Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Siku moja alipikiwa chakula Moroni, akasema: "Mwenye

kula chakula hiki ataingia peponi, na mwenye kukila kwa nia

yoyote atapata muradi wake". Akachukua kila mmoja katika

walio kuwepo tonge tonge akawachukulia watu wa nyumbani.

Palikuwa na mwanamke Tasa akala kwa nia Mwenyi Ezi Mungu

ampe mtoto na Mungu akampa na hekaya hii inajulikana

Ngazijah na imeenea kwenye watu wa huko.

Baadaye alimpelekea Assayyid khabari asafiri

aende Hinzwani Sayyid akamjibu kuwa, "hapana marikebu

inayokwenda huko". Akamjibu "Andaeni safari kwani nyinyi

mtasafiri kesho inshaallah". Wala hapakuwa merikebu pwani

ilipokuja siku aliyowaambia kuwa safari yao itakuwa, alisikia

mjini kuwa pamedhihiri jahazi ya matanga pwani lakini jahazi

hiyo haikusogea mjini watu walitoka kuiangalia wakaikuta kama

ilivyosemwa. Paliteremshwa Ngalawa kutoka Jahazini

wakateremka baadhi ya waliokuwa na katika wao alikuwa

mwenye Jahazi, Muhammed Bin Silim yeye alikua ana mke na

marafiki Moroni ilipita kuwazuru tu. Assayyid alimuuliza

mnaendea wapi? " akajibu Muwali" akasema "Sisi tunataka

kusafiri pamoja na nyinyi" Jawabu ilikuwa kwa mapenzi na

Ukarim akasafiri siku hiyo pamoja na Sheikh Abdallah Ali fundi

na Ahmad Bin Nakhodha hata wakafika Muwali wakateremka

baadae walisafiri kwenda Hinzwani katika Jahazi nyingineyo

wakateremka Bamoni wakapita njia ya barabara hata wakifika

Mtsamudu. Siku hiyo ilikuwa Ijumaa Mwezi 24 mfungo Tisa

mwaka 1299 Hijriyya walipofika hapo alikutana na Ssayyid

Ahmad Al-Kabir Muhammed Al Arab na Muhammed Abood na

Abdu-Rab na wote wakawa katika Muridi wa Kishadhili.

Baadaye Sayyid alijiweka kuwapa Ijaza kila alietaka wakachukua

Ijaza kutokana naye watu namna nyingi, alikuwa husimamisha

Daira msikiti wa Ijumaa kila usiku baada ya sala ya Isha. Watu

wa msikitini walimwambia: "Ungeligura ukenda mahali pengine

ingelikuwa bora kwani sisi tunashawishika ikisimamishwa Daira

hapa na sisi tuna nyiradi hatuwezi kuzisoma". Kwa hiyo alihamia

Masjid Ar-rhmani hakuwa akisimamisha Daira msikiti wa

Ijumaa ila baada ya sala ya Ijumaa na sikukuu zote mbili.

Baadae alielekea Wani ili kutoa Ijaza akakaa huko kiasi ya

wiki walichukua Ijaza kwake aghlabu ya watu wa huko akampa

Sheikh Muhammed Bin Abubakar Ukhalifa juu yao.

7