You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
YA

AL HABBIB SAYYEID

NA

Yamefasiriwa kwa Kiswahili na:

Al habbib Sayyeid Umar Bin Sayyeid Abdallah

(Mwinyi Baraka).

First addition.

03 Sept, 2005.

28 Rajab, 1426. HR.

i
MANAQIB YA AL-MAARUF

Baada ya yote haya ni Manaqibu ya Walii Mkubwa kabisa

aliyetajwa kwa jina hapo juu, yaliandikwa na mmoja katika

makhalifa wake wakubwa Sayyid Ahmad bin Abdul Rahmani Ibn

Sultan Alawi. Yalifasiriwa na Al Allama Sayyid Kaab Ibn Sayyid

Ahmad Zakiy Al-Masalah.

Sasa inafasiriwa kwa Kiswahili na mtoto wa ndugu yake

Walii huyo, Omar Abdallah Bin Sheikh Ahmad ambaye

hujulikana kwa jina la Mwinyi Baraka.

Huyu mfasiri kwa Kiswahili ameazimia dua zote aziache bila

kufasiriwa kwani muhimu ni kulumiwa kama zilivyopokewa.

ii.
MAISHA YAKE.

Sasa naanzia:

Utajo wa kuzaliwa kwake Mwenyi Ezi Mungu atakase siri

yake Bwana Al-Maarufu alizaliwa mwaka Saf 1270 Hijra katika

mtaa wa Bajanani, Moroni Ngazija.

Alizaliwa katika nyumba iitwayo "Shashanyongo". Baba

yake ndiye aliyemlea. Alisoma kuran Ngazija akawa anasoma

kwa Tajwidi.

Baadaye Baba yake alimpeleka Zanzibar si kwa

jingine lolote ila kutafuta ilmu. Alikaa Unguja kiasi ya miaka

mine, takriban akazijua vilivyo fani za Tajwidi, Fiqih, Nahw na

kiasi cha kutosha katika ilmu za hadithi na kuran. Ilmu zote hizi

alizichukua kutokana na mjomba wake Sayyid Ali Bin Sultan

Ahmad.

Wakati wa safari yake, Babu yake upande wa mama

yake Sultan Ahmad alimwambia; "Tutafutie ilmu ya haqiq

(undani wa mambo yaliyohusiana na Uungu) kwani sisi hatujui

vilivyo".

Baada ya kusoma ilmu hizo alirejea Ngazija, akashughulika

kukunjua ilmu zote hizi na kuita watu kwa Mwenyi Ezi Mungu

katika msikiti wa Ijumaa. Alianza kusomesha katika tafsiri ya

kuran Jalalain katika wanafunzi wake waliosoma kwake fanni ni

mwalimu wake wa Tajwidi Musa Bin Ahmad.

Muhimu:

Baba yake Sayyid, Mungu amuie Radhi ilikuwa

hakupata mtoto mwanaume. Basi alipohiji akakusudia Madina

kumzuru babu yake, Rehema ya Mwenyi Ezi Mungu na Amani

yake ziwe juu yake, alimuomba Mwenyi Ezi Mungu katika Quba

la mtume (SAW) amruzuku mtoto mwanaume kwa mke wake

mlahirifu Mwana mkuu Bint Sultan Ahmad. Aliweka nadhiri

hapo ikiwa Mwenyi Ezi Mungu kamruzuku mtoto mwanamme

1.
atapeleka pesa kidogo kwenye kuba la Mtume (SAW) kwa

matumizi ya watumikiao alipolala Mtume. Mwenyi Ezi Mungu

alipokea dua yake. Baada ya kurejea Ngazijah, mkewe alishika

mimba akamzaa anayeandikwa habari zake hapa. Baba yake

alimwita MA'ARUF. Na akapeleka zile pesa Madina kutekeleza

nadhiri yake.

Nasabu yake tukufu yeye ni Bwana wangu (Mwenyi

Ezi Mungu atakase siri yake kubwa), Muhammed Bin Sheikh

Ahmad Bin Sayyid Abubakar Bin Sayyid Ahmad Bin Sayyid

Abubakar Bin Sayyid Abdallah Bin Sayyid Salim Bin Sayyid

Ahmad Bin Sayyid Abdallah Bin Sayyid Ali Bin Alfakhir Ash-

Sheikh Abubakar Bin Salim, Aliyetawafu Einat katika

Hadhramaut. Hii ni kwa upande wa Baba yake, na kwa puande

wa Mama yake, yeye ni mtoto wa Mwana Mkuu Bint Sultan

Seyyid Ahmad na yeye ana nasibika na Abubakar Bin Salim.

