12.07.2015 Views

Read - Al-Faqeer

Read - Al-Faqeer

Read - Al-Faqeer

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Zinaandama athari, kwa bwana mwenye ulumuAlieacha dahari, nyoyoni mwa wanaadamu.Jumla na Asrari, ziloondoa zidi hamu.Swala watu wa Salamu, Mpenzi Maulaya.Dhati ya nyoyoni mwetu, Mola anatufamu.Juu ya Mtume wetu, mwenye Badru tamamu.Kumpenda haki yetu, ilo kubwa Adhimu.Swala watu wasalamu, Mpenzi Maulaya.Rabi Sala zenye Huba, mfikizie Hashimu.Kadhaali na sahaba, pia wote Maimamu.Pasiwepo na hijabu, hapa mpaka kiyamu.Ndie Shafii Anamu, Mpanzi wa Maulauyaiii

No.1. Dibaji.2. Utangulizi.3. Imaani.Yaliyomo:Ukurasa.4. Undani wa Ngome ya Kwanza.5. Ufafanuzi juu ya Moyo.6. Ufafanuzi wa Roho.7. Ufafanuzi juu ya Nafsi.8. Nafsi, Roho, Moyo na Akili kuingia ndani ya kiwiliwili9. Majaribio katika Uhai.10. Mabadiliko ya Nafsi hadi kuungana na roho.11. Insaan.12. Kumalizika Mwili.13. Neema za Dunia na Neema za Akhera.14. Malipo ya Pepo kwa wapendanao Lillahi.15. Askari na Adui za Moyo.16. Mnyezi Mungu, Binadamu na Maumbile.17 Undani wa Kutekeleza Faradhi.18. Uislamu ndani ya Swala.19. Undani wa kutekeleza wajibati.iv.

Dibaji:Kitabu hiki kilichoandikwa na Mtoto wetu kimekusanyamengi yenye maana kubwa na ya msingi wa Kiislamu.Amejulisha Umoja wa Mwenyezi Mungu na Mapenzi yakejuu ya Mtume Muhammad Saw. Aya alizozitia katika kitabu hikizinathibitisha kuwa yeye Sayyidna Muhammad ni Mjumbe wamwisho kabisa wa pekee ambaye hapana njia yoyote nyingine yakumjua Mwenyezi Mungu, ya Kumtii na kujisogeza kwake ila yeyeMustafa, aliyechaguliwa.Ahmad amefanya vizuri kutaja baadhi yalolazimu juu yaUislamu na yaloharamishwa, na kuonyesha alama za kweli zaMuumini, katambulisha umuhimu wa kutengeneza Moyo, kwanivitendo vya viwili wili, ijapokuwa Muislamu hana budi navyo.Havitoshi ikiwa Moyo umeachiwa uwe Mchafu.Moyo ukiwa safi ndipo vitendo vitapokubaliwa, hapanashaka kuwa tabia njema ndio lengo la Dini ya Kiislam, na kitabuhiki kimewacha wazi hayo. Alhasili atayekisoma kwa Insaafu nakuzingatia atapata faida ni nyingi zilohusu Islamu, Imaani na Ihsan.Mwenyezi Mungu ambariki aliyekitungaOmar Abdallah.v.

Dibajivi.

Dibajivii.

“Bila shaka mnao mfano mwema (Ruwaza nzuri) kwaMtume wa Mwenyezi Mungu, kwa mwenyekumuogopa Mwenyezi Mungu na siku ya mwishona kumtaja Mwenyezi Mungu sana”.Qur an: At-Tawba:9:103.“Chukua Sadaka katika mali zao, uwasafishe kwaajili ya hizo (Sadaka zao) na kuwataja kwa vizuri(mbele yangu) – na Uwaombee Dua. Hakikakuwaombea kwako kutawapa utulivu(watengenekewe), na Mwenyezi Mungu ndiyeasikiaye na ajuaye”.Na jaha ya Bwana Mtume SAW pamoja na kutawassuli naekunaonekana wazi katika Ayah ii iliopo kwenye Juzuu ya tano:Qur an:Annisa: 4:64.“Na hatukumleta Mtume yeyote ila atiiwe kwa amriya Mwenyezi Mungu. Na lau wangalijuawalipojidhulumu nafsi zao (kwa kwenda kuhukumiwa,xi.

“Apendae hana dawa”.“Mwenye kupenda haoni”.“Sili silali nakuwaza wewe”.“Kufa afadhali kuliko kukukosa wewe”.Bila shaka ipo tofauti kubwa, lakini vipimo vya Imaani yakeMtu ina yeye mwenyewe mtu, kwani hakukosea MnyeziMungu kusema:Qur an: Al Qiyama:75:14.“Bali mtu ni shahidi juu ya Nafsi yake, ingawaanatoa nyuzuru zake za uongo”.Maana Halisi ya Imaani – ii, hatukuweza kuitoa pamojakatika kitabu cha kwanza kwa sababu ya uwezo wa kifedha hasakatika gharama za kupanga herufi (type setting) na gharama zakuchapisha kwa vile sahifa (pages) zilibidi ziwe nyingi ambapotulikua tushindwe. Lakini kwa uamuzi wa pamoja na washaurituliamua kutoa pole pole kwa kadiri ya uwezo wetu, na huenda piatukapunguza, ili tujaalie kuepo kitabu cha iii.Tumekwisha onyesha katika sehemu ilotangulia vipiImaani ilivyokusudiwa kuemo mwenye Ngome sita ambazo nimuhimu sana:1. Yaqini.2. Ikhla-s.3. Kutekeleza fardhi.4. Kuacha yaliyo haramishwa.5. kutekeleza wajibati na6. Kutekeleza Sunna.Na mwisho wa yote ni Kutekeleza Adabu. Katika Ngome 6ambazo Imaani imezungushiwa nazo, hii Ngome ya Saba, nayo nimuhimu kama zilivyo hizo sita.Bwana Mtume SAW ameonyesha sura ya Adabu katikaWajihi chungu nzima ndani ya maisha; na ni yenye kuonyesha wazikua bila ya Adabu, Imaani ya Mtu huenda ikawa dhaifu.xiv.

iv. Al Akh Sleiman Dodo na wale ambaowamesababisha kutoka kwa sura ya kitabuchenyewe kwa safari hii:v. Ahmed S. Bamgha.vi. Muhammad Adan – Hodhan International.vii. Ibrahim I. Juma.viii. Muhammad Is-Haq – Scandinavia Bus Service(kwa mara ya pili). Naix. Ahlil Majaalis El Qadiriyya wote kwa Jumlachini ya Ukhalifa wa Sheikh Aly MzeeComorian, na mwisho Sheikh Ally Said waAgip Dar es salaam kwa msaada wake wakuzichapisha Nuskha zetu.Wafaqana Llahu limaa yuhibbu wa-yardhwa.Mnyezi Mungu awanufaishe nacho kitabu hiki kila msomajiWasalla-Llahu wa salaam ala Seyyidna Muhammad wa alihi walhamdu-lillahiRabil Ala-meen.Wabillahit-Tawfeeq.Al Faqeer, Ahmed Sheikh,Majaalis El Ulaa El Qadiriyya,P. o. Box 15170.Dar es salaam.xvii.

IMAANI.Amesema Bwana Mtume Muhammad S.A.W:-“Al Insaan hadithun baada-hu fakun hadithan ahsanaliman-dha-a".“Mtu hua ni hadithi tu (mazungumzo) baada yake, (basi)kua hadithi nzuri kwa watakaoipiga baada yako."Bila shaka katika mazingatio ya kweli juu ya hadithi hii ni lazimaManeno: “Hadithi Baada yake” yatupatie upana wa maana zaidi ya viletunavyodhani katika daraja ya kawaida. Kwa kawaida na mazoea, neno:"Hadithi" tunalielewa kua ni masimulizi ya jambo au tukio lililopitaau linaloendelea. Ni sawa sawa ikiwa masimulizi yake ni mafupi, yakadri au marefu.Na neno "Baada yake" katika daraja la kawaida husema:"Ni nyuma yake mtu”, amma alikuwepo mahala, halafu aliondoka nakadhalika. Amma kuondoka, ni namna mbili:-1) kuondoka kwa safari fupi na ndefu, na kurudi.2) kuondoka safari ya moja kwa moja, na bila ya kurudi.Kuondoka kulikokusudiwa mno, ni kwa pili ambako kuna maanisha:"Kufa" na sio rahisi kurudi (labda kwa njia ya miujiza. kama alivyofanza Naby iIssa bin Maryam, zama alipofufua baadhi ya waliokwisha kufa, kwaidhini ya Mnyezi Mungu, wakarudia kwenye uhai mara ya pili, lau kwamuda mfupi). Neno hilo ukilitamka kwa sauti ya ndani yako iliujisikizishe wewe mwenyewe, "Kuufaa" huenda ukahisi kumilikimoja ya hali mbili hizi:1. Chuki: Yaani kama ambae hupendi, wala kupendelea kuiacha duniyana starehe zake, mambo ambayo yalikupumbaza kwa kila hali ya raha.hupendi kuachana na wapenzi maridhawa; watoto mali zako na mafedha uliorunuliyorundikisha - benki kwa muda mrefu.2. Woga: Unadhani labda huenda ukatokewa na kifo kweli pengine saahiyo hiyo, au punde kidogo hivi. katika hali hiyo unaanza kujiulizamasuala mengi mengi, mfano wa haya; "Vipi itakuwa hali yangu nikifa?,Ni amali gani ambazo nimeshazitanguliza huko niendako” (yaani akheraambako kwenye uhai wa milele?), na kadhalika.1.

Qur an: Luqman. 31:33.“Wala asikudanganyeni yule mdanganyifu mkubwa,(Iblisi) katika (mambo ya) Mwenyezi Mungu".Amesema msanifu mmoja wa kizungu:-“As we are in the midst of death we are in the nist of life”.“Kama vile tukiwa katikati ya mambo ya kifo ndivyo hapohapo tunavyokua kindibwa ndibwa katikati ya maisha".Amesema Al marhu-m Sheikh Hassan bin Ameir Ash-shirazi katikasherhe yake ya "Tabaraka dhul-ula" (hiyo mada-rijil-ullah) katikafasiri ya ubeti nambari 5-6, kua;“Ala ayyuhal maghruri ma lakatal- abu, tuammilua-ma -lan wa mawtuka aqrabu" ."Oh! ewe mdanganyika vipi kucheza kumekusibu umezipatamaa fika na mautiyo yako karibu"."Kam min mustaqbalin - la - yastakmilihu wamuntadhwirun - ghadan la yablughuhu walawnadhwartum ilal ajal wa masiriruhu - la –abghadhtumul amala wa ghururahu"."Wangapi siku waloifikia wala hawajaikamilisha na wangapiwalotegemea kufika kesho, haikuwafikisha na falau Ajalimwendoe mungeuangalia, basi tamaa na ghururi mngezichukia".Amesema Bwana Mtume S.A.W;-“Man ahabbad dunya adhwarrabi a-khiratuhu""Mwenye kuipenda dunia hudhuru akhera yake".Na pia amesema:-2.

“Hubbud duniya raas kullu khati-a""Kupenda dunia ni kichwa cha kila dhambi (makosa)".Na ma-damu unapenda dunia, basi lazima utakua na tamaa (Tulamal). Kuna msemo unaosema hivi:-"Tamaa mbele mauti nyuma"Mara nyingi watu hufikia kufa wakiwa wameacha mambomengi sana nyuma yao hayajamalizwa. (Man proposes, Godopposes). lakini wapi! mauti yakishawadia, hua hayamsaili mtu.humhujumu tu, yakaacha kiwiliwili nyuma yake kikililiwa. Daimatungekua watu wa kujiandaa na mauti lau tungetia maanani kauli yahakika kama hii, iliyofunuliwa katika:Qur an: Al-muna-fiqu-n. 63:11."…Lakini Mwenyezi Mungu hataighairisha Nafsi yeyoteinapokuja ajali yake; na Mwenyezi Mungu anazohabari za mnayoyatenda (yote)”.Pia Anasema:Qur an: A`araf. 7:34."Na kila watu wana muda wao (wa kuondoka ulimwenguniutakapofika muda wao huo, hawatakawia (hata) saa moja,wala hawatatangulia (kabla haujafika)”Na hatari zaidi ni kwamba hakuna ajuaye lini atakufa au wapi atafia.Kama alivyosema Mnyezi Mungu katika:Qur an: Luqma-n. 31:34."…..Na nafsi yeyote haijui ni nini itachuma kesho, walanafsi haijui itafia ardhi gani".3.

Qur an: Nisaa. 4: 78."Popote mlipo mauti yatakufikieni, na hata mkiwaKatika ngome madhubuti"."Out brief candle, life is but a walking shadow"."Uhi ni kama kivuli cha kupita tu, mshumaa mfupi,mara moja, hun`gaa kisha huo, haupo tena".Ghururi za dunia, mwisho wake hua kama hivyo kama mtuasipojirudi nafsi yake, ambayo haizeeki ikachakaa ikaonekana,lakini huzeeka kiwiliwil, mara ukawa huwezi tena; juu yakujikusuru kwako.kila siku mtu hujiona mtoto tu, shauri ya ghururi, basi usisubirimpaka ukafikia hali ile iloelezewa ndani ya:Qur an: Muuminun. 23:99."Hata yanapomfikia mmoja wao Mauti husema "Molawangu nirudishe (ulimwenguni)".Basi kama ni lazima (kwa mtu ) kuifwata dunia, basi nasaha yamaana juu yake, na iwe kama ile alioelezea Bwana Mtume S.AW:-"Mwenye kuitaka dunia basi juu yake awe na ilimu,na mwenye kuitaka akhera, juu yake awe na ilimu,na mwenye kutaka yalioko kati ya dunia na akherabasi juu yake awe na ilmu".Zipo na chungu ya hadithi mfano wa hiyo, juu ya dunia na mamboyake ya khadaa, bali tumefupisha tu. pia zipo beti zinazoelezeamwenye "Taba-ra ka dhul ulaa. Uk. 75” zinasema:-"Inna lil lahi iba-dan futwana tarkuud-dunya wakhaful fitana”.(Hakika Mnyezi Mungu Anao waja, wenye akili kweli kweli,4.

(ambao) wameiacha dunia kwa ajili ya kuchelea fitna yake)."Nadharuu fiha falamma alimu anna laysat lil hayyifi-hawatwa -nun".(Wameiangalia (na kuichunguza ) ndani yake, na pindiwalipojua, kwamba haimpi makazi (makao ya kudumu)yeyote (yule) alie hai)."Jaalu-ha luj-jatan wat-takhadhu swali-hal aamal fi-hasufunun".(Walijaalia kua ni kama wimbi la kupita (la bahari ) tu naWakafanza amali njema ndani yake ni kama meli (zakuwanusuru na gharka)".Ni mafanikio yalioje lau tungepatikana miongoni mwetu kwamaelfu elfu wa mfano huo!.Mweyezi Mungu hampendi mtu ambae hujifanyia mambo bilaujuzi, na hata kama amali yenyewe ni nzuri yenye thawabu kubwakweli mfano wa "Swala" basi haitatosha kitu.“Waman bighayri ilmin yaamalan Aama-luhu mardudatanlan taqbalan"(Na ambae bila ilmu yuwajifanyia tu (mambo yake )basi amalizake zote ni zenye kurudishwa hazitapokelewa hata kidogo).Na anaefanya amali kwa ujuzi basi Mola Sub-hana wa Taalahumpenda sana na angaa amali yenyewe ni chache.Tazama ninianasema Bwana Mtume S.A.W. juu ya jambo hilo:"Innal Laha Taala yuhibbu kullu man atqana bi amalihi".(Hakika Mnyezi Mungu alietukuka, humpenda kila ambaehuifanza amali yake vizuri sana (yaani kwa Ilimu).Katika hadithi hiyo pana hikaya ambayo, kwa thamani iwaa yeyotelazima tuipate kwani si yenye kutoka katika zungumzo letu - Wenyekuipenda dunia na kuchukia mauti - Hikaya yenyewe ni hii nainaanza hivi:-“Katika zama za Naby Mussa As palikuepo Mtaabad (yaani mchaMungu sana) aliekuwa akifanza ibada zake, kwa muda wa miaka 80nje ya mji, penye jabali. Hata pale alipokuwa akisujudu, palifanza5.

athali ya kishimo hasa. Kwa upande mwengine alikuwepo mlevi wakupindukia, hakua na amali nyengine yeyote zaidi ya pombe.Mtihani kati yao ulikuwa juu ya uwezo wa Mnyezi Mungu katikakumpitisha Ngamia mzima ndani ya tundu ya sindano (hii hainauhusiano wowote na aya 40 katika Suratil Aara-f ambapo MnyeziMungu anasifia juu ya roho za makafiri kua hazitapenya mbingunilabda hata atapopenya ngamia ndani ya tundu ya sindano. Aya hiyoilikua mbali na aya hii).Basi matokeo ya mtihani wao yalikua hivi: Yule mcha Mungukwa muda wa miaka 80 alizingazinga moyoni mwake akasema(nafsini mwake) "Amma Mitume hawasemi urongo, lakini!! Aa!! hiihabari ya kupitishwa ngamia mzima mzima ndani ya tundu yasindano!!!!. Amma kwa yule mlevi ilikuwa hivi: Mara baada yakuelezwa kisa kile, yeye alijibu kwa kutaassaf na kuhuzunika:"Yaani kalimal lah (ewe mwenye kusemezana na Mnyezi Mungu)Mnyezi Mungu ni muweza wa kuipitisha dunia nzima ndani yatundu ya sindano, nini ngamia katika ukubwa?".Na kwa upande wa pili wa zile hisia mbili ziwezazo kuta-atharikutokana na kujiuliza mtu juu ya KUFA - ikiwa utapata woga maratu baada ya kujisikizisha binafsi yako, basi itaonyesha wazi kua ikotamaa kwako kurejea kwa Mola wako na kuiacha dunia na ghururizake, kwani hiyo ni dalili ya kuipa nyongo. Bwana Mtume S.A.Wamesema:“Iz- had fid - dunya yuhbibkal llah""Ipe nyongo dunia atakupenda Mnyezi Mungu"."waz - had ma - fin nas yuhbibkan - na-s"."Na yape nyongo yalo na watu watakupenda watu".Na hii huenda ikawa ni kumbusho kwako, toka kwa Mola wakobasi, fanza haraka kwani, huenda hiyo ikawa ndo nafasi yako yapekee na sio rahisi kwa nafasi kumjia mtu mara mbili (opportunitynever comes twice and misfortune never comes single).Kwa yote hayo, yafikirie mauti vipi yanavyomuhujumu mtu,iweje wewe kughafilika nayo?Bwana Mtume SAW anasema:“Hayakumbuki mtu mauti illa atazidisha mambomema, na atapunguza maasi”Kwa hivyo, kwa muumini kuyakumbuka mauti ni ibada kubwa sana.6.

