08.06.2013 Views

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

kusakwa na kuuawa. Ndiyo sababu Yesu aliwaambia waamini wa Uyahudi wakimbilie

milimani bila kukawia, wakiomba kwamba kutoroka kwao kusizuiwe na sababu yoyote

ile.

Wazo langu ni kwamba ingekuwa vizuri kwa waamini wote duniani kukimbilia

maeneo yaliyofichika wakati huo, maana tukio hilo litatangazwa duniani kote kwa njia ya

televisheni. Maandiko yanatuambia kwamba dunia nzima itadanganywa na mpingakristo

na kudhani yeye ndiye Kristo wao, nao watampa mamlaka na heshima zote.

Atakapojitangaza kwamba ni Mungu, watamwamini na kumwabudu. Atakaponena

makufuru dhidi ya Mungu wa kweli – Mungu wa Wakristo – atashawishi dunia yote

iliyodanganyika ili kuwachukia wale wanaokataa kumwabudu (ona Ufunuo 13:1-8).

Yesu aliahidi ukombozi kwa ajili ya watu Wake mwenyewe kwa “kukatisha” hizo

siku za dhiki, vinginevyo, “asingeokoka mtu yeyote” (24:22). Huko “kukatizwa” siku

hizo Naye “kwa ajili ya wateule” bila shaka ni kitu kinachohusu Yeye kuwakomboa

wakati atakapoonekana na kuwakusanya mawinguni. Yesu hata hivyo hatuambii hapa

kwamba ukombozi huo utatokea muda gani baada ya mpingakristo kujitangazia uungu.

Vyovyote vile – tunarudia kusema hapa tena kwamba Yesu aliwaacha wasikilizaji

Wake siku hiyo wakiwa wanajua kwamba wangeishi na kumwona mpingakristo

akitangaza uungu wake, na kupigana vita na Wakristo. Hili linapingana kabisa na wazo la

wale wanaosemakwamba waamini watanyakuliwa kabla ya tukio hilo. Kama

ungemwuliza Petro, Yakobo au hata Yohana kwamba Yesu angerudi kuwaokoa kabla ya

tamko la mpingakristo kwamba ni Mungu, wangekujibu, “Si hivyo”.

Vita Dhidi Ya Watakatifu

Katika sehemu zingine, Maandiko yanatabiri juu ya mateso ya mpingakristo kwa

waamini. Kwa mfano: Yohana alifunuliwa, naye akaandika hivi katika kitabu cha

Ufunuo:

Naye [mpingakristo] akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya

makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.

Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na

maskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na

watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na

lugha na taifa (Ufunuo 13:5-7. Maneno mepesi kukazia).

Ona hapo kwamba mpingakristo atapewa “uwezo wa kufanya kazi yake” kwa miezi

arobaini na mbili, au, miaka mitatu na nusu kamili. Huu ndiyo wakati unaoitwa nusu ya

wakati wa kipindi cha Dhiki ya miaka saba. Ni sawa kabisa kufikiri kwamba ni ile miezi

arobaini na mbili ya mwisho ya Dhiki, ndipo mpingakristo atakapopewa “uwezo wa

kufanya kazi yake,” kwa sababu mamlaka yake yataondolewa kabisa wakati Kristo

atakaporudi kufanya vita naye na majeshi yake wakati wa kumalizika kwa Dhiki.

Ni dhahiri kwamba “uwezo wak ufanya kzi yake” kwa miezi arobaini na mbili maan

ayake ni mamlaka maalum, maana mpingakristo atapewa mamlaka kiasi fulani na Mungu

katika wakati wake wa kumiliki. Haya “mamlaka maalum ya kufanya kazi” yanaweza

kuwa ni muda atakaopewa wa kuwashinda watakatifu, maana, tunasoma hivi katika

kitabu cha Danieli:

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!