Ama mabibi zake wataharifu, mama yake baba yake Wamwinyi

Bint Sayyid Eidarus anaye jukuliwa na Abubakar Bin Salim na

mama yake ni Sayyidat Khadija Bin Sheikh Salim; na yeye vile

vile anajukuliwa na Abubakar Bin Salim. Basi imejulikana kuwa

nasabu yake amezungukwa na Sheikh Abubakar Bin Salim

upande wa mabababa na upande wa mamama Mwenyi Ezi

Mungu atunufaishe na yeye na wazee wake Amin.

Wake zake watahilifu na utajo wa kubariki baba yake. Mke

wake wa mwanzo ni mtoto wa ndugu yake mama yake Sayyidat

Sittinaa Bint Sultan Sayyid Omar Bin Sayyid Hassan katika

kabila ya Almasaiha BA-ALAWI ambaye baba yake ndie

aliemposea na akamuoza baba yake mkewe Sultan Sayyid Omar

alietajwa hapo juu kwa mahari ya wanawake mfano wake aliingia

nyumbani hapo Moroni. Siku ya Tisa tangu kuingia nyumbani

baba yake alifariki (Faida; Ijumaa ya mwanzo baada ya kuingia

nyumbani Sayyidina Muhammed Bin Sheikh alimtuma mtu

akamtakie Jokho kwa baba yake ili avae kwenda kuhudhuria sala.

Sheikh Ahmad alimjibu "Mwambie mwanangu asubiri kwani

Jokho hilo litakuwa lake baada ya siku chache. Siku hizo hizo

mzee akafariki.- Nyongeza hii ni ya Mfasiri).

Bibi huyu yaani Sayyidat Sittinaa alizaa nae watoto watatu

Khadija, Hawdhat na Shama. Baadaye alimuoa Maryam Bint

Beja, akazaa naye Sayyid Ahmad. Tena alimuoa Bint Sayyid

Aqil na mwishoni kwa Ngazijah alimuoa bibi Halimah Bint Ilyas.

2.
Unguja alimuoa Bibi Khadijah Bint Ali aliezaliwa Ngazija na

mama yake ni Mngazija alizaa naye Sayyid Ali na Sayyidat

Batul. Baadaye alimuoa Bint Naqib Assayf Al-Kisadi akazaa

naye Sayyidat Sharifah na Ismail ambaye alikufa mtoto hata baba

yake hakuwahi kumuona ama Sharifah alikufa baada ya kufariki

baba yake.

Safari zake:

Mwanzo alikwenda Unguja kutafuta elimu kama

ilivyotajwa kabla katika safari zake. (Mwenyi Ezi Mungu amuilie

radhi na amwidhishe). Ni safari ya Makka tukufu alikwenda

kuhiji pamoja na mama yake na ukhti yake Sayyidat Alawiyya na

waliyofuatana nae alipokuwa Makka alikutana na mmoja katika

Mawalii wakubwa akawa humtukuza akamuusia achukue Tarika

ya AL IMAM ASH-SHADHIL akampa khabari kuwa

kufunguliwa kwake kumo katika Tarika hiyo mambo yakawa

kama alivyomkhubiria Walii huyo, katika baadhi ya mikusanyiko

yake na Walii huyo huyu Walii alimuuliza "Umekuja kwa sababu

ya yule mgonjwa wa akili ambaye anazunguka Ngazija?" Na

ilikuwa niya ya As-Sayyid ni kumuombea dua, yule walii

alimkashif. Jawabu yake ilikuwa: "Naam". Akamjibu keshapona.

Aliporejea kamkuta kweli keshapona kama alivyomwombea,

Mwenyi Ezi Mungu atanufaishe kwa siri zao. Katika safari hii

alikusudia Madina iliyojazwa Nuru ili kumzuru babu yake

(S.A.W) huko alipokea vilitokea kwa Mungu kuletewa mbele ya

Muhammed. Alikaa Madina siku kadha wa kadha katika baadhi

ya ziara zake ndani ya Kuba la Mtume takatifu aliingia yeye na

mama yake. Mama yake aliona ndani ya Kuba Mtu anapendeza,

mzuri, anatabasam. Mama yake alimuuliza mtoto wake "Nani

huyu? As-Sayyid Alimuashiria mama yake anyamaze. Walipo

rejea huko walikoshukia alimwambia mamake "Yule mtu

uliyemuona ni Mtume (S.A.W) mwenyewe kwani mahali pale

haingii mtu.

Alipomaliza ibada zake za hija na ziara aliingia Anzwani

pamoja na mama yake na ukhti yake wakakaa huko siku kadha

wa kadha yeye ndie wa mwanzo kuwapelekea Maulid ya

Barzanji alikuwa anapenda kuyasoma na kuyahudhuria kwa

taadhim na heshima kubwa alikuwa akikataza kucheka na

kucheza na kutafuna tambuu wakati wa kuyasoma kwa

kumuadhimisha mjumbe wa Mwenyi Ezi Mungu (S.A.W).