Na ambae anajitia hamnazo, akidhani kua atayakwepa auatayakimbia, basi Mnyezi Mungu anatwambia na kutukumbushakatika:Qur an: Suratil Juma - a: 62:8.“Sema: Hakika mauti haya mnayoyakikimbia bilashaka yatakutana nanyi kisha mtarudishwa kwamjuzi wa siri na dhahiri hapo atakujulisheni yotemliyokuwa mkiyatenda”.Basi katika aya ambazo ni za kumkatisha tamaa yule adhaniaekua atadumu hapo duniani kwa ujanja wake akifaulu kuyakimbiamauti ni hayo na juu ya hivyo Mnyezi Mungu hapendi desturi yakukata tamaa kwani hiyo ni tabia ya makafiri. yeye humpendeleamja wake matumaini ya hakika. kwa hivyo Bwana Mtume SAWametufundisha njia nzuri ya kuishi nayo ni kama hii; njia nzuri yakuishi kwa sababu dunia inatubidi na akhera pia inatubidi ni hii:“Jishughulishe na dunia kama kwamba utaishi milelena ujishughulishe na akhera kama kwamba utakufakesho”.Na vile vile amesema:“Hakua mbora wenu ambae anaacha dunia kwa ajili yaakhera yake, wala yule mwenye kuacha akhera kwaajili ya dunia yake, bali mbora wenu ni yule mwenyekushikamana na vyote hivyo kwani dunia ndio kiwasilishocha akhera’’.7.

UNDANI WA NGOME YA KWANZA.Yaqini:Qur an: Waqia: 56:81 – 96.“Je! Mnabeza hadithi hii? (Mnayapuuza yaliyokatika kitabu hiki?)”.“Na mnafanya kuikadhibisha ndiyo (shukrani ya)pato lenu (alilokuruzukuni?)”“Basi mbona (roho) ifikapo kooni, na nyinyi wakatiule mnatizama”.“Nasi tunakaribiana naye zaidi (huyo anayetoka raho)kuliko nyinyi, wala nyinyi hamuoni. Kama nyinyihamuoni katika mamlaka (yangu)”8.

“Kwa nini hamuirudishi (hiyo Roho) ikiwa mnasemakweli (kua hamumo katika mamlaka yangu)”.“Basi akiwa (mtu huyo anayekufa) ni miungoni mwawale walio karibishwa (na Mnyezi Mungu) basi niraha (kubwa) na manukato (mazuri) na mabustaniyenye neema (zinamngojea)”.“Na kama akiwa ni miungoni mwa watu wa kheri.Basi ataambiwa. Ni salama kwako (daima) (uliye)miungoni mwa watu wa kheri”.“Na kama akiwa ni miungoni mwa waliokadhibisha,wapotofu (wapotevu), basi karamu (yake) ni majiya moto yachemkayo na kuwaka motoni”.“Bila shaka hii ndiyo haki yenye yakin (yaqini) Basilitukuze jina la Mola wako mwenye Utukufu”.Tumeanza kufahamisha undani wa Yakini (Yaqini) kwakunasibisha hakika yake kwa kuopoa baadhi ya aya ziliopo mwishowa Suratil Waqiah (56) katika fungu la Qur an, kuanzia aya ya 81hadi 96, ambazo zina utajo mzuri juu ya neno hilo – Yaqini – Ziposehemu, nyinginewe ndani ya kitabu hicho ambako pia, limetajwa sihasha.Kwa upande mwingine Yakini (Yaqini) hua na maana ya kifohakika yake imeelezewa mwisho wa Sura Al-Hijr 15: 99. paleinaposema.9.

Kwa vile kuna mkusanyiko wa mawazo mabaya, Chuki,Mapenzi, Husda, Tamaa na Unyimi, Ubakhili na kadhalika Sukhaa,na Ndimo alimoweka Imaani, Yeye Mnyezi Mungu. Jumla yamambo yote hayo yamo ndani ya Moyo, na takriban yote ni maalumukwako, hakuna lililo geni kwako hata moja. Lakini hebu jiulize Nafsiyako katika Aya mbili hizi zifwatazo, ili ujitazame kama dai lakokatika kuyajua mambo yote tuliyochambua hapo nyuma, ni kweli aubabaisha tu?.Qur an: Ar-Rahman: 55:14.“Amemuumba Mtu kwa udongo wa Mfinyanzi(Utoao sauti) kama vyombo vya udongo”.Qur an: Suratil Twa-riq: 86:5 – 7.“Hebu na ajitazame Mtu ameumbwa kwa kitu gani?Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa (Yatokayokatikati ya mifupa ya mgongo na kifua”.Ufumbuzi: Ikiwa jawabu lako ni kutokana na aya ya kwanza, basibado kujijua Nafsi yako, na ikiwa jibu lako ni kutokana na aya ya pili,basi maana ni sawa.Kwa nini iwe hivyo? Kwa sababu, Mtu ambaye ametajwa katikaaya ya awali Ni baba yetu Naby Adam Asw, ambaye ndiye pekeewa kwanza kuumbwa moja kwa moja, (Directly). kutokana naudongo.Wa pili, kufuatia alikuwa mkewe, ambaye katika masalia yaudongo ule ule aliumbwa yeye (Mama Hawwa). Na wa tatu, lakinikatika njia ambayo iliwashangaza watu tangu siku hizo hadi leo, niNaby Isa As ambaye Mnyezi Mungu Muumba alitwambia jinsialivyowaumba wote wawili ni mfumo mmoja tu:Qur an: A`al Imran: 3:59.11.

“Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu nikama hali ya Adam: Alimuumba kwa udongokisha akamwambia “kuwa” basi “Akawa”.Lakini: Waliobaki wote (katika jamii ya Mtu) ni walioumbwakutokana na maajabu ya Aya ya pili - “Tumeumbwa kwa majiyatokayo kwa kuchupa” (yakitoka bila mchupo pana mashaka kuwani yenyewe, au kuwa ni mazima) – Bila ya shaka yeyote hayo nimanii ( Mbegu ya uzazi).Wana Sayansi wamechunguza na kugundua ndani ya hiyombegu ya uzazi wako wadudu wa uhai - Waitwao Amoeba(Amiba) ambao hawana umbo maalumu, kwa hivyo siyo rahisikuchoreka. Vidudu hivyo visivyoweza kuonekana kwa machomatupu ni vyenye kubadilika umbo hadi umbo kila dakika hukuvikiongezeka idadi yake mpaka kufikia kujenga umbo kamili.Qur an: Al Muminuun: 23:13 - 14.“Kisha tukamuumba kwa tone la manii (mbeguya uzazi) lililowekwa katika makao yaliyohifadhikakisha tukalifanya tone hilo kuwa pande ladamu……….”Upo ushahidi mzuri wa kuweka mkazo juu ya hakika hiyondani ya:Qur an: Al-furqa-n:25 : 54.12.

"Naye ndie aliyemuumba Mwanadamu kwa maji, kishaakamfanyia nasabu (ya damu) na ujamaa wa ndoa,Na Mola wako ni mwenye uwezo (wa kila jambo)".Basi, ukizingatia ufafanuzi mfupi kama huu kuhusu majibu yakokatika aya mbili hizo:"Ameumba mtu kwa udongo wa ufinyazi (utoaosauti) kama vyombo vya udongo". (Ar-Rahman 55:14).Na"Hebu na ajitazame Mtu ameumbwa kwa kitugani? ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,yatokayo katikati ya mifupi ya mgongona kifua”. (Twa-riq: 86: 5-7)Hutakosa, kuona ya kwamba kwa njia moja (direct) au nyengine(indirect) vijidudu hivyo (amoeba) ambavyo hupatikana:a. Mwenye Udongo wa maziwa ya maji, nab. Mwenye manii (mbegu ya uzazi) ni vyenye kuingia huku(kwenye umbo la mtu wa kwanza) na huku (kwenye umbo la mtuwa pili mfano wako wewe na mimi). Kiasi ambacho mwenye akilihawezi kupata taabu ya kusarifu mambo ya ajabu ya muumba:ambayo yametapakaa mno, sio kwetu tu (kama alivyosema MnyeziMungu katika:Qur an: Suratil Rom: 30 : 20."Na katika ishara zake za kuonyesha uwezo wakeni huku kukuumbeni kwa udongo, kisha mumekuwawatu mnaonea (kila mahala)”.Na kama vile ilivyo kwenye:Qur an: Dh-dha riyat: 51 : 21.13.

"Na katika nafsi zenu (pia zimo alama yaanizenye maajabu ya mambo ) je hamuoni?".Bali ajabu hizo zimetapakaa kila mahali katika ujudi, mfanowa Mbingu, Sayari, Upepo, Hewa, Milima ambayo utadhaniimesimama, lakini ni yenye kuzunguka na hali kadhalika. Nayote hayo yalomuhusu Mtu na mtoto mtu, yamo ndani yakichambuliwa, Moyo jee haikustajabishi? Katika undani wayakini (yaqini) Moyo ni chombo muhimu chenye kuendeshauhai na maslahi ya maisha yetu hapa ulimwenguni na ndomaana Bwana Mtume SAW akasema kwa mkazo sana juuyake;"...Likitengemaa kimetengemaa kiwiliwili kizima.....”KUWEMO NDANI YA KICHAMBUO - MOYO:kumbuka tena kwa mazingatio ya hali juu kabbisa sio vileulivyozoea tu, laa, haitoshi kwani suala hilo ni lenye kukuhusuwewe suala, hilo ni la kukutayarisha wewe kuipokea na kuisarifuvile ipasavyo - Amana (Toka kwa Mnyezi Mungu - ukiwa niMuislam au si Muislam). Basi pengine huenda baada ya kwisha patafununu yake ukaona ya kua ulipoteza muda mrefu ukijifanyiamambo ambayo sivyo kabbisa, Huenda wewe mwenyewe ukatwaauamuzi mpya kuanza upya.Na tuanze na Aya ifuatayo ambayo iko katika:Qur an: Suratul Fus-swilat: 41 : 53.1. "Tutawaonyesha (ukweli wa) maneno yetu haya katikanchi za mbali, na katika nafsi zao wenyewe mpakaiwabainike kwamba haya ni kweli. je! Haitoshi kwa14.

4. "Wala usifuate (ukipita ukisema au kuyafanya)usiyo na Ilimu (ujuzi) nayo. Hakika masikio namacho na Moyo, hivyo vyote vitaulizwa".Tupate kuzingatia mapema mapema suala la Moyo huo. Tuangaliekatika:Qur an: Suratin Nnass: 114:1 - 6.5. "Sema najikinga kwa Bwana mwenye kuwalea, Mfalmewa watu muabudiwa wa watu, na shari ya mwenyekutia wasiwasi mwenye kurejea nyuma, atiayewasiwasi nyoyoni mwa watu (ambaye ni) katikamajini na watu".Nini muradi wa Mnyezi Mungu kwa mkusanyiko wa kauli zotehizo kutoka katika Sura mbali mbali?Naam, mkusanyiko wa aya zote hizo na nyingi mfano wa hizo,zimekusudiwa huo Moyo ili utayarishike sawa sawa katika yakini(yaqini); na lengo lake ni kumtambua Mnyezi Mungu mmoja. Nahuko ndiko kumuabudu. Kuabudu au Ibada ni neno ambalowaarabu haliwapi taabu, lakini kwa kiswahili unaposema kuabuduni kuabudu, au kufanza ibada inakua bado hatujafasiri kitu, napengine huenda tukakwama tukilifasiri kua ni kuswali aukumuomba Mnyezi Mungu. Wakati tukiulizwa juu ya mfano wandugu zetu Mabaniyani wanapolikabili jua saa likichomoza, huawanafanza nini?.Kuabudu ni kutambua, tena kwa yakini (yaqini) kua MnyeziMungu ni mwenye kupatikana na ni ambae Hapasi kuabudiwa kwayakini (yaqini) Asiye kuwa yeye.Na sasa tunaanza na ufafanuzi ambao, Inshallah utatufikishakatika kudhihirikiwa kua huo Moyo sio ni wewe tu, bali ndio Nafsi16.

hawakuhitilafiana sana katika jitihada zao: wao wameona mbalizaidi ya madaktari:Kwanza: Wameona kua katika kiwiliwili kizima hakuna ambakopanamvutia na kumuhimu mno Mnyezi Mungu kama hapo, na kwasababu gani mpaka iwe hivyo? Kwa sababu: Ndo mahala pekeeanapopatizama Mnyezi Mungu, Hadithi inathibitisha hayo:“Mnyezi Mungu hatizami sura zenu wala mali nawatoto wenu. Lakini Mnyezi Mungu anatizamanyoyo zenu na matendo yenu".Mnyezi Mungu anaupitia moyo wa kila mtu mara 360 kila siku. Naukiwa mtu wa akili na mazingatio utaona kua inastahili iwe hivyoushirikiano ulioko baina ya Moyo, Akili na Roho, ndani ya mwiliwa mtu wa ajabu. Na hasa inapofikia Roho kutaka kuueleza moyoambao ndani yake ndo kwenye Nuru ya Akili kutaka kuelezea juuya Siri ya uhai.Pili: Ndio utaulizwa (mas-uwl) na Mnyezi Mungu, kamailivyoonyesha hapo nyuma katika aya namba 4 katika sura ya 17 ayaya 36 (Bani Israel). Ikiwa hiyo ndo hakika ya mamboyatavyokwenda, mtu ungeweza kufikiria njia yake mwenyewe jinsivile ungejibu suala la kuulizwa ambae alizikwa bila moyo wakendani ya kiwiliwili.Tatu: Ndio utaoonja Raha au Mateso hiyo siku ya hesabu.Nne: Ndio wenye Nuru ndani yake ambayo kwayo mtu husarifuchungu ya mambo muhimu. Kwayo (hiyo akili) Mtu hua mukalif(mkalifiwa au mbidiwa na jukumu la sharia (Islam). Aya nambari 2ambayo imenukuru Surat Hajj 22: 46 inahusika. Angalia kwamakini jinsi gani Mnyezi Mungu amejaalia huo huo Moyo kua naakili ndani yake. Hii ni fununu tu kwako, basi ikiwa ni yenyekulingana na kupewa funguo mikononi, juu yako ni kufungua kilaunapopataka Wewe!.Tano: Ndio ambao huwekwa (na mwenyewe Mnyezi Mungu)Imaani ndani yake, na ikiwa ndio hivyo basi mfano wa waumini wadini mbalimbali ni wenye kututosha.18.

ya “Kafu” na “Nuni” tu, yaani – “Kun Fayaku-n”, angeweza bilashaka yeyote kumtumbukiza Mtu mzima mzima ndani ya moyomdogo kama ule ulotolewa na Daktari; na kwamba siku ya kiyamaakamtoa tena Mtu yule yule toka kwenye mchanga (Bi Dunia) lakiniHajaagiza hivyo. sio rahisi aende kinyume na alivyokwishapanga.Qur an: Surat Fa-tir: 35 : 43.….."….Wala hutapata mabadiliko katika kawaida yaMwenyezi Mungu". (Na kadhalika hutapata kuonazikihama – kawaida hiyo ni tangu zamani imetanguliakuwepo kwake).Na kama ndo hivyo, kwamba mambo yake Mnyezi Munguhayawezi kubadilika badilika ovyo ovyo tu, basi - Moyo lazima uwena sura nyengine zaidi ya ile tuliyoizoea, haijakudhihirikia tu, kua,huu Moyo, nini hukmu yake?.MOYO NI WEWE:Bila shaka yeyote Akili inakubali bila upinzani wowote naingawaje Mtu amekipita kila kitu kwa ubishi, kwamba ikiwa (niMoyo) ndo unaotamka. ndio wenye Imaani na Uislam, ndoUnofikiria, ndo Unaoamrisha mpaka matendo yakafanzika, ndoutaoonja raha na kumiliki yote miongoni mwa neema na fadhilakubwa zilizoahidiwa kupewa, mfano wa isemayo aya hii katikaQur an: Wa-qian: 56 : 22-24."Na wanawake wenye macho mazuri na makubwa (yavikombe) (wanapendeza na safi) Kama kwamba nilulu zilizofichwa (katika machaza yake ndio kwanzazinapasuliwa), ni jaza ya hayo waliyokua wakiyatenda".Ikiwa ndo hivyo basi, ni kweli na yakini (kua ndio mimi ndie yeye).20.

UFAFANUZI WA ROHO:"War ru-h maa-akhbara an-hal mujtaba fanumsikulmaqala an-ha adaba""Na Roho hakuielezea juu yake mteule mtegemewa(Bwana Mtume SAW kwa hivyo ni uzuri ) kujizuiakusema chochote juu yake, Kwa ajili ya kuraiadabu!!".Na falau Mnyezi Mungu amesema kua ametupa ujuzi kidogojuu yake."Na wanakuuliza habari ya Roho. sema: “Roho niJambo lililokhusika na Mola wangu (Mnyezi Mungu)Nanyi hamkupewa katika (ujuzi) ila kidogo kabisa.(Nayo ni ilmu ya vitu visivyokhusika na roho)".Na juu ya kufunuliwa kiduchu tu, ambacho sio hasa hasakihusikacho na Roho yenyewe, mtu amefanza ya kushangaza kabisajee? ingekuwa kiduchu hiyo hiyo ni juu ya Roho halisi labdaungefikia kusema ulamaa hawangekufa. Wazoefu juu ya mambo yakiroho (practical spiritual Experts) nao hufanza mambo mengi yakiajabu ajabu kiasi cha kushindwa mtu wa kawaida kuyabeba ndaniya Tasdike (kukubali).Kwa upande mwengine tuangalie mfano wa Mwanachupa(The taste tube baby) mtu amefikia hadi hio ya kutoa mtoto bilakupitia njia yake ya ada (bil kul sio kwamba wao wameumba laabalini kwamba wamijitahidi katika kufanzia majaribio chungu yaaya mbazo Mnyezi Mungu Mtukufu ameonyesha waziwazi jinsi vileanavyotoa mtoto kutokana na tone la manii kama ndani ya kitabuhiki (Tulivyokwisha elezea huko nyuma tukanukuru aya ya 13-14 yaSurat ya 23 Al Muuminun). Na pia katika Surat Zumar 39:6."Amekuumbeni katika nafsi moja kisha akamfanyamwenzie (mkewe) katika jinsi ile ile, na akakuteremshieni(akakuumbieni) wanyama wanane (hawawenye nafuu kubwa kwenu) madume na majike.(Ngamia, Ng'ombe, kondoo na mbuzi) ( Huumba)hukuumbeni matumboni mwa mama zenu umbobaada ya umbo - katika viza vitatu huyu ndieMnyezi Mugu wenu: ufalme ni wake hakuna21.

aabudiwaye kwa haki illa yeye basi nyinyimnageuzwa -wapi?"PANDE LA DAMU:wakati Bwana Mtume SAW alipojulisha juu ya hilo pande ladamu, bila ya shaka yeyote alimaanisha Roho - kwani hiyo damuchafu ndio chanzo cha Roho(Man-bair-ruh) Na huenda kiwiliwili kizima mfano wa Nuru ya taainavyozagaa katika chumba. Si rahisi kuashiria kwa mkato nuru-ikosehemu gani khususi, ndani ya chumba hicho. Hiyo Roho iliumbwazamani, kabla ya kiwiliwili, haipungui miaka alfu nne kabla; ilamiaka yote hiyo huenda ukashangazwa kuona kua ni makadirio yasiku nne mbele za Muumba Sub-hana wa Taala. Hiyo, katikakutafutiana, na kutofanana na yeyote amenasibisha siku yake mojakwa hisabu zetu za hapa duniani ni, kadiri ya miaka Alfu moja;imeonyeshwa katika:Qur an: Surat As-sajada: 32 : 5."Anapitisha mambo yote yaliyo baina ya mbingu naardhi, kisha yanapanda kwake kwa siku moja tuambayo kipimo chake ni miaka elfu mnayotumianyinyi katika kuhisabu kwenu"Na katika makadirio hayo Mnyezi Mungu alitangulia kuumba Rizikina akaitanguliza hapa duniani ambako alikwisha panga kumletakhalifa (Viceregent) kama ilivyo katika:Qur an: Sura ya 41:10.22.

