08.06.2013 Views

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa

kwenu). (2Wathes. 1:6-10. Maneno mepesi kukazia)

Paulo alisema kwamba wakati ambao Yesu angerudi kuwapa nafuu Wathesalonike

waliokuwa wanateswa (ona 1Wathes. 1:4, 5), angetokea “pamoja na malaika wake katika

mwali wa moto” ili kuwaadhibu wale waliokuwa wanawatesa wao, kutoa hukumu ya

haki, inayostahili. Hii haifanani na kile kinachosemwa na wengi, kwamba Unyakuo

utatokea kabla ya dhiki, na kanisa kunyakuliwa na Kristo kabla ya kile kipindi cha dhiki

cha miaka saba kuanza. Hii pia huitwa kuja kwa siri kwa Yesu ili kunyakua kanisa Lake.

Hapana kabisa! Maelezo haya yanafanana na kile ambacho Yesu alieleza katika Mathayo

24:30, 31 – kurudi Kwake karibu au mwishoni mwa kipindi cha dhiki kuu –

anapowanyakua waaminio na kumimina hasira Yake juu ya wasoiamini.

Siku Ya Bwana

Baadaye, katika barua hiyo hiyo, Paulo aliandika hivi:

Basi ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu

Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake, kwamba msifadhaishwe upesi

hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala

kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana

imekwisha kuwapo (2Wathes. 2:1, 2).

Kwanza: Ona kwamba mada ya Paulo ni kurudi kwa Kristo na Unyakuo. Aliandika

kuhusu “kukusanyika kwetu mbele zake,” akitumia maneno yale yale ambayo Yesu

alitumia katika Mathayo 24:31, alipozungumza juu ya malaika ambao “wangekusanya”

wateule Wake “kutoka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho ule.”

Pili: Ona kwamba Paulo anayaita matukio hayo kuwa ni “siku ya Bwana,” sawa na

alivyofanya katika 1Wathesalonike 4:13 hadi 5:2. Hilo liko wazi kabisa.

Kisha anaendelea hivi:

Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja

kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa

uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho

Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la

Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu (2Wathes.

2:3, 4. Maneno mepesi kukazia).

Wakristo Wathesalonike walikuwa wanadanganywa kwa namna fulani kwamba siku

ya bwana – ambayo kulingana na Paulo lazima ianze kwa Unyakuo na kurudi kwa Kristo

– ilikuwa imekwisha fika. Akatamka wazi wazi kwamba haiji mpaka baada ya ule

ukengeufu (labda ndiyo kule kurudi nyuma ambako Yesu alizungumzia katika Mathayo

24:10) na baada ya mpingakristo kujitangaza kwamba ni Mungu kutoka hekalu la

Yerusalemu. Basi, Paulo anawaambia waamini Wathesalonike wazi wazi kwamba

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!