fauzia. Siku moja usiku,

ukiwa unaanza kupata usingizi, unamsikia juujuu mama yako akiongea na shangazi zako. Unanyatia karibu na

kuwasikiliza kisiri huku wakipanga maandalizi ya harusi yako. Unaamka na kuwauliza juu ya nini kinachoendelea.

Mama yako anakwambia, “Kuna tajiri mmoja kijijini ambaye anataka kutoa mahari kwa ajili yako! Anataka

mke atakayemzalia mtoto wa kiume. Wake zake wengine wawili wamemzalia watoto wa kike tu. Betty tunajua

utailetea sifa familia hii.” Unakosa la kusema.

Asubuhi inayofuatia, kila mtu anajiandaa tayari kwa harusi yako. Wanawake wanapaka mwili wako kwa

mafuta na manukato za mitishamba kukuandaa kwa harusi yako jioni hiyo na nguo nzuri sana zimeshonwa

kwa ajili yako. Siku ya harusi yako ndipo unakutana na mumeo kwa mara ya kwanza. Ni mzee sana. Watu

wanaokuzunguka wanafurahi na kusherehekea. Wewe huelewi kihalisi aina ya maisha utakayoishi na mzee

huyu. Unajawa na hofu.

Usiku wa kwanza wa ngono baada ya harusi kuisha anatoboa utando wa ngozi ulioziba pamoja na kovu

lililotokana na kukeketwa. Maumivu unayopata wakati wa kushiriki tendo la kujamiana ni makali sana karibu

sawa na yale ya wakati ulipokeketwa. Lakini unajaribu kuvumilia na kutimiza wajibu wako kwa uadilifu, ukifanya

kazi za bustani kwa bidii, kutunza mji, na kujaribu kadri uwezavyo kujizuia kulia kwa maumivu unayopata wakati

wa kujamiana. Kuna siku nyingine unahisi kama uke wako unapasuliwa lakini unajua kwamba kama mke wa

mtu hupaswi kulalamika.

Ni pale tu maumivu yanapongezeka zaidi ambapo unaamua kutafuta msaada.

Ikiwa unataka kwenda kwenye kituo cha afya kilicho karibu na wewe, nenda kwenye Huduma za Matibabu

na uchukue kadi namba 1.

Ikiwa unaamua kuomba ushauri kutoka kwa wazee wa kijiji, nenda kwenye Viongozi wa Kijadi na uchukue

kadi namba 1.

Ikiwa unaamua kuongea na mama yako, nenda kwenye Familia na uchukue kadi namba 2.

Hadithi ya Betty B5

Hadithi ya Betty

Huduma za Matibabu 1

A6

Huduma za Matibabu 1

Unafika kituo cha afya. Kimefurika na watu kama kawaida kwa sababu matibabu ni bure, lakini hata

hivyo unapata sehemu ya kukaa. Unahisi maumivu makali. Ni kama vile unachomwa chomwa na visu

mwili mzima. Daktari anapokufikia, anakupa kipimo cha mimba. Pia anakumiminia dawa kwenye

kidonda na anakuelezea kuwa ni kawaida kidonda kuhuishwa hapo mwanamke anaposhiriki kitendo

cha kujamiana kwa mara ya kwanza baada ya kukeketwa. Anakwambia ujikaze na usilalamike, kwa

sababu tatizo hilo hutokea kwa wanawake wengi. Pia daktari anakwambia una ujauzito. Unafurahia

sana. Unawazia kwamba hatimaye angalau jambo zuri limetokea katika ndoa yako iliyojaa machungu.

Unaamini kwamba kwa sababu una ujauzito mume wako hatataka kulala na wewe tena.