“Na akaweka humo milima juu yake (ya uso wake), naAkabariki humo na akakadiria humo chakula chake(cha kuwatosha watakao kaa humo, amefanya haya) katikasiku nne, (mida mine). Haya ni sawa kabisa kwahao wanaouliza (mambo wakataka kuyajua)”.Hiyo Roho, Maulamaa wengine wanakubali kuwa ndiyo Nafsina baadhi yao wanakubali kuwa ni sehemu ya Roho iliyojitengasiku ilipoumbwa. Na ni kutokana na tendo hilo ndipo ilihutubiwakwa jina la Nafsi.Roho imeshikana na Moyo, (lau siyo Moyo ule uliotolewa naDaktari) wa Mtu katika kiwiliwili chepesi ambacho ndiyo hakikaya Mtu mwenyewe. Siyo mwili wenye manyama ambao Asili yakeni udongo huu huu wa ardhini.Katika kuufahamu undani wa yakini (yaqini) ni jambo labusara kuzingatia suala la Moyo ambao ni: Kiwiliwili chepesichenye Roho ya Mola, ambacho ndani yake lipo hilo pande laDamu ambalo ni chanzo cha Roho ikiwa humo ndani ya Moyo ndioilikoanzia.Katika Moyo wa Roho, na Moyo wa kawaida pana uhusianofulani ambao kwa ajili ya kurai adabu, ingekuwa bora kutokuingiliasuala lake.UFAFANUZI WA AKILIKila mwenye Akili hakosi kua na fununu ya kitu ambachokimeweza kumpambanua yeye na Mnyama ni nini? Ni Akili.Taba-an lakini wakati ukiulizwa “Iko wapi hiyo akili?” Huendaukajibu iko kichwani utafikiri labda unajua kua yule “Mwendawazimu” kichwani mwake hakuna kitu, au imepungua kidogo. Naimekwenda wapi? Au wakati ametibiwa na kupona na huwaimeingia kutoka wapi? Je mtoto mchanga, mdogo na kijana wamiaka kumi na mbili utaeleza nini juu ya akili zao? Ikiwa mtotomchanga ni hana akili basi labda atakua kama mwenda wazimu?.Hayo yote ndio miungoni mwa harakati za kutafuta jibu halisi;lakini bila shaka umeanza kulitilia wasi wasi jibu la kuemo akili23.

ndani ya kichwa. Akili imo ndani ya Moyo, na ndo Johari yakehasa. Akili ni kitu azizi sana, ambacho Mnyezi Munguhumuhukumu mja wake kwa kadiri ya akili yake. Na ambae hanayobasi hua hana hukumu yeyote juu yake. Na hapo ndo mfano wamwenda wazimu na mtoto unapovutika. Wa kwanza (mwendawazimu) mas-ala yake yanajulikana; kwani kuhisabiwa kwake nikabla ya kupata ugonjwa huo. Amma mtoto atahesabiwa kuanziamiaka 9 hadi 15. miaka tisa, kama ametokewa na manii katika umrihuo au hadi kufikia miaka kumi na mitano.Kuhusu kukua kwa akili ya mtoto kila miaka inapomsogeambele sio rahisi kuelezea, lakini ukweli ni kwamba inasaidiana naUbongo. wa mbele ya kichwa (ambao wanasayansi wanauita –Cerebrium) na pia kusaidiana na ubongo wa katikati ya kichwa(Cerebellum) na ule wa uchogoni (medula oblongata). Na huzidina kupungua. Amma kuzidi kwake ni kwa kadri ya majaribio(Experimentations), na pia kwa kusoma Qur an kama alivyosemaBwana Mtume SAW.UISLAMU NDANI YA AKILI:Mnyezi Mungu alipoiumba Akili aliiamrisha kugeuka nyuma(mfano wa askari kwenye mafunzo-about-turrn, Right-turrn- nyumageuka, kulia geuka, na kadhalika) ikageuka - Mnyezi Mungualifurahikiwa nayo na kusema:“Sikuumba baada ya Mohamad (Nuru yake) Kitubora kuliko wewe, na sitakuweka ila kwa walewenye kupendeza sana mbele zangu”.Na ni kutokana na sababu hiyo leo kila mwenye akili hupendwasana na watu.Kitendo cha Akili katika Utu wake mbele ya Mnyezi Mungu,kwa mujibu wa misingi ya uislamu (principales of Islam) ni chenyekuonyesha Uislamu. Kwa hivyo kila mwenye akili hatokosa kuwamnyenyekevu. Hatokosa kua mwenye kumuogopa Mnyezi Mungu,nako ni kufwata maamrisho yake.Mpaka sasa hakuna alielezea Akili ni kitu gani hasa na juu yakuzidisha uchunguzi juu yake. Wana Elimu ya viumbe (Biologists)24.

aada ya jitihada hizi na hizi katika kutafuta hakika ya akiliwameandika hivi (katika kitabu “Exploring Biology”):“We know from Experimentation that the cerebrumis the centre of intelligence, but we DO NOT as yetKNOW just what intelligence is. ONE great advancestep we have made is in discovaring that consciousnessand intelligence are centred in th cerebrum.Intelligence is a function of the cerebrum just aslife is a function of Protoplasm”.Maana yake:“Tuna jua kutokana na majaribio tulokwisha yafanza, kuacerebrum (sehemu moja katika tatu, ya ubongo) ni iliokokatikati ya akili (ni kitovu cha akili yote ) lakini badohatujafikia kujua hiyo akili ni kitu gani. Hatua moja kubwatulioipiga katika maendeleo ni iliopo katika kugundua yakwamba akili mahiri (tambuzi) na hio akili yenyewe ni ziliopokati kati ya cerebrum. Akili ikiwa matenda kazi yake niyenye kutokana na hio cerebrum, kama ilivyo kua uhai kuamatenda kazi yake ni yenye kutokana na misingi (ya tabiya)ute (wa uhai)”.Basi kutokana na kushirikiana pamoja (Nuru ya akili iliokondani ya Moyo) (na Bongo zote tatu zilizoko kichwani) ndipo mtuanapomudu kuswarifu mambo sawa sawa. Amma ikizimika Nuruya akili Ubongo peke yake haumudu kufanza kazi zote pekee.Kwani huonekana mtu ni mwenda wazimu, na kusamehewa mambomengi juu yake.Ni hiyo akili kutokana na kua kwake kitu cha ajabu, angaliajinsi tunavyo weza kujua na kusarifu mambo hata mingha-iri yakuyaona kwa macho, katika hali kama hizi, mathalan:1. Maji yamiminikao chini toka nyumba ya tatu ambayo ina kukupia.2. Nyama ya mbuzi inachomwa jirani yako; na nguru jirani yakomwingine, na kuunguliwa na nguo toka kwa jirani yako wambele.3. Uko mbele ya umati lakini katikati ya mgongo wako yuko chawaau ndorobo.25.

Akisema Bwana Mtume SAW:“Usimlilie aliekufa, mlilie aliepungua akili yake.Basi kwa kadiri ya upungufu katika hisia tano, Ndipo piamazingatio ya upungufu wa akili yake kwa jumla. Hisi zote tanohushindwa kufanya kazi kama mtu akilala usingizi.Kila kitu kina sifa, na akili nayo ina sifa zake. Katika hadithiiliopokelewa kwa Bi Aisha (R.a) hakika amesema Bwana MtumeSAW:“Akili inayo sehemu kumi, kati ya hizo zimegawanyika ndani yamafungu mawili:1. Dhwa-hiri na 2. Ba-tini.Sifa tano zilizomo ndani ya kundi la:Dhwa-hiri ni hizi:-1. Samt. Yaani ukimya kwani amesema Bwana MtumeSAW: “Mwenye kuzidisha maneno yake huzidikuanguka (kuporomoka) kwake”(Speech issilver silence is gold) kusema sema ni fedha,kunyamaza ni dhahabu.2. Hilm: Upole.3. Tawa-dhui: Unyenyekevu ikiwa ni ile hali ya kujitupa chini nahata kama Mnyezi Mungu amekufanza mfalme,kwani hapo ndipo hasa pahala pake, kasema BwanaMtume SAW:-“Mwenye kujiweka chini, Mnyezi Munguhumrufaisha (Humnyanyua, Humpandishacheo juu)”.4. Kuamrisha mema na kukataza maovu: Maana yake ni dha-hirikabisa kwani kilicho toa ubora kwa UmatMuhammad SAW mbele za Mnyazi Mungu ni sifahiyo.5. Amal swa-lih: Kuwa na amal njema ipendeleayo kheri kila mara.Sifa tano za Ba-tin:-6. Tafakkur: Hali ya kufikiri fikra hasa mambo mengi mengi tuya ajabu, ambayo Mnyezi Mungu ameyaumba,26.

“Na kwa Nafsi (Roho) na aliezitengeneza. Kishaakaifahamisha uovu wake na wema wake. Bilashaka amefaulu alietakasa (Nafsi yake) Na bilashaka amejihasiri alieiviza (Nafsi yake)”.Alimaanisha kuuhusisha wakati wa kabla ya kuingia ndani ya viwiliwili vya udongo. Akili inapiga picha (khayal) kiasi cha kuona labdaulikuepo hapo awali na kwamba hivi sasa unajishughulisha kufikiri,ambaye anapata shauku ya misemo ya Mnyezi Mungu yenye mifanokama hiyo. Basi mfano mwingine ni kama ule uliomo mwenye:Qur an: Sura Al-a`araf: 7:172.“Na (kumbuka) Mola wako alipowaleta mwanadamukutoka Migongoni mwao kizazi chao na akawashuhudishaJuu ya nafsi zao (akawambia) “je mimi siyeMola wenu? Wakasema” Ndio, tunashuhudia (kuwawewe ndiye Mola wetu) (Akawaambia MwenyeziMungu ) “Msije mkasema siku ya kiyama kuwa sisitulikua tumeghafilika na haya (hatuyajui)”.Aya hiyo inashadidia siku ya Ahadi na Mithaki wakatiambao viumbe vyote havikua vimevaa miili ya udongo. Na kamailivyoashiria Suratish-shams, Ukweli ni kwamba:-“Kisha akaifahamisha (Nafsi uovu wake na wema wake)”.Maelezo ya aya zote mbili hizi ni yenye kuonyeha wazi wazi28.

uhakika mzito kweli kweli kwamba tulikueko kabla.Siri ya Ibin Adamu ajuae ni Mnyezi Mungu peke yake, lakinikwa shuhuda nyingi zilizotapakaa mote mwenye Qu ran, inaonyeshawazi wazi kua Ibin Adamu mbele ya Muumba anayo nafasi mahsusna ya pekee juu ya viumbe wengine. Moja ya kiungo kikubwa chasiri hio na ajabu zake ni Nafsi ambayo imo ndani ya miili yetu.NAFSI, ROHO, MOYO NA AKILI KUINGIANDANI YA KIWILIWILI CHA UDONGO:Qur an:Ad-dahr: 76:1.“Hakika ulimpitia Binaadamu wakati mrefukatika Dahari hakua kitu kinachotajwa(Binadamu ndie kiumbe cha mwishokuletwa ulimwenguni)”.Baada ya kuumba dunia na kuweka kila kinachohitajiwa,Mnyezi Mungu aliweka viumbe mbali mbali kwa madhumuni yaIbada lakini walishindwa.Viumbe hivyo vilomtangulia mtukuishi hapa duniani vinaonyesha kua ni Majini, kutokana nauchunguzi wa kauli ya Mnyezi Mungu, tazama:Qur an: Al Hijr:15:27.“Na Majini tuliwaumba kabla, kwa moto waupepo wenye joto (kubwa kabisa)”.Hiyo ni hakika ya wazi wazi kua tulitanguliwa na viumbe wenginewalio tofauti kabisa na sisi. Lau sio Binadamu kama wanavyodaiwatu wa Elimu ya machimbo (Archeologists) mfano wa Dr. Leacky29.

ambaye ni mashuhuri zaidi Afrika Mashariki (Tumeelezea kwakirefu katika kitabu chetu “El-makhuluq”)Mnyezi Mungu alipendelea kuweka kiumbe kingine, tenakutokana na Ardhi hii hii, na ndipo aliposema:Qur an Al Hajr:15:28.“Na (kumbaka) Mola wako alipowaambia Malaika:“Hakika mimi nitaumba mtu kwa udongo mkavuunaotoa sauti, wenye kutokana na matope meusiyaliyovunda”.Qur an:Hijr:15:29.“Basi nitakapomkamilisha na kumpulizia Rohoinayotokana na Mimi basi mumuangukie nakumtii”.Na ijapokua Malaika waliingilia kati kutaka kufupisha azmaya Mnyezi Mungu juu ya kuumbwa Mtu, lakini mwishoewalisujudu (lau sijda hiyo siyo kama ile ya kwenye swala. Hii nikuinamisha kichwa tu, kuonyesha kumtukuza huyo umsujudiaye).Kwa heshima na taadhima hiyo Mnyezi Mungu anatukumbushakatika sehemu nyingi mfano wa hii, mwenye:Quran:Israh:17:70.“Na hakika tumewatukuza wanadamu na tumewapavya kupanda bara na baharini, na tumewaruzukuvitu na tumewatukuza kuliko wengi katika wale30.

Kwa hivyo baada ya Nafsi hiyo kuwekwa ndani mwetu imekuani majaribio tosha kwetu kumtafautisha Mtu na Mnyama, na Mtuna Malaika. Vipi habari hiyo?Mtu anakua Mnyama akiifwata Nafsi yake na pengine Mnyamaakawa afadhali kwa sababu ya akili. Na Mtu anakua kama Malaika,akiipinga Nafsi yake akatekeleza yote aliyoamrishwa na MnyeziMungu bila kuasi, na papo atamzidi Malaika kwa sababu yamatamanio, ambayo Malaika hakupewa.Kwa hiyo wakati ukhabithi wake (Nafsi) ni zaidi ya Mashetwanisabini, basi ni wazi kabisa kua Shetwani mmoja hawezi lolote juu yaMtu. Ndo, sawa na kusema afanzapo mtu kosa, si rahisi kukubalikakua amezidiwa nguvu na Shetwani kuliko kua ni Nafsi yakemwenyewe. Nafsi hiyo inaweza kubadilika kama mtu mwenyeweanataka.MABADILIKO YA NAFSI HADI KUUNGANANA ROHO:Kama tulivyoona ya kua asili ya Nafsi ni Roho, na kwambailipata usugu baada ya kuchangukana nayo, basi inaweza kurudiakuungana na Roho.Qur an:Ash-Shams:91:9 -10“Bila shaka amefaulu alieitakasa (Nafsi yake) nabila shaka amejihasiri alieiviza (Nafsi yake )”..Safari ya kujitakasa inaanza pale anapokwisha tenda kosa na kuanzakujuta. Kwani ni lazima ajilaumu. Basi anapofikia hadi hiyo, huaamebadilika toka:1. Amma-ra – imeingia katika Nafsil:2. Law-wama – Amma anapotubia mtu akarudi kwa Mola wake,pamoja na kuazimia kufanza kheri tu, basi hua ni mwenye Nafsil:3. Mul-hama – Hii ndiyo Nafsi ambayo Mnyezi Mungu aliikhitari32.

Kuifahamisha ule uovu wake Nafsi na wema wake. Na akizidi Mtukujitakasa kwa kuongeza mambo mema, basi huingia kwenyeutawala wa Nafsil:4. Mut-mainna – Ambayo huwa ni ile ilotulizana kabisa. Penginehuitwa Moyo, Pengine huitwa Roho, pengine huitwa Akili, (hizini jitihada za Ulamaa).Nafsil Mut-mainna imetajwa ndani ya Suratil Fajr:Qur an:Fajr:89:27.“Ewe Nafsi yenye kutua”.Mtu hupata utulivu mzuri sana ambao husababisha Moyo, Akili, naRoho kutua kabisa kama siye alokua na vituko. Badilika badilika hiiinaenda toka hapa mpaka kuingia katika:5. Ra-dhiya – Ambayo ni hali ya kurudi kabisa kwa Mola wakeMtu, na zaidi ya kuridhiwa pia na Mola wake Mtu hapo hua:6. Mardhiyya – Ambayo ndiyo iko katika kukwea sana. Na Nafsil:7. Kamila au Swafiyya – Ambayo ni Nafsi ilosafika kabbisa. Nazama ikishafika hali hiyo hurudi ikajiunga na Roho, na ikishafikahali hiyo basi haitazamiwi kutoka tena hapo. Na hapo ndipo Mtuanapokua “Minal fa-izina”. – Qad aflah man zakkah.Ipo Falsafa kubwa sana katika jambo zima la Nafsi, lakini natutosheke na lile la kupatikana nguzo ya sita ya Imaan ndani ya haliya Nafsi Mar-dhiyya:“Khayri-hi wa Sharri-hi Mina Llahi Ta`ala”.Na haimkiniki kuyakatia tamaa majaribio ya Mnyezi Munguwakati Mtu anafahamu wazi wazi kua maisha ya hapa dunianiyamepangwa sehemu kubwa ya mitihani ambayo ili kuifaulu, basimisuko suko yake ni mingi ambayo anatakiwa Mtu kuifungiakibwebwe.Qur an:Al-A`nkabuut:29:1 -2.“Alif Lam Mym, je watu wanadhani wataachwa33.