Baada ya hapo alirejea kwenye watani wake hali ya kuwa ni

3
mwenye kutizamwa kwa jicho la kusaidiwa na kutengenezewa

kutokana na bwana Muumbaji khalafu alisafiri kwenda Zanzibar

akakutana na Sheikh Uways na akachukua Tarika ya Qadiria

kutokana naye akarejea Ngazija baadaye akenda Nzwani wakati

huo anadhikri kwa Tarika ya Qadiriya wala hakumpa yeyote Ijaza

ya Tarika hiyo, bali baadhi ya nyakati alikuwa hujitenga faragha

akadhikiri peke yake baadae hurejea kwa wapenzi wake.

Aliporejea Ngazija haikuchukua muda mrefu ila alifika

Sheikh Abdallah Darwesh alikuwa kafuatana na ndugu yake

Sayyid Abdal Rahman Bin Sheikh na mama yake Sayyidat

Mwana Mkuu wakaja katika jahazi moja.

Sayyid alikutana na Sheikh Abdallah Darwesh alie

mchukulia amana na pakapatikana baina yao mahaba kwa

mtizamano wa mwanzo.

Hayo yalitokea kwa hekima ya Mwenye Ezi Mungu

aliyeumba akatengeneza kila jambo na vipawa vya kukusudiwa.

Sheikh Abdallah alitelemka kwenye kisiwa cha Ngazija

akaingia katika vingi katika vijiji vyake. Alipokuwa anazunguka

katika vijiji hivyo aliona katika baadhi ya njia zake ndege wawili,

mmoja akatoa ubait huu:

شرتث شراب السر مه خمر الصفاء

Wapili nae akatoa ubait huu:

فسكرت لو حقا ومالي منا زعا

Sheikh akaongeza juu ya ubait huu Abyat nyingine kama ilivyo

katika kasida ijulikanayo Ubait wa mwanzo wa qasida hiyo ni:

سقاء في سعاىاالحثية فلم ارى

سواه علي اال طالقا فىاكون المع

mpaka mwisho.

Baadae Sheikh Abdallah alifanya makazi mahali alipozaliwa.

Itsandaa mjini (Huko ndiko alipozaliwa mrithi wa Ahwal za

Mawalii na Maqamat yao Seyyidna Al-Habib Omar Bin Ahmad

Bin Sumeit رضوان هللا عايو na baba yake alizaliwa huko huko,

babu yake Al-Habib Abubakar ndiye aliyetoka Shibam

Hadhramaut kuja Ngazija- Mfasiri).

Huko kwao Itsandaa Sheikh Abdallah alifungua chuo

cha kusomesha watoto kur-an tukufu na baadhi ya vyuo vidogo

vidogo. Baadhi ya watoto walikua wakikhitimu kuran takatifu

kwa muda wa chini ya miezi sita kwa baraka zake hata wengi

4
katika watu wa Moroni waliwapeleka watoto wao ili

awasomeshe vile vile alifungua Daira ya Dhikri huko aliwapa

watu ijaza katika Tarika ya Shadhili – Yashrutii khabari ilifika

Moroni Bwana wangu (anakusudia Al Ma`aruf ) akakusudia

Itsandaa kwa kutaka Ijaza akapewa Ijaza na Ukhalifa katika

Tarika Shadhiliyya Yashrutyya. Sanad yake katika Tarika

(NjiaTarika iliyomfikilia kutokana na Mtume (S.A.W) Alichukua

Tarika kutokana na Abu Saith Arif Billah (amjuaye Mungu)

Sheikh Abdallah Bin Said ajulikanae kwa jina la Darwesh yeye

huyu akapokea kutokana na Ustadh mkamilifu kabisa Sayyid Ali

Al-Yashruti (Bwana huyu alitoka Afrika ya kaskazini akaja Akka

katika Flastin akafanya makazi Sheikh Abdalllah Darweshi katika

mzunguko wake kumtafuta Khutbu Al –Ghawth alifika huka

Akka, akakaa chini na Sayyidina Ali Al-Yashruti kwa miaka hata

akapata Al Fat-hu Al Akbar. Akapewa ruhusa arejee Ngazija

kama wasita baina ya Sayyidina Ali na Sayyidina Al Ma`aruf,

yeye Sheikh Abdallah Darwesh alipompa Al Ma`aruf amana yake

alimwambia “Hii kazi yenu nyinyi Ahl- Bait Rasulillah. Mfasiri).