Maumivu uliyokuwanayo yanapungua unapowazia kupata mtoto wako. Unajaribu hata kuota hali

itakavyokuwa ikiwa utapata mtoto wa kiume. Labda mume wako atakuruhusu umalizie masomo

yako! Unatamania kuwaambia mume wako na mama yako kuhusu mimba yako. Unaanza kuchagua

majina ya kiume. Baada ya kumshukuru sana kila mtu, unatoka nje na kurudi nyumbani. Ghafla dunia

haionekani kuwa mbaya sana kwako kama wakati ulipoingia hapo hospitalini. Kama Fauzia angekuwa

anaishi eneo jirani, angefurahia sana kusikia habari zako njema, lakini anaishi mbali sana pamoja na

mume wake wa hivi majuzi. Unajiuliza kama yeye amekwisha mpata mtoto au bado. Unaharakisha

kurudi nyumbani ili ukampashe habari hizi mume wako.

Nenda kwenye Kurudi Nyumbani na uchukue kadi namba 1.

Hadithi ya Betty B6

Hadithi ya Betty

Familia 2

A7

Familia 2

Mama yako anakusikiliza na kukuhurumia. Hata hivyo, anakwambia kwamba ni jambo la kawaida

kuhisi maumivu wakati wa kujamiana, na kwamba maadamu utazaa mtoto wa kiume, tunza mji

wako, usije ukaleta aibu kwa mume wako, kila kitu kitakuwa sawa. Anakukumbusha kwamba

mumeo alilipa mahari nzito na anakuuliza iwapo umemfanyia jambo lolote lililomuudhi mume

wako. Unapomwambia kwamba ulikuwa mtiifu kwa kila kitu, ndipo anakwambia ukae kwake kwa

siku kadhaa mpaka utakapopata nafuu. Anakuonya kwamba ni lazima urudi kwa mume wako baada

ya majeraha kupona.

Unaangalia vitabu vyako vya shule ya msingi, unafunuafunua kwa shauku lakini ghafla unavitupia

nje kwa hasira kwa sababu unajua hutavitumia tena. Unaviwashia kiberiti na kuvitazama vikiteketea

kwa moto kama yalivyo maisha yako. Unawaza kuhusu Fauzia ambaye pia amekwishaolewa na

hujui anaendeleaje, na pia kama mume wake anaishi naye kwa raha, au kama ndoa yako ndiyo hali

kielelezo ya wanawake wote walioolewa.

Mama yako anahisi moshi na anataka nje kukuchungulia. Anapoona vitabu vinateketea hadi kuwa

majivu, anakaa chini pembeni na wewe. “Ni bora kuziacha ndoto hizo ziteketee, Betty. Unatakiwa

kuzingatia kupata watoto. Isitoshe, kwa nini kesho usiende hospitali kupimwa kama una ujauzito?”

Ikiwa unaamua kwenda kuongea na wazee wa kijijji, nenda kwenye Viongozi wa Kijadi na uchukue

kadi namba 1.

Ikiwa unaamua kwenda moja kwa moja kwenye kliniki, nenda kwenye Huduma za Matibabu na

uchukue kadi namba 1.

Hadithi ya Betty B7

Hadithi ya Betty

Kiongozi wa Jadi 1

A8

Kiongozi wa Jadi 1

Wakati wowote kunapotokea tatizo kubwa kijijini, watu huenda kuzungumza na wazee. Unayakumbuka

macho ya ukarimu ya Bwana Moses tangu ukiwa bado mdogo sana. Unaamua kwenda nyumbani

kwake kuzungumza naye.

Unapofika nyumbani kwake, unamkuta akiwa na mtu mwingine wa kutoka kijijini kwenu. Msichana

anakuletea kigoda na unaketi kivulini ukisubiri amalize mazungumzo yake. Anapomaliza na

kukupungia mkono uje kwake, unapiga magoti kumtukuza na kumsalimia. Anainamisha kichwa chake

na kisha anakuuliza ni tatizo gani limekufanya uende kumuona. Unamwelezea kwamba uliachishwa

masomo na kulazimishwa kuolewa na mwanamume mzee sana, na kwamba mwili wako unakuuma,

na umepoteza fursa yako ya kupata elimu. Anacheka kicheko cha chinichini na kukupapasa kichwani

kama vile bado u mtoto mdogo. “Betty,” anafunga macho yake wakati anaongea na wewe, “Hili ni

jukumu lako katika maisha – kuwa mke mzuri na mama pia. Bwana tajiri sana amekulipia mahari

kubwa kwa ajili yako, hivyo lazima uwe mtiifu kwa mumeo na usilete aibu kwa kijiji chetu.”