(wasitiwe katika misukosuko) kwa kuwa wamesema“Tumeamini”, basi ndiyo wasijaribiwe (wasipatemitihani?)”.Zaidi ya mfano huo ni aloutoa Mnyezi Mungu ndani ya:Qur an: Suratil Baqara:2:214.“Mnadhani kuwa mtaingia peponi, na hamjajiwa namfano wa (yale yaliyowajia) wale waliopita kablayenu? Yaliwapata mashaka na madhara na wakatetemeshwasana hata mitume na walioamini pamojanao wakasema: “Nusura ya Mwenyezi Mungu itafikalini? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ikokaribu”.Ipo sababu moja tu ya maana katika taabu taabu zote hizo, nayoni ile iloambatana na hadithi ya Bwana Mtume SAW kua:“Hakika ya Mnyezi Mungu anapompenda mja wake,basi humtia mabalaa, akisubiri basi humkinga, naakiridhia humchagua”.Hakuna njia ya kututhibitishia lile penzi la Mnyezi Mungu juuya mja, kama katika hadithi hii. Ni kitu wazi wazi kabbisa lakiniMtu anapofikwa na mashaka na misuko suko kama hiyo, basihutokwa na Imaani mara moja na kuanza kuelekea kwenye IshrakiKama kwamba siye Bwana Mtume SAW aliyemuelezea hadithihiyo ilopita.“Basi Ad-duniya (Dunia) sijnul Muumin, ni jela yawalioamini (Mnyezi Mungu mmoja – Allah) Wa Janntulkafir. Na ni pepo ya kafiri”.34

“Na law thamani ya Dunia mbele za Mnyezi MunguIngelingana na thamani ya ubawa wa mbu, basi(kila ) kafiri asingekunywa funda la maji”.Kwa hivyo kila taabu zinavyozidi kwa Muumini ndiokuthubutika kwa maneno ya Bwana Mtume SAW na ndiokukamilika kwa neno Insaan.“…..Likitengemaa hilo, kimetengemaa kiwili wili kizima,na likiharibika hilo umeharibika mwili mzima”.Ni wazi kuwa katika kulitengeneza hilo pande la Damu chafuambalo ndo chanzo cha Roho na Nafsi panahitajika matendo yawema katika kila njia. Na yote hayo yatekelezeke na Ikhlas. Katikamlango ufwatao zipo nasaha zote zile ambazo zitamnufaishamwenye mapenzi ya kweli katika kujitakia maslahi ya Nafsi yake,vile alivyotupendelea Bwana Mtume SAW.35

Qur an:Al Infitar:82:6.INSAAN“Ee Mwanadamu! Ni nini kikudanganyacho naMola wako Mtukufu (hata ukamuasi)”.Ewe Insaan, Mtu bila ya kutazamwa viungo vyake auUbinadamu wake, lakini ni Insaan. Wala Mayyiz zake namnaanavyomili, tabia alizopewa mara asimange mara afurahi, haya sioyanayotizamwa hapo. Wala haitazamwi Aadami – Mara kachoka,mara usingizi, lakini - Insaan.Haya ni maneno matatu tofauti. Insaan ni yule Mtu, yule“yeye” au “wewe” au “mimi”; anaeazimia, anaekusudia,anaechagua. Anapochagua Insaan kwenda pahala aliechagua ninani? Insaan.Sehemu ya Ubinaadamu imetumwa tu. Miguu imetumwa tu,na viungo vingine vimetumwa tu. Inaweza na Ubashari ukawaumekuja kati, labda kuna mkate na mchuzi Ubashari unatamanimkate na mchuzi ukazidi kukutia hamu uende. Lakini Insaan yuleanaependa, anaehusudu, anaechukia, anaetakia watu wema,anaekumbuka Uungu, anaekumbuka kiyama. Hata mwili ukifa“yeye” yuko na yeye, ndiye anaeulizwa kaburini, anaeulizwaBarzakh.Kwa hiyo Qur an inapotaka kusemea Mtu namna hiyohumwambia “Insaan” – Mtu, humwambia Insaan – Haikuambiwa“Ya Adami”, “Yaa ayyuha Adam” au “Yaa ayyuha Bashari”.“Yaa ayyuhal Insaan” ndo inamtofautisha baina yake yeyena Malaika, baina yake yeye na Wanyama wenginene, ni kuaInsaan – Wewe Insaan si kwa Mwili (bali) kwa Roho.KUMALIZIKA MWILI36.

Kutumikia Mwili upatie matamanio yake, uupe nguvu, basiuuhudumie Mwili, uwe na nguvu tu au starehe zake mwili tu.“Atat lubur rib hu fiima fiihi khusran nu…”“Unatafuta faida katika kitu ambacho ndani yakemna khasara.”Kila unapomuona mtu mzima, hakuwa namna hiyo alikuakijana, na ujana wake ulitumika kwa sehemu ya Ubinadamu,sehemu ya Ubashari na Insaan ndio aliesemezwa akaongozamwili, sasa unatumika mwili tu. Na mwili unapotea kila siku kidogokidogo na kwa bahati kijana akifika utu uzima ni lazima siku mojamwili utamtoka.“...Atat lubur rib hu fiima fiihi khusran nu aqbil alannafsi au ruhu…”“Kaabil juu ya Nafsi au Roho”.“…..Was-takmil fadha-iluha”“Ukamilishe fadhila zake (virtues) zake”.Uwe una Sa-ir, iwe kitu cha Nafsi au Roho, Fadhail uwekarim, hichi kitu cha Roho uwe unawapendelea watu wema, iweunampenda Mtume SAW , unajishughulika na kumtaja MnyeziMungu na kumtumikia Mnyezi Mungu, hayo yote ni mambo yaRoho. Shughulika na hayo “Aqbil alan Nafs”. Usiwe nawe ni mtuwa kujipima nguvu (Exercise) tu, unatizama Nafsi inakuaje kila sikuunajipima; unashindana kuvuta kamba, kua shujaa:“Washujaatus sabri saa”“Unavutwa na matamanio wewe ukapigana namatamanio ukasubiri”.Na Twariqa yote ukisikia kuna, Twariqa ni kumtengenezaInsaan yule anaeitwa Insaan, tena sehemu ya Ubinaadamu.Mikutano ya kheyri, ya Dhikri, macho yanatizama njia ya kupita.Lakini hasa Twariqa inamuongoza Insaan imfanye ana mahabakatika Moyo wake. Anampenda Mnyezi Mungu na Mtume wakeSAW na viumbe vya Mnyezi Mungu. Awe karimu, asiwe Mwizi,asiwe mjanja si madhambi ya Nafsi, madhambi ya Roho. Madhambi37.

ya Nafsi yanakuwa makubwa sana, mbali kuliko madhambi yamwili. Hata Mtu akiiba unaokwiba si mkono, unatumwa tu, ndiomaana Mtu asiekua na uaminifu hana Imaan:“Laa Imaan liman laa amanata Llahu”“Hapana Imaani kwa Mtu ambae hana uaminifu”.Kwa sababu uaminifu si kitu cha mkono, wala cha kichwa,wala cha miguu. Ni Nafsi ni Roho, ndio inaovunja Uaminifu.Mkono unatumwa ufanye lisilo la twaa:“Laa Imaan lima laa amanata-Llahu” .Yaa ayyuhal Insaan, Aqbil alan Nafsi was sstqbil fadhailihafa-anta bin-Nafsi au bi Ruhi laa bil jismi Insaan”.Si kwa kiwiliwilli Insaan, usidhani kuwa wewe ni kwa kiwiliwiliInsaan .MTU MNYAMA:Kwa kiwiliwili wewe ni kama Ng`ombe, Mbuzi Sungura,Panya; wao ndio sehemu ya kiwiliwili ulionacho wewe “Mammal”(Biologists - wanawaita). Lakini Insaan Twariqa iko hapo. KatikaSulu-k kupata njia kijitengenezea njia ya Dini, ukatafuta ubora kwanjia ya Dini. Ukatafuta mali kwa njia ya Dini, njia kwa kumtajaMnyezi Mungu, na huku unayo yako ya kidunia. Insaan hapoanakuwa katika hatari.“Ee Mwanaadamu ni nini kikudanganyacho na Molawako Mtukufu (hata ukamuasi)”.Una wazee wawili huwatii una mke humtizami inavyolazimu,mke ana mume hakai nae kwa Insaafu. “Nini kilichokukhadaa naRabu wako wewe ni karimu, kakukarimu wewe Insaan kakupaUbinaadamu huo, una macho, una miguu, una viungo, una mambokadhaa wa kadhaa.“Alladhi khalaqaka”“Ambaye kakuumba (akakupa mwili huo)”38.

“Fasaw – waaka”“Akakufanya sawa, (mikono imekaa sawa na miguu,macho kila kitu kakiumba kimekaa sawa)”.Ingeweza ukawa miguu mirefu, mkono mmoja mrefu mmoja mfupi.Na yote hajakufanyia haya. Kakutengeneza bara-bbara.“Faadalaka”“…Akakufanya ulingane”.“Fi-ayyi suratin maa – sha-a”.“…Katika sura yeyote anayotaka yeye Mnyezi Mungu”.“Rak-kabaka”.“…Kakutengeneza (kakupandanisha)”(Kakupa sura unyoitaka, watu wangapi kuna mamilioni Waislamu tuduniani, wanaambiwa leo wako milioni alfu, na kila mmoja ninamna yake na sura yake na wewe una yako. Fikiri, kaa ufikiriusende kinyama, mnyama anakwenda kwa mwili tu - mambo yakimwili).Sasa kinchokuzuia baada ya kuwa umeonywa, baada yakuwa umeshazinduliwa, baada ya kuwa umezaliwa katika Uislamu,baada ya kuwa umesikia mambo ya Mungu na mambo ya tabia nzurina Roho zinazotakiwa Mtu awe nazo – Wema Insaaf, nini ufikirikilichokuzuia usiwe hivyo?“Bal tukadh dhibuna bid-diin”.“Mnakanya Mnakadhibisha hukumu siku ya kiyama”.Ungekuwa una Yaqini, mimi ntahukumiwa, kwa ninoyafanyaungeyakimbia yaliokatazwa. Yakikufika utafwata Qur aninavyokwambia (yalokatazwa) mbio unarejea kwa Mnyezi Mungu.KUREJEA KWA MNYEZI MUNGU:“Wastagh firul Laha innallah Ghafuwrun Rahi-m”.Wanaomtaka Maghfira Mnyezi Mungu–Innallah–Ghafurun-Rahim.39.

Hakufukuzi sasa mbona umeshindwa, laa.“Innal ladhi-nat-taqaw”.“Hakika watu wenye Taqwa”.“Idhaamas-sat humut twaifun minash shaytwani”.“Wakiguswa na sehemu katika Shaytwani”.“Tadhakkaruw”“Wanakumbuka”Khalafu Sheytwani anaweza kukuta sehemu ya Basharia yaInsaan anapita kwa njia ya basharia, anaingia katika Insaan,anamukhadaa katika njia ya matamanio, katika njia ya majivuno yakujiona, njia ya kughafilika. Usifanye hivyo, ukifanya hivyoukamsahau Mungu kabisa, umekhadaika na Mungu, mambo yaMungu umeyaachilia mbali. Huna Sala tano, huna saumu, hunachochote huna kutumikia walo kulazimu uwatumikie, huna Insaaf,huna uaminifu Mungu hatambui, inaonyesha nini:“Tukadh- dhibuna bid-dini”.“Mnakanya, Mnakataa, mnakadhibishahukmu na kila kitu kinaandikwa”.Kuna Malaika kazi yao kuandika:“Wainna alay kum laha-fidhii-na”.“Na hakika juu yenu (wako) wenye kuhifadhihayo mnayoyafanya (na kila kitu)”.“Kira-man ka-tibi-na”.“Waandishi”.“Maa yalfidh min qawlin illa laday-hi raqib-un atiid”.“Hatamki mtu neno ila mbele yake yuko Raqib na Atid”.Raqib anaandika mema. Ati-d anaandika maovu. Akifanya ovu Atid,kwanza huzuiwa. “Mwache labda atakumbuka, atarejea kwa MnyeziMungu”. Na ni mwepesi ikiwa mambo yenyewe hayajakamatana na40.

haki ya binaadamu, Mnyezi Mungu hukusamehe.Ikiwa haki yaBinaadamu, kakosea mtu - kaharibia mtu nyumba, ameharibia watuwatoto wao majumbani. Haki ya binaadamu inakuwa taabu. Lakiniyako wewe Nafsi yako na Mnyezi Mungu, ukikumbuka ukarejeaMnyezi Mungu anakupokea:“Wal ladhina idha faalu fa-hishatan ““Na wale watu wema wanapofanya (Fa-hishatan)uchafu (Aw-dhala-mu anfusa-hum) – auwakadhulumu nafsi zao (dhakarul Lah)Wanakumbuka Mnyezi Mungu.“Fastaghfiru li-dhunubi-him”.“Wanataka maghfira kwa Mnyezi Mungukwa dhambi zao”.“Waman- yaghfiru dhunu-b illa Llahu”.“Na nani mwenye kughufiria madhambi ilaMnyezi Mungu”.Anakutaka Mnyezi Mungu wende kwake wakakutakiemaghfira, ukijiachia basi, Malaika wataandika wala hapana kua:“Aa miye Mungu ananighufurilia kwa hivyo ntaasi”, wakati huoupate yanotakiwa uwe nayo Majuto na Tawba, kua ndo sababu yawewe kughufuriliwa.Hiyo ni kua tabia (Environment) pahali palipokuzunguka,dunia yako ulonayo mambo kadhaa wa kadhaa yamekuvuta,umefanya silo- sio umezoweya kusema uongo ulipokuwa mdogounakutoka vile vile kwa sababu ya mazoeya ya uongo, hayo ndiyoyanosemwa sio kua “Aa, Mungu yupo atanisamehe, ntastaghfiru “.Huwezi, Istighfari sio kusema “Astaghfirrullah”, ni kutakaakughufirilie, na hakughfirilii mpaka ajue kwa kweli umejuta ikiwando hivi, hata ukichupa mpaka vipi kwa ubaya, unaingia katikaanaowaambia:“Yaa iba-diyal ldhina asrafu ala- anfusi-himu”.“Enyi waja angu ambao wamechupa mpakajuu ya Nafsi zao”.Pengine Mtu kakulia pamoja na kikundi cha watu wabaya, kaingiaulevini, akazoeya uongo - anaongopa - kazoeya kufwatia mbio41.

wanawake au wanawake wanojiweka kutafuta wanaumeakakumbuka “Inna lillahi” “Ninafanya nini haya ndo ya motoni”.Haya ndo ya Insaan anoambiwa – “Nini kinakukhadaa, yaaInsaan” , haya ndo yale ya unyama, si ya Uinsaan, si ya Insaania, yaUnyama. Anataka kuepuka nayo moja kwa moja yamesha mvaa kilayakimjia anajuta anatamani yamtoke kabisa anaambiwa”“Laa taqnatwu”Watu wa namna hao wanaambiwa:“Msikate tamaa na Rehema ya Mnyezi Mungu”.Iwe basi, Mnyezi Mungu Sub hana wa Taala, madamu nimemuasindo lazima atakutia motoni - hakusema labda – Laa la hasha.“Innal Llaha yaghfiru dhunu-ba jami`a”.“Mnyezi Mungu anaghufirilia madhambi yote”.“Innahu huwal ghafuw - rur rahim’.Yeye anaghufirilia (hapana hata kubwa vipi linalomshindakughufirilia) Anarehemu sana lakini:“Waaniibu ilaarabbikum”.Rejeeni bila kurejea kwake hapana tamaa inataka urejee kwa kujutana Tawba, ikiwa mali ya watu kwa kiasi unavyoweza kurejesha.Ikiwa umemtukana mtu au umemsema mtu, ukamtake radhi kwakiasi ya kupata salama ukiona mambo yatazidi tena haki yabinaadam hii nikisema mambo yatazidi hapo hatari:“Waaniibu ila Rabbikum”.“Rejeeni kwa Rabbu wenu (makafiri hawana pa kurejea)”.“Dhaalika biannal ladhiina aa-manut tabaul haqwa annal ka-irina laa mawla lahum”.Kumbuka kuna Malaika wanaandika. Na kufanya makosa siajabu kwa Insaan madam anao Ubashiria na Uadamiyyi. Ukifikwa42.

“ni kua mazoea tu yamemfika na anapigana na nafsi yakeanaisemeza nafsi:-“Yaa nafsi walihubbik, mtawaani”“E! Nafsi nakuonea huruma mpaka lini unajiakhirikuniakhirika namna hii”.Na kila ukiacha mapema na ukenda mwendo mzuri mapemando inakua wepesi kwako wewe, ukikawia, inakua kama mtiumeuacha umetia mizizi ukitaka kuung’oa taabu, na ni uzitokuung’oa mti ule, Na raha sana kuwa mwema mtu, na utakuaukijambia:-“Yaa ayyuhal ashbaan, maa gharraka birabbikalkarim al ladhi khalaqaka fasaw aaka faadalakafi ayyi swu-ratin maashaa-arak –kabaka, kalla baltukadh-dhibuna bid-diini wa inna alaykum lahaafidhinakiraaman ka-tibina yaalamuw-na maa tafaluna-innalabraala lafii naiim a (wa Innal fujja-ralafi-jahiim).Hakika watendaji wema wako katika neema kubwa wawe ndaniya Neema (hapa duniani kabla ya Akhera, sikwambii watakapofikaAkhera).NEEMA ZA DUNIANI NA NEEMA ZAAKHERA:“Wainnal fujjaara la fii jahiim”.WATU waovu wachafu matata mifujjaari, mijitu matata (malaghaiImaani zao za ujanja) la fii jahim – wako ndani ya moto hapaduniani.Inawataabisha - Conscious –dhamiri yao.“Yas - lawnaha yawmad -diin”.43.

“Jahiim” hiyo wataingia siku ya hukumu, watakwendawakahukumiwe wakutikane na maovu mengi kuliko mema, maovuyale hayajafutwa kwa Toba, hayajafutwa kwa Istighfaar - kwakumtaka Maghfira Mungu, hayajafutwa kwa iitiraaf - kukubali kuamtu ni muovu, anataka Mungu amtengenenze.“Laa – ilaha – illa – Llah”.“Yas- lawnaha yawmud-din”.Wataingia siku hiyo (ambayo mambo yote yanategemea uzito waamali zikiwa nyepesi yuko katika hatari mtu).“Fa-amma man thaqulat mawaazii-nuhu”“Mtu ambae amali zake zimekua nzito”.“Fahuwa fii iishatin raadhiya”“Yuko katika maisha yenye kuridhiwa atayaridhiayeye mwenyewe”.Amali nzito kama kukutana pahala (kama pale penye Dhikri)amali zinaongezeka zinakua nzito. Unakwenda Msikitini unaswaliunatumwa nyumbani unatumika katika mambo ya kheri.Unawapenda (Mawalii) Wa a`malas-swa-lihati-waudi ilalladhina aamanuw - Watatiwa watu ambao wenye kuaminiwakafanya mema - Jan-naatin ajri min tahtihal an-har -Mabutsani katika pepo inapita chini yake mito - lakini inatakakila mmoja kwa kiasi chake, njia zake - Wa udkhilal- ladhina a-manu wa amilus swa-liha-ti janna-tin ajri min tahthal an har -Siku hiyo ambayo watu wengine watakuamo katika hatari.“yawmud- diin” - Siku ya hukumu , ndo maana katika Alhamdutunaita:Maliki yawmid-diin - Mwenye (kumiliki) siku ya hukumu- ndo Yawmud Diin.“Wainna alaykumu laha-fidhi-na kira-man katibunna wama-hum an –ha bigha-ibin”.“Wala hawakua wao na moto ni wenye kua hawapo, hatasiku moja ( They are never absent from the fire)”.44.

Kila ikija list ya kuitwa majina “fulani fulani” “Labbeka” yupo –hathubutu kukimbia akawa (absent).“Wa ma-hum anha bigha-ibina wa ma-adraka-Maa yaumud-diin”.“Nini kitachokujulisha kitafanya ujue nini hiyo sikuya hukmu”.“Thuma ma-adra-ka ma-yawhud diin”“Nini baada ya hapa kitacho kujulisha nini siku yahukmu”.“Yawm-laa tamliku nafsi linafsi shay-an”.“Hapana nafsi itomiliki kumiliki nafsi nyingine kwakitu chochote.(Hapana nafsi yoyote itathubutu kuja bila Amri ya Mnyezi Munguna kukubaliwa na Mnyezi Mungu, “Aa, mimi namuombea huyumtu wangu”. “Huyu Swahiba wangu”, “Huyu mwanangu”, “HuyuMuriidi wangu”, Sharti Mnyezi Mungu Ampe ruhusa kwanza).“Walaa yash-fauw-na illa limanir tadhaa”Wala hawashufii ila wale Mungu alowaridhia kwanza, kua “huyuanaweza kuwashufaiya; a” huyu alikua mtu; unaambiwa kachupamipaka, katoka kwenye (cycle) ya kushufaiwa”. Si mambo yakuyafanyia maskhara, inataka mtu akae afikiri na mamboyanamngojea kila mtu.“Yawma laa tamliku nafsi linafsi shay an walamru yawmaidhin lillah.”“Na amri-jambo siku hiyo lina Mwenyezi Mungu”.Al hayyul qayyumu Mnyezi Mungu hakuna Mola ila yeye (na)ndiye mwenye Uhai wa maisha msimamia kila jambo, Anayejuayote - Laa- taakhudhuhu sinatu walaa-nawm - Haumchukuiusingizi, kusinzia wala usingizi. Yaalamu ma-bayna aydi-him -Anayajua yalo mbele yao watu wote - Wamaa-khalfahum - nayalo nyuma yao - Walaa yuhiitwuna- Wala hawazungukii akiwajua45.

