08.06.2013 Views

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Yakobo asingekuwa na haja ya kuwashauri wasomaji wake kuvumilia kuhusu kitu

ambacho kisingetokea maishani mwao. Yeye aliamini kwamba kuja kwa Bwana

“kunakaribia.” Kimantiki, Yakobo aliandika barua yake wakati kanisa lilipokuwa

linapitia mateso makali (ona Yakobo 1:2-4), wakati ambapo waamini wangetamani sana

kurudi kwa Bwana wao.

Paulo vile vile aliamini kwamba Yesu angeweza kurudi wakati wa maisha ya

wenzake. Anaandika hivi:

Lakini ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije

mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana ikiwa twaamini

ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika

Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twaambieni haya kwa

neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja

kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa

sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko,

na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika

Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa

pamoja nao katika mawingu ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa

pamoja na Bwana milele. Basi farijianeni kwa maneno hayo (1Wathes.

4:13-18. Maneno mepesi kukazia). 1

Kutokana na hayo tunajifunza pia kwamba wakati Yesu atakaporudi kutoka

mbinguni, miili ya waamini waliokufa itafufuliwa, kisha, pamoja na waamini walio hai

wakati wa kuja Kwake, “kunyakuliwa ili kumlaki Bwana hewani” (Unyakuo). Kwa kuwa

Paulo naye alitaja kwamba Yesu angewaleta wale waliokufa “ndani Yake” kutoka

mbinguni, tunachoweza kusema ni kwamba wakati wa Unyakuo, roho za waamini

walioko mbinguni zitaunganishwa na miili yao iliyofufuliwa punde tu.

Petro naye aliamini kwamba kuja kwa Kristo kulikuwa karibu sana, alipoandika barua

yake ya kwanza kabisa.

Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa

utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. …Lakini

mwisho wa mambo yote umekaribia, basi iweni na akili, mkeshe katika sala.

… Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika

ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe (1Petro 1:13; 4:7, 13.

Maneno mepesi kukazia). 2

Na Yohana naye, alipoandika barua zake kwa makanisa, aliamini kwamba mwisho

ulikuwa karibu, na kwamba wasomaji wa siku zake wangeona kurudi kwa Yesu.

1 Maandiko mengine yenye kuonyesha imani ya Paulo kwamba Yesu angeweza kurudi katika wakati wa

uhai wake ni Wafilipi 3:20; 1Wathes. 3:13; 5:23; 2Wathes. 2:1-5; 1Timo. 6:14, 15; Tito 2:11-13;

Waebrania 9:28.

2 Maandiko mengine yenye kuonyesha imani ya Petro kwamba Yesu angeweza kurudi wakati wa uhai

wake ni 2Petro 1:15-19; 3:3-15.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!