Unainamisha kichwa chako kwa huzuni. Unajua huwezi kujadiliana naye suala la maumivu unayopata

kwa sababu ni mtu wa heshima sana kama yeye, hivyo unamshukuru na kumwomba uondoke.

Unapotembea kurudi nyumbani unawazia juu ya nini utachofanya. Hutaki kuleta aibu kwa familia

yako, lakini pia hutaki kuishi katika maumivu ya kudumu. Uamuzi wako wa mwisho ni kwenda

hospitalini iliyo karibu ili upate kusaidiwa.

Nenda kwenye Huduma za Matibabu na uchukue kadi namba 1.

Hadithi ya Betty B8

Hadithi ya Betty

Kurudi Nyumbani 1

A9

Kurudi Nyumbani 1

Leo ni siku tofauti na siku nyingine unapohofia kurudi kwa mume wako. Leo unamwandalia chakula

akipendacho zaidi, nyama ya mbuzi, mboga za majani, siagi ya karanga pamoja na viazi vikuu.

Anakula chakula chake akiwa amekaa kwenye kigoda huku wewe ukiwa unamsubiri kwa heshima

amalize kula. Anapomaliza kula, unamshirikisha habari mpya kwamba una ujauzito. Kwa mara ya

kwanza tangu uanze kuishi naye anatabasamu, na anaonyesha kwa dhati furaha yake kwako.

“Asante kwa kunizalia mtoto wa kiume, najua atakuwa wa kiume kwa sababu nililipa mahari kubwa

sana kukuoa wewe. Najua hatimaye nitapata mrithi.”

Anaendeleza burudani kwa kukunyenyua na kukuingiza chumba cha kulala. Unamwambia jinsi

unahisi maumivu kutokana na majeraha ya hivi karibuni na kwamba daktari amesema unahitaji

kupumzika kwa muda mpaka upone. Hakusikilizi. Anajijali yeye mwenyewe. “Hakuna sababu ya

kuwa na wasiwasi,” anakwambia. Unapoendelea kukataa na kugeukia pembeni, anapata hasira.

Anakuamuru utulie na anakukandamizia kitandani huku ukilia na kumwomba akuache.

Miezi inapita wakati mimba yako inazidi kuwa kubwa kila siku. Ulifikiri mimba yako itamridhisha

mumeo na aache kujamiana na wewe, lakini anaendelea kukulazimisha kufanya ngono. Umejifunza

kutolia wala kulalamika kwa sababu ukifanya hivyo inamfanya awe mkorofi zaidi. Unaendelea kuamini

kwamba kuna wakati mimba itakuwa kubwa zaidi kiasi cha kumfanya awe mbali nawe kwa ngono.

Mara muda wa kujifungua kwako umefika. Wake wenzio wanamleta mkunga wa kijadi akuhudumie.

Uchungu wa kujifungua unakushika kwa muda mrefu sana, zaidi ya siku mbili. Hatimaye, mkunga

wako anamshauri mumeo akupeleke hospitalini.

Nenda kwenye Huduma za Matibabu na uchukue kadi namba 2.

Hadithi ya Betty B9

Hadithi ya Betty

Huduma za Matibabu 2

A10

Huduma za Matibabu 2

Hospitalini, daktari anakusaidia kujifungua. Hatimaye mtoto anapotoka, ni mtoto wa kiume, lakini kwa

bahati mbaya amefariki. Unalia sana wala huwezi kunyamaza. Daktari anajaribu kukueleza kwamba

ni jambo la kawaida kwa msichana mwenye umri mdogo kujifungua kwa shida na kwamba kichanga

chako kilikwama kwenye njia ya uzazi. Mama yako na wake wenzio wanajaribu kukunyamazisha na

kukuambia kwamba usihofie kwani bado unafursa ya kujaribu tena, lakini huachi kujilaumu na kuhisi

kuwa ni amkosa yako.