Yeye Sayyidina Ali Al-Yashruti alipokea kwa khutbu wa zama

zake As Sayyid Muhammed Bin Hamza Dhafir Al-Madani

kutokana na Sharif Al Husainy baba yake Ahmad Al Arab

Addarqawi kutokana na Ali Al-Imran kutokana na Al Arab Bin

Ahmad Bin Abdallah kutokana na baba yake Ahmad Bin

Abdallah kutokana na Qassim Al Khassas kutokana na Abdul

Rahman Al fasi kutokana na Muhammed Bin Abdallah Al Kabir

baba yake Sayyidina Ahmad na wao wote wawili kutokana na

Yusuf Al Fasi kutokana na Abdul Rahman Al Majdhub kutokana

na Ali As-Sanhaji, kutokana na Ahmad Zarruq (Bwan huyu ni

katika nguzo kubwa kabisa za Silsila hii alikusanya kila namna za

elimu hata Falsafa, Mantiq (Logic) Sayansi na Mathematic.

Kasema maneno makubwa makubwa kama alivyosema Sultan Al

Awliyaa Seyyidina Abdul Qadir Jailan- Mfasiri)

Zarruq alikuwa khalifa wa Ahmad Bin Uqba Al

Hadhrami bwana huyu alilelewa Tarim Hadharamawt na

Seyyidna Abdallah Bin Abubakar Al-Aidarus akafikilia daraja

kuwa katika Uwalii Mwenyi Enzi Mungu akamchagua awe

mmoja katika Mqutbu wa Silsila hii ya Shadhili akampeleka

Misri akalazimiya na Yahya Al-Qadiri alipofariki huyo alirithiwa

na Al Hadhrami –Mfasiri).

5.
Yahya Al-Qadiria alipokea Ali Wafaa na yeye aliwapokea

kutokana na baba yake Bahr Safa kutokana na Daud Al-Bakhili

kutokana na Ahmad Bin Attaillah Assakandari kutokana Abi Al-

Abbas Al Mursi (Huyu kaitwa Al Mursi kwa sababu alizaliwa

Mercia, Spain wakati Spain ilikuwa ya kiislam baada ya waislamu

kukaa huko kwa miaka wakatia misingi ya kila namna ya masomo

na ustaarab huko ulaya. Al-Mursi alikuwa anakwenda kuhiji Jahazi

ilivunjika wakazama watu wote akaokotwa hapo alipokuwa Qutba

mkubwa kabisa Sayyidina Abdul Hassan Ash-Shadhili alimlazimu

bwana huyu hata akawa yeye ndiye khalifa wake mkubwa kabisa -

Mfasiri).

Seyyidina Al-Imam Abdul Hassan alimrithi Abdu

Ssalaam Bin Mashish na yeye alipokea kwa Abdulrahman Al

Madani Azzayyat kutokana na Taqiyyuddin Al Fuqayyir kutokana

na Al Qutb Fakhruddin kutokana na Qutb Nuruddin Abdul Hassan

kutokana na Al Qutb Tajuddin kutokana Al Qutb Shamsuddin

Assiwasi kutokana na Al Qutb Zainuddin Al Qazwimi kutokana na

Al Qutb Abi Is-Haq Ibrahim Ali Bisry kutokana na Al Qutb Abu

Qassim Ahmad Al Marwany kutokana na Qutb Abu Muhammed

Said kutokana na Al Qutb Saad kutokana na Al Qutb Fathu Suud

kutokana na Al Qutb Said Al Qazzani kutokana na Al Qutb Abi

Muhammed Jabir kutokana na Qutb wa mwanzo Sayyiduna Al

Hassan kutokana na baba yake Sayyidina Ali Bin Abi Twalib na

yeye kapokea kwa Bwana wa mwanzo na wa mwisho Bwana wetu

Muhammed S.A.W. Hapa Silsila imemalizika.

Sheikh Abdallah alimwambia Al Maaruf "Chukueni kazi

yenu hii nyinyi Ahl Bait Rasulillah. Sisi ni watumishi wenu katika

kazi hii".

Al Maaruf alipopewa ukhalifa alirejea Moroni akasimamisha

Daira na akawa anawapa watu Ijaza wakakusanyika kwake watu

namna nyingi Sheikh Abdallah alikuwa huja Moroni na

kuhudhuria Daira pamoja naye hata bwana wangu (Siri yake

imetakaswa alimchukua Sheikh Abdallah nyumbani kwake ili

awape Ijaza watu wa huko nyumbani Sheikh Abdallah akampa

ijaza mama yake Assayid na ndugu zake wanawake Sayyidat

Alawiyyah, Sayyidat Batul, Sayyidat Fatuma na Sayyidat Ihsan

ndugu zake baba mmoja mama mmoja aliendelea Sheikh

Abdallah kwenda Moroni na kurudi Itsandaa.

6
Siku moja alipikiwa chakula Moroni, akasema: "Mwenye

kula chakula hiki ataingia peponi, na mwenye kukila kwa nia

yoyote atapata muradi wake". Akachukua kila mmoja katika

walio kuwepo tonge tonge akawachukulia watu wa nyumbani.

