08.06.2013 Views

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Dhiki Inaaza Katika Dunia Nzima

Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa

watu wa kuchukuwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu. Ndipo wengi

watakapojikwaa, nao watasalitiana na kuchukiana. Na manabii wengi wa

uongo watatokea, na kudanganya wengi. Na kwa sababu ya kuongezeka

maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho,

ndiye atakayeokoka. Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika

ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho

utakapokuja (Mathayo 24:9-14. Maneno mepesi kukazia).

Hapa tena – kama ungewauliza wale waliomsikiliza Yesu siku hiyo swali hili: “Je,

mnatazamia kuwa hai ili kuona kutimia kwa mambo hayo?” bila shaka wangejibu ndiyo

kwa uhakika sana, maana Yesu alisema nao moja kwa moja.

Kama tulivyosoma – mara tu baada ya “utungu” kuna tukio ambalo kweli halijatokea,

la wakati wa Wakristo duniani kote kuteswa. Tutachukiwa na “mataifa yote”. Yesu

alikuwa anazungumza juu ya wakati fulani ambapo hayo yangetokea – si kipindi cha

jumla cha miaka mia nyingi, maana alisema hivi baada ya hayo, “Ndipo wengi

watakapojikwaa,nao watasalitiana na kuchukiana.”

Bila shaka anachosema hapo kinahusu kurudi nyuma kwa waamini Wakristo ambao

baada ya hapo watawachukia waamini wengine, maana wasioamini hawawezi

“kuanguka,” tena, wanachukiana tayari. Basi, mateso ya dunia nzima yatakapoanza,

kutakuwa na kurudi nyuma kwa watu wengi wanaodai kwamba ni wafuasi wa Kristo.

Kama ni wakweli au ni waamini bandia – yaani kondoo au mbuzi – wengi sana

wataanguka, nao watafichua majina ya waamini wengine kwa watesaji, wakiwachukia

wale waliodai kuwapenda. Matokeo ni kwamba kanisa duniani kote litasafishwa.

Halafu tena kutakuwa na ongezeko la manabii wa uongo, na mmoja anatajwa sana

katika kitabu cha Ufunuo kuwa mwenzake mpinga Kristo (ona Ufunuo 13:11-18; 19:20;

20:10). Maasi yataongezeka na kufikia mahali pa kumaliza kabisa upendo kidogo

utakaokuwa umesalia mioyoni mwa watu, na wenye dhambi watakuwa wabaya kukithiri.

Wafia Dini Na Watakaosalia

Ingawa Yesu alitabiri kwamba waamini watapoteza maisha yao (ktk 24:9), si wote,

maana aliahidi kwamba wale watakaovumilia mpaka mwisho wataokolewa (ona 24:13).

Yaani, kama hawataruhusu wadanganywe na wale makristo wa uongo au manabii wa

uongo, na kama watashinda jaribu la kuacha imani yao na kuanguka, wao wataokolewa

na Kristo wakati anaporudi ili kuwakusanya mawinguni. Huu wakati wa dhiki baadaye

pamoja na ukombozi wake ulifunuliwa kidogo kwa nabii Danieli pia. Yeye aliambiwa

hivi

Na kutakuwa wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza

kuwapo taifa hata wakati uo huo; na watu wako wataokolewa; kila mmoja

atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Tena, wengi wa hao

walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa

milele, wengine aibu na kudharauliwa milele (Danieli 12:1, 2).

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!