Unataka tu kurudi nyumbani, lakini hali bado haijawa nzuri sana. Akiongea na wewe pamoja na

mama yako kwa faragha, daktari anawaarifu kuwa hapo wakati wa kujifungua umepata tundu ukeni,

yaani fistula na hivyo hutaweza kudhibiti mkojo. Mkojo utakuwa tu unatiririka mfululizo.

Unakasirishwa sana na taarifa hiyo kiasi kwamba hakuna mtu anayeweza kukufariji tena. Unatumaini

mume wako atalipia gharama za kukufanyia upasuaji na kuziba sehemu yenye tundu ili usije ukawa

unatoa harufu mbaya na kusumbuliwa kama daktari alivyokuelezea. Lakini mumeo anazipokea

habari hizo shingo upande…

Nenda kwenye Ukatili Watokea na uchukue kadi namba 3.

Hadithi ya Betty B10

Hadithi ya Betty

Familia 3

A11

Familia 3

Wake wenza wanakukaribisha, lakini wanaonyesha chuki. Wanakushutumu kwamba unajivunia

ilihali umeshindwa kumzalia mumeo mtoto wa kiume. Wanasema kutiririka mkojo ndiyo malipo

unayostahili. Unatoa harufu mbaya sana kiasi kwamba wanakutenga mbali wakati wa chakula.

Haupiti muda mrefu, harufu yako mbaya inazidi kuwa kali zaidi na utunzaji wa kila siku ambao

unahitaji unawakera sana wake wenza na wanakulazimu uanze kulala nje ambako harufu yako

haitawasumbua na kuwafanya wakeshe bila sababu. Wakati wote wanakuzungumzia wewe na jinsi

ambavyo umechezea maisha yako kwa sababu hakuna mwanamume ambaye anaweza kukutaka

tena.

Hatimaye mmoja wao anakwambia,“Unanuka sana kiasi kwamba hatuwezi tena kulimana na

wewe bustanini. Hatuwezi kufuatana na wewe hadi madukani kwa sababu unatuaibisha. Watu

hawatutembelei tena kwa sababu yako. Unatakiwa uondoke.” Asubuhi yake unafungasha kifurushi

kidogo cha nguo zako na kuondoka mapema kabla hakujapambazuka.

Ikiwa unaamua kwenda kwa wazazi wako, nenda kwenye Familia na uchukue kadi namba 4.

Ikiwa unataka fursa nyingine kwa kuruhusiwa kumrudia mumeo, nenda kwenye Fursa na uchukue

kadi namba 1.

Hadithi ya Betty B11

Hadithi ya Betty

Ukatili Watokea 3

A12

Ukatili Watokea 3

Unapofika nyumbani unakuta mume wako anakusubiri kwa hamu. Anapopata taarifa kwamba

umejifungua mtoto wa kiume aliyekufa, anaghadhabika. Anakufokea na kukutupia bakuli kichwani.

Anakushutumu kwamba wewe ni mchawi aliyeolewa ili umtese na anasema hakuna kilichobaki kati

yenu. Akikusukumia pembeni, anakuambia upotelee mbali na ukatafute sehemu mahali pengine pa

kuishi.

Hupati hata fursa ya kumwambia kuhusu fistula wala kumuomba akulipie gharama za upasuaji kabla

haja kutimua nje na kukutupia nguo zako uondoke.

Ikiwa unaamua kwenda kuishi na wake wenza, nenda kwenye Familia na uchukue kadi namba 3.

Ikiwa unaamua kutafuta msaada kutoka kwa mganga wa jadi kijijini kwenu, nenda kwenye Mganga

wa Jadi na uchukue kadi namba 1.

Hadithi ya Betty B12

Hadithi ya Betty

Mganga wa Jadi 1

A13

Mganga wa Jadi 1

Unamkumbuka mwanamke aliyekukeketa miaka mingi iliyopita na kwamba wanajamii wanamuamini

kuwa ni mganga bora kuliko wengine pale kijijini. Baada ya kukukeketa aliahidi kwamba unaweza

kwenda kumuona wakati wowote unapokuwa na shida. Unaamini atakusaidia kutibu tatizo lako.