Palikuwa na mwanamke Tasa akala kwa nia Mwenyi Ezi Mungu

ampe mtoto na Mungu akampa na hekaya hii inajulikana

Ngazijah na imeenea kwenye watu wa huko.

Baadaye alimpelekea Assayyid khabari asafiri

aende Hinzwani Sayyid akamjibu kuwa, "hapana marikebu

inayokwenda huko". Akamjibu "Andaeni safari kwani nyinyi

mtasafiri kesho inshaallah". Wala hapakuwa merikebu pwani

ilipokuja siku aliyowaambia kuwa safari yao itakuwa, alisikia

mjini kuwa pamedhihiri jahazi ya matanga pwani lakini jahazi

hiyo haikusogea mjini watu walitoka kuiangalia wakaikuta kama

ilivyosemwa. Paliteremshwa Ngalawa kutoka Jahazini

wakateremka baadhi ya waliokuwa na katika wao alikuwa

mwenye Jahazi, Muhammed Bin Silim yeye alikua ana mke na

marafiki Moroni ilipita kuwazuru tu. Assayyid alimuuliza

mnaendea wapi? " akajibu Muwali" akasema "Sisi tunataka

kusafiri pamoja na nyinyi" Jawabu ilikuwa kwa mapenzi na

Ukarim akasafiri siku hiyo pamoja na Sheikh Abdallah Ali fundi

na Ahmad Bin Nakhodha hata wakafika Muwali wakateremka

baadae walisafiri kwenda Hinzwani katika Jahazi nyingineyo

wakateremka Bamoni wakapita njia ya barabara hata wakifika

Mtsamudu. Siku hiyo ilikuwa Ijumaa Mwezi 24 mfungo Tisa

mwaka 1299 Hijriyya walipofika hapo alikutana na Ssayyid

Ahmad Al-Kabir Muhammed Al Arab na Muhammed Abood na

Abdu-Rab na wote wakawa katika Muridi wa Kishadhili.

Baadaye Sayyid alijiweka kuwapa Ijaza kila alietaka wakachukua

Ijaza kutokana naye watu namna nyingi, alikuwa husimamisha

Daira msikiti wa Ijumaa kila usiku baada ya sala ya Isha. Watu

wa msikitini walimwambia: "Ungeligura ukenda mahali pengine

ingelikuwa bora kwani sisi tunashawishika ikisimamishwa Daira

hapa na sisi tuna nyiradi hatuwezi kuzisoma". Kwa hiyo alihamia

Masjid Ar-rhmani hakuwa akisimamisha Daira msikiti wa

Ijumaa ila baada ya sala ya Ijumaa na sikukuu zote mbili.

Baadae alielekea Wani ili kutoa Ijaza akakaa huko kiasi ya

wiki walichukua Ijaza kwake aghlabu ya watu wa huko akampa

Sheikh Muhammed Bin Abubakar Ukhalifa juu yao.

7
Alirejea tena Mtsamudu, lakini hakukaa hapo mda mrefu

akatakiwa kwenda Bombo akaenda pamoja na baadhi ya Muridi,

akakaa huko siku kadha wa kadha aliwapa Ijaza huko watu wengi

akafanya khalifa juu yao Sayyid Jaafar baadae alirejea Mtsamudu

akadumu katika Masjid Ar hmani katika kumtaja Rabbu wake.

Hakuwa akienda msikiti wa Ijumaa ila siku ya Ijumaa.

Kupingwa na Sheikh Fadhil na Jawabu ya Sayyid na

yaliyopita baina yao kwa ufupi.

(Mungu awalie Radhi wote wawili na atunufaishe kwa wote)