Vilivyo. Bi shay- in min ilmihi - Katika yaliyo katika IImu yake,llla bima-sha-a - Illa anachokitaka, Wasia kursiyyuhus-samawa-tiwal ardh - kiti chake cha ufalme kimeenea mbingu zote naardhi, Walaa yauw-duhu hifdhuhuma wa huwal aliyyul adhi-m -Hakumchoshi kuhifadhi Samawati wal ardhi.Siku hiyo watu wa mwanzo watostahiki watopata kheri kubwasiku hiyo watu wenye kupendana kwa ajili ya Mnyezi Mungu.46.

MALIPO YA PEPO KWAWAPENDANAO LILAHI:Itanadiwa:-“Aynal muta-ha-bbi-na- lijala-li adhilluhum tahta dhilliyawma laa dhillu illa dhili”.“Wako wapi wanaopendana kwa ajili ya Utukufu wanguniwafunike chini ya kivuli changu, siku ambayo (leo)hapana kivuli illa kivuli changu”“Wajabat mahabbati lilmutahabbi-na-fiiya”“Yamepasa mapenzi yangu kwa wenye kupendanakwa sababu yangu”.“Al-mutajali-sin fiiya”“Wenye kukaa pamoja kwa ajili yangu”Na kuna watu saba: “Yudhillu-humu llah tahta dhilluhu yawmala dhillu-hu”. Mmoja Imam -A-adil - Waja wake wenye kufanyauadilifu. Na katika hao waliotajwa, “Shabun Nashaa fii twa-atiilaha”. Kijana kakulia katika twaa, fi ibadatil-laha – katika ibada yaMnyezi Mungu (kama vijana ambao wana Swala zao tano,wanakutana kwa ajili ya Mnyezi Mungu Al-hamdu-lillah inatakawashukuru. Na alama kubwa ya kushukuru ni kuepukana nakumuudhi Mnyezi Mungu kadiri unavyoweza.“Sha-bbun nasha-a fii twa-ati llahi warajula-ni tahabbafil-la-hi”“Watu wawili wamependana kwa ajili ya Mnyezi Mungu ““ljtamaa alay-hi”.“Wamekusanyika kwa sababu ya Mnyezi Mungu”“Wa-tafarraqa alay-hi”.“Wamefarikiana kwa sababu ya Mnyezi Mungu”.47.

“Wa-rajulun”Na mtu”“Da-at-hu”“Amemuita mtu yule”“Mra-atun”“Mwanamke”“Dha-tu Mansibun”“Mwenye cheo”,“Wa jama-lin”“Na uzuri”“Faqala inni akhafu Llah”,“Akasema mimi namuogopa Mnyezi Mungu”.(Hapana kusema wanavyosema vijana wa kisasa “Aa, si katakamwenyewe” – inatosha wapi umuogope Mnyezi Mungu).Na mwengine kutoa mkono wake wa kulia, mkono wa kushotohauna habari. Yaani katoa sadaka kafanya kwa lilah hatta hapanaanaejua. Mradi, wote saba, watu ambao Mnyezi Munguatawaambia siku ya kiyama-“Tahiyyatu-hum fii-ha sala-m”Maamkio yao – Mnyezi Mungu kuwaamkia ni “Sala-m”. Hawawanatokota motoni, na hawa Mnyezi Mungu anawaamkia “Sala-mqawlan min rabbi rahiim”. Na wao wenyewe wanaamkiana “Salamtahiyyatu-hum fii-ha sala-m”. Wanaamkiana wenye “Sala-m”kuna salama tu – (peace) basi.Pepo ya Kiislam ina amani, hapana mtu atosikia neno la kumuudhi,Hapana chochote – La-ila-ha-illa llah. Yaa Rab Amani Salam - baliwanaanza kuipata tangu wanapoondoka duniani. Malaikawanawafisha na huku Malaika wanawaambia:“Salam aleykum al-ladhi-na tawaf-fata humul Mala-ikat48.

tayyibi-n Sala-mun alaykum -ud-khulul jannat”.“Ingieni peponi”, pepo gani? Pepo ya Barzakh, kiyama bado(haijafika) hakijaja. “Ud-khulul jan-nat” – “ingia Peponi” Namwengine Barzakh wanataabika, kama Firawni na watu wake“Anna-ru yuuradhu-na alay-ha (him)”.“Moto unakabilishwa juu yao asubuhi, na jioni”.“Ghuduwan wa ashiyyan, wa yawma taquw-mus-sa-ati” - Na siku(ya) kiyama kitaposimama. “Ad-khilu – watieni-Alafir-awni”.- Firauni na watu wake. “Ashad-dal adha-ba” - Adhabu kali kabisahiiwapi – “Sab-han, wa Masa-an”. “Ghuduw-wan au “Wa shiyyan”– Barzakh. Ukipita kwenye makaburi unaona bas. Kuna watu wakokatika taabu kubwa, na wengine wamo katika raha kubwainategemea umetengeneza nini huko.Basi, muhimu ni Sulu-k kujaribu kujitengeneza, uwe natabia nzuri, hata ukionekana uwe unajulikana.49.

ASKARI NA ADUI ZA MOYO:Mfano wa Mtu (wewe) ni wa ajabu kupita yote ambayo MnyeziMungu ameieka mbele ya macho yetu. Na tuchukue mfano waviumbe vidogo sana kama vile Nyuki jinsi walivyo. Umma wakutosha wenye nguvu na umoja, (a perfect Emperial Kingdom).Amesema Mnyezi Mungu katika:Qur an: Surat Al-Muddath-thir: 74:31.وَماَجَعَهْىاَ‏ اصْحَةَ‏ انىَاز اِآلّ‏ مَهَكَة وَماَ‏ جَعَهْىَا عِدَتَهُمْ‏ االّ‏ فِتْىَةً‏نِهَرِيْهَ‏ كَفَسُوا نِيَسْتَيْقِهَ‏ انَرِيْهَ‏ اُوْ‏ تُىاانْكِتَةَ‏ وَيَزْ‏ دادَ‏ انَّرِيْهَ‏ اَمَىُىْااِيْمَاوَاوَّالَيَسْ‏ تاَبَ‏ انَّرِيْهَ‏ِِااوْ‏ تُىا انْكِتَةَ‏ وَانْمُؤْ‏ مِىُىنَ‏ وَنِيَقُىْلَ‏ انَرِيْهَ‏ فيِ‏ قُهُىْ‏ تِهِمْ‏ مَسَ‏ ‏ٌضوَّانْكَفِسُوْ‏ نَ‏ ماَذَا ازَاَدَهللاُ‏ تِهَرَا مَثَإلَ‏ كَرَنِكَ‏ يُضِمُ‏ هللا مَهْ‏ يَشَاءُ‏ وَيَهْدِي مَهْ‏يَشَاءُ‏ وَماَ‏يَعْهَمُ‏ جُىُدَ‏ زَتِّكَ‏ االَ‏ هُىَ‏ وَمَا هِيَ‏ اِالَّ‏ ذِكْسَي نِهْثَشَسِِ‏Basi ni vyake yeye Mnyezi Mungu vyote viliomo Nyoyoni naRohoni na kwingineko, katika ulimwengu wa majeshi (yalowekwatayari tayari kwa wingi).Tukijihusisha kwa majeshi ya Nyoyoni, tutaona kua yako mawilijeshi ambalo linaonekana kwa macho jeshi ambalo halionekani kwamacho – ila kwa wale wenye kuona kweli kweli. Amma katikahukmu, ni kama mfano wa nyuki, ambako kuna Mfalme, Majeshi,Watumishi, Mawaziri, Hal-mashauri, na wasaidizi. Hii ndo maanaya jeshi. Jeshi (l) ni kama lifuatalo:MkonoMguuJichoSikio50.

Ulimi na viungo vingine vya dhahir. vyote hivyo vinatumikia Moyokwa sababu Mnyezi Mungu ameshavisakhirisha kwa ajili yake(Moyo) na katika kutekeleza amri vinafanana na Malaika waMnyezi Mungu ambao hawaasi hata siku moja na hufanya yaleambao wameamriwa. (Tafauti na itikadi za baadhi ya watu ambaowanaamini kua Malaika wanaweza kukhini, na wakafikiliza amritofauti na vile walivyoamriwa na Mola wao).Kiwiliwili ni Marikebu ya Moyo, na ndicho ambacho hukipanda, nakuuzidisha ilmu na kumakinisha sawa-sawa. Basi mwenyekujifanzia zawadi Moyo wake, maslahi yake baadae – hua ametimiaAkili.Miongoni mwa askari wa (ii) Ba-tini ambao hawaonekani kwamacho ni matundu ya ubongo – Dima-gh (Cerebruim, cerebellumna medula Oblongata).1 . Mtu baada ya kuona kitu (jambo) hukifutika na (kuipata) kuijuasura ya kitu kile ndani ya nafsi yake kwa njia ya khayali (mfano wamwenye kutoa) sura ile hubaki nayo katika kumbukumbu.Anaeisababisha kua hivyo ni askari wa kuhifadhi.2 . Kisha hufikiria kile alokihifadhi ambapo hua mwenyekukipandanisha baadhi kwa baadhi. Ikiwa iko haja anawezakurejea sura yote akaikusanya pamoja ili ajenge maana kamiliyenye kuweza kuhusika ndani kwa ndani au kuzishirikisha vileapendavyo katika tandhimu (utungo) hii inapatikana:-Tafakuri.Kumbukumbu.Hadithi.Na Kupinga picha (khayali).Na lau Mnyezi Mungu hangeumba Askari khao, basiubongo (Brain) ungeachia, si ajabu kila kitu cha maana ambachokingeachiwa kwa muda.MFANO WA MTU NDANI YA KIWILIWILI:Mtu anapokuwa ndani ya kiwiliwili anakua na mfano waMfalme katika Mamlaka yake ametulia kabisa. Jina ki - wili-wilipeke yake linamfahamisha kila mwenye Akili ilosalimika kua nivitu viwili, Sio kimoja. Ni umbo lenye jingine ndani yake. Na ndomaana siku ya kufa Mtu akaachana na kiwiliwili chake, kiwiliwili51.

huanguka na yeye Mtu hujitenga akenda kwengine (Barzakhyaanipahali pa mapumziko na mateso ya muda tu hadi kufikasiku ya kiyama na siku ya hukumu).viungo na nguvu za ndini:Hivi, kwa upande hua ni silaha, lakini kwa kweli niwahandishi (San-nai) kwa mambo.Kiwiliwili:Akili:Ni mfano wa Mji, Marikebu, ambayo Moyoimependa.Mfalme mwelewa, na nguvu zake zinatokana nahawasi za dha-hiri na ba-tini ambazo ni kama Askariwake, na Viungo ni kama Raiya.Na hata Bwana Mtume Saw alikua na maana kubwa aliposemajuu ya viungo kama:-Nguvu za Akili“Kullukum ra-in-wa kullu ra-ni mas-uw-lunan raiyyatihi”.“Nyote ni wachunga (khalifa) na kila mchunga nimwenye kuulizwa kwa vichungwa (raiya ) vyake”.Nguvu za kufikiri.Matendo – A`maliHao ni halmashauri na ni Mawaziriwake Mtu.ADUI ZAKE MTUShah-wa:Ghadhabu najoto lake:Yaani matamanio ya Nafsi, ni mtumishi muovusana ambaye kila mara anaazimia kumuhilikishaMtu. Hana wema hata mara moja juu ya Mtu, nadaima husubiana na Sheytwan-rajiim.Ni kama Askari muongo, hadaa zimejaa tele na nikhabithi kweli kweli. Daima hujifunza Mtu mzuri52.

wa nasaha wakati chini ya nasaha yake iposumu kali yenye kuweza kuua mara moja.Ujinga:Fidhuli ndani ya mji na nje yake – yeye huharibu kilahatua yenye sura ya kuendelea. Na daima hua peke,kwani kila anaemsogelea humkwepa.Bwana Mtume Saw amesema:“Ja-hil ni adui wa Nafsi yake mtu, vipiatakua rafiki wa mwengine?”.Chuki na husda: Hawa ni katika maadui ambao hua ni ugojwawenye madhara mazito yenye kufwatiliza kuhilikikwake mtu mara moja. Na mwisho ni:-Nafsi:Ambayo kama isipotayarishwa vile ipasavyo hasa,basi haiwezi kuitwa Mtu mwanaume alie Kamilikayaani: Rijaal.WATU WA KWELI KWELI:Amma wanaofaa kuitwa Rijaal si (kwa ajili ya) ghasia tu urijalini kuweza kupigana na Nafsi yako ukiwa umo ndani ya(mapambano ya) kupigana ili mwishoni uwe Mtu unaekwendamwendo mwema. Hata Mtu mmoja anawataja watu wakubwaAnasema :“Humur rijaal”Wao hao ndio Rijaal – (Wanaume) wa kweli”“Wa-ayb-an yuqa-lu liman-lam yattaswif fi maaniwaswfihir rijaalu”.“Aybu kusema kwa mtu asie sifika na sifa zao, kuayeye ni Rajul (Mwanaume)”. (Kafiri awe Rijaal, Fa-sikawe Rijaal, Mujrimu awe Rijaal – Itakuwaje!!).Rijaal wanoshughulika na Mnyezi Mungu na Iqamu Swala-ti nakusimamisha Swala.Yakha-funa yaw-ma - Wanaogopa siku,53.

“Tataqallabu fii-hil qulub wal-abswa-r”.“Zitageuka ndani yake (ndani ya siku hiyo) nyoyo na maoni”.“Liyajzia – humu-Llahu kulla nafsin ma-amilat”“Mungu apate kuilipia kila nafsi kilichochuma (kila nafsiitalipwa kilichochuma)”.“Fa-man yaamal mith-qala dhar-ratin khayran yara-hu”“Mwenye kufanya uzito wa chembe ndogo ya kheri ataiona”.“Waman yaamal mith-qala dhar-ratin shar-ran yara-hu”.“Na mwenye kufanya uzito wa chembe ndogo ya shari ataiona”Anasema Mnyezi Mungu katika Hadithil Quds:-“Hakika si vingine, ni vitendo vyenu nyie wenyewe –Nakuthibitieni – Faman wajada khyran fal - yahmidulLah – Mwenye kukuta kheri na amshukuru MnyeziMungu–Waman wajada ghyra dha-lika falaa yalumuIlla nafsiha. Mwenye kukuta kisichokua kheri asilaumuila nafsi yake”Kila Mtu atapewa chuo chake,“Iqra-a kita-baka”“Soma chuo chako - Soma daftari lako”.“Kafa binafsikal yawma alayka hasi-ba”“Utatosha leo wewe kujifanyia hesabu, huna haja hataufanziwe hisabu na mwenginewe (utatizama mwenyewe)”.“Manih tadaa fa-innama yahtadi linafsih”.“Mwenye kuongoka (akiwa sehemu nyingine) ndo anaongokakwa sababu ya nafsi yake”.“Waman dhal-la innama yadhil lu alayhi”.“Mwenye kupotea anapotea juu ya Nafsi yake mwenyewe”.“Walaa taziru wa-ziratu”“Habebi mwenye kubeba”.54.

“Wizra ukhra”“Mzigo wa Mtu mwingine”.Kila mmoja atakuwa na yake. Lakini tuamrishwa tukionyana, natukikumbushana na tukisaidiana katika kheri. (Mafanikio yakokatika kheri yatategemea) kufwatia (kwako) kheri (na) kua pamojana watu wema:“Ya-ayyuhal ladhina a-manut-taqul- laha”“(Enyi ambao mumeamini), mcheni Mnyezi Mungu”“Wa-kunu – maa-swa-diqi-na”“Muwe pamoja na wakweli”.55.

MNYEZI MUNGU, BINAADAMU NAMAUMBILE:Mnyezi Mungu aliyetukuka ametengeneza na kujaalia kitu kwaajili ya Binaadamu, na Amemtengeneza Binaadamu kwa ajili yakeyeye.Na ajaribu Mtu kuhisabu, kuanzia popote pale alipo ataonakua kila kiliopo mbele yake kimekusudiwa yeye. Hiyo ajabu kubwana neema isiokua na kipimo maalum. Ukiacha hayo yote ukatizamayaliokaribu zaidi, utaona Mnyezi Mungu pia amekuumba,akakuekea macho, na maono (Baswari) na jamii ya viungo ambavyosi mgeni navyo kwa sababu viko mwilini mwako. Na wako ambaoMnyezi Mungu mwenyewe amewanyima, basi ni kwa Hikma yakeamefanza hivyo, sio kwa dhulma. Kwani yeye hawi mwenyekudhulumu Mtu, au kiumbe.Basi baada ya kuumba kila kitu kwa ajili ya Mtu(Mwanaadamu) Amemuumba Mwanaadamu kwa ajili ya MnyeziMungu (Mwenyewe) na ndo maana akasema katika:Qur an: Suraul Bayyinah: 98:5.“ Wala hawakuamrishwa ila kumuabudu MwenyeziMungu kwa kumtakasia Dini, wawache Dini za upotofuna wasimamishe Sala na kutoa Zakah – Hiyondiyo Dini iliyo sawa. (Nao wameikataa)”.Kwa ushahidi huo, ni yenye kuonyesha kua saa yeyote ileanapokengeuka na yule ambaye kwa ajili yake ndo ameumbwaanakua katika makosa ya kuchukiza kabisa, na hasa ikiwa anajua(sio mjinga ambae anaishi mbali na mji au jijini). Umekwisha patafununu nzuri ya kujijua wewe ni nani na kuja kwako hapa duniani nikwa madhumuni gani. Kwa hivyo, mpaka kufikia hapa wewe siomjinga tena. Na ikiwa haya yaliomo ndani humu si yenye kutokakichwani mwangu kwa matamanio ya Nafsi, yangu bali ni56.

mafundisho walofundisha maulamaa ambao ndo warithi wa MtumeSaw. Basi kitabu hii kitatosha kua shahidi juu yako YawmulQiyama (Qiyama). Sasa ilobaki ni kuzidi kujiendeleza na kuyatiamajaribuni yale ulokwisha yajua ikiwa ni pamoja na haya yafuatayohapa:KUACHA YALOHARAMISHWA:Undani wa suala hili si mzito sana, kwa sababu:-i. Mnyezi Mungu hakuamrisha jambo lolote ila linafaidaii.na maslahi na Mwanaadamu; naHakukataza jambo lolote ila lina hasara na madhara naMwanaadamu.Mfano wa Kamari - Ukicheza ukapata basi kwa vile ni tendolilokatazwa na Mnyezi Mungu pato lake litakua ni haramu na kulayake, vaa yake, na zaa yake itakua ni haramu. Na twaa ya Mtuambae vitu vyake ni vya haramu haisimami. Hukumu yake ni kamakuweka msingi juu ya maji ya bahari.Maafa ya kamari ni makubwa, na zaidi hua si ya khasara tupeke yake, bali yana madhara, wenye kufutwa (Kuliwa) aghlabuhupigana na pengine huua, kwa ghadhabu. Katika kamari nyinginewenye kufutwa huwarubuni wake zao wakawaacha siku mbili tatumpaka kumudu kuwakomboa, huo ni Udayuthi. (yaani ni kukosaari), na kila Dayuthi mwisho wake ni kuingia motoni.Mnyezi Mungu hakumuumba Mwanaadamu akampenda,akamtukuza juu ya viumbe vyote, ili aje amtie motoni – Hasha.Mfano mlevi - Amekatazwa kuukaribia wacha kuunywa; kwanigha-lib huharibika akili ya Mtu, ukiwa Mtu hujui nini usemalo. Napengine ukazusha ugomvi na kuumizana. Na mwisho ukipatausingizi hujui nini lipitalo, na hata ukijua unabaki kupayuka payukatu. hayo yote ni maafa makubwa. Mnyezi Mungu anasema katika:Qur an: Suratil Baqara: 2:219.57.

“Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari, sema: katikahivyo mnamadhara makuu na (baadhi) ya manufaakwa (baadhi) ya watu. Lakini madhara yake nimakubwa zaidi kuliko manufaa yake. Na wanakuulizawatoe nini? Sema: “Vilivyokuzidieni.” Namna hiviMwenyezi Mungu anakubainishieni Aya (zake) mpatekufikiri”.Na kwa nini amali mbili hizi zina madhara makubwa mno? Sababusi nyingine isipokua ile ya kua kwake fungu katika mambo yasheytwani, Mnyezi Mungu anabainisha hivyo katika:Qur an: Suratil Ma-idah 5:90.“Enyi Mliomini! Bila shaka ulevi na kamari, nakuabudiwa (kuombwa ) asiyekuwa MwenyeziMungu, na kutazamia kwa mishare ya kupigiaramli (Na kwa vinginevyo) (yote haya) ni uchafu(na) katika kazi ya sheytani. Basi jiepusheninavyo. Ili mpate kufaulu (kutengenekewa)”.Mfano wa Kuzini: katika kijishughulisha na wanawake tu kwakuzini nao, badala ya kuoa ukatulizana au na baada ya kuoa piaukawa unazini – basi huko ni kuutumia mwili vibaya, nakuudhoofisha afya na nguvu hupungua sana. Kwani walopimamchupo wa manii, wamegundua kua katika kila tone moja kunamatone sabini ya damu. Damu ni kitu azizi ndani ya mwili, nayo iliipatikane kwa wingi unotosha kutuweka katika hali ya afya,tunapaswa kutumia vyakula vizuri ambavyo tunavinunua toka58.

sokoni na madukani.Zinaa ni za namna mbiliYa kwanza: Ni ya mwenye kufanza hali ya kua na Mke (au Mume)na ile ya mjane (Bechula) au (Aazib). Ya kwanza ndo yenye dhambizaidi na hata adhabu yake ni nzito zaidi, kwani ni lazima apigwekwa mawe ndani ya handaki mpaka afe.Ya pili: Ni ya kupigwa mijeledi Mia moja. Na zinaa ya macho,katika kutizama Mwanamke asie kuhusu.Lakini vyovyote itavyokua, Bwana Mtume Saw anasema:“Azzinaa Yuw rithul faqr”.“Zinaa inarithisha ufukara”.Na ukichunguza kwa uadilifu hutokosa kuthibitisha kauli yake hiyokuwa ni kweli.Mfano wa Liwati na Kusagana (Maji ya ndimu). Liwati niaina ya fiili kati ya Mume na Mume. Badala ya kuoa Mke ambapondo iloruhusiwa na sheria, Mtu huoa Mume mwenzake pasinamanufaa yeyote bali kumwaya damu tu na kudhoofisha afya. Namaafa yake nayo ni makubwa, kwani wote hao hua na Laana zaMnyezi Mungu. “Ra-kib wal Marku-b” Mwenye kupanda namwenye kupandwa – wote hao.Amali mbaya hii ilianza wakati wa Naby Lut As.Haipungui miaka elfu sita nyuma, na ndo maana ikapewa jina hilo –Qawmu Luut- Basi watu wake waliangamizwa kwa kupinduliwa,chini juu pamoja na nchi yao.Amma kusagana ni kati ya Mke na Mke. Vitendoambavyo havielekei hata kidogo. Lakini kwa vitu vya Sheytani ndohupamba moto kati ya watu. Ni mambo hata wanyama hawafanzi,kwa hivyo, Mtu mwenye akili inataka afanze – jitihada aviachevitendo hivyo.Mfano wa kula Nguruwe Mnyama huyu mwenye mafutamengi mwilini na wadudu puani, anayo tarikh ndefu. Na hapahatuna makusudio ya kumbainisha hivyo (Kitabu chetu: “Jua namiezi 24 – juu ya ujao wa Mitume 25” - Tumeelezea habari zakehuenda kikatoka – Insha Allah).Nguruwe ni namna mbili:Wa kwanza: Ni Mwenye kutokana na ubichi ubichi wa kinyesi.Wa pili: Ni Banii Israel (Binaadamu) walogeuzwa NguruweMaafa yake ni makubwa, lakini yenye madhara sana hakuna kama59.

Udayuthi (yaani kuondokewa na ari). Na inatosha kumchunguzaNguruwe mwenyewe katika maisha ya ngono. Nguruwe wanawezakufanza fiili mbele ya Nguruwe mwenzao bila kuingiliana kati kamawalivyo wanyama wengine, ambapo huzuia kufanzika kwake –labda waende mbali huko wasikoonekana na wenzao.Basi na kila mwenye kumtumia mwisho wake hivyo naMnyezi Mungu hapendi Mtu akose Ari. Kwa hivyo katika kuachayalo haramishwa kutapatikana fursa nzuri, si ya kujitakasa tu bali yakujenga Taqwa. Mfano mdogo tu unaonekana katika:Qur an Suratil Maidah: 5:93“Si dhambi juu ya walio amini na wakatenda memakwa vile walivyovila (kabla ya kuharimishwa)madamu wakimcha (kwa vile alivyowaharimishiawakati huo) na wakiamini (alivyowaamrishawakatihuo) na wakitenda mema…”“Thummat taqaw wa-amanu thummata-qawwa ahsanu wal Lah yuhibul muhsiniina!”.“Tena wakamcha (vile vile alipowakataza makatazomengine) na wakafanya mema (mengine alivyowaamrisha) na Mungu huwapenda wafanyao mema)Huo ni mfano mdogo tu ambao unaonyesha vipi hali yaMasahaba ilivyokuwa ya khofu kubwa kwa Maswahaba wenzaowaliokwisha kufa kabla kutelemka Aya hiyo, hali ya kua wakinywapombe. Ni katika mwaka wa sita wa Al hijra zama ilipokatazwamno kunyewa pombe, lakini Mola Sub hana wa Taala ni muadilifualibainisha wazi kua: Laysa jun-ahun – Si dhambi - kwao ambaohawakudiriki amri ya makatazo.Na katika mabaya yaloharamishwa ni mfano wa Riba,yaani kukopesha kwa masharti ya kulipa zaidi baadae, ambapodaima huiliki mkopaji. Mnyezi Mungu ameiharamisha amali hiyo naameikaripia sana sana kiasi cha kusema yeye yuko katika vita na60.

Yeyote alae Riba, kwani makamio yake ni katika daraja moja nawanyang`anyi wa kuuwa na maharamia.Suala hili ni refu na zito sana, lakini inatosha kulielewakwa ufupi, kiasi kile ambacho Mnyezi Mungu mwenyeweamekielezea katika baadhi ya Sura za Qur an kama ile ya:Qur an: Baqara: 2:275 – 280.“Wale wanaokula Riba, hawasimami (kuendesha yao)ila kama anavyosimama yule ambae Shetani kamzugakwa kumsawaa – (Wao mbioni tu hawana kituo). (Na)haya ni kwa sababu wanasema Biashara ni kama Ribahali Mnyezi Mungu amehalalisha Biashara naameharamisha Riba. Na aliyefikiwa na mauidha kutokakwa Mola wake (ya huku kukatazwa Riba ), kishaakajizuia, basi yamekwisha mthibitikia yale (mali)yaliyopita (aliyokwisha yapata: na hukumu yake ikokwa Mwenyezi Mungu . Lakini wanaorejea (kula Riba)basi hao ndio watu wa Motoni, humo watakaa milele”.“Mwenyezi Mungu huyafutia (baraka mali ya) riba; nahuyatia baraka (mali yanayotolewa) sadaka, na MwenyeziMungu hapendi kila kafiri (na ) afanyae dhambi.61.

“Hakaika wale walioamini na kufanya vitendo vizurina kusimamisha Sala na kutoa Zaka, wao watapataujira wao kwa Mola wao, wala haitakuwa khofu juuyao, wala hawatahuzunika”“Enyi Mlioamini mcheni Mwenyezi Mungu, naacheni yaliyobaki katika Riba, ikiwa mmeamini”.“Na kama hamtafanya (hivyo), basi fahamunimtakuwa na vita na Mwenyezi Mungu. Na mkiwammetubu, basi mtapata rasilmali zenu; msidhulumuwala msidhulumiwe”.“Na kama (mkopi) ana dhiki, basi (mdai) angojempaka afarijike. Na kama nyinyi (mnaodaimkizisamehe deni zenu) mkazifanya sadaka,62.

asi ni bora kwenu. Ikiwa mnajua haya (basifanyeni)”.Katika utawala wa Kiislamu amal hii hupuuzwa na kuondoshwakabbisa kabbisa; na kufikia hata kuuawa ambae anakopesha kwafaida au kufungwa jela mpaka atoe maelezo ya kukoma kufanzakazi hiyo (Tazama maelezo yake katika tafsiri ya Qur an kwakiingereza, ya Abul Ala Maudud. Vol: 1. Page: 72).Na miungoni mwa mambo matatu ambayo Bwana Mtume Sawalipendelea apate miangaza zaidi juu yake - Ribaa ni moja wapo.Lakini hakuwahi – (Tazama pia maelezo yake, katika tafsiri yakiingereza ya Sheikh Yusuf Aly. No. 324, sahifa No. 111).Kadhalika na katika mifano mikubwa ambayo ni maarufu kwako,lakini unaipita bila ya nadhari ni ile ya: Kuuwa bila kukusudia(Fatal Accidents/Manslaughter).Amma kuua kwa makusudi tena Muislamu mwenzako, jazaa yakeni Jahannam, kama ilivyoelezea aya 93, ya Suratil Nnisaa ambayoSheikh Abdallah Swaleh El Farsy ameielezea vizuri khabari zakekatika ukurasa wa 124 wa Tafsiri yake.Lakini kuua bila kukusudia, mfano wa waendesha magari auwawindaji na kama hivi, wajue ya kwamba watatakiwa kuacha hurumtumwa mmoja, au kama hana anunue, kisha awalipe Diya watu wamarehemu. Na hiyo Diya ilokusudiwa na Mnyezi Mungu ni Ngamiamia moja, au thamani yake kama hazipatikani. Laa ikwa aliyemuuaakiwa ni Muislamu, lakini jamaa zake ni makafiri wanaopingana naWaislamu, basi itampasa ile haki ya Mnyezi Mungu tu ya kumfanyamtumwa huru. Tafauti na ikiwa makafiri wenyewe si wenyekupigana na Waislamu (haya yalihusika zama za vita vya Uhud,wakati Waislamu walipofadhaishwa na makafiri baada yakuzungukwa ikawa hawajui Waislamu wepi na makafiri wepi, kwahio walitokea kuuana kwa bahati mbaya).Bwana Mtume Saw alikadiria diya kua Ngamia 100, auNgombe mia mbili au Mbuzi Alfu mbili au Dinari 800 za Dhahabuau Dirham ya Fedha Alfu Nane.(tazama Maududi katika tafsiri yakeya kiingerezapage 157). Na anapokosekana mtumwa, basi nikufunga miezi miwili ya kufwatana, ambapo udhuru wa kufungaSwaumu ya kawaida hautatosha katika Swaumu hii ya toba. Naakiacha basi italazimu aanze upya.Basi lazima tuelewa ya kua faini zinazotolewa mahakamani63.

Hazitatosha kumkomboa mtu na dhima mbele ya Mnyezi Mungu.Ni lazima pia tutoe na faini ya Mola.Mifano ya mambo ya haramu mingine ni ile ya Uongo naKudanganya – Ghushi, ambayo Bwana Mtume Saw amesema juuyake kama vile:“Man ghaash-sha falaysa min-na”.“Mwenye kudanganya (ghush - Cheating) sipamoja na sisi (si katika – sisi).64.

UNDANI WA KUTEKELEZA FARDHI:Qur an: Baqara:2 : 110.“Na simamisheni Swala, na toeni Zakaa na kherimtakazozitanguliza, kwa ajili ya Nafsi zenu,mtazikuta kwa Mwenyezi Mungu anayeona(yote) mnayoyafanya”.Swala na Zakaa ni miungoni mwa Fardhi alizotuwekea MnyeziMungu, kama alivyowawekea waliotangulia kabla yetu wakatiUislamu haukua umekamilika. Baada ya Swala na Zakaa, zinafwatiaSwaumu na Hajji.Amma Swala ni dua, au maombi kwa Mnyezi Mungukiunganisho kati ya Mja na Mola wake. Na pia ni Ibada mahsusiilioekewa nyakati zake mahsusi, na ndiyo ifarakishayo bainaMuislamu na Kafiri. Anaeacha Kuswali – hua Kafiri wa kweli kwahadithi ya Rasuli – Tahadhari nakwambia.Zakaa ni kutoa fungu maalumu katika mali iliyowajibikiazakaa juu yake. Na kuitoa kwa mwenye kustahiki. Fungu hilolinaweza kuchukuliwa kwa nguvu kwani sio lake Mtu, bali ni laMnyezi Mungu.Na Hijja ni kuikusudia Nyumba ya Mnyezi Mungu (Makka)kwa Ibada walau mara moja katika uhai; kwa mwenye uwezo (hasafedha) wa kwenda.Uchache wa Faradhi ni huo, na kwazo, unapatikana Uislamu.Lakini kwa vile hawezi asiyekuwa Muislamu, baleghe mwenyeakili, kupokelewa amali (zake) zozote katika hizo. Imelazimikakutamka “Laa ilaha illal lahu Muhammada Rasulullahi” (Kwawakati huu, kwani kwa zama za Nabii Isa As ingebidi iwe: “Laa -65.

Ilaha illal - lahu Isa Rasulu Llahi” au Yahaya, Zakaria, Musa,hadi Adam – Rasulu Llahi).Katika tamko hilo ambalo hujulikanwa kama: “Shahada mbili”Ipo maana nzima ya “Tawhiid” yaani kumpekwesha MnyeziMungu (Divine Unity) Neno hilo ni zito sana na si kutamkwa kwaulimi tu peke yake, bali kwa Moyo (ule ambao ndio wewe mzimamzima Roho, Nafsi na Akili). Na hivyo ndio kukira kwa kweli,ambako matokeo yake hua kama hivi: Kafiri hua Muislamu.Hupanda Daraja ya juu toka chini . Huwa Mrehemewa badala yaMbughudhiwa. Huvuta mapenzi ya Muumba badala ya chuki zake(Sakhtwa). Humkimbiza Shetwani akawa mbali na Moyo wake Mtu.Lau baada ya tamko hilo unafikiwa na Mauti, basi kwa hadithiya Bwana mtume Saw, unakwenda peponi duna shakki- pasi nashaka yeyote ile, kwa sababu neno hilo lina uzito katika mizani kiasiambacho si mbingu na ardhi , wala Arshi na Kursi na Dunia zote,ambazo uzito wao unaweza kuinua “Laa Ilaha Illa Llahu”. MnyeziMungu Anasema katika:Qur an: Suratil Qaariah: 110: 6-9.Basi yule ambae mizani yake itakuwa nzito.Huyo yuka katika maisha yanayompendeza”.“Na yule ambaye mizani yake itakuwa nyepesi.Huyo maskani yake yatakuwa katika (huo moto )Hawiya”.Aya hii halikadhalika inawasaidia waumini kutatua mfano watatizo la waliokufa wawili bila kutambulikana majina anwani yaona Dini. Nguo sare, nywele sawa, na wote wamevaa vidani bangilina herein sikio moja (mfano wa vijana wetu wa kileo ambaowameacha nyendo za Jadi zao na Dini yao na kufuata utamaduni wakigeni ambao lengo lao ni kuudhoofisha Uislamu unaoingia kwakasi Duniani. Lakini hakuna wa kumudu kuuzuia au kuupiga vita(Basi inatumiwa mbinu za namna hiyo ili vijana wetu wawe66.

Wenyewe waharibu nchi (Dini) lakini Dua za Waislamu zitawavutaInsha Allah wazinduke wao wenyewe waipiganie Dini yao zaidi yavile wanavyopigania kuunga mkono mambo ya wageni ambayohayawahusu ndewe wala sikio. Haimkiniki kuwa baada ya kujuakutokana na mafunzo ya Dini: Amelaaniwa Mwanamume anaovaavazi la kike, na Mke avaae vazi la Kiume bila udhuru wa sheria,kisha awe yeye ndo wa mwanzo kupinga amri hiyo ya MnyeziMungu na Mtume Saw). Yule mzito ndo Mwislamu na kafiri hataakiwa Mnene vipi atakuwa mwepesi tu.Basi sharti ya Shahada Mbili itapatikana, ndo sasa inafwatautekelezaji wa Fardhi kwa vitendo. Amma fardhi iliyo kubwa sanakatia Uislamu baada ya shahada mbili, hakuna kama Kuswali.Qur an Suratil Hud:11 : 114.“Na simamisheni Sala katika ncha mbili za mchana(Nayo ni Adhuhuri na Laasiri) na nyakati za usikuzilizo karibu na mchana (Nayo ni Magharibi na Isha –ziko karibu na mwisho wa mchana, na Al fajr ipokaribu na mwanzo wa mchana). Hakika memahuondoa maovu huu ni ukumbusho kwawanaokumbuka. ( Haya ni mawaidha kwawanaokubali kuwaidhika)”.Katika kuswali umo Uislamu wote; kwa maana ya nguzo zaUislamu Tano:-1. Shahada mbili, Sawa na kusema kwa Kiarabu “Ashhaduan laa ilaaha illal Lahu”. Maana yake: “Nakiri kwaMoyo ( wewe binafsi yako na Roho na Akili yako) nakubaini kwa ulimi kuwa hapana wa kupasa kuabudiwa kwahaki illa Mnyezi Mungu “Wa Anna MuhammadunRasulul Lah” ( Na ninakiri kwa Moyo na kubaini kwaulimi kuwa) Hakika ya Muhammad ni Mjumbe wa MnyeziMungu.2. Kusimamisha Swala Tano,i. Asubuhi - Rakaa mbili.ii. Adhuhuri - Rakaa nne.67.

i.)iii. Al asr - Rakaa nne.iv. Magharibi - Rakaa tatu.v. Ishai - Rakaa nne.Wakati wake kwa siku za joto huingia saa 10.30. saa za msikiti(sio kwa saa ya Zone).ii.) Inaingia saa 6.30 ama saa7 mchana.iii.) Inaingia saa 9.30 ya Msikiti.iv.) Inaingia saa 12.10.v.) Inaingia saa 1.30 usiku.Na kila unapokurubia wakati wa Swala gha-lib huepo mwenyekuweta watu (Muadhini) kwenda Msikitini kwa ajili ya Ibada hiyo.3. Kutoa Zakaa. ( Nayo ni fungu maalum) la mali nakuwapa wale wanaostahili miungoni mwa Mafakiri,Masikini, wapiti njia, wanaozitumikia kugawa mafungu,wageni katika Uislamu, walopewa Uhuru, Wenyemadeni, Katika kuipigani (Dini) Uislamu.Mali zipasazo zakaa:1. Mali ya biashara ( Rasilimali ndiyo itolewayo Zakaa Shs.2.50katika Mia) Na baaada kupitiwa na mwaka, sio kila Ramadhani( kama wafanzavyo wengi wa matajiri kwa uchache wa elimu)utafikiri wote walianzia biashra tarehe moja, pia faida.2. Nafaka za punje punje zote kila gunia kumi, utatowa moja, nanusu yake kama umenyesheleza.3. Tende na Zabibu kila mizo mitano ( kiasi cha kilo 1000).4. Mbuzi na kondoo: zikifikia kiwango cha arubaini utatoambuzi jike wa mwaka mmoja (au Thaniyya mwenye miakamiwili). Na wakifikia 121 utatoa mbuzi wawili. Na 201 mbuziwatatu. Na 400 mbuzi wanne. Na wanaozidi kiwango hicho,basi kila mia utatoa mbuzi mmoja.5. Ng`ombe – kiwango chake cha Zakaa ni zinapofikia 30 –(Thalathini) utatoa ndama wa mwaka mmoja. Wakifikia 40ndama jike la miaka miwali.6. Dhahabu na Fedha: (Madini sio Fedha ya sarafu) ) Naisiyokuwa ya pambo la mke iliyo halali). Itapofika Mithqaliishirini. Dhahabu itatolewa Robo ya kumi. - Sawa na 2.50%.7. Zakatil Fitri: Hii hutolewa na kila Muslamu baada kumalizikaRamadhani na ambayo pia hujuzu hata kwa mwanzo waRamadhani. Lakini ilo bora ni kuitoa baina ya Magharibi ya68.

