Download TPS, East Africa 2008 Annual Report - Serena Hotels
Download TPS, East Africa 2008 Annual Report - Serena Hotels
Download TPS, East Africa 2008 Annual Report - Serena Hotels
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
Taarifa ya Mwenyekiti (yaendelea)

Sehemu ya nje ya Hoteli ya Ngorongoro Serena

Hatimaye, kwa mara nyingine, Hoteli za Serena zilitwaa

nafasi za juu kwenye shindano la jarida la Travel News

Magazine kwa utuzaji bora. Mpango huu wa uzawadiaji

unatekelezwa kupitia utafiti wa wateja, utendaji bora katika

sekta mbali mbali za utalii Afrika Mashariki. Hata kama

kulikuwa na changamoto zilizotajwa hapo awali, ukarabati

mdogo ulitekelezwa katika raslimali mbali mbali za Kundi

kuhakikisha kuwepo kwa utekelezaji bora wa shughuli bila

kuathiri ubora wa sura ya majumba.

Kujitolea kwa Serena kuzindua mkakati wa habari na

mawasiliano ambao unakamilisha mikakati mingine ya

biashara na mipango uliendelea mwaka 2008. Ningependa

kufafanua kwamba ingawa mwaka ulikuwa mgumu,

usimamizi haukusitisha uzinduzi wa mipango muhimu

ambayo endapo ingecheleweshwa ingehatarisha ushindani

wa muda mrefu wa Kampuni. Kwa sababu hiyo, Kampuni

sasa inatoa huduma za mawasiliano ya mtandao ya moja kwa

moja kwa wageni wake katika hoteli zake. Mpango wa

kuweka pamoja habari uko katika hatua za mwisho za

uzinduzi baina ya afisi kuu mbili nchini Kenya na Tanzania

ambao utasaidia kuafikia ulipiaji huduma/vyumba mapema

na mifumo ya fedha na kupelekea kuwepo kwa utendaji bora

wa kazi, usimamizi na uthibiti bora. Mwisho, ufanisi

umepatikana kuhusiana na uuzaji wa biashara kupitia mfumo

wa elektroniki ambapo hoteli za Serena zilianza kutumia

mbinu hiyo mwezi Agosti mwaka 2008 huku kukiwa na

mfumo wa utumaji maombi unaopatikana kupitia wavuti wa

makundi yote ya hoteli yaliyoko mijini na fuo za bahari.

Kundi linazidi kuamini kwamba wafanyakazi wake ni raslimali

muhimu katika hazina ya biashara mambo yanapokuwa

magumu. Licha ya changamoto za kibiashara, utuzaji wa

wafanyakazi, utoaji mafunzo ya hali ya juu, uimarishaji wa

uwezo ulibakia kuwa swala lililopewa kipaumbele. Wakati

wa kipindi hiki cha mwaka, Kundi lilimwajiri Meneja wa

Utoaji Mafunzo na Maendeleo ambaye kwa sasa anaendesha

mkakati wa kuimarisha uzalishaji.

Kama mnavyofahamu, wasafiri wa sasa wamejitolea

kuhakikisha raslimali wanazotumia zinatoa mchango wao

kuimarisha maendeleo miongoni mwake kupitia uhifadhi wa

mifumo ya ikolojia na kuongoza katika ustawi bora wa utalii.

Kundi linazidi kutekeleza wajibu wake katika jamii kwa

kuhusisha pamoja shughuli hizo kwenye mkakati wake wa

kibiashara. Kufikia sasa, shughuli za Kampuni katika wajibu

wa jamii zinazidi kuangazia utalii wa ikolojia, uhifadhi wa

mazingira, utoaji mafunzo, Afya ya Umma na maendeleo ya

jamii. Mnamo mwezi Juni 2008, TPSEA ilichapisha jarida lake

la pili la wajibu wake kwa jamii linalojulikana kama Serena

Outreach to Society (SOS) ambalo linaangazia shughuli hizi.

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na wajibu wa Kampuni kwa

jamii tafadhali rejelea ukurasa 20 na 21 wa ripoti hii.

Kundi limebakia kuwa mchangiaji mkuu kwa hazina ya

serikali za Kenya, Tanzania na Zanzibar. Kwa wastani Kundi

lililipa kiwango sawa na Shilingi milioni 648 pesa za Kenya

kwa ushuru wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja.

Pia lilitoa Shilingi milioni 121 kwa mabaraza ya serikali za

wilaya kama ada ya nia njema/ukodishaji katika miliki mbali

mbali mwaka 2008.

Halmashauri na wasimamizi wanakadiria kuwepo kwa

mazingira magumu ya biashara mwaka 2009 na athari za

kushuka kwa uchumi wa dunia na kuzidi kuwepo kwa wasi

wasi wa kifedha. Hali hii inatarajiwa kuchochewa na maswala

mengine, masoko yasiyoaminika na kushuka kwa imani

miongoni mwa wateja hali inayotarajia kuendelea kuathiri

mahitaji ya utalii duniani kwa muda wa miezi 12 ijayo.

Kama ilivyoshuhudiwa muhula wa kwanza wa mwaka 2009,

kipindi cha mwaka kilichosalia kitazidi kukumbwa na

changamoto ambazo zitaathiri gharama za uendeshaji

biashara kutokana na ugumu wa maisha unaosababishwa na

mfumuko wa bei, njaa iliyoko na gharama zilisizotarajiwa za

kawi. Kwa sasa, majibu kutoka kwa waendeshaji wakuu wa

biashara kuhusiana na maagizo ya vyumba katika vituo vyote

vya mapumziko ni ya kutia shaka. Wasimamizi wametambua

ukodishaji wa vyumba kwa muda mfupi siku za hivi karibuni.

Hali hii ni ya kutia moyo.

Chajio kando ya moto katika Hoteli ya Ngorongoro Serena

12 TPS EASTERN AFRICA LIMITED | ANNUAL REPORT AND FINANCIAL STATEMENTS 2008