katika muda huu Sheikh Fadhili alimpinga Sayyid katika

kuwapa Ijaza ya Tarika watu wa Hunzuwani pamoja na kuwa

wao si Ahli kama alivyodai yeye hali ya kutoa Dalili kwa hadithi

"Msiwape hekima wasiostahiki msije mkadhulumu" na katika

hadithi nyingine au utimilifu wa hii au hadith khutba na mimi

ndie Mufti wa Sawahil yote tangu Ras hafun mpaka Ras torfi na

mimi nimezuia dhikri juu yenu au kuisoma mbele yangu. Seyyid

alisimama akasema "Huna njia ya kuzuia dhikri", wakati huo

zogo lilizuka kwa wingi msikitini watu walisimama na kelele

zikaja juu. Kila mmoja akakamata silaha yake, Sayyid nae

alinyanyua upanga wake Sayyid Abdallah Bin Sheikh alitoa nje

upanga wake Sayyid Abdallah Bin Omar Khajar lake akelekea

kwa Sayyid Abdallah Bin Omar aliyeitwa Abood Bin

Muhammad Bin Omar, mtoto wa nduguye Abdallah Bin Omar ni

katika Muridi wa Sayyid. Hapo hapo alimpiga kofi Ami yake

kwa sababu ya wivu juu ya Sheikh wake hivi ndo anavyokuwa

Muridi. Sultan Abdallah alikuwapo msikitini askari wake

wakamzunguka Sayyid akatoka nje ya msikiti akanadi anaetaka

Ijaza na ahudhurie wakahudhuria mbele yake wengi na yeye

pamoja waliokua pamoja naye wanataka jina la Mwenyi Ezi

Mungu. Baadae alitoa sauti akatoa nje upanga wake mbele ya

Sultan Abdallah. Askari walipoona upanga walikimbia, Sayyid

alimshika Sultan mkono akamwambia: "Sema Allah" akawa

anasema pamoja naye wakafuatana nyumbani na waliokuwapo

waliwafuata na wote wanataja jina tukufu mpaka Sultan akaingia

nyumbani kwake.

Assayyid alielekea Mirontsi na kikundi katika Muridi wake

walimfuata lakini hawakufika pamoja naye kwenye msikiti wa

8.
Mironts ila watu kumi katika hao ni nduguye Sayyid Ali.

Hapakupita ila dakika chache mara ukawafikia mwito

kutokana na askari wa Sultan Abdallah, waliokuwa

wamemzunguka wakamwambia amnilikie Sultan, yeye akajibu

" Ndivyo" .Alipotoka Msikitini wale askari walitaka kuchukua

upanga wake na yeye akajizuia. Nduguye Sayyid Ali

akamwambia: "Hii ni amri ya Sultan anahitajia tuitii". Hapo

akawapa upanga baadae alichukuliwa pamoja na aliokua nao

kutoka Morots na huko wanapigwa na kutolewa maneno na

msukumo mkubwa hata mwisho Sayyid alitupwa baharini

akatupiwa mawe. Baharini palikuwa Jahazi ya baadhi ya wahindi

Sayyid alipanda akabaki humo siku saba baadae akasafiri pamoja

nao mpaka Nusbee.

Ijumaa ya mwanzo baada ya vituko hivyo walikuja

watu wake kutoka Bambao na katika hao ni Sayyid Jaafar na

Sayyid Salim Bin Sultan Abdallah wakamkuta kesha safiri

wakahudhuria Sala na wakasimamisha Daira. Waliapa kuwa

ataewaingilia watamuuwa. Hapana aliewaingilia., Daira ilidumu

kama ilivyokuwa katika Masjid Ar rahmani kila Ijumaa na

sikukuu mbili ilikuwa ikisimamishwa Msikiti wa Ijumaa.

Sayyid alirejea kutoka Nusbee akateremka Maote

alimuamrisha Sayyid Ahmad Bin Abdulrahman na Abood Bin

Muhammad warejee Hinzwan na yeye mwenyewe alielekea

Ngazijah pamoja na nduguye Sayyid Ali na Muhammad Al arab.

Alipofika Ngazijah alipokelewa na Sheikh Abdallah Darwesh na

alikuwa pamoja nae kwa namna iliokuwa njema kabisa kuliko

walivyopata kuwa.

Baadae alimpeleka nduguye Hinzwani ili afanye

upya mfungano wao na Tarika akampa Ijaza. Yeye alikaa

Hinzwani miezi. Siku yane na ya tano ya kufika kwake Hinzwani

alifariki Sheikh Fadhil ( Mungu amrehemu). (Sayyid alitoa amri

asomewe wadhifa aombewe dua. Haya yanaonyesha kuwa Sheikh

Fadhil hakumpinga Sayyid kwa inadi bali jitihada. Alijitahidi

akakosana, na Sayyid akamuombea Dua aghufuriwe - Mfasiri)

Sayyid Ali alirejea Ngazija akamkuta Sheikh Abdallah

Darwesh kasafiri kwenda Zanzibar baada ya kufariki Sayyidat

Alawiyya. Bibi huyo alikuwa na cheo kikubwa kwa Bwana ambae

maisha yake yanaandikwa. Hapa mauti yalipomhudhuria alikuwa

anataja jina tukufu la Mwenyi Ezi Mungu. Sayyid alimwambia:

"Msalie Mtume" Bibi alijibu "Huyu hapa Mjumbe

9
wa Mwenyi Ezi Mungu ananiamrisha nitaje Ismul-Jalala".

Sayyidat Alawiyya huyu ndiye ambaye Sheikh Abdallah

Darwesh alisema katika kumtaja kumpa cheo chake:

"Wangegawika Muridi mimi ningekuwa pamoja na kikundi

alichomo Sayyidati Alawiyya".

Katika siku hizo alikwenda Sayyid kwenye Bustani ya

mama yake ijulikanayo kwa jina la Buzini akakaa huko siku

nyingi awemo ndani ya Khalwa (Muepukano na kila kitu kwa

kushughulika na Mwenyi Ezi Mungu) Hapo ilimjilia kwa daraja

kubwa hali wapatao Mawalii wakubwa ilirejea nayo Mironi

akaingia nyumbani kwa Sheikh Abdallah Bin Himid, akabaki

pamoja naye huko siku tatu bila ya kuingia huko nyumba yoyote.

