30.01.2013 Views

Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices

Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices

Hadithi ya Betty Utambulisho - Raising Voices

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Ukatili Watokea 1

Leo wewe na Fauzia mnakimbia mkirudi nyumbani kutoka shuleni huku mmejitwika vizuri kichwani vitabu

vyenu kuona ni nani atafika wa kwanza pasipo vitabu vyake kuanguka. Unapofika nyumbani mama yako

anakwambia kesho asubuhi mtaamka mapema na mtaenda sehemu fulani maalumu. Hupati picha halisi

juu ya jambo analozungumzia, lakini huna uhuru wa kumuuliza maswali mengi.

Umelala tongo macho kwa shauku uliyonayo, na leo badala ya kwenda shuleni, mama yako anakuongoza

kuelekea njia iendayo sokoni. Unawazia kwamba huenda anaenda kukununulia nguo mpya. Mnasimama

kwenye kibanda kilichopambwa vizuri. Unawaona wanawake vikongwe wawili wamesimama mlangoni.

Mmoja wao ni mganga anayetibu wanawake kule kijijini. Mwanamke huyo ni maarufu sana na watu

wanasema ndiye mwanamke tajiri sana kuliko wote kijijini. Mama yako anakukumbatia na kukutakia kila

la heri. Kichwa chako kinaanza kuwayawaya huku ukikaribishwa uani ambako kumetapakaa wanawake

wengi wagonjwa. Huko ndani unaona beseni lenye maji, na beseni jingine lina maji ya kijani, visu

viwili, na chini kuna pia sahani yenye pamba. Mwanamke mmoja anakwambia ulale chini. Mwanamke

mwingine anakaribia na kukushika miguu na mikono kwa kuikandamiza chini kwa nguvu. Kabla hujajua

kinachoendelea, tayari imeshavuliwa chupi yako na yule mganga ameanza kukata. Huwezi kuelezea

maumivu makali unayoyapata mwilini, utafikiri kaa la moto limewekwa sehemu zako za siri. Unatoa macho

na kuanza kupiga kelele kwa maumivu lakini mwanamke mmoja anakuziba mdomo, akikwambia maumivu

yatapoa muda si mrefu. Hatimaye maumivu yanapungua taratibu na wale wanawake wanakuweka pamba

yenye unyevunyevu kwenye sehemu za maumivu. Maumivu yanaonekana kusambaa mwili mzima. Mtu

fulani anakunyanyua kutoka chini kwenye uchafu na kukuingiza ndani kwenye mkeka ambapo unalala

kwa maumizi tele.

Masaa yanapozidi kwendelea unawaona wasichana wengine wakiingia na kutoka ndani ya nyumba hiyo.

Moyo wako unashtuka unapomuona Fauzia akiingia, lakini huna nguvu za kumuita akipita na kuingia

kwenye chumba kingine chenye giza. Unapitiwa na usingizi na kulala mpaka wakati wanapokuja kukusafisha

kidonda chako. Pia wanawaletea chakula kizuri mpate kula, lakini hata hivyo maumivu hayatoweki.

Ikiwa unataka kumtafuta Fauzia, nenda kwenye Marafiki na Majirani na uchukue kadi namba 1.

Ikiwa unaamua kwenda nyumbani kumuona mama yako, nenda kwenye Familia na uchukue kadi

namba 1.

Hadithi ya Betty B2

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!