Unarundi kwenye mazingira ya nyumba ambapo uliumia na kuishi kwa maumivu makali ulipokuwa

bado mdogo, na unasita kidogo wakati unavuta kumbukumbu, lakini unaendelea kwenda na

kumuona huyo mama ambaye sura yake utaikumbuka daima. “Shikamoo, ni mimi Betty,”unataja jina

lako ukitarajia atakukumbuka. Lakini sura yake inaonesha hakumbuki kitu na kisha anaonesha kuhisi

vibaya anaposikia harufu ya mkojo. Unafanya haraka kumwambia kilichokupata na unamuomba

akusaidie. Anakutazama kuanzia juu mpaka chini, anaangalia mikono yako mitupu pamoja na sketi

yako iliyolowa mkojo. “Siwezi kukusaidia,”anakwambia huku akitikisa kichwa. “Hakuna chochote

ninachoweza kukufanyia. Harufu hiyo ni mbaya sana kwangu na unaweza kuharibu dawa zangu.

Unatakiwa kuondoka sasa hivi.” Anakuashiria uondoke halafu anakwenda zake.

Ni mateso makali sana kwa ahadi na ndoto ulizokuwa nazo. Unahisi upweke usio na matumaini

yoyote.

Ikiwa unaamua kujaribu kuona kama wake wenza watakubali uishi nao, nenda kwenye Familia na

uchukue kadi namba 3.

Ikiwa unaamua kwamba mtu pekee atakaye kupokea kwa sasa ni mama yako, nenda kwenye

Familia na uchukue kadi namba 4.

Hadithi ya Betty B13

Hadithi ya Betty

Fursa 1

A14

Fursa 1

Huoni kama kutakuwa na maendeleo yoyote iwapo hutafanikiwa kufanyiwa upasuaji na kutibiwa

fistula. Kimbilio lako pekee ni mume wako, hivyo unakwenda kwenye nyumba yake wakati akiwa

bado hajarudi na unamuandalia chakula maalumu cha jioni. Anapofika nyumbani, anakuona na

kutaka kujua unafanya nini hapo nyumbani. Humjibu chochote, lakini unamuomba akusikilize.

Anakupuuza mwanzoni lakini hukati tamaa kwa kuendelea kumsihi mpaka hatimaye anakusikiliza.

Unamwelezea jinsi utakavyomzalia mrithi. Unamkumbusha kwamba umeshazaa mtoto wa kwanza

wa kiume, lakini ni kukosekana kwa huduma nzuri za kitabibu ambako kumesababisha kifo cha

mtoto huyo. Unamwahidi kwamba iwapo atakupa fursa nyingine tena, utajitunza vizuri pamoja na

kutapata huduma bora za kitibabu. Unamuona akianza kushawishika, na unamhakikishia kabisa

kwamba utamzalia mtoto wa kiume. Hatimaye anakubali kulipa gharama za kufanyiwa upasuaji ili

kuziba fistula na anakuruhusu urudi tena kukaa kwenye nyumba yake.

Kwa bahati nzuri, upasuaji unafanyika kwa mafanikio. Na muda si mrefu unashika mimba nyingine.

Safari hii mumeo anajitoa kwa gharama zote kuhakikisha anapata mtoto wa kiume mwenye afya

nzuri na ambaye atarithi mali zake kwa sababu yeye amezeeka.

Anakupa matunzo mazuri sana kwa kuwatowajali wake zake wengine, jambo ambalo linawafanya

wakuchukie zaidi. Wanakwambia unajivuna na huna shukurani, lakini unajitahidi kutowajali sana.

Unajihisi kama vile umepewa fursa nyingine, lakini…

Nenda kwenye Ukatili Watokea na uchukue kadi namba 4.

Hadithi ya Betty B14

Hadithi ya Betty

Familia 4

A15

Familia 4

Harufu inayotoka mwilini mwako ni mbaya sana kiasi kwamba unaacha kukaa pamoja na watu kwa

mazungumzo. Unajihisi kutengwa na mpweke. Watu hawakukaribishi tena majumbani mwao wala

kwenye matukio muhimu ya kijamii. Tumaini lako pekee ni kwamba mama yako atapata suluhu ya

tatizo lako.