Baada ya hapo alitoka Sheikh Abdallah Bin Himid

na Sayyid akapanda juu ya sakafu ya nyumba akafika ukingoni

akaanguka, nduguye Sayyid alimchukua mpaka nyumbani kwa

mama yake akabaki nyumbani kiasi ya miezi sita na Ahwal zake

zikizidi hatuwezi kukisia aliyoyapata katika yajayo kutoka na

Mwenyi Ezi Mungu pamoja na yanayoteremka na miminio

alipokuwa katika hali hiyo mara yumo ndani ya صحو mara

nyingine محو pengine huwa عينةkatika na pengine katika

(Maneno haya hayafasirika kwani ni Istilahi za Mabwana حضو ر

Masufi. Hayana maana ya lugha wenyewe wanatambua kwa

Dhawq. Kuyaonja na ekspiriense. - Mfasiri). Aliendelea hata

akapata ambayo hatwezi kuyatambua vilivyo na tunahemewa na

kudiriki hakika yake.

Jadhba hii ni mash-hur Ngazija kwa Muridi wote. Yeye

Sayyid alisema wakati katika Jadhba yake "Mimi ni kitu Azizi

mimi ni kitu kilichotokana na Mtume (S.A.W) na ni hasha

Mtume kumpa baba yangu kitu kidhalilifu". Alisema:

(Mwenyi Ezi Mungu atunufaishe kwa baraka zake ) "Ingekuwa

bahari ni wino na miti kalamu ili kudhibiti niliyoyaona

bahari ingekwisha na miti ingemalizika kabla ya kumalizika

mambo niliyoyaona katika Jadhba yangu hii".

Baada ya hapo alirejea kukaa na watu kama ada yake ya

mwanzo akasafiri kwenda Hinzwani akateremka Mtsamudu.

Sultan Abdallah alikuwa Bambao alimtaka Sayyid aende huko na

yeye akenda pamoja na baadhi ya Muridi. Sultan Abdallah

akampokea kwa taadhima na mtukuzo, na yeye alikuwa

akijihisabu kuwa ni katika jumla ya Muridu. Katika baadhi ya

10.
siku alimwonyesha mkono Sayyid kwa kutaka kumpa

mapesa. Sayyid alisema: "Nimepokea zawadi yako, lakini

sasa sina haja ya kitu basi kaa nayo mpaka wakati wa haja".

Baadae alifika Sheikh Abdallah bin Himid kutoka

Ngazija akakutana na Sayyid akampa khabari ya kifo cha

Sayyidat Fatuma Bint Sheikh Ahmad. Ukhti yake Sayyid

baba mmoja mama mmoja, alimuomba arejee Ngazija.

akakubali akasafiri pamoja. Hii ndio safari ya mwisho ya

Hinzwani hakurejea tena.

Baada ya kufika Ngazija, watu wa huko walikhtalifiana

na mfalme wao Sultan Sayyid Ali Bin Sultan Sayyid Omar

Al-Masily walimtaka Sayyid awe pamoja nao na

walimkhubiri kuwa watamuuzulu Sayyid Ali. Wakati huo

ada ilikurubia kutoa kabisa hukumu za sheria iliyo

tahirishwa jambo ambalo haridhii nalo Mwenyi Ezi Mungu

na Mjumbe wake. Sayyid mara nyingi alikuwa akiyataja

lakini hakumpata wa kunusuru sheria kwa hiyo alipotakiwa

awe pamoja na alietaka kumuuzulu Sultan Sayyid Ali,

waliomtaka walimpa miadi madhubuti kuwa watabatilisha

ada yenye kwenda kinyume na sheria, watasimamisha

sheria imara. Aliwakubalia na ikawa sababu kubwa ya

kusalimika Sulatn Sayyid Ali nafsi yake kwani wale

waliotaka kumuuzulu, walikusudia kumuua, lakini Sayyid

hakuwaachia bali alibaki anawarairai na anawachukua kwa

upole na kuwalainishia maneno kwa kumuonea huruma

mtoto wa ndugu mama yake (Hakika ya mambo alihisi

kuwa kisharia hakustahiki kuuliwa. Ingelikuwa sii hivyo

angeliwaachia wakamuua kwani yeye ni wa mbele katika

ambao hawatizami mhusiano mbele ya sheria ya Mungu -

Mfasiri).

