18.06.2013 Views

Download TPS, East Africa 2008 Annual Report - Serena Hotels

Download TPS, East Africa 2008 Annual Report - Serena Hotels

Download TPS, East Africa 2008 Annual Report - Serena Hotels

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Notisi ya Mkutano wa Pamoja wa Mwaka

NOTISI inatolewa hapa kwamba, Mkutano Mkuu wa Thelathini na Saba wa Mwaka wa Kampuni utafanyika kwenye jumba la

mikutano la Kimataifa la Kenyatta (Kenyatta International Conference Centre), Nairobi, Juni 4, 2009, saa tano asubuhi, ili

kushughulikia maswala yafuatayo:

Shughuli za Kawaida:

1. Kuthibitisha kumbukumbu za mkutano wa Thelathini na Sita wa mwaka uliofanyika Mei 30, 2008.

2. Kupokea, kuangazia na endapo itaonekana kuwa sawa, kukubali hesabu kwa kipindi cha mwaka uliomalizika Desemba

31, 2008, pamoja na ripoti ya wakurugenzi na ile ya wakaguzi wa hesabu.

3. Kupitisha malipo ya mwisho ya mgawo wa faida ya 2008 wa Shilingi 1.25 kwa kila hisa za thamani ya Shilingi 1.00,

kwa kutegemea ushuru ulioshikiliwa pale inapohitajika kwa wanachama ambao majina yao yatakuwa kwenye rejista

kufikia kipindi cha biashara Juni 4, 2009. Malipo ya mgawo wa faida yatatolewa kabla au karibu na Julai 6, 2009.

4. Kuwachagua wakurugenzi

a) Bw. Jean-Loius Vinciguerra atastaafu kwa zamu kwa mujibu wa vifungu nambari 110, 111 na 112 vya sheria za

kampuni na kwa kuwa anastahili, amejitokeza tena kuchaguliwa.

b) Bw. Jean Philippe Prosper anastaafu kwa zamu kwa mujibu wa vifungu nambari 110,111 na 112 vya sheria za

kampuni na kwa kuwa anastahili, anajitokeza tena kuchaguliwa.

c) Bw. Ali Mufuruki anastaafu kwa zamu kwa mujibu wa vifungu nambari 110,111 na 112 vya sheria za kampuni na kwa

kuwa anastahili, anajitokeza tena kuchaguliwa.

5. Kupitisha malipo ya wakurugenzi ya 2008.

6. Kufahamu kwamba mkaguzi wa hesabu, PricewaterhouseCoopers, ataendelea mbele na jukumu lake kwa mujibu wa

sehemu ya 159 (2) ya sheria za kampuni nchini Kenya chini ya kifungu nambari 486. Mhasibu PricewaterhouseCoopers

ameonyesha nia ya kutaka kuendelea na jukumu hili.

7. Kupitisha malipo ya wakaguzi wa hesabu ya 2008 na wakati huo kuwaidhinisha wakurugenzi kuamua malipo yao

ya mwaka 2009.

8. Kuangazia maswala mengine ya kawaida wakati wa mkutano wa pamoja wa mwaka.

Shughuli Maalum:

9. Kuangazia na endapo itaonekana kuwa sawa, kupitisha azimio lifuatalo ambalo litachukuliwa kama swala maalum:

''KWAMBA kuambatana na mapendekezo ya Halmashauri, asilimia 100 ya umiliki wa Jaja Limited kama chombo maalumu

cha Tourism Promotion services (Kenya) Limited, kuchukua jukumu la ustawishaji wa maendeleo ya raslimali zilizoko

Nanyuki na Elmentaita kwa mujibu wa mkakati wa kundi wa kupanua biashara zake iwe hivyo na kwamba imepitishwa.

Istoshe, kuthibitisha kupatikana kwa sehemu katika kampuni ya Jaja Limited na Tourism Promotion Services (Kenya)

Limited hadi Kshs 400,000,000.00 kuwa hivyo na kupitishwa ''

KWAMBA wakurugenzi wamepewa idhini kushughulikia maswala yote yanayohitajika kufanya maazimio yaliyotajwa hapo

juu kufanyika''.

Kwa Amri ya Halmashauri

D.A Angulu (Bi)

Katibu wa Kampuni

Imenukuliwa Machi 30, 2009

Muhimu:

Mwanachama mwenye uwezo wa kuhudhuria na kupiga kura wakati wa mkutano wa pamoja wa mwaka na akawa hawezi

kufanya hivyo, anaweza kumtuma wakala/mwakilishi wake kufanya hivyo kwa niaba yake. Sio lazima kwa wakala/mwakilishi

kama huyo kuwa mwanachama wa Kampuni. Ili kuhudhuria, Fomu ya Wakala ambayo imeambatanishwa na ripoti hii lazima

ijazwe vyema na mwanachama na kupokelewa katika ofisi ya usajili ya Kampuni kabla ya saa tano asubuhi, Juni 2, 2009.

TPS EASTERN AFRICA LIMITED | ANNUAL REPORT AND FINANCIAL STATEMENTS 2008 7

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!