Nyumbani kwa mama yako, unamsalimia na anakukaribisha ndani vizuri kwa ukarimu. Anakushika kwa

muda kidogo na kuonyesha masikitiko yake juu ya mtoto wako uliyefariki. Anasema unakaribishwa

nyumbani wakati wowote lakini hutakaa kwenye nyumba kuu kwa sababu harufu yako ile mbaya

itamsumbua baba yako. Kwa huzuni kubwa, anakusindikiza kwenye kibanda kidogo kilichopo nyuma

ya nyumba na ambacho hakijatumika kwa miaka kadhaa iliyopita. Anakusaidia kufungua na kuweka

vizuri nguo zako chache ulizokuja nazo na kisha anakuletea maji ya kuoga.

Hivi ndivyo unavyoishi sasa – mpweke, aliyetengwa na jamii, na usiyekaa katika familia yoyote. Ndoto

na matarajio yako yote vimegeuka kuwa kumbukumbu za ukatili.

MWISHO

Huu ndio mwisho wa hadithi ya Betty. Tumia dakika chache kukaa kimya na utafakari tajiriba yake

Betty. Unapokuwa tayari, muombe mwezeshaji akupe hadithi ya mwanamke mwingine.

Hadithi ya Betty B15

Hadithi ya Betty

Ukatili Watokea 4

A16

Ukatili Watokea 4

Unapokaribia kujifungua unapanga kwenda kwenye kituo cha afya kilichoko karibu na mnakoishi,

punde tu unapoanza kuhisi uchungu wa kujifungua.

“Safari hii, kichanga chako kitakuwa salama,” unamhakikishia mumeo wakati unaondoka kwenda

hospitalini. Bila kupata shida yoyote, daktari anakusaidia na masaa machache baadaye unajifungua

mtoto wa kike mwenye afya njema.

Unafurahi kwamba mtoto ni mzima na kwamba hukupata shida yoyote katika kujifungua, lakini

kujifungua mtoto wa kike kutaleta matatizo. Unamshika vizuri mtoto wako kama wahudumu

wanavyokuelekeza na unaanza kumyonyesha.

Unapofika nyumbani siku chache baadaye, mume wako anakataa hata kukuangalia wewe wala

mwanae wa kike. Anawaambia wake wenzako wakutolee nje vitu vyako vyote kwa sababu

hutaendelea kukaa kwenye nyumba yake tena. Safari hii, wake wenzio wanakubeza na kukuambia

kwamba hawawezi kulea mtoto mwingine wakati na wao wana watoto. Huna njia mbadala isipokuwa

kurudi nyumbani kwa mama yako.

Nenda kwenye Familia na uchukue kadi namba 5.

Hadithi ya Betty B16

Hadithi ya Betty

Familia 5

A17

Familia 5

Unamlea binti yako ukiwa nyumbani kwa mama yako. Mama yako hakuulizi kwa nini mumeo

amekufukuza, wala hakutupii lawama kwa nini umezaa mtoto wa kike. Badala yake, anakusaidia

kumlea mtoto wako kwa malezi bora kadri inavyowezekana. Unampatia jina Muujiza kwa sababu

kwako wewe, ni Muujiza ambao umekufundisha mambo mengi kuhusu mapenzi na maisha.

Baada ya kumwachisha kunyonya, unapata kibarua kwenye mkahawa wa pale kijijini kwa kusafisha

pale baada ya kufunga. Unatumia pesa hizi japo ni kidogo, kugharamia mahitaji ya nyumbani na

kuweka akiba kidogo kwa ajili ya kumsomeshea Muujiza. Japokuwa ndoto zako zimefutika, utafanya

kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba binti yako anapata elimu ya kutosha na pia kwamba hata

ataweza kutembelea jiji.

MWISHO

Huu ndio mwisho wa hadithi ya Betty. Tumia dakika chache kukaa kimya na utafakari tajiriba yake

Betty. Unapokuwa tayari, muombe mwezeshaji akupe hadithi ya mwanamke mwingine.

Hadithi ya Betty B17

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!