Azma ya kumuuzulu iliposhika nguvu walimuamrisha

khatibu asimtaje katika khutba ya Aljumua na yeye alukhutubu

pasina kumuombea dua, ilipothibiti kwa Sultan Sayyid Ali kuwa

waliloliazimia na jambo la matatizo alisafiri kwa kujificha mpaka

Muali, na kutoka huko mpaka Maote akaifikishia dolla ya

kifaransa yaliyomfika. Dola ya kifaransa iliandalia marikebo

ikachukua idadi ya askari marekebo iliingia Ngazija ikateremsha

11.
askari ambao walitafuta baadhi ya watu wajulikanao

wakawachukua baadhi yao. Walimtafuta As-Sayyid lakini yeye

alijificha hawakuweza kutambua alipokuwa. Mitsamhuli

ilikuwapo jahazi inakwenda Zanzibar, Sayyid alipanda usiku

wakati ambao wanaomtafuta wameghafilika walipokuwa

hawakumpataSayyid, nchi kavu wazungu walipanda kwenye

jahazi ili watizame ikiwa hajajificha humo jahazini. Walipoingia

jahazini wakaanza kupekua, palivuma upepo mkali na mawimbi

yakachafuka, hapo hapo waliteremka bila ya kumuona, "Na wapi

jicho pofu litaona jua?" wakati huo mnyororo uliofungiwa jahazi

na nanga ulikatika na Jahazi ikaingia baharini matanga

yakapandishwa na jahazi ikatweka kuelekea Zanzibar.

Imewachukua Sayyid na Muridi wake wawili Ahmad

Nakhodha na Abdul-R-rabb jahazi ilipokuwa mbali na nchi kavu

Sayyid alisimama juu ya sitaha akababaika mmoja katika muridi

wake akasema: "Eeh bwana wangu, umejitokeza watu watakuua

iwe sababu ya sisi kuangamia", akajibu "Usihuzunike na sisi kwa

kupenda Mwenyi Ezi Mungu baada ya salat aljumaa tutaingia

Zanzibar. Safari yake ilikuwa jioni ya jumanne. Ikatokea vile vile

kama alivyosema kwani waliingia Zanzibar baada ya salat

aljumaa.

Aliishi Sayyid Unguja hata mpaka alipotolewa Sultan

Sayyid Ali Ngazija Dola ya kifaransa ndio iliyomtoa. Hapo

alirejea Ngazija na hakusafiri kamwe. Hakuondoka huko hata

Mwenyi Ezi Mungu akamchukua hali ya kuwa yeye Sayyid

karidhia na karidhiwa.

منا فيو رض هللا عنو

12.
Mtoto wa Al habbib Sayyeid Muhammed Al Ma`aruf aliyezaliwa

Zanzibar.

13.
Al habbib Sayyeid Muhammed Bin Sayyeid Alliy Al Ma`aruf.

15.
Mfasiri kwa Kiswahili mtoto wa ndugu yake Sayyeid Al Ma`aruf.

Al habbib Nassib Sayyeid Umar Bin Sayyeid Abdallah

Mwinyibaraka.

17
Khalifa wa mwanzo wa Majaalis-el ulaa – Mwinyi Baraka-

Uwesia – Qa-diriyya. Al Faqeer Sheikh Ahmad Bin Sheikh

Muhammed Msiha.

18
Vitabu vilivyokwishatoka ni:

*1. Maana halisi ya Imaan. (i) (1 st , 2nd & 3rd addition).

*2. Njia nyepesi ya kuijua nafsi yako.

*3. Njia nyepesi ya kujua kitu juu ya uongofu.

*4. Knowledge vision & ecstacy.

*5. Mwinyi Baraka katika ulimwengu wa kiislamu.

*6. Waislamu na Sayansi - Ulu-m.

*7. Kuhifadhi Burda.

*8. Maana halisi ya Imaan (ii).

*9. Muhammad SAW katika ulimwengu wa ghayb.

*10. Siri ya Balaa.

*11. El makhlouq (Viumbe)

*12. Njia nyepesi ya kujua juu ya uongofu. (2nd addition)

*13. Manaqib ya Al habbib Sayyeid Al Ma`aruf.

Vitabu ambavyo tunategemea kuvitoa muda si mrefu

(Insha Allah) ni:

*1. Waislamu na Sayansi - Ulu-m. (2nd addition)

*2. Njia nyepesi ya kuijua nafsi yako. (2nd addition).

*3. Mwinyi Baraka katika ulimwengu wa kiislamu ( 2nd. add).

*4. Njia nyepesi ya kujua kitu juu ya Uongofu.

*5. Some aspects of concepts of facility in medevial Islamic

Philosophy by Mwinyibaraka.

Kwa maulizo kuhusu vitabu wasiliana nasi:

Majaalis El Ulaa-MwinyiBaraka-Uwesia- El Qadiriyya Sinza,

P.o. Box 15170,

Tel: 0747483553

Tel: 0748595958.

Tel: 0744 023703.

Tel: 0741 235091.

Tel: 0744 299597.

Dar es salaam.