Usiku wa Iddi hadi kufikia al fajiri na baadae kidogo, lakiniisifikie hadi Kuswaliwa Sala ya Iddi – itakua haramukuichelewesha hivyo. Kuitoa kwake ni Vibaba 4 kiasi yaPishi au kilo 2 na Thuluth. Kwa kila anayekutegemea wewechakula (wengine wamejuzisha - awe Muislamu).(Kwa yote hayo tazama “HidayatulAtfal” kurasa wa 53 cha SheikhAl Amin bin Aly, na “Mahadi ya Fiqhi” juz 3 ukurasa wa 44 chaSheikh Abdul Jabbar).8. Madini na Rikazi: Utatolea baada kuuza, sio kungojaMwaka4. Kufunga Mwezi wa Ramadhani:Siku Thalathini – Isipokuwa mtoto mdogo, Mwendawazimu, Asiyekuwa Muislamu, Mwenye Edhi na Nifasi,Mzee, Mgonjwa na Msafiri.5. Kuhiji Makka:Kwa mwenye uwezo katika Waislamu, Mwenye Akili,Wakubwa na Huru – Kwani hizo ndio shuruti zake Hijja,Swaumu, Zakka na baadhi ya Ibada zingine ni miongonimwa zenye kupasa kujifundisha wakati wa shida. LakiniIlmu nyingi ni lazima saa yeyote uwe unajua amma sivyoitakuwa umemukhalifu Bwana Mtume Saw…..Uislamu ndani ya Swala:Amesema Bwana Mtume Saw:“Aswalatu Imaadud diin, faman aqa-mah aqaamaddiniin, Waman adhaa-aha afaqad hadamad diin”“Swala ni nguzo ya Dini, (basi) mwenye kusimamishaSwala, huwa amesimamisha Dini, na mwenye kuicha(kuipuuza – kuipoteza) hua ameibomoa Dini”.Hadithi hii inawafiki kiupande na maelezo yaliomo ndani ya Ayanamba 42 – 49 ya Suratil Al Mudath thir – 74.69.

Qur an: Al Mudath thir: 74: 42 - 49.Tafsiri yake inafululiza kama hivi:“Ni kipi kilichokupelekeni motoni? Waseme: “HatukuwaMiungoni mwa waliokuwa wakisali wala hatukuwatukilisha masikini. Na tulikuwa tukizama (katika maasia)pamoja na waliokuwa wakizama. Na tulikuwatukikadhibisha siku ya hukumu mpaka mauti yakatujia.Basi hautawafaa uombezi wa waombezi (wowote wale)”.Basi kwa nini wanapuuza onyo hili!? Swala imethibiti kuwa Ibadakubwa sana, sio kwa vile ndio Ibada aliyoipenda sana kuifanza kwawingi Bwana Mtume Saw, hasa saa za usiku hata ikamvimba miguuyake tu, bali kwa kusema kwake kua:“Amali ya kwanza kuulizwa mja siku ya hisabu niSwala, ikikutwa imetimia, basi zitakubaliwa napamoja na amali zake zote zilizobaki”.Kwa hikma tu itakudhihirikia kuepo kwa Falsafa nzito ndani yakauli hiyo na hakika yake. Anaposimama Mtu kuswali anahakikishakuwa hana mabaki ya chakula kwenye meno yake, kwa hadhari kua,kula ndani ya Swala huivunja kufaa kwake. Kwa tendo hilo anaswirimtu kuwa Swaim (Aliyefunga) nayo ndiyo Nguzo ya tatu yaUislamu na Swala yenyewa ni Nguzo ya pili. Katika kurukuu,Kuitadili ( yaani kurudi kusimama baada ya kuinama) na kwendaSijida hadi kukaa Tahiyyatu – ni moja amali zenye mfano wa Hijja,Nguzo ya tano ya Uislamu.Katika Atahiyyatu yapo matamko ya “Ash – hadu an laailaha illal Lahu wa ash-hadu anna Muhammadan Rasulullah”.Hiyo ni nguzo ya kwanza ya Uislamu. Na katika Kumswalia BwanaMtume Saw kutokana na hadithi yake kua:“Swalat alan Naby ni Swadaka”.70.

Na Sadaka ni mfano wa Zakaa inapatikana Nguzo ya nne yaUislamu. Basi mpaka akitoa salam mwenye Kuswali huaameutimiza Uislamu wote. Kwa hiyo ikikutwa Swala yake imetimiazitakubaliwa na Amali zake zote, inayo maana nzito.1. Kusubiri na Kuswali ni Ibada mbili pekee ambazo ni ngumu nanzito sana. Bwana Mtume Saw amisemea “Subra” kua hainamalipo ila pepo. Na mara kadhaa wa kadhaa Mnyezi Munguamewasifu wenye kusubiri, kwani Yeye Mnyezi Mungu huapamoja na wenye kusubiri. Basi mwenye macho haitajikuambiwa “tizama”.Mambo ya faida kama hayo hayafai kuyawacha, lakini piakatika kuyapapia haifai kujingikiwa nayo kwa hivyo ni vyemakuijua Subra ni nini, na pia Swala. Amma Subra kwa kifupiinatosha kuidala vyema baada yakuijua ilivyogawanyika kwakekatika mafungu manne.Kusubiri katika Twaa ya Mnyezi MunguQur an Al Imraan: 3:200.“Enyi Mlioamini subirini na muwashinde makafiri(katika kusubiri) na kuweni imara (nyoyo zenu)na Mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu(Kufuzu)”.2. Kusubiri katika maasi ya Mnyezi Mungu. Nafsi yako ina milikatika maasi, wewe ukapigana nayo ukaifunga.3. Kusubiri katika kadhaa ya Mnyezi Mungu. Na utaacha wapikusubiria yaliyokwisha kukadiriwa juu yako na hali una aminikuwa “Khayrihi wa Sharhrihi minal Lahi?”.Mnyezi Mungu Anasema:Qur an Suratul Baqara: 2:155 – 156.71.

“Na tutakutieni katika msukosuko wa (baadhi yaMambo haya). Hofu na njaa na upungufu wamali na wa watu na wa matunda. Na wapashehabari njema wanaosubiri. Ambao wapatapomsiba husema: “Hakika sisi ni wa MwenyeziMungu, na yeye tutarejea ( atatupa jaza yake)”.4. Kusubiri katika Akhlake (Tabiya). Tafauti za viumbevya Mnyezi Mungu, kwani wapo ambao hazipatani tabiazenu wala kulingana.Amesema Bwan Mtume Saw:“Mcheni Mnyezi Mungu popote ulipo – Na uendelezemema katika mabaya yako, yatafuta. Na ukae nawatu kwa Khulka nzuri”.Amma kwa upande wa Maarifa ya Swala inatosha kujua yakwamba imejengewa katika usafi kama ulivyojengewa Uislamumzima katika unadhifu.Kasema Bwana Mtume Saw:“Uislamu ni unadhifu, basi jinadhifisheni, kwanihaingii peponi ila mnadhifu”.Kwa hiyo ili iswihi Swala ya mtu ni lazima kuzingatia suala la:-Twahara: Kutwahirika (kutokana) na Hadathi ndogo (mkojo) nakubwa (Mavi) mwilini na kwenye nguo na pahala pakuswalia. Pia atwahirike najsi ipasayo kuoga (mfano waJanaba) Hedhi na nifasi.Janaba: Ni lenye kupatikana kwa kumuingilia Mwanamke auMnyama, kwa kadiri ya kichwa cha dhakar kiasi chakupotea ndani ya ule mzungo wa kichwa.72.

Hedhi:Nifasi:Ni damu imtokayo Mwanamke mkubwa, kila mwezi(Monthly period) naNi damu ya uzazi.Mwenye Kuswali awe amesitiri uchi wake, ambao ni baina yakitovu na magoti – na Mwanamke kiwiliwili chake chote isipokuwauso na vitanga vya mikono. Wakati wa kuswali uwe umeshaingia,na ajue mwelekeo (Kibla) iko wapi na atambue kuwa Swala niFardhi juu yako.Ili uhakikishe kuwa umejitayarisha sawa ni lazima kujuahukumu ya maji aina saba:a. Ya mvua.b. Ya kisima.c. Ya mto.d. Ya bahari na Ziwa.e. Ya thaluji.f. Ya barafu.g. Na ya chem-chem.Hukumu yake ni kuwa:a. Kidogo: ambayo hayatimii madebe kumi na mbili (yaaniQullaten) ambayo yanaweza kunajisika kwa kuingiliwa nanajisi, na ingawaje hayajaharibika rangi, harufu au tamuyake.b. Mengi: ambayo hayawezi kunajisika hata yakiingiwa nanajisi ndani yake. Amma yakibadilika rangi, Harufu autamu yake hapo yatakuwa mas-ala mbali.Udhu:Maandalizi ya Swala ikiwa ni madhumuni ya Mja kukutanana kuzungumza na Mola wake, ambaye pia ni Mola wa Dunia zote,yalotaalaki mno na usafi kwa sababu Mnyezi Mungu Mwenyewe siomchafu. Kwa hivyo kabla ya kufikia, hatua hiyo, na baada ya Mtukuepukana na iana zote za uchafu (najisi) mavi, mkojo,damu, usaha,73.

matapishi, pombe hata tone dogo tu au mnuso wa Mbwa naNguruwe ambao haisafishiki isipokuwa kwa kuoshwa mara saba(osha moja ikiwa limechanganywa na mchanga), janaba, hedhi nanifasi. Ataingia birikani kutawadha, na hata ikiwa ametoka kuoga.Na kutawadha kuna shuruti zake. Uislamu, na kujua halali naharamu (Mumayyizi) na ikosekane katika viungo vya kutawadhakitu chochote kizuiacho kufikilia maji kwenye ngozi (Mafuta, lamiau zafarani) na asiitakidi kuwa ni Sunna yeyote katika Faradhi zaUdhu ambazo ni Sita:i. Nia, hasa unapoanza kuosha mwanzo wa fungu katikauso.ii. Kuosha uso, ambao ni sehemu iliopo baina ya maoteoya nywele hadi mwisho wa kidevu, na kutoka sikio hadisikio.iii. Ni kuosha mikono miwili, au sehemu iliyobaki kamamkono ndo umekatwa labda. Kwa mkono mzima oshayako ifike hadi penye vifundo au kupita. Na kwa wenyemakucha marefu ambayo yangemudu kumficha mduduchungu ndani bila taabu, ataosha chini yake.iv. Ni kupaka kichwa kwa maji, na ni uzuri katikamipako mitatu uweze kuhisi kuwa maji yamegusa ngoziya kichwa. Baadhi ya watu hupitisha dharau katikakupaka maji kichwa, na hasa wenye nywele ndefuambazo kwa mujarrad hujitingisha tu nazo huwezazikajigawa ikawa katika mpako wa pili zile zilizojigawahazipati tena nafasi ya kusibu maji – udhu hautafaa(swihi). Na usipofaa udhu haifai Swala.v. Kupaka maji miguuni, mpaka kwenye kifundo chamguu.vi. Ni taratibu, yaani utawadhe kwa mpango sio kwambamradi vipate maji vile viungo vinihusika tu basi – laa,haitatosha.Ni Sunna katika kutawadha kutanguliza mswaki, ila baada yakulingana jua kwa mwenye kufungu. Kuosha vitanga viwili vyamikono ambavyo kwa nia pengine huchukua mahala pa kata, uoshekabla kuitumbukiza ndani ya chombo chenye maji kidogo, (Nuia:SunnatiIghtirafi – Nanuia kuyachota maji kwa mikono yangu).Kupiga “Bismillahi” mbele ya kila kitu. Pia kusukutua, kupanza74.

Maji Puani, kuosha kichwa chote na masikio mawili nje na ndani.Kuasua vidole vya mikono na miguu. Kuasua ndevu nyingi nakutingisha pete. Ni Sunna kutanguliza kulia juu ya kushoto, nakufanza mara tatu tatu pamoja na kufawatanisha matendo yotepamoja na kujisugua kabla kuleta Dua ya Udhu ambayo ni:“Allahumma jalni minal taw-waab-ii na.“Mola wangu nijaalie miungoni mwa wajawako wenye kutubia mbele zako.“Wajaalni minal mut-twah-irina.“Na unifanze mimi kuwemo miungoni mwawaja wako waliosafika”.“Wajaalni minal Ibadikas-swa-lihiin”“Na unijaalie mimi kuwa miungoni mwa wajawako walio wema”.Pengine udhu wako huweza ukavunjika kabla kuanza kuswali,kwa kudhihirikiwa na moja ya mambo manne haya:1. Kutokwa na ushuzi au chochote katika tupu ya mbele aunyuma.2. Kutokwa na akili hata kwa kitambo kidogo, imma kwawazimu au kuzimia au ulevi au kwa usingizi. Tofauti naambaye amekaa akiambatanisha makalizi yake (matako)kwenye ardhi.3. Kugusana na mwanamke min-ghairi ya kuwepo kizuizichochote katikati (tafauti na madhehebu mengine).4. Kujigusa dhakar kwa matumbo ya vidole vya mikono.Lakini ikiwa umesalimika na hayo yote, basi utaingiakuswali bila taabu yeyote.SwalaNdani ya Ibada hii mabayo ni muhimu mno katika mzunguko aulile duara la Uislamu, ni lenye shuruti za kufaa kuziangalia sana kwasababu bila ya kuzijua mbele huenda ukawa huna hata cha kulipwa75.

chochote. Mnyezi Mungu anapendelea ufanze amal zako kwa ujuzi,kama tilivyokwisha tangulia kusema. Basi shurti zake ni kamazifuatazo, ambazo kwa idadi ni kumi na saba:Shurti za Swala:1. Kusimama kwa mwenye kuweza.2. Nia, nayo ni kusema: “ Uswalli fardhis-swalaatis sub-hirakaa teyni”. Ni Swala ya Sub-hi (laa Swala nyingine basiutaitaja hivyo Swala na Rakaa zake)3. Takbira ya kuhirimia Swala, nayo ni kusema (baada yaneno Rakaa teyni au idadi yenyewe katika Swala) “AllahuAkbar” kwa sharti, usivute alifu tukufu kiasi cha kusikikakama “Aa-llahu”. Wala usivute “Hee” kisi cha kusikikakama “Aallaahuuw” utafikiri iko “Waw” mbele yake. piatamko la “Akbar” lisitamkwe ovyo ovyo, mfano wakulegeza ulimi hata ikazaliwa “Waw” baina “Allaa”“Hu-wa-akbar” au usivute “Be” kiasi cha kusikika kamahivi: “Akbaa-ru”. Swala haitasihi na kama u-maamumabasi jambo la maana ni kupitisha nia moyoni ya kumkhalifu(kuachana naye Imam nawe utakuwa hapo hapo safunilakini unaswali peke yako – Utapa fadhila za jamaa kamakawaida).4. Kusoma Suratil Fat-ha pamoja na “Bismillahi” ikiwa niaya amma sivyo katika aya ya saba “Ghayril maghudhubialay him” – Lazima uifanze ndo aya, na “Walaadhdhwaal-liin” aya, wakati pamoja na “Bismillahi” hizozote hua ni aya moj tu.Shuruti za kusoma Fa-tiha:Nguzo hii ni yenye nguvu sana kwa sababu hata ukisomaSura 113 uiwache Sura hii, Swala yako haitafaa, kinyume nakuwacha kusoma hizo (Sura zote 113) ukasoma Fa-thia, Swalaitafaa.76.

Herufi za Suratil Fa-tiha ni 156 pamoja na kusoma“Maaliki” kwa alifu (kama alivyoelezea hivyo Seyyid Abu Bakarbin Abdillahi bin Abdur Rahman bin Sumeyt el Alawy Sherehe ya“Tiryaaqin Naafii” - Babu ukurasa wa 32), kwani haijuzukupunguza hata moja katika herufi hizo.Ni sharti ya nguvu sana kuzitoa “Tashididi” (au lama yakukaza) zake zote 14.1. katika Lam ya Bismillahi.2. katika Ree ya Rrahmaani.3. katika Ree ya Ar rhiim.4. katika Lam ya Al-hamdulillahi.5. katika Bee ya Rabbi.6. katika Ree ya Ar rahmaani.7. katika Ree ya Ar rahiimi.8. katika Daal ya Yawmi-diin.9. katiak Yee ya Iy-yaaka-naabudu.10. katika Tee ya Iy-yaka nasta-iinu.11. katika Swa-d ya Swiraatal mustaqiim.12. katika Laam ya Lladhina.13. katika Dhwa-d ya Dh-dhwaa.14. katika Laam ya Lliina.Katika Sharti zake ni kukosekana kuisoma “Ddhaad” kwa“Dhwaad” amma sivyo haitaswihi kusoma kwake na isiposwihi,Swala pia haitafaa, na hiyo ndo khatari ikiwa atakusudia kusomahivyo na hapo Swala yake haitabatilika. Ingekuwa jambo la maanasana lau Maimamu wa Misikiti wangekuwa wakichukua hata dakikatano kila siku kuwaelimisha watu mambo haya, kwani yule ambayehaipatii vizuri atakuwa ameilimika akipata mawaidha ya dakika tanohizo.Na imesunniwa baada Kuhirimia Swala, (Sharti ya tano)kuleta dua ya kufungulia Swala, kama hivi:“Waj jahtu Waj hiya lil-ladhi Fatwaras Samaawaatiwal Ardhi, Haniifan Musliman wa maa ana minalmush-rikina anna S-swalaati wa nusuki wa mahyaa-yawa mamatti lillahi Rabila a-lamiin laa shariika Llahuwa bidhalika umirtu wa anaa minal Muslimina.77.

5. Kurukuu.6 Kujituliza, kiasi cha kusema “Sub-hana Rabbiyal adhwimi wa Bihamdihi” x 3.7. Kuitadil, (kurudi wima) huku ukisema: “SamialLahu limn hamida” x 3. (Maamuma atasema: “Rabbana lakal hamdi” kwa kifupi).8. Kujituliza, ndani yake.9. Kusujudu mara mbili.10. Kujituliza.11. Kitako, baina sijda mbili.12. Kujituliza, ndani yake.13. Kitako ajili ya Tashahudi.14. Tashahudi katika kitako cha mwisho (yaanikusoma Tahiyyatu).15. Kumswalia Mtume Saw.16. Kutungamanisha (Taratibu).17. Kutoa Salamu, kulia na kushoto unageuza usowako.Mwenye Kuswali akiacha nidhamu hiyo kusudi, mfanoakitanguliza nguzo ya kitendo - kama Kusujudu kabla ya Kurukuuna kuitadili, basi Swala yake itavunjika.Basi ipo maana nzito na yenye hakika na ithibati kamamwenye kauli ya Bwana Mtume Saw:“Amali ya kwanza kuulizwa mja, siku ya hisabuni Swala ikikutwa imetimia basi zitakubaliwa napamoja na amali zake zote zilizobaki”.78.

UNDANI WA KUTEKELEZA WAJIBATI:Ni wajibu wa kila mja, sio Muislamu tu kumjua MnyeziMungu. Lakini katika Kumtambua kikweli, hapo ndipo penyemfarakano baina waumini wa kweli.Wana Adamu huweza kuzusha ubishani mkubwa juu yachombo kidogo mfano wa saa – huyu akasema: “Sanaa ya Japan”(made in Japan), mwingine akasema: “Laa ni U.K” (made in U.k).Lakini ajabu, si kawaida kufuma watu wakizoza katika suala la BinAdam, kajiumba mwenyewe, (au kaumbwa na sheytwani nakadhalika).Katika kumjua Mnyezi Mungu ziko faida nyingi ambazoMwanadamu hawezi kuzidhibiti zote. Inatosha (lau Mnyezi Munguhafanani kinamna hiyo), kuangalia mfano wa Mtu anavyofanyarafiki mpya.Mwislamu anatosha kuitwa “A-llim” (yaani mjuzi sio –mjinga), kwa kuyajua majina (ya Mnyezi Mungu 99 - Tisinin natisa) maarufu kwa “Asmaaul Lahil husna – Majina ya MnyeziMungu, yalio matukufu na mazuri mazuri”.Twaba-an katika kujiandaa kumjua kwako, kama si kwahayo Majina 99 ambayo yamekusanya Swifa chungu nzima, basihata yale 20 au13 ambayo ndio Wa-jibu, hutakosa kujua kua yeyeyupo, na haiwezekani kukosekana – kwa sababu kukosekana ni sifapungufu ambapo si laiki yake (yaani na hazimstahiki hata kidogo).Sifa yeyote ya Mnyezi Mungu ambayo Akili ya Mtu (ikiwa ndochombo pekee kilicho madhubuti kuweza kuhukumu majambo yoteMtu kwenye uhai kinjia ya miujiza ilokwea kabisa) haiwezikuikubali, basi sio yake kweli. Na bila kuilisha kuilisha mfano wamasuala kama: “Mnyezi Mungu kakosekana. Jee kaenda wapi?“Nani badala yake alishika nafasi yake?” Na “Waja wakewalikiabudu nini alipokosekana? Kwa hali yeyote ile sifa kamahizo akili haiwezi kuzikubali.Mnyezi Mungu sio mjinga kwa hiyo yeyote anayejiandaakumjua ni wajibu kua na Ilimu – basi kwa uchache hata kwa kuulizawale wajuzi ili wakueleweshe vizuri.Katika sifa za Mnyezi Mungu zilizoepukika na Upungufu(nuksani) 99 ndani yake muna kila jambo linalohusu (Manufaa)79.

na maslahi ya Uhai wetu hapa duniani. Angalia vile alivyosemakatika:Qur an: A`arafa: 7:180.“Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri mazuri,muombe kwayo. Na wacheni wale wanaoharibuutakatifu wa majina yake. Karibuni hivi watalipwayale waliyokuwa wakiyatenda”.Neno: “Muombeni kwayo” si neno jepesi kwa wenyeakili, kwa wenye Tadabbur kwa sababu Ulamaa wamegundua mengindani ya maneno machache kama hayo . Mathalan ukizingatia tangupale aliposema:Qur an: Dhaariyaat: 51: 56.“Sikuwaumba Majini na Watu ila wapate kuniabudu”.Na aliposema:Qur an Banu Isra-el: 17: 110.“Sema, muombeni (mwenyezi Mungu) kwa (Jina la)Allah au muombeni (kwa jina la) Rahmaan, kwajina lolote mnalomwita (katika haya itafaa) kwaniana majina mazuri mazuri”.Ni (hakika) yenye kuonyesha jinsi wazi kuwaMnyeziMungu anapenda kuombwa (kinyume na sisi ambao huchukiakuombwa sana sana hata tukiwa matajiri au wakwasi vipi), na80.

Anachukia asipoombwa.Na isitoshe kaonyesha jinsi (njia Method) ya kumuombakwa kusema:“Muombeni (Mwenyezi Mungu) kwa (Jina la)Allah au muombeni (kwa jina la) Rahmaan”.Ikionyesha kua kila tunapopatwa na shida yeyote ndani yamaisha yetu, basi tumuombe Mnyezi Mungu kwa jina lenyemnasaba na ile shida yenyewe; na lazima litakuepo tu jina lenyekunasibiana na shida hiyo , amma sivyo ingembidi Mnyezi Munguaongeze majina mengine.Kwa hivyo katika mazingatio ya Maulamaa juu ya hakikahii wametupanua mawazo yetu kwa kuweka wazi njia za kuombea.Kwa ufupi tu njia mbili hizi zenye kutoshekeza mahitaji (aumatakwa yetu).1. Kumuomba kwa namna hiyo hiyo aloifahamisha yeyeMwenyewe wazi wazi kabisa “Allah – au –Rahmaan” Jina moja Allah ikiwa ndo kama Kubwalenye kutosheleza kwa jumla inamaanisha kua kwashida yeyote ile utafanikiwa tu ukilitumia jina hilo.Khilafi na Rahmaan ambalo linaweza kujihusisha namambo ya Neema kubwa kubwa au Rehma. Kwahivyo, kwa kufwata mfano huo pindi tukiwa na shidamfano wa “Ugonjwa” na tumeshindwa kuvumilia,tunahitaji kupona, basi tutatizama katika Majina 99tuone ni Jina lipi la Mnyezi Mungu mahususi kwatatizo letu? Bila shaka ni “Afuwwu” – “MwenyeKuafu” au “Shaafi” – “Mwenye Kuponyesha” basitutaomba uzima wetu kwa jina lake hilo.Mfano mwingine tuko hohe hahe, tunahitaji hali yauwezo wa kifedha, basi bilkul Mnyezi Mungu ni“Ghaniyyi” tutamtegemea yeye kwa jina lake hilo. Aukama tunachohitaji ni matayassar tu, basi bila shakayeyote Mnyezi Mungu pekee ndiye “Ra-zaq”Mwenye kuruzuku. Tutaomba kwa jina lake“Ra- zaq” au “Ba-switu” kwani ndiyo majina laaikkwa shida kama hizo.Amma Wakulimawanapokwisha kupanda wakawa wanategemea Molaawaletee Mvua ili kuotesha mbegu zao, basi81.

wangestahiki wamuombe kwa Jina lake la“Muqiitu”, na halkadhalika Wanafunzi wa Vyuoniau Shule, madamu haja yao ni Ilmu, basi MnyeziMungu ni “A-lim” na “A-liim” wangetakawangeomba (pamoja na kujifunza kwao –sio kukaa nyumbani kuomba tu “Ya A-lim,Ya Aliim) kwa jina lake moja kati ya mawili hayo.Huo ni mfano mmoja tu ambao Mnyezi MunguAmetuonyesha, basi sio atuonyeshe kwa kila namnatena. Katika Qur an ambayo imekusanya kilalinalohitajiwa kwa njia ya mifano ya muhtasari.2. Kuomba kwa Majina hayo hayo lakini kwa njia yaidadi. Kila jina lina idadi yake, na kila jina linwatumishiwake mahususi katika Malaika Ruhania. Tizamakwa ufinyu tu, Mnyezi Mungu alipoelezea:Qur an: Al Muddath-thir:74:30 - 31.“Juu yake wako (walinzi) kumi na tisa. Na hatukuwekawalinzi wa huo moto ila malaika, walahatukufanya idadi yao (hiyo ya 19) illa kuwa mtihanikwa wale waliokufuru…….”.Hadi mwisho wa aya hiyo ya 31.Na hizo idadi ziko ndogo, nazo ni zile zijulikanazo kama“Hijaiya” kwa kufwatana kwa “Alifu” ni moja “Bee” mbili, “Tee”Tatu hadi kufikia “Yee” ambayo ndo herufi ya mwisho katika“Hijaiya”, sawa na 29 au 30 kwa pamoja na “Hamza”- ambayo nisawa na “Alifu” kwa upande.Idadi kubwa ni “Abjadia” namna alivyoteremshiwa Naby AdamAsw, nayo ni “Alifu” ni moja, “Bee” – 2, “Jim” – 3, “Dal” – 4, na“Tee” ambayo katika “Hijaiya” ni – 3, katika “Abjadia” ni - 400– Hisabu hizo utazikuta katika baadhi ya vijuzuu vya Sura Amma82.

mwisho wa “Ka-ida” ambapo herufi ya mwisho ni “Ghain” nayoni 1000. Na ambayo “Kihijaya” ni 19. Halafu katika hiyo hiyo njiakubwa ipo njia nyingine tofauti kidogo. Na inapoingia hiyo basi, hiiambayo ndo kubwa inarudi kuwa ya kati na kati. Njia hiyo ni yakupatika herufi kama itamkwavyo moja moja. Mfano “Alif” ni –Alif, Lam, Fa. Kwa hiyo badala ya kua ni 1 (moja) inakua mia nakumi na moj (111) kwa sababu: Alif ni 1, Lam ni 30, na Fa ni 80.Kwa hivyo mfano wa Kumuomba Mnyezi Mungu kwaJina lake “Allah” itatubidi tutimize idadi yake mara 66 (Sitini nasita). Kwa njia zote hizo, Mnyezi Mungu humpa kila anaetakakupewa .Amesema Bwana Mtume Saw:“Mnyezi Mungu amekipa kila kitu silaha na silahaya muumini ni Dua”.Kwa hivyo kila mwenye akili lazima ajue matumizi yaSilaha vizuri kwani kisu kile kile ulichokinunua ili kikatiwe nyanyana vitunguu, kinweza pia kuhudhurishwa mahakamani kamakielelezo katika kesi ya kuua (Murder case).Vyovyote itavyokuwa, mategemeo yapo kwa muombajimwenyewe, katika kua na moyo kwake pamoja na matumaini(Confidence) mbele ya Mola wake. Kila siku tu anatakiwa awe namatumaini – Asikate tama kwa sababu: “Hawakati tamaa illa watumakafiri”.Ni kawaida kwa Mwanadamu kuelekeza mambo yakekwa yule ambae anajua ndie mwenye nacho kile akitakacho, na anamatumaini kua atampa au atapata tu kutoka kwake. Basi kulikokiumbe, Mnyezi Mungu ndie ahakki wa kua na kila tunachokitaka,mradi tu tuweke matumaini ya hali ya juu kua tutapata. Kwa sababutunamuomba Ambae hapungukiwi hata siku moja.Lakini inapotokea kukosa yale uliyoyaomba, basijichunguze wewe mwenyewe kwanza kwa sababu Mnyezi Mungu sirahisi kuvunja alichoahidi – Huenda sababu ikawa ni yenyekutokana na wewe mwenyewe au ikawa umeyakosea mashrti yakuomba. Basi jaribu tena utafanikiwa tu Insha Allah.Qur an: Baqara:2:186.83

“Na waja wangu watakapo kukuuliza hakikayangu (waambie kuwa) Mimi niko karibu nao.Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba.Basi na waniitikie na waniamini ili wapatekuongoka”.Sharti la Kwanza ni:1. Kumuitikia Mnyezi Mungu kwani anaita katika wema.2. Kumuamini Mnyezi Mungu.3. Unyenyekevu (Tawadhu-i).4. Woga (Khofu).5. Tamaa (kua utapata tu – Confidence).6. Kufanza mema haswa wazazi wawili (kwani BwanaMtume Saw. Amesema:“Ambaye wazazi wake wawili hawako Radhi nae,basi asiwe na haja na mimi”.Basi tuzingatie vizuri sharti kabla kujilaumu. Wengine hutangulizaSwadaka kwa kuwapa watoto (hasa yatima ambao wamekatikiwakabisa), basi Mnyezi Mungu hufurahi na hujibu haraka haraka Duaya mwombaji. Wengine hulisha masikini kwanza kabla ya kuombaDua zao. Tuelewe kwamba masikini wako karibu sana kwa MnyeziMungu, na ndo maana Bwana Mtume Saw akiwapenda sana. Wao piaWataingia mwanzo peponi. Bwana Mtume Saw ameeleza kua:“Ameonyeshwa Pepo akaona wengi ya wakazi wakeni masikini, na akaonyeshwa motoni akaona wengiya wakazi wake ni wanawake”.Maswahaba walipomuuliza juu ya wake zao ambaoWanaswali na kufanza khairati chungu nzima – AliwafahamishaSababu hasa ambayo ndo itofanza wengi waingizwe motoni, nayo ni:a) Kusahau Ihsani za Waume zao kwa kitu kidogo sana.b) Kuwakhini Waume zao.Waombaji wengine hueka Nadhiri kabla maombi yao. LakiniMnyezi Mungu hakopeshwi, kuliko kutumia siasa ya watoto ya:“Nipe Nikupe”. Wewe toa halafu uone utapata au laa?84.

Ufunguo ndo huo, basi kila tuonapo mafanikio, na Tumswalie sanaBwana Mtume Saw, Kwani ndo Mwalimu Mkuu.Allahuma Swalli Wasallim alaa SayyidnaMuhammad wa aalihi.Wabillahi Tawfiq85.

Vitabu vilivyokwishatoka ni:*1. Maana halisi ya Imaan. (i) (1 st , 2nd & 3rd addition).*2. Njia nyepesi ya kuijua nafsi yako.*3. Njia nyepesi ya kujua kitu juu ya uongofu.*4. Knowledge vision & ecstacy.*5. Mwinyi Baraka katika ulimwengu wa Uislamu (i) .*6. Waislamu na Sayansi - Ulu-m.*7. Kuhifadhi Burda.*8. Maana halisi ya Imaan (ii).*9. Muhammad SAW katika ulimwengu wa ghayb.*10. Siri ya Balaa.*11. El makhlouq (Viumbe)*12. Njia nyepesi ya kujua kitu juu ya uongofu. (2nd addition)*13. Manaqib ya Al habbib Sayyeid Al Ma`aruf.*14. Some aspects of concepts of facility in medevial IslamicPhilosophy by Mwinyibaraka.*15 maana halisi ya Imaani I (3rd. Addittion)*15. Njia nyepesi ya kuijua Nafsi yako. (2nd addition).*16. Mwinyi Baraka katika ulimwengu wa Uislamu ii.*17. Maana halisi ya Imaani ii (2 nd . Addition).Vitabu ambavyo tunategemea kuvitoa muda si mrefu(Insha Allah) ni:*1. Mwinyi Baraka katika Ulimwengu wa Uislamu I (2 nd . Addi.).*2. Muhammad SAW Bwana wa Mabwana*3. Muhammad SAW katika ulimwengu wa Ghayb.*4. Waislamu na Sayansi - Ulu-m. (2nd addition)Kwa maulizo kuhusu vitabu wasiliana nasi:Majaalis El Ulaa - El Qadiriyya Sinza,86.P.o. Box 15170,Tel: 0747 483553Tel: 0748 595958.Tel: 0744 023703.Tel: 0741 235091.Tel: 0744 299597.Dar es salaam.

Ujumbe waAhly Majaalis:Assalam Alaykum:Ndugu Msomaji lengo la kitabu hiki siyo biashara;Madhumuni makubwa ni kuwa Waislamu wanufaike namafundisho ya Dini yao, kwani si wengi waliobahatika kupataIlmu ya madrasa eidha ukubwani au wakati wa utoto wao.Kutokana na gharama za uchapishaji kuwa kubwa ndiyoimetubidi tukiuze kitabu hiki ili kufidia gharama na tuendeleekutoa vitabu vingine.Kama Muislamu yeyote atakuwa yuko tayari kutoagharama za uchapishaji ili avitowe bure hivi vitabu, basi sisituko tayari. Awasiliane nasi ili tufanikishe hilo kwa ajili yaAllah.Wabillahi Tawfiq.87.

Al habib Al Faqeer Ahmed Sheikh Mohamed Sheikh Msiha, amezaliwaSingida mkoa wa Dodoma, mwaka 1938. Amepata elimu ya sekula Ungujana amebahatika kupata elimu ya juu katika chuo maarufu Afrika yaMashariki Makerere Uganda.Elimu yake ya Dini ameipata hapo hapo Unguja toka kwa Masheikh mbalimbali, baadhi yao ni:Sheikh Sleiman Alwi (Muhib Rasul) (Al Marhum).Sheikh Seyyid Mansab.Maalim Himid (Al marhum).Maalim Hemed Muhamed El Buhry.Sheikh Mohammed Qamus.Sheikh Muawwiya Ibn Abdul Rahman.Sheikh Ally Muhamed Comorian.Sheikh Ibrahim Mzee Ahd.Sheikh Haj Mzee Ahmad Msiha.Amma Elimu ya Nafsi na Roho Amepata Ijaza yake toka kwa A`limumkubwa Duniani Al Habib Seyyid Omar Bin Abdallah (Mwinyi Baraka).Sheikh Ahmad amewahi kufanya kazi katika jeshi la Polisi Tanzania Barakatika mikoa mbali mbali mpaka alipostahafu.Katika umri wake wote Sheikh Ahmad alijahid katika kuendeleza Uislamukwa kusomesha na kuandika vitabu vya mada na maudhui mbali mbali katikaUislamu. Pia alianzisha Majaalis Sehemu mbali mbali ambazo ziko mpaka leo,Mtaa wa Pemba, Sinza, Bungoni, kijito nyama, Sadani (Ilala) na Kibaha(Misugusugu) ambapo ndipo ilipo Dhwariha lake (alipozikwa).Sheikh Ahmad ametwawafu 27. 8. 2001. ( Mwezi 7 jumadda thany 1421H.R.). Akiwa na umri wa miaka 63, vile vile alivyokuwa akiomba aishi umri uleule alioshi kipenzi chake Bwana Mtume Muhammad SAW.Insha Allah Mnyezi Mungu amjaze kheri na alizidishie Nuru dhwariha lake(Amin).Majaalis El Ulaa El Qadiriyya,Sinza Dar es Salam.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!