08.06.2013 Views

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Hakuna shaka yoyote kwamba Unyakuo wa kanisa utafanyika wakati fulani katika hiyo

miaka saba, au karibu na hiyo miaka saba.

Je, Unyakuo Ni Lini Hasa?

Swali ambalo mara nyingi linawagawa Wakristo ni wakati hasa wa Unyakuo. Kuna

wanaosema kwamba Unyakuo utatokea kabla ya ile miaka saba ya dhiki. Kwa maana

hiyo, unaweza kutokea wakati wowote. Wengine wanasema utatokea katikati ya ile

miaka saba ya dhiki. Na wengine tena wanasema utatokea punde tu baada ya dhiki ya

miaka saba kufika katikati. Na kuna wengine nao wanaosema kwamba Unyakuo utatokea

wakati wa Yesu kurudi na ghadhabu nyingi, mwishoni mwa kipindi cha Dhiki.

Hilo si swala la kugawanyikia, na makundi yote manne yanapaswa kukumbuka

kwamba yote yanakubali kwamba Unyakuo utatokea wakati fulani katika kipindi hicho

cha baadaye cha dhiki ya miaka saba, au karibu nacho. Hilo ni dirisha dogo sana katika

upana wa miaka maelfu ya historia. Hivyo, badala ya kugawanyika kutokana na

kutokubaliana kwetu, ni afadhali tufurahie makubaliano yetu! Tena, si kitu tunaamini nini

maana haitabadilisha kitakachotokea.

Baada ya kusema hayo, sina budi kusema kwamba, kwa miaka ishirini na mitano ya

kwanza katika maisha yangu ya Kikristo, niliamini kwamba Unyakuo utatokea kabla ya

Dhiki ile ya miaka saba. Niliamini hivyo kwa sababu ndivyo nilivyofundishwa, na pia

kwa sababu sikutaka kupitia mambo ninayosoma habari zake katika Kitabu cha Ufunuo!

Ila, nilipoendelea kujifunza Maandiko, nilianza kupata mtazamo tofauti. Hebu kwa

pamoja tutazame Biblia inavyosema, na tuone tutafikia maamuzi gani. Hata kama

sitafanikiwa kukushawishi ujiunge na upande wangu, hebu tuendelee kupendana!

Mafundisho Pale Mlima Wa Mizeituni

Hebu tuanze kwa kutazama sura ya 24 ya Injili ya Mathayo, sehemu ya Maandiko

ambayo ni ya msingi sana kwa habari ya matukio ya nyakati za mwisho na kurudi kwa

Yesu. Pamoja na sura ya 25, sehemu hiyo huitwa Mafundisho Pale Mlima Wa Mizeituni,

kwa sababu sura hizo mbili ni taarifa ya mahubiri ambayo Yesu alitoa kwa baadhi ya

wanafunzi Wake wa karibu sana 3 hapo mlimani. Tunaposoma mafundisho hayo,

tutajifunza kuhusu matukio mengi ya nyakati za mwisho, nasi tutaona uwezekano wa

wanafunzi wa Yesu kufikiri muda wa Unyakuo ni upi, waliposikia mafundisho yenyewe.

Yesu akaenda zake, akatoka hekaluni. Wanafunzi wake wakamwendea ili

kumwonyesha majengo ya hekalu. Naye akajibu akawaambia, ‘Hamyaoni

haya yote? Amin nawaambieni, halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo

halitabomoshwa.’Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni,

wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha wakisema, ‘Tuambie! Mambo

hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa

dunia?’ (Mathayo 24:1-3).

3 Katika Marko 13:3 wanatajwa wale wanne waliokuwepo: Petro, Yakobo, Yohana na Andrea. Mafundisho

ya pale Mlima wa Mizeituni yanapatikanapia katika Marko 13:1-37 na Luka 21:5-36. Utapata habari kama

hizo katika Luka 17:22